Ilipoishia “James, ni wazi bado unampenda Matilda, ni wazi kua ipo sikuย utakuja kunitelekeza na Mimba yangu kitu ambacho sipo tayariย kitokee” akasema Neema akiwa anamsogelea Jamesย
“Neema sikutegemea kama ungekua katili kiasi hiki, hukupaswaย kumtesa Matilda kiasi hiki hata kama lengo lilikua aondoke..”ย
“Ishia hapo hapo, James ulinipa ruksa ya kufanya kila jambo,ย inaonekana kua moyo wako umerudi nyuma, umerudisha mapenziย kwa Matilda si ndiyo?” akauliza Neema lakini James hakujibuย chochote huku macho yake akiwa ameyapeleka kwa Matilda ambayeย alikua njia panda sababu aligundua kua James alikua na niaย njema kwake na wala hakushiriki kumtesa kiasi kile.ย
“Vizuri James, niliyajua yote haya pale niliposikia kuaย ulienda polisi kumwona Matilda, Sasa James inabidi uchagueย kitu kimoja, ilipofikia siko tayari kupoteza chochote” Jamesย akasimama baada ya kusikia Hivyoย
“Unamaanisha nini?”ย
“Nitamwacha Matilda endapo utakubali kufunga ndoa nami”ย Akasema Neemaย
“Najua hilo lazima likupe wakati Mgumu sana sababu tukiachanaย tutalazimika kugawana Utajiri ulio nao, kama hilo ni ngumuย kwako basi Nitamuuwa Matilda” James hakua na jibu lolote laย kumpa Neema.ย
Hadi kufikia Usiku hakukua na taarifa yoyote kuhusu Matildaย ni wapi alipo, Mtu pekee aliyefanikiwa kujua alikua ni James,ย hilo lilimpa mawazo sana, alikunywa pombe huku akitafakariย yale aliyoambiwa na Neema, achague moja, kumwoa Neema auย kukubali Matilda afe, kingine kilichompa mawazo ni kwambaย Neema ni Mjamzito, kiu yake kubwa ilikua ni kupata Mtoto japoย alikua na Mtoto na Matilda lakini Mtoto huyo alimkataa sababuย alikua ni Mlemavu, Usiku huo hakutaka kuzungumza na Mtuย yeyote zaidi ya kunywa pombe akiwa nyumbani kwake. Akajikutaย akichanganikiwa kabisa, alikua na pesa nyingi lakini hakuaย mwenye furaha, sababu kubwa iliyopelekea kutokua na furaha niย maamuzi yake ya kumkataa Mtoto wake.ย
Siku iliyofuata, bado Matilda aliendelea kutafutwa bilaย mafanikio yoyote yale huku Mtoto wa Matilda akipatiwaย matibabu Muhimbili kwa hisani ya Mama yake James,ย wakahangaika kila kona kumsaka Matilda, polisi badoย wakaendelea kushikilia msimamo kua Matilda aliachiwa huru
Upande wa James aliamua kuelekea Hospitali ili amwone Patraย kabla hajafanya maamuzi yoyote yale, akaambiwa kua Mtotoย alisha hamishwa hapo siku tatu zilizopita, akapewa anuani yaย Muhimbili, haraka akaelekea huko hadi kwa Daktari ambayeย alikua na jukumu hilo la kumtibia Patraย
Akapelekwa hadi kwenye Wodi ambayo alikuwepo Patra, moyoย wangu ukaingiwa na uchungu sana, akalia ndani ya moyo wake,ย ni kweli Patra ni Mtoto wake lakini kilichomfanya amkatae niย ile aibu kua Mtoto huyo ni mlemavu, Bilionea kama Yeye awe naย Mtoto mlemavu hakutaka kabisa kukubali ndiyo maana akawekaย nguvu kwa Neema kuhakikisha anamzalia Mtoto, mambo yakaanzaย kwenda kombo huku tumaini la furaha likiingia huzuniย
“Mbona unalia, una uhusiano gani naye?” akauliza Daktari,ย maana James alijitanbulisha kama Mfadhili, chozi likiwaย linamtoka akimtazama Binti yake ambaye alikua ameshafanyiwaย upasuaji, kilichomliza zaidi James ni kuhusu Matilda ambayeย alikua akipewa mateso na Neema.ย
“Nimeguswa tu na Maisha yake, pengine anastahili kilicho boraย zaidi” Akasema James huku akiwa anafuta chozi lake, kwa maraย ya kwanza alijisikia vibaya sana kuhusu Patra.ย
“Usijali hali yake itaanza kuimarika kadili siku zitakavyokuaย zinasonga, tatizo lililokua likimsumbua tayariย tumeshaliondoa” Akasema Daktari huyo.ย
Wakati huo Mama yake James na Mama Naomi wakiwa wanakuja hapoย Hospitalini, Baada ya kushuka kwenye gari Mama Jamesย akamwambia Mama Naomiย
“Sikulala usiku wa jana, japo sijamwona huyo Binti aliyezaaย na James lakini nimejikuta nikimuwazia sana, sijuiย anafananaje” Alisema akiwa anafunga mlango wa gariย
“Mama hata Mimi sipati usingizi tokea alipokua polisi, wakatiย mwingine nachoka lakini nikifikiria kuhusu yule Mtotoย najikuta napata nguvu ya kuja hospitalini” Akasema Mama Naomiย wakiwa wanaanza kutembea kuelekea wodiniย
“Hongera hakika wewe ni miongoni mwa wanadamu wachache ambaoย wana mioyo bora sana hapa Duniani”ย
“Mama Usijali sana namchukulia Matilda kama Mdogo wangu hivyoย chochote chake ni changu pia” Maongezi yaliendelea wakiwaย wanasogea wodini wakati huo James akiwa anamwambia Daktari
“Nitasimamia matibabu kuanzia sasa, kadi yangu ya Mawasilianoย ni hii hapa, kwa chochote nijulishe” Akampatia kadi Daktariย
“Mungu akuongoze ukaguse Maisha ya wengine wenye uhitaji Mr.ย James” Akasema Daktari bila kujua kua aliyekua mbele yakeย ndiye Baba wa Mtoto, Basi James akamuaga Daktari kishaย akatoka wodini wakati huo Mama yake akiwa anafika hapo,ย wakapishana kidogo tu, James anageuza kisogo Mama naye ndiyoย anaingia akamkuta Daktari Daktari akiwa ameshikilia kadiย
“Karibu Mama, karibuni sana” Akasema Daktari huyo kishaย akaitia kadi mfukoniย
“Hali ya Mtoto inasemaje?” akauliza Mama James huku Mamaย Naomi akiwa anatabasamu kwa namna mashine zilivyokuaย zikionesha hali ya Patraย
“Hali yake Mungu anasaidia sana tena ashukuliwe zaidi naย zaidi sababu pasi na yeye hakuna Uhai wa Binadamu yeyote”ย Wote wakatabasamu kwa maneno ya Busara ya Daktariย
Mchungaji George akawatangazia waumini wa kanisa lake juu yaย Mwenendo mzima wa Matilda na Binti yake sababu baada yaย mchango ule hakusimama Madhabauni na kuzungumza, akawaambiaย hali halisi ya kinachoendelea huku akiwataka waumini kutoaย taarifa endapo watasikia au kumwona Matilda, kila mmojaย alisikitika sana, ikawa gumzo kanisani hapoย
“Ikibidi tufunge na kusali ili Mungu atuoneshe ni wapi alipoย Matilda” Akasema Mchungajiย
“Ameen” Waumini wakaitikiaย
Mchungaji George akaanza maombi pamoja na waumini wote iliย Matilda apatikane popote alipo, pia hali ya Mtoto wa Matildaย iimarike zaidi na zaidi.ย
“Mama, ilipofikia naona kama naenda kushindwa” Akasema Neemaย mbele ya Mama yake, macho ya Mama Neema yakagongana na yaย Binti yake kisha akamtazama Masudiย
“Kwanini unasema hivyo?”
“James amerudi kwa Matilda. Nimefanya kama ulivyoniagizaย lakini inaonekana wazi kua ameanza kurejea upande wa Matilda”ย Akasema Neema huku akiketi kwenye sofaย
“Kwa dawa ambazo ulikua ukimpa kwa kipindi chote sidhani kamaย anaeza akathubutu kufanya hivyo, maisha yetu yamebadilikaย Neema, hii ni ishara kua dawa zinafanya kazi. Cha Msingi niย kuvuta subra ili aamue jambo letu”ย
“lakini Mama anachosema Neema kina ukweli sababu jamaaย haeleweki sasa hivi, si kama zamani…” Akadakia Masudiย
“James hawezi kubadilika isipokua ni hofu zenu tu,ย tulishamtengeneza vya kutosha, kala limbwata za kutoshaย inawezekana vipi ndani ya muda mfupi mseme amebadilika?ย kumbukeni huu ni mpango wa kufanikisha kupata pesa kwake,ย kama ni hivyo basi Ujauzito hauna maana tena” Akasema Mamaย yake Neemaย
“Bado namshikilia kwanza Matilda ili nione msimamo wa Jamesย utakua vipi, alafu pili nataka nijue Hospitali aliyolazwaย Mtoto wa Matilda, hiyo inaweza kua karata nyingine sababuย Hospitali ya Mwanzo hayupo” akasema Neema huku akiangaliaย Ujauzito wake ambao ulianza kukuaย
“Neema nafikili ulifanya makosa pale mwanzo, ulipaswa kumuuwaย Mtoto akiwa tumboni na siyo kumfanya azaliwe kilema, hayaย yote yasingejitokeza sasa hivi, huu mvutano unatokana na yuleย Mtoto, sasa inabidi tumuuwe tu hakuna njia nyingine” Akasemaย Mama yake Neemaย
“Mama, Kwasasa nakusikiliza wewe tu. Chochote ambachoย utakiamua nitakifwata sababu naona mambo yanataka kuniendeaย kombo”ย
“Basi mpigie simu Babu yako, Mwambie amuuwe Mtoto usiku waย leo ili asubuhi kuwe na habari nyingine, kama ulivyosemaย karata pekee inayoweza kutufanya tukatimiza adhma yetu niย kumuuwa yule Mtoto kwanza” Akasema Mama Neema kisha akaketiย pia huku Masudi akifuatia kuketiย
Mpango mpya mbele yao ukawa kwanza kujua Mtoto amelazwaย Hospitali gani, kama alivyosema Mama yake, Neema akampigiaย simu Babu yake ambaye alikua Mchawi haswa na ndiyeย aliyesababisha Matilda akazaa Mtoto mlemavu. Babu yake alikuaย haishi mbali sana na Jiji la Dar, alivyopata simu ya Neema,ย haraka akaingia Dar akitokea Kiluvya – Kibaha.
Babu yake Neema aliyeitwa Mzee Mapinduzi, akajaribu kuangaliaย namna ya kufanya lakini ikawa ngumu kujua Mtoto mahali ganiย alipo, Maombi ya Mchungaji George yalionekana kuzuia jamboย hilo kufanyika, akawaambiaย
“Simwoni Mtoto, Mna hakika yupo hai?” akauliza Mzee Mapinduziย wakiwa sebleniย
“Babu, Mtoto yupo hai, Hospitali ya mwanzo alihamishwa”ย Akasema Neemaย
“Simwoni ndiyo maana nauliza, kuna kitu gani kinachozuiaย hapa?…”ย
“Basi Babu, nitafanya jitihada za kujua yupo Hospitali gani,ย kesho tutajua Hospitali ambayo Mtoto amelazwa” Akasema Neemaย
Wakati Neema na familia yake wakipanga namna gani wafanye,ย Usiku huo Mama yake James akamwita James nyumbani kwake,ย Haikumpa Mshituko James sababu alijua Mama yake hafahamuย chochote kile kinachoendelea, Mama yake James hakutakaย kumwonesha chochote kijana wake kua anajua kinachoendelea,ย akamuulizaย
“Hivi Neema anaendeleaje, Maana tokea ile siku umemleta hadiย hivi leo sijamtia machoni, nawe husemi chochote kile” Sura yaย James ikapoteza Uchangamfu kidogo baada ya kusikia swali laย Mama yake, akamjibuย
“Neema anaendelea vizuri tu Mama, ni majukumu ya hapa na paleย ndiyo maana unaona kimya, hata hivyo nilipanga kuja naye ilaย nikaona ni usiku nikamwacha apumzike”ย
“Hivi James, katika pitapita zako hauna hata Mtoto waย kusingiziwa kweli Mwanangu?” akauliza Mama yake kwa utaniย hivi huku akitabasamu, James naye akatabasamu kidogo lakiniย moyoni swali hilo lilimpa pigo takatifuย
“hapana Mama, sitaki litokee hilo, unajua ukishakua na helaย basi kila Mwanamke atataka kusema hivyo, siwapi nafasiย kabisa, Mjukuu pekee yupo kwa Neema, tarajia mazuri” Akasemaย na kujichekesha,ย
“Haya Mwanangu, Nami Mama yako natarajia mazuri kutoka kwakoย na Neema, natamani sana kuitwa Bibi..”
“Usijali Mama yangu, muda siyo mrefu utapata Mjukuu wako…”ย Wakazungumza kwa dakika kadhaa kabla ya James kuondoka.ย
Maisha ya James yalibadilika hasa kutokana na kile kilichokuaย kikiendelea, akahisi labda ni Mkosi wa kumkana Mtoto ndiyoย umepelekea kuingia katika nyakati ngumu ambayo kuingia kwakeย ilikua rahisi lakini kutoka ikawa ngumu sana, alipewa sikuย tatu na Neema ili atoe jibu kama yupo tayari kwa ndoa,ย akilini mwake alishajua Mwanamke huyo alikua na tamaa yaย kuupata Utajiri wake lakini hakua na njia ya kumkwepa sababuย aliamini ana Mtoto wake tumboni, aliendesha gari kwa spidiย sana hadi nyumbani kwa rafiki yake Chiloย
Mara nyingi alipokwama alipewa ushauri na Chilo lakini sikuย hiyo ilikua tofauti sana, Chilo alikua na Mke wake, alizionaย simu za James zikiingia lakini Mke wake akamwambiaย
“Mwache Dunia imfunze, hiyo ni laana ya kumkataa Mtoto, usikuย huu akusumbue Mume wangu Akhaaa” Alisema akiwa anamkumbatiaย Chilo ambaye aliyakubali maneno ya Mke wake, James alipigaย sana honi bila mafanikio yoyote yale kitu ambacho hakikuaย kawaida, akashuka na kugonga geti kwa nguvu lakini hakunaย aliyefungua geti, akajaribu kumwita Chilo lakini hakupokeaย jibu lolote lile, akazidi kuchanganikiwa, akarudi kwenyeย gari, akaketi kumsubiria Chilo akiamini huwenda hajarudiย Usiku huo, akajikuta amepitiwa na Usingizi Mzito sana.ย
Alipokuja kushtuka palikua tayari pamepambazuka, alishtuka,ย hakuamini Bilionea kama yeye alale ndani ya gari, Mara Mke waย Chilo akafungua geti wakati James akiendelea kujikagua,ย haraka akashuka kwenye gari huku akipiga mihayo ya Uchovuย
“Habari Shem, mbona asubuhi mapema hivi kuna tatizo?”ย aliuliza Mke wa Chilo kama vile siyo yeye aliyesababishaย James akalala kwenye gari, James alipoona Mke wa Chilo hajuiย kama yeye alilala hapo akajifanya kuzugaย
“Nilikua na Mihadi na Chilo, ndiyo nimekuja lakini kamaย hajaamka, basi kuna mambo naenda kuweka sawa kishaย nitawasiliana naye” akasema James kisha akarudi kwenye gari,ย akaondoa gari hapo huku Mke wa Chilo akitabasamu tuย
“Na bado. wanaume wa namna hii wanaishia kuishi Maisha yaย Kimasikini sababu ya laana za kujitakia” Akasema hukuย akilisindikiza kwa macho gari la Jamesย
Mahali ambapo Matilda alihifadhiwa alihamishwa na kupelekwaย sehemu nyingine sababu James alikua ameshapajua, mpango ulioย mbele ni kumuuwa Mtoto wa Matilda ili James akose nguvu.ย
Akatumwa Masudi kupeleleza ni wapi ambapo Mtoto amepelekwa,ย Akaelekea Magomeni Hospitali, akaambiwa kua Mtoto yupoย Muhimbili, haraka akampigia simu Neeema na kumpa taarifa,ย
Taarifa hiyo hiyo ikamfikia pia Mzee Mapinduzi, akamwambiaย Neemaย
“Chukua hii, katupe Muhimbili, katikati ya Hospitali,ย inaonekana kuna nguvu inayonizidi ndiyo maana simwoni Mtoto”ย Akasema Mzee Mapinduzi, akampatia Neema kitu mfano wa pipiย tena akamsistizaย
“Hakikisha mahali hapo Mtu hawezi kuokota wala kuigusa, ikaeย hapo ili nimshughulikie” Haraka Neema, akaingia kwenye gariย akawaacha Mama yake na Babu yake wakiendelea kuzungumza hukuย wakisubiria Neema akafanye tukio hilo.ย
Ndani ya Hospitali, mambo yalikua shwari kabisa sababu haliย ya Patra ilianza kukaa sawa, maombi ya Mchungaji na Matibabuย ambayo Mama James aligharamia yaliimarisha afya ya Mjukuuย wake japo alifanya kwa siri James asijuwe, Patra alikuaย akitabasamu huku akitazama walio mzunguka, alionekanaย kuhitaji kuuliza ni wapi alipo Mama yake lakini Mtoto huyoย alizaliwa akiwa hajui kuzungumza kutokana na Uchawi ambaoย familia ya Neema ilimfanyia, Mbele ya Patra alikua amesimamaย Mama James ambaye ni Bibi yake, Mama Naomi, na Mchungajiย Georgeย
“Hakika Mungu aliye hai ametenda miujiza” Alisema Mchungajiย George kwa Furaha kubwa kutokana na hali ya Patra ilivyokuaย ikiimarikaย
“Asante sana Mchungaji, maombi yako yamesaidia sana, mara yaย kwanza nilivyomwona Mtoto huyu roho yangu iliumia sana,ย Malaika asiyejua chochote alikua akiteseka sana, hadi kuaย hivi leo ni Miujiza tu” Alisema Mama Yake Jamesย
“Itakua siyo busara kama tutasahau kumshukuru Mama Naomi, niย ngumu Dunia ya sasa kupata Jirani kama Mama Naomi hasa katikaย Jiji hili ambalo kila Mtu yupo bize” Akasema Mchungajiย
“Ni kweli kabisa, Asante Mama Naomi, Mjukuu anaendeleaย vizuri. Sasa kilicho mbele yangu ni kuhakikisha tunampataย Matilda ili ashuhudie Muujiza huu” Akasema Mama yake Jamesย
Muda huo Magari mawili yalikua yakiingia Hospitalini hapo kwaย kupishana dakika tano, aliyekua wa kwanza kuingia alikua niย James, alipotoka tu kwa Chilo aliona ni bora alekee Hospitaliย kumwona Patra sababu nafsi ilikua ikimsuta sana. Akaketiย
kwenye gari iliyo Paking kwa dakika kadhaa akitafakari namnaย mambo yalivyokua yakiendelea, Gari ya pili ilikua ni gari yaย Neema, kila mmoja aliegesha gari kwa upande wake lakini Jamesย alikua na nafasi ya kumwona Neena sababu alikua amepakiย sehemu yenye magari mengi, akaliona gari la Neema likiingiaย akajiuliza Neema amefuata nini pale Hospitalini. Endeleaย
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya NANE Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx
16 Comments
Waooooo
Story nzuri sana, hongera sana, inafundisha, inasisimua na inatupa burudani
Moto unawaka lazima Mungu ajitambulishe kawaida kila mashauri ya Shetani na Mawakala wake lazzima ya simame
Nikizeeka nitawasimulia wajukuu iih story nitawaambia ilimkuta mjamaa mmoja anaitwa adimini aaahaa
Next please ๐ yaan Ni๐ฅ
Ujawahi kukosea admini
Jaman si utoe asubihi na jion Admin maana hii ki2 ni ๐ฅ๐ฅ
Alaniwe nakila mwenye mipango yakudhuru kwa mwenzake
Inazidi kunoga
daaah! Neema anakwenda kuumbuka
Mambo ni moto inazid kuwa fire
NOMAAA๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
ahsante admin nasubir sehem ya nane
Glory to God
e1pfqz
m3omfe