Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya saba
“Naomba niongee na Shayo haraka” Alisema Rais, mara moja Waziri Mkuu alipiga simu kwa mkuu wa kitengo cha Usalama wa Taifa ambaye hadi kufikia wakati huo hakujuwa Faudhia alikuwa wapi, ni mzima au amekufa ila Faudhia alikuwa barabarani kuelekea Dar kwa ajili ya kuzuia mpango wa Mzee Shomari.
Mara moja simu ya Mzee Shayo ilipokelewa na maongezi kati ya Mzee Shayo na Rais yalianza, Rais alisikika kwa kupoa sana tofauti na mwanzo ambapo alionesha hasira sana kwa Mzee Shayo
“Shayo!!” Aliita Rais
“Naam Mkuu” Aliitika Mzee Shayo . ENDELEA
SEHEMU YA NANE
“Wewe ni Mtu pekee ambaye unaweza ukadhibiti kila kitu na kuleta sifa kwa Taifa hili, ruhusu Vijana wako waishambulie Benki sasa hivi” Alisema Rais kisha mwisho alisema kwa kukaza sauti tofauti na mwanzo alivyoanza.
“Mkuu, ndani ya Benki kuna Raia wasio na hatia, shambulio lolote lile tutakalo lifanya litasababisha madhara makubwa sana. Hiyo siyo suluhu ya jambo hili Mkuu, busara ni kuhakikisha Mateka wote wanatoka salama” Alijibu Mzee Shayo
“Mimi ndiye Rais wa Nchi hii nataka uamrishe walengaji wako waishambulie Benki haraka iwezekanavyo” Alisema tena Rais kwa sauti ya kufoka huku akijuwa fika kuwa Mzee Shayo hawezi kukubaliana na wazo hilo.
“Hilo haliwezekani Mkuu, tuvute subra kwa masaa kadhaa nitakuja na mpango wa nini tufanye” Alisema tena Mzee Shayo
“Shayo! Narudia tena Mimi ndiye Rais wa hii Nchi, hakuna Rais mwingine wala amiri jeshi Mkuu. Kama utashindwa kufanya hivyo nitatengua uteuzi wako haraka sana” Alisema Rais kwa sauti ile ile ya kufoka
“Mkuu siwezi kutoa amri hiyo kwa vijana wangu, hii kazi inahitaji…”
“Shayo siwezi kukubembeleza” Alisema Rais kisha simu ilikatika, Mzee Shayo alibakia akiwa njia panda, alijaribu tena kuipiga simu ya Faudhia lakini haikuita kabisa, alijiuliza kama Faudhia atakuwa ameshakufa basi hakutokuwa na jambo lolote la kuzuia amri ya Rais huyo, alichoka na kujitupa Kitini huku akitafakari afanye kitu gani.
Mwendo wa Bakora huko Bagamoyo Road, Matilda aliendesha gari kama dereva wa mshindano ya Formula one, ilikuwa ni safari yenye matumaini, Bado Mzee Shayo aliendelea kumtafuta Faudhia huku Mzee Shomari akipewa taarifa kuwa Diana alikuwa ameshauawa na mzigo ulikuwa umechukuliwa, taarifa hiyo ilimpa wazimu sana Mzee Shomari, alimpigia tena Chogo na kumwambia kuwa wana chini ya masaa mawili kuhakikisha wanachomoka ndani ya Benki hiyo haraka sana, wakati huo huo baada ya kumaliza kuongea na Chogo alipiga simu na kuagiza Helkopta isogee lilipo jengo la China plaza ili aweze kuondoka baada ya kuhakikisha akina Chogo wanatoka salama.
Akiwa ofisini Mzee Shayo, ilikuwa ni baada ya saa moja kupita aliingia Mwanaume mmoja aliyejulikana kama Samuel Dinonga, alikuwa ni Mkuu wa jeshi la polisi, iliwapasa kumpa salamu aliyostahili kisha Dinonga alimueleza Mzee Shayo kuwa yeye ndiye aliyepewa jukumu la kuongoza idara ya Usalama wa Taifa kwa wakati huo, Mzee Shayo alipaswa kukiacha kitengo haraka sana. Yalikuwa ndiyo maamuzi ya Rais, hakukuwa na namna, Mzee Shayo aliacha kila kitu na kuondoka ofisini hapo.
Lengo la Rais lilikuwa ni kuishanbulia Benki hiyo bila kujali kuwa kulikuwa na Gavana na Mke wake pia kilikuwa na wafanykazi wa Benki na wateja wa Benki hiyo ambao hawakuwa na hatia yoyote ile, muda huo alilielekea gari lake ili aweze kutimka eneo hilo la Makao makuu ya Kitengo cha Usalama wa Taifa, alipofika ndani ya gari simu yake iliita.
Aliitilia mashaka kidogo simu hiyo sababu ilipigwa kwa namba ambayo hakuifahamu kabisa, alisubiria kidogo kisha aliipokea
“Hello!” Alisema Mzee Shayo kwa umakini wa hali ya juu sana.
“Baba!!” Alisikia sauti ya Faudhia ikimuita, hakuamini masikio yake ni kama vile alisikia kitu kisichomuingia akilini
“Faudhia uko wapi?” Alihoji Mzee Shayo
“Nipo Barabarani nakuja huko Baba, naomba unisikilize kwa makini sana” Alisema Faudhia
“Ndio ndio”
“Ndani ya jengo la China plaza ndimo alipo Mkuu wa kikosi hicho, si mwingine ni Mzee Shomari! Chukua askari nenda kamdhibiti haraka sana mimi muda siyo mrefu nitakuwa Dar” Alisema Faudhia kwa umakini sana
“Kwasasa mimi siyo Mkuu wa Kitengo Faudhia, sina mamlaka ya kuamrisha askari wa kitengo tena” Alisema Mzee Shayo
“Oooh! Shit, basi jitahidi uwende mwenyewe maana ndani ya hicho kitengo kuna Watu wanafanya kazi ya kukwamisha juhudi” Alisema Faudhia
“Sawa ngoja nisogee huko” alisema Mzee Shayo kisha simu ilikatika, aliangalia kwenye gari yake aliona silaha aina ya Bastola, hakujuwa uzito wa ulinzi wa huko ndani ya jengo la china plaza ila aliamini Bastola hiyo itamsaidia, aliondoa gari kitengo na kuelekea China plaza.
Mkuu mpya wa kitengo Bwana Dinonga alifuata maagizo ya Rais wa Nchi, ilikuwa ni lazima aunganishe jeshi la polisi na askari wa kitengo ambao walikuwa eneo la tukio kuifanya kazi kwa pamoja. Aliondoa idadi kubwa ya Askari pale makao makuu kwa ajili ya kuelekea Benki ili kuishambulia benki hiyo, lengo likiwa kuuwa kila aliye ndani ya jengo hilo ili siri ya pesa zile iendelee kubakia wakiamini kuwa Chemba haikuweza kuonekana wakati chemba ya siri ilikuwa imeshafunguliwa.
Upande wa pili, Helkopta iliyoitwa kwa ajili ya kumchukua Mzee Shomari ilikuwa ikijongea taratibu kuelekea hapo, Mzee Shayo naye akiwa ndani ya gari lake alikuwa akifikiria ni jinsi gani ataweza kukabiliana na Magaidi hao ndani ya jengo la China plaza, safari ya kutoka Kigamboni hadi Mjini ilikuwa fupi tu ukizingatia hakukuwa na shughuli zozote zilizokuwa zikifanyika ndani ya Jiji hili la kibiashara, muda huo Faudhia alikuwa akiingia Dar, mwendo wao haukuwa wa kawaida, walipofika Tegeta Matilda alimwambia Faudhia kuwa anahisi kizunguzungu kutokana na spidi ya gari aliyokuwa nayo, ilimlazimu Faudhia amwambia Matilda kuwa asimamishe gari
haraka, Basi Matilda alifanya hivyo wakiwa maeneo ya kwa Ndevu – Tegeta
“Pole sana, Asante pia” Alisema Faudhia, Matilda alishindwa hata kumjibu Faudhia alipoteza fahamu akiwa ameshikilia usukani. Faudhia alishuka na kuielekea pikipiki iliyokuwa imesimama kando ya Barabara, aliiwasha na kuondoka eneo hilo.
Ukimya ulikuwa mkubwa sana alipofika maeneo ya Mnazi mmoja, alilazimika kushuka na kutembea kwa mguu kuelekea China plaza, japo alikuwa Mzee lakini hakusahau mbinu zake zilizompa umaarufu miaka ya 90, Mzee Shayo alikuwa ni zaidi ya komando wa vita, alisogea kwa kasi ya ajabu kwa kutumia njia za ndani kama anaelekea Shimoni kariakoo, alijuwa fika kuwa kama ni kweli magaidi hapo ndipo walipoweka kambi yao basi ulinzi wake utakuwa mkubwa sana. Alikuwa ndani ya suti ya kijivu iliyomkaa vizuri, alivua koti akabakiwa na shati jeupe litakaloweza kumpa urahisi wa kuifanya kazi yake. Alikuwa akitembea huku akiangalia saa yake aliyoweka muda maalum wa kufika eneo husika kabla kitengo cha Usalama wa Taifa hakijashambulia Benki na kuuwa Watu wasio na hatia, alikuwa na nusu saa tuu iliyobakia, muda huu alikuwa ameshazunguka hadi Msimbazi polisi, alikuwa sasa eneo la Msikiti wa Shekh Idrisa, alikuwa makini kuliko wakati wowote katika Maisha yake, alijuwa hiyo ndiyo nafasi pekee na pengine ingelikuwa kazi yake ya mwisho kutokana na umri wake na pia kuondolewa kwake kwenye kitengo na Rais.
Kwa mbali asikia sauti ya Helkopta ambayo ilikuwa ikielekea China plaza kwa ajili ya kumchukua Mzee Shomari, muda huo Faudhia alikuwa ameshafika upanga kwenye msikiti wa Maamur ili kuingia kwenye hiyo chemba itakayotumika kutorosha pesa kutoka Benki kuu. Alipofika hapo aliona Watu watatu wenye asili ya kiarabu wakiwa wamekaa kwa nje, aliwatazama kwa jicho la kijasusi aligundua Watu hao ambao ni wanaume walikuwa na silaha walizozificha kwenye viuno vyao, Faudhia alifikiria atumie njia gani kufika pale, alifikiria kwa zaidi ya dakika mbili huku ile presha kuwa muda unaisha ilizidi kumjaa aliona ni bora aamuwe kufanya kitu kimoja.
Alisogea hadi kwenye ukuta kimya kimya pasipo wale Wanaume kushtuka huku wanaume hao wakionekana kusoma vitabu ya dini, alijuwa ulikuwa mtego ili watu wasishtuke chochote, aliona pia baadhi ya Watu wakitoka na kuingia Msikitini hapo, ilikuwa ngumu kwake kujuwa kuwa Watu hao walikuwa wema au maadui. Pembezoni aliona nguo zilizokuwa zinetundikwa na zilikuwa ni za kiume, haraka Faudhia alizichukua na kuzivaa.
Alihakikisha anaonekana kama Mwanaume, na kweli alifanikiwa kwenye hilo, alivuta pumzi zake ili kujiondoa wasiwasi kisha aliitoa bastola aliyoichukua baada ya kumuuwa Diana, aliangalia Bastola hiyo yenye risasi tatu pekee aliona isingeliweza kumfaa ila ingelimsaidia kwa kiasi fulani, aliiweka sawa Bastola yake kisha aliingia barabara ya lami akawa anasogea, Wale Wanaume walipomuona Faudhia walionekana kumkagua kwa kutumia macho yao yaliyojaa wizi huku wakijifanya wengine kusoma na mwingine kuchezea tasbihi. Walipeana isharaka kisha mmoja akaingia ndani wawili wakabakia pale, Faudhia alisogea hadi lango la Msikiti. Mwanaume mmoja aliyekaa alimsalia Faudhia kwa Salam ya Kiislam
“Asalaam Alaykum?” Alisalimia huku akimtazama Faudhia ambaye alikuwa amevalia kiremba na kuificha sura yake kwa kuangalia pembeni, yule Mwanaume alimsalimia tena Faudhia
“Asalam Alaykum Shekh” Alisalimia bila wasiwasi, Faudhia alihema sana akijuwa kuwa jamaa huyu alikuwa ameshamshtukia, kisha Mwanaume huyo aliinuka na kumsogelea Faudhia ambaye hakutaka kuonesha sura yake.
Sura ya Mwanaume huyo ilianza kubadilika na kuwa ya hasira, alikuwa tayari ameshamtilia Mashaka Faudhia. Alizidi kusogea kisha alimuuliza Faudhia
“Wewe ni nani?” Aliuliza kwa rafudhi ambayo ilionesha wazi kuwa Mwanaume huyo alijifunza kiswahili siku si nyingi, mapigo ya moyo ya Faudhia yalizidi kwenda mbio. Yule Mwanaume akawa anasogea kuitazama sura ya Faudhia, endapo atagundua kuwa Faudhia si Mwanaume itakuwa shida kwa Faudhia
Yule Mwanaume alisogeza mkono ili amshike Faudhia amgeuze, Faudhia alifumba macho yake kuwa asingeliweza kufurukuta hapo, ghafla kabla hata hajamgusa Faudhia liliingia gari la kubebea maiti lililoleta maiti kwa ajili ya kuswaliwa. Purukushani za watu zikawa nyingi na kwakuwa walisimama katikati ya lango iliwapasa kulipisha gari hilo, Faudhia alibakia upande wa kulia na yule Mwanaume alirudi upande wa kushoto kisha gari ikapita katikati yao. Fumba na kufumbua Macho yule Mwanaume aligundua kuwa Faudhia ameshatoweka pale, haraka alipiga simu kwa wenzake kuwa eneo hilo si salama tena, aliwavuka Watu na kuelekea kwenye mlango wa kuzidi kuzama ndani ya Msikiti huo.
Naam!! Sasa, Mzee Shayo alikuwa ameshafika chini ya Jengo la China plaza, jengo hilo lilikuwa refu lenye vioo, Mzee Shayo alipochungulia kwa mbele aliona kuna Watu waliokuwa
wamesimama pembezoni, alijuwa tu Watu hao siyo watu salama kwake, muda huo Helkopta ilikuwa hewani juu ya Ghorofa hilo, alijuwa ndiyo wakati sahihi wa kuanza kukiwasha ili kuzuia Mzee huyo asitoweke eneo la tukio. Haraka alisogea mbele ya jengo, alimvizia mlinzi wakwanza kisha alimnyonga kwa kutumia kamba ya kiatu chake, alimvuta hadi mahali ambako kulikuwa na jenereta kubwa la kuzalisha umeme, huyu wa pili alikuwa amempa mgongo Mzee Shayo hivyo ilikuwa ni rahisi kumalizana naye, alimpiga kiwiko eneo la shingo, alifanya kimya kimya kisha alimvuta na kumsogeza pembeni, alihakikisha anawasachi na kuchukua silaha zao. Alikuwa ni Mtu makini sana ambaye aliijuwa thamani ya kazi aliyokuwa akiifanya, alisogea hadi mlango wa kuingilia, jengo lilikuwa kimya sana na hakukuwa na dalili kuwa Kulikuwa na mitembeo ya Mtu zaidi ya sauti ya Helkopta iliyokuwa juu ya Jengo, humo ndani Mzee Shomari alidhamiria kuhakikisha kuwa anachukua kila kitu kabla ya kutimka, alichotaka ni kuhakikisha Chogo anatoroka na pesa hizo ndani ya benki kwanza kabla yeye hajaondoka sababu alishajuwa ni wapi watakutana kwa ajili ya kugawana kiasi hicho
Alimpigia Chogo na kumwambia kuwa ni muda wa kuondoka, upande huo wa Benki tayari Chogo alikuwa na kiasi hicho cha pesa ndani ya mabegi kilichobakia kilikuwa ni kuondoka tuu, aliwaambia vijana wake kuwa
“Tunaenda kuwa Mamilionea leo” Alisema Chogo kwa tabasamu, aliamuru waifuate Chemba kwa ajili ya kuondoka, tayari alikuwa ameshawaweka vijana huko wakawa wanachimba na kuunganisha chemba hiyo ambayo hadi kufikia muda huo ilikuwa tayari kilichobakia kilikuwa wao kuondoka tuu. Alipofika kwenye Korido alikumbuka kuna kitu amesahau kisha aliwaambia vijana wake kuwa wamsumbirie kwenye chemba, Chogo alienda kwenye Chumba ambacho alimuacha Selina. Huwezi amini Chogo alikuwa ameshampenda Selina, alipofika alimtazama Selina ambaye alikuwa analia akiwa amekaa juu ya meza, chogo alijawa na huruma huku simu yake ikiwa inazidi kuita, alikuwa ni Mzee Shomari ndiye aliyekuwa akimpigia simu.
Upande mwingine ndani ya Msikitini, Mtafutano ulikuwa mkubwa mno, Faudhia aliijuwa ramani ya ilipo chemba hiyo ya utoroshwaji wa pesa ndani ya Benki, alijificha mahali ambapo aliamini ingelikuwa rahisi kuwaona Wanaume hao, wanaume walipofika ndani waliufunga mlango huo ili kisisikike chochote kutokea humo na kwenda kule Msikitini ambako kulikuwa na harakati za kuanza ibada ya kuisalia Maiti.
Walifunga viwanbo vya kuzuia sauti kwenye Bastola zao ili kuhakikisha hakuna kitakachosikika ili wasije haribu mpango wao. Faudhia alikuwa kwenye moja ya vyumba ambavyo vilikuwa ndani ya Eneo hilo, wale wanaume waligawana Majukumu ya kumsaka Faudhia.
Chumba alichojificha Faudhia kilikuwa kina dirisha la Kioo hivyo ilimpa urahisi wa kuona na kuonwa pia endapo adui yake atatazama kwenye kioo, mlango ulitekenywa huku Faudhia akiwa amjibanza ukutani, bastola yake ilikuwa kiunoni sababu aliamini matumizi ya Bastola yangelimfanya agundulike. Wale magaidi waliambiana kuwa wanapaswa kuingia kwa pamoja kwenye vyumba na kutoka pamoja hivyo endapo mmoja hatotoka basi chumba hicho ndicho ambacho adui yao atakuwa yumo.
Wakati kitasa kinatekenywa, Faudhia aliona Upanga kwenye kona ya Chumba hicho, aliuchukua taratibu bila kupiga kelele ya aina yoyote ile, alijiweka sana huku kioo kikiwa ndio msaada pekee kwake, yule Mwanaume alivyotokeza kichwa alikutana na upanga ambao ulizama kichwani, haraka Faudhia alimvuta Mwanaume huyo ndani kisha alichukua Bastola ya Mwanaume huyo alafu akasikia sauti ya kwanza ikisema
“Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba kingine ikisema
“Safi” wakimaanisha kuwa vyumba vyao vipo salama hapo ndipo Faudhia aliposhtuka kuwa anapaswa kuwa nje ya chumba haraka sana ili awawahi Wanaume hao, alifanya hivyo upesi sana huku akiwa ameelekeza Bastola yake mbele mahali ambako sauti hizo zilitoka, wale wanaume hawakuisikia sauti ya tatu ya mwenzao ndipo walipotoka nje haraka ila walikuwa wamechelewa, walikutana na mishale ya risasi kutoka kwa Faudhia, Msichana kutoka Mbeya, aliwamaliza kimya kimya bila kusikika popote sababu bastola ilikuwa na kiwambo cha kuzuia sauti .
Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA TISA
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
8 Comments
Thanks alot kijiwen
But mnafanya niunge megabyte zangu always ili tyu kupata hii zaid ya story
Kubali Sanaa faudhia people ya green city
hatarii
hizi ndio tunataka sio za kichawi usiku hatulali
Hatar sqna kiongozi
Iko pw ila inachelewa sana kupostiwa tupia inayofuata
Story Nzuri Saana Ila Tunaomba Jaman Mnazichelewesha Saana Ni Inasisimua Saana Hiii
Daaah!! nzuri saaana, sehemu ya 9 tafadhari naisubiria kwa hamu.
f8qmc5
Good 👍👍