Ilipoishia Sehemu Ya Pili
“Kazi imeisha!” Alisema Diana kwa njia ya simuย
“Waoo Good Girl ( Vizuri Msichana mzuri ) ” ilisikika sautiย nzito ya kizeeย
“Rudi Tanzania” Alimalizia kusema Mwanaume huyo kwa njia yaย simu, simu hiyo ilikatika, tayali polisi walishafika nje yaย Hoteli hiyo, Diana alichofanya ni kuingia kwenye chemba yaย maji machafu akaenda kutokea mbali na eneo hilo.ย Endeleaย ย
SEHEMU YA TATUย
Tayali ilifahamika ni wapi ambapo Faudhia angepatikana niย mpaka wa Namanga, ilihitaji auawe kabla hajafika Tanzania.ย
Mishale ya saa 11 Alfajiri vijana wa Khalid Bangalaย walijaribu kumtafuta Bosi wao bila mafanikio, hawakujuwaย wafanye nini sababu maelekezo yote walikuwa wakipewa na Bosiย wao ambaye alikuwa ameshauawa Hotelini, majadiliano yaoย yalimuamsha Faudhia akiwa ndani ya Sanduku.ย
“Unafikiri tutafanya nini, Simu ya Khalid haipatikani,ย tufanyaje na tunakaribia eneo lenye askari” Alisema mmoja waย Vijana hao, Faudhia aliposikia hivi alihisi kuna hatari,ย kutokana na mafunzo aliyoyapitia aligundua pengine kuna jamboย halipo sawa, aligonga afunguliwe huku akisema amebanwa sanaย na Haja. Vijana hao walisimamisha gari hilo, walikuwa juu yaย mlima, kulikuwa kunapambazuka na iliwahitaji kutembea chiniย ya Kilometa 15 kufika Mpakani. Faudhia hakutaka kujioneshaย kuwa amehisi jambo lisilo la kawaida, hakutaka kuwaamini mojaย kwa moja, walikuwa na bunduki ambazo walizificha, mmojaย alimsindikiza Faudhia kujisaidia huku akiwa amemshikiliaย Bunduki kwasababu alikuwa bado hajawalipaย
“Pale ni wapi?” Alihoji Faudhia akiwa anazidi kusogea sehemuย ya kujisaidiaย
“Longido” alijibu Mwanaume huyoย
“Unamaanisha Tanzania?”ย
“Ndio, unapaswa kutulipa kwanza sababu umeshafika eneo husikaย ambalo sisi hatuwezi kusogea huko, kuna ulinzi wa Askari waย mpakani.” Alisema Mwanume huyo
“Simama hapo basi au unataka kunichungulia!” Aliuliza Faudhiaย na kumfanya Mwanaume huyo asimame lakini akiwa anamuoneshaย Bunduki Faudhia ambaye alikuwa tayali ameashaanza kujisaidia.ย
Akiwa anajisaidia alisikia milio ya Risasi za haraka kishaย ukimya ulitanda, yule aliyemsindikiza alirudi kule harakaย akakuta wenzake tayari wameuawa, lilikuwepo kundi la watuย tano ambalo lilitokea msituni na kumtaka Mwanaume huyoย anyanyue mikono yake juu. Wanaume hao walikuwa wakiongeaย rafudhi ya Kenya, haraka Faudhia alifungua kibegi chakeย kidogo akatoa bastola yake, ukimya ulitawala, Faudhiaย alijaribu kuchungulia eneo la tukio ndipo alipowaona Wanaumeย hao, haraka alizama kwenye kichakaย
“Msichana yupo wapi?” Alihoji mmoja wa Watu hao huku akiwaย amenyooshea bastola yule kijana wa Khalid aliyebakia, yuleย Mwanaume hakuwa na chaguo ilibidi aoneshe mahali ambapoย Faudhia alikuwa ameingia kwa ajili ya kujisaidia, alipigwaย risasi yule Mwanaume kisha lile kundi liliongoza mahaliย ambapo Faudhia alikuwa ameingia, ilikuwa inakaribia saa 12ย asubuhi, kulishaanza kupambazuka.ย
Faudhia alishajuwa hali ya hatari ilikuwa imenukia eneo hilo,ย alichofanya ni kuanza kukimbia kuelekea mpaka wa Namangaย upande wa kaskazini ambako ndipo ilipo Wilaya ya Longido,ย alikuwa na maelekezo maalum ya eneo gani anapaswa kupitaย ambalo litakuwa salama lakini kutokana na milio ya Risasiย kusikika iliwashtua askari wa mpakani wakatoka kwa ajili yaย kuangalia kulikuwa na tatizo gani.ย
“Yule pale” Alisema kiongozi wa kundi hilo la Watu watano,ย walipewa amri ya kumuuwa Faudhia kutoka kwa Mtu ambayeย hakujulikana hadi kufikia wakati huo, ila Faudhia alijuwa niย kwanini Watu hao walikuwa wakimfuatilia ila hakujua wametumwaย na nani.ย
Milio ya Risasi iliendelea kurindima msituni hapo, Faudhiaย alijitahidi kukimbia ili kuokoa Maisha yake. Ulikuwa niย mtafutano wa zaidi ya dakika 10 bila mafanikio kwa Wanaume waย kundi hilo kumpata Faudhia ambaye alishahitimu mafunzo yaย ujasusi huko Mexico, Faudhia alifuata maelekezo maalum iliย aonane na Mtu mwenye gari msituni hapo, bahati mbaya akiwaย anakaribia alikutana na Askari wa mpakani ambao walikuwaย wakifuatilia milio ya Risasi, Faudhia alisimama kwa sekundeย kadhaa huku akiwa anatazama na Askari hao ambao walikuwaย mbele yake Mita kadhaa tuu kutokea aliposimama, pumzi zaย Faudhia zilimwambia kuwa hatuna jinsi bali kufa auย kujikamatisha mikononi mwa Askari hao.
“Weka silaha yako chini” Alisema mmoja wa Askari hao, Kilaย hesabu aliyokuwa anaipiga Faudhia haikumpa jibu linalotakiwa,ย alijikuta akijisalimisha mwenyewe, Askari walianza kusogeaย taratibu kwa makini sana eneo ambalo Faudhia alikuwaย amesimama, wale wanaume wa kundi la Kigaidi hawakujua kuwaย Faudhia alikuwa amesimama mbele ya kundi la Askari polisi,ย walitokea eneo hilo na kushtukizwa na askari polisi kishaย mashambulizi ya Risasi yalianza kusikika huku haraka Faudhiaย akichumpa na kujitupa kwenye poromoko dogo, Milio ya Risasiย iliendelea kusikika lakini haikufamfanya Faudhia asimame walaย arudi nyuma, alizidi kusonga mbele hadi alipofika mpaka waย Namanga, alivuka na kuingia Tanzania.ย
Mashambulizi baina ya Askari polisi wa mpakani na Lile kundiย yaliendelea na kumpa uhuru Faudhia kukutana na Mtuย aliyepangiwa kukutana naye mpakani hapoย
“Ingia kwenye gari haraka tuondoke eneo hili” alisemaย Mwanaume mmoja ambaye ndiye aliyetakiwa kumchukua Faudhiaย mpakani na kumfikisha Arusha Mjini, Faudhia aliingia ndani yaย gari na safari ilianza kuelekea Arusha Mjini.ย
โขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขย
Jeshi la polisi liliizunguka Benki kuu ( B.O.T ) iliย kuhakikisha hakuna anayetoka humo benki, ndani ya Benki hiyoย alikuwepo Mtu hatari aliyeitwa Chogo, tayari alikuwa amemtekaย Mke wa Gavana na Gavana mwenyewe ambao wote walikutwa ndaniย ya Benki hiyo, nje ya Benki zilionekana maiti za Askariย kadhaa ambao walikuwa wakitaka kufanya jaribio laย kushambuliana na Magaidi hao ambao walionekana kuzungumzaย kiswahili kizuri, ilikuwa ni mishale ya saa 1 asubuhi juaย lilikuwa likichomoza, ukimya uliendelea kutawala na hakukuwaย na Raia aliyekuwa akifanya safari. Muda huo huo Mzee Shayoย aliwasili akiwa na gari yake, alikutana na Mkuu wa operesheniย hiyo aliyeitwa Sir Jeff, waliitana chemba kwa ajili yaย mazungumzo, wote walionekana kuanza kukata tamaa kwa jinsiย Magaidi hao walivyokuwa na mbinu kali za kukabiliana naย Askari.ย
“Niambie mpango unaendaje?” Aliuliza Mzee Shayo hukuย akitazama saa yakeย
“Gavana na Mke wake wameshikiliwa ndani ya Benki” alijibu Sirย Jeff akiwa anamtazama Mzee Shayoย
“Hawajasema wanataka nini?” Aliuliza tena Mzee Shayo
“Hakuna hata mmoja aliyezungumza hadi hivi sasa zaidi yaย ishara tu kupitia kioo kikubwa”ย
“Shenzi sana!!” alisema Mzee Shayo, punde simu yake iliita,ย alipoangalia aliona ni Faudhia alikuwa akimpigia kwa njia yaย Whatssap, alisogea pembeni kuipokea sababu hakutakaย kunshirikisha yeyote juu ya Ujio wa Faudhiaย
“Baba!! Nipo Arusha” Alisema Faudhia, hivi ndivyo ambavyoย Faudhia alikuwa akimchukulia Mzee Shayo, alimchukulia kamaย Baba yake mzazi baada ya kumsaidia kumtoa kwenye mikonoย hatari ya Mzee Shomari miaka mingi iliyopitaย
“Sawa Faudhia! Nakutumia picha, nataka uchunguze huyo Mtuย anafahamika vipi hapo Arusha, ndiye mshukiwa namba Moja waย tukio hili la Ugaidi” Alisema Mzee Shayo kisha alimtumiaย picha Faudhia, ilikuwa ni picha ya Martin Gimbo ambayeย alijitambulisha kwa askari kama Chogo. Mara moja Faudhiaย alianza kazi ndani ya Jiji la Arusha. Mfumo wa serikaliย ulishawekwa kwenye kiganja cha Faudhia, alitumia kompyutaย mpakato ambayo alitumiwa na Mzee Shayo kupitia jamaaย aliyemchukua pale Mpakani, kompyuta hiyo ilikuwa naย mawasiliano na Kitengo cha Usalama wa Taifa, muda huo Faudhiaย alikuwa Hotelini akiifanya kazi hiyoย
Aliingiza picha kwenye mtandao wa Idara ya Usalama wa Taifa,ย alimuona jamaa huyo aliyeitwa Martin Gimbo. Taarifa za Jamaaย huyo zilionesha kuwa alizaliwa Arusha Mjini, aliona ni wapiย alisoma hivyo ilikuwa ni kazi rahisi kwa Faudhia, juaย lilikuwa limeshaweka makazi katika anga kwa ajili yaย kuimulika Dunia, Faudhia aliutumia usafiri wa gari waliyotokaย nayo mpakani akiwa na jamaa aliyeitwa Mohd, walienda kwenyeย shule ambayo waliona kuwa Martin Gimbo alisoma, bahati nzuriย ilikuwa ni siku ya Shule, waliingia hadi ofisi ya Mwalimuย Mkuu, walienda shule ya Sekondari ambapo waliamini taarifa zaย Martin zingepatikana.ย
Walikaribishwa na Mwalimu mkuu wa shule hiyo ambaye mudaย mchache baadaye aliketi kuwasikiliza huku akionekanaย kuzishangaa sura za akina Faudhiaย
“Naitwa Undercover Mohd kutoka kitengo cha Usalama wa Taifa”ย alijitambulisha yule jamaa huku Faudhia akiwa kimya, Mohdย alitoa kitambulisho ili kumuaminisha Mwalimu huyo ambayeย alikuwa akitetemeka kutokana na woga sababu taarifa za ugaidiย zilizizima katika Miji mikuu ya Dodoma na Dar-es-salaam.ย Baada ya kujiridhisha Mwalimu huyo alishusha pumzi zake kishaย aliondoa mawani
“Haikuwa rahisi kuwaamini sababu Wanafunzi na Waalimuย wameanza kukimbia Mji huu kwasababu ya uvumi kuwa baada yaย Dodoma na Dar utafuata Mji huu kuwa chini ya Magaidi” alisemaย Mwalimu huyo kisha alishushia maji yaliyo ndani ya chupa,ย alionekana kuwa na mengi ya kusema, alinyanyuka na kwendaย kufunga mlango kisha ndani kukawa giza aliwasha taaย
“Niwasaidie nini vijana?” Aliuliza Mwalimu huyo ambayeย alikuwa na mvi kiasi kuashiria kuwa umri wake ulikuwaย umeenda. Faudhia alitoa picha ya Chogo akamuonesha Mwalimuย huyo, Mwalimu aliichukua picha hiyo kisha aliisogeza kwenyeย Mwanga, alishtuka baada ya kumuona chogo kisha alimpatiaย picha Faudhiaย
“Unamfahamu huyo Mtu?” Alihoji Mohdย
“Hapana” Alijibu Mwalimu baada ya kukaa kimya kwa sekundeย kadhaaย
“Mwalimu, ukweli wako utaliweka Taifa hili huru. Sura yakoย inaonesha unamfahamu, tuambie anaishi wapi na unamfahamuย vipi?” Alidakia Faudhiaย
“Nimesema simjui mnanilazimisha ili iweje? Simjui huyo Mtuย hebu nendeni” alisema Mwalimu kwa hasira huku akifoka mithiriย ya chatu aliyejeruhiwaย
“Unamjuwa huyu Mtu ndio maana unajaribu kuficha, Mwalimuย tuambie huyu Mtu anaishi wapi na unamfahamu vipi?” Alisemaย Mohd kwa sauti iliyokaukaย
“Nimesema simjui, hebu ondokeni ofisini kwangu haraka sana”ย Alisema Mwalimu kwa sauti ile ile huku akinyanyuka kitiniย mfano wa Mtu aliyetaka kuondoka ofisini hapo, Faudhiaย alichomoa bastola na kumuonesha Mwalimu huyo.ย
Bastola ilimfanya Mwalimu anywee kidogoย
“Endapo utaendelea kukanusha nitapasua ubongo wako sasa hivi,ย unamjuwa huyu Mtu anaitwa Martin Gimbo. Alisoma hapa kwaย miaka minne” Alisema Faudhia akiwa amemshikilia Bastolaย Mwalimu,ย
“Sisi siyo Watu wabaya ila unatulazimisha kufanya huo ubaya,ย kama hutaki kusema hebu tupatie faili la Martin” Alisema Mohdย
Mwalimu hakuwa na neno jasho lilikuwa likimtiririka, alivutaย droo la meza alitoa faili lenye maelezo yanayomuhusu Martinย Gimbo, Faudhia alipolifunua Faili hilo, halikuwa na picha yaย
Martin, halikuwa na maelezo kuwa Martin alikuwa akiishiย sehemu ganiย
“Taarifa zimeenda wapi?” Alihoji Faudhiaย
“Msijaribu kulifuatilia hilo jambo, hamtafanikiwa nawaambia,ย mtakufa kabla ya kujuwa chochote kile” Alisema Mwalimu huyoย
“Ona hii” Alisema Mohd baada ya kuangalia kwa makini walionaย namba ya simu nyuma ya faili hilo, ilibidi walichukue failiย hilo, Mohd alichukua bastola na kumpiga mwalimu huyo.ย
“Kwanini unauwa?” Alihoji Faudhiaย
“Hana faida yoyote” Alisema Mohdย
“Tuondoke haraka sana” Aliongeza Mohd kisha waliingia ndaniย ya gari na kutoweka eneo hilo, wakiwa ndani ya gari waliipigaย namba hiyo, ilipokelewa na Mwanamke mwenye sauti dhaifu sana,ย ilionekana alikuwa mgonjwa maana alikuwa akikohoa sanaย
Faudhia aliutumia ujanja wa mafunzo yake, walielekezwa alipoย mpokeaji wa simu hiyo, walienda kuonana naye lakini njianiย Faudhia alijiuliza Kwanini Mohd alimuuwa Mwalimu Mkuu baadaย ya kuyatamka maneno yale? Hakutaka kuyapa kipaumbele,ย walisogea hadi eneo husika, walikutana na Mama mmoja dhaifuย sana wa mwili wake, alikuwa akiishi na Mjukuu wake wa miakaย 16ย
Walimsalimia Mama huyo kisha walimuulizaย
“Hapa ni nyumbani kwa Martin Gimbo?” Alipouliza hivi huyoย Mama alipata nguvu hata ya kukaa, Mjukuu wake alishangaa sanaย kwa Mama huyo kuketi mwenyewe wakati mara zote alikuwaย akimsaidia kukaa, Mama huyo alikaa kimya sanaย
“Je? Wewe ni Mama yake Martin?” Alihoji Faudhia, Mama huyoย aliwatazama kisha aliwaulizaย
“Mnamuulizia Martin Gimbo?” Aliuliza kama vile Mtu aliyetakaย kupata uthibitisho wa alichokisikiaย
“Ndio, Martin Gimbo, unamfahamu?” Alihoji Mohdย
“Ndio, ni Mwanangu! Miaka mingi sasa tangia Martinย alipofariki kwa ajali ya gari akiwa anaelekea Mjini, tanguย siku hiyo sikuwahi kuamka na kukaa tena hata ongea yanguย ilikuwa ya shida, Martin alikuwa ndiyo Mwanangu wa pekeeย niliyempenda, tumaini la Maisha yangu lilikuwa kwa Kijanaย wangu Martin baada ya Baba yake kufukiwa na kifusi hukoย Merelani akiwa anafanya kazi za mgodi” Alisema Mama huyo,ย kisha alimuomba Mjukuu wake amsindikize mahali.ย
“Nifuateni” Alisema Mama huyo ambaye alijitambulisha kamaย Mama yake Martin Gimbo ambaye alikuwa akitajwa kama gaidiย kiongozi wa kundi la ESS .
Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA NNE
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
16 Comments
https://shorturl.fm/m8ueY
Hii Ik0 0n ๐ฅ
Noma sana
Inakuja Kwa Wakati Saana Jamani Hadi Raha Ahsante Admn
Wanaenda kufanywa nn… Kama ye ndo mkuu wa kitengo ๐๐ฝโโ๏ธ๐๐ฝโโ๏ธ๐๐ฝโโ๏ธ๐ฅฑ๐ฅฑ
Tupe nyingine admin
Nzuri sana Admin
Hii ya Moto Sana Admin
Mama anajambo lake,๐ค admin tunahitaji mwendelezo kwa wakati tafadhal,,,simulizi nzuri sana๐
https://shorturl.fm/68Y8V
https://shorturl.fm/TbTre
https://shorturl.fm/9fnIC
https://shorturl.fm/6539m
https://shorturl.fm/xlGWd
https://shorturl.fm/f4TEQ
https://shorturl.fm/nqe5E