Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tano-05)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)
    Hadithi

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJune 3, 2025Updated:June 4, 202524 Comments21 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nneย 

    “Assssh” aligumia Faudhia kutokana na maumivu ya kujigongaย  kwenye meza, Mohd hakutaka kusubiri alimrushia ngumiย  mfululizo, ngumi ambazo zilimpekeka Fuadhia ukutani, bahatiย  mbaya ngumi nyingi zilimpata na kumfanya aumie usoniย 

    Mohd alimpiga Faudhia mateke mfululizo eneo la mbavu hukuย  akimwambiaย 

    “Unakufa leo” Alisema huku akiwa anamuangalia Faudhia akiwaย  anaanguka chini. Endelea

    SEHEMU YA SITA

    Mohd alimsindikiza Faudhia kwa teke kali lililomzimishaย  Faudhia, Mohd alitoa kifaa kidogo ambacho kilikuwa na sindanoย  ya sumu ndani yake, aliitoa kisha alimkita Faudhia eneo laย  shingo.ย 

    Baada ya kuhakikisha amemdunga alielekea Kuvuta kochi kishaย  aliitafuta simu yake ambayo ndiyo ilikuwa muhimu sana kishaย  Bastola yake ambayo ingekuja kuwa ushahidi pale, aliichukuaย  Bastola na simu kisha aliondoka eneo hilo.ย 

    Sekunde kumi na tano baadaye sindano ya sumu ilianza kufanyaย  kazi yake, Faudhia alishtuka huku akiwa anateswa na sumuย  ambayo ilikuwa ikisambaa kwa kasi mwilini, alijikuta akianzaย  kuishiwa nguvu, alijivuta kisha alifungua kibegi chake kidogoย  alitoa sindano, alivuta dawa haraka kutoka kwenye chupaย  kidogo kisha alijidunga sindano akiwa anavuja damu, kishaย  alianguka chini na kuzima.ย 

    Usiku huo, Mzee Shomari alikuwa akisubiria simu ya Mohd iliย  kumpa taarifa ya kifo cha Faudhia. Alikuwa kwnye kiti chaย  walemavu akitembea sebleni ndani ya Jengo la China plazaย  jengo ambalo walilifanya kuwa makao yao ya siri walipoanzaย  kupanga mipango ya Kigaidi, jengo hilo lilikuwa la rafikiย  yake aliyeko Uholanzi ambaye ndiye aliyekuwa anafadhiliย  ugaidi.ย 

    Alianza kukumbuka miaka mingi iliyopita katika Jiji la Mbeya.ย 

    Siku ambayo alikamatwa Baada ya kumuuwa Mama yake Diana,ย  alimtazama kwa hasira sana Faudhia, alijenga chuki na kisasiย  kwa Faudhia. Mzee Shomari alipelekwa Kituo cha polisi,ย  alipewa mateso makali sana ikiwemo kuwekwa kwenye beseniย  lenye maji na kukosa pumzi, alikumbuka jinsi alivyopigwa hadiย  kuvunjwa mguu na ndiyo sababu ya yeye kuwa mlamavu ndiyoย  maana anatembea kwenye kiti cha walemavu.ย 

    Alipelekwa mahakamani baada ya kupata matibabu ya mguu kishaย  alihukumiwa kifungo cha Maisha jela, alipofika huko alikutanaย  na mzungu aliyeitwa Damian, alijenga urafiki na Mzungu huyoย  ambaye alikuwa na kesi ya kusafirisha madini kinyume chaย  sheria kutoka Tanzania kwenda Thailand, walishibana wakiwaย  gerezani.ย 

    Akiwa anaendelea kuwaza kilichotokea baada ya kufungwa, simuย  ya Mzee Shomari iliita alipopokea alisikia sauti ya Mohdย  ikimwambiaย 

    “Faudhia ni damu baridi” Alisema akiwa na maana kuwaย  ameshamuuwa, Mzee Shomari alishangaa sana kwa jinsi ambavyoย  alimuuwa Faudhia kisha alimuuliza

    “Upo wapi?”ย 

    “Nipo njiani narudi Dar” Alisema Mohdย 

    “Tukio lilikuwaje?” Alihoji Mzee Shomari kwa unakini mkubwaย  huku akionekana alikuwa mwenye akili sanaย 

    Mohd alimsimulia Mzee Shomari tukio lilivyotokea kisha Mzeeย  Shomari alisemaย 

    “Ukifika Chalinze utaona kuna prado nyeusi, itumie” Alisemaย  Mzee Shomari kisha alikata simu. Alisogea na kutazama chini,ย  aliliona namna jiji la Dar lilivyokuwa likiwaka taa hukuย  barabara ya kutoka Karume kwenda Kariakoo ikiwa nyeupe hakunaย  Mtu wala gariย 

    Alinyanyua simu yake akapiga simu mahali kisha akasemaย 

    “Case Clossed ( Kesi imeisha ) ” alikata simu akajisukuma naย  kuingia kwenye chumba kingine.ย 

    Masaa matano baadaye Mohd alifika Chalinze usiku sana akiwaย  na gari yake aina ya Toyota V8, mji ulikuwa kimya kabisa,ย  alilliona Prado likiwa linawasha hazard kuashiria kuwaย  lilikuwa ndiyo gari ambalo Mohd alitakiwa kulitumia, harakaย  alishuka na kulielekea gari hilo, alipoingia aliangaza ndaniย  ya gari hilo ili kuona kama kulikuwa na Mtu lakini gari hiloย  halikuwa na Mtu, alivuta funguo na kuiwasha, kitendo chaย  kuwasha tu gari hilo lililipuka, Mohd alifia ndani ya gariย  hilo, pembezoni kulikuwa na roli, ndani ya Roli kulikuwa naย  Mtu ambaye alisikika akiongea na simu akisemaย 

    “Target eliminated ( Mlengwa amemalizwa )” kisha roli hiloย  liliwashwa na kueleka Upande wa morogoro.ย 

    Siku iliyofuata, Chogo alipewa kazi na Mzee Shomari yaย  kuhakikisha anaifahamu ilipo chemba ya siri ambayo pesa hizoย  za Kimarekani zilikuwa zimehifadhiwa, Mtu pekee ambayeย  alidhaniwa kuwa anajuwa ilipo alikuwa ni Gavana wa Benkiย  hiyo. Pesa ambazo akina Chogo walikuwa wanazitaka zilikuwa niย  pesa za siri ambazo Tanzania iliyauzia madini Nchi ya Saudiย  Arabia. Chogo alirudi ndani ya chumba ambacho Gavanaย  alikuwemo na Mke wake, alikuwa ameweka rehani maisha ya mmojaย  wa wafanyakazi wa Benki hiyo ili Gavana aseme mahali ambapoย  pesa hizo zilikuwa zimehifadhiwa.ย 

    Gavana alimuuliza Chogo amajuwaje kama ndani ya Benki kunaย  pesa za siri ambazo zilitokana na mauzo ya madini

    “Acha kuuliza maswali ambayo kamwe hutoweza kupata majibuย  yake, sema ilipo chemba ya siri vinginevyo namuuwa huyu!!”ย  Alisema Chogo huku Bastola ikiwa kichwani kwa Mfanyakazi huyoย 

    Gavana alikaa kimya hakuonekana kumtetea Mfanyakazi asiuawe,ย  alimtazama Mke wake kisha alirudisha macho kwa chogo.ย 

    “Umejuwaje?” Aliuliza tena kwa mshangao mkubwa sana, Chogoย  alionekana kuwa ni Mtu katili mwenye hasira sana, alimpigaย  risasi mfanyakazi kisha akamwambia Gavanaย 

    “Nakupa masaa matatu uoneshe ilipo chemba ya siri” Chogoย  alisema kisha aliondoka ndani ya chumba hicho.ย 

    Upande wa pili, Mzee Shayo alianza kuingiwa na wasiwasiย  kuhusu vijana wake wawili aliowatumainia, simu ya Mohdย  haikupatikana baada ya kuuawa ndani ya gari, simu ya Faudhiaย  iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa, ilimpa mashaka juu yaย  usalama wao, alijitahidi sana kupiga simu lakini simu yakeย  haikuweza kumpa majibu ya nini kilichokuwa kimetokea hukoย  Arusha kwenye operesheni ya kujuwa kuhusu Chogo, alitumaย  Askari wengine wa Kitengo kuelekea Arusha kwa ajili yaย  kuwatafuta Mohd na Faudhia.ย 

    Punde alipokea simu ya Rais iliyomtaka aende Ikulu harakaย  sana, kutoka Kigamboni yalipo makao makuu ya Kitengo cha siriย  cha Usalama wa Taifa ilimchukua dakika kadhaa, tayali hali yaย  tahadhari ilitangazwa hivyo hakukutakiwa Mtu yeyote kutokaย  ndani, Jiji lilikuwa kimya sana kama makazi yaliyotelekezwa,ย  Mzee Shayo alifika hadi Ikulu kisha alienda kwenye chumba chaย  siri ambacho Rais na Waziri Mkuu walikuwa wamehifadhiwa.ย 

    Rais alihitaji kujuwa Mzee Shayo alifikia wapi katikaย  harakati za kupambana na Kikosi hicho cha Kigaidi, waliketiย  watu watatu na kuanza kuzungumza, Mzee Shayo alimwambia Raisย  kuwa ametuma vijana kuelekea Arusha mbako inaaminika kuwaย  Gaidi namba moja aliyeiteka Benki kuu anatokea hukoย 

    “Huo ni ujinga Shayo! Unafuatilia historia ya Mtu badala yaย  kupambana naye sasa hivi, hadi umalize kuijuwa historia yakeย  pengine gaidi atakuwa amemaliza kazi yake na kuondoka Nchini.ย  Benki ipo chini yao Shayo, historia histori historiaย  itasaidia nini?” Aliuliza Rais akionekana kuwa mwenye hasiraย 

    “Mkuu kila jambo linahitaji taaluma katika utendaji, kabla yaย  kutatua tatizo ni lazima tuangalie lilipoanzia itatusaidiaย  kujuwa ukubwa wake!” Alijitetea Mzee Shayo

    “Hivi kweli ulistahili kuwa Mkuu wa Kitengo cha Usalama waย  Taifa? Magaidi wamechukua silaha Lugalo na makambi mengine,ย  tayari Nchi hii imekuwa kisiwa cha vita unayajuwa madharaย  yake? Kiasi kikubwa vita hii utapigana wewe na vijana wako,ย  jeshi lipo katika hali ngumu ya kujinasua” Alisema Rais hukuย  akionekana kuanza kususa mazungumzo hayo, Waziri Mkuuย  akamwambia Mzee Shayoย 

    “Kuna hazina kubwa sana pale Benki pengine ndiyo sababu yaย  Ugaidi huu, hakikisha unafaulu Shayo, vinginevyoย  hatutokuelewa” Alisema Waziri Mkuu kisha Mzee Shayoย  alinyanyuka na kuaga, alipoondoka Rais alimuuliza Waziri Mkuuย 

    “Nani anajuwa ilipo chemba iliyohifadhiwa pesa?” Aliulizaย  akiwa makini sanaย 

    “Kuna Mdada wa pale Benki anaitwa Selina, yeye bahati mbayaย  yupo ndani ya Benki na ameshikiliwa kama watafanikiwaย  kumtambuwa basi mpango wote utavurugika” Alisema Waziri Mkuuย  na kumpa muda wa kutafakari Raisย 

    “Una hakika Gavana hajui chochote?” Aliuliza Raisย 

    “Gavana anajuwa kuhusu pesa iliyohifadhiwa Benki ila hajuiย  iliwekwa wapi sababu mpango ulifanywa kuwa siri kamaย  ulivyoagizwa”. Alijibu Waziri Mkuuย 

    “Nina uhakika hawawezi kuchukua pesa za Kitanzania watahitajiย  zile Dola, hili jambo sitaki lifahamike popote na kamaย  itatokea Mtu amejuwa basi katisha Maisha yake” Aliagiza Raisย 

    Naaam!! Mzee Shayo alipotoka Ikulu alihitaji kwendaย  kutembelea makazi yake yaliyopo Mikocheni B, alikuwaย  akitembea kwa siri sana hadi alipofika, Kisha aliingia kwenyeย  chumba ambacho alikuwa akikitumia kufanya kazi zake, aliketiย  ili kujipa utulivu huku akifikiria afanye nini.ย 

    โ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขย 

    Nje kidogo ya Jiji la Arusha, kulionekana gari moja nyeusiย  aina ya prado ikiwa imeacha barabara na kukita kwenye Mtiย 

    Tukio hilo lilionekana kutokea muda mrefu uliopita kutokanaย  na ukimya ambao ulikuwepo, ndani ya gari hiyo alikuwemoย  Faudhia akiwa ameegemea usukani, alikurupuka kama Mzimuย  kutoka kifo.ย 

    “Uhhhh” alisikia maumivu makali ya kichwa, alionekana kuchokaย  sana, alifungua mlango na kutoka ndani ya gari, alijivutaย hadi chini ya Mti, aliitoa simu yake kisha aliiangaliaย  alikuwa ametafutwa na Nani, aliona ni Mkuu wa Kitengo alikuwaย  amempigia zaidi ya mara 40, alimpigia Mkuu huyoย 

    “Aah Baba!!” Alisema Faudhia akionekana kuwa na maumivuย  makali kisha alikohoa na kuanza kumtia hofu Mzee Shayoย 

    “Faudhia upo sawa?” Alihoji Mzee Shayoย 

    “Nilichungulia mlango wa kuzimu lakini bahati nzuri mafunzoย  yamenisaidia kujinasua” Alisema Faudhiaย 

    “Mohd yuko wapi?” Alihoji Mzee Shayoย 

    “Baba!! Mohd ndiye aliyetaka kunipeleka kuzimu, nimeshtukaย  anafanya kazi upande wa Magaidi, anatumika upande huo naย  sijui ametumika kwa muda gani, alipewa agizo la kunimaliza”ย  Alisema Faudhiaย 

    “What? ( Nini? )” aliuliza kwa mshituko sana Mzee Shayo.ย 

    “Ndio…alafu, Mhusika Mkuu wa ugaidi ni Mzee Shomari”ย  Alisema Faudhia na kumuacha kinywa wazi Mzee Shayoย 

    “Una uhakika na maneno yako Faudhia? Mzee Shomari si yupoย  gerezani?” Aliuliza Mzee Shayo,ย 

    “Hapana, nina uhakika na ninachozungumza na yeye ndiyeย  aliyetoa maagizo ya kuuawa kwangu, nahisi ni yeye ndiyeย  aliyehitaji kunimaliza kabla sijavuka mpaka wa Namanga”ย  Alisema Faudhiaย 

    “Shit!! Sasa kwanini wametumia nguvu kubwa ya kuzuia habariย  za Chogo ikiwa gaidi namba moja ni Mzee Shomari?” Aliulizaย  Mzee Shayoย 

    “Kuna mtego mahali, inavyoonekana kuna mchezo unachezwa hapaย  Baba” Alisema Faudhiaย 

    “Upo wapi kwa sasa?” Alihoji Mzee Shayoย 

    “Nipo nje kidogo ya Jiji la Arusha, jiji hili si salama tenaย  Kwasasa”ย 

    “Sikia Faudhia, ni lazima umalize hiyo kazi, fuatilia ujuweย  ni kwanini Chogo anafichwa, kuna ufunguo wa hili jambo katikaย  Maisha ya Chogo, hujapata fununu yoyote?”

    “Tulionana na Mama yake Chogo, alisema Mwanaye alifarikiย  Miaka mingi kwa ajali ya gari na alituonesha na kaburi lake,ย  lakini pia alituonesha picha ya Mtu aliyeleta Maiti ya Chogoย  alikuwa ni Mzee Shomari” Alisema Faudhiaย 

    “Hapo kuna taarifa juu ya taarifa, tukio juu ya Tukio, hiyoย  picha iliyopigwa Mzee Shomari alikuwa katika pozi lipi?”ย  Aliuliza Mzee Shayo akiwa nyumbani kwake Mikocheniย 

    “Ilionekana ni picha iliyopigwa bila Mzee Shomari kujiandaa,ย  alikuwa akiongea na Mtu mwingine”ย 

    “Yes! Yes! Rudi Arusha haraka sana Faudhia, hakikishaย  unafahamu stori nzima, naelekea gerezani kujuwa kuhusuย  taarifa ya Mzee Shomari”ย 

    “Sawa Baba” Alisema Faudhia kisha alikata simu, alishushaย  pumzi zake, alikuwa na kazi nzito iliyojaa hatari mbele yake.ย 

    Waligawana majukumu, Faudhia alirudi Arusha, Mzee Shayoย  alielekea gereza la Segerea haraka sana, alitumia usafiri waย  pikipiki ambao aliamini asingeliweza kuchelewa walaย  kudhurika, Watu wachache sana ndio waliokuwa wakifanya safariย  za hapa na pale ila shughuli zilikuwa zimesimama kabisa,ย  ilimchukua takribani dakika 50 kutoka Mikocheni hadi Lilipoย  gereza la Segerea, alikuwa akifahamika hivyo aliingia mojaย  kwa moja hadi kwa Mkuu wa gereza na kumuuliza kuhusu Mzeeย  Shomari, alichojibiwa kilimchosha sana. Naaam!! Alipewa sasaย  simulizi ya Mzee Shomari akiwa gerezani hadi alivyotowekaย 

    “Baada ya kufungwa alikaa miezi kadhaa tuu, baadaye kulitokeaย  uvamizi hapa na hatimaye alitoroshwa ila ilifahamika kuwaย  baada ya kutoroka aliondoka Nchini na rafiki yake Mzunguย  ambaye alikuwa mfungwa mwenzake wakaelekea Uholanzi” Alielezaย  Mkuu wa Magerezaย 

    “Shit!” Alisema Mzee Shayo na kukumbuka wakati tukio hiloย  linatokea yeye alikuwa mapumziko Nchini Morocoย 

    “Asante!” Alisema kisha aliondoka gerezani hapo akiwa naย  uhakika kuwa maneno ya Faudhia yalikuwa kweli ila alijiulizaย  sababu hasa ya ugaidi huo ilikuwa nini.ย 

    Aliondoka hapo kichwa kikiwa kimejaa moto, mzigo mzito waย  kupambana ulikuwa kichwani pake, Rais alikuwa akimkalia kooniย  kila wakati asijuwe afanyaje.ย 

    Upande wa Faudhia alikuwa tayari amerejea ndani ya Jiji laย  Arusha kuendelea kuutafuta ukweli kuhusu Chogo, alishaambiwaย ni Hospitali gani ilitoa gari kwa ajili ya kusafirisha mwiliย  wa Chogo, gari gani alipata nalo ajali, alifikiria aanzieย  wapi, aliona ni bora awasiliane na kampuni ya usafirishajiย  ambayo ilidaiwa gari lao ndio lilipata ajali na kupelekeaย  kifo cha Chogo, alipfika aliambiwa kampuni hiyo imefungwa kwaย  muda mrefu. Alikutana na mdada mmoja ambaye alionekana kuwaย  mfanyakazi wa kampuni hiyo, alijaribu kumbembeleza ili asemeย  chochote lakini mdada huyo aligoma kabisa, aliona ni boraย  aondoke.ย 

    Alipofika kwenye gari, aliketi na kutafakari aingilie wapi,ย  alipata wazo la kwenda Hospitalini. Lakini akiwa anawashaย  gari alitazama Side Mirror aliona kuna Mtu akitoka hapo akiwaย  na kikaratasi mfano wa tiketi hivi, alishangaa wakatiย  aliambiwa hakuna huduma katika kampuni hiyo, aliona ni boraย  azuge anaondoka, Naam! Alisogeza gari na kuificha mahaliย  kisha alirudi taratibu na kukuta mlango wa kampuniย  umefunguliwa wote wakati mwanzo ulikuwa umefungwa, kulikuwaย  na watu kadhaa ambao walikuwa wakitoka hapo, alifikiriaย  huenda wakawa wateja, alipoona Watu wameisha, aliingia humoย  kisha haraka alitoa bastola yake na kumuonesha Mdada huyo.ย  Faudhia Aligeuza maneno ya kibao kilichoandikwa HUDUMAย  INAPATIKANA akaweka TUMEFUNGA KWA MUDA.ย 

    Mdada huyo alionekana kujawa na hofu sana asijuwe anapaswaย  kufanya nini,ย 

    “Ulisema huduma zimesitishwa muda sasa lakini kumbe ulikuwaย  unajuwa unachokifanya si ndiyo?” Mdada aliendelea kutetemekaย  sanaย 

    “Niambie unafahamu nini kuhusu ajali mbaya ya gari iliyotokeaย  Miaka iliyopita, unamfahamu vipi Chogo? Ukifanya ujanjaย  wowote nazibua kichwa chako” Alisema Faudhiaย 

    “Naomba tafadhali usiniuwe nina ndugu ambao wananitegemeaย  Mimi” Alisema Mdada huyo akiwa analiaย 

    “Kama unataka nisikuuwe basi sema ukweli unafahamu niniย  kuhusu Chogo na kwanini ulikuwa unaficha jambo?” Aliuliza kwaย  masistizo Faudhia huku akijuwa fika kuwa eneo hilo halikuwaย  salama sana kwake, kwa hofu ya kuuawa Mdada alianza kufungukaย 

    “Nitasema kila kitu ila naomba usiniuwe”ย 

    “Mimi ni Undercover wa kitengo, unapaswa kusema ukweli sababuย  bila hivyo shingo yako itakuwa halali ya risasi nitakayoย  ifyatu hapa” Alisema Faudhia kwa msistizo sana.

    “Ilikuwa ni siku ya Jumatano, nilikuwa ndiyo kwanza nimeanzaย  ajira hapa, alikuja Baba Mmoja mlemavu wa mguu, umri wakeย  ulikuwa umeenda na kusema kuwa anahitaji kuongea na Bosiย  wetu, bahati nzuri Bosi alikuwa ofisini kwake, Baba huyoย  alionekana kuwa ni Mtu mwenye fedha nyingi. Alienda kwa Bosiย  na sikujuwa kuwa alikuwa anaongea nini na Bosi, baadayeย  alitoka kisha aliniaga kuwa anaondoka, Baada ya dakika 15ย  Bosi alikuja na kuniambia kuwa kuna kijana atakuja kwa ajiliย  ya kusafiri, nafikiri ndiyo huyo ambaye unamuulizia ila jnaย  lake siwezi kulikumbuka, aliniambia akija nimuoneshe mahaliย  pa kwenda kulala, ilikuwa ni ndani ya Ofisi hii kablaย  haijajengwa upya. Nilichukulia ni jambo la kawaida tuu,ย  alipokuja kijana majira ya saa moja usiku nilimkatia tiketiย  kisha nilimuonesha mahali pa kwenda kulala, inaonesha Yuleย  Baba alkuwa akimfuatilia kijana huyo maana baada ya kijanaย  huyo kwenda kulala yule Baba alikuja”ย 

    “Aliniuliza Kijana yupo wapi, nilimuelekeza alipo sababuย  nilimjuwa Baba huyo baada ya kuja mchana na kuzungumza naย  Bosi, muda mchache baadaye Bosi naye alikuja kisha aliniulizaย  alipo kijana nilimueleza alipo, alielekea huko na ukimyaย  ulitawala, nilianza kusinzia lakini baadaye nilishtuka baadaย  ya Bosi kuniita na kuniambia kuwa napaswa kuondoka usiku huo,ย  nilikuwa na zamu ya kukesha hivyo kuambiwa vile nilifurahiย  ili nikalale, lakini nilipoangalia vizuri niligundua yuleย  Baba alikuwa akimsubiria Bosi nje ila alitoka na begi kubwaย  hivi ambalo hata sikuliona wakati linaingia, nilifunga naย  kuondoka zangu!!” Alisema Mdada huyo huku akihema juu juu,ย  Faudhia alishusha Bastola yake baada ya kugudua sasa alikuwaย  akiongea ukweli, alijuwa Baba huyo alikuwa ni Mzee Shomari.ย 

    “Enhee ilikuwaje baada ya hapo?”aliuliza tena Faudhiaย 

    “Baada ya hapo, siku iliyofuata niliambiwa nisiende kaziniย  ila nitalipwa pesa ya siku kitu ambacho kilizidi kunipaย  furaha, Mchana kupitia taarifa ya habari nilisikia taarifaย  kuwa basi la Kampuni yetu lilipata ajali wakati likiwaย  linafanya safari, Hakuna aliyepona katika ajali hiyo…lakiniย  Bosi alinisistiza sana nisije nikasema chochote kuhusu yuleย  Baba kuja usiku na yule kijana” Alisimulia Mdada huyo ambayeย  alikuwa mnene kiasiย 

    “Sasa usiri wako umepelekea Nchi kuzama kwenye Lindi laย  Ugaidi wa kutisha, muda siyo mrefu jiji hili litakuwa chiniย  ya ESS, kama unaweza kuongozana na mimi twende” Alisemaย  Faudhia akimwambia Mdada huyo ambaye alishapukiaย 

    Alionekana kuchanganikiwa, waliingia kwenye gari kisha gariย  liliondoka eneo hilo kuelekea yalipokuwa makazi ya Mama yakeย Martin Gimbo, miili ya Mama Martin na Mjukuu wake ilishaanzaย  kutoa harufu humo ndani, Faudhia aliingia kutafuta chochoteย  kitakachomuwezesha kufukua kaburi hilo ambalo lilisemekanaย  kuwa ni kaburi la Martin Gimbo.ย 

    “Naomba unisaidie hapa, tukishamaliza tunaondoka” Alisemaย  Faudhia kisha alimpatia chepe mdada huyo, walianza kufukuaย  kaburi hilo. Iliwachukua zaidi ya saa nzima hadi kumaliza,ย  chini walikutana na sanduku kubwa ambalo kwa kawaida lilikuwaย  ni sanduku la kuhifadhia mwili wakati wa kuzika. Walifanikiwaย  kulivuta juu, wakati huo walianza kusikia milio ya Risasi kwaย  mbali huku gari za polisi zikiliza ving’ora vyake.ย 

    Faudhia alianza kuligonga ili lifunguke, bahati nzuri alipataย  nyundo ndani ya nyumba hiyo kisha alifanikiwa zoezi laย  kulifungua Sanduku hilo, yule Mdada alitazama pembeni kwaย  hofu ya kuona mabaki ya mwili wa marehemu Martin Gimbo,ย  bahati mbaya ndani ya Sanduku hilo kulikuwa na brifkesi ndogoย  na siyo mifupa wala mabaki ya mwili wa Martin Gimboย 

    “Yes! Martin Gimbo ndiye Chogo” Alisema Faudhia hukuย  akimtazama Mdada huyo ambaye hakulijuwa hata jina lake.ย  Alilichukua Brifkesi hilo lakini hata kabla hawajapiga hatuaย  hata moja, Faudhia alisindikizwa chini na teke kaliย  lililopigwa kwa ustadi wa hali ya juu, ghafla alihisi ganziย  mkono wa kulia, aliliachia brifkesi hilo huku akiwa anaangukaย  chini, Sanduku lilidakwaย 

    Faudhia alishangaa namna upigaji wa teke hilo ulivyotumiaย  akili na ustadi wa hali ya juu sana, aligeuka kumtazamaย  aliyekuwa amempiga teke hilo, alikutana na sura aliyoifahamu.ย  Naaam! Alikuwa ni rafiki yake wa zamani Diana, Diana alikuwaย  ndani ya Koti jeusi, sketi nyeusi, pia alikuwa amevalia wigiย  jeusi.ย 

    “Diana ni wewe?” Alihoji Faudhia, hakutegemea kukutana naย  Diana katika nyakati hizo, aliona kama yupo ndotoni japoย  alishatumiwa picha ya Miongoni mwa Watu waliokuwa wakiendeshaย  ugaidi Tanzania.ย 

    Faudhia alijivuta na kusimama japo kwa maumivu makali, tekeย  alilopigwa lilimfanya ahisi kizunguzungu.ย 

    “Umewezeje?” Aliuliza Faudhiaย 

    “Kwasababu nimekusubiria kwa zaidi ya miaka 7 Faudhia,ย  nimekusubiri kwa lengo moja tu la kukupeleka kuzimu” Alisemaย  Diana kisha aliweka Brifkesi pembeni, yule Mdada alivyoonaย  hivyo alikimbia eneo hilo sababu alijuwa kuna hatari kubwaย  inaenda kutokea hapo muda mchache ujao.

    “Ulinisubiria unipeleke kuzimu?” Alihoji Faudhia “Ndiyo! Kwasababu ulimuuwa Mama yangu” alisema Dianaย 

    “Diana itakuwa umekosea njia, mimi nimemuuwa Mama yako? Inaย  maana nawe umeingia kwenye mtego wa Mzee Shomari? Dianaย  mnatumika na huyo Mzee ili atimize lengo lake, nisikilizeย  rafiki yangu!! Mimi sikuuwa Mama yako bali yeye Mzee Shomariย  ndiye aliyefanya hivyo na hiyo ndiyo sababu ya yeye kukaaย  jela, amka kutoka usingizini Diana” Alisema Faudhiaย 

    “Leo tutaona Faudhia kati yangu Mimi na wewe nani yupoย  Usingizini, Ukifa naondoka na Brifkesi, nikifa unaondoka naย  Brifkesi” Alisema Diana huku akijiandaa kupambana na Faudhiaย 

    “Diana hebu nisikilize, hujapoteza kila kitu katika Maishaย  yako, una muda wa kubadilisha kila kitu, ungana na Mimiย  tumdhibiti Mzee Shomari” Alisema Faudhia, maneno ya Faudhiaย  hayakubadilisha Chochote, Diana alikaa mkao wa kuanzaย  kumshambulia Faudhia. Alianza kumfuata Faudhia kama Simbaย  mwenye njaa huku Faudhia akiwa anarudi nyuma ili afikirieย  namna ya kumzuia Diana.ย 

    Faudhia aligundua haraka kuwa Diana alikuwa anatumia piganoย  maarufu nchini China linaloitwa Wing Chun, alijuwa sasa kumbeย  Diana alikuwa na taaluma ya mapigano ya Martial artsย 

    Alipomfikia alitua kwenye mapaja ya Faudhia kisha alijirushaย  na kumzunguka kwa nyuma kisha aligusa mfupa hadimu sana nyumaย  ya mgongo wa Faudhia, kilikuwa ni kitendo cha haraka sana,ย  Faudhia alihisi kukatika kwenye uti wa mgongo ila alijikazaย  asianguke, alifanya haraka na kumgeukia Diana kishaย  alijipanga kupambana naye, alimwambiaย 

    “Acha Diana, Acha unachofanya kumbuka sisi ni marafiki”ย  Alisema Faudhiaย 

    “Ningekuwa rafiki yako usingelithubutu kuniulia Mama yangu,ย  alikukosea nini yule?” Alisema Diana huku akionekana kuzidiย  kujawa na hasira, alijiandaa tena kumpa pigo lingine la Wingย  Chun…Faudhia alijitahidi kuisoma mikimbio ya Diana ambayoย  ilikuwa ya haraka mno.ย 

    Alifanya kama vile anamkimbia, alimpa mgongo kisha alipohisiย  Diana yupo nyuma karibu na kumnasa alimchumpa na kugusa mguuย  mmoja kwenye mti kisha alijipindua na kukutana na Dianaย  ambaye hakutegemea kama Faudhia angejifyetua kisha Faudhiaย  alimpa teke la Maana Diana, alisogezwa pembeni huku akitemaย  damu, ilizidi kumpa hasira, alimfuata tena na kufanyaย mpambano huo uzidi kuwa mtamu. Ilikuwa ni vita kati yaย  marafiki wawili waliogeuka kuwa maadui, ndipoย  walipothibitisha kuwa kuna Msitari mwembamba sana kati yaย  Upendo na chuki.ย 

    Ulikuwa ni mpambano mkali sana, vita ya kurushiana ngumiย  ilitanda, Ilikuwa kama vile walikuwa wakipeana zamu, dakikaย  tatu kwa Faudhia na dakika tatu kwa Diana. Wakati wanapiganaย  lile Brifkesi lilikuwa pembeni, Faudhia hakujuwa kulikuwa naย  jambo gani ndani ya Bridkesi hilo jeusi.ย 

    Jua lilikuwa likiendelea kuwaka kwa ukali wake. Kutokana naย  ile sumu ambayo iliingizwa mwilini mwake na Mohd japoย  alijitahidi kuizuia kwa kujichoma sindano ila ilianzaย  kumletea shida alianza kutokwa jasho, ndio muda ambao Dianaย  aliutumia kumfanyia kitu mbaya Faudhia.ย 

    Alipeleka ngumi zaidi ya 10 mfululizo, Faudhia alijitahidiย  kadiri ya uwezo wake kuzipangua lakini hakuwa na nguvu yaย  kuzipangua zote alijikuta akiruhusu mwili wake kukutana naย  ngumi nzito za Diana, alijikutana akishuka chini na kupigaย  magoti, Diana alilichukua lile brifkesi kisha alimwambiaย  Faudhiaย 

    “Onja uchungu wa kifo ambao ulimpatia Mama yangu” Alichomoaย  sindano ili aweze kumchoma Faudhiaย 

    “Diana! Umesahau kila kitu? Kumbuka wewe ni nani, Mzeeย  Shomari anakutumia” Alisema Faudhia japo kwa shida sana hukuย  akihisi kizunguzungu, Diana alitoa kichupa kidogo kishaย  alifyonza sumu kwa kutumia sindanoย 

    “Niliwahi kusimuliwa kuwa Mtu anayekaribia kufa huwa naย  majuto sana ila nakushangaa wewe Faudhia bado unakaidi kuwaย  hukumuuwa Mama yangu” Diana alimsongelea Faudhia, alimshikaย  nywele na kupindisha shingo kisha alimchoma sindano, kablaย  hajaruhusu sumu iweze kusambaa mwilini mwa Faudhia, alipigwaย  na kitu kizito kichwani, Diana alishindwa kumalizia zoezi,ย  alijitahidi kugeuka lakini alishindwa alijikuta akiangukaย  chini na kupoteza fahamu. Nyuma yake alisimama yule Mdadaย  ambaye alimpa taarifa ya ajali ya Basi, Naam! Ndiyeย  aliyempiga na kitu kizito Diana.ย 

    Faudhia alimwambia Mdada huyo kuwaย 

    “Chukua Brifkesi tuondoke hapa, si unajuwa kuendesha gari?”ย  Aliulizaย 

    “Ndio najuwa”

    “Tuondoke hapa haraka sana” Alisema Faudhia, hakutakaย  kummaliza Diana siku hiyo sababu licha ya uadui badoย  alimtambuwa Diana kama rafiki yake, yule Mdada alimsaidiaย  Faudhia kuingia kwenye gari walilokuja nalo, Milio ya risasiย  ilitanda kila kona ya Jiji la Arusha, isingelikuwa salama kwaย  Faudhia kuendelea kukaa hapoย 

    “Tunaenda wapi?” Alihoji mdada akiwa anaingia barabara kuuย 

    “Dar-es-salaam” Alisema Faudhia huku akilifungua Brifkesiย  hilo ili ajuwe ndani yake kulikuwa na nini na kwaniniย  lilizikwa.ย 

    โ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขย 

    Jina la Selina lilifika mikononi mwa Chogo, aliambiwa kuwaย  ndiye anayefahamu ilipo chemba ya siri iliyohifadhi kiasiย  kikubwa cha pesa, Chogo alitoka kwenye moja ya Chumba baadaย  ya kumaliza kuzungumza na Mzee Shomari na kupewa taarifa hiyoย  kuwa kuna Mwanamke anaitwa Selina na yupo ndani ya Benki,ย  yeye pekee ndiye anayefahamu ilipo chemba ya siri. Chogoย  alitoka akiwa ameshikilia Bunduki aina ya AK47ย 

    Mateka walikuwa wamekaa chini kando ya sehemu ya Mapokezi,ย  alipofika aliulizaย 

    “Selina ni nani?” Ilikuwa ni sauti iliyojaa mamlaka sana,ย  aliuliza kwa kumaanisha kuwa alikuwa akimuhitaji Mdada huyo.ย  Selina mwenyewe aliposikia hivyo alijuwa ni kitu gani Magaidiย  hao walikuwa wakihitaji, baadhi ya Magaidi sura zaoย  walizificha Ila baadhi hawakuzificha akiweno Chogo ambayeย  waliamini hawezi kutambulika kwa urahisi.ย 

    “Selina ni nani?” Aliuliza tena Chogo kisha aliiandaa bundukiย  kwa lengo la kuleta kitishoย 

    “Mimi hapa” alijitokeza huyo aliyeitwa Selina akiwa amevaliaย  sare za wafanyakazi wa Benki, alikuwa Mwanamke mmoja mzuriย  mweusi mwenye rasta asilia.ย 

    “Mleteni” Alisema Chogo, mara moja Selina alisogezwa mahaliย  aliposimama Chogo, Selina alionekana kuwa muoga sana, Chogoย  alimwambia Selinaย 

    “Usiogope sababu una kazi moja tu ya kufanya, ukishamalizaย  nitakuacha huru sawa?” Alisema akiwa anatabasamu, Selinaย  aliitikia kwa woga kisha Chogo alisema

    “Tuongozane” Alimpa ishara Selina amfuate kwenye moja yaย  chumba.ย 

    Nje ya Benki polisi walizingira benki hiyo wakiwa na silahaย  za moto huku wakiwa na tahadhari kubwa, walikuwa wakitumiaย  kipaza sauti kuzungumza, Chogo alipofika Chumbani na Selinaย  alimwambiaย 

    “Nisubirie hapa, naenda kuongea na polisi” Alisema kishaย  alichukua AK47 na kuelekea nje ya Benki hiyo.ย 

    Kitendo cha Chogo kutoka nje ya Benki kilileta utayari kwaย  polisi na vitengo vyote vilivyokuwa makini na Benki, Chogoย  alitoka akiwa hajavaa shati, mwili wali wake ulijaa michoroย  mingi, alionekana kujiamini sana huku polisi wakiambiana kuwaย  wanapaswa kumsikiliza sababu alikuwa na mateka ndani ya Benkiย 

    Chogo alisimama katikati ya Barabara iliyotoka kivukoniย  kwenda mjini kisha aliwauliza polisiย 

    “Mlitaka nitoke ndani, nimeshatoka, mlikuwa mnasemaje?”ย  Aliuliza kwa ujasiri, kipaza sauti kilisikikaย 

    “Kwanza tunahitaji usalama wa mateka wote walio ndani yaย  Benki, pili tunataka kujuwa mnahitaji nini?”ย 

    “Oooh! Siwezi kuuwa Raia ambao hawana kosa lolote, ilaย  mkileta ujanja nitauwa kila Mtu ndani ya Benki, masaa 24ย  yajayo nitaiachia Benki hii” Alisema Chogo kisha alirudiย  ndani ya Benki, hakuna askari hata mmoja aliyejaribuย  kumshambulia Chogo, moja kwa moja alienda kwenye kile chumbaย  alichomuacha Selina, aliweka Bunduki pembeni kisha alifungaย  mlango, Chogo alimtazama Selina kwa jicho la kumtamani sanaย  ukizingatia sketi ya Selina ilikuwa imepasuka kidogo hivyoย  paja lilikuwa njeย 

    Selina alikuwa mwingi wa kutetemeka, Chogo alimfuata Selinaย  kisha alimtandika busu, alimshika matiti na Makalio, alimvuaย  nguo Selina na kumbaka, baada ya kumaliza alimwambia Selinaย 

    “Kama lilivyo tamu penzi lako, basi nahitaji uniambie wapiย  ilipo chemba ya siri iliyohifadhi pesa za Kimarekani” Alisemaย  Chogo akiwa anavaa nguo zake, alipomaliza alikuwa badoย  hajapata jibu kutoka kwa Selina ambaye alikuwa akitetemekaย  kwa wogaย 

    “Ukimya wako unaashiria kuwa ni bora ufe kuliko kusema ilipoย  Chemba si ndiyo?” Aliuliza tena Chogo, safari hiiย  alibadilisha sura yake na kujaza hasira

    “Tafadhali usiniuwe, ipo chumba namba 43” Alisema Selinaย 

    LEO NIMEWEKA NDEFU SANA COMMENTS ZIKIWA CHACHE NARUDI KWENYE KUWEKA FUPI

    Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA SABA

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย 

    riwaya za bure riwaya za kijasusi riwaya za kusisimua riwaya za kusoma mtandaoni riwaya za kuvutia

    24 Comments

    1. Octavian simplisius kazikulima on June 3, 2025 11:58 am

      Leo kwel ni ndefu had nimefulai

      Reply
      • Bunju5 on June 4, 2025 3:29 pm

        Hongera

        Reply
    2. Fadhili magimba on June 3, 2025 2:33 pm

      Nimeipenda

      Reply
    3. Luccah on June 3, 2025 2:48 pm

      Haha admini usitunyanyase ww weka unay0jiskia fupi au ndefu ss tunas0ma t ๐Ÿ˜‚

      Reply
    4. Adam on June 3, 2025 2:55 pm

      Leo Kweli Nimefrahia Saana Kuusoma Hii Story

      Reply
    5. Rifai on June 3, 2025 4:04 pm

      Hongera san ni nzur na ya kuvutia unasoma lkin kam vile ni video ipo mbele yko unaiagalia๐Ÿ’ฏ

      Reply
    6. Benedict juma yanga on June 3, 2025 4:17 pm

      Hongera ndefu alafu tamu

      Reply
    7. David ben on June 3, 2025 5:50 pm

      Asante sana leo ndefu

      Reply
    8. Ignas talsis mumba on June 3, 2025 5:51 pm

      Nzuri sana

      Reply
    9. Josephat on June 3, 2025 6:01 pm

      Ndo kusema chogo alikua na ugwadu๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ

      Reply
    10. Sulee on June 3, 2025 7:23 pm

      Nzur sana boss leo mzigo wa uhakika

      Reply
      • Salma Ibrahim on June 3, 2025 9:40 pm

        Leo imefika mahala pake..

        Reply
      • Salma Ibrahim on June 3, 2025 9:41 pm

        Mashaallah asante

        Reply
    11. Samwel mkangi on June 3, 2025 11:03 pm

      Imekaa pouuuwaa

      Reply
    12. Gervase on June 4, 2025 7:03 am

      Aah Admin we nouma ,, Leo ndefu Hadi Raha๐Ÿ’ช

      Reply
    13. Lucas George on June 4, 2025 8:24 am

      Apo sawa admin ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

      Reply
      • Azimara rajabu on June 5, 2025 11:18 am

        nzuri san

        Reply
    14. Maestro05 on June 4, 2025 8:52 am

      Ya Leo imekuwa ndefu pia nzuri..Bigup Sana Admin

      Reply
    15. Masoud on June 4, 2025 11:05 am

      Aisee kuipata yote tunabonyeza ngapi mkuu๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…โœ…๏ธ

      Reply
    16. KASIBETH NDIKUMWAMI on June 4, 2025 3:26 pm

      Story nzuri inavutia sana inanifanya kila saaa niwe naingia kwenye kundi kuitafta jitahdi luifanya iwe ndefu pia itoke kwa wakati

      Reply
    17. Safina on June 4, 2025 6:13 pm

      Mbona ya Saba hutoi Admin sio poa bwana

      Reply
      • Safina on June 4, 2025 6:14 pm

        Tumesubir sana huweki

        Reply
    18. Azimara rajabu on June 5, 2025 11:19 am

      nzuri sana

      Reply
    19. ๐Ÿ”“ + 1.333214 BTC.NEXT - https://yandex.com/poll/76RuKke5vYn6W1hp2wxzvb?hs=64f1178154d728143e05eb423d7c652a& ๐Ÿ”“ on June 5, 2025 6:25 pm

      7x51ai

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 4, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya sita “Kama lilivyo tamu penzi lako, basi nahitaji uniambie…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tano-05)

    Ratiba Kamili Ya FIFA CLUB WORLD CUP 2025

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.