Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 05

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Tisa (09)
    Hadithi

    Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Tisa (09)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 21, 2024Updated:October 28, 202411 Comments9 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Ndiyo! Unapaswa kukubali kuolewa na Osman ili apone naย  afanyiwe upasuaji wa kupandikiza figo” Mama alirudia kauliย  yake, akili yangu ilihama na kumuwaza Mosses, manenoย  aliyoyasema wakati naondoka kwake, achilia mapenzi yanguย  kwakeย 

    “Mama naweza vipi kuolewa na Osman, siyo chaguo langu lile,ย  wala siyo aina ya Mwanaume ninayemtaka katika Maisha yangu,ย  Mama nina Mtu wangu….Siwezi” Nilisema huku nikiwa ninalia,ย  chozi lilikuwa likinivuja. Endeleaย 

    SEHEMU YA TISA

    Aliingia Bilionea Dhabi, alitukuta tukiwa katikati yaย  maongezi yetu. Mzee Dhabi aliponiona alitabasamu tuu, alikuwaย  ameongozana na Mke wake ambaye ni Mama Mzazi wa Osman,ย  Alinisogelea kisha aliniambiaย 

    “Jacklin! Hujakosea, upo sahihi, ni ngumu sana kuolewa naย  Mwanaume ambaye hayupo ndani ya moyo wako, upo sahihi sababuย  huwezi ndiyo maana uliondoka jana Usiku. Lakini Jacklin, hebuย  tazama macho ya Mama yake Osman, ona lile chozi kwanza”ย  Niligeuza macho yangu kumtazama Mama yake Osman, Ni kweliย  alikuwa akivuja mchoziย 

    “Analia kwasababu Osman ni Mtoto wake wa kipekee, hana Mtotoย  mwingine kama ulivyo wewe kwa Mama yako, lile chozi ndiloย  ambalo Mama yako alikuwa akilia wakati alipopoteza tumaini laย  wewe kuishi. Unakumbuka kilichotokea, Mungu alimleta Osmanย  katika Maisha yako, alipambana hata kutoa figo lake iliย  upone, hakufanya kwa ajili ya mapenzi bali kwa huruma yakeย  kwa Mama yako, ulilala Jacklin hukumuona Mama yako alivyokuwaย  anahangaika hata kutaka kutoa figo lake akuwekee wewe”ย  Bilionea Dhabi alizungumza maneno mazito sana ambayoย  yalimfanya Mama ajiinamie akiwa analiaย 

    “Nakuomba sana Jacklin, okoa Maisha ya Mwanangu, hatuna Mtotoย  mwingine zaidi yake, Osman ndiye Maisha yetu, kufa au kuponaย  kwa Osman kunakutegemea wewe Jacklin” Alisema Mzee Dhabiย  kisha alienda kuketi kando ya Mke wake, maneno yakeย  yalinifanya nishindwe kuendelea kuketi pale sebleniย  nilikimbilia chumbani kwangu. Ni kweli Osman alijitoa naย  kuhakikisha Maisha yangu yanarudi, tumaini la Mama yanguย  linarudi, leo yupo Kitndani na Mimi ndiye ninayepaswaย  kumuamsha, Daaah roho iliniuma sana.ย 

    “Usilie Mama Jacklin, Binti yako ni Mtu mzima anajuwaย  anachokifanya. Kama amekataa kumsaidia Osman hakuna njiaย  nyingine tutaondoka naye kuelekea Dubai tukajaribu huko,ย  ikishindikana basi haikuwa ridhki yetu kuwa na Osman” Alisemaย  Baba yake Osman, Mama yake Osman alikuwa akilia huku akiwaย  amejifunika na kitambaa alishindwa hata kusema chochote, Mamaย  yangu alinyanyuka na kunifuata chumbani, alinikuta nikiwaย  nimeshikilia simu yangu, alisogea kisha aliketi kando yanguย  kwa upole sana alisemaย 

    “Jacklin Mwanangu! Nilikuzaa na kukulea katika Mazingira yaย  kujuwa nini Maana ya utu na shida, pengine ndiyo nguvuย  iliyomvuta Osman kuja kwenye Maisha yako, alikuja kama Masiaย  akaokoa Maisha yako, leo amegeuka kikwazo cha furaha yako.ย  Nikiwa kama Mama yako nakueleza jinsi ninavyojisikia Jacklin”ย  Alisema Mama kisha alifikicha jicho lake moja ambalo lilikuwaย  likimwaga chozi

    “Moyo wangu umevunjika Jacklin, furaha imenitoweka kamaย  Kizimikavyo kibatari wakati wa upepo Mkali, Jacklin Mama yakoย  nimeumia sana. Siku Osman akiondoka hapa Duniani ndiyoย  itakuwa mwisho wako kusikia sauti yangu, yule Kijanaย  alirudisha tumaini kwenye moyo wangu, alinifanya nijisikieย  amani sana lakini leo umeiondoa yote” Mama alisema,ย  nilitamani kumjibu na Kumwambia kuwa kama nitaolewa na Osmanย  basi Mosses atasambaza video zangu za faragha, hadi Mamaย  anaondoka chumbani kwangu mdomo wangu ulikuwa mzito sana kamaย  samaki aliyejaza maji mengiย 

    Niliangalia ujumbe ambao Mosses aliutuma, alikuwaย  akinikumbusha kuwa endapo nitamuacha atasambaza hizo video,ย  nilivujisha chozi machoni mwangu. Yalikuwa ni maumivu makaliย  sana ambayo hata sikuwahi kuyahisi katika Maisha yangu.ย  Nilipaswa kuokoa Maisha ya Osman kama ambavyo aliokoa yanguย  ila ningefanya kitu gani? Kama video zitasambaa naweza hataย  kujitoa uhai kukwepa aibu nzito lakini je Mama yangu Mzaziย  akiziona video hizo naye atakuwa katika hali gani? Vipiย  Familia ya Osman itajisikia vipi, ndio maana nasema kilikuwaย  ni kipindi kizito na kigumu kwangu.ย 

    Mama aliporudi Sebleni hakuwakuta Baba na Mama yake Osman,ย  aliangusha kilio kama kuna Mtu amefariki, nilishtuka naย  niliumia sana. Nyumba ilikosa ile amani iliyokuwepo Mwanzo,ย  ukimya ulitawala hakuna aliyetoa neno lolote zaidi ya sautiย  za kufungwa na kufunguliwa kwa milango. Nilijitupa kitandaniย  nikawaza sana nifanye jambo gani ili kumsaida Osman bilaย  kuchukua uamuzi ambao ungesababisha kusambaa kwa video hizoย  za faragha. Kadili nilivyokuwa natulia kitandani ndivyo pichaย  ya tukio la kukataa kuvishwa pete na Osman lilivyokuwaย  linajirudia katika akili yangu, nilikosa utulivu kama Mtuย  anayesumbuliwa na mizimu, niliamka bado Mama alikuwaย  akiendelea kulia, nikiwa kama Mtoto nilijivuta kwendaย  kumbembeleza.ย 

    Nilimkuta akiwa amekaa chini ameegemea sofa, niliketi kwaย  adabu na utulivu mkubwa sana, Mama alihisi ujio wanguย  alitulia kimya huku akihema sana. Nilishusha pumzi zanguย  kisha nilisemaย 

    “Samahani Mama najuwa nimekuvunja moyo ila..” Kabla hataย  sijamaliza nilichokitaka kukisema Mama alinikatishaย 

    “Ishia hapo hapo Jacklin, Wazazi ambao Mtoto wao aliokoa uhaiย  wako wameondoka kwasababu umekataa kuokoa uhai wa Mtoto wao,ย  nimeonekana Mama mbaya sana, Mama mbinafsi ambaye hajaliย  kuhusu Mtoto wa mwingine” Alisema Mama kisha aliendelea

    “Kama Osman atakufa basi juwa ni kwasababu yako, hupaswiย  kusameheka katika hilo Jacklin” Alimaliza kusema kishaย  alinyanyuka na kwenda zake chumbani kwake, choziย  lilinimwagika Mimi Jacklin niliona kila Kiti kipo dhidiย  yangu, sikuwa na Mtu wa kunisemea kabisa.ย 

    Usiku ulipofika niliondoka nyumbani nilienda kulala Hotelini,ย  nilihitaji muda wa kuwa peke yangu ili niweze kutafakariย  mambo kwa umakini zaidi. Nilizima simu zangu ili nisipateย  usumbufu wowote ule, hakuna aliyejuwa niko wapi, Si Mossesย  wala Mama yangu niliyemwambia, nilitaka kutafakari ili nijuweย  nafanya nini katika kipindi kigumu kama hiki.ย 

    Hali ya Osman haikuwa nzuri kabisa kule Hospitalini, alikuwaย  kila azindukapo anataja jina langu tu, alikuwa anachomwaย  sindano za usingizi ili kumtuliza. Familia ya Bilionea Dhabiย  iliingia gizani, tumaini lao juu yangu liliondoka kabisa,ย  wakiwa nyumbani kwao Mke wa Bilionea Dhabi alimwambia Mumeย  wakeย 

    “Twende kwa mara ya mwisho kuzungumza na Jacklin kamaย  atakataa kwa kinywa chake basi hatutokuwa na namna nyingineย  bali kuondoka na Osman” Alisema kwa sauti ya Kimama iliyojaaย  maumivu ya kumuona Mtoto wake akiwa kitandani na hana tumainiย  lolote lileย 

    “Sasa hata kama tutafanya hivyo Mama Osman, Binti haweziย  badili msimamo wake, hampendi Osman na hilo lipo wazi sana”ย  Alijibu Baba yake Osman, Mara mlango uligongwaย 

    “Ingia” Alisema Bilionea Dhabi baada ya kumtambua aliyekuwaย  akigonga, alikuwa ni Mlinziย 

    “Samahani Baba na Mama, kuna mgeni hapo nje anasema anahitajiย  kuonana na Osman” Alisema Mlinzi huyo baada ya kuwa tayariย  ameingia ndani, Mzee Dhabi aliangalia saa yake aliona niย  mishale ya saa 4 za Usiku alimuuliza Mlinziย 

    “Huyo Mtu yupoje?”ย 

    “Mwanamke, mweupe” Alisema Mlinzi kisha alitabasamu tu baadaย  ya alichotaka kukisema kuhisi hakina maana hapo mbele ya Mzeeย  Dhabi na Mke wake lakini Mzee Dhabi alimuelewa Mlinziย  akamrahisishiaย 

    “Mzuri Eeh” Basi mlinzi alitoa tabasamu zitoย 

    “Mh! Atakuwa Nani huyo!” Alisema Bilionea Dhabi kishaย  alitafakari

    “Utamjuwa vipi bila kumuona, Mlete” Alidakia Mke wa Mzeeย  Dhabi. Mara moja Mlinzi aliondoka, dakika moja baadayeย  alirudi akiwa ameambatana na Mgeni huyoย 

    Mzee Dhabi na Mke wake walisimama kwa Mshangao Mkubwa sanaย  baada ya kumuona Mgeni huyo kisha Mzee Dhabi alisemaย 

    “Mlinzi nenda” Mlinzi aliondoka zakeย 

    • โ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขย 

    “Zahra?”ย 

    “Zahra?” Mzee Dhabi na Mke wake alisema kwa pamoja baada yaย  kumuona Zahra mbele yao, Si unamkumbuka Zahra? Ni yuleย  Mwanamke aliyechota kiasi kikubwa cha pesa na kutimkia zakeย  Ughaibuni, alikuwa ni mpenzi wa Osman ambaye aliuteka moyo waย  Osman miezi kadhaa iliyopita aliondoka na kusema kuwa anaย  Mwanaume mwingine hivyo Osman asihangaike kumtafuta, tukioย  hilo lilisababisha Osman kupata Mshituko na kukimbizwaย  Hospitalini.ย 

    Zahra alishtuka kuwaona Wazazi wa Osman, alitetemeka kwa Hofuย 

    “Hebu keti” Alisema Mzee Dhabi, wote waliketi kisha Mzeeย  Dhabi na Mke wake walitazamanaย 

    “Ni wewe Zahra au tunaota ndoto ya Mchana?” Aliuliza Mamaย  yake Osmanย 

    “Ni Mimi Mama naomba msamaha wenu kwa kila kilichotokea,ย  natamani kumuomba msamaha Osman na ndiyo sababu ya kuja hapa”ย  Alisema Zahraย 

    “Unataka kumuomba Msamaha Osman?”ย 

    “Ndiyo Baba! Najuta kwa kila nilichomfanyia.ย 

    “Nifuate” Alisema Mzee Dhabi, walitoka ndani Bilionea Dhabiย  na Zahra, waliingia kwenye gari ya kifahari ya Mzee huyoย  kisha safari ilianza, Zahra hakujuwa alikuwa akipelekwa wapiย 

    “Baba tunaenda wapi?” Alihoji Zahraย 

    “Si umesema unataka kumuomba msamaha Osman? ”ย 

    “Ndiyo Baba”ย 

    “Tunaenda alipo Osman”

    Usiku huo nilikuwa nimeamua jambo moja, kumsaidia Osmanย  kwasababu alisaidia Maisha yangu, akili yangu iliniambia kuwaย  Osman alikuwa mwenye huruma na mapenzi ya kweli kuliko Mossesย  ambaye alianza kutishia kusambaza video zangu za Faragha.ย  Niliondoka Hotelini nikaelekea nyumbani, Nilipochunguliaย  ndani nilimuona Mama akiwa amekaa kando ya Mlango waย  kuingilia ndani nilijuwa tu alikuwa akinitafuta japoย  alinichunia, nilitabasamu sababu Mama yangu alikuwa ni Mamaย  mwenye upendo wa Hali ya juu sana kwangu, nilifuangua geti,ย  nilitupa macho upande wa kushoto nililiona lile gariย  aliloninunulia Osman kwenye siku yangu ya Kuzaliwa, moyoย  uliniuma sana.ย 

    Nilisogea alipo Mama kisha nilimwambiaย 

    “Mama nipeleke Hospitalini alipo Osman” Kauli yangu ilimfanyaย  Mama anitazame mara mbili mbiliย 

    “Mama moyo wangu unaniambia tufanye haraka sana” Nilisemaย  nikiwa kwenye hali ya Haraka, lilikuwa ni jambo ambalo Mamaย  alikuwa akilisubiria. Haraka alikimbilia ndani akatoka naย  mtandio, tulitoka tukachukua Tax kisha safari ya kuelekeaย  Hospitali ilianza.ย 

    Upande wa pili, Baba Osman na Zahra walikuwa wanaingiaย  Hospitalini, walisogeza gari kwenye maegesho kisha walielekeaย  Wodini ambako Osman alikuwepoย 

    “Baba Osman anaumwa? Mbona umenileta Hospitalini?” Aliulizaย  Zahraย 

    “Ndiyo Osman ni Mgonjwa sana ndiyo maana nimekuleta hapaย  Zahra” Alijibu Baba Osman, walishuka kisha walielekea ilipoย  wodi hiyo. Bahati nzuri walikutana na Dokta Simon ambayeย  alikuwa akitoka wodini humo, alipomuona Zahra alishangaa sanaย 

    “Najuwa una maswali mengi Simon lakini hiyo ndiyo haliย  halisi” alielezea Mzee Dhabi baada ya kuisoma sura ya Doktaย  Simon ilivyokuwaย 

    “Lakini Mzee, Osman hapaswi kushtushwa na jambo lingineย  mnaweza kumpoteza kabisa, kwanini aje leo?”ย 

    “Maswali yako Simon hayawezi kujibiwa kwasasa, nina imani naย  hiki atakachokiona Osman” Aliesema Mzee Dhabiย 

    “Lakini sikushauri kabisa kwenda huko Mzee Kwasasa yupo Machoย  angalau anajisikia vizuri mgesubiria kidogo basi” alisemaย  Dokta Simon

    “Mimi ni Baba yake Osman, najuwa nini nafanya Simon….Twendeย  Binti” Alisema Mzee Dhabi akiwa amemshika mkono Zahra,ย  waliingia wodini bila kusikiliza alichokisema Dokta Simonย 

    Kitendo cha kufungua mlango kilihamisha macho ya Osman,ย  aligeuza na kuangalia aliposikia sauti ya Mlango kufunguliwa.ย  Alitoa macho yake, alijaza hewa kwenye kifua baada ya kumuonaย  Zahra Mwanamke ambaye alimfanya ayachukie Mapenzi, Mwanmkeย  ambaye alimtafuta sana Ughaibuni bila Mafanikio.ย 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI Ya PUMZI YA MWISHO

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMย ย 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย 

    ย ย 

    Pumzi ya mwisho

    11 Comments

    1. Aguero on October 21, 2024 5:06 pm

      https://whatsapp.com/channel/0029VarTsGt1t90TiJVyWi0J

      Reply
    2. RickkyHarry on October 21, 2024 5:17 pm

      Dah toa nyingine ata usiku wa leo๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ

      Reply
    3. Sir yowas on October 21, 2024 5:23 pm

      Nimepumua baada ya kumaliza kusoma

      Reply
    4. Roda on October 21, 2024 6:06 pm

      Dah naona kesho mbal tuendeleee hadith imejoga sasa apo kwa akili ya haraka haraka julieth akimuona zarha atagoma ten kumhudumia osman ๐Ÿคž๐Ÿคž๐Ÿคžuwiiiiiiiiiiii hadith tam nyie ๐Ÿ’”๐Ÿ’”๐Ÿ’”๐Ÿ’”๐Ÿ’”๐Ÿ’”๐Ÿค•๐Ÿค•๐Ÿค•๐Ÿค•๐Ÿค•NATAFTA MPENZ KAMA OSMAN๐Ÿค•

      Reply
    5. Chamalo on October 21, 2024 6:55 pm

      Lete mbili juzi uliruka

      Reply
    6. Calvin paul on October 21, 2024 8:18 pm

      Mshtuko umuue osman wazazi wa osman wamfukuze jack moses amuache jack mama yake ammchukie hyo pumzi itakuwa ya mwsho

      Reply
      • Themanini on October 21, 2024 9:02 pm

        Mtunzi apewe maua yake ๐Ÿ’ ๐ŸŒน

        Reply
    7. Sabitimussa23 on October 21, 2024 9:44 pm

      Jmn wanawake!!! ๐Ÿค”๐Ÿค” khaa

      Reply
    8. Elijahh on October 22, 2024 8:12 am

      Sehemu ya nane IPO wapi

      Reply
    9. ๐Ÿ”‹ Message; Operation 1,563140 bitcoin. Receive > https://yandex.com/poll/WDrLYhyq1Mc7jMHFgAW85q?hs=7c6499f0a696868c72ae6119e22c7be5& ๐Ÿ”‹ on June 4, 2025 2:26 pm

      gu8eva

      Reply
    10. ๐Ÿ“ Message- TRANSACTION 1,850337 BTC. GET >> https://yandex.com/poll/enter/12JSER8t8KDJewYyTprg7K?hs=7c6499f0a696868c72ae6119e22c7be5& ๐Ÿ“ on June 17, 2025 5:09 am

      wwyvk2

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi September 15, 2025

    In the name of LOVE – 05

    Ilipoishia sehemu ya tatu ya In the name of LOVE โ€œBasi hakuna shida Zaylisa, mnaweza…

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    In the name of LOVE – 02

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.