Ilipoishia sehemu ya tatu 

“Ndio, ni Mwanangu! Miaka mingi sasa tangia Martin  alipofariki kwa ajali ya gari akiwa anaelekea Mjini, tangu  siku hiyo sikuwahi kuamka na kukaa tena hata ongea yangu  ilikuwa ya shida, Martin alikuwa ndiyo Mwanangu wa pekee  niliyempenda, tumaini la Maisha yangu lilikuwa kwa Kijana wangu Martin baada ya Baba yake kufukiwa na kifusi huko  Merelani akiwa anafanya kazi za mgodi” Alisema Mama huyo,  kisha alimuomba Mjukuu wake amsindikize mahali. 

“Nifuateni” Alisema Mama huyo ambaye alijitambulisha kama  Mama yake Martin Gimbo ambaye alikuwa akitajwa kama gaidi  kiongozi wa kundi la ESS. Endelea

SEHEMU YA NNE

Walizunguka nyuma ya nyumba, aliwaonesha kaburi la Martin  Gimbo, kaburi hilo lilikuwa dogo tu kuashiri kuwa Martin  alifariki akiwa bado Kijana Mdogo, hii iliwashangaza Faudhia  na Mohd ambao ndimi zao zilikuwa kimya sana, Faudhia aliketi  juu ya tofali moja akionesha kuchanganywa na maelezo ya Huyo  Mama 

“Hakuna aliyewahi kuja kumuulizia Martin Gimbo, nimeshtuka  baada ya miaka mingi nyie kuja kumuulizia Martin, kwanini  mmekuja kumuulizia?” Alihoji Mama huyo. 

“Mama una hakika Martin amefariki?” Alihoji Mohd 

“Ndiyo! Martin alizikwa hapa! Ilikuwa ni siku ngumu sana  kwangu. Siku ambayo siwezi kuisahau katika Maisha yangu”  Aliendelea kuelezea Mama Martin Gimbo, Faudhia alitoa picha  ya Martin Gimbo kisha alimpatia Mama huyo ili kuona kama  naweza akamtambua 

Mama huyo aliiangalia picha kwa umakini sana, kisha  aliwatazama Faudhia na Mohd 

“Mnamaanisha nini?” Aliwauliza 

“Mama, sisi ni Undercover kutoka kitengo cha Usalama wa  Taifa, kama unavyojuwa sasa hivi tunakabiliwa na ugaidi hapa  Nchini, huyo pichani ni mshukiwa namba moja, umemfahamu?”  Alisema Mohd huku akiamuachia swali Mama huyo 

Mama huyo aliirudia kuiangalia tena ile picha kisha alitikisa  kichwa chake na kusema 

“Anafanana na Martin! Lakini mbona Martin wangu alifariki  miaka mingi iliyopita na alizikwa hapa” Alisema Mama huyo  ambaye hali yake ilianza kubadilika baada ya kuanza  kushtushwa na taarifa alizokuwa akizisikia 

“Kifo cha Martin wako kilitokeaje?” Alihoji Faudhia haraka  baada ya kutambua kuwa Mama huyo alikuwa kwenye hali mbaya  ambayo ingepelekea kushindwa kuzungumza baada ya dakika  kadhaa. Mama huyo alianza kusimulia ilivyokuwa siku ya kifo  cha Mwanaye japo alikuwa akisimulia kwa shida

“Martin alipomaliza elimu ya sekondari, aliniaga kuwa anaenda  kwa Baba yake Mkubwa huko Tabora, lakini majira ya mchana  nilipokea taarifa kuwa gari alilopanda Martin lilipata ajali  mbaya na kusababisha Mwanangu apoteze uhai, mwili wa Martin  uliharibika mno ila kwasababu alipata ajali hapa hapa Arusha  ilibidi aletwe kwa ajili ya maziko” Alisema Mama huyo huku  akikohoa, chozi lilikuwa linambubujika 

“Nani alitoa taarifa ya Kifo cha Martin?” Alihoji tena  Faudhia kwa umakini sana, Mama huyo alikuwa na picha ambayo  alipiga yeye na Mtu aliyetoa taarifa ya kifo cha Martin 

“Huyu ndiye aliyenipigia simu, aliongozana na Watu wa Gari la  kubebea maiti kuja hapa” Aliitoa picha iliyomuonesha Mtu  aliyeenda na maiti ya Mwanaye Martin ikiwa imeharibika, Mohd  aliiangalia picha hiyo kisha alimpatia Faudhia 

Kilichomshtua Faudhia ni huyo Mtu aliyeleta maiti ya Martin  Gimbo, hakuamini macho yake hadi presha ilimpanda, Mohd  akamuuliza 

“Unamfahamu huyo Mtu?” Aliuliza Mohd, Faudhia alimtazama Mohd  kisha alisema 

“Ndio namfahamu huyu Mtu, ni miaka mingi sana imepita sasa.  Siamini kama baada ya makosa yale aliachiwa mapema hivyo”  Alisema Faudhia, huku akirejea kuiangalia tena picha hiyo,  alionekana Mzee Shomari ambaye alikuwa ni Baba wa kambo wa  Faudhia akiwa amepiga picha na Mama yake Martin 

“Huyu Mtu alikuja tena hapa?” Aliuliza 

“Sikupata kumuona tena, hakuna aliyekuja hata kunipa pole,  nilibakia Mimi na Dada yake Martin ambaye naye alifariki na  kuniachia huyu Mjukuu” Alisema Mama yake Martin Gimbo. 

“Mama una hakika kuwa huyu Mtu alikuja na Maiti hapa?” 

“Ndio” alijibu Huyo Mama huku akianza kutetemeka kutokana na  maradhi yaliyokuwa yakimsibu. 

“Faudhia, unahisia gani?” Alihoji Mohd 

“Kwa jinsi nilivyoishi na Mzee Shomari, simulizi nilizosikia  kuhusu yeye na matukio aliyoyafanya, napata mashaka kuwa  huwenda yeye ndiye aliyemtengeza Chogo kuwa gaidi, sina  uhakika na ninachokihisi lakini hisia zangu zinaweza kunipa  majibu kutokana na picha hii, mwaka ambao Martin amefariki ni  miezi michache baaada ya Mzee Shomari kufungwa kwa kosa la 

Mauwaji huko Mbeya, najiuliza aliweza vipi kutoka? Kwa  vyovyote yupo mfadhili katika haya yote, hayupo peke yake”  Alisema Faudhia. 

••••••••••••••••••••••••••••••••• 

Jioni ilikuwa imeshangia, Chogo alikuwa ndani ya Benki hiyo,  aliagiza Diana aende ndani ya Benki kuu. Muda huu alikuwa  ndani ya chumba cha kuhifadhia pesa, chumba hicho kilikuwa na  mateka wawili, Gavana na Mke wake ambao walikuwa wamefungwa  kamba kwenye mikono yao. 

Chogo alikuwa akiweka risasi kwenye Bastola yake, Mwanaume  huyo alikuwa mweusi mwenye kipara, Gavana alimuuliza Chogo 

“Mnataka nini?” Chogo hakujibu swali la Gavana 

“Nakuuliza wewe, kwanini mmetuteka mnataka pesa?” Aliuliza  tena Gavana wa Benki kuu 

Chogo alikasirika kisha alimfuata Gavana kwa hasira akamshika  shingoni 

“Hata ukijuwa sababu huwezi kulipa kwa chochote, thamani ya  nilichokipoteza haiwezi kufananishwa na pesa yenu chafu  iliyojaa damu” Alisema Chogo kisha alimuachia Gavana ambaye  alianza kukohoa 

“Ukirudia tena kuuliza maswali ya kipuuzi nitakata shingo  yako” Chogo alisema kisha alinyanyuka na kurudi alipokuwa  amekaa, kisha alipomaliza kuweka risasi kwenye Bastola  aliondoka chumbani hapo, Gavana alimsogelea Mke wake ambaye  alikuwa akilia tu huku akisema 

“Naogopa sana sijui hatma itakuwaje, sijui kesho itakuwa  vipi!” Alisema maneno yaliyomfanya Gavana aseme 

“Sesilia huna sababu ya kulia maana hata kama ukifanya hivyo  huwezi kubadilisha chochote kile, cha msingi ni kuangalia  tunafanya kitu gani” alisema Gavana 

“Tutafanya nini mbele ya hawa Watu walioizidi akili Serikali?  Sisi wawili hatujapitia hata mafunzo ya ujeshi hata mgambo  tutafanya nini mbele yao?” Alisema Mke wa Gavana  aliyejulikana kama Sesilia, Gavana alijisogeza kwa Mke wake  akamwambia 

“Unaiona ile meza ndogo?” Alisema Gavana huku akimuonesha Mke  wake

“Ndio naiona” alijibu Mke wa Gavana 

“Nyuma yake kuna Chemba ndogo ambayo kama ukiifikia na  kubonyeza basi chumba hiki kitazungukwa na ngao ya Umeme,  hawataweza kuingia humu tena kisha hapo hapo kuna swichi  ambayo ukiibonyeza inazibua ukuta sababu pale kuna mlango wa  siri sana” Alisema Gavana kisha Mke wake alimtazama Mume wake  sehemu ya Mguu na kuona jinsi damu ilivyokuwa ikimmwagika  Gavana. 

“Mguu wangu una maumivu makali sana, unapaswa kufanya hivyo  Sesilia vinginevyo tutafia humu” Alisema Gavana lakini  alitambuwa kuwa Mke wake alikuwa mwenye woga sana, alikuwa  akitetemeka na kulia, kabla hawajazungumza chochote aliingia  Mlinzi kwa ajili ya kuwaangalia Gavana na Mke wake, maongezi  yalikoma hapo baada ya kumuona Mlinzi. 

Upande wa pili, ndani ya Ghorofa la China plaza maeneo ya  Karume, floo ya mwisho kabisa, alionekana Mzee mmoja mwenye  mvi nyeupe na kitambi, Mzee huyo alikuwa akizungumza na simu 

“Hakikisha taarifa inatoka sasa hivi” Alisistiza Mzee huyo  kisha alikata simu, alipogeuka nyuma yake alikuwepo Diana  rafiki wa Faudhia, Mzee huyo alikuwa ni Mzee Shomari. Diana  alionekana kutaka kusema jambo, Mzee Shomari alimkaribisha  akae kwanza kisha alimpatia kinywaji 

“Vipi mpango umeenda sawa?” Aliuliza Mzee Shomari 

“Faudhia amekwepa mtego wa kifo, yupo Arusha anamfuatilia  Martin Gimbo” alisema Diana 

“Shit!!” Alisema Mzee Shomari 

“Wameenda hadi shule aliyosoma Martin lakini Mkuu wa Shule  alifanya kama tulivyomwambia lakini walimuuwa” Alielezea tena  Diana 

“Hakikisha Utambulisho wa Chogo haufahamiki, tuma Watu  wamuuwe Mama yake Chogo, endapo Chogo atafahamu kuwa  tumemdanganya basi ngoma itakuwa ngumu sana, ni lazima  tufanikishe mpango ulio mbele yetu haraka sana” Alisema Mzee  Shomari, haraka Diana alinyanyua simu na kumpigia Mtu 

“Uwa panya bila kelele” Alisema Diana, Mzee Shomari akiwa  amekaa kwenye kiti cha walemavu alitabasamu sana kisha  alisema

“Nakuaminia sana Mtoto wangu, hakika wewe ni simba jike  unayewinda kimya kimya” Alisema Mzee Shomari 

“Siku zote nimeishi na kisasi ndani ya moyo wangu, kifo cha  Mama yangu ni lazima Faudhia akilipie, nafanya yote  kuhakikisha Mama yangu anafurahi huko alipo” Alisema Diana 

“Na siku zote Muuwaji hawezi kuishi, ndiyo maana nilikutoa  gerezani ili uje kuitafuta haki iliyoporwa na Faudhia”  Alikazia Mzee Shomari kisha alimruhusu Diana kuelekea ndani  ya Benki, mpango wa Mzee Shomari ulikuwa ni Kumuuwa Faudhia,  kisha kuiba pesa za kimarekani ambazo zilihifadhiwa ndani ya  Benki hiyo katika chemba ya siri, ilikuwa ni zaidi ya Dola  Bilioni 900 , alimtumia Chogo kama ngao ya kufanya mambo yake  huku akiweka ubia na rafiki yake wa zamani ambaye alikuwa  akiishi Uholanzi, ndiye aliyemtoa jela na kumfadhili pesa za  kufanya ugaidi Tanzania, hivyo Mzee Shomari alikuwa ndiye  Gaidi aliyekuwa akiratibu mipango yote, alikusanya vijana na  kuwapatia silaha nzito, akiwemo Diana na Martin Gimbo maarufu  kama Chogo 

Jinsi alivyowapata Diana na Chogo utakuja kufahamu mbele,  hebu tosonge.. 

Usiku ulikuwa umeingia, ndani ya Jiji la Arusha, Faudhia  alikuwa akimlaumu Mohd kwa kosa la Kumuuwa Mama yake na  Martin Gimbo.

Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA NNE

JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

9 Comments

  1. Leynecy Omary on

    𝑱𝒐𝒎𝒐𝒏𝒊 𝒚𝒂 5 𝒊𝒔𝒊𝒄𝒉𝒆𝒍𝒆𝒘𝒆,,,,𝒊𝒘𝒆 𝒏𝒅𝒆𝒇𝒖 𝒏𝒅𝒆𝒇𝒖

Leave A Reply

Exit mobile version