Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Pigo Takatifu Sehemu Ya Pili (02)
    Hadithi

    Pigo Takatifu Sehemu Ya Pili (02)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaSeptember 13, 2024Updated:September 18, 202411 Comments9 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Pigo Takatifu
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia ย “James una hakika kuwa hii ni Mimba yako?” Lilikua ni swaliย  aliloulizwa James, walikuwa chemba na Mama yake wakimuachaย  Neema akiwa sebleniย 

    “Ndiyo Mama kwanini unauliza hivyo?” Alihoji James akiwaย  anamtazama Mama yake, alikua ameenda kumtambulisha Neema kwaย  Mama yake huko Kiwalaniย 

    “Nimekuuliza tu sababu imekuwa ghafla sana James”ย  Endeleaย 

    SEHEMU YA PILI

    “Ha!ha!ha! Mama hilo lisikupe presha kabisa nilipangaย  kukufanyia sapraizi Mama yangu sababu najua ulikua na hamu yaย  Mjukuu. Baada ya kutafuta pesa nyingi niliona furaha pekeeย  kwako ni Mjukuu Mama” Alisema James akiwa anatabasamu, Mamaย  yake akachungulia sebleni akamtazama Neema kisha machoย  akayarudisha kwa Jamesย 

    “Sawa Mwanangu, sijui kwanini Moyo wangu unaniambia tofauti,ย  ila Usijali Baba” Alisema Mama yake Jamesย 

    “Basi Mama uchangamke ili Mgeni asijisikie vibaya sawa?” “Sawa Baba”ย 

    Baada ya Maongezi walirejea Sebleni, Neema hakujua chochoteย  kile, aliona mambo yakiwa kawaida, Mama yake James akaongezaย  uchangamfu kwa Neemaย 

    “Karibu Mkwe wangu, nimesikia taarifa kuwa una kichanga chaย  Mwanangu” Alisema Mama yake James akiwa anatabasamu, hataย  James alitabasamuย 

    “Ndiyo Mama, nategemea kupata Mtoto kwa Majaliwa yake Mungu”ย  Alisema Neema akiwa anatabasamu pia, furaha ikawa kubwa sana.ย  Baada ya muda waliopanga kuwa hapo kuisha iliwalazimu warudiย  wanapoishi kwenye jumba la Kifahari la James.ย 

    Kutokana na furaha aliyokua nayo James alimuahidi vingi Neemaย  kama atamzalia Mtoto mzuri wa kiume, alimuhesabia vituย  ambavyo angempa ni pamoja na kampuni yake ya kuuza Magari,ย  Jengo la Ghorofa lililopo Kurasini na Gari jipa aina ya BMWย  X6. James Kyando alikua na pesa nyingi lakini hakubahatikaย  kupata Mtoto katika Maisha yake hivyo alihitaji Mtoto aje kuaย  Mrithi wa mali zake.ย 

    Neema aliishi Maisha ya kifahari sana, akaahidiwa ndoa endapoย  Mtoto atazaliwa, James akahakikisha anamuajiri daktari Maalumย  kwa ajili ya kuchunguza afya ya Mtoto na Neema mwenyewe, kilaย  alichotaka Neema alikua akikipata sababu furaha ya Jamesย ย 

    ilikua ni Mtoto tu.ย 

    “Baby Naamini utaniheshimisha sana, nitapata heshima kubwaย  kuliko hivi sasa. Mtoto akizaliwa wa Kiume nitamwita Lameck”ย  alisema James akiwa amelishika tumbo la Neemaย 

    “Kama atazaliwa wa kike?”

    “Akizaliwa Malikia wa kike nitamwita Princes Ana” Alisemaย  Jamesย 

    “Waoooh Jina zuri sana James wangu” Alisema Neema. Pale paleย  simu ya James iliita ikakatisha maongezi yao, aliangaliaย  aliyekua akipiga akaona ni Matildaย 

    “Eeeh huyu Mwanamke Usiku huu anataka nini tena?” aliulizaย  James Kyando, haraka Neema akaipora simu ya Jamesย 

    “Unamuendekeza baby, si umfukuze pale jamani? ningekua Niย  Mimi yaani wala nisingemuendekeza kiasi hiki hadi anisumbueย  Usiku kama huu” Alisema Neema, James akaipokea simu hiyoย 

    “Unasemaje Matilda huoni kama ni Usiku mwingi sasa hivi?”ย  alihoji James, hakujua kua Matilda alikua katika nyakatiย  ngumu sana ya kumpambania Mtoto Hospitalini, sauti ya kilioย  ikasikika, Matilda akaongea akiwa analiaย 

    “James Mtoto yupo Hospitali anatakiwa kufanyiwa upasuajiย  kusafisha Mapafu..” Alisema Matilda huku kwikwi ikiwaย  imemshikaย 

    “Kwahiyo unaniambia hivyo kwani Mimi ni daktari, ina maanaย  kupiga simu usiku wote huu ni kwa ajili ya ndondocha wako?”ย  alisema Jamesย 

    “James usiwe mkatili namna hiyo, Patra ni damu yako,ย  usimuache akaangamia kisa Mlemavu” Alisema Matilda akizidiย  kuliaย 

    “lengo la kunipigia ni nini?”ย 

    “Upasuaji unahitaji Milioni 8 nami sina hiyo pesa James”ย  Alisema Matildaย 

    “Tuwasiliane asubuhi” Alisema James kisha alikata simu yaย  Matilda, akamtazama Neema ambaye alikua amenunaย 

    “Baby ina maana umekasirika?” aliuliza Neemaย 

    “Unaongea na Mwanamke mbele yangu alafu unataka nifurahie siย  ndiyo? Hivi james kwanini unataka kunipa presha isiyo naย  msingi wakati unajua fika kuwa Mimi ni Mjamzito?” aliulizaย  Neema.ย 

    “Nalijua hilo ndiyo maana nimemwambia anipigie asubuhiย  nimsikilize anataka kusema nini?”

    “Unaniona mimi Mtoto si ndiyo James, si nimesikia hapo kuaย  Mtoto amelazwa Hospitali, hivi James yule Mtoto ni wako au siย  wako?”ย 

    “Nawezaje kuwa na Mtoto mlemavu na pesa zote hizi Neema? Siย  Mtoto wangu yule isipokua huruma yangu kwake ni kwasababuย  alikubali kutoroka kwao Njombe na kuja Dar kwa ajili yangu,ย  kuna wakati naingiwa na Moyo wa huruma sana”ย 

    “Nitaamini vipi kama si Mtoto wako? Unajua sitaki Mtoto wanguย  atakapozaliwa akute marumbano, sitaki aanze kusikia kunaย  mtoto mwingine tena mlamavu”ย 

    “Unataka nifanye nini Neema?”ย 

    “Mfukuze pale, mpe pesa arudi kwao. Napata kichefu chefu kilaย  saa anakupigia na kukulilia, ona sasa hivi tulikuaย  tunazungumza mambo ya Maana matokeo yake anapiga simu naย  kuanza kujiliza kisa Mtoto ambaye si wako” Alisema Neema,ย  James hakujibu chochote kile.ย 

    *****ย 

    “Mtoto akiendeela kuwa katika hali ya usaidizi wa Mashine niย  gharama pia Neema” Alisema Daktari ambaye alikua akimhudumiaย  Patra Hospitaliniย 

    “Dokta hali yangu unaijua, nahangaika huku na kule ili kuokoaย  uhai wa Binti yangu, tusubirie hadi kesho asubuhi pengineย  naweza kupata tumaini lolote juu ya hali ya Binti yangu”ย  Alisema Matilda, ulikua ni usiku akiwa ameketi nje ya chumbaย  cha uangalizi maalum ambacho Binti yake alikua amelazwaย 

    “Kwani Baba yake anasemaje?” Aliuliza Daktari, Tayari Matildaย  alikua ameshadondosha chozi, akalifutaย 

    “Baba yake amemkataa sababu ni mlemavu Dokta, roho inaniumaย  sana, katika vitu ambavyo namuomba Mungu katika hii Duniaย  basi ni kuhusu Binti yangu kupona sababu najua huu mzigo niย  wangu peke yangu” Alisema Matilda akiwa analia, Dokta akaketiย  ili amsikilize vizuriย 

    “Usilie Matilda, hebu nieleze ilikuwaje?” Aliuliza Dokta,ย  Matilda alianza kumsimulia Dokta namna ilivyokua japo alikuaย  analia lakini alimudu kueleza

    Wakati Matilda akiwa shule huko Kijijini Njombe alikutana naย  James kwenye Mashamba ya Maparachichi, James alikua akilimaย  Maparachichi huko, walipokutana kwa mara ya kwanza Matildaย  alipokua akiomba kazi ya kuvuna Maparachichi, James alivutiwaย  sana na Matildaย 

    Alimpatia kazi katika Shamba hilo kubwa la kisasa ili aweย  kibarua ili tu apate kua karibu naye, akamueleza jinsiย  alivyovutiwa naye siku moja wakiwa shambaniย 

    “Mmh!! Mimi masikini hivi nije kuwa na wewe, haitowezekanaย  tafuta Msichana mnayelingana kifedha” Alisema Matildaย 

    “Mapenzi ni upofu Matilda, moyo hauna macho wala hauoni,ย  popote hutua kama ndege kwenye Bustani nzuri ya Maua” Alisemaย  James, maneno ya James yalimuingia Matilda akawa anatabsamuย  tuย 

    “Ukikubali kua na Mimi na ukanizalia Mtoto nitakupa nusu yaย  Mali zangu Matilda, utajiri huu utakua wako na nitakuowa,ย  pamoja na hela zote nilizo nazo Mimi sina Mtoto hata waย  kusingiziwa” Alisema jamesย 

    Matilda aliomba muda wa kutafakari jambo hilo, hakutakaย  kukurupuka sababu bado alikua mwanafunzi wa chuo cha ufundiย  veta, Baada ya siku tatu alimpa jibu Jamesย 

    “Najua kwanini inakua ngumu kwako, sababu unaogopa wazaziย  wako lakini nataka kukwambia kitu Matilda, endapo utakubaliย  basi utaokoa Maisha ya familia yako itaondokana na Umasikiniย  kabisa” Alisema James wakiwa ndani ya gari ya Jamesย 

    “Nataka uje kuishi na Mimi Dar, nitakutunza kama Malkiaย  Matilda” Maneno ya James yalimshawishi sana Matilda, Jamesย  aliporudi Dar baada ya kumaliza mavuno, aliwasiliana naย  Matilda kupitia simu ambayo alimnunulia,,Matilda akatorokaย  kwao Njombe akaenda kuishi Dar na James.ย 

    Wakati Matilda anamsimulia Dokta, mara ikaja taarifa kuwaย  hali ya Patra imebadilika, Dokta akakimbilia chumba chaย  Uangalizi kwa ajili ya kuangalia hali ya Patra.ย 

    Matilda alikesha akimuomba Mungu asimchukue Binti yake kwaniย  bado anampenda sana, asubuhi ilimkuta akiwa macho. Mama Naomiย  alikuja Hospitalini asubuhi hiyo kwa ajili ya Kumjulia haliย  Patraย 

    “Hali ya Patra ilibadilika Usiku, hata hivyo hadi sasa hakunaย  taarifa yoyote ile Mama Naomi” Alisema Matilda

    “Mungu atampigania Binti yako, Usijali sana Matilda, wewe niย  Jasiri sana” Alisema Mama Naomi, akampatia Matilda chupa yaย  chai na Chapati ili apate kifungua kinywa maana tokea janaย  hakula chochote zaidi ya kulia. Mara simu ya Matilda iliita,ย  aliyekua akipiga alikua ni James, akafuta chozi kishaย  akapokea haraka sana.ย 

    “JM hospital, Magomeni Mapipa” Alisema Matilda kisha simuย  ilikatwaย 

    “Nani huyo?”ย 

    “James”ย 

    “Anakuja?”ย 

    “Ndiyo Mama Naomi”ย 

    “Asante Mungu pengine huu mzigo atakutua Matilda, nilikwambiaย  Mungu yupo macho anaona” Matilda aliitikia kwa kutumia kichwaย  huku akivuta pumzi kubwa, chozi lilikua likimbubujika mudaย  wote hata alipokua akilifuta halikuacha kudondoka, Mama Naomiย  aliona ni jinsi gani Matilda alikua katika wakati mgumu sanaย 

    Mama Naomi aliketi kando kisha akamnyonyesha Naomi maanaย  alikua bado Mdogo, kilichokua kinamsukuma zaidi Mama Naomiย  kumsaidia Matilda ni kwasababu hata yeye amepitia Maisha hayoย  bada ya kujifungua, Baba Naomi alimtelekeza na kwenda kuishiย  na Mwanamke mwingine, alimuacha akiwa hajui atakula nini walaย  ataishi vipi, alishawahi mwambia Matilda kua atasimama nayeย  bega kwa bega hadi pale Mambo yatakapokua sawa.ย 

    ********ย 

    “Umemwambia Maimuna?” Aliuliza Baba yake Matildaย 

    “Ndiyo huwenda ameenda Njombe Mjini kama atafanikiwa kumwonaย  basi amueleze kua sisi tunamtafuta sana, arejee tu walaย  hatuwezi kua na hasira naye” Ilikua ni kauli ya Mama yakeย  Matildaย 

    Familia ilikua katika nyakati nzito zilizojaa maumivu ndaniย  yao, walikua masikini waliotegemea vibarua katika Mashamba yaย  Parachichi. Matilda alikua ni Mtoto pekee kwao.ย 

    Yalipita masaa matatu, James aliwasili JM Hospital akiwa naย  gari yake ya kifahari, jinsi alivyo ilitosha kukwambia kuaย 

    alikuwa na kila kitu katika Maisha yake, aliposhukaย  hakuhitaji kuhangaika akavuta simu akampigia Matilda, Maraย  moja Matilda alifika alipo James,ย 

    Chozi lilikua likimbubujika, James alifanana sana na Patraย  kila alipomuangalia alizidi kuumia ndani ya nafsi yake,ย  alisimama mbele ya James aliyekua akitabasamu, ilionekanaย  wazi kua alikua akimdhihaki Matilda, akavua Miwani kishaย  akamuuliza Matildaย 

    “Utaendelea kuishi kwenye kivuli cha Patra hadi lini?” “Unasemaje James?”ย 

    “Umenisikia, sikia nikwambie Matilda, ni bora urudi kwenuย  sababu muda utafika na hautokua na sehemu ya kuishi, nitakupaย  pesa umtibie Mtoto wako na pia uondoke hapa Mjini” Alisemaย  Jamesย 

    “James!! tumepima DNA na majibu unayajua kua Patra ni Mtotoย  wako, kwanini damu yako unaiacha iteseke kisa ulemavu?”ย  alisema Matilda, alipigwa kofi hadi waliokua karibuย  walishtukaย 

    “Wewe Mshenzi sitaki urudie hiyo kauli, nakwambia nitakufanyaย  kitu kibaya endapo utaendelea kusema kua yule kiwete ni Mtotoย  wangu, Mtoto halali kwangu atazaliwa kwa Neema na siyoย  vinginevyo, kwanini unapenda kuniharibia siku Mjinga wewe?”ย  alifoka James, japo alikua kijana mtanashati lakini alikua naย  hasira sana.ย 

    Matilda alikasirika, sababu alipigwa mbele za Watu, Mamaย  Naomi alikua akiona pia japo alikua kwa mbali kidogo lakiniย  ilikua ni aibu kubwa, alikimbilia Hospitalini. James nayeย  aliondoka huku akiacha minong’ono kwa kilichotokea hapo,ย  aliondoa gari haraka sana.ย 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TATU Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMย ย 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

    Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx

    Pigo Takatifu Pigo Takatifu Kijiweni Riwaya ya Pigo Takatifu

    11 Comments

    1. Amayner on September 13, 2024 12:52 pm

      Next please

      Reply
    2. G shirima on September 13, 2024 3:55 pm

      Well done

      Reply
      • Richmao on September 13, 2024 6:27 pm

        Ni story inayofundisha na kuelimisha jamii ya sasa ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

        Reply
        • GIDMAS on September 14, 2024 2:51 pm

          Hongera kwa utunzi mzuri wa stori kunakitu Cha kujifunza

          Reply
    3. Mike on September 13, 2024 5:56 pm

      Tupe nyingine mkuu
      U

      Reply
    4. Director SanJO ๐ŸŽฌ on September 13, 2024 6:05 pm

      James anakiti chake sehem๐Ÿ™„๐Ÿ™„

      Reply
    5. Leokadia Haule on September 13, 2024 9:20 pm

      fupi Sana alafu inachelewa Sana,, but tamu sana

      Reply
    6. Amosi sanga on September 14, 2024 9:01 am

      Ni elimu tosha katika kizazi hiki

      Reply
    7. Siwema malekwa on September 17, 2024 9:17 am

      Jamani inauma pole dada

      Reply
    8. [email protected] on September 18, 2024 3:48 pm

      Nzuri sana

      Reply
    9. ๐Ÿ“ Message; SENDING 1.502407 BTC. GET =>> https://yandex.com/poll/7HqNsFACc4dya6qN3zJ4f5?hs=b599ffa8fa41d85d67d3aae4f5317756& ๐Ÿ“ on June 3, 2025 11:03 am

      oremy4

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Hadithi February 23, 2026

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Ilipoishiaย  Kwanza nilijiuliza ni Nani anayeweza kuja kwetu, kama Mama Amida tayariย  tulishazungumza. Nilimeza funda…

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (07)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.