Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    ZAINABU ( 01)

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Nne (04)
    Hadithi

    Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Nne (04)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 14, 2024Updated:October 28, 202436 Comments8 Mins Read6K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Alipotoka Hospitalini Osman alikuwa mwenye mawazo na maumivu  makali sana, alipigiwa simu na Wazazi wake na kumtaka aachane  na mpango wa kutaka kutoa figo kwani haitokuwa na faida  yoyote kwake, Wazazi wa Osman waliamini kuwa Osman alikuwa  akitaka kutoa figo kwa ajili ya Mapenzi, walinuonya sana kwa  kile kilichomtokea kwa Zahra ila Osman aliwaambia Wazazi wake  kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Mimi bali ni ubinadamu tu  wa kutaka kuhakikisha afya yangu inaimarika. 

    Osman aliwasiliana na Hospitali nyingine ambayo ingefanya  operesheni ya kupandikiza figo kwenye mwili wangu, kutokana  na utajiri alionao aliweza kupata Hospitali Nchini India,  tulisafiri kwenda huko. Osman alishauriwa na kuambiwa kila  kitu kiafya kuhusu uamuzi wake. Endelea

    SEHEMU YA NNE

    alikubali kutoa figo. 

    Baada ya siku tatu, tulifanyiwa Operesheni, Osman aliondolewa  Figo yake ambayo ilikuwa safi kabisa, Mimi niliondolewa Figo zangu ambazo zilikuwa na matatizo kisha ilipandikizwa Figo ya  Osman katika mwili wangu. Mama yangu alikuwa ni Mtu wa kulia  na kuomba Mungu kila jambo liende sawa, siku zilienda, unafuu  ulianza kuniingia, hata Osman unafuu ulimuingia, sikujuwa  kilichokua kimetokea. 

    Ilipita miezi miwili tukiwa Hospitalini India, hali yangu  ilizidi kuimarika siku hadi siku hatimaye nilipona kabisa,  Mimi na Osman tulipona, tuliruhusiwa tukarudi Nchini.  Tulifikia kwenye jumba la kifahari sana ambalo Osman  alitununulia, Maisha yalibadilika sana kwetu, Osman  alitufungulia Biashara kubwa. Nilisimuliwa kila kilichotokea,  niliuona upendo wa Osman, pia niliuona upendo feki wa Mosses 

    Siku moja Osman alinipeleka kwa Wazazi wake huko Dubai,  Walifurahika kuniona. Walitupokea kwa shamra shamra sana,  familia yao ilikuwa ni familia ya kitajiri sana. 

    “Karibu Jacklin katika Familia yetu” Alisema Baba yake Osman  tukiwa tunapata chakula 

    “Asante Baba, nafurahika kuwaona” nilijibu 

    “Usijali Jacklin, wewe ni damu yetu sababu una kiungo cha  Mtoto wetu, naona hata sura ya Osman imeng’aa kwa furaha,  natumaini hautofanya kama alichokifanya Zahra” Alisema Mama  yake Osman, nilishtuka kidogo sababu nilikuwa simjui huyo  Zahra, nilimtazama Osman akanipa ishara ya kutabasamu tu kuwa  atanieleza kila kitu, kilichonishangaza ni yale maongezi yao,  ilionesha kuwa wao walikuwa wakijuwa kuwa Mimi na Osman ni  wapenzi wakati hatukuwahi kuongelea kuhusu Mapenzi. 

    Baada ya Chakula tulioneshwa chumba cha kulala, kilikuwa ni  chumba kimoja tu tulale mimi na Osman, tulipofika Chumbani  nilimuuliza Osman 

    “Zahra ni nani?” Nilimuuliza nikiwa nimekaa kitandani, yeye  alikuwa ameketi juu ya kiti. 

    “Mwanamke niliyempenda sana, aliyenifanya nikalia na kupoteza  kila kitu katika Maisha yangu” alisema Osman 

    “Kwahiyo ulinisaidia ili unitumie Osman, umewaambia nini  Wazazi wako na kwanini waseme maneno yale? Lengo lako nije  kuonekana mbaya mbele za macho yao wakati unajuwa hali halisi  kuwa nina mpenzi?” Nilisema japo Mosses alikataa kutoa figo  na kumjibu Mama vibaya, niliamini pengine kuna jambo  hawakuelewana tuu ila bado alikuwa akinipenda nami nilikuwa  nikimpenda.

    “Una mpenzi? Aliyekuacha ufe wakati alikuwa na uwezo wa  kukusaidia?” Alisema Osman akiwa anakaa vizuri 

    “Yeye alikataa ila wewe umenisaidia ili unitumie Osman, huna  tofauti na mtu anayetoa msaada na kusubiria kulipwa. Mosses  ni Mwanaume anayenipenda sana pamoja na yote yaliyotokea”  Nilisema nikiwa ninajilaza 

    “Samahani Jacklin, usiwachukie Wazazi wangu wala usiumie,  sikukusaidia ili niwe na wewe ila samahani sana kwa kukufanya  uhisi hivyo” Alisema Osman, sikumjibu chochote kile, niliona  alikuwa akinipenda sana ila sikuwa na hisia za kimapenzi na  Osman, moyo wangu ulikuwa kwa Mosses. Tuliishi Dubai kwa wiki  mbili, tulikuwa tukiongea mbele ya Wazazi wa Osman lakini  tukiwa wawili kila mmoja alikuwa kimya, tulirudi Nchini,  nilifurahika sana kuonana na Mama yangu kwa mara nyingine  tena. 

    “Maisha ya huko yalikuwaje Mama” Aliuliza Mama yangu, wakati  huo Osman alikuwa ameshaondoka 

    “Mazuri sana Mama, nimefurahi sababu ilikuwa ndiyo mara ya  kwanza naenda nje ya Nchi” Mama alinikumbatia akaniambia 

    “Muweke Osman katika Maombi yako kila siku Mwanangu, jitihada  zake zimeokoa Maisha yako, usilisahau hilo” Alisema Mama 

    “Sawa Mama ngoja nikapumzike” Sikutaka kumwambia chochote  Mama sababu niliamini yupo upande wa Osman, nilielekea  chumbani kwangu, ilikuwa ni nyumba nzuri ambayo sikuwahi  kuiota katika Maisha yangu, umasikini tuliupa mkono wa  kwaheri. 

    Nilitazama nje niliiyona gari yangu aliyoninunulia Osman,  nilikumbuka kipindi ambacho nilikuwa natembea kwa mguu,  nilikumbuka siku ambayo homa ilinianzia jinsi nilivyokuwa  nikitetemeka kwenye baridi, jinsi Osman alivyojitolea kiungo  chake ili kuokoa Maisha yangu, nilimshukuru kwa kumtumia  ujumbe lakini hakujibu kabisa. 

    Siku iliyofuata nilipigiwa simu na Mmoja wa Wafanyakazi wa  kampuni ya JM Motors kuwa natakiwa kuanza kazi, japo nilikuwa  na uchovu ila kazi hiyo ilikuwa ni ndoto yangu, pia niliona  ni bora nifanye kazi kwa Osman ili kumshukuru kwa ukarimu na  msaada wake, basi nilijiandaa kisha nilielekea kazini kwa  kutumia usafiri wa kukodi maana nilikuwa sijui kuendesha  gari. Nilipokelewa vizuri sana, nilioneshwa ofisi yangu,  ilikuwa ni ofisi iliyotengenezwa kwa ajili yangu, nilikuta  picha yangu ukutani

    Nikitabasamu sababu nilijuwa kuwa ni Osman ndiye aliyefanya  hivyo, nilianza kazi rasmi katika kampuni ya JM Motors,  mahusiano yangu na Osman yalipungua kwa kiasi kikubwa,  alikuwa akinisalimia tu kisha kila Mtu alikuwa akiendelea na  Maisha yake. Siku moja nilihitaji Mafaili kutoka kwenye ofisi  yake, bahati mbaya hakuwepo ofisini, nilizungumza na Msaidizi  wake akaenda kunichukulia Mafaili hayo. 

    Aliponiletea nilianza kazi yangu, lilikuwa ni faili la Watu  waliokuwa wanasubiria mzigo wa Magari ambao ulitakiwa kuingia  kesho yake, nilitakiwa kuhakiki taarifa zao, wakati naendelea  kufungua mafaili hayo nilikutana na picha ya Mwanamke mzuri  sana, tena Mzuri kuliko Mimi, yaani mzuri hadi ukimtazama  unagundua kuwa alikuwa mzuri kuliko mfano. Sikujuwa Mwanamke  huyo alikuwa akiitwa nani, nilipogeuza nyuma ya picha  nilikutana na jina limeandikwa “ZAHRA” 

    Nilishusha pumzi zangu kisha niliigeuza tena ile picha, ooh!  Huyo Zahra kumbe ndiye huyu? Anastahili kuugalagaza moyo wa  Osman,,hakika ni mzuri sana. Nilisema na Moyo wangu,  niliirudisha picha nilipoitoa. 

    Katika hali ambayo sikuielewa nilijikuta nikikosa raha hata  kufanya kazi nilishindwa nilihisi moyo unaniuma, ilikuwa ni  mishale ya saa saba Mchana, nilimuaga Mtu wa Usaidizi pale  kazini kisha niliondoka, nilifanya safari kwenda anapoishi  Mosses maana simu yake ilikuwa haipatikani, nilitumia usafiri  wa gari ya kukodi, nilipofika niligonga mlango kwenye chumba  cha Mosses, alikuwa ni Kijana mwenye Maisha ya kati tu.  Nilisubiria mlango ufunguliwe, aliyefungua alikuwa ni Mosses  mwenyewe, alinishangaa kisha alitabasamu, dimpozi zake  zikajiachia. Mosses alikuwa anajuwa kuugalagaza moyo wangu  vile atakavyo, pamoja na yote kukataa kunitolea figo bado  nilikuwa nikimpenda na sikufikiria hata siku moja kama  ningelimpenda Mwanaume mwingine, alinikumbatia akiwa amevalia  taulo tu. Mwili ukaanza kunisisimka kama napandwa na sisimizi  hivi, mikono ya Mosses ilikuwa kama sumaku vile yaani hata  anishike wapi alikuwa akinipandisha ashki zangu. 

    Nilivuta hewa kisha nilimwambia Mosses 

    “Nimekumiss sana Mosses” nilisema nikiwa nimemkumbatia kwa  nguvu, nilikuwa na hisia kali sana kwa Mosses 

    “Nimekumiss pia Jacklin, pole kwa matatizo yaliyokupata,  siamini kama bado unaishi, nilijuwa umeshakufa ndio maana  niliamuwa kubadilisha namba” Alisema Mosses akiwa ananipiga  busu shingoni, nilifumba macho kwa utamu wa Busu, nilikuwa  nusu Chizi kwa Mwanaume huyu

    “Naishi kwa ajili yako Mosses, kama siyo wewe ningelikuwa  nimekufa zamani sana ila nguvu ya Mapenzi niliyonayo juu yako  ndiyo iliyonipa uhai nikaamka tena” Nilisema pia, aliniachia  akanitazama jinsi nilivyokuwa nimependeza ilitosha kumfanya  Mosses atambuwe kuwa maisha yangu yalikuwa yamebadilika kwa  kiasi kikubwa sana. 

    “Nakupenda sana Mosses” Nilimwambia, naye alirudisha jibu  zuri sana 

    “Umenipa sababu ya kuendelea kuishi Jacklin, niliposikia kuwa  huwezi kupona nilihisi unakufa, nilitamani kufanya kila kitu  ili niokoe uhai wako” Alisema Mosses, nilijuwa ni uwongo  lakini nguvu ya mapenzi iliniambia kuwa anachokisena Mosses  kina ukweli 

    “Tuachane na hayo Mosses naomba tuongee ndani” Nilisema kisha  tuliingia chumbani kwa Mosses. Nilitazama jinsi chumba cha  Mosses kilivyo, sikupenda aendelee kuishi hapo, nilikuwa na  uwezo wa kubadilisha Maisha ya Mosses sababu nilikuwa  nikimpenda sana. 

    “Mosses kwasasa nafanya kazi, Maisha yangu yamebadilika sana.  Sitopenda uendelee kuishi hapa nitakupangia sehemu nzuri ya  kuishi” Nilimwambia Mosses 

    “Jamani kweli Jacklin?” Aliuliza kama Mtu ambaye alikuwa  amechanganikiwa 

    “Ndiyo! Hadhi yako ndani ya moyo wangu ni kubwa sana  hustahili kuishi hapa, tafuta nyumba eneo lililotulia  nitalipia kila kitu na kununua vitu vipya” Nilisema, mara  moja Mosses alinivaa na kuanza kunipiga mabusu ambayo  yaliamsha hisia zangu, nilijikuta nikiwa na hamu ya kufanya  Mapenzi na Mosses, daktari alisema sipaswi kufanya hivyo hadi  miezi sita itakapoisha lakini nilijikuta nikifanya mapenzi na  Mosses, baada ya kumaliza nilimshukuru Mosses kwa penzi tamu  alilonipa. 

    “Usijali Jacklin nipo kwa ajili yako mara zote” alisema  Mosses na kunifanya nitabasamu kwa uchovu, shughuli ilikuwa  pevu na vile nimetoka kuumwa basi nilichoka sana nikalala  palepale. 

    Osman alipofika ofisini alihitaji kuniona ila aliambiwa kuwa  nimetoka, akiwa kama Bosi wangu alihitaji kujuwa niko wapi,  alinipigia sana simu lakini haikupokelewa maana nilikuwa  nimelala chakali, basi alipiga kwa Mama na kumuuliza kama  nitakuwa nimeenda nyumbani, Mama alimwambia Osman kuwa sipo  nyumbani.

     

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TANO Ya PUMZI YA MWISHO

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOM  

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    SOMA KISASI CHANGU HAPA  

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx 

    Pumzi ya mwisho
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views
    Ligi Kuu ya NBC

    RATIBA YA LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2025/2026

    August 29, 202513K Views
    Don't Miss
    Hadithi March 23, 2026

    ZAINABU ( 01)

    NAITWA ZAINABU ALIYU! Hii ni Hadithi ya Maisha yangu…..!!  Mimi ni Mtoto wa kwanza kati…

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.