Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Saba (07)
    Hadithi

    Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Saba (07)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 18, 2024Updated:October 28, 202412 Comments10 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Yote yaliyo mema, mazuri na yenye uelekeo mzuri zaidi, mudaย  siyo mrefu maono yangu yatadhihirika” Sikutaka kuendeleaย  kumuuliza, nilimwambiaย 

    “Sawa Mama nasubiria hayo Mema, nipo chumbani kwangu”ย  Nilisema kisha nilielekea Chumbani kwangu, tulikuwa tukiishiย  Watu watatu tu, yaani Mimi, Mama na Mdada wa kazi. Hadiย  naondoka sikujuwa Mama na Osman walikuwa wamewasiliana naย  kuambiana kuwa nilienda kwa Osman. Endeleaย 

    SEHEMU YA SABA

    Ila ndani ya moyo wangu nilihisi amani sababu tayari nilikuwaย  nimeshamuomba msamaha Osman, na pia nilikuwa nimeweka mamboย  sawa kwa Mama yangu. Siku zilipita, niliendelea na kazi,ย  Mapenzi yangu kwa Mosses yaliendelea bila tatizo lolote tenaย  alikuwa akininyenyekea sana tofauti na mwanzo, kaziย  ziliendelea kule kwenye kampuni ya Osman, niliendelea kupataย  uzoefu huku ukaribu kati yangu na Osman ukizidi kuongezeka.ย  Osman alikuwa akiumwa sana ila alikuwa akijikaza mno mbeleย  yangu ila sura yake ilionesha wazi kuwa alikuwa akiumwa,ย  sikutaka kumuuliza sana sababu kama ningekuwa na unuhimu waย  kulijuwa hilo angelikuwa ameshaniambia muda mrefu.

    Alinipeleka sehemu mbalimbali, ndani na nje ya Nchi,ย  alinifundisha vingi sana Osman. Namna tulivyokuwa tumezoeanaย  kama ikitokea umetuona kwa mara ya kwanza ingekuwa rahisiย  kuhisi ni wapenzi, Osman alikuwa akijaribu kunionesha hisiaย  zake lakini hakusema kwa kinywa chake, nakumbuka siku yanguย  ya kuzaliwa alininunulia gari aina ya Cadilac, aliniandaliaย  kila kitu kwa ajili ya siku yangu ya kuzaliwa, nilimuarikaย  Mosses kwasababu ndiye Mwanaume aliyekuwa akinipa furaha.ย 

    Mama aliniita pembeni, akaniulizaย 

    “Hivi Jacklin unatumia ubongo wako vizuri kuwaza?” Aliulizaย  kwa sauti ya Juu sababu kulikuwa na kelele za Mziki, wakatiย  huo Watu ndio walikuwa wakifika nyumbani kwetu kwenye hiyoย  sherehe ya siku ya kuzaliwaย 

    “Mama! Nimefanya kitu gani kibaya?” Nilimuulizaย 

    “Mosses amefuata nini hapa? Hii ni sherehe yako wewe, Osmanย  amefanya kila kitu bado unashindwa hata kumuheshimu?” Alisemaย  Mama ilinibidi nishushe mzuka wanguย 

    “Hivi Mama kwanini tunaishi kwa kuhofia fulani atasema nini?ย  Osman ni rafiki yangu, na Bosi wangu. Kuniandalia shereheย  haimaanishi mimi na yeye ni wapenzi Mama, Nitasherehekea vipiย  siku yangu ya kuzaliwa bila Mosses?” Nilimuuliza Mamaย 

    “Huyo Mosses anajulikana na nani? Amekusaidia nini hadi hiviย  sasa kama siyo kula pesa yako ambayo imetokana na Osman?ย  Jacklin, hujui kilichopo kichwani kwa Osman na hujui kwaniniย  aliandaa hii sherehe yako ya kuzaliwa. Unaiyona ile gariย  pale? Ile ni zawadi kutoka kwa Osman, huyo Mosses wakoย  anaweza kukununulia japo Pikipiki?” Mama alisema na nilionaย  wazi alikuwa amepaniki.ย 

    “Samahani Mama” Nilisema, nilikuwa sipendi kumuona Mama yanguย  akiwa katika hali ya kuhuzunika kisa Mimiย 

    “Mwambie huyo Mosses aondoke hapa kabla Osman hajafika, Osmanย  ni mfadhili wetu hivyo ni lazima tuheshimu hisia zake” Mamaย  alisema Maneno ya mwisho kisha aliondoka pale, aliniacha naย  mawazo lukuki sana nikajiuliza maswali mengi ambayo sikuwa naย  majibu yakeย 

    Nikiwa nimesimama alikuja Mosses akiwa ameshikilia glasiย  yenye kinywaji, aliniulizaย 

    “Mama alikuwa anasemaje? Nimewaona kama mlikuwa mkigombanaย  hivi” nilimtazama Mosses kisha nilitabasamu tu nikamwambia

    “Hapana kuna jambo alikuwa ananielekeza ndio tukawaย  hatuelewani, lakini usijali” nilisemaย 

    “Mlisema Sherehe inaanza saa moja usiku, sasa inakimbilia saaย  mbili, anasubiriwa nani?” Aliuliza Mosses, nilikosa chaย  kumjibu. Mara zilisikika honi za gari huko nje,ย 

    “Wageni hao hebu twende” Nilisema lakini Mosses alinishikaย  mkono akanivuta pembezoni kwenye mnazi. Alitupa glasiย  pembeni, akaanza kunila mate yangu. Nilishindwa kujizuiaย  nikajikuta namba sapoti Mosses, eneo ambalo sisi tulikuwaย  tumesimama lilikuwa na mwanga hafifu sana.ย 

    Wakati magari yanaingia sisi tulikuwa bize kupeana mate paleย  kwenye mnazi, bahati mbaya Osman aliangalia tulipo japoย  hakunitambua kutokana na lile giza. Alikuwa ameingia na Babaย  na Mama yake, Zilipokuja kuwashwa taa zote ndipo tuliposhtukaย  tukaacha ule mchezo, ila mashine ya Mosses ilikuwa imesimama.ย  Tuligawana njia, mimi nilipitia upande wangu na Mosses upandeย  wake, nilipowaona Wazazi wa Osman nilishangaa sana sababu waoย  walikuwa Dubai au inamaana walikuja kwa ajili ya Shereheย  yangu ya siku ya kuzaliwa tu au kulikuwa na jamboย  lililowaleta pale? Nilisimama kwa sekunde kadhaa kabla yaย  kujitokeza huku bado mawazo yakiwa yananizonga kichwaniย  kwangu, sikuamini Sherehe yangu ya kuzaliwa ihudhuriwe naย  Bilionea Mkubwa kama Baba yake Osman?ย 

    Nilipojitokeza sikuonesha dalili yoyote kuwa nilikuwaย  nimetingwa na mawazo, nilienda kumsalimia Baba yake Osman,ย  alikuwa akinipenda sana na mara zote alikuwa akisema natembeaย  na kiungo chao japo alikuwa akisema kama utani ila ilikuwa niย  kweli nilikuwa natembea na figo ya Osman, tulicheka pamoja,ย  nilipogeuka nilikutana na Mama yake Osman naye alitabasamu,ย  tulisalimiana vizuri sana, ilikuwa ni sherehe ndogoย  iliyobadilika na kuwa kubwa tena yenye heshima sana hadi Watuย  tuliowaarika walishangaa. Walinionesha mahali alipo Osman,ย  alikuwa amesimama na rafiki zake, nilienda kumsalimia hukuย  macho yangu yakimtafuta Mosses alipo, Osman alinikumbatiaย  kisha alinishika mkono huku akiendelea kuniuliza maswali yaย  hapa na paleย 

    Punde shughuli ilianza, Mama yangu sikumuona kabisa licha yaย  kupepesa macho huku na kule. MC wa shughuli aliniita katikatiย  ya Watu waliokuwa wamesimama, nilitembea taratibu sababuย  nilivalia gauni refu lenye rangi ya Dhahabu. Nijisifie tuย  maana ukisubiria kusifiwa hapa Duniani utazeeka, nilipendezaย  mno.

    “Leo ni siku nzuri na nyenye baraka kutoka kwa Mungu, nduguย  yetu Jacklin leo ametimiza miaka 28. Bahati ilioje kwake niย  kwamba sherehe yake imehudhuriwa na Bilionea ambaye ndiyeย  Baba wa Osman ambaye pia ameandaa shughuli hii kwa ajili yaย  Jacklin” Alisema MC kisha Watu walipiga makofi mengi sana,ย  bado nilikuwa nikiangaza macho yangu kumtafuta Mosses, bahatiย  nzuri nilimuona akiwa amesimama nyuma akiwa anaangalia tukioย  lilivyokuwa likiendelea.ย 

    Nilitabasamu ili tu mambo yaende ila nilipoteza uwezo waย  kujiamini kabisa, MC aliendeleaย 

    “Namkaribisha Osman Dhabi aje mbele atuambie siku ya leoย  amemuandalia nini Jacklin” Makofi mengi yalipigwa, Bilioneaย  Mzee Dhabi naye alikuwa akifurahi pamoja na Mke wake hapoย  ndipo nilipomuona Mama yangu akiwa amesimama kando ya familiaย  hiyo ya Kitajiri, Mama alinipa ishara ya kukubaliย  kitakachotokea pale, nilishindwa kumuelewa ni kwaniniย  nikubali kwasababu sikujuwa kilichotaka kwenda kutokea. Osmanย  alipofika karibu na Mimi alisemaย 

    “Wakati nakutana na Jacklin kwa mara ya kwanza nilimuona niย  Mwanamke Msumbufu, asiyejali, mkorofi lakini nilivyokujaย  kumuelewa niligundua ni Mwanamke wa tofauti sana” Alisemaย  Osman, wote walipiga makofi hata Mimi nilitabasamu maanaย  nilikumbuka jinsi nilivyokutana na Osman kuanzia kwenyeย  Pikipiki hadi kwenye mvua, nilicheka.ย 

    “Kwa muda mfupi anenitengenezea kumbukumbu zisizofutikaย  katika Maisha yangu, leo kwenye siku yake ya kuzaliwaย  nilifikiria ni zawadi gani naweza kumpa ili afurahi, nilionaย  nimnunulie gari aina ya Cadilac escaled ya Mwaka 2021”ย  Shangwe ziliibuka pale, makofi yalipigwa sanaย 

    “Gari hii ina thamani ya Milioni 600, ni zawadi ambayo moyoย  wangu umeridhia kwake lakini pia napenda kumuomba Jacklin”ย  Alisema Osman kisha alipiga magoti akanitazama, nikaiyonaย  ishara kuwa anataka kunivika pete kidoleni, nilishtukaย  nilipomuona Akitoa pete kwenye mfuko wa koti lake la sutiย 

    “Nipe ruhusa niwe Mumeo Jacklin, maneno haya si rahisi Mtotoย  akayazungumza mbele ya Wazazi wake lakini nimeshindwaย  kufikisha hisia hizi kwako, nimeona leo ni wakati sahihi waย  kufanya hivi” Nilimtazama Osman kama vile nataka kumuulizaย  maswali ambayo hata sikujuwa niulizaje, nilipogeuza machoย  nilikutana na Mosses, Mama na Wazazi wa Osman, wote walikuwaย  kimya kusikiliza nitasemaje. Niliishiwa nguvu jamani

    Osman alinishika mkono akawa ananivisha ile pete taratibu,ย  nilikuwa kama Mgonjwa wa koma, ghafla nilishtuka nikasemaย 

    “Hapana Osman, siwezi” nilisema kisha niliivua ile peteย  nikamtupia Osman, Watu walijawa na mshangao mkubwa sana,ย  Chozi lilimbubujika Osmanย 

    “Jacklin tafadhali, fanya kwa ajili ya Wazazi wangu nakuomba”ย  Alisema Osmanย 

    “Siwezi Osman, siwezi kuidhurumu nafsi yangu, siwezi kuuzaย  upendo wangu Osman, unajuwa fika nina Mtu wangu” Nilisema,ย  Watu walikuwa kimya sana kusikiliza maongezi yetuย 

    “Jacklin, hili ni ombi langu kwako, baada ya hapa sitakuwa naย  uwezo wa kukuomba chochote tena, tafadhali” Alisema Osmanย  kisha aliushika mkono wangu ili anivishe tena ile pete,ย  nilimsukuma kisha niliondoka pale, nilikimbilia nje kabisa,ย  Mosses alinifuata huko nje, tulichukua Bajaji na kuondokaย  pale nyumbani. Nilipomsukuma Osman alianguka, hali yakeย  ilibadilika alikimbizwa Hospitalini, Hekaheka ilikuwa kubwaย  pale nyumbani, Watu walikuwa wakijiuliza kulikoni, Mzee Dhabiย  alihangaika kwa ajili ya Mtoto wake. Muda mchache watuย  waliondoka pale nyumbani, alibakia Mama akiwa analia tu, namiย  nilikuwa nikilia ndani ya Bajaji, siyo kwamba nilikuwaย  simpendi Osman ila tayari nilikuwa na Mwanaume niliyempendaย  ambaye ni Mosses.ย 

    Nilikuwa nimeshabadilisha hali ya hewa, nililia sana nikiwaย  ndani ya Bajaji, Mosses alinibembeleza hadi tulipofika kwake.ย 

    Tukiwa chumbani aliniulizaย 

    “Nini kinaendelea Jacklin?” Aliniuliza akiwa amekaa pembeni,ย  chozi lilikuwa likinibubujika, nilimuwaza Mama yangu,ย  nilijuwa nimemkosea sana.ย 

    “Mosses, hakuna chochote kinachoendelea kati yangu na Osman,ย  nimeshangaa ameita wazazi wake kwenye sherehe yangu yaย  kuzaliwa istoshe hakuwahi kuongelea kuhusu mapenziย  nimeshangaa alipotaka kunivesha pete” Nilisema huku nikiwaย  najifuta mchozi, simu yangu ilikuwa ikiita sana na aliyekuwaย  akinipigia alikuwa ni Mama yangu, niliamuwa kuizima kabisa.ย 

    “Yule ndiyo amebadilisha Maisha yenu?” Aliniuliza “Ndiyo Mosses, ni yeye”

    “Haiingii akilini Mtu aje tu atake kukuvesha pete, lazimaย  kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea kati yenu”ย 

    “Mosses tafadhali naomba uniamini, nisingelimkimbia kwa ajiliย  yako, ile ni familia ya kitajiri sana. Kama siyo weweย  ningelikuwa nimekubali lile jambo ila upo wewe Mwanaumeย  nikupendaye Mosses” nilisema kisha nilimuona Mossesย  akitafakari jambo, kilio changu kilikata nikawaza labdaย  alikuwa anataka aniacheย 

    “Hebu tuliza akili yako Jacklin, kesho asubuhi tutaongeaย  jambo moja” Alisema Mosses, nilipata muda wa kupumzika.ย 

    โ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขย 

    Mama yangu hakulala, hakula chakula, alikesha kunipigia simuย  bila kupokea majibu yoyote. Usiku ulikuwa mwingi ilimbidiย  aingie ndani, Usiku huo taarifa kutoka maabara zilisema haliย  ya Osman inaweza kuwa mbaya zaidi baada ya miezi mwiliย  kutokana na figo lingine kufanya kazi kwa kiwango kidogoย  sana. Taarifa hii ilikuwa mbaya na isiyopendeza kabisa, Mzeeย  Dhabi na Mke wake walihuzunika sana, walimuuliza Dokta Simonย 

    “Kwanini hukusema kabla Osman hajachukua uamuzi wa kuondoaย  figo moja?” Ilikuwa ni sauti yenye maumivu sana iliyotokaย  kwenye kinywa cha Bilionea Dhabiย 

    “Niliongea naye kabla ya kuchukua uamuzi huo, cha ajabuย  alimuhamisha mgonjwa na kwenda kufanya upasuaji India,ย  aliniomba nisiwaambie chochote kwasababu alikuwa na uhakikaย  wa kupata figo haraka iwezekanavyo. Tukio lililotokea leoย  siyo tu limemletea mshituko bali mfadhahiko mkubwa ndaniย  yake” Alisema Dokta Simon, Chozi lilimbubujika Mama yakeย  Osman, alikuwa ndiyo Mtoto wao wa pekee hawakubatika kupataย  Mtoto mwingineย 

    “Laiti kama mioyo ingekuwa inahamishika basi ningehamishaย  moyo wa Osman, mara zote tuliamini tukimpa pesa nyingi Mtotoย  wetu itampa jeuri na kuondoa mapenzi katika Moyo wake lakiniย  Osman amekuwa dhahifu sana linapokuja suala la Mapenzi” Mzeeย  Dhabi alimtuliza Mke wakeย 

    “Dokta inahitajika huduma gani kwa Mtoto wangu, Hospitaliย  gani Duniani, Pesa Kiasi gani? Nipo tayari kutoa nusu yaย  utajiri wangu kwa ajili ya Osman” Alisema Mzee Dhabi, Doktaย  Simon alimwambia Mzee Dhabiย 

    “Unaweza ukapata figo, ukapata kila kitu lakini huweziย  kuuondoa mfadhahiko alionao Mwanao. Kitu cha kwanza niย kumuondolea mfadhahiko Osman ili kumuandaa kwa ajili yaย  upasuaji wa kupandikiza figo” Alisema Dokta Simonย 

    “Pesa siyo tatizo Simon, niambie hiyo huduma inapatikanaย  Hospitali gani Duniani, kiasi gani kinahitajika?” Aliulizaย  Bilionea Dhabi, walionesha kumpenda sana Mtoto wao.ย 

    “Mfadhahiko huondolewa na kilichosababisha mfadhahiko,ย  tumaini alilokuwa nalo ndilo lenye kuuondoa huo mfadhahiko waย  Osman”ย 

    “Unamaanisha nini?”ย 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya NANE Ya PUMZI YA MWISHO

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMย ย 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย 

    Pumzi ya mwisho

    12 Comments

    1. catherine Arod on October 18, 2024 2:53 pm

      Duh ya moto sana.

      Reply
    2. Samuel FA on October 18, 2024 4:17 pm

      Duuuuh….. Si mchezoooo๐Ÿ™†๐Ÿ”ฅ

      Reply
    3. Fredy on October 18, 2024 4:19 pm

      Hadithi tamu Sana

      Reply
    4. Qassim Ituja on October 18, 2024 5:09 pm

      Pumzi ya mwisho kipande kimoja Ni kitamu sana, ladha haiishi, ongeza viwe viwili kwa siku chief

      Reply
    5. Charz jr๐Ÿ˜Ž on October 18, 2024 5:30 pm

      ๐Ÿ˜Š๐Ÿ˜Š mpka kieleweke

      Reply
    6. Roda on October 18, 2024 8:17 pm

      Huyo dada anatia hasira ๐Ÿ˜ค๐Ÿ˜ฃ๐Ÿ˜ hv ana akili zote mpuuzi huyoooo

      Reply
    7. G shirima on October 18, 2024 8:52 pm

      Aise imenigusa sana dah

      Reply
      • Azimara on October 19, 2024 5:07 pm

        Hadithi tamu balaaa

        Reply
    8. Hamis on October 19, 2024 5:49 am

      Kwan adinimi story unatowa wap mbon kama muvi iv tunaangalia jamani

      Reply
    9. Agustine on October 19, 2024 11:57 am

      Admin nikutmie shingap unitmie vipande vyote

      Reply
      • Yulia kimario on October 19, 2024 4:47 pm

        ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

        Reply
    10. Chrispin on October 20, 2024 9:14 pm

      Nzurii

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi July 14, 2025

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya pili Alipiga magoti na kujiinamia huku chozi likimtoka Zahoro,…

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.