Ilipoishia “Umenisaliti eeh?” Aliuliza Mosses kama kawaida yake alikuwaΒ na tabia ya wivu sanaΒ
“Siwezi kukusaliti Mosses, unanijuwa vizuri. Sina ujanjaΒ kwako” nilisema lakini bila kumaanisha chochote na ilikuwaΒ ndiyo mara ya kwanza nasema kitu mbele ya Mosses bilaΒ kumaanisha, katika nyakati fulani nilijikuta nikianzaΒ kujichukia Mwenyewe.Β
Mosses alitabasamu tuu kisha alinivuta na kunipiga busu, namiΒ nilitoa tabasamuΒ
“Tulale” alisema Mosses, Basi tulilala Usiku huo hadiΒ kulipopambazuka. EndeleaΒ
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
Siku iliyofuata ilikuwa ni Jumatatu iliyoanza kwa jua kali laΒ mvua, nilimuaga Mosses, nilirudi nyumbani kujiandaa kwa ajiliΒ ya kwenda kazini japo Mosses aliniambia niache kazi, hataΒ Mama aliniulizaΒ
“Ulilala wapi na unaenda wapi?” Aliniuliza nikiwa tayari kwaΒ ajili ya kutoka nyumbani kuelekea kaziniΒ
“Shikamoo Mama!!” Nilimsalimia kwanzaΒ
“Marahaba! Siku hizi unaamuwa tu kulala unapopajuwa wewe,Β kufanya unachowaza wewe si ndiyo?” Aliniuliza, niliutupaΒ mkoba kwenye sofa kisha niliketi Mama akiwa amesimamaΒ
“Mama nililala Hotelini” Nilimjibu Mama huku Moyo ukinisuta “Na unaenda wapi?” Aliniuliza
“Naenda kazini” Nilimjibu Mama nikiwa ninafinya vidoleΒ vyangu, Basi Mama alisogea kisha aliketi kando yanguΒ
“Jacklin ningekushauri usiende huko sababu ile ni kampuni yaΒ Osman na Baba yake, kilichotokea baina yetu na ile FamiliaΒ hakiwezi kuleta picha nzuri endapo tutaendelea kujihusisha naΒ ile Familia” Alisema MamaΒ
“Mama chochote kilichotokea hakina mahusiano ya moja kwa mojaΒ na kazi ninayoifanya kwao, hii ni kazi ambayoΒ Β
tumeandikishiana mikataba labda waamuwe kuvunja mikataba”Β NilisemaΒ
“Inatosha Jacklin, usiende huko Mwanangu” Alisema Mama lakiniΒ sikutaka kumsikiliza, moyo wangu uliniambia kuwa napaswa kuwaΒ karibu zaidi na Osman japo yupo Hospitalini lakini kuwaΒ ofisini kwake kungefanya moyo wangu utulieΒ
“Mama najuwa ninachokifanya, usijali kila kitu kitaenda sawa”Β Nilisema kisha nilinyanyuka na kuondoka zangu.Β
Nilizongwa na mawazo kichwani, nilizongwa na hisia kali ndaniΒ ya moyo wangu, hisia ambazo zilinikosesha raha kabisa.Β Niliingia ofisini kwangu na kuanza kazi, nilitekelezaΒ majukumu yangu ndani ya kampuni ya JM Motors. Siku hiyo MzeeΒ Dhabi alikuja kwenye kampuni kukagua utendaji wa kaziΒ unavyoendelea, hakujuwa kama Mimi ni mmoja wa wafanyakazi,Β aliponiona aliniulizaΒ
“Wewe ni miongoni Mwao?” Akimaanisha hao Wafanyakazi “Ndiyo Baba” Nilimjibu tukiwa wawili tu ofisiniΒ
“Usiniite Baba, Niite Mzee Dhabi inatosha” Alisema MzeeΒ Dhabi, hapo ndipo nilipokumbuka maneno ya Mama kuwa siyoΒ busara sana kurudi kufanya kazi ndani ya kampuni ya BilioneaΒ Dhabi kutokana na kilichotokea kati yangu na Kijana wakeΒ
“Mbona katika orodha ya Wafanyakazi wewe haupo, OsmanΒ alikuajili vipi?” Aliuliza Mzee Dhabi kisha aliketi,Β niliiyona chuki ndani yake, nilijawa na kigugumiziΒ
“Mbona nilishajaza mkataba na kupewa hii Ofisi” nilijibuΒ
“Hapana, Mimi ndiye Mwenye hii kampuni, Osman anasimamiaΒ sababu ni Kijana wangu! Sikutambui, hakuna mkataba ulio mbeleΒ yangu” Alisema Bilionea Dhabi tena kwa sura kavu sana
“Lakini mbona nilifanya usahili hapa na kujaza mkataba waΒ kazi iweje leo nisitambulike” NiliulizaΒ
“Ni huruma ya Osman ambayo imemteketeza ndiyo iliyokufanyaΒ wewe kuwa hapa lakini hukupaswa kuwa hapa, nikiwa kamaΒ Mmiliki wa hii kampuni, sihitaji kukuona hapa kuanzia mudaΒ huu, kusanya kila kilicho chako” Alisema Bilionea Dhabi kamaΒ vile hakuwahi kuniona kabla, ujuwe nilichoka sana kuanziaΒ roho hadi mwili, ningesema nini na aliyesimama mbele yanguΒ alikuwa ndiye mmiliki wa kampuni hiyoΒ
Nilifanya kama alivyosema tena akiwa amenisimamia, niliondokaΒ kwenye kampuni ya JM Motors, nilijuwa chuki aliyoionesha MzeeΒ Dhabi ilitokana na jinsi nilivyokataa kuokoa uhai wa KijanaΒ wake japo dakika za mwisho niliufungua moyo wangu ilaΒ nilikuwa nimeshachelewa, Chozi lilinibubujika. Tayari mvuaΒ ilikuwa imeanza kunyesha.Β
Nilitembea kwenye mvua huku nikikumbuka siku ya kwanza kabisaΒ ambayo Osman alinisaidia kwenye mvua, nilipofika nyumbaniΒ nilimsimulia Mama kile kilichotokea.Β
“Nilikwambia Mwanangu lakini hata Usijali sana sababu umesomaΒ utapata kazi sehemu nyingine na Maisha yataendelea” alisemaΒ MamaΒ
“Lakini Mama, natamani sana kulipa fadhila za Osman,Β amebadilisha Maisha yetu kutoka kwenye Umasikini, ameokoaΒ Maisha yangu kutoka kifo, nilichelewa kuiyona thamani yaΒ Upendo na huruma yake” Nilisema nikiwa nimeegemea ukutaΒ
“Usijutie kwa chochote sababu anayepanga kila kitu ni MunguΒ pekee, Maisha lazima yaendelee” Alisema Mama, mara tulisikiaΒ honi ya gari. Mama alichungulia, aliona gari ya Mzee DhabiΒ ikiingia,Β
“Baba yake Osman anakuja” Alisema, nilikuwa nimelowa kutokanaΒ na ile mvua hivyo nilihitaji kubadilisha nguo haraka,Β nilielekea chumbani kwangu kubadilisha nguo, nilipotokaΒ niliwakuta Mama na Bilionea Dhabi wakiwa wameketi hapanaΒ shaka walikuwa wakinisubiria Mimi.Β
Niliketi kwa utulivu sana, nilimtazama Bilionea Dhabi ambayeΒ alikuwa ameongozana na Mke wake.Β
“Shikamoo Mama” Nilimsalimia Mama yake Osman ambaye hataΒ hakuitikia, nilipata ishara kuwa hawakuja kwa lengo zuri,Β alianza Bilionea Dhabi kusema
“Tumekuja kwa ajili ya mambo mawili makubwa, moja ni kuchukuaΒ magari ambayo Osman alikununulia, mbili ni kuchukua nyumbaΒ hii ambayo mnaishi” Alisema Mzee Dhabi kwa sura kavu sana.Β Mama alishtuka sanaΒ
“Unasemaje?” AlihojiΒ
“Pesa iliyotumika hapa ni pesa yangu Mimi, maamuziΒ ninayoyatoa yanatoka kwangu Mimi pia. Iwe mlipewa hati auΒ hamkupewa Hati ya Hapa, mnaondoka na jeuri yenu” AlisemaΒ Bilionea DhabiΒ
“Baba tafadhali sana hebu fikiria tutakwenda wapi sisi?Β Fikiria kwa kipindi hiki tutafanya nini?” Alisema Mama akiwaΒ analia, nilizidi kuumia ndani ya nafsi yanguΒ
“Kwani zamani mlikuwa mnaishi wapi? Mlikuwa mnaishi vipiΒ kabla ya kuanza kutumia pesa za Osman?” Aliuliza BilioneaΒ Dhabi, nilikaa kimya bila kusema chochote sababu sikuwa naΒ cha kusemaΒ
“Nionee huruma Mimi, Mimi ni mtu mzima nitaishi vipi Baba,Β fikiria hilo ina maana makosa ya Binti yangu yanatufanya tuweΒ maadui?” Aliuliza Mama akiwa katika hali ile. Ile ya kilioΒ
“Siyo maadui tu bali ni maadui wa Maisha, adui wa Maisha yaΒ Kijana wangu ni adui yangu pia, mna siku mbili za kuhakikishaΒ mnahama hapa, gari zinaondoka sasa hivi” Alisema BilioneaΒ Dhabi kisha yeye na Mke wake walinyanyuka, Mke wa BilioneaΒ Dhabi hakusema chochote kama ambavyo Mimi sikusema chochote,Β Mama na Bilionea Dhabi ndio ambao walikuwa wakirushianaΒ manenoΒ
“Nakuomba tuonee huruma sisi, tutaenda wapi, siku mbiliΒ jamani Aaah” Mama alisema lakini hakukuwa na maelewano, MzeeΒ Dhabi aliondoka bila hata kuchukua Funguo za Magari. NililiaΒ sana, nilikumbuka kuwa Kulikuwa na pesa kwenye akaunti yaΒ Benki zaidi ya Milioni 60 ambazo Osman alinipatia, kadiΒ ilikuwa kwa Mosses, haraka nilimpigia na kuhitaji kuonanaΒ naye.Β
Alinielekeza alipo niliondoka na kumuacha Mama akiwa analia,Β nilienda kuonana na Mosses. Nilimsimulia kilichotokea,Β nilihitaji Milioni 40 ili kununua nyumba ya kuishi Na MamaΒ ila majibu ya Mosses yalinigandisha damu, alisema Pesa zoteΒ aliziweka kwenye Biashara yake ya Mazao hivyo nisubirie ndaniΒ ya mwezi mmoja angenipatia pesa hizo.
“Lakini Mosses mbona hukuniambia kama unafungua Biashara?Β Unafikiria ndani ya huo mwezi Mimi na Mama tutakuwa tunaishiΒ wapi?” Nilimuuliza MossesΒ
“Sasa Jacklin unafikiria pesa inahifadhiwa benki kama pamboΒ la nyumba? Pesa ni lazima izunguke ili izae halafu Mimi niΒ Mwanaume nimefanya maamuzi ya kiume” Alisema Mosses, suraΒ yake ilianza kutanda hasira. Sikutaka kuendelea kubishanaΒ naye nilimkubaliaΒ
“Sawa Mume wangu! Nakutegemea wewe kwasasa” nilisema “Usijali” alijibu Mosses, nilimuaga nikarudi nyumbani kwetu.Β
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI NA MBILI Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ
14 Comments
π₯π₯π₯π₯π₯π₯π₯π₯
Thank you, hapo good,
Fupi sana Jamani dah
Anakumbuka shuka kumesha kucha
Mambo ni Fire oooooohπ₯π₯π₯π₯π₯ amechezea bahati ona anavyopata tabu…! Hivi dunia ya sasa wapo watu kama kina jack maaaana oh mie weeee mapema na kwa haraka sana ningemkubalia osman I donβt care na mahusiano yanguπ€ͺπ€ͺππΌππΌππΌππΌ
Unyama liwaya zuri
Kwann hamna comment ya voice note jmn duuh ila admin endelea ubaya ubwelaπ₯π₯π₯π₯π₯
Kilanga koma
π€£ukiskia mtot kautak ndy huku saaa π€£kibur hakisaidii kitu jack na kibur chak cha uzima xhek xxπ€£π
Ya leo umetuonea fupi sana..
Au kwasababu ya utamu?
Ivi mnaniruhusu nmtukane Jack maana nnavompatia hasira jaman π€¨π
Jaman jack amazingatia mno mapenz kuliko maokoto
Shida yangu afee tuu uyo binti
Jack chanπ€π€
6ciw4u