Mashindano ya TotalEnergies Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024 yameingia hatua ya mtoano, baada ya michezo ya mwisho ya makundi kumalizika kwa msisimko Jumanne usiku, na ratiba ya robo fainali kuthibitishwa.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya CAF, mashindano makubwa yanaandaliwa kwa pamoja na mataifa matatu ya Kenya, Tanzania na Uganda na yote matatu yamefuzu hatua ya robo fainali, jambo linalohakikisha tamasha la kandanda linaendelea kuvutia mashabiki kwa wingi.
Ufanisi wa pamoja wa wenyeji umelipa nguvu zaidi kaulimbiu ya mashindano haya βPamojaβ, huku Afrika Mashariki ikijiandaa kwa raundi nyingine ya viwanja vya kujaza na mashabiki wenye shauku kubwa.
Kenya Yaongoza Kundi A kwa Mara ya Kwanza
Harambee Stars ya Kenya imekuwa moja ya simulizi kubwa ya mashindano haya, baada ya kushangaza wengi katika kampeni yao ya kwanza ya CHAN na kuibuka vinara wa Kundi A.
Bao la dakika za mwisho la Ryan Ogam dhidi ya Zambia liliipa Kenya ushindi wa 1-0 na kuithibitishia nafasi ya kileleni wakiwa na pointi 10. Kikosi cha Benni McCarthy kimefungwa bao moja pekee katika mechi nne, kikidhihirisha nidhamu yao ya kiulinzi.
Sasa watabaki Nairobi kucheza dhidi ya Madagascar siku ya Ijumaa katika Uwanja wa Moi International Sports Centre Kasarani. Wakiwa na sapoti ya nyumbani na morali ya ushindi, Kenya imebadilika haraka kutoka kuwa wanyonge hadi kuwa wapinzani hatari.
Tanzania Yaibuka Kinara Kundi B
Taifa Stars ya Tanzania pia imemaliza kileleni, ikikusanya pointi 10 katika Kundi B. Wameonyesha kandanda la kuvutia kwa kushinda mechi tatu na kutoka sare moja, wakionesha ubora wa kushambulia na uthabiti. Mchezo pekee walioteleza ulikuwa ni dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambao haukuwa na maana kwa nafasi yao ya kufuzu.
Watakabiliana na Morocco Ijumaa usiku jijini Dar es Salaam, mechi ambayo inatarajiwa kuwa ngumu zaidi kwenye raundi hii. Atlas Lions, mabingwa mara mbili wa CHAN, walimaliza nafasi ya pili Kundi A nyuma ya Kenya.
Uganda Yaivunja Laana
Baada ya kushindwa mara sita mfululizo kufuzu hatua ya mtoano, Uganda hatimaye imefika robo fainali za CHAN. Sare ya kusisimua ya 3-3 dhidi ya Afrika Kusini jijini Kampala iliwatosha kuongoza Kundi C wakiwa na pointi 7. Penalti ya dakika za nyongeza ya Rogers Torach ilisababisha shangwe kubwa katika Uwanja wa Kitaifa wa Mandela.
Uganda itachuana na Senegal Jumamosi usiku, mchezo unaotarajiwa kuvutia idadi kubwa ya mashabiki kuliko mechi yoyote nyingine ya mashindano haya.
Kundi D Lamalizika Zanzibar
Huko Zanzibar, Sudan na Senegal walitoka sare tasa ya 0-0 iliyowaweka wote katika hatua ya robo fainali. Sudan, chini ya kocha Kwesi Appiah, walimaliza kileleni kwa tofauti ya mabao, huku mabingwa watetezi Senegal wakiridhika na nafasi ya pili.
Sudan watabaki Zanzibar kucheza dhidi ya Algeria Jumamosi alasiri, huku Senegal wakielekea Kampala kwa pambano lao la robo fainali dhidi ya Uganda.
Ratiba ya Robo Fainali
Ijumaa, 22 Agosti 2025
- Kenya π Madagascar β Saa 11:00 jioni, Uwanja wa Moi International Sports Centre, Nairobi
- Tanzania π Morocco β Saa 2:00 usiku, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam
Jumamosi, 23 Agosti 2025
- Sudan π Algeria β Saa 11:00 jioni, Uwanja wa Amaan, Zanzibar City
- Uganda π Senegal β Saa 2:00 usiku, Uwanja wa Mandela National, Kampala
SOMA RIWAYA HAPAΒ :Β Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)
2 Comments
Kazi iendeleeπ¨βπ» nikutakie field
ar272i