Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nneΒ
“Assssh” aligumia Faudhia kutokana na maumivu ya kujigongaΒ kwenye meza, Mohd hakutaka kusubiri alimrushia ngumiΒ mfululizo, ngumi ambazo zilimpekeka Fuadhia ukutani, bahatiΒ mbaya ngumi nyingi zilimpata na kumfanya aumie usoniΒ
Mohd alimpiga Faudhia mateke mfululizo eneo la mbavu hukuΒ akimwambiaΒ
“Unakufa leo” Alisema huku akiwa anamuangalia Faudhia akiwaΒ anaanguka chini. Endelea
SEHEMU YA SITA
Mohd alimsindikiza Faudhia kwa teke kali lililomzimishaΒ Faudhia, Mohd alitoa kifaa kidogo ambacho kilikuwa na sindanoΒ ya sumu ndani yake, aliitoa kisha alimkita Faudhia eneo laΒ shingo.Β
Baada ya kuhakikisha amemdunga alielekea Kuvuta kochi kishaΒ aliitafuta simu yake ambayo ndiyo ilikuwa muhimu sana kishaΒ Bastola yake ambayo ingekuja kuwa ushahidi pale, aliichukuaΒ Bastola na simu kisha aliondoka eneo hilo.Β
Sekunde kumi na tano baadaye sindano ya sumu ilianza kufanyaΒ kazi yake, Faudhia alishtuka huku akiwa anateswa na sumuΒ ambayo ilikuwa ikisambaa kwa kasi mwilini, alijikuta akianzaΒ kuishiwa nguvu, alijivuta kisha alifungua kibegi chake kidogoΒ alitoa sindano, alivuta dawa haraka kutoka kwenye chupaΒ kidogo kisha alijidunga sindano akiwa anavuja damu, kishaΒ alianguka chini na kuzima.Β
Usiku huo, Mzee Shomari alikuwa akisubiria simu ya Mohd iliΒ kumpa taarifa ya kifo cha Faudhia. Alikuwa kwnye kiti chaΒ walemavu akitembea sebleni ndani ya Jengo la China plazaΒ jengo ambalo walilifanya kuwa makao yao ya siri walipoanzaΒ kupanga mipango ya Kigaidi, jengo hilo lilikuwa la rafikiΒ yake aliyeko Uholanzi ambaye ndiye aliyekuwa anafadhiliΒ ugaidi.Β
Alianza kukumbuka miaka mingi iliyopita katika Jiji la Mbeya.Β
Siku ambayo alikamatwa Baada ya kumuuwa Mama yake Diana,Β alimtazama kwa hasira sana Faudhia, alijenga chuki na kisasiΒ kwa Faudhia. Mzee Shomari alipelekwa Kituo cha polisi,Β alipewa mateso makali sana ikiwemo kuwekwa kwenye beseniΒ lenye maji na kukosa pumzi, alikumbuka jinsi alivyopigwa hadiΒ kuvunjwa mguu na ndiyo sababu ya yeye kuwa mlamavu ndiyoΒ maana anatembea kwenye kiti cha walemavu.Β
Alipelekwa mahakamani baada ya kupata matibabu ya mguu kishaΒ alihukumiwa kifungo cha Maisha jela, alipofika huko alikutanaΒ na mzungu aliyeitwa Damian, alijenga urafiki na Mzungu huyoΒ ambaye alikuwa na kesi ya kusafirisha madini kinyume chaΒ sheria kutoka Tanzania kwenda Thailand, walishibana wakiwaΒ gerezani.Β
Akiwa anaendelea kuwaza kilichotokea baada ya kufungwa, simuΒ ya Mzee Shomari iliita alipopokea alisikia sauti ya MohdΒ ikimwambiaΒ
“Faudhia ni damu baridi” Alisema akiwa na maana kuwaΒ ameshamuuwa, Mzee Shomari alishangaa sana kwa jinsi ambavyoΒ alimuuwa Faudhia kisha alimuuliza
“Upo wapi?”Β
“Nipo njiani narudi Dar” Alisema MohdΒ
“Tukio lilikuwaje?” Alihoji Mzee Shomari kwa unakini mkubwaΒ huku akionekana alikuwa mwenye akili sanaΒ
Mohd alimsimulia Mzee Shomari tukio lilivyotokea kisha MzeeΒ Shomari alisemaΒ
“Ukifika Chalinze utaona kuna prado nyeusi, itumie” AlisemaΒ Mzee Shomari kisha alikata simu. Alisogea na kutazama chini,Β aliliona namna jiji la Dar lilivyokuwa likiwaka taa hukuΒ barabara ya kutoka Karume kwenda Kariakoo ikiwa nyeupe hakunaΒ Mtu wala gariΒ
Alinyanyua simu yake akapiga simu mahali kisha akasemaΒ
“Case Clossed ( Kesi imeisha ) ” alikata simu akajisukuma naΒ kuingia kwenye chumba kingine.Β
Masaa matano baadaye Mohd alifika Chalinze usiku sana akiwaΒ na gari yake aina ya Toyota V8, mji ulikuwa kimya kabisa,Β alilliona Prado likiwa linawasha hazard kuashiria kuwaΒ lilikuwa ndiyo gari ambalo Mohd alitakiwa kulitumia, harakaΒ alishuka na kulielekea gari hilo, alipoingia aliangaza ndaniΒ ya gari hilo ili kuona kama kulikuwa na Mtu lakini gari hiloΒ halikuwa na Mtu, alivuta funguo na kuiwasha, kitendo chaΒ kuwasha tu gari hilo lililipuka, Mohd alifia ndani ya gariΒ hilo, pembezoni kulikuwa na roli, ndani ya Roli kulikuwa naΒ Mtu ambaye alisikika akiongea na simu akisemaΒ
“Target eliminated ( Mlengwa amemalizwa )” kisha roli hiloΒ liliwashwa na kueleka Upande wa morogoro.Β
Siku iliyofuata, Chogo alipewa kazi na Mzee Shomari yaΒ kuhakikisha anaifahamu ilipo chemba ya siri ambayo pesa hizoΒ za Kimarekani zilikuwa zimehifadhiwa, Mtu pekee ambayeΒ alidhaniwa kuwa anajuwa ilipo alikuwa ni Gavana wa BenkiΒ hiyo. Pesa ambazo akina Chogo walikuwa wanazitaka zilikuwa niΒ pesa za siri ambazo Tanzania iliyauzia madini Nchi ya SaudiΒ Arabia. Chogo alirudi ndani ya chumba ambacho GavanaΒ alikuwemo na Mke wake, alikuwa ameweka rehani maisha ya mmojaΒ wa wafanyakazi wa Benki hiyo ili Gavana aseme mahali ambapoΒ pesa hizo zilikuwa zimehifadhiwa.Β
Gavana alimuuliza Chogo amajuwaje kama ndani ya Benki kunaΒ pesa za siri ambazo zilitokana na mauzo ya madini
“Acha kuuliza maswali ambayo kamwe hutoweza kupata majibuΒ yake, sema ilipo chemba ya siri vinginevyo namuuwa huyu!!”Β Alisema Chogo huku Bastola ikiwa kichwani kwa Mfanyakazi huyoΒ
Gavana alikaa kimya hakuonekana kumtetea Mfanyakazi asiuawe,Β alimtazama Mke wake kisha alirudisha macho kwa chogo.Β
“Umejuwaje?” Aliuliza tena kwa mshangao mkubwa sana, ChogoΒ alionekana kuwa ni Mtu katili mwenye hasira sana, alimpigaΒ risasi mfanyakazi kisha akamwambia GavanaΒ
“Nakupa masaa matatu uoneshe ilipo chemba ya siri” ChogoΒ alisema kisha aliondoka ndani ya chumba hicho.Β
Upande wa pili, Mzee Shayo alianza kuingiwa na wasiwasiΒ kuhusu vijana wake wawili aliowatumainia, simu ya MohdΒ haikupatikana baada ya kuuawa ndani ya gari, simu ya FaudhiaΒ iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa, ilimpa mashaka juu yaΒ usalama wao, alijitahidi sana kupiga simu lakini simu yakeΒ haikuweza kumpa majibu ya nini kilichokuwa kimetokea hukoΒ Arusha kwenye operesheni ya kujuwa kuhusu Chogo, alitumaΒ Askari wengine wa Kitengo kuelekea Arusha kwa ajili yaΒ kuwatafuta Mohd na Faudhia.Β
Punde alipokea simu ya Rais iliyomtaka aende Ikulu harakaΒ sana, kutoka Kigamboni yalipo makao makuu ya Kitengo cha siriΒ cha Usalama wa Taifa ilimchukua dakika kadhaa, tayali hali yaΒ tahadhari ilitangazwa hivyo hakukutakiwa Mtu yeyote kutokaΒ ndani, Jiji lilikuwa kimya sana kama makazi yaliyotelekezwa,Β Mzee Shayo alifika hadi Ikulu kisha alienda kwenye chumba chaΒ siri ambacho Rais na Waziri Mkuu walikuwa wamehifadhiwa.Β
Rais alihitaji kujuwa Mzee Shayo alifikia wapi katikaΒ harakati za kupambana na Kikosi hicho cha Kigaidi, waliketiΒ watu watatu na kuanza kuzungumza, Mzee Shayo alimwambia RaisΒ kuwa ametuma vijana kuelekea Arusha mbako inaaminika kuwaΒ Gaidi namba moja aliyeiteka Benki kuu anatokea hukoΒ
“Huo ni ujinga Shayo! Unafuatilia historia ya Mtu badala yaΒ kupambana naye sasa hivi, hadi umalize kuijuwa historia yakeΒ pengine gaidi atakuwa amemaliza kazi yake na kuondoka Nchini.Β Benki ipo chini yao Shayo, historia histori historiaΒ itasaidia nini?” Aliuliza Rais akionekana kuwa mwenye hasiraΒ
“Mkuu kila jambo linahitaji taaluma katika utendaji, kabla yaΒ kutatua tatizo ni lazima tuangalie lilipoanzia itatusaidiaΒ kujuwa ukubwa wake!” Alijitetea Mzee Shayo
“Hivi kweli ulistahili kuwa Mkuu wa Kitengo cha Usalama waΒ Taifa? Magaidi wamechukua silaha Lugalo na makambi mengine,Β tayari Nchi hii imekuwa kisiwa cha vita unayajuwa madharaΒ yake? Kiasi kikubwa vita hii utapigana wewe na vijana wako,Β jeshi lipo katika hali ngumu ya kujinasua” Alisema Rais hukuΒ akionekana kuanza kususa mazungumzo hayo, Waziri MkuuΒ akamwambia Mzee ShayoΒ
“Kuna hazina kubwa sana pale Benki pengine ndiyo sababu yaΒ Ugaidi huu, hakikisha unafaulu Shayo, vinginevyoΒ hatutokuelewa” Alisema Waziri Mkuu kisha Mzee ShayoΒ alinyanyuka na kuaga, alipoondoka Rais alimuuliza Waziri MkuuΒ
“Nani anajuwa ilipo chemba iliyohifadhiwa pesa?” AliulizaΒ akiwa makini sanaΒ
“Kuna Mdada wa pale Benki anaitwa Selina, yeye bahati mbayaΒ yupo ndani ya Benki na ameshikiliwa kama watafanikiwaΒ kumtambuwa basi mpango wote utavurugika” Alisema Waziri MkuuΒ na kumpa muda wa kutafakari RaisΒ
“Una hakika Gavana hajui chochote?” Aliuliza RaisΒ
“Gavana anajuwa kuhusu pesa iliyohifadhiwa Benki ila hajuiΒ iliwekwa wapi sababu mpango ulifanywa kuwa siri kamaΒ ulivyoagizwa”. Alijibu Waziri MkuuΒ
“Nina uhakika hawawezi kuchukua pesa za Kitanzania watahitajiΒ zile Dola, hili jambo sitaki lifahamike popote na kamaΒ itatokea Mtu amejuwa basi katisha Maisha yake” Aliagiza RaisΒ
Naaam!! Mzee Shayo alipotoka Ikulu alihitaji kwendaΒ kutembelea makazi yake yaliyopo Mikocheni B, alikuwaΒ akitembea kwa siri sana hadi alipofika, Kisha aliingia kwenyeΒ chumba ambacho alikuwa akikitumia kufanya kazi zake, aliketiΒ ili kujipa utulivu huku akifikiria afanye nini.Β
β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’Β
Nje kidogo ya Jiji la Arusha, kulionekana gari moja nyeusiΒ aina ya prado ikiwa imeacha barabara na kukita kwenye MtiΒ
Tukio hilo lilionekana kutokea muda mrefu uliopita kutokanaΒ na ukimya ambao ulikuwepo, ndani ya gari hiyo alikuwemoΒ Faudhia akiwa ameegemea usukani, alikurupuka kama MzimuΒ kutoka kifo.Β
“Uhhhh” alisikia maumivu makali ya kichwa, alionekana kuchokaΒ sana, alifungua mlango na kutoka ndani ya gari, alijivutaΒ hadi chini ya Mti, aliitoa simu yake kisha aliiangaliaΒ alikuwa ametafutwa na Nani, aliona ni Mkuu wa Kitengo alikuwaΒ amempigia zaidi ya mara 40, alimpigia Mkuu huyoΒ
“Aah Baba!!” Alisema Faudhia akionekana kuwa na maumivuΒ makali kisha alikohoa na kuanza kumtia hofu Mzee ShayoΒ
“Faudhia upo sawa?” Alihoji Mzee ShayoΒ
“Nilichungulia mlango wa kuzimu lakini bahati nzuri mafunzoΒ yamenisaidia kujinasua” Alisema FaudhiaΒ
“Mohd yuko wapi?” Alihoji Mzee ShayoΒ
“Baba!! Mohd ndiye aliyetaka kunipeleka kuzimu, nimeshtukaΒ anafanya kazi upande wa Magaidi, anatumika upande huo naΒ sijui ametumika kwa muda gani, alipewa agizo la kunimaliza”Β Alisema FaudhiaΒ
“What? ( Nini? )” aliuliza kwa mshituko sana Mzee Shayo.Β
“Ndio…alafu, Mhusika Mkuu wa ugaidi ni Mzee Shomari”Β Alisema Faudhia na kumuacha kinywa wazi Mzee ShayoΒ
“Una uhakika na maneno yako Faudhia? Mzee Shomari si yupoΒ gerezani?” Aliuliza Mzee Shayo,Β
“Hapana, nina uhakika na ninachozungumza na yeye ndiyeΒ aliyetoa maagizo ya kuuawa kwangu, nahisi ni yeye ndiyeΒ aliyehitaji kunimaliza kabla sijavuka mpaka wa Namanga”Β Alisema FaudhiaΒ
“Shit!! Sasa kwanini wametumia nguvu kubwa ya kuzuia habariΒ za Chogo ikiwa gaidi namba moja ni Mzee Shomari?” AliulizaΒ Mzee ShayoΒ
“Kuna mtego mahali, inavyoonekana kuna mchezo unachezwa hapaΒ Baba” Alisema FaudhiaΒ
“Upo wapi kwa sasa?” Alihoji Mzee ShayoΒ
“Nipo nje kidogo ya Jiji la Arusha, jiji hili si salama tenaΒ Kwasasa”Β
“Sikia Faudhia, ni lazima umalize hiyo kazi, fuatilia ujuweΒ ni kwanini Chogo anafichwa, kuna ufunguo wa hili jambo katikaΒ Maisha ya Chogo, hujapata fununu yoyote?”
“Tulionana na Mama yake Chogo, alisema Mwanaye alifarikiΒ Miaka mingi kwa ajali ya gari na alituonesha na kaburi lake,Β lakini pia alituonesha picha ya Mtu aliyeleta Maiti ya ChogoΒ alikuwa ni Mzee Shomari” Alisema FaudhiaΒ
“Hapo kuna taarifa juu ya taarifa, tukio juu ya Tukio, hiyoΒ picha iliyopigwa Mzee Shomari alikuwa katika pozi lipi?”Β Aliuliza Mzee Shayo akiwa nyumbani kwake MikocheniΒ
“Ilionekana ni picha iliyopigwa bila Mzee Shomari kujiandaa,Β alikuwa akiongea na Mtu mwingine”Β
“Yes! Yes! Rudi Arusha haraka sana Faudhia, hakikishaΒ unafahamu stori nzima, naelekea gerezani kujuwa kuhusuΒ taarifa ya Mzee Shomari”Β
“Sawa Baba” Alisema Faudhia kisha alikata simu, alishushaΒ pumzi zake, alikuwa na kazi nzito iliyojaa hatari mbele yake.Β
Waligawana majukumu, Faudhia alirudi Arusha, Mzee ShayoΒ alielekea gereza la Segerea haraka sana, alitumia usafiri waΒ pikipiki ambao aliamini asingeliweza kuchelewa walaΒ kudhurika, Watu wachache sana ndio waliokuwa wakifanya safariΒ za hapa na pale ila shughuli zilikuwa zimesimama kabisa,Β ilimchukua takribani dakika 50 kutoka Mikocheni hadi LilipoΒ gereza la Segerea, alikuwa akifahamika hivyo aliingia mojaΒ kwa moja hadi kwa Mkuu wa gereza na kumuuliza kuhusu MzeeΒ Shomari, alichojibiwa kilimchosha sana. Naaam!! Alipewa sasaΒ simulizi ya Mzee Shomari akiwa gerezani hadi alivyotowekaΒ
“Baada ya kufungwa alikaa miezi kadhaa tuu, baadaye kulitokeaΒ uvamizi hapa na hatimaye alitoroshwa ila ilifahamika kuwaΒ baada ya kutoroka aliondoka Nchini na rafiki yake MzunguΒ ambaye alikuwa mfungwa mwenzake wakaelekea Uholanzi” AlielezaΒ Mkuu wa MagerezaΒ
“Shit!” Alisema Mzee Shayo na kukumbuka wakati tukio hiloΒ linatokea yeye alikuwa mapumziko Nchini MorocoΒ
“Asante!” Alisema kisha aliondoka gerezani hapo akiwa naΒ uhakika kuwa maneno ya Faudhia yalikuwa kweli ila alijiulizaΒ sababu hasa ya ugaidi huo ilikuwa nini.Β
Aliondoka hapo kichwa kikiwa kimejaa moto, mzigo mzito waΒ kupambana ulikuwa kichwani pake, Rais alikuwa akimkalia kooniΒ kila wakati asijuwe afanyaje.Β
Upande wa Faudhia alikuwa tayari amerejea ndani ya Jiji laΒ Arusha kuendelea kuutafuta ukweli kuhusu Chogo, alishaambiwaΒ ni Hospitali gani ilitoa gari kwa ajili ya kusafirisha mwiliΒ wa Chogo, gari gani alipata nalo ajali, alifikiria aanzieΒ wapi, aliona ni bora awasiliane na kampuni ya usafirishajiΒ ambayo ilidaiwa gari lao ndio lilipata ajali na kupelekeaΒ kifo cha Chogo, alipfika aliambiwa kampuni hiyo imefungwa kwaΒ muda mrefu. Alikutana na mdada mmoja ambaye alionekana kuwaΒ mfanyakazi wa kampuni hiyo, alijaribu kumbembeleza ili asemeΒ chochote lakini mdada huyo aligoma kabisa, aliona ni boraΒ aondoke.Β
Alipofika kwenye gari, aliketi na kutafakari aingilie wapi,Β alipata wazo la kwenda Hospitalini. Lakini akiwa anawashaΒ gari alitazama Side Mirror aliona kuna Mtu akitoka hapo akiwaΒ na kikaratasi mfano wa tiketi hivi, alishangaa wakatiΒ aliambiwa hakuna huduma katika kampuni hiyo, aliona ni boraΒ azuge anaondoka, Naam! Alisogeza gari na kuificha mahaliΒ kisha alirudi taratibu na kukuta mlango wa kampuniΒ umefunguliwa wote wakati mwanzo ulikuwa umefungwa, kulikuwaΒ na watu kadhaa ambao walikuwa wakitoka hapo, alifikiriaΒ huenda wakawa wateja, alipoona Watu wameisha, aliingia humoΒ kisha haraka alitoa bastola yake na kumuonesha Mdada huyo.Β Faudhia Aligeuza maneno ya kibao kilichoandikwa HUDUMAΒ INAPATIKANA akaweka TUMEFUNGA KWA MUDA.Β
Mdada huyo alionekana kujawa na hofu sana asijuwe anapaswaΒ kufanya nini,Β
“Ulisema huduma zimesitishwa muda sasa lakini kumbe ulikuwaΒ unajuwa unachokifanya si ndiyo?” Mdada aliendelea kutetemekaΒ sanaΒ
“Niambie unafahamu nini kuhusu ajali mbaya ya gari iliyotokeaΒ Miaka iliyopita, unamfahamu vipi Chogo? Ukifanya ujanjaΒ wowote nazibua kichwa chako” Alisema FaudhiaΒ
“Naomba tafadhali usiniuwe nina ndugu ambao wananitegemeaΒ Mimi” Alisema Mdada huyo akiwa analiaΒ
“Kama unataka nisikuuwe basi sema ukweli unafahamu niniΒ kuhusu Chogo na kwanini ulikuwa unaficha jambo?” Aliuliza kwaΒ masistizo Faudhia huku akijuwa fika kuwa eneo hilo halikuwaΒ salama sana kwake, kwa hofu ya kuuawa Mdada alianza kufungukaΒ
“Nitasema kila kitu ila naomba usiniuwe”Β
“Mimi ni Undercover wa kitengo, unapaswa kusema ukweli sababuΒ bila hivyo shingo yako itakuwa halali ya risasi nitakayoΒ ifyatu hapa” Alisema Faudhia kwa msistizo sana.
“Ilikuwa ni siku ya Jumatano, nilikuwa ndiyo kwanza nimeanzaΒ ajira hapa, alikuja Baba Mmoja mlemavu wa mguu, umri wakeΒ ulikuwa umeenda na kusema kuwa anahitaji kuongea na BosiΒ wetu, bahati nzuri Bosi alikuwa ofisini kwake, Baba huyoΒ alionekana kuwa ni Mtu mwenye fedha nyingi. Alienda kwa BosiΒ na sikujuwa kuwa alikuwa anaongea nini na Bosi, baadayeΒ alitoka kisha aliniaga kuwa anaondoka, Baada ya dakika 15Β Bosi alikuja na kuniambia kuwa kuna kijana atakuja kwa ajiliΒ ya kusafiri, nafikiri ndiyo huyo ambaye unamuulizia ila jnaΒ lake siwezi kulikumbuka, aliniambia akija nimuoneshe mahaliΒ pa kwenda kulala, ilikuwa ni ndani ya Ofisi hii kablaΒ haijajengwa upya. Nilichukulia ni jambo la kawaida tuu,Β alipokuja kijana majira ya saa moja usiku nilimkatia tiketiΒ kisha nilimuonesha mahali pa kwenda kulala, inaonesha YuleΒ Baba alkuwa akimfuatilia kijana huyo maana baada ya kijanaΒ huyo kwenda kulala yule Baba alikuja”Β
“Aliniuliza Kijana yupo wapi, nilimuelekeza alipo sababuΒ nilimjuwa Baba huyo baada ya kuja mchana na kuzungumza naΒ Bosi, muda mchache baadaye Bosi naye alikuja kisha aliniulizaΒ alipo kijana nilimueleza alipo, alielekea huko na ukimyaΒ ulitawala, nilianza kusinzia lakini baadaye nilishtuka baadaΒ ya Bosi kuniita na kuniambia kuwa napaswa kuondoka usiku huo,Β nilikuwa na zamu ya kukesha hivyo kuambiwa vile nilifurahiΒ ili nikalale, lakini nilipoangalia vizuri niligundua yuleΒ Baba alikuwa akimsubiria Bosi nje ila alitoka na begi kubwaΒ hivi ambalo hata sikuliona wakati linaingia, nilifunga naΒ kuondoka zangu!!” Alisema Mdada huyo huku akihema juu juu,Β Faudhia alishusha Bastola yake baada ya kugudua sasa alikuwaΒ akiongea ukweli, alijuwa Baba huyo alikuwa ni Mzee Shomari.Β
“Enhee ilikuwaje baada ya hapo?”aliuliza tena FaudhiaΒ
“Baada ya hapo, siku iliyofuata niliambiwa nisiende kaziniΒ ila nitalipwa pesa ya siku kitu ambacho kilizidi kunipaΒ furaha, Mchana kupitia taarifa ya habari nilisikia taarifaΒ kuwa basi la Kampuni yetu lilipata ajali wakati likiwaΒ linafanya safari, Hakuna aliyepona katika ajali hiyo…lakiniΒ Bosi alinisistiza sana nisije nikasema chochote kuhusu yuleΒ Baba kuja usiku na yule kijana” Alisimulia Mdada huyo ambayeΒ alikuwa mnene kiasiΒ
“Sasa usiri wako umepelekea Nchi kuzama kwenye Lindi laΒ Ugaidi wa kutisha, muda siyo mrefu jiji hili litakuwa chiniΒ ya ESS, kama unaweza kuongozana na mimi twende” AlisemaΒ Faudhia akimwambia Mdada huyo ambaye alishapukiaΒ
Alionekana kuchanganikiwa, waliingia kwenye gari kisha gariΒ liliondoka eneo hilo kuelekea yalipokuwa makazi ya Mama yakeΒ Martin Gimbo, miili ya Mama Martin na Mjukuu wake ilishaanzaΒ kutoa harufu humo ndani, Faudhia aliingia kutafuta chochoteΒ kitakachomuwezesha kufukua kaburi hilo ambalo lilisemekanaΒ kuwa ni kaburi la Martin Gimbo.Β
“Naomba unisaidie hapa, tukishamaliza tunaondoka” AlisemaΒ Faudhia kisha alimpatia chepe mdada huyo, walianza kufukuaΒ kaburi hilo. Iliwachukua zaidi ya saa nzima hadi kumaliza,Β chini walikutana na sanduku kubwa ambalo kwa kawaida lilikuwaΒ ni sanduku la kuhifadhia mwili wakati wa kuzika. WalifanikiwaΒ kulivuta juu, wakati huo walianza kusikia milio ya Risasi kwaΒ mbali huku gari za polisi zikiliza ving’ora vyake.Β
Faudhia alianza kuligonga ili lifunguke, bahati nzuri alipataΒ nyundo ndani ya nyumba hiyo kisha alifanikiwa zoezi laΒ kulifungua Sanduku hilo, yule Mdada alitazama pembeni kwaΒ hofu ya kuona mabaki ya mwili wa marehemu Martin Gimbo,Β bahati mbaya ndani ya Sanduku hilo kulikuwa na brifkesi ndogoΒ na siyo mifupa wala mabaki ya mwili wa Martin GimboΒ
“Yes! Martin Gimbo ndiye Chogo” Alisema Faudhia hukuΒ akimtazama Mdada huyo ambaye hakulijuwa hata jina lake.Β Alilichukua Brifkesi hilo lakini hata kabla hawajapiga hatuaΒ hata moja, Faudhia alisindikizwa chini na teke kaliΒ lililopigwa kwa ustadi wa hali ya juu, ghafla alihisi ganziΒ mkono wa kulia, aliliachia brifkesi hilo huku akiwa anaangukaΒ chini, Sanduku lilidakwaΒ
Faudhia alishangaa namna upigaji wa teke hilo ulivyotumiaΒ akili na ustadi wa hali ya juu sana, aligeuka kumtazamaΒ aliyekuwa amempiga teke hilo, alikutana na sura aliyoifahamu.Β Naaam! Alikuwa ni rafiki yake wa zamani Diana, Diana alikuwaΒ ndani ya Koti jeusi, sketi nyeusi, pia alikuwa amevalia wigiΒ jeusi.Β
“Diana ni wewe?” Alihoji Faudhia, hakutegemea kukutana naΒ Diana katika nyakati hizo, aliona kama yupo ndotoni japoΒ alishatumiwa picha ya Miongoni mwa Watu waliokuwa wakiendeshaΒ ugaidi Tanzania.Β
Faudhia alijivuta na kusimama japo kwa maumivu makali, tekeΒ alilopigwa lilimfanya ahisi kizunguzungu.Β
“Umewezeje?” Aliuliza FaudhiaΒ
“Kwasababu nimekusubiria kwa zaidi ya miaka 7 Faudhia,Β nimekusubiri kwa lengo moja tu la kukupeleka kuzimu” AlisemaΒ Diana kisha aliweka Brifkesi pembeni, yule Mdada alivyoonaΒ hivyo alikimbia eneo hilo sababu alijuwa kuna hatari kubwaΒ inaenda kutokea hapo muda mchache ujao.
“Ulinisubiria unipeleke kuzimu?” Alihoji Faudhia “Ndiyo! Kwasababu ulimuuwa Mama yangu” alisema DianaΒ
“Diana itakuwa umekosea njia, mimi nimemuuwa Mama yako? InaΒ maana nawe umeingia kwenye mtego wa Mzee Shomari? DianaΒ mnatumika na huyo Mzee ili atimize lengo lake, nisikilizeΒ rafiki yangu!! Mimi sikuuwa Mama yako bali yeye Mzee ShomariΒ ndiye aliyefanya hivyo na hiyo ndiyo sababu ya yeye kukaaΒ jela, amka kutoka usingizini Diana” Alisema FaudhiaΒ
“Leo tutaona Faudhia kati yangu Mimi na wewe nani yupoΒ Usingizini, Ukifa naondoka na Brifkesi, nikifa unaondoka naΒ Brifkesi” Alisema Diana huku akijiandaa kupambana na FaudhiaΒ
“Diana hebu nisikilize, hujapoteza kila kitu katika MaishaΒ yako, una muda wa kubadilisha kila kitu, ungana na MimiΒ tumdhibiti Mzee Shomari” Alisema Faudhia, maneno ya FaudhiaΒ hayakubadilisha Chochote, Diana alikaa mkao wa kuanzaΒ kumshambulia Faudhia. Alianza kumfuata Faudhia kama SimbaΒ mwenye njaa huku Faudhia akiwa anarudi nyuma ili afikirieΒ namna ya kumzuia Diana.Β
Faudhia aligundua haraka kuwa Diana alikuwa anatumia piganoΒ maarufu nchini China linaloitwa Wing Chun, alijuwa sasa kumbeΒ Diana alikuwa na taaluma ya mapigano ya Martial artsΒ
Alipomfikia alitua kwenye mapaja ya Faudhia kisha alijirushaΒ na kumzunguka kwa nyuma kisha aligusa mfupa hadimu sana nyumaΒ ya mgongo wa Faudhia, kilikuwa ni kitendo cha haraka sana,Β Faudhia alihisi kukatika kwenye uti wa mgongo ila alijikazaΒ asianguke, alifanya haraka na kumgeukia Diana kishaΒ alijipanga kupambana naye, alimwambiaΒ
“Acha Diana, Acha unachofanya kumbuka sisi ni marafiki”Β Alisema FaudhiaΒ
“Ningekuwa rafiki yako usingelithubutu kuniulia Mama yangu,Β alikukosea nini yule?” Alisema Diana huku akionekana kuzidiΒ kujawa na hasira, alijiandaa tena kumpa pigo lingine la WingΒ Chun…Faudhia alijitahidi kuisoma mikimbio ya Diana ambayoΒ ilikuwa ya haraka mno.Β
Alifanya kama vile anamkimbia, alimpa mgongo kisha alipohisiΒ Diana yupo nyuma karibu na kumnasa alimchumpa na kugusa mguuΒ mmoja kwenye mti kisha alijipindua na kukutana na DianaΒ ambaye hakutegemea kama Faudhia angejifyetua kisha FaudhiaΒ alimpa teke la Maana Diana, alisogezwa pembeni huku akitemaΒ damu, ilizidi kumpa hasira, alimfuata tena na kufanyaΒ mpambano huo uzidi kuwa mtamu. Ilikuwa ni vita kati yaΒ marafiki wawili waliogeuka kuwa maadui, ndipoΒ walipothibitisha kuwa kuna Msitari mwembamba sana kati yaΒ Upendo na chuki.Β
Ulikuwa ni mpambano mkali sana, vita ya kurushiana ngumiΒ ilitanda, Ilikuwa kama vile walikuwa wakipeana zamu, dakikaΒ tatu kwa Faudhia na dakika tatu kwa Diana. Wakati wanapiganaΒ lile Brifkesi lilikuwa pembeni, Faudhia hakujuwa kulikuwa naΒ jambo gani ndani ya Bridkesi hilo jeusi.Β
Jua lilikuwa likiendelea kuwaka kwa ukali wake. Kutokana naΒ ile sumu ambayo iliingizwa mwilini mwake na Mohd japoΒ alijitahidi kuizuia kwa kujichoma sindano ila ilianzaΒ kumletea shida alianza kutokwa jasho, ndio muda ambao DianaΒ aliutumia kumfanyia kitu mbaya Faudhia.Β
Alipeleka ngumi zaidi ya 10 mfululizo, Faudhia alijitahidiΒ kadiri ya uwezo wake kuzipangua lakini hakuwa na nguvu yaΒ kuzipangua zote alijikuta akiruhusu mwili wake kukutana naΒ ngumi nzito za Diana, alijikutana akishuka chini na kupigaΒ magoti, Diana alilichukua lile brifkesi kisha alimwambiaΒ FaudhiaΒ
“Onja uchungu wa kifo ambao ulimpatia Mama yangu” AlichomoaΒ sindano ili aweze kumchoma FaudhiaΒ
“Diana! Umesahau kila kitu? Kumbuka wewe ni nani, MzeeΒ Shomari anakutumia” Alisema Faudhia japo kwa shida sana hukuΒ akihisi kizunguzungu, Diana alitoa kichupa kidogo kishaΒ alifyonza sumu kwa kutumia sindanoΒ
“Niliwahi kusimuliwa kuwa Mtu anayekaribia kufa huwa naΒ majuto sana ila nakushangaa wewe Faudhia bado unakaidi kuwaΒ hukumuuwa Mama yangu” Diana alimsongelea Faudhia, alimshikaΒ nywele na kupindisha shingo kisha alimchoma sindano, kablaΒ hajaruhusu sumu iweze kusambaa mwilini mwa Faudhia, alipigwaΒ na kitu kizito kichwani, Diana alishindwa kumalizia zoezi,Β alijitahidi kugeuka lakini alishindwa alijikuta akiangukaΒ chini na kupoteza fahamu. Nyuma yake alisimama yule MdadaΒ ambaye alimpa taarifa ya ajali ya Basi, Naam! NdiyeΒ aliyempiga na kitu kizito Diana.Β
Faudhia alimwambia Mdada huyo kuwaΒ
“Chukua Brifkesi tuondoke hapa, si unajuwa kuendesha gari?”Β AliulizaΒ
“Ndio najuwa”
“Tuondoke hapa haraka sana” Alisema Faudhia, hakutakaΒ kummaliza Diana siku hiyo sababu licha ya uadui badoΒ alimtambuwa Diana kama rafiki yake, yule Mdada alimsaidiaΒ Faudhia kuingia kwenye gari walilokuja nalo, Milio ya risasiΒ ilitanda kila kona ya Jiji la Arusha, isingelikuwa salama kwaΒ Faudhia kuendelea kukaa hapoΒ
“Tunaenda wapi?” Alihoji mdada akiwa anaingia barabara kuuΒ
“Dar-es-salaam” Alisema Faudhia huku akilifungua BrifkesiΒ hilo ili ajuwe ndani yake kulikuwa na nini na kwaniniΒ lilizikwa.Β
β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’Β
Jina la Selina lilifika mikononi mwa Chogo, aliambiwa kuwaΒ ndiye anayefahamu ilipo chemba ya siri iliyohifadhi kiasiΒ kikubwa cha pesa, Chogo alitoka kwenye moja ya Chumba baadaΒ ya kumaliza kuzungumza na Mzee Shomari na kupewa taarifa hiyoΒ kuwa kuna Mwanamke anaitwa Selina na yupo ndani ya Benki,Β yeye pekee ndiye anayefahamu ilipo chemba ya siri. ChogoΒ alitoka akiwa ameshikilia Bunduki aina ya AK47Β
Mateka walikuwa wamekaa chini kando ya sehemu ya Mapokezi,Β alipofika aliulizaΒ
“Selina ni nani?” Ilikuwa ni sauti iliyojaa mamlaka sana,Β aliuliza kwa kumaanisha kuwa alikuwa akimuhitaji Mdada huyo.Β Selina mwenyewe aliposikia hivyo alijuwa ni kitu gani MagaidiΒ hao walikuwa wakihitaji, baadhi ya Magaidi sura zaoΒ walizificha Ila baadhi hawakuzificha akiweno Chogo ambayeΒ waliamini hawezi kutambulika kwa urahisi.Β
“Selina ni nani?” Aliuliza tena Chogo kisha aliiandaa bundukiΒ kwa lengo la kuleta kitishoΒ
“Mimi hapa” alijitokeza huyo aliyeitwa Selina akiwa amevaliaΒ sare za wafanyakazi wa Benki, alikuwa Mwanamke mmoja mzuriΒ mweusi mwenye rasta asilia.Β
“Mleteni” Alisema Chogo, mara moja Selina alisogezwa mahaliΒ aliposimama Chogo, Selina alionekana kuwa muoga sana, ChogoΒ alimwambia SelinaΒ
“Usiogope sababu una kazi moja tu ya kufanya, ukishamalizaΒ nitakuacha huru sawa?” Alisema akiwa anatabasamu, SelinaΒ aliitikia kwa woga kisha Chogo alisema
“Tuongozane” Alimpa ishara Selina amfuate kwenye moja yaΒ chumba.Β
Nje ya Benki polisi walizingira benki hiyo wakiwa na silahaΒ za moto huku wakiwa na tahadhari kubwa, walikuwa wakitumiaΒ kipaza sauti kuzungumza, Chogo alipofika Chumbani na SelinaΒ alimwambiaΒ
“Nisubirie hapa, naenda kuongea na polisi” Alisema kishaΒ alichukua AK47 na kuelekea nje ya Benki hiyo.Β
Kitendo cha Chogo kutoka nje ya Benki kilileta utayari kwaΒ polisi na vitengo vyote vilivyokuwa makini na Benki, ChogoΒ alitoka akiwa hajavaa shati, mwili wali wake ulijaa michoroΒ mingi, alionekana kujiamini sana huku polisi wakiambiana kuwaΒ wanapaswa kumsikiliza sababu alikuwa na mateka ndani ya BenkiΒ
Chogo alisimama katikati ya Barabara iliyotoka kivukoniΒ kwenda mjini kisha aliwauliza polisiΒ
“Mlitaka nitoke ndani, nimeshatoka, mlikuwa mnasemaje?”Β Aliuliza kwa ujasiri, kipaza sauti kilisikikaΒ
“Kwanza tunahitaji usalama wa mateka wote walio ndani yaΒ Benki, pili tunataka kujuwa mnahitaji nini?”Β
“Oooh! Siwezi kuuwa Raia ambao hawana kosa lolote, ilaΒ mkileta ujanja nitauwa kila Mtu ndani ya Benki, masaa 24Β yajayo nitaiachia Benki hii” Alisema Chogo kisha alirudiΒ ndani ya Benki, hakuna askari hata mmoja aliyejaribuΒ kumshambulia Chogo, moja kwa moja alienda kwenye kile chumbaΒ alichomuacha Selina, aliweka Bunduki pembeni kisha alifungaΒ mlango, Chogo alimtazama Selina kwa jicho la kumtamani sanaΒ ukizingatia sketi ya Selina ilikuwa imepasuka kidogo hivyoΒ paja lilikuwa njeΒ
Selina alikuwa mwingi wa kutetemeka, Chogo alimfuata SelinaΒ kisha alimtandika busu, alimshika matiti na Makalio, alimvuaΒ nguo Selina na kumbaka, baada ya kumaliza alimwambia SelinaΒ
“Kama lilivyo tamu penzi lako, basi nahitaji uniambie wapiΒ ilipo chemba ya siri iliyohifadhi pesa za Kimarekani” AlisemaΒ Chogo akiwa anavaa nguo zake, alipomaliza alikuwa badoΒ hajapata jibu kutoka kwa Selina ambaye alikuwa akitetemekaΒ kwa wogaΒ
“Ukimya wako unaashiria kuwa ni bora ufe kuliko kusema ilipoΒ Chemba si ndiyo?” Aliuliza tena Chogo, safari hiiΒ alibadilisha sura yake na kujaza hasira
“Tafadhali usiniuwe, ipo chumba namba 43” Alisema SelinaΒ
LEO NIMEWEKA NDEFU SANA COMMENTS ZIKIWA CHACHE NARUDI KWENYE KUWEKA FUPI
Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA SABA
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa HapaΒ
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896Β
27 Comments
Leo kwel ni ndefu had nimefulai
Hongera
Nimeipenda
Haha admini usitunyanyase ww weka unay0jiskia fupi au ndefu ss tunas0ma t π
Leo Kweli Nimefrahia Saana Kuusoma Hii Story
Hongera san ni nzur na ya kuvutia unasoma lkin kam vile ni video ipo mbele yko unaiagaliaπ―
Hongera ndefu alafu tamu
Asante sana leo ndefu
Nzuri sana
Ndo kusema chogo alikua na ugwaduπ€£π€£π€£π€£
Nzur sana boss leo mzigo wa uhakika
Leo imefika mahala pake..
Mashaallah asante
Imekaa pouuuwaa
Aah Admin we nouma ,, Leo ndefu Hadi Rahaπͺ
Apo sawa admin π₯π₯
nzuri san
Ya Leo imekuwa ndefu pia nzuri..Bigup Sana Admin
Aisee kuipata yote tunabonyeza ngapi mkuuπ π π β οΈ
Story nzuri inavutia sana inanifanya kila saaa niwe naingia kwenye kundi kuitafta jitahdi luifanya iwe ndefu pia itoke kwa wakati
Mbona ya Saba hutoi Admin sio poa bwana
Tumesubir sana huweki
nzuri sana
7x51ai
Tamu na ndefu hadi raha
cgnsok
Good ππ