Ilipoishia sehemu ya tatuย
“Ndio, ni Mwanangu! Miaka mingi sasa tangia Martinย alipofariki kwa ajali ya gari akiwa anaelekea Mjini, tanguย siku hiyo sikuwahi kuamka na kukaa tena hata ongea yanguย ilikuwa ya shida, Martin alikuwa ndiyo Mwanangu wa pekeeย niliyempenda, tumaini la Maisha yangu lilikuwa kwa Kijanaย wangu Martin baada ya Baba yake kufukiwa na kifusi hukoย Merelani akiwa anafanya kazi za mgodi” Alisema Mama huyo,ย kisha alimuomba Mjukuu wake amsindikize mahali.ย
“Nifuateni” Alisema Mama huyo ambaye alijitambulisha kamaย Mama yake Martin Gimbo ambaye alikuwa akitajwa kama gaidiย kiongozi wa kundi la ESS. Endelea
SEHEMU YA NNE
Walizunguka nyuma ya nyumba, aliwaonesha kaburi la Martinย Gimbo, kaburi hilo lilikuwa dogo tu kuashiri kuwa Martinย alifariki akiwa bado Kijana Mdogo, hii iliwashangaza Faudhiaย na Mohd ambao ndimi zao zilikuwa kimya sana, Faudhia aliketiย juu ya tofali moja akionesha kuchanganywa na maelezo ya Huyoย Mamaย
“Hakuna aliyewahi kuja kumuulizia Martin Gimbo, nimeshtukaย baada ya miaka mingi nyie kuja kumuulizia Martin, kwaniniย mmekuja kumuulizia?” Alihoji Mama huyo.ย
“Mama una hakika Martin amefariki?” Alihoji Mohdย
“Ndiyo! Martin alizikwa hapa! Ilikuwa ni siku ngumu sanaย kwangu. Siku ambayo siwezi kuisahau katika Maisha yangu”ย Aliendelea kuelezea Mama Martin Gimbo, Faudhia alitoa pichaย ya Martin Gimbo kisha alimpatia Mama huyo ili kuona kamaย naweza akamtambuaย
Mama huyo aliiangalia picha kwa umakini sana, kishaย aliwatazama Faudhia na Mohdย
“Mnamaanisha nini?” Aliwaulizaย
“Mama, sisi ni Undercover kutoka kitengo cha Usalama waย Taifa, kama unavyojuwa sasa hivi tunakabiliwa na ugaidi hapaย Nchini, huyo pichani ni mshukiwa namba moja, umemfahamu?”ย Alisema Mohd huku akiamuachia swali Mama huyoย
Mama huyo aliirudia kuiangalia tena ile picha kisha alitikisaย kichwa chake na kusemaย
“Anafanana na Martin! Lakini mbona Martin wangu alifarikiย miaka mingi iliyopita na alizikwa hapa” Alisema Mama huyoย ambaye hali yake ilianza kubadilika baada ya kuanzaย kushtushwa na taarifa alizokuwa akizisikiaย
“Kifo cha Martin wako kilitokeaje?” Alihoji Faudhia harakaย baada ya kutambua kuwa Mama huyo alikuwa kwenye hali mbayaย ambayo ingepelekea kushindwa kuzungumza baada ya dakikaย kadhaa. Mama huyo alianza kusimulia ilivyokuwa siku ya kifoย cha Mwanaye japo alikuwa akisimulia kwa shida
“Martin alipomaliza elimu ya sekondari, aliniaga kuwa anaendaย kwa Baba yake Mkubwa huko Tabora, lakini majira ya mchanaย nilipokea taarifa kuwa gari alilopanda Martin lilipata ajaliย mbaya na kusababisha Mwanangu apoteze uhai, mwili wa Martinย uliharibika mno ila kwasababu alipata ajali hapa hapa Arushaย ilibidi aletwe kwa ajili ya maziko” Alisema Mama huyo hukuย akikohoa, chozi lilikuwa linambubujikaย
“Nani alitoa taarifa ya Kifo cha Martin?” Alihoji tenaย Faudhia kwa umakini sana, Mama huyo alikuwa na picha ambayoย alipiga yeye na Mtu aliyetoa taarifa ya kifo cha Martinย
“Huyu ndiye aliyenipigia simu, aliongozana na Watu wa Gari laย kubebea maiti kuja hapa” Aliitoa picha iliyomuonesha Mtuย aliyeenda na maiti ya Mwanaye Martin ikiwa imeharibika, Mohdย aliiangalia picha hiyo kisha alimpatia Faudhiaย
Kilichomshtua Faudhia ni huyo Mtu aliyeleta maiti ya Martinย Gimbo, hakuamini macho yake hadi presha ilimpanda, Mohdย akamuulizaย
“Unamfahamu huyo Mtu?” Aliuliza Mohd, Faudhia alimtazama Mohdย kisha alisemaย
“Ndio namfahamu huyu Mtu, ni miaka mingi sana imepita sasa.ย Siamini kama baada ya makosa yale aliachiwa mapema hivyo”ย Alisema Faudhia, huku akirejea kuiangalia tena picha hiyo,ย alionekana Mzee Shomari ambaye alikuwa ni Baba wa kambo waย Faudhia akiwa amepiga picha na Mama yake Martinย
“Huyu Mtu alikuja tena hapa?” Aliulizaย
“Sikupata kumuona tena, hakuna aliyekuja hata kunipa pole,ย nilibakia Mimi na Dada yake Martin ambaye naye alifariki naย kuniachia huyu Mjukuu” Alisema Mama yake Martin Gimbo.ย
“Mama una hakika kuwa huyu Mtu alikuja na Maiti hapa?”ย
“Ndio” alijibu Huyo Mama huku akianza kutetemeka kutokana naย maradhi yaliyokuwa yakimsibu.ย
“Faudhia, unahisia gani?” Alihoji Mohdย
“Kwa jinsi nilivyoishi na Mzee Shomari, simulizi nilizosikiaย kuhusu yeye na matukio aliyoyafanya, napata mashaka kuwaย huwenda yeye ndiye aliyemtengeza Chogo kuwa gaidi, sinaย uhakika na ninachokihisi lakini hisia zangu zinaweza kunipaย majibu kutokana na picha hii, mwaka ambao Martin amefariki niย miezi michache baaada ya Mzee Shomari kufungwa kwa kosa laย
Mauwaji huko Mbeya, najiuliza aliweza vipi kutoka? Kwaย vyovyote yupo mfadhili katika haya yote, hayupo peke yake”ย Alisema Faudhia.ย
โขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขย
Jioni ilikuwa imeshangia, Chogo alikuwa ndani ya Benki hiyo,ย aliagiza Diana aende ndani ya Benki kuu. Muda huu alikuwaย ndani ya chumba cha kuhifadhia pesa, chumba hicho kilikuwa naย mateka wawili, Gavana na Mke wake ambao walikuwa wamefungwaย kamba kwenye mikono yao.ย
Chogo alikuwa akiweka risasi kwenye Bastola yake, Mwanaumeย huyo alikuwa mweusi mwenye kipara, Gavana alimuuliza Chogoย
“Mnataka nini?” Chogo hakujibu swali la Gavanaย
“Nakuuliza wewe, kwanini mmetuteka mnataka pesa?” Aliulizaย tena Gavana wa Benki kuuย
Chogo alikasirika kisha alimfuata Gavana kwa hasira akamshikaย shingoniย
“Hata ukijuwa sababu huwezi kulipa kwa chochote, thamani yaย nilichokipoteza haiwezi kufananishwa na pesa yenu chafuย iliyojaa damu” Alisema Chogo kisha alimuachia Gavana ambayeย alianza kukohoaย
“Ukirudia tena kuuliza maswali ya kipuuzi nitakata shingoย yako” Chogo alisema kisha alinyanyuka na kurudi alipokuwaย amekaa, kisha alipomaliza kuweka risasi kwenye Bastolaย aliondoka chumbani hapo, Gavana alimsogelea Mke wake ambayeย alikuwa akilia tu huku akisemaย
“Naogopa sana sijui hatma itakuwaje, sijui kesho itakuwaย vipi!” Alisema maneno yaliyomfanya Gavana asemeย
“Sesilia huna sababu ya kulia maana hata kama ukifanya hivyoย huwezi kubadilisha chochote kile, cha msingi ni kuangaliaย tunafanya kitu gani” alisema Gavanaย
“Tutafanya nini mbele ya hawa Watu walioizidi akili Serikali?ย Sisi wawili hatujapitia hata mafunzo ya ujeshi hata mgamboย tutafanya nini mbele yao?” Alisema Mke wa Gavanaย aliyejulikana kama Sesilia, Gavana alijisogeza kwa Mke wakeย akamwambiaย
“Unaiona ile meza ndogo?” Alisema Gavana huku akimuonesha Mkeย wake
“Ndio naiona” alijibu Mke wa Gavanaย
“Nyuma yake kuna Chemba ndogo ambayo kama ukiifikia naย kubonyeza basi chumba hiki kitazungukwa na ngao ya Umeme,ย hawataweza kuingia humu tena kisha hapo hapo kuna swichiย ambayo ukiibonyeza inazibua ukuta sababu pale kuna mlango waย siri sana” Alisema Gavana kisha Mke wake alimtazama Mume wakeย sehemu ya Mguu na kuona jinsi damu ilivyokuwa ikimmwagikaย Gavana.ย
“Mguu wangu una maumivu makali sana, unapaswa kufanya hivyoย Sesilia vinginevyo tutafia humu” Alisema Gavana lakiniย alitambuwa kuwa Mke wake alikuwa mwenye woga sana, alikuwaย akitetemeka na kulia, kabla hawajazungumza chochote aliingiaย Mlinzi kwa ajili ya kuwaangalia Gavana na Mke wake, maongeziย yalikoma hapo baada ya kumuona Mlinzi.ย
Upande wa pili, ndani ya Ghorofa la China plaza maeneo yaย Karume, floo ya mwisho kabisa, alionekana Mzee mmoja mwenyeย mvi nyeupe na kitambi, Mzee huyo alikuwa akizungumza na simuย
“Hakikisha taarifa inatoka sasa hivi” Alisistiza Mzee huyoย kisha alikata simu, alipogeuka nyuma yake alikuwepo Dianaย rafiki wa Faudhia, Mzee huyo alikuwa ni Mzee Shomari. Dianaย alionekana kutaka kusema jambo, Mzee Shomari alimkaribishaย akae kwanza kisha alimpatia kinywajiย
“Vipi mpango umeenda sawa?” Aliuliza Mzee Shomariย
“Faudhia amekwepa mtego wa kifo, yupo Arusha anamfuatiliaย Martin Gimbo” alisema Dianaย
“Shit!!” Alisema Mzee Shomariย
“Wameenda hadi shule aliyosoma Martin lakini Mkuu wa Shuleย alifanya kama tulivyomwambia lakini walimuuwa” Alielezea tenaย Dianaย
“Hakikisha Utambulisho wa Chogo haufahamiki, tuma Watuย wamuuwe Mama yake Chogo, endapo Chogo atafahamu kuwaย tumemdanganya basi ngoma itakuwa ngumu sana, ni lazimaย tufanikishe mpango ulio mbele yetu haraka sana” Alisema Mzeeย Shomari, haraka Diana alinyanyua simu na kumpigia Mtuย
“Uwa panya bila kelele” Alisema Diana, Mzee Shomari akiwaย amekaa kwenye kiti cha walemavu alitabasamu sana kishaย alisema
“Nakuaminia sana Mtoto wangu, hakika wewe ni simba jikeย unayewinda kimya kimya” Alisema Mzee Shomariย
“Siku zote nimeishi na kisasi ndani ya moyo wangu, kifo chaย Mama yangu ni lazima Faudhia akilipie, nafanya yoteย kuhakikisha Mama yangu anafurahi huko alipo” Alisema Dianaย
“Na siku zote Muuwaji hawezi kuishi, ndiyo maana nilikutoaย gerezani ili uje kuitafuta haki iliyoporwa na Faudhia”ย Alikazia Mzee Shomari kisha alimruhusu Diana kuelekea ndaniย ya Benki, mpango wa Mzee Shomari ulikuwa ni Kumuuwa Faudhia,ย kisha kuiba pesa za kimarekani ambazo zilihifadhiwa ndani yaย Benki hiyo katika chemba ya siri, ilikuwa ni zaidi ya Dolaย Bilioni 900 , alimtumia Chogo kama ngao ya kufanya mambo yakeย huku akiweka ubia na rafiki yake wa zamani ambaye alikuwaย akiishi Uholanzi, ndiye aliyemtoa jela na kumfadhili pesa zaย kufanya ugaidi Tanzania, hivyo Mzee Shomari alikuwa ndiyeย Gaidi aliyekuwa akiratibu mipango yote, alikusanya vijana naย kuwapatia silaha nzito, akiwemo Diana na Martin Gimbo maarufuย kama Chogoย
Jinsi alivyowapata Diana na Chogo utakuja kufahamu mbele,ย hebu tosonge..ย
Usiku ulikuwa umeingia, ndani ya Jiji la Arusha, Faudhiaย alikuwa akimlaumu Mohd kwa kosa la Kumuuwa Mama yake naย Martin Gimbo.
Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA NNE
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
17 Comments
Ya 5๐๐ฝ๐๐ฝ๐๐ฝ๐๐ฝ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ช๐ฝ๐ช๐ฝ๐ช๐ฝ
Nouuuuumaaaa
Duuuh kwa hyo mohd nae ni mmoja wa magaidi au next plz
aaaaaah! muongeze kdg hii ni ๐ค๐ฅ๐ฅ
Mbona fupi ila ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
๐ฑ๐๐๐๐๐ ๐๐ 5 ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐,,,,๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐
https://shorturl.fm/eAlmd
https://shorturl.fm/MVjF1
https://shorturl.fm/PFOiP
https://shorturl.fm/PFOiP
https://shorturl.fm/DA3HU
Iko fire sana
Good
https://shorturl.fm/YZRz9
https://shorturl.fm/PFOiP
https://shorturl.fm/I3T8M
https://shorturl.fm/uyMvT