Ilipoishia “Umenisaliti eeh?” Aliuliza Mosses kama kawaida yake alikuwaย na tabia ya wivu sanaย
“Siwezi kukusaliti Mosses, unanijuwa vizuri. Sina ujanjaย kwako” nilisema lakini bila kumaanisha chochote na ilikuwaย ndiyo mara ya kwanza nasema kitu mbele ya Mosses bilaย kumaanisha, katika nyakati fulani nilijikuta nikianzaย kujichukia Mwenyewe.ย
Mosses alitabasamu tuu kisha alinivuta na kunipiga busu, namiย nilitoa tabasamuย
“Tulale” alisema Mosses, Basi tulilala Usiku huo hadiย kulipopambazuka. Endeleaย
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
Siku iliyofuata ilikuwa ni Jumatatu iliyoanza kwa jua kali laย mvua, nilimuaga Mosses, nilirudi nyumbani kujiandaa kwa ajiliย ya kwenda kazini japo Mosses aliniambia niache kazi, hataย Mama aliniulizaย
“Ulilala wapi na unaenda wapi?” Aliniuliza nikiwa tayari kwaย ajili ya kutoka nyumbani kuelekea kaziniย
“Shikamoo Mama!!” Nilimsalimia kwanzaย
“Marahaba! Siku hizi unaamuwa tu kulala unapopajuwa wewe,ย kufanya unachowaza wewe si ndiyo?” Aliniuliza, niliutupaย mkoba kwenye sofa kisha niliketi Mama akiwa amesimamaย
“Mama nililala Hotelini” Nilimjibu Mama huku Moyo ukinisuta “Na unaenda wapi?” Aliniuliza
“Naenda kazini” Nilimjibu Mama nikiwa ninafinya vidoleย vyangu, Basi Mama alisogea kisha aliketi kando yanguย
“Jacklin ningekushauri usiende huko sababu ile ni kampuni yaย Osman na Baba yake, kilichotokea baina yetu na ile Familiaย hakiwezi kuleta picha nzuri endapo tutaendelea kujihusisha naย ile Familia” Alisema Mamaย
“Mama chochote kilichotokea hakina mahusiano ya moja kwa mojaย na kazi ninayoifanya kwao, hii ni kazi ambayoย ย
tumeandikishiana mikataba labda waamuwe kuvunja mikataba”ย Nilisemaย
“Inatosha Jacklin, usiende huko Mwanangu” Alisema Mama lakiniย sikutaka kumsikiliza, moyo wangu uliniambia kuwa napaswa kuwaย karibu zaidi na Osman japo yupo Hospitalini lakini kuwaย ofisini kwake kungefanya moyo wangu utulieย
“Mama najuwa ninachokifanya, usijali kila kitu kitaenda sawa”ย Nilisema kisha nilinyanyuka na kuondoka zangu.ย
Nilizongwa na mawazo kichwani, nilizongwa na hisia kali ndaniย ya moyo wangu, hisia ambazo zilinikosesha raha kabisa.ย Niliingia ofisini kwangu na kuanza kazi, nilitekelezaย majukumu yangu ndani ya kampuni ya JM Motors. Siku hiyo Mzeeย Dhabi alikuja kwenye kampuni kukagua utendaji wa kaziย unavyoendelea, hakujuwa kama Mimi ni mmoja wa wafanyakazi,ย aliponiona aliniulizaย
“Wewe ni miongoni Mwao?” Akimaanisha hao Wafanyakazi “Ndiyo Baba” Nilimjibu tukiwa wawili tu ofisiniย
“Usiniite Baba, Niite Mzee Dhabi inatosha” Alisema Mzeeย Dhabi, hapo ndipo nilipokumbuka maneno ya Mama kuwa siyoย busara sana kurudi kufanya kazi ndani ya kampuni ya Bilioneaย Dhabi kutokana na kilichotokea kati yangu na Kijana wakeย
“Mbona katika orodha ya Wafanyakazi wewe haupo, Osmanย alikuajili vipi?” Aliuliza Mzee Dhabi kisha aliketi,ย niliiyona chuki ndani yake, nilijawa na kigugumiziย
“Mbona nilishajaza mkataba na kupewa hii Ofisi” nilijibuย
“Hapana, Mimi ndiye Mwenye hii kampuni, Osman anasimamiaย sababu ni Kijana wangu! Sikutambui, hakuna mkataba ulio mbeleย yangu” Alisema Bilionea Dhabi tena kwa sura kavu sana
“Lakini mbona nilifanya usahili hapa na kujaza mkataba waย kazi iweje leo nisitambulike” Niliulizaย
“Ni huruma ya Osman ambayo imemteketeza ndiyo iliyokufanyaย wewe kuwa hapa lakini hukupaswa kuwa hapa, nikiwa kamaย Mmiliki wa hii kampuni, sihitaji kukuona hapa kuanzia mudaย huu, kusanya kila kilicho chako” Alisema Bilionea Dhabi kamaย vile hakuwahi kuniona kabla, ujuwe nilichoka sana kuanziaย roho hadi mwili, ningesema nini na aliyesimama mbele yanguย alikuwa ndiye mmiliki wa kampuni hiyoย
Nilifanya kama alivyosema tena akiwa amenisimamia, niliondokaย kwenye kampuni ya JM Motors, nilijuwa chuki aliyoionesha Mzeeย Dhabi ilitokana na jinsi nilivyokataa kuokoa uhai wa Kijanaย wake japo dakika za mwisho niliufungua moyo wangu ilaย nilikuwa nimeshachelewa, Chozi lilinibubujika. Tayari mvuaย ilikuwa imeanza kunyesha.ย
Nilitembea kwenye mvua huku nikikumbuka siku ya kwanza kabisaย ambayo Osman alinisaidia kwenye mvua, nilipofika nyumbaniย nilimsimulia Mama kile kilichotokea.ย
“Nilikwambia Mwanangu lakini hata Usijali sana sababu umesomaย utapata kazi sehemu nyingine na Maisha yataendelea” alisemaย Mamaย
“Lakini Mama, natamani sana kulipa fadhila za Osman,ย amebadilisha Maisha yetu kutoka kwenye Umasikini, ameokoaย Maisha yangu kutoka kifo, nilichelewa kuiyona thamani yaย Upendo na huruma yake” Nilisema nikiwa nimeegemea ukutaย
“Usijutie kwa chochote sababu anayepanga kila kitu ni Munguย pekee, Maisha lazima yaendelee” Alisema Mama, mara tulisikiaย honi ya gari. Mama alichungulia, aliona gari ya Mzee Dhabiย ikiingia,ย
“Baba yake Osman anakuja” Alisema, nilikuwa nimelowa kutokanaย na ile mvua hivyo nilihitaji kubadilisha nguo haraka,ย nilielekea chumbani kwangu kubadilisha nguo, nilipotokaย niliwakuta Mama na Bilionea Dhabi wakiwa wameketi hapanaย shaka walikuwa wakinisubiria Mimi.ย
Niliketi kwa utulivu sana, nilimtazama Bilionea Dhabi ambayeย alikuwa ameongozana na Mke wake.ย
“Shikamoo Mama” Nilimsalimia Mama yake Osman ambaye hataย hakuitikia, nilipata ishara kuwa hawakuja kwa lengo zuri,ย alianza Bilionea Dhabi kusema
“Tumekuja kwa ajili ya mambo mawili makubwa, moja ni kuchukuaย magari ambayo Osman alikununulia, mbili ni kuchukua nyumbaย hii ambayo mnaishi” Alisema Mzee Dhabi kwa sura kavu sana.ย Mama alishtuka sanaย
“Unasemaje?” Alihojiย
“Pesa iliyotumika hapa ni pesa yangu Mimi, maamuziย ninayoyatoa yanatoka kwangu Mimi pia. Iwe mlipewa hati auย hamkupewa Hati ya Hapa, mnaondoka na jeuri yenu” Alisemaย Bilionea Dhabiย
“Baba tafadhali sana hebu fikiria tutakwenda wapi sisi?ย Fikiria kwa kipindi hiki tutafanya nini?” Alisema Mama akiwaย analia, nilizidi kuumia ndani ya nafsi yanguย
“Kwani zamani mlikuwa mnaishi wapi? Mlikuwa mnaishi vipiย kabla ya kuanza kutumia pesa za Osman?” Aliuliza Bilioneaย Dhabi, nilikaa kimya bila kusema chochote sababu sikuwa naย cha kusemaย
“Nionee huruma Mimi, Mimi ni mtu mzima nitaishi vipi Baba,ย fikiria hilo ina maana makosa ya Binti yangu yanatufanya tuweย maadui?” Aliuliza Mama akiwa katika hali ile. Ile ya kilioย
“Siyo maadui tu bali ni maadui wa Maisha, adui wa Maisha yaย Kijana wangu ni adui yangu pia, mna siku mbili za kuhakikishaย mnahama hapa, gari zinaondoka sasa hivi” Alisema Bilioneaย Dhabi kisha yeye na Mke wake walinyanyuka, Mke wa Bilioneaย Dhabi hakusema chochote kama ambavyo Mimi sikusema chochote,ย Mama na Bilionea Dhabi ndio ambao walikuwa wakirushianaย manenoย
“Nakuomba tuonee huruma sisi, tutaenda wapi, siku mbiliย jamani Aaah” Mama alisema lakini hakukuwa na maelewano, Mzeeย Dhabi aliondoka bila hata kuchukua Funguo za Magari. Nililiaย sana, nilikumbuka kuwa Kulikuwa na pesa kwenye akaunti yaย Benki zaidi ya Milioni 60 ambazo Osman alinipatia, kadiย ilikuwa kwa Mosses, haraka nilimpigia na kuhitaji kuonanaย naye.ย
Alinielekeza alipo niliondoka na kumuacha Mama akiwa analia,ย nilienda kuonana na Mosses. Nilimsimulia kilichotokea,ย nilihitaji Milioni 40 ili kununua nyumba ya kuishi Na Mamaย ila majibu ya Mosses yalinigandisha damu, alisema Pesa zoteย aliziweka kwenye Biashara yake ya Mazao hivyo nisubirie ndaniย ya mwezi mmoja angenipatia pesa hizo.
“Lakini Mosses mbona hukuniambia kama unafungua Biashara?ย Unafikiria ndani ya huo mwezi Mimi na Mama tutakuwa tunaishiย wapi?” Nilimuuliza Mossesย
“Sasa Jacklin unafikiria pesa inahifadhiwa benki kama pamboย la nyumba? Pesa ni lazima izunguke ili izae halafu Mimi niย Mwanaume nimefanya maamuzi ya kiume” Alisema Mosses, suraย yake ilianza kutanda hasira. Sikutaka kuendelea kubishanaย naye nilimkubaliaย
“Sawa Mume wangu! Nakutegemea wewe kwasasa” nilisema “Usijali” alijibu Mosses, nilimuaga nikarudi nyumbani kwetu.ย
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI NA MBILI Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย
14 Comments
๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Thank you, hapo good,
Fupi sana Jamani dah
Anakumbuka shuka kumesha kucha
Mambo ni Fire ooooooh๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ amechezea bahati ona anavyopata tabu…! Hivi dunia ya sasa wapo watu kama kina jack maaaana oh mie weeee mapema na kwa haraka sana ningemkubalia osman I donโt care na mahusiano yangu๐คช๐คช๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ
Unyama liwaya zuri
Kwann hamna comment ya voice note jmn duuh ila admin endelea ubaya ubwela๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Kilanga koma
๐คฃukiskia mtot kautak ndy huku saaa ๐คฃkibur hakisaidii kitu jack na kibur chak cha uzima xhek xx๐คฃ๐
Ya leo umetuonea fupi sana..
Au kwasababu ya utamu?
Ivi mnaniruhusu nmtukane Jack maana nnavompatia hasira jaman ๐คจ๐
Jaman jack amazingatia mno mapenz kuliko maokoto
Shida yangu afee tuu uyo binti
Jack chan๐ค๐ค
6ciw4u