Mzee Shayo alikuwa ameketi katika kiti chake huku akitingisha mguu wake ambao ulikuwa ndani ya kiatu cheusi chenye kung’aa sana. Mbele yake kulikuwa na picha halisi ya matukio yaliyokuwa yakiendelea kurindima, taarifa za Habari kutoka Aljazeera, DW, Sky News zilikuwa zikirusha kuhusu matukio yaliyokuwa yakiendelea Nchini humo. Pembezoni kulikuwa na bendera ndogo ya Tanzania iliyokuwa ikipeperushwa na upepo wa feni ya juu.
Chozi lilimbubujika Mzee Shayo, simu zake zilikuwa bize kuita lakini hakuzipokea sababu alikuwa katika msongo mzito wa mawazo.
Hadithi inaanzia katika Eneo la Majengo pacha, Posta Jijini Dar-es-salaam ilipo Benki kuu ya Tanzania, kutokana na hali ya machafuko ulinzi mkali unaimarishwa kuhakikisha hakutokei wizi wa aina yoyote ile, Gavana wa Benki hiyo aliyejulikana kama Profesa Maliki anafikiria kukiondoa kiasi kikubwa cha pesa kwa kutumia ndege ya Shirika la Emirates kuelekea Nchini Marekani.
Akiwa ofisini ndani ya Benki hiyo alijaribu kumpigia simu Mkuu wa kitengo cha Usalama wa Taifa aliyeitwa Ezekiel Shayo maarufu kama Mzee Shayo, simu yake haikupokelewa, taarifa aliyokuwa nayo Mzee Shayo wakati huo akiwa katika ofisi yake ya Usalama ilikuwa ni kutekwa kwa Jiji la Dodoma na kundi dogo la kigaidi lililofahamika kama ESS
“Bado hajapokea simu?” Aliuliza Waziri Mkuu wa Tanzania alipokuwa akizungumza na Profesa Maliki ili kuangalia uwezekano wa kuhamisha fedha hizo
“Hapokei simu yake, napata mashaka kama yupo hai au amekufa” Alijibu Gavana huyo huku kukiwa na taarifa kuwa majira ya Mchana Benki hiyo itavamiwa na kundi hilo la ESS ambalo lilikuwa likiongozwa na Mtu mmoja aliyefamika kwa jina moja tu la Chogo.
“Umezungumza na Waziri wa Ulinzi?” Aliuliza Waziri huyo aliyeitwa Jackson Ikuda
“Ndio, ameniongezea ulinzi hapa” alijibu Profesa Maliki kwa sauti iliyoonesha kuwa alikuwa ni mwenye kukata tamaa
“Andaa Magari hakikisha kiasi kikubwa cha fedha kinahamishwa hapo, naelekea Ikulu. Mengine nitakupa taarifa baada ya kuzungumza na Mkuu wa Nchi, ndege zipo tayali, kilichobaki ni wewe kuhamisha fedha tu” Alisema Waziri Jackson Ikuda.
Upande wa pili yaani kule ofisini kwa Mkuu wa Kitengo cha usalama wa Taifa kwa Mzee Shayo, alikuwa ameshasimama huku akiziangalia ‘Screen’ zilizo mbele yake, zilikuwa zikionesha baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar-es-salaam, Benki kuu ilikuwa ikionekana kwa kutumia kamera iliyopewa jina la Nyati.
“Upsss!” Aliwaza na kuwazua nini afanye ili kuhakikisha anazuia jaribio la kuvamiwa kwa Benki kuu ya Tanzania. Muda huo huo simu yake iliita akiwa ametumbua macho yake aliona ni namba ngeni ikiwa inaita, alitoka chumba cha kuongoza kamera alirudi ofisini kwake. Alijitupa kitini huku akiitafakari simu hiyo iliyopigwa kwa kodi za nje ya Nchi
“Hello!” Aliitika Mzee Shayo baada ya kuwa ameiweka simu sikioni huku kijasho chembamba kikiwa kinamtiririka, ilikuwa ni sauti iliyoonesha ukomavu wa maigizo sababu kiukweli Mzee Shayo pamoja na ukuu wake wa kitengo lakini hakuwahi kukumbana na nyakati ngumu kama hizi.
“Shayo!” Ilisikika sauti nzito kiasi iliyoambatana na uvutaji wa hewa kama vile alikuwa akivuta sigara, Mzee Shayo alikaa kimya kumsikiliza mpigaji ambaye alikuwa akiongea kwa kupangilia sana maneno yake.
“Nilikwambia kitengo hakiwezi kuzuia chochote nilichokipanga, sio jaribio tena baada ya kuliteka Jiji la Dodoma sasa ni zamu ya Dar-es-salaam” alisema Mwanaume huyo ambaye jina lake halikutajwa
“Wewe ni Nani na unataka nini hasa?” Alihoji Mzee Shayo huku akimuita msaidizi wake aweze kuangalia simu hiyo ilipigwa kutokea wapi.
“Shayo! Ni Mimi rafiki yako katika Ujenzi wa Taifa hili, Miezi kadhaa iliyopita nilikuwa nikikutumia Barua pepe kuwa Kitengo chako ni dhaifu sana mjiandae kwa kazi maalum!!” Alisema Jamaa huyo kisha alicheka sana
“Unahitaji nini sasa?” Aliuliza Mzee Shayo huku mkono wake ukiwa unatetemeka, msaidizi wa Mzee Shayo aliligundua hilo, hakuamini kama Mzee huyo alifikia ukomo wa kuweza kufikiria sababu alikuwa na sifa nyingi zilizotukuka ndani ya Taifa hili.
“Siku moja nitakupa hadithi ya kusisimua sana kabla hujafa Shayo! Naitwa Chogo” Alisema kisha alikata simu haraka, muda huo huo simu ya Chogo ilikuwa imefanikiwa kutambulika kuwa alikuwa akiongelea kutokea wapi lakini cha ajabu na kilichomshangaza na kumuogopesha Mzee Shayo, simu ya Chogo ilipigwa kutokea pale pale makao makuu ya Kitengo cha Usalama wa Taifa.
“Mkuu simu imepigwa hapa hapa kutoka chumba cha kuongoza Kamera za Jiji hili” Alisema msaidizi wa Mzee Shayo, haraka Mzee Shayo alikurupuka kuelekea chumba cha uongozaji wa Kamera hizo.
Pembezoni kwenye meza moja kulikuwa na simu juu yake, simu hiyo ilikuwa ikiita. Mzee Shayo aliifuata na kuiokota kisha aliipokea haraka, ilisikika sauti ya Chogo ikisema
“Nilikwambia kitengo chako ni dhaifu sana Mzee Shayo, Najiuliza kitengo kinachosimamia usalama wa Nchi kinakuwa legelege namna hiyo!” Alisema Chogo, haikujulikana huyo Chogo alikuwa ni nani na hata picha yake haikuweza kupatikana zaidi ya sauti ambayo ukiisikiliza vizuri utagundua ilikuwa imechezewa.
Haraka Mzee Shayo alipata wazo la kutazama Screen zilizokuwa zikionesha baadhi ya maeneo ya Jiji, simu ilikuwa hewani, akili yake ilifanya kazi mara mia zaidi ya uwezo wake wa kawaida
“Niwekee kamera Nyati haraka sana” Alisema Mzee Shayo huku akiwa amekata kinasa sauti kwenye simu hiyo alafu akakirudisha huku akiwa makini kuitazama kamera nyati, mara moja simu ilikatwa
“Rudisha nyuma rekodi ya Kamera nyati kwa dakika mbili zilizopita” Alisema Mzee Shayo baada ya kuanza kuhisi jambo, muda ambao alikuwa akizungumza na Chogo alikuwa akisikia sauti ya Pantoni, hivyo haraka alihisi Chogo alikuwa karibu na eneo la Benki kuu.
“Simamisha, vuta hiyo picha” Alisema Mzee Shayo baada ya kumuona Mtu aliyevalia koti la Njano akiwa anazungumza na simu huku akiwa amesimama mbele ya Benki hiyo.
“Ni nani huyo?” Aliuliza Mzee Shayo, haraka kitengo husika kilianza kazi ya kuifahamu sura hiyo ilikuwa ni sura ya Nani.
“Anaitwa Martin Gimbo mkazi wa Mkoa wa Arusha, miaka 34” Alisema Mtaalamu huyo huku akiwa anampatia picha Mzee Shayo
“Piga simu kwa Gavana wa Benki kuu profesa Maliki haraka sana kisha niwekee niongee naye” alisema Mzee Shayo akiwa ndani ya suti nyeusi, ya mikono mifupi maarufu kama Kaunda suti.
“Maliki, kuna Mtu ameingia hapo amevaa koti la njano, jinzi nyeusi, hakikisha anakamatwa haraka sana” Alisema Mzee Shayo, kabla hata Profesa Maliki hajajibu chochote zilisikika alamu kuashiria kuwa tayali kulikuwa na hali ya Hatari
“Tumevamiwa” alijibu Profesa Malikini kisha mawasiliano yalikatika.
“Ni yeye” Alisema Mzee Shayo huku akiwa anakuna macho yake.
“Weka kamera nyati kwenye kioo kikubwa” Alisema Mzee Shayo akionekana kupagawa kwa namna Benki kuu ilivyovamiwa na Mtu aliyeitwa Chogo. Muda huo huo simu iliita kwa Mzee Shayo, aliipokea, sauti iliyosikika ilikuwa ni sauti ya Chogo ikisema
“Nipo mahali ambapo utajiri wa Nchi unapatikana, ni muda wa kufanya nilichokwambia kwa Barua pepe zangu ambazo ulikuwa ukizipuuza” Alisema Chogo kisha alikata simu.
Maongezi yaliamuacha Mzee Shayo akiwa Hoi bin taabani, alirudi nyuma kisha aliketi kwenye kiti, ilikuwa ni majira ya saa 6 Mchana, Jiji la Dar-es-salaam lilizizima kwa muda mchache tu baada ya taarifa kuwa Benki kuu ya Tanzania ( BOT) imevamiwa na gaidi aliyeitwa Chogo, kupitia kamera nyati walifanikiwa kuliona gari jeupe likiingia ndani ya benki hiyo kupitia Geti la nyuma
“Mkuu gari hili si la Benki, ni gari spesho. Hapana shaka Magaidi ndio wanaingia” Alisema msaidizi wa Mzee Shayo!!
“Shika hatamu kwasasa hapa ndani Gibson, natoka mara moja” Alisema Mzee Shayo, aliondoka Kitengo cha Usalama wa Taifa akiwa ndani ya gari ndogo aina ya Subaru! Alipofika getini alisimama kisha alilitazama jengo la Usalama wa Taifa ambalo
lilikuwa chini huku juu yake kukiwa na kanisa la KKT, kitengo kilikuwa eneo la Kigamboni.
Kupitia daraja la Kigamboni, Mzee Shayo aliendesha Subaru kama yupo kwenye mbio za Magari, wakati huo Barabara zilikuwa nyeupe, Watu wengi waliogopa kupoteza uhai wao, walibakia majumbani mwao huku wachache wakiendelea kufanya safari, ilimuwezesha Mzee Shayo kufika Ikulu ya Magogoni haraka sana, alikuta ulinzi umeimarishwa hapo lakini alipowatazama Walinzi hao alijikuta akikata tamaa, aliona ni ngumu sana kupambana na huyo Mwanaume anayeitwa Chogo . Nini Kitaendelea
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
17 Comments
Haiyaaaaa , lakin admin story fupi sana et
Ila ch0g0 😆
Chogo kaxhawasha moto uko 🔥🔥🔥🔥
Daaaah
Chogo hachekesh🤣
Chogo uku kakiwasha aah
Chogo kama chogo
Mbn hujamalizia riwaya iliyopita admin
https://shorturl.fm/N6nl1
https://shorturl.fm/5JO3e
https://shorturl.fm/5JO3e
https://shorturl.fm/m8ueY
Shida stori inaanza sterling anakurupuka badala ya kutumia plan za kijasusi😀😀
Anyway ngoja tusubir mwendelezo huenda tukapata yaliyo mazur zaiz🔥🔥🔥
Let mambo
https://shorturl.fm/5JO3e
https://shorturl.fm/a0B2m
https://shorturl.fm/68Y8V