Ilipoishia “Fanya haraka” Akaelekezwa mahali ambapo angemwona Matilda,ย japo dakika mbili zisingetoshea kuzungumza naye ila alihitajiย kumwona na kupata uhakika kua ana Mtoto na Bosi wake,ย akapelekwa chumba kimoja ambacho kilikua rasmi kwa ajili yaย kuonana na Mahabusu, akasubiria hapo Matilda aletwe, sekundeย chache Matilda akafika hapo akiwa ameongozana na yule Polisiย
Hakumkumbuka Jack sababu alimwona kwa Mara ya kwanza paleย ofisini kwa James hivyo ilikua rahisi kwake kukubali kuonanaย na Jack, akaketi huku akiwa anamtazama sana Jackย
“Samahani na pole Matilda, Naitwa Jack” Alijitambulisha Jackย
“Unanifahamu Mimi?” akauliza Matilda akionekana alikuaย ameteswa sana, uso ulikua na majeraha kadhaaย
“Ndiyo nakufahamu japo si sana”ย Endelea
SEHEMU YA SITAย
“Mbona Mimi sikufahamu?” akauliza Matildaย
“Mimi ni mfanyakazi wa James, nimekuja nahitaji kujua baadhiย ya vitu kutoka kwako” Akasema Jackย
“Kwahiyo James amekutuma uje kwangu unilaghai kwa kutegemeaย kua nitakubali si ndiyo, sikia nikwambie kitu kimoja,ย Nimeamua kuishi Maisha ambayo sitaki kuitwa Msaliti na Mtotoย wangu, nitasimama naye hadi mwisho na kama unafikiria utawezaย basi nakwambia katu hautoweza kunishawishi kwa chochote kile,ย nenda kamwambie James, kama Mtoto wangu atakufa basi atabebaย msalaba na kamwe sitakubali” Alisema kwa hasira sana Matildaย hadi yule polisi akaona ni bora amrejeshe Mahabusu maanaย kusingezungumzika kabisaย
“Sina nia hiyo Matilda nakuomba unisikilize” akazungumzaย lakini Matilda aliondolewa hapo, kisha baadaye yule polisiย akamfuata Jackย
“Usirudi tena, hii ilikua nafasi pekee”ย
“Lakini sikua na nia ya kumkasirisha kabisa, nilihitajiย kumsaidia” Akasema Jackย
“Hayo hayanihusu Mimi, nimetenda wema niliopaswa kukutendea,ย utamsaidiaje ni juu yako” Akasema Polisi huku akimtaka Jackย aondoke Kiunyonge sana tofauti na alivyoingia kituoni, Jackย alionekana akishusha ngazi kwa kutumia kiatu chake kirefu,ย Macho yake yakatua waliposimama Mchungaji na Mama Naomi, Maraย moja wakasogea karibu kumpokeaย
“Vipi umefanikiwa kumwona?” akauliza Mchungajiย
“Anaendeleaje?” akauliza Mama Naomi huku nyuso zao zikioneshaย shahuku kubwa ya kutaka kujua kilichotokea huko ndaniย
“Hataki kuzungumza na Mimi, inaonesha ana maumivu makaliย sana” Akasema Jack akiwa anasogea karibu na gari yake,ย Mchungaji na Mama Naomi wakiwa wanamfuataย
“Yupo salama?” akauliza Mchungaji, Jack akatikisa kichwa kamaย ishara ya kua Matilda hayupo salama.ย
“Niambie Matilda amekuaje?” alihoji Mchungaji, yeye ndiyeย aliyempokea Matilda kanisani kwa mara ya kwanza. hivyoย Matilda kwake ni sawa na Mtoto wa kumzaa.ย
“Siwezi kuzungumza nahitaji kutuliza akili kuona ninamsaidiaย vipi, Tutawasiliana” akasema Jack kisha akaingia kwenye gariย yake na kuondoka hapo haraka sana, akawaacha Mchungaji naย Mama Naomi wakiwa hawajui kilichoendelea kati ya Jack naย Matilda.ย
“Ni bora angeeleza kiilichotokea kuliko kukaa kimya, hapanaย shaka amemwona Matilda, roho inaniuma sana” Alisema Mamaย Naomi akionekana kujawa na uchungu, chozi lilimlenga, alikuaย hajatulia tokea asubuhi kwa ajili ya Matildaย
“Naomba urudi nyumbani giza linaanza kuingia, pesa hiiย itakusaidia. Mimi narudi kanisani kwa ajili yaย maombi….Najua shetani yupo mahali anafanya kazi yake”ย Akasema Mchungaji kisha akampatia noti ya Elfu Kumi Mamaย Naomiย
“Lakini Mchungaji natamani nilale hapa ili nijue Matildaย anapitia wakati gani, naona kama tunamzika Matilda bilaย kusikia kilio chake” Akasema Mama Naomi akiwa ameshika notiย mkononi huku chozi likianza kuvujaย
“Usilie..Hakuna marefu yasiyo na Ncha, kua na imani kua Munguย atatenda na Matilda atatoka”
“Sawa Mchungaji” Alisema Mama Naomi, akaita Bajaji kwa ajiliย ya kurejea anapoishi maana kwa muda huo ingekua shughuli pevuย kupata daladala, kwa wanaoishi Dar wanajua liingiapo gizaย vurugu za kugombania usafiri zinavyochukua sura tofauti.ย
Mchungaji alisubiria hadi Mama Naomi alipoondoka ndipo nayeย akaondoka kituoni.ย
********ย
Mawazo chungu mzima yalikua yakipita kwenye kichwa chaย Bilionea James, alikunywa pombe ili kuondoa mawazo yaliyokuaย kichwani pake, moyo wake haukua na pingamizi kua Mtoto Patraย alikua ni damu yake lakini Neema alikua na ujauzito ambaoย aliamini wazi ni wake.ย
Alikua na tumaini kubwa la kupata Mtoto ambaye angekuja kuaย Mrithi wa utajiri wake uliokithiri, hakupokea simu ya Neemaย wala Mama yake Neema, alizidi kuchanganikiwa, licha yaย utajiri alio nao lakini alijikuta katika wakati mgumu sanaย kisa Mtoto, akifikiria namna Matilda na Mtoto wanavyotesekaย anajikuta akikuna kichwa chake, alitamani sana kumsaidiaย Matilda lakini pia wazo la kua Mtoto afe lilikua likimtawala,ย kauli ya Matilda kua atahakikisha anamfilisi ilianza kumyimaย raha, akamtafuta Chilo ili apate ushauriย
“Yupo sahihi sababu ana Mtoto ambaye akipimwa DNAย itagundulika wazi ni wako, akikufungulia kesi unafikiriaย utatokea wapi Kaka? Hii serikali haiangalii una pesa kiasiย gani, kwa kifupi alichosema ana uhakika nacho James” Alisemaย Chilo wakiwa wameketi mahali wakipeana Ushauriย
“Sasa nifanye nini, Nimhudumie Mtoto kisha nimtoe Matilda?”ย
“Kama amekataa kurejea kwao hata kama utafanya yote badoย atakugandamiza James, Kama nilivyokwambia serikali ipo machoย sana kwa kesi za namna hii”ย
“Sasa unanishauri lipi Kaka”ย
“Kubali kua Patra ni Binti yako, mlee kama Binti yako, mfanyeย Matilda aone mpo pamoja kisha mfanye wa siri ili Neema asijueย chochote hadi pale atakapojifungua”ย
“Ushauri wako ni mzuri sana, nimetafakari usiku kuchaย nawezaje kumaliza hili jambo katika namna ambayo itaniachaย salama”ย
“Ikishindikana njia hiyo Kaka juwa kua hilo jambo ni gumuย kuliko ufikiliavyo, hapana shaka Matilda ana hasira naweย kwasababu anahisi wewe umeshilikiana na Neema ili kumwekaย yeye ndani” Alisema Chiloย
“Naamini Patra akipatiwa matibabu hilo haliwezi kua shida kwaย Matilda, ikibidi nitamtibia nje ya Nchi ili Matilda aende naย Mtoto huko, hadi wao watakaporejea Nchini nitakuwaย nimejipanga vizuri kuhakikisha hakuna kinachoharibika”ย
“Tena hapo utakua umeuwa ndege wawili kwa jiwe moja Kaka,ย Acha Neema aamini kua Matilda amerudi kwao lakini upande waย pili unapambana kuhakikisha anatibiwa, naamini utashinda”ย
Haikua rahisi kwa Jack kupata Usingizi usiku huo, taswira yaย Patra namna anavyoteseka Hospitalini iliendelea kujirudiaย katika Ufahamu wake wa akili, alijikuta akiwa katika nyakatiย ambayo kila alichokiwaza kilizidi kuibomoa akili yake, ikawaย ngumu kuukubali ukweli kua Bosi wake James alikua ametendaย unyama ule.ย
*****ย
Asubuhi mapema, Jack akaondoka katika makazi yake, alifungaย safari kuelekea kwa Mama yake James. Naam! alihitaji zaidiย kujua baadhi ya mambo ambayo yangemfanya apate njia yaย kulianza jambo hilo ambalo aliona wazi lilimhitaji kwa kiasiย kikubwa, alipahafahamu kwa Mama yake James, hata Mama yakeย James alikua akimfahamu sana Jack, alipomwona alimkaribishaย ndani.ย
Jua lilikua tayari limeshaanza kuchoma na kuunguza ngozi,ย chai ikawa tayari, wakaketi mezani kwa ajili ya kuzungumza,ย Mama James alishagundua kua kuna jambo lililomleta Jack paleย
“Karibu sana Jacklin” Alisema Mama yake Jamesย
“Ahsante Mama”ย
“Umenisusa sana Mwanangu”ย
“Aaah Mama unajua majukumu ni mengi nakosa hata muda wa kujaย huku siku hizi”ย
“Wala usijali naelewa”ย
“Mama kuna jambo linanitatiza sana katika akili yangu,ย limekua ni jambo lililobadili kabisa mtazamo wangu juu yaย James” Alisema Jack kisha alimtazama Mama yake James ambayeย alikaa vizuri kumsikiliza huku chai ikiwa inatoa mvuke
“Jambo lipi hilo mbona unanitisha Jack”ย
“Mama….sijui hata nianzie wapi, naomba kujua, James anaย watoto wangapi?” aliuliza Jack, Mama James akashusha pumziย baada ya kusikia swali hiloย
“James hana Mtoto..”ย
“Una hakika Mama?”ย
“Jack, Mimi ndiye Mama Mzazi wa James, akiwa na jambo niย lazima anishirikishe……Hajawahi niambia chochote kileย kuhusu kua na Mtoto, isipokua yupo Msichana anayetarajiaย kumzalia Mtoto, huyu namfahamu sababu alishawahi kumletaย Hapa, zaidi ya hapo hakuna Jack…sijui ni kwanini umeulizaย ย hilo swali”ย
“Mama naomba nikwambie hili jambo, pengine nitatua mzigoย fulani kichwani pangu, James ana Mtoto ana miaka mitatu sasaย anaitwa Patra” Alisema Jack, Mama James akashtuka kidogoย
“James ana Mtoto? hilo haliwezekani Jack, hawezi kua na Mtotoย alafu anifiche Mimi, angeniambia tu” akasema Mama Jamesย
“Hata Mimi nilishtuka na sikuamini kama wewe ambavyo huamini,ย Mama,,James kua na Mtoto siyo tatizo ila tatizo ni kwanbaย amemkataa huyo Mtoto kwasababu ni Mlemavu, na Hapaย ninapozungumza Mtoto huyo yupo Hospitali Magomeni hali yakeย siyo nzuri, Mama wa Mtoto yupo polisi kwa kesi ambayoย inaonekana wazi kua James ameitengeneza…”ย
“Jack hivi unajua unazungumza maneno mazito sana ambayoย hayaingii akilini mwangu, James hajawahi niambia kua anaย Mtoto. Hili jipya kulisikia.”ย
“Mama hiyo ndiyo hali halisi, Mtoto amefanana sana na James.ย Nimekuja hapa sababu sitaki Mjukuu wako azidi kuteseka,ย sikujua kama James hakukwambia kuhusu hili, Mama nakuombaย fanya jambo katika hili vinginevyo Mtoto anaweza kufarikiย kule Hospitalini” Akasema Jack akiwa na uso ulio poteza nuru,ย alihitaji huruma ya Mama James kuingilia kati huku akiaminiย fika kua si rahisi kumfikia James ambaye ndiye Bosi wakeย
“Jack nahitaji kwanza kumwona huyo Mtoto ”ย
“Kama tunaweza ongozana Hospitali muda huu itakua vizuriย Mama”
“Sawa!!” Mama James na Jack wakakubaliana kua waelekeeย Hospitali kwa ajili ya kumwona Patra.ย
Asubuhi hiyo, Neema akaelekea kituo cha polisi, akazungumzaย na yule polisi ambaye alishapewa pesa ili kumshikiliaย Matilda, wakazungumza kwa dakika kadhaa kisha Neema akaondokaย hapo, kitendo cha kupokea simu ya polisi kua James aliendaย Polisi kilimfanya atengeneze mpango mwingine kwa ajili yaย kutekeleza takwa lake kwa Matilda ambaye kadili mudaย ulivyokua ukienda alikua akiendelea kuteseka pale kituo chaย polisi, yule polisi akarudi ndani ya kituo maana maongeziย yalifanyika ndani ya gari ya Neema.ย
Masaa matatu yakapita baada ya polisi kuzungumza na Neema,ย Mchungaji George alikua nje ya kituo hicho huku akimpa Mamaย Naomi jukumu la kushinda kule Hospitali, gari ya polisiย ikatoka. Mchungaji akaitazama sana gari hiyo pasipo kujuaย kulikua na mpango ambao Neema alikua amepanga kuufanya.ย Matilda alikua akihamishwa hapo kituoni muda huo huku ndaniย ya kituo cha polisi kukiwa na jarada la kuachwa huru kwaย Matilda, nje kidogo ya kituo Neema aliingia kwenye gari baadaย ya kuliona gari la Polisi likitoka hapo, akalifuata kwaย nyuma.ย
*********ย
“Dada, huyu ni Mama yake James” Ilikua ni sauti ya Jack, Mamaย Naomi alimuona Mama James kwa mara ya kwanza, akamsalimia kwaย heshima sanaย
“Mama huyu ni kama ndugu kwa Matilda ndiye anayeshinda hapaย Hospitali kuangalia hali ya Mjukuu wako” Alisema Jack, Mamaย James hakutaka kuyaamini maneno ya Jack hadi paleย atakapomwona Patra, wakapewa ruhusa na Daktari kishaย wakaingia ndani ya wodi, Mama James akamwona Patra kwa maraย ya kwanza, alikua katika Mshangao Mkubwa sana, sura ya Patraย ilikua imefanana sana na sura ya James, Chozi la Mama Jamesย likaanza kutiririka kila alivyozidi kumwangalia Patra, siyoย tu kwasababu ni Mjukuu wake bali kilichomliza ni jinsiย ambavyo Patra alikua juu ya kitanda akipigania uhai wake,ย Mashine pekee ndizo zilizokua zikimpa uhai Mtoto huyoย
“Kwanini hukuniambia James?” aliuliza Mama yake James akiwaย ameshikilia kitanda kwa uchungu mkubwa sana, Jack akasogea naย kumshika Mkono Mama James akimtaka atulize hasira zakeย
“Mama hiyo ndiyo hali halisi, jinsi unavyoumia wewe ndivyoย ambavyo Mama wa Mtoto huyu anaumia akiwa kituo cha polisi”ย Alisema Jack huku Mama Naomi akiwa ametulia kimya
“Jack, miaka yangu 65 katika huu uso wa Dunia, sikuwahiย kuumia kama ambavyo leo naumia, hili ni Pigo Takatifu kwangu,ย najiuliza kwanini James hakutaka kusema juu ya ujauzito hadiย Mtoto anazaliwa, Sina Mtoto mwingine zaidi ya James, pengineย sina Mjukuu zaidi ya huyu aliyelala hapa, lazima nipiganieย uhai wake” Alisema Mama yake James.ย
“Lakini Mama pamoja na yote, sitaki James agundue kua Mimiย ndiye niliyekupa hizi taarifa”ย
“Hilo usijali Jack, kikubwa ni huyu Mtoto awe salama,ย atahamishwa hapa na kutibiwa kwa siri, kwakua James alimkataaย huyu Mimi nitalifanya hili kwa siri sana, pia nipo tayariย kuandaa wakili kwa ajili ya huyo Msichana aliye polisi,ย nitalimaliza hili bila kuharibu upande wowote ule” Akasemaย Mama yake Jamesย
Muda wote huo Mama yake Naomi alikua akilia kwa furaha baadaย ya mzigo huo kutuliwa, mzigo ulikua mzito upande wao maanaย ilikua ni ngumu sana kupata pesa za matibabu ya Mtoto.ย
Mama James akazungumza na uongozi wa Hospitali kwa ajili yaย kumhamisha Patra kumpeleka Muhimbili kwa ajili ya Upasuaji,ย jambo hilo likafanyika haraka sana, Gari maalum ya wagonjwaย ikaondoka na Patra na Mama Naomi huku Jack na Mama Jamesย ย
wakielekea Polisi kwa ajili ya kuzungumza na Matilda, hadiย kufikia muda huo hakuna aliyajua kua Matilda alikuaย ameondolewa kituo cha polisi huku mpango huo ukisukwa naย Neema.ย
Safari ya gari ya polisi ilikua ni nje kabisa ya Jiji laย Dar-es-salaam, palikua na jumba moja lililo kando ya Msitu,ย Matilda akaingizwa ndani ya jumba hilo lililoonekana kutuliaย sana, Neema akaingia pia.ย
“Kua Makini nimefanya kwa upande wangu, nahitaji hicho kiasiย kabla ya kupambazuka ili kama kuna kitakachotokea nisife kamaย Mzoga” Akasema Polisi ambaye alicheza mchezo huo waย kumhamisha Matilda na kuaandaa Jarada kua aliachiwa huruย
“Ndani ya Masaa 12 kuanzia sasa kiasi kitakua ndani yaย akaunti yako, ondoa shaka. Ahsante kwa hili, nikwambie tu kuaย kazi yako imeishia hapa lakini si mwisho wa Mimi na wewe, huuย ni mwanzo mzuri” Alisema Neema kisha akatoa bahasha ambayoย ilikua imetuna akampatia Polisi huyo, Polisi akachunguliaย akaona alichokiona ambacho kilimfanya atabasamu, kishaย akaondoka hapo mara moja.
Matilda hakujua amepelekwa wapi, Nani aliye nyuma ya mchezoย huo, mara akasikia mlango ukifunguliwa katika chumba ambachoย alikuwepo, akamwona Neema akiingia, aliongozana na Wanaumeย wawili ambao walijazia vizuri, Matilda hakusema chochoteย baada ya kumwona Neemaย
“Ulihisi natania Matilda, pengine hujui wewe ni kikwazo kiasiย gani katika mipango yangu, uwepo wako ni tatizo kubwa kwangu”ย Alisema Neemaย
“Mimi sijakuzuia kumzalia James, lakini siwezi kuishiย mafichoni kisa wewe” Akasema Matilda, akapigwa kofiย
“Hivi unajua unazungumza nini wewe Mshenzi? James ana Mtotoย mmoja tu, huyu aliye tumboni na si vinginevyo, kwanini unakuaย king’ang’anizi, sasa utakua hapa na Dunia itakutafuta sanaย Matilda, hakuna atakayekuja kukusaidia hapa, na kamaย utaendelea kuleta ubishi basi nitamuuwa Binti yako” Alisemaย Neema, alionesha wazi kua hakua Mtu wa masiala kabisaย
“Unasemaje….Umuuwe Mtoto wangu? laiti kama kitamkutaย chochote Patra basi nitakulipiza”ย
“Hata haumaanishi, utatokaje hapa hilo ni suala unalopaswaย kujiuliza kisha ndiyo uwaze utanizuia vipi…” Neema akatoaย simu yake kisha akamwonesha video ambayo ilivuruga akili yaย Matilda, video hiyo ilimwonesha Neema akiwa katika wodiย ambayo Patra alikua amelazwa, ilimdhihirishia wazi Matildaย kua Neema anaweza akafanya chochote kwa ajili ya kumdhuruย Patra.ย
Tayari Mama James na Jack walikua wamefika kituoni, wakatoaย maelezo kua wanahitaji kumwona Matilda, wakaambiwa kuaย Matilda alikua ameachiwa huru muda mchache uliopita,ย iliwashangaza sana sababu kama angelikua ameachiwa huru basiย wangemwonaย
“Afande Mimi nimekaa hapo nje kwa takribani masaa matano,ย kama angekua ameachiwa basi ningemwona lakini sikumwona hebuย angalia vizuri” Akadakia Mchungaji Georgeย
“Jarada lake hili hapa, sisi tunafanya kazi kwa maandishi,ย tayari ameachiwa huru. Hatukuona sababu ya kumshikilia kwaniย Mlalamikaji alikuja na kusema kua haitaji kuendelea na kesi”ย Alisema tena yule polisiย
“Polisi Mimi ni Mama wa mlalamikaji, nimekuja kwa ajili yaย kumwona huyo Binti tafadhali” Alisema Mama James
“Jamani nimeshawaambia kua Msichana ameachiwa, jukumu laย kujua yupo wapi ni la kwenu sababu kwetu ameshatoka”ย Akasistiza polisi huku akionekana haitaji kuendelea kubishanaย naoย
Taratibu watatu wakashusha ngazi hadi chini, Jack akapigaย simu Hospitali ambako walikua wameenda kwa ajili ya Matibabu,ย wakapata taarifa kua Matilda hakwenda huko. Taharuki ikawaย kubwa, hakuna aliyejua mahali ambapo Matilda alikua ameendaย
“Sasa atakua ameenda wapi au ameelekea kule Hospitali ambakoย Mtoto amehamishwa?” akauliza Jack, akili zao zikawaza kwaย pamoja kua huwenda Matilda akawa ameenda huko, mara moja Mamaย James na Jack wakaelekea Magomeni ilipo Hospitali ya JM.ย
Wakati wao wanatoka kituo cha polisi, gari nyingine nyeusi yaย kifahari ikaingia hapo, akashuka James, yaani kama angewahiย kidogo tu angekutana na Mama yake na Mfanyakazi wake hapoย Kituoni, James alihitaji kuzungumza na Matilda, hakujua kuaย Matilda alikua ameondolewa hapo na Neema, akaingia naย kujitambulisha, akapewa maelezo yale yale ambayo Akina Jackย walipewa, haraka akatoka hapo akajaribu kuipiga simu ya Matilda lakini haikuita, akampigiaย simu Neemaย
“Neema Nahitaji kuongea nawe sasa hivi, nieleze mahali ulipo”ย Akasema James, akaelezwa mahali ambapo Neema alikuwepo,ย akawasha gari kuelekea huko.ย
Ilikua ni nje kabisa ya Mji, kitu ambacho kilianza kumpaย Mashaka James, akasogea hadi kwenye jengo ambalo Neemaย alikuwa amemuelekeza James aende, Palikua ni msituni. Jengoย hilo lilikua katika eneo la peke yake kabisa, Jamesย aliposhuka macho yake yakawa kwenye jengo hilo lililo kimyaย sana, James akasogea kama alivyoelekezwa na Neemaย
Alipoingia alisikia sauti ya Matilda ikiita, akashtuka sanaย akaenda hadi kwenye hicho chumba akamkuta Matilda akiwaย amefungwa kambaย
“Matilda?” akaita James kisha akamkimbilia Matilda alipokuaย amekaa, Chozi lilikua likimbubujika Matilda, James akamwambiaย Matildaย
“Nataka nikutoe hapa sawa?” Akawa anafungua kamba lakiniย akasikia Watu wakija kwenye chumba hicho, James akashtuka,ย alipogeuka akamwona Neema, Masudi na wanaume wengine wawiliย
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya SITA Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx
11 Comments
Leo wa kwanza Mimi jamani but story is very very ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Mambo ni motooo
Jins nlivyonashauku natamn miendelez Sasa hv
Wow nautamani uo mwisho wa neema๐ฅ
Inavitia kuendelea kusoma hadi rahaaa,tuone ni kitakiri kwa jemsi na maltida wake
Daaaah jmn huyu Neema ana roho mbaya kiasi hiki ๐ญ๐ญ๐ญ
Yaani hi dunia jamaa anapigania mimba ambayo syo yake ..wanaume tuna tabu sana..
Adimini una baya ukifa uhozi ukiozo unuki twend Kaz sanaoma simulizi kama naangalia TV yan yan dah
Namuona James akitapeliwa, Neema kuishia pabaya
r97ubn
9xirvd