Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Tisa (09)
    Hadithi

    Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Tisa (09)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 21, 2024Updated:October 28, 202411 Comments9 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Ndiyo! Unapaswa kukubali kuolewa na Osman ili apone naΒ  afanyiwe upasuaji wa kupandikiza figo” Mama alirudia kauliΒ  yake, akili yangu ilihama na kumuwaza Mosses, manenoΒ  aliyoyasema wakati naondoka kwake, achilia mapenzi yanguΒ  kwakeΒ 

    “Mama naweza vipi kuolewa na Osman, siyo chaguo langu lile,Β  wala siyo aina ya Mwanaume ninayemtaka katika Maisha yangu,Β  Mama nina Mtu wangu….Siwezi” Nilisema huku nikiwa ninalia,Β  chozi lilikuwa likinivuja. EndeleaΒ 

    SEHEMU YA TISA

    Aliingia Bilionea Dhabi, alitukuta tukiwa katikati yaΒ  maongezi yetu. Mzee Dhabi aliponiona alitabasamu tuu, alikuwaΒ  ameongozana na Mke wake ambaye ni Mama Mzazi wa Osman,Β  Alinisogelea kisha aliniambiaΒ 

    “Jacklin! Hujakosea, upo sahihi, ni ngumu sana kuolewa naΒ  Mwanaume ambaye hayupo ndani ya moyo wako, upo sahihi sababuΒ  huwezi ndiyo maana uliondoka jana Usiku. Lakini Jacklin, hebuΒ  tazama macho ya Mama yake Osman, ona lile chozi kwanza”Β  Niligeuza macho yangu kumtazama Mama yake Osman, Ni kweliΒ  alikuwa akivuja mchoziΒ 

    “Analia kwasababu Osman ni Mtoto wake wa kipekee, hana MtotoΒ  mwingine kama ulivyo wewe kwa Mama yako, lile chozi ndiloΒ  ambalo Mama yako alikuwa akilia wakati alipopoteza tumaini laΒ  wewe kuishi. Unakumbuka kilichotokea, Mungu alimleta OsmanΒ  katika Maisha yako, alipambana hata kutoa figo lake iliΒ  upone, hakufanya kwa ajili ya mapenzi bali kwa huruma yakeΒ  kwa Mama yako, ulilala Jacklin hukumuona Mama yako alivyokuwaΒ  anahangaika hata kutaka kutoa figo lake akuwekee wewe”Β  Bilionea Dhabi alizungumza maneno mazito sana ambayoΒ  yalimfanya Mama ajiinamie akiwa analiaΒ 

    “Nakuomba sana Jacklin, okoa Maisha ya Mwanangu, hatuna MtotoΒ  mwingine zaidi yake, Osman ndiye Maisha yetu, kufa au kuponaΒ  kwa Osman kunakutegemea wewe Jacklin” Alisema Mzee DhabiΒ  kisha alienda kuketi kando ya Mke wake, maneno yakeΒ  yalinifanya nishindwe kuendelea kuketi pale sebleniΒ  nilikimbilia chumbani kwangu. Ni kweli Osman alijitoa naΒ  kuhakikisha Maisha yangu yanarudi, tumaini la Mama yanguΒ  linarudi, leo yupo Kitndani na Mimi ndiye ninayepaswaΒ  kumuamsha, Daaah roho iliniuma sana.Β 

    “Usilie Mama Jacklin, Binti yako ni Mtu mzima anajuwaΒ  anachokifanya. Kama amekataa kumsaidia Osman hakuna njiaΒ  nyingine tutaondoka naye kuelekea Dubai tukajaribu huko,Β  ikishindikana basi haikuwa ridhki yetu kuwa na Osman” AlisemaΒ  Baba yake Osman, Mama yake Osman alikuwa akilia huku akiwaΒ  amejifunika na kitambaa alishindwa hata kusema chochote, MamaΒ  yangu alinyanyuka na kunifuata chumbani, alinikuta nikiwaΒ  nimeshikilia simu yangu, alisogea kisha aliketi kando yanguΒ  kwa upole sana alisemaΒ 

    “Jacklin Mwanangu! Nilikuzaa na kukulea katika Mazingira yaΒ  kujuwa nini Maana ya utu na shida, pengine ndiyo nguvuΒ  iliyomvuta Osman kuja kwenye Maisha yako, alikuja kama MasiaΒ  akaokoa Maisha yako, leo amegeuka kikwazo cha furaha yako.Β  Nikiwa kama Mama yako nakueleza jinsi ninavyojisikia Jacklin”Β  Alisema Mama kisha alifikicha jicho lake moja ambalo lilikuwaΒ  likimwaga chozi

    “Moyo wangu umevunjika Jacklin, furaha imenitoweka kamaΒ  Kizimikavyo kibatari wakati wa upepo Mkali, Jacklin Mama yakoΒ  nimeumia sana. Siku Osman akiondoka hapa Duniani ndiyoΒ  itakuwa mwisho wako kusikia sauti yangu, yule KijanaΒ  alirudisha tumaini kwenye moyo wangu, alinifanya nijisikieΒ  amani sana lakini leo umeiondoa yote” Mama alisema,Β  nilitamani kumjibu na Kumwambia kuwa kama nitaolewa na OsmanΒ  basi Mosses atasambaza video zangu za faragha, hadi MamaΒ  anaondoka chumbani kwangu mdomo wangu ulikuwa mzito sana kamaΒ  samaki aliyejaza maji mengiΒ 

    Niliangalia ujumbe ambao Mosses aliutuma, alikuwaΒ  akinikumbusha kuwa endapo nitamuacha atasambaza hizo video,Β  nilivujisha chozi machoni mwangu. Yalikuwa ni maumivu makaliΒ  sana ambayo hata sikuwahi kuyahisi katika Maisha yangu.Β  Nilipaswa kuokoa Maisha ya Osman kama ambavyo aliokoa yanguΒ  ila ningefanya kitu gani? Kama video zitasambaa naweza hataΒ  kujitoa uhai kukwepa aibu nzito lakini je Mama yangu MzaziΒ  akiziona video hizo naye atakuwa katika hali gani? VipiΒ  Familia ya Osman itajisikia vipi, ndio maana nasema kilikuwaΒ  ni kipindi kizito na kigumu kwangu.Β 

    Mama aliporudi Sebleni hakuwakuta Baba na Mama yake Osman,Β  aliangusha kilio kama kuna Mtu amefariki, nilishtuka naΒ  niliumia sana. Nyumba ilikosa ile amani iliyokuwepo Mwanzo,Β  ukimya ulitawala hakuna aliyetoa neno lolote zaidi ya sautiΒ  za kufungwa na kufunguliwa kwa milango. Nilijitupa kitandaniΒ  nikawaza sana nifanye jambo gani ili kumsaida Osman bilaΒ  kuchukua uamuzi ambao ungesababisha kusambaa kwa video hizoΒ  za faragha. Kadili nilivyokuwa natulia kitandani ndivyo pichaΒ  ya tukio la kukataa kuvishwa pete na Osman lilivyokuwaΒ  linajirudia katika akili yangu, nilikosa utulivu kama MtuΒ  anayesumbuliwa na mizimu, niliamka bado Mama alikuwaΒ  akiendelea kulia, nikiwa kama Mtoto nilijivuta kwendaΒ  kumbembeleza.Β 

    Nilimkuta akiwa amekaa chini ameegemea sofa, niliketi kwaΒ  adabu na utulivu mkubwa sana, Mama alihisi ujio wanguΒ  alitulia kimya huku akihema sana. Nilishusha pumzi zanguΒ  kisha nilisemaΒ 

    “Samahani Mama najuwa nimekuvunja moyo ila..” Kabla hataΒ  sijamaliza nilichokitaka kukisema Mama alinikatishaΒ 

    “Ishia hapo hapo Jacklin, Wazazi ambao Mtoto wao aliokoa uhaiΒ  wako wameondoka kwasababu umekataa kuokoa uhai wa Mtoto wao,Β  nimeonekana Mama mbaya sana, Mama mbinafsi ambaye hajaliΒ  kuhusu Mtoto wa mwingine” Alisema Mama kisha aliendelea

    “Kama Osman atakufa basi juwa ni kwasababu yako, hupaswiΒ  kusameheka katika hilo Jacklin” Alimaliza kusema kishaΒ  alinyanyuka na kwenda zake chumbani kwake, choziΒ  lilinimwagika Mimi Jacklin niliona kila Kiti kipo dhidiΒ  yangu, sikuwa na Mtu wa kunisemea kabisa.Β 

    Usiku ulipofika niliondoka nyumbani nilienda kulala Hotelini,Β  nilihitaji muda wa kuwa peke yangu ili niweze kutafakariΒ  mambo kwa umakini zaidi. Nilizima simu zangu ili nisipateΒ  usumbufu wowote ule, hakuna aliyejuwa niko wapi, Si MossesΒ  wala Mama yangu niliyemwambia, nilitaka kutafakari ili nijuweΒ  nafanya nini katika kipindi kigumu kama hiki.Β 

    Hali ya Osman haikuwa nzuri kabisa kule Hospitalini, alikuwaΒ  kila azindukapo anataja jina langu tu, alikuwa anachomwaΒ  sindano za usingizi ili kumtuliza. Familia ya Bilionea DhabiΒ  iliingia gizani, tumaini lao juu yangu liliondoka kabisa,Β  wakiwa nyumbani kwao Mke wa Bilionea Dhabi alimwambia MumeΒ  wakeΒ 

    “Twende kwa mara ya mwisho kuzungumza na Jacklin kamaΒ  atakataa kwa kinywa chake basi hatutokuwa na namna nyingineΒ  bali kuondoka na Osman” Alisema kwa sauti ya Kimama iliyojaaΒ  maumivu ya kumuona Mtoto wake akiwa kitandani na hana tumainiΒ  lolote lileΒ 

    “Sasa hata kama tutafanya hivyo Mama Osman, Binti haweziΒ  badili msimamo wake, hampendi Osman na hilo lipo wazi sana”Β  Alijibu Baba yake Osman, Mara mlango uligongwaΒ 

    “Ingia” Alisema Bilionea Dhabi baada ya kumtambua aliyekuwaΒ  akigonga, alikuwa ni MlinziΒ 

    “Samahani Baba na Mama, kuna mgeni hapo nje anasema anahitajiΒ  kuonana na Osman” Alisema Mlinzi huyo baada ya kuwa tayariΒ  ameingia ndani, Mzee Dhabi aliangalia saa yake aliona niΒ  mishale ya saa 4 za Usiku alimuuliza MlinziΒ 

    “Huyo Mtu yupoje?”Β 

    “Mwanamke, mweupe” Alisema Mlinzi kisha alitabasamu tu baadaΒ  ya alichotaka kukisema kuhisi hakina maana hapo mbele ya MzeeΒ  Dhabi na Mke wake lakini Mzee Dhabi alimuelewa MlinziΒ  akamrahisishiaΒ 

    “Mzuri Eeh” Basi mlinzi alitoa tabasamu zitoΒ 

    “Mh! Atakuwa Nani huyo!” Alisema Bilionea Dhabi kishaΒ  alitafakari

    “Utamjuwa vipi bila kumuona, Mlete” Alidakia Mke wa MzeeΒ  Dhabi. Mara moja Mlinzi aliondoka, dakika moja baadayeΒ  alirudi akiwa ameambatana na Mgeni huyoΒ 

    Mzee Dhabi na Mke wake walisimama kwa Mshangao Mkubwa sanaΒ  baada ya kumuona Mgeni huyo kisha Mzee Dhabi alisemaΒ 

    “Mlinzi nenda” Mlinzi aliondoka zakeΒ 

    • β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’Β 

    “Zahra?”Β 

    “Zahra?” Mzee Dhabi na Mke wake alisema kwa pamoja baada yaΒ  kumuona Zahra mbele yao, Si unamkumbuka Zahra? Ni yuleΒ  Mwanamke aliyechota kiasi kikubwa cha pesa na kutimkia zakeΒ  Ughaibuni, alikuwa ni mpenzi wa Osman ambaye aliuteka moyo waΒ  Osman miezi kadhaa iliyopita aliondoka na kusema kuwa anaΒ  Mwanaume mwingine hivyo Osman asihangaike kumtafuta, tukioΒ  hilo lilisababisha Osman kupata Mshituko na kukimbizwaΒ  Hospitalini.Β 

    Zahra alishtuka kuwaona Wazazi wa Osman, alitetemeka kwa HofuΒ 

    “Hebu keti” Alisema Mzee Dhabi, wote waliketi kisha MzeeΒ  Dhabi na Mke wake walitazamanaΒ 

    “Ni wewe Zahra au tunaota ndoto ya Mchana?” Aliuliza MamaΒ  yake OsmanΒ 

    “Ni Mimi Mama naomba msamaha wenu kwa kila kilichotokea,Β  natamani kumuomba msamaha Osman na ndiyo sababu ya kuja hapa”Β  Alisema ZahraΒ 

    “Unataka kumuomba Msamaha Osman?”Β 

    “Ndiyo Baba! Najuta kwa kila nilichomfanyia.Β 

    “Nifuate” Alisema Mzee Dhabi, walitoka ndani Bilionea DhabiΒ  na Zahra, waliingia kwenye gari ya kifahari ya Mzee huyoΒ  kisha safari ilianza, Zahra hakujuwa alikuwa akipelekwa wapiΒ 

    “Baba tunaenda wapi?” Alihoji ZahraΒ 

    “Si umesema unataka kumuomba msamaha Osman? ”Β 

    “Ndiyo Baba”Β 

    “Tunaenda alipo Osman”

    Usiku huo nilikuwa nimeamua jambo moja, kumsaidia OsmanΒ  kwasababu alisaidia Maisha yangu, akili yangu iliniambia kuwaΒ  Osman alikuwa mwenye huruma na mapenzi ya kweli kuliko MossesΒ  ambaye alianza kutishia kusambaza video zangu za Faragha.Β  Niliondoka Hotelini nikaelekea nyumbani, NilipochunguliaΒ  ndani nilimuona Mama akiwa amekaa kando ya Mlango waΒ  kuingilia ndani nilijuwa tu alikuwa akinitafuta japoΒ  alinichunia, nilitabasamu sababu Mama yangu alikuwa ni MamaΒ  mwenye upendo wa Hali ya juu sana kwangu, nilifuangua geti,Β  nilitupa macho upande wa kushoto nililiona lile gariΒ  aliloninunulia Osman kwenye siku yangu ya Kuzaliwa, moyoΒ  uliniuma sana.Β 

    Nilisogea alipo Mama kisha nilimwambiaΒ 

    “Mama nipeleke Hospitalini alipo Osman” Kauli yangu ilimfanyaΒ  Mama anitazame mara mbili mbiliΒ 

    “Mama moyo wangu unaniambia tufanye haraka sana” NilisemaΒ  nikiwa kwenye hali ya Haraka, lilikuwa ni jambo ambalo MamaΒ  alikuwa akilisubiria. Haraka alikimbilia ndani akatoka naΒ  mtandio, tulitoka tukachukua Tax kisha safari ya kuelekeaΒ  Hospitali ilianza.Β 

    Upande wa pili, Baba Osman na Zahra walikuwa wanaingiaΒ  Hospitalini, walisogeza gari kwenye maegesho kisha walielekeaΒ  Wodini ambako Osman alikuwepoΒ 

    “Baba Osman anaumwa? Mbona umenileta Hospitalini?” AliulizaΒ  ZahraΒ 

    “Ndiyo Osman ni Mgonjwa sana ndiyo maana nimekuleta hapaΒ  Zahra” Alijibu Baba Osman, walishuka kisha walielekea ilipoΒ  wodi hiyo. Bahati nzuri walikutana na Dokta Simon ambayeΒ  alikuwa akitoka wodini humo, alipomuona Zahra alishangaa sanaΒ 

    “Najuwa una maswali mengi Simon lakini hiyo ndiyo haliΒ  halisi” alielezea Mzee Dhabi baada ya kuisoma sura ya DoktaΒ  Simon ilivyokuwaΒ 

    “Lakini Mzee, Osman hapaswi kushtushwa na jambo lingineΒ  mnaweza kumpoteza kabisa, kwanini aje leo?”Β 

    “Maswali yako Simon hayawezi kujibiwa kwasasa, nina imani naΒ  hiki atakachokiona Osman” Aliesema Mzee DhabiΒ 

    “Lakini sikushauri kabisa kwenda huko Mzee Kwasasa yupo MachoΒ  angalau anajisikia vizuri mgesubiria kidogo basi” alisemaΒ  Dokta Simon

    “Mimi ni Baba yake Osman, najuwa nini nafanya Simon….TwendeΒ  Binti” Alisema Mzee Dhabi akiwa amemshika mkono Zahra,Β  waliingia wodini bila kusikiliza alichokisema Dokta SimonΒ 

    Kitendo cha kufungua mlango kilihamisha macho ya Osman,Β  aligeuza na kuangalia aliposikia sauti ya Mlango kufunguliwa.Β  Alitoa macho yake, alijaza hewa kwenye kifua baada ya kumuonaΒ  Zahra Mwanamke ambaye alimfanya ayachukie Mapenzi, MwanmkeΒ  ambaye alimtafuta sana Ughaibuni bila Mafanikio.Β 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI Ya PUMZI YA MWISHO

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ 

    Β Β 

    Pumzi ya mwisho

    11 Comments

    1. Aguero on October 21, 2024 5:06 pm

      https://whatsapp.com/channel/0029VarTsGt1t90TiJVyWi0J

      Reply
    2. RickkyHarry on October 21, 2024 5:17 pm

      Dah toa nyingine ata usiku wa leo😭😭

      Reply
    3. Sir yowas on October 21, 2024 5:23 pm

      Nimepumua baada ya kumaliza kusoma

      Reply
    4. Roda on October 21, 2024 6:06 pm

      Dah naona kesho mbal tuendeleee hadith imejoga sasa apo kwa akili ya haraka haraka julieth akimuona zarha atagoma ten kumhudumia osman 🀞🀞🀞uwiiiiiiiiiiii hadith tam nyie πŸ’”πŸ’”πŸ’”πŸ’”πŸ’”πŸ’”πŸ€•πŸ€•πŸ€•πŸ€•πŸ€•NATAFTA MPENZ KAMA OSMANπŸ€•

      Reply
    5. Chamalo on October 21, 2024 6:55 pm

      Lete mbili juzi uliruka

      Reply
    6. Calvin paul on October 21, 2024 8:18 pm

      Mshtuko umuue osman wazazi wa osman wamfukuze jack moses amuache jack mama yake ammchukie hyo pumzi itakuwa ya mwsho

      Reply
      • Themanini on October 21, 2024 9:02 pm

        Mtunzi apewe maua yake πŸ’ 🌹

        Reply
    7. Sabitimussa23 on October 21, 2024 9:44 pm

      Jmn wanawake!!! πŸ€”πŸ€” khaa

      Reply
    8. Elijahh on October 22, 2024 8:12 am

      Sehemu ya nane IPO wapi

      Reply
    9. πŸ”‹ Message; Operation 1,563140 bitcoin. Receive > https://yandex.com/poll/WDrLYhyq1Mc7jMHFgAW85q?hs=7c6499f0a696868c72ae6119e22c7be5& πŸ”‹ on June 4, 2025 2:26 pm

      gu8eva

      Reply
    10. πŸ“ Message- TRANSACTION 1,850337 BTC. GET >> https://yandex.com/poll/enter/12JSER8t8KDJewYyTprg7K?hs=7c6499f0a696868c72ae6119e22c7be5& πŸ“ on June 17, 2025 5:09 am

      wwyvk2

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneΒ  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.