Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Nne (04)
    Hadithi

    Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Nne (04)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 14, 2024Updated:October 28, 202432 Comments8 Mins Read6K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Alipotoka Hospitalini Osman alikuwa mwenye mawazo na maumivuΒ  makali sana, alipigiwa simu na Wazazi wake na kumtaka aachaneΒ  na mpango wa kutaka kutoa figo kwani haitokuwa na faidaΒ  yoyote kwake, Wazazi wa Osman waliamini kuwa Osman alikuwaΒ  akitaka kutoa figo kwa ajili ya Mapenzi, walinuonya sana kwaΒ  kile kilichomtokea kwa Zahra ila Osman aliwaambia Wazazi wakeΒ  kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Mimi bali ni ubinadamu tuΒ  wa kutaka kuhakikisha afya yangu inaimarika.Β 

    Osman aliwasiliana na Hospitali nyingine ambayo ingefanyaΒ  operesheni ya kupandikiza figo kwenye mwili wangu, kutokanaΒ  na utajiri alionao aliweza kupata Hospitali Nchini India,Β  tulisafiri kwenda huko. Osman alishauriwa na kuambiwa kilaΒ  kitu kiafya kuhusu uamuzi wake. Endelea

    SEHEMU YA NNE

    alikubali kutoa figo.Β 

    Baada ya siku tatu, tulifanyiwa Operesheni, Osman aliondolewaΒ  Figo yake ambayo ilikuwa safi kabisa, Mimi niliondolewa Figo zangu ambazo zilikuwa na matatizo kisha ilipandikizwa Figo yaΒ  Osman katika mwili wangu. Mama yangu alikuwa ni Mtu wa kuliaΒ  na kuomba Mungu kila jambo liende sawa, siku zilienda, unafuuΒ  ulianza kuniingia, hata Osman unafuu ulimuingia, sikujuwaΒ  kilichokua kimetokea.Β 

    Ilipita miezi miwili tukiwa Hospitalini India, hali yanguΒ  ilizidi kuimarika siku hadi siku hatimaye nilipona kabisa,Β  Mimi na Osman tulipona, tuliruhusiwa tukarudi Nchini.Β  Tulifikia kwenye jumba la kifahari sana ambalo OsmanΒ  alitununulia, Maisha yalibadilika sana kwetu, OsmanΒ  alitufungulia Biashara kubwa. Nilisimuliwa kila kilichotokea,Β  niliuona upendo wa Osman, pia niliuona upendo feki wa MossesΒ 

    Siku moja Osman alinipeleka kwa Wazazi wake huko Dubai,Β  Walifurahika kuniona. Walitupokea kwa shamra shamra sana,Β  familia yao ilikuwa ni familia ya kitajiri sana.Β 

    “Karibu Jacklin katika Familia yetu” Alisema Baba yake OsmanΒ  tukiwa tunapata chakulaΒ 

    “Asante Baba, nafurahika kuwaona” nilijibuΒ 

    “Usijali Jacklin, wewe ni damu yetu sababu una kiungo chaΒ  Mtoto wetu, naona hata sura ya Osman imeng’aa kwa furaha,Β  natumaini hautofanya kama alichokifanya Zahra” Alisema MamaΒ  yake Osman, nilishtuka kidogo sababu nilikuwa simjui huyoΒ  Zahra, nilimtazama Osman akanipa ishara ya kutabasamu tu kuwaΒ  atanieleza kila kitu, kilichonishangaza ni yale maongezi yao,Β  ilionesha kuwa wao walikuwa wakijuwa kuwa Mimi na Osman niΒ  wapenzi wakati hatukuwahi kuongelea kuhusu Mapenzi.Β 

    Baada ya Chakula tulioneshwa chumba cha kulala, kilikuwa niΒ  chumba kimoja tu tulale mimi na Osman, tulipofika ChumbaniΒ  nilimuuliza OsmanΒ 

    “Zahra ni nani?” Nilimuuliza nikiwa nimekaa kitandani, yeyeΒ  alikuwa ameketi juu ya kiti.Β 

    “Mwanamke niliyempenda sana, aliyenifanya nikalia na kupotezaΒ  kila kitu katika Maisha yangu” alisema OsmanΒ 

    “Kwahiyo ulinisaidia ili unitumie Osman, umewaambia niniΒ  Wazazi wako na kwanini waseme maneno yale? Lengo lako nijeΒ  kuonekana mbaya mbele za macho yao wakati unajuwa hali halisiΒ  kuwa nina mpenzi?” Nilisema japo Mosses alikataa kutoa figoΒ  na kumjibu Mama vibaya, niliamini pengine kuna jamboΒ  hawakuelewana tuu ila bado alikuwa akinipenda nami nilikuwaΒ  nikimpenda.

    “Una mpenzi? Aliyekuacha ufe wakati alikuwa na uwezo waΒ  kukusaidia?” Alisema Osman akiwa anakaa vizuriΒ 

    “Yeye alikataa ila wewe umenisaidia ili unitumie Osman, hunaΒ  tofauti na mtu anayetoa msaada na kusubiria kulipwa. MossesΒ  ni Mwanaume anayenipenda sana pamoja na yote yaliyotokea”Β  Nilisema nikiwa ninajilazaΒ 

    “Samahani Jacklin, usiwachukie Wazazi wangu wala usiumie,Β  sikukusaidia ili niwe na wewe ila samahani sana kwa kukufanyaΒ  uhisi hivyo” Alisema Osman, sikumjibu chochote kile, nilionaΒ  alikuwa akinipenda sana ila sikuwa na hisia za kimapenzi naΒ  Osman, moyo wangu ulikuwa kwa Mosses. Tuliishi Dubai kwa wikiΒ  mbili, tulikuwa tukiongea mbele ya Wazazi wa Osman lakiniΒ  tukiwa wawili kila mmoja alikuwa kimya, tulirudi Nchini,Β  nilifurahika sana kuonana na Mama yangu kwa mara nyingineΒ  tena.Β 

    “Maisha ya huko yalikuwaje Mama” Aliuliza Mama yangu, wakatiΒ  huo Osman alikuwa ameshaondokaΒ 

    “Mazuri sana Mama, nimefurahi sababu ilikuwa ndiyo mara yaΒ  kwanza naenda nje ya Nchi” Mama alinikumbatia akaniambiaΒ 

    “Muweke Osman katika Maombi yako kila siku Mwanangu, jitihadaΒ  zake zimeokoa Maisha yako, usilisahau hilo” Alisema MamaΒ 

    “Sawa Mama ngoja nikapumzike” Sikutaka kumwambia chochoteΒ  Mama sababu niliamini yupo upande wa Osman, nilielekeaΒ  chumbani kwangu, ilikuwa ni nyumba nzuri ambayo sikuwahiΒ  kuiota katika Maisha yangu, umasikini tuliupa mkono waΒ  kwaheri.Β 

    Nilitazama nje niliiyona gari yangu aliyoninunulia Osman,Β  nilikumbuka kipindi ambacho nilikuwa natembea kwa mguu,Β  nilikumbuka siku ambayo homa ilinianzia jinsi nilivyokuwaΒ  nikitetemeka kwenye baridi, jinsi Osman alivyojitolea kiungoΒ  chake ili kuokoa Maisha yangu, nilimshukuru kwa kumtumiaΒ  ujumbe lakini hakujibu kabisa.Β 

    Siku iliyofuata nilipigiwa simu na Mmoja wa Wafanyakazi waΒ  kampuni ya JM Motors kuwa natakiwa kuanza kazi, japo nilikuwaΒ  na uchovu ila kazi hiyo ilikuwa ni ndoto yangu, pia nilionaΒ  ni bora nifanye kazi kwa Osman ili kumshukuru kwa ukarimu naΒ  msaada wake, basi nilijiandaa kisha nilielekea kazini kwaΒ  kutumia usafiri wa kukodi maana nilikuwa sijui kuendeshaΒ  gari. Nilipokelewa vizuri sana, nilioneshwa ofisi yangu,Β  ilikuwa ni ofisi iliyotengenezwa kwa ajili yangu, nilikutaΒ  picha yangu ukutani

    Nikitabasamu sababu nilijuwa kuwa ni Osman ndiye aliyefanyaΒ  hivyo, nilianza kazi rasmi katika kampuni ya JM Motors,Β  mahusiano yangu na Osman yalipungua kwa kiasi kikubwa,Β  alikuwa akinisalimia tu kisha kila Mtu alikuwa akiendelea naΒ  Maisha yake. Siku moja nilihitaji Mafaili kutoka kwenye ofisiΒ  yake, bahati mbaya hakuwepo ofisini, nilizungumza na MsaidiziΒ  wake akaenda kunichukulia Mafaili hayo.Β 

    Aliponiletea nilianza kazi yangu, lilikuwa ni faili la WatuΒ  waliokuwa wanasubiria mzigo wa Magari ambao ulitakiwa kuingiaΒ  kesho yake, nilitakiwa kuhakiki taarifa zao, wakati naendeleaΒ  kufungua mafaili hayo nilikutana na picha ya Mwanamke mzuriΒ  sana, tena Mzuri kuliko Mimi, yaani mzuri hadi ukimtazamaΒ  unagundua kuwa alikuwa mzuri kuliko mfano. Sikujuwa MwanamkeΒ  huyo alikuwa akiitwa nani, nilipogeuza nyuma ya pichaΒ  nilikutana na jina limeandikwa “ZAHRA”Β 

    Nilishusha pumzi zangu kisha niliigeuza tena ile picha, ooh!Β  Huyo Zahra kumbe ndiye huyu? Anastahili kuugalagaza moyo waΒ  Osman,,hakika ni mzuri sana. Nilisema na Moyo wangu,Β  niliirudisha picha nilipoitoa.Β 

    Katika hali ambayo sikuielewa nilijikuta nikikosa raha hataΒ  kufanya kazi nilishindwa nilihisi moyo unaniuma, ilikuwa niΒ  mishale ya saa saba Mchana, nilimuaga Mtu wa Usaidizi paleΒ  kazini kisha niliondoka, nilifanya safari kwenda anapoishiΒ  Mosses maana simu yake ilikuwa haipatikani, nilitumia usafiriΒ  wa gari ya kukodi, nilipofika niligonga mlango kwenye chumbaΒ  cha Mosses, alikuwa ni Kijana mwenye Maisha ya kati tu.Β  Nilisubiria mlango ufunguliwe, aliyefungua alikuwa ni MossesΒ  mwenyewe, alinishangaa kisha alitabasamu, dimpozi zakeΒ  zikajiachia. Mosses alikuwa anajuwa kuugalagaza moyo wanguΒ  vile atakavyo, pamoja na yote kukataa kunitolea figo badoΒ  nilikuwa nikimpenda na sikufikiria hata siku moja kamaΒ  ningelimpenda Mwanaume mwingine, alinikumbatia akiwa amevaliaΒ  taulo tu. Mwili ukaanza kunisisimka kama napandwa na sisimiziΒ  hivi, mikono ya Mosses ilikuwa kama sumaku vile yaani hataΒ  anishike wapi alikuwa akinipandisha ashki zangu.Β 

    Nilivuta hewa kisha nilimwambia MossesΒ 

    “Nimekumiss sana Mosses” nilisema nikiwa nimemkumbatia kwaΒ  nguvu, nilikuwa na hisia kali sana kwa MossesΒ 

    “Nimekumiss pia Jacklin, pole kwa matatizo yaliyokupata,Β  siamini kama bado unaishi, nilijuwa umeshakufa ndio maanaΒ  niliamuwa kubadilisha namba” Alisema Mosses akiwa ananipigaΒ  busu shingoni, nilifumba macho kwa utamu wa Busu, nilikuwaΒ  nusu Chizi kwa Mwanaume huyu

    “Naishi kwa ajili yako Mosses, kama siyo wewe ningelikuwaΒ  nimekufa zamani sana ila nguvu ya Mapenzi niliyonayo juu yakoΒ  ndiyo iliyonipa uhai nikaamka tena” Nilisema pia, aliniachiaΒ  akanitazama jinsi nilivyokuwa nimependeza ilitosha kumfanyaΒ  Mosses atambuwe kuwa maisha yangu yalikuwa yamebadilika kwaΒ  kiasi kikubwa sana.Β 

    “Nakupenda sana Mosses” Nilimwambia, naye alirudisha jibuΒ  zuri sanaΒ 

    “Umenipa sababu ya kuendelea kuishi Jacklin, niliposikia kuwaΒ  huwezi kupona nilihisi unakufa, nilitamani kufanya kila kituΒ  ili niokoe uhai wako” Alisema Mosses, nilijuwa ni uwongoΒ  lakini nguvu ya mapenzi iliniambia kuwa anachokisena MossesΒ  kina ukweliΒ 

    “Tuachane na hayo Mosses naomba tuongee ndani” Nilisema kishaΒ  tuliingia chumbani kwa Mosses. Nilitazama jinsi chumba chaΒ  Mosses kilivyo, sikupenda aendelee kuishi hapo, nilikuwa naΒ  uwezo wa kubadilisha Maisha ya Mosses sababu nilikuwaΒ  nikimpenda sana.Β 

    “Mosses kwasasa nafanya kazi, Maisha yangu yamebadilika sana.Β  Sitopenda uendelee kuishi hapa nitakupangia sehemu nzuri yaΒ  kuishi” Nilimwambia MossesΒ 

    “Jamani kweli Jacklin?” Aliuliza kama Mtu ambaye alikuwaΒ  amechanganikiwaΒ 

    “Ndiyo! Hadhi yako ndani ya moyo wangu ni kubwa sanaΒ  hustahili kuishi hapa, tafuta nyumba eneo lililotuliaΒ  nitalipia kila kitu na kununua vitu vipya” Nilisema, maraΒ  moja Mosses alinivaa na kuanza kunipiga mabusu ambayoΒ  yaliamsha hisia zangu, nilijikuta nikiwa na hamu ya kufanyaΒ  Mapenzi na Mosses, daktari alisema sipaswi kufanya hivyo hadiΒ  miezi sita itakapoisha lakini nilijikuta nikifanya mapenzi naΒ  Mosses, baada ya kumaliza nilimshukuru Mosses kwa penzi tamuΒ  alilonipa.Β 

    “Usijali Jacklin nipo kwa ajili yako mara zote” alisemaΒ  Mosses na kunifanya nitabasamu kwa uchovu, shughuli ilikuwaΒ  pevu na vile nimetoka kuumwa basi nilichoka sana nikalalaΒ  palepale.Β 

    Osman alipofika ofisini alihitaji kuniona ila aliambiwa kuwaΒ  nimetoka, akiwa kama Bosi wangu alihitaji kujuwa niko wapi,Β  alinipigia sana simu lakini haikupokelewa maana nilikuwaΒ  nimelala chakali, basi alipiga kwa Mama na kumuuliza kamaΒ  nitakuwa nimeenda nyumbani, Mama alimwambia Osman kuwa sipoΒ  nyumbani.

    Β 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TANO Ya PUMZI YA MWISHO

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ 

    Pumzi ya mwisho

    32 Comments

    1. Lus twaxie on October 14, 2024 9:57 pm

      Huyu dada n jauuuuuuuuu

      Reply
      • G shirima on October 14, 2024 10:33 pm

        Uyu dada wawapi vp mbona siyo muelewa kweli mapenzi ni giza

        Reply
    2. Farnoush on October 14, 2024 10:11 pm

      Mbona fupiiii leo
      Ila jackline ni kiazi sanaπŸ˜‚πŸ˜‚

      Reply
    3. France on October 14, 2024 10:34 pm

      Dah bora uyu mdad angekufa2😒

      Reply
      • Wiga son Tz on October 14, 2024 11:29 pm

        MH!

        Reply
      • Ngeleja on October 15, 2024 1:56 am

        Jacqueline hafai hata kwa kulumagia Dah!!😭😭😭😭😭

        Reply
    4. Maxwell on October 14, 2024 10:42 pm

      Ivi hii ndo maana ya β€œ the when a woman loves….β€πŸ˜° namhurumia Osman

      Reply
    5. Sadick on October 14, 2024 11:01 pm

      Maskini osmani daah!! Jacklin bora angekufa mwandishi naomba hii story isituboe

      Reply
      • Charz jr😎 on October 15, 2024 12:05 pm

        Siyo kuboa tuu inaweza kukuliza huko mbeleeπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

        Reply
    6. Ebia Dastanie on October 14, 2024 11:19 pm

      Yani ishaanza kuboa ila sisi wanawake basi tu jacklin wewe mmhπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

      Reply
    7. Wiga son Tz on October 14, 2024 11:30 pm

      MH!

      Reply
    8. Huncho on October 14, 2024 11:42 pm

      Sjawahi Comment Ila WANAWAKE JAU πŸ˜’πŸ˜’πŸ˜’

      Reply
      • Jacqueline Henry on October 15, 2024 7:58 am

        Fear women..

        Reply
    9. yahaya on October 14, 2024 11:45 pm

      kesho muendeleze jaman kali kinoma

      Reply
    10. yahaya on October 14, 2024 11:47 pm

      kesho muendeleze jaman kali

      Reply
    11. Oppa on October 15, 2024 1:09 am

      Jau kubabeq

      Reply
    12. [email protected] on October 15, 2024 1:43 am

      Adimn kuchoshana ww andik zeEND…..mosses anamzurum jack……akn bado Osman anamsamehe

      Reply
      • Charz jr😎 on October 15, 2024 12:03 pm

        Ahahahaha siyo kumdhulumu atakuja kumcheat uyo demu….. hii story naifananisha na tamthiliya moja inaitwa mfadhili yaani ni mule mule..badae kati ya osman ama uyo jack mmoja atakufa

        Reply
        • Angel on October 15, 2024 9:21 pm

          Kumbe na ww umeona eh…huyu ni dania kabisa yan…

          Reply
    13. Malongo on October 15, 2024 3:31 am

      Jacklin, sio

      Reply
    14. Calvin paul on October 15, 2024 6:37 am

      Fwalaaa sanaa mpaka hasira zimenipandaa wanawake bhanaa afukuzwe hata kazi tuu ubwa huyu

      Reply
    15. Yudah on October 15, 2024 7:27 am

      Madem jau sana duuh

      Reply
    16. Sabiti Mussa23 on October 15, 2024 7:46 am

      πŸ’”

      Reply
    17. Abdul (young daddy) on October 15, 2024 11:44 am

      Dah huyu dad ni zaidi ya shetan ani

      Reply
    18. Mkandarasi on October 15, 2024 11:59 am

      Mwenye huruma hanaga bahati

      Reply
    19. Charz jr😎 on October 15, 2024 12:07 pm

      EWAAAH!! DATS KAMA MLIFATILIA COMMENT ANGU YA SIKU ZA NYUMA…NILISEMA HAPO LAZIMA KUNA NAMNA ITAKUWA ANI UYO JACKLINE MPKA AJE KUFUNGUKA AKILI NI BAADAE SANA WAKATI MAMB YAMEHARIBIKAπŸ₯²πŸ₯²πŸ₯² KAMA UNAE MOYO MDGO UTALIA πŸ˜„πŸ˜„ ILA KI UHALISIA WATU NDO WALIVO JMNIII

      Reply
    20. Best mbwilo son on October 15, 2024 3:00 pm

      Wakina moses mikono juuu…….yaaan zitoke tatu kwa siku

      Reply
    21. Sir yowas on October 15, 2024 6:45 pm

      Sasa osmad anashida gani, anatongoza kwa kuhonga, binafsi sijaona kosa la jackline, kwani wameshakubaliana kuwa wapenzi?????

      Reply
    22. Dj Shoti on October 15, 2024 11:38 pm

      πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜…

      Reply
    23. Robbiey on October 16, 2024 12:19 pm

      figo ya kiume imeingiliwa au figo haina jinsia

      Reply
    24. Jackson Felician on October 18, 2024 7:54 am

      Kama ni Mimi naenda kuchukua Figo yangu

      Reply
    25. πŸ“‹ + 1.591965 BTC.GET - https://yandex.com/poll/76RuKke5vYn6W1hp2wxzvb?hs=9fd2933a2e60b65ec47a79a56b0b0662& πŸ“‹ on June 4, 2025 2:25 pm

      qqw0kc

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneΒ  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.