Ilipoishia Β “James una hakika kuwa hii ni Mimba yako?” Lilikua ni swaliΒ aliloulizwa James, walikuwa chemba na Mama yake wakimuachaΒ Neema akiwa sebleniΒ
“Ndiyo Mama kwanini unauliza hivyo?” Alihoji James akiwaΒ anamtazama Mama yake, alikua ameenda kumtambulisha Neema kwaΒ Mama yake huko KiwalaniΒ
“Nimekuuliza tu sababu imekuwa ghafla sana James”Β EndeleaΒ
SEHEMU YA PILI
“Ha!ha!ha! Mama hilo lisikupe presha kabisa nilipangaΒ kukufanyia sapraizi Mama yangu sababu najua ulikua na hamu yaΒ Mjukuu. Baada ya kutafuta pesa nyingi niliona furaha pekeeΒ kwako ni Mjukuu Mama” Alisema James akiwa anatabasamu, MamaΒ yake akachungulia sebleni akamtazama Neema kisha machoΒ akayarudisha kwa JamesΒ
“Sawa Mwanangu, sijui kwanini Moyo wangu unaniambia tofauti,Β ila Usijali Baba” Alisema Mama yake JamesΒ
“Basi Mama uchangamke ili Mgeni asijisikie vibaya sawa?” “Sawa Baba”Β
Baada ya Maongezi walirejea Sebleni, Neema hakujua chochoteΒ kile, aliona mambo yakiwa kawaida, Mama yake James akaongezaΒ uchangamfu kwa NeemaΒ
“Karibu Mkwe wangu, nimesikia taarifa kuwa una kichanga chaΒ Mwanangu” Alisema Mama yake James akiwa anatabasamu, hataΒ James alitabasamuΒ
“Ndiyo Mama, nategemea kupata Mtoto kwa Majaliwa yake Mungu”Β Alisema Neema akiwa anatabasamu pia, furaha ikawa kubwa sana.Β Baada ya muda waliopanga kuwa hapo kuisha iliwalazimu warudiΒ wanapoishi kwenye jumba la Kifahari la James.Β
Kutokana na furaha aliyokua nayo James alimuahidi vingi NeemaΒ kama atamzalia Mtoto mzuri wa kiume, alimuhesabia vituΒ ambavyo angempa ni pamoja na kampuni yake ya kuuza Magari,Β Jengo la Ghorofa lililopo Kurasini na Gari jipa aina ya BMWΒ X6. James Kyando alikua na pesa nyingi lakini hakubahatikaΒ kupata Mtoto katika Maisha yake hivyo alihitaji Mtoto aje kuaΒ Mrithi wa mali zake.Β
Neema aliishi Maisha ya kifahari sana, akaahidiwa ndoa endapoΒ Mtoto atazaliwa, James akahakikisha anamuajiri daktari MaalumΒ kwa ajili ya kuchunguza afya ya Mtoto na Neema mwenyewe, kilaΒ alichotaka Neema alikua akikipata sababu furaha ya JamesΒ Β
ilikua ni Mtoto tu.Β
“Baby Naamini utaniheshimisha sana, nitapata heshima kubwaΒ kuliko hivi sasa. Mtoto akizaliwa wa Kiume nitamwita Lameck”Β alisema James akiwa amelishika tumbo la NeemaΒ
“Kama atazaliwa wa kike?”
“Akizaliwa Malikia wa kike nitamwita Princes Ana” AlisemaΒ JamesΒ
“Waoooh Jina zuri sana James wangu” Alisema Neema. Pale paleΒ simu ya James iliita ikakatisha maongezi yao, aliangaliaΒ aliyekua akipiga akaona ni MatildaΒ
“Eeeh huyu Mwanamke Usiku huu anataka nini tena?” aliulizaΒ James Kyando, haraka Neema akaipora simu ya JamesΒ
“Unamuendekeza baby, si umfukuze pale jamani? ningekua NiΒ Mimi yaani wala nisingemuendekeza kiasi hiki hadi anisumbueΒ Usiku kama huu” Alisema Neema, James akaipokea simu hiyoΒ
“Unasemaje Matilda huoni kama ni Usiku mwingi sasa hivi?”Β alihoji James, hakujua kua Matilda alikua katika nyakatiΒ ngumu sana ya kumpambania Mtoto Hospitalini, sauti ya kilioΒ ikasikika, Matilda akaongea akiwa analiaΒ
“James Mtoto yupo Hospitali anatakiwa kufanyiwa upasuajiΒ kusafisha Mapafu..” Alisema Matilda huku kwikwi ikiwaΒ imemshikaΒ
“Kwahiyo unaniambia hivyo kwani Mimi ni daktari, ina maanaΒ kupiga simu usiku wote huu ni kwa ajili ya ndondocha wako?”Β alisema JamesΒ
“James usiwe mkatili namna hiyo, Patra ni damu yako,Β usimuache akaangamia kisa Mlemavu” Alisema Matilda akizidiΒ kuliaΒ
“lengo la kunipigia ni nini?”Β
“Upasuaji unahitaji Milioni 8 nami sina hiyo pesa James”Β Alisema MatildaΒ
“Tuwasiliane asubuhi” Alisema James kisha alikata simu yaΒ Matilda, akamtazama Neema ambaye alikua amenunaΒ
“Baby ina maana umekasirika?” aliuliza NeemaΒ
“Unaongea na Mwanamke mbele yangu alafu unataka nifurahie siΒ ndiyo? Hivi james kwanini unataka kunipa presha isiyo naΒ msingi wakati unajua fika kuwa Mimi ni Mjamzito?” aliulizaΒ Neema.Β
“Nalijua hilo ndiyo maana nimemwambia anipigie asubuhiΒ nimsikilize anataka kusema nini?”
“Unaniona mimi Mtoto si ndiyo James, si nimesikia hapo kuaΒ Mtoto amelazwa Hospitali, hivi James yule Mtoto ni wako au siΒ wako?”Β
“Nawezaje kuwa na Mtoto mlemavu na pesa zote hizi Neema? SiΒ Mtoto wangu yule isipokua huruma yangu kwake ni kwasababuΒ alikubali kutoroka kwao Njombe na kuja Dar kwa ajili yangu,Β kuna wakati naingiwa na Moyo wa huruma sana”Β
“Nitaamini vipi kama si Mtoto wako? Unajua sitaki Mtoto wanguΒ atakapozaliwa akute marumbano, sitaki aanze kusikia kunaΒ mtoto mwingine tena mlamavu”Β
“Unataka nifanye nini Neema?”Β
“Mfukuze pale, mpe pesa arudi kwao. Napata kichefu chefu kilaΒ saa anakupigia na kukulilia, ona sasa hivi tulikuaΒ tunazungumza mambo ya Maana matokeo yake anapiga simu naΒ kuanza kujiliza kisa Mtoto ambaye si wako” Alisema Neema,Β James hakujibu chochote kile.Β
*****Β
“Mtoto akiendeela kuwa katika hali ya usaidizi wa Mashine niΒ gharama pia Neema” Alisema Daktari ambaye alikua akimhudumiaΒ Patra HospitaliniΒ
“Dokta hali yangu unaijua, nahangaika huku na kule ili kuokoaΒ uhai wa Binti yangu, tusubirie hadi kesho asubuhi pengineΒ naweza kupata tumaini lolote juu ya hali ya Binti yangu”Β Alisema Matilda, ulikua ni usiku akiwa ameketi nje ya chumbaΒ cha uangalizi maalum ambacho Binti yake alikua amelazwaΒ
“Kwani Baba yake anasemaje?” Aliuliza Daktari, Tayari MatildaΒ alikua ameshadondosha chozi, akalifutaΒ
“Baba yake amemkataa sababu ni mlemavu Dokta, roho inaniumaΒ sana, katika vitu ambavyo namuomba Mungu katika hii DuniaΒ basi ni kuhusu Binti yangu kupona sababu najua huu mzigo niΒ wangu peke yangu” Alisema Matilda akiwa analia, Dokta akaketiΒ ili amsikilize vizuriΒ
“Usilie Matilda, hebu nieleze ilikuwaje?” Aliuliza Dokta,Β Matilda alianza kumsimulia Dokta namna ilivyokua japo alikuaΒ analia lakini alimudu kueleza
Wakati Matilda akiwa shule huko Kijijini Njombe alikutana naΒ James kwenye Mashamba ya Maparachichi, James alikua akilimaΒ Maparachichi huko, walipokutana kwa mara ya kwanza MatildaΒ alipokua akiomba kazi ya kuvuna Maparachichi, James alivutiwaΒ sana na MatildaΒ
Alimpatia kazi katika Shamba hilo kubwa la kisasa ili aweΒ kibarua ili tu apate kua karibu naye, akamueleza jinsiΒ alivyovutiwa naye siku moja wakiwa shambaniΒ
“Mmh!! Mimi masikini hivi nije kuwa na wewe, haitowezekanaΒ tafuta Msichana mnayelingana kifedha” Alisema MatildaΒ
“Mapenzi ni upofu Matilda, moyo hauna macho wala hauoni,Β popote hutua kama ndege kwenye Bustani nzuri ya Maua” AlisemaΒ James, maneno ya James yalimuingia Matilda akawa anatabsamuΒ tuΒ
“Ukikubali kua na Mimi na ukanizalia Mtoto nitakupa nusu yaΒ Mali zangu Matilda, utajiri huu utakua wako na nitakuowa,Β pamoja na hela zote nilizo nazo Mimi sina Mtoto hata waΒ kusingiziwa” Alisema jamesΒ
Matilda aliomba muda wa kutafakari jambo hilo, hakutakaΒ kukurupuka sababu bado alikua mwanafunzi wa chuo cha ufundiΒ veta, Baada ya siku tatu alimpa jibu JamesΒ
“Najua kwanini inakua ngumu kwako, sababu unaogopa wazaziΒ wako lakini nataka kukwambia kitu Matilda, endapo utakubaliΒ basi utaokoa Maisha ya familia yako itaondokana na UmasikiniΒ kabisa” Alisema James wakiwa ndani ya gari ya JamesΒ
“Nataka uje kuishi na Mimi Dar, nitakutunza kama MalkiaΒ Matilda” Maneno ya James yalimshawishi sana Matilda, JamesΒ aliporudi Dar baada ya kumaliza mavuno, aliwasiliana naΒ Matilda kupitia simu ambayo alimnunulia,,Matilda akatorokaΒ kwao Njombe akaenda kuishi Dar na James.Β
Wakati Matilda anamsimulia Dokta, mara ikaja taarifa kuwaΒ hali ya Patra imebadilika, Dokta akakimbilia chumba chaΒ Uangalizi kwa ajili ya kuangalia hali ya Patra.Β
Matilda alikesha akimuomba Mungu asimchukue Binti yake kwaniΒ bado anampenda sana, asubuhi ilimkuta akiwa macho. Mama NaomiΒ alikuja Hospitalini asubuhi hiyo kwa ajili ya Kumjulia haliΒ PatraΒ
“Hali ya Patra ilibadilika Usiku, hata hivyo hadi sasa hakunaΒ taarifa yoyote ile Mama Naomi” Alisema Matilda
“Mungu atampigania Binti yako, Usijali sana Matilda, wewe niΒ Jasiri sana” Alisema Mama Naomi, akampatia Matilda chupa yaΒ chai na Chapati ili apate kifungua kinywa maana tokea janaΒ hakula chochote zaidi ya kulia. Mara simu ya Matilda iliita,Β aliyekua akipiga alikua ni James, akafuta chozi kishaΒ akapokea haraka sana.Β
“JM hospital, Magomeni Mapipa” Alisema Matilda kisha simuΒ ilikatwaΒ
“Nani huyo?”Β
“James”Β
“Anakuja?”Β
“Ndiyo Mama Naomi”Β
“Asante Mungu pengine huu mzigo atakutua Matilda, nilikwambiaΒ Mungu yupo macho anaona” Matilda aliitikia kwa kutumia kichwaΒ huku akivuta pumzi kubwa, chozi lilikua likimbubujika mudaΒ wote hata alipokua akilifuta halikuacha kudondoka, Mama NaomiΒ aliona ni jinsi gani Matilda alikua katika wakati mgumu sanaΒ
Mama Naomi aliketi kando kisha akamnyonyesha Naomi maanaΒ alikua bado Mdogo, kilichokua kinamsukuma zaidi Mama NaomiΒ kumsaidia Matilda ni kwasababu hata yeye amepitia Maisha hayoΒ bada ya kujifungua, Baba Naomi alimtelekeza na kwenda kuishiΒ na Mwanamke mwingine, alimuacha akiwa hajui atakula nini walaΒ ataishi vipi, alishawahi mwambia Matilda kua atasimama nayeΒ bega kwa bega hadi pale Mambo yatakapokua sawa.Β
********Β
“Umemwambia Maimuna?” Aliuliza Baba yake MatildaΒ
“Ndiyo huwenda ameenda Njombe Mjini kama atafanikiwa kumwonaΒ basi amueleze kua sisi tunamtafuta sana, arejee tu walaΒ hatuwezi kua na hasira naye” Ilikua ni kauli ya Mama yakeΒ MatildaΒ
Familia ilikua katika nyakati nzito zilizojaa maumivu ndaniΒ yao, walikua masikini waliotegemea vibarua katika Mashamba yaΒ Parachichi. Matilda alikua ni Mtoto pekee kwao.Β
Yalipita masaa matatu, James aliwasili JM Hospital akiwa naΒ gari yake ya kifahari, jinsi alivyo ilitosha kukwambia kuaΒ
alikuwa na kila kitu katika Maisha yake, aliposhukaΒ hakuhitaji kuhangaika akavuta simu akampigia Matilda, MaraΒ moja Matilda alifika alipo James,Β
Chozi lilikua likimbubujika, James alifanana sana na PatraΒ kila alipomuangalia alizidi kuumia ndani ya nafsi yake,Β alisimama mbele ya James aliyekua akitabasamu, ilionekanaΒ wazi kua alikua akimdhihaki Matilda, akavua Miwani kishaΒ akamuuliza MatildaΒ
“Utaendelea kuishi kwenye kivuli cha Patra hadi lini?” “Unasemaje James?”Β
“Umenisikia, sikia nikwambie Matilda, ni bora urudi kwenuΒ sababu muda utafika na hautokua na sehemu ya kuishi, nitakupaΒ pesa umtibie Mtoto wako na pia uondoke hapa Mjini” AlisemaΒ JamesΒ
“James!! tumepima DNA na majibu unayajua kua Patra ni MtotoΒ wako, kwanini damu yako unaiacha iteseke kisa ulemavu?”Β alisema Matilda, alipigwa kofi hadi waliokua karibuΒ walishtukaΒ
“Wewe Mshenzi sitaki urudie hiyo kauli, nakwambia nitakufanyaΒ kitu kibaya endapo utaendelea kusema kua yule kiwete ni MtotoΒ wangu, Mtoto halali kwangu atazaliwa kwa Neema na siyoΒ vinginevyo, kwanini unapenda kuniharibia siku Mjinga wewe?”Β alifoka James, japo alikua kijana mtanashati lakini alikua naΒ hasira sana.Β
Matilda alikasirika, sababu alipigwa mbele za Watu, MamaΒ Naomi alikua akiona pia japo alikua kwa mbali kidogo lakiniΒ ilikua ni aibu kubwa, alikimbilia Hospitalini. James nayeΒ aliondoka huku akiacha minong’ono kwa kilichotokea hapo,Β aliondoa gari haraka sana.Β
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TATU Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx
11 Comments
Next please
Well done
Ni story inayofundisha na kuelimisha jamii ya sasa π₯π₯π₯π₯
Hongera kwa utunzi mzuri wa stori kunakitu Cha kujifunza
Tupe nyingine mkuu
U
James anakiti chake sehemππ
fupi Sana alafu inachelewa Sana,, but tamu sana
Ni elimu tosha katika kizazi hiki
Jamani inauma pole dada
Nzuri sana
oremy4