Ilipoishia “Yaani Mama kisa tu ana hela basi umechanganikiwa kiasiย hicho, kweli umasikini mbaya sana Mama, ila usijali siku siyoย nyingi nitaanza kazi nitakufanyia kila kitu, sawa Mama?”ย
“Mmh! Sawa” Mama alisema kisha aliondoka zake ila aliniachaย na jambo la kufikiria ndani ya akili yangu, nilikumbukaย kitendo chake cha kuondoka pale wodini baada ya Mossesย kuingia, ila ni yeye ndiye aliyempigia simu Mosses baada yaย kuchukua namba kwenye simu yangu.ย Endelea
SEHEMU YA TATU
Sikutaka sana kuanza kufikiria hilo jambo, niliona ni boraย niwasiliane na Mosses maana baada ya kuachana naye kuleย Hospitali sikuongea naye kabisa, simu ya Mosses ilikuwaย imezimwa, ilinipa maumivu makali sana ndani ya moyo wangu,ย nilijigeuza geuza kisha Usingizi ulinichukua.ย
Kulipopambazuka nilianza kuhisi hali ya tofauti, mwiliย ulianza kuchoka hadi nilijishangaa, Mama aliendeleaย kunihudumia huku akiendelea kutafuta uwezekano wa kupataย Figo, alienda kwa daktari ambaye aliunganishwa na Osman,ย upatikanaji wa Figo ulikuwa mgumu sana huku hali yanguย ikizidi kudhohofu, nilikuwa napewa dawa tu nimeze, maumivuย niliyokuwa nikiyasikia kwenye tumbo langu yalikuwa makaliย sana nilitamani hata kufa kabisa, kwa siku zote hizoย sikumuona wala kumpata Mosses kwenye simu, ilizidi kunifanyaย niwe mgonjwa zaidi.ย
“Mama Mosses hapatikani leo siku ya kumi na mbili”ย Nilimueleza Mamaย
“Usijali pengine amepatwa na tatizo kama hapa anapajuwa basiย atakuja siku moja” Alisema Mama, angalau alinipa moyo naย tumaini, lakini nilimuuliza
“Haya maumivu makali yanatokana na nini Mama? Mwili wanguย hauna nguvu kabisa nazidi kudhohofu” Nilipomuuliza nilionaย macho ya Mama yaliyojaa maumivu, alitamani kulia lakiniย hakusema shida iliyokuwa ikinisumbuaย
“Utapona Mwanangu! Mungu ni mwingi wa huruma, atakujalia afyaย njema Binti yangu” Alisema Mama kisha alininywesha ujiย
“Hivi umewasiliana na Osman Mama?” Nilimuuliza Mamaย
“Ndiyo usiwe na wasiwasi ukipona tu utaanza kazi, pumzika kwaย sasa” Mama alikuwa ameshamaliza kuninywesha uji, alinifuta naย kuondoka zake, alipofika chumbani kwake alilia sana sababuย tumaini la Mimi kupona lilikuwa hafifu sana, siku zilisogea.ย
Mama pamoja na daktari walijitahidi kutafuta Mtu wa kunitoleaย Figo, walitangaza dau kubwa kadili siku zilivyokuwa zikiendaย ila waliojitokeza walikuwa ni Watu wenye Afya zisizoridhisha,ย figo zao pia zilionekana kuwa na Hitilafu, hazikufaa.ย Ilipofika siku ya 20 nilipekwa Hospitalini nikiwa katika haliย mbaya sana, nilikuwa sijitambui kabisa. Mama yangu alikuwaย Mtu wa kulia kila wakati, pesa ilipatikana kwa ajili ya Figoย lakini mtoaji wa figo hakupatikana, daktari alimwambia Mamaย
“Hakuna namna tunaweza kufanya, nahisi kukata tamaa Mamaย Jacklin” Alisema Daktari wakiwa ofisini kwa Daktari huyoย aliyeitwa Dokta Simonย
“Unaposema hivyo daktari unanipa wakati mgumu wa kuangaliaย mbele, sitaki kuamini kama siku za kuishi za Jacklin zimefikaย mwisho, Huyu ndiye Binti yangu wa pekee, sisi ni masikiniย sana, basi toa figo yangu kwa ajili ya Binti yangu” Alisemaย Mama, ilifika wakati ambao Mama alishindwa kuhimili maumivuย aliyokuwa akiyasikia katika kifua chakeย
“Mama Jacklin, umri wako na hilo jambo haviwezi kwendaย sambamba. Najuwa tumaini ni dogo sana katika jambo hili,ย lakini…”ย
“Dokta, kama kufa Mimi kutamsaidia Binti yangu hilo siyoย tatizo, hajawahi kuishi Maisha ya furaha katika Maisha yake,ย ndiyo kwanza alikuwa amepata kazi….leo afe aaaah hapana”ย Alisema Mama akiwa analia, alionesha uchungu wake kwanguย
“Sawa Mama! Ngoja tuiangalie kama itafaa” Alisema Doktaย Simon, kisha waliongozana hadi chumba cha Uchunguzi. Mamaย alitakiwa kufanyiwa uchunguzi wa figo yake ili niwekewe Mimiย nipate kunusuru Maisha yangu ambayo yalikuwa hatua za mwishoย sana.
Huu ndiyo upendo ambao Mama huwa nao kwa Mtoto wake,ย watakukimbia wote katika Maisha lakini Mama yako atasimamaย kwa ajili yako kila siku za Maisha yako, Mama alianzaย kufanyiwa uchunguzi. Bahati mbaya figo ya Mama ilikuwa naย Mawe hivyo isingeliweza kunifaa, Mama alilia sanaย
“Dokta weka hiyo hiyo ili Jacklin aamke, tumaini langu niย yeye pekee” Mama alilia hadi Dokta Simon alidondosha Choziย lakeย
“Mama usilie, tuna siku 10 zilizobakia, Mungu atafanya wepesiย wa hili jambo, kwasasa Jacklin anahitaji Maombi” Alisemaย Dokta Simon, Mama alifikiria afanye nini, alichukua namba yaย Mosses kisha aliipiga akiwa Hospitaliniย
Bahati nzuri siku hiyo simu ya Mosses iliita aliipokea, Mamaย alimueleza Mosses hali ya afya yangu kwa wakati huo, Mossesย alimwambia Mama kuwa alipata tatizo ndiyo maana alishindwaย kuja akaahdi kuwa atakuja Hospitalini. Kweli, Mchana Mossesย alifika Hospitalini, aliishuhudia hali ya Afya yangu ambayoย alisimuliwa kama hadithi za Amza Stories, alikubali kuwa Mimiย nilikuwa mgonjwa sana kwa jinsi nilivyodhohofu, pumua yanguย ilikuwa ya shida mnoย
“Hali ndiyo hiyo, leo siku ya tatu haongei wala hafumbuiย Macho. Kama unampenda Jacklin jitolee Mosses Mungu atakulipaย kwa wema wako” Mama alisema, walikuwa wodini wakiwa na yuleย Daktari Simonย
“Mama Mimi nitajitoa kwenye nini tena ikiwa mmetangaza dauย kubwa na bado figo haijapatikana, tumuombee Jacklin pengineย Mungu atampa nafuu” Alisema Mossesย
“Kuomba tunaomba lakini hatuwezi kukaa kimya bila kufanyaย jitihada zozote Baba, mimi leo siku ya tatu sijala chochote,ย nione sina raha kwasababu ya Jacklin” Alisema Mama hukuย akibubujika Mchozi, Dokta Simon aliingilia kati akamwambiaย Mossesย
“Ndugu najuwa inaweza kuwa ngumu kwako lakini kama huyu Mtuย ana umuhimu kwako jitolee figo moja kwa ajili ya kumuamsha”ย Alisema Dokta, Mosses alishtuka akaulizaย
“Nitoe nini?”ย
“Figo kwa ajili ya Mpenzi wako” Alijibu Dokta Simon huku Mamaย akiwa analia pembeni,
“Nitoe figo? Hiyo ni hatari sana Dokta nitafanya vyote lakiniย siyo kutoa figo yangu, ingekuwa wote wanaopendana wanatoleanaย viungo basi hii Dunia ingejaa walemavu kila kona” Alisemaย Mosses, Maneno yake yalimchukiza sana Mama alinyanyuka naย kumpiga kofi Mossesย
“Mama hupaswi kufanya hivyo hapa ni Hospitalini istoshe niย wodini ambako panahitaji utulivu sana” Alisema Dokta Simonย
“Dokta huyu ni mshenzi anawezaje kusema maneno ya kikatiliย namna hiyo hakuona neno lingine la kusema? Huyu si ndiyeย ambaye alikuwa akikupa furaha, leo amelala hujali tena siย ndiyo?” Alihoji Mama huku akiwa anahema juu juuย
“Unathubutu vipi kunipiga Mimi? Unanijuwa Mimi? Kama Maishaย yake ni muhimu kwangu basi hata kwako ni Muhimu kwanini weweย usitoe hiyo figo? Siwezi kutoa kiungo kisa Mapenzi tena kwaย kiumbe anayeitwa Mwanamke, Jacklin akipona Mimi nipo akifaย Maisha yataendelea” Alisema Mosses kisha aliondoka Wodini,ย Mama alilia sana, kauli ya Mosses ilizidi kumfanya akateย tamaa, Dokta Simon alimwambia Mamaย
“Siku bado zipo tuzidi kufanya jitihada na Maombi” Alisemaย kisha aliondoka zake, Mama aliendelea kulia kwa kukata tamaaย alinisogelea akasemaย
“Jacklin nimekuzaa kwa shida sana, nimekulea kwa tabu mno,ย leo nakupoteza Mama kwa shida sana, Nisamehe Mama yakoย nimefanya jitihada zote lakini nimeshindwa Mimi sababu hataย Mungu hayupo upande wangu tena” Maneno ya Mama niliyasikia,ย Chozi lilinivuja, sikuwa na nguvu ya kufanya chochote kileย
โขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขย
Ndani ya Dubai, Kilichompeleka Osman Dubai kilikuwa niย kumtafuta Zahra, achana na kiasi kikubwa cha pesa ambachoย Mwanamke huyo aliondoka nacho na kwenda huko kuishi naย Mwanaume mwingine, Osman alikuwa akimpenda sana Mwanamkeย huyo, jitihada za kumpata Zahra ziligonga mwamba. Alirudiย Nchini, aliitafuta Familia ya Zahra lakini wazazi wa Zahraย walionekana kufurahia ambacho Bitni yao alikifianya.ย
Hawakuwa na huruma, Osman alijitoa sana kuhakikisha Maisha yaย Wazazi wa Zahra yanakuwa bora, aliwajengea jumba la kifahari,ย aliwanunulia magari ya kutembelea, alibadilisha Maisha yaoย kwa kiasi kikubwa sana, Osman aliondoka na kwenda kwenyeย gari, alikumbuka jinsi ambavyo aliishi kwa furaha na amani naย Zahra, alilia sana, Maumivu yalijaa ndani ya kifua chakeย alipoikumbuka meseji ya mwisho ambayo Zahra aliituma, mesejiย hiyo ilisema
“Osman! Najua ujumbe wangu utakupa maumivu makali sana lakiniย inabidi uupokee sababu ndiyo maamuzi yangu, asante kwaย kubadilisha Maisha ya Wazazi wangu kwa kiasi kikubwa lakiniย hukuwa chaguo la Moyo wangu japo ulinipenda sana, kwasasaย mimi nipo Dubai na Mwanaume ambaye ninampenda. Usiwazumbueย wazazi wangu wala usinitafute, pesa zote zilizo kwenyeย akaunti yako ya Benki nimezichukua, unaweza kujiona Mjingaย lakini hiyo ndiyo nguvu ya Mapenzi ambayo ninayo, nilikufanyaย ukawa dhahifu kwangu! Nakutakia Maisha Mema, ni Mimi Zahra”ย
Ulikuwa ndiyo ujumbe wa Zahra baada ya hapo simu yakeย haikupatikana tena,, alipoupata ujunbe huo Osman alipotezaย fahamu akaenda kuzinduka kwenye Hospitali ya Dokta Simon,ย aliishi Maisha yaliyojaa maumivu na aliapa kuwa hatokujaย kupenda tena.ย
Basi, alifuta chozi akiwa ndani ya gari yake ya kifahari,ย alipotoka kwa Wazazi wa Zahra alikuja moja kwa mojaย Hospitalini maana aliwasiliana na Mama na akaambiwa kuwa haliย yangu siyo nzuri na haina tumaini.ย
Alimkuta Mama akiwa analia nje, Osman alimuuliza Mama “Hali yake kwasasa ipoje Mama?” Alimuuliza baada ya salamย
“Kama nilivyokueleza Baba, hali ya Jacklin ni mbaya sana,ย ninahofu juu ya uhai wake” Alisema Mama akiwa anaendeleaย kumwaga choziย
“Pole Mama, wakati mwingine Dunia inakuwa katili sana, naombaย nikamuone” Alisema Osman, walirudi wodini, Osman aliponionaย hakuamini kama ni Mimi ndiye niliyemchachafya siku kadhaaย zilizopita, nilikuwa nimekonda sana, nilikuwa nikipumua kwaย shida sana, alidondosha chozi akamuuliza Mamaย
“Upatikanaji wa figo?” Mama alitikisa kichwa kuashiria kuwaย hakukuwa na uwezekano wa kupatikana figo kabisa japoย zilisalia siku 10ย
“Nitarudi Mama” Osman alitoka haraka akaelekea ofisini kwaย Dokta Simon.ย
“Bilonea Kijana karibu sana” Alisema Dokta Simon sababuย alikuwa akimfahamu sana Kwa ukaribu Osmanย
“Dokta Simon, Mama Jacklin amesema uwezekano wa kupatikanaย Figo ni mdogo sana, nataka kusikia kutoka kwako!”ย
“Huo ndiyo ukweli Osman, kilichobakia ni kudra za Mwenyeziย Mungu pekee, tumepima Watu wengi lakini hakuna hata mmojaย mwenye figo yenye afadhali alafu kibaya zaidi Mpenzi wa huyoย Jacklin amegoma kufanya hivyo” Alisema Dokta Simonย
“Nitatoa Figo yangu” Alisema Osman, kauli hii ilimshtua sanaย Dokta Simonย
“Unatoa figo yako? Umefikiria mara mbili Osman? Hii familiaย inakuhusu nini wewe ikiwa mpenzi wa Jacklin amekataa, ufanyeย hivyo wewe kama Nani? Umesahau kilichokutokea Osman?”ย Aliuliza Dokta Simonย
“Natoa kama Binadamu niliyeguswa na hili Dokta Simon, Maishaย ya yule Msichana ni tunu Kwa Mama yake, ni furaha kwenyeย macho ya Mama yake ambaye muda wote analia. Umewahi kufikiriaย jinsi Mama yule anavyokosa raha kwasbabu ya Binti yake?ย Unajuwa ni furaha kiasi gani ataisikia endapo Binti yakeย atasimama tena?” Aliuliza Osman kwa hisia kali sanaย
“Fikiria mara mbili sikushauri kufanya hivyo Osman, wewe niย Bilionea Mkubwa hupaswi kuishi Maisha yenye kasoro kiasiย hicho!”ย
“Mkamilifu ni Mungu pekee, nitatoa Figo yangu kuokoa Maishaย yake” Alisema Osman kisha aliondoka akarudi Wodini, Doktaย Simon hakukubaliana na uamuzi wa Osman alinyanyua simu naย kuwapigia Wazazi wa Osman, aliwapata taarifa hiyo ambayoย iliwakasirisha sana Wazazi wa Osmanย
Basi, Osman aliporudi alimwambia Mama kuwa nitapona na kuanzaย kazi mara moja, japo Mama alikuwa katika hali ya huzuni sanaย ila maneno ya Osman yalimjaza tumaini.ย
Alipotoka Hospitalini Osman alikuwa mwenye mawazo na maumivuย makali sana, alipigiwa simu na Wazazi wake na kumtaka aachaneย na mpango wa kutaka kutoa figo kwani haitokuwa na faidaย yoyote kwake, Wazazi wa Osman waliamini kuwa Osman alikuwaย akitaka kutoa figo kwa ajili ya Mapenzi, walinuonya sana kwaย kile kilichomtokea kwa Zahra ila Osman aliwaambia Wazazi wakeย kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Mimi bali ni ubinadamu tuย wa kutaka kuhakikisha afya yangu inaimarika.ย
Osman aliwasiliana na Hospitali nyingine ambayo ingefanyaย operesheni ya kupandikiza figo kwenye mwili wangu, kutokanaย na utajiri alionao aliweza kupata Hospitali Nchini India,ย tulisafiri kwenda huko. Osman alishauriwa na kuambiwa kilaย kitu kiafya kuhusu uamuzi wake.ย
Nini Kitaendelea? Osman atatoa FIGO? Usikose Sehemu Ya NNE Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย
14 Comments
Duuuh Osman ni mwanaume wa maana๐
Ila sas ili ujue binadamu jau๐๐๐ au ngoja …. nisiharibu uhondo siku ikifikia ntakwambiaa…hii tamthiliya inaweza kuliza watu huko mbele ๐ฅฒ๐ฅฒ๐ฅฒ me siyo mtabiri akin
๐ mule mule baba admin…..hujai kosea
Sas huyu binti akitaka kutukera apone af arud kumpenda mosses tena wakat osman katoa figo hap๐
Wanaume kama osman tumebaki wachache sanaa
Calvin kabisa ๐๐๐๐
Huyu dada nna was was akipona …atanboaaaa
Niko njia Panda naomba mosses
Afutwe uhusika๐ฃ
Huu uzi sio poa hatariii kama ungekuwa unaachia mbili mbili vile daah hatarii๐ฅ๐ฅ
Yani wanawake sisi Sijui kama atakumbuka wema Na fadhila
๐
Mmmh tusubili namba 04 ๐ค๐ค
NAUZA FIGO +255788414957
!!!!!!!! Kuna mtu ata ๐
๐๐