Ilipoishia “Asante Yesu” Mikono yake ikiwa juu, Mchungaji akaja naย kumwinuaย
“Matilda, kanisa linakuhitaji useme neno” Mchungaji Georgeย alimsogeza Matilda hadi Madhabauni, akampa kipaza sauti.ย Aseme nini? ndicho ambacho Matilda alikua akiwaza, umatiย ulikua mwingi hapo kanisani, macho yote yakawa kwa Matildaย Msichana wa miaka 28ย
Alikua akitetemeka kwa kila alichofikiria kukisema, alikuaย kama amepigwa shoti vile, alimtazama Mama Naomi ambaye alimpaย ishara ya kumtia moyo kua aseme chochote hapo kanisani. Endelea
SEHEMU YA NNE
“Asanteni kwa wote, asanteni sana. Nilikata tamaa kabisaย lakini roho mtakatifu ameniinua kupitia nyie” Alisemaย Matilda, Chozi lilimbubujika kilio kikamzidi maarifa akawekaย kipaza sauti huku akimpa ishara Mchungaji kua haweziย kuzungumza kabisa.
Kanisa kikazizima, hadithi ya Maisha ya Matilda ikawalizaย wengi, bahati nzuri muda huo wataalam wa kuhesabu pesaย walikuwa tayari wamemaliza, Mchungaji akawatangazia kuaย wamepata Milioni tano, Matilda hakuamini masikio yakeย
“Sikutegemea kabisa kama kwa taarifa hii iliyo ghaflaย tungeweza kukusanya kiasi kikubwa namna hii, pesa hii itaendaย moja kwa moja Hospitali muda huu ili Mtoto aanze matibabu”ย Alisema Mchungaji, Akawaambia waumini waendelee na ratibaย zingine, yeye, Mama Naomi na Matilda wakaingia kwenye gari yaย kanisa, safari ya kuelekea Hospitali ikaanza.ย
“Mama Matilda, napata hisia mbaya juu ya Mtoto wetu” Alisemaย Baba Matilda akiwa ameketi kwenye Mkeka, Mama Matilda alikuaย akimalizia kuweka kuni jikoni, kauli ya Mume wake ikamfanyaย aache alichokua anakifanya, akapiga hatua za taratibu hukuย sura yake ikijawa na Mshangao akamsogelea Mume wake,ย akajishika kiunoย
“Kwanini unasema hivyo Baba Matilda?”ย
“Jana usiku nimeota ndoto mbaya sana kuhusu Matilda, sinaย hakika kama Atakua hai na kama yupo hai basi anaishi kwaย Mateso ya Golgota” Akasema Baba Matilda huku akikunja vizuriย goti lake wakati huo Mama Matilda akivuta kigoda na kuketiย huku macho yake yakiwa bize kwenye sura ya Mume wakeย
“Mungu amuepushe Binti yetu na majaribu yoyote yale, hujuiย jinsi roho yangu inavyouma Baba Matilda” Akasema Mama Matildaย huku akifuta chozi lakeย
“Tokea nikiwa shambani leo sijisikii vizuri kabisa,ย nimeliweka jambo moyoni kama Mwanaume lakini Mwisho wa sikuย nimeshindwa nimeona ni bora nilitoe, Huu wasiwasi sijuiย utaondoka lini”ย
“Baba Matilda Mtoto yupo hai, na anatukumbuka sana. Eweย Yehova tenda kwa ajili ya Binti yetu popote alipo, mpe rohoย ya kurejea nyumbani ili sisi tuwe na Amani” Akasema Mamaย Matilda mikono ikiwa juu, Hakika familia hii ilikua yenyeย misingi thabiti ya dini.ย
“Kama siyo huu umasikini basi ningeenda Mjini kumtafutaย Matilda, hatuna Mtoto mwingine sisi” Jinsi Baba Matildaย alivyokua akilalamika alizidi kumfanya Mama Matilda adondosheย chozi lake.ย
“Baba Matilda moyo unaniuma sana tena zaidi ya sana, nikiwaย kama Mama naumia kuliko unavyofikiria” Alisema Mama Matildaย kisha akaingia ndani akiwa analia, alimuacha Baba Matildaย akiwa amejishika tama.ย
Mchungaji, Matilda na Mama Naomi walikua kwenye kordo laย Hospitali tayari kuelekea kwa daktari kwa lengo la kukabidhiย pesa ili upasuaji uanze. Ghafla polisi waliwasimamisha,ย sintofahamu ikatawalaย
“Sisi ni Maafisa wa polisi, Matilda upo chini ya ulinziย kuanzia sasa..” Alisema askari mmoja, Matilda alishtuka
“Mimi?”ย
“Ndiyo” Akasema polisiย
“Afande…huyu Binti amefanya nini?” alihoji Mchungaji Georgeย kwa Mshangao Mkubwa sana.ย
“Utajua ukifika kituoni, ruhusa ya kukamatwa kwake hii hapa”ย Alioneshaย
“Polisi nimefanya nini Mimi jamani, tafadhali msinifanyieย hivyo. Binti yangu ni mgonjwa sana anahitaji matibabu”ย Alisema Kwa kilio Matilda lakini tayari pingu zilikuaย zimeshafungwa kwenye mikono yake, pesa zilikua mkononi mwake,ย haraka Mchungaji akataka kuzichukua lakini polisi wakazuiaย
“Chochote mtakachokifanya hapa kitatumika kama Ushahidiย Mahakamani”ย
“Vijana, tafadhari sana hizo ni pesa kwa ajili ya matibabu yaย Mtoto, kama mnamkamata Matilda basi hizo pesa hazihusiani naย sababu yoyote ile ya Kumkamata, hizi ni pesa kutoka kanisani”ย Alisema Mchungaji George akitaka pesa ziachwe lakini polisiย hao walikua tayari wameanza kumchukua kwa nguvu Matildaย ambaye alikua akipiga mayowe ya kutaka aachwe ili akamtibieย Binti yake Patra.ย
Aliyeucheza mchezo huu alikua amejibanza mahali akiangaliaย namna mpango wake unavyofanikiwa, Neema akashangilia baada yaย Matilda kutupwa kwenye difenda ya polisi, gari hiyo ikaondokaย haraka sana. Mchungaji na Mama Naomi wakatazamana kwaย mshangao mkubwa hawakujua waende wapi, waingie kwa daktariย bila pesa au waelekee Kituo cha polisi ambacho walikuaย wametajiwa.ย
“Mchungaji nenda Polisi Mimi naenda kwa Mzazi mwenzake”ย Alisema Mama Naomi huku taharuki ikizidi kuwa kubwa ndani yaoย
“Kwa Mzazi mwenzake wakati amemkataa Mtoto? Twende pamojaย polisi kujua nini chanzo cha kukamatwa kwake”ย
“Na vipi kuhusu hali ya Mtoto Mchungaji?” Aliuliza Mama Naomiย
“Oooh hapa sasa nachanganikiwa Mimi, basi baki hapaย ukiangalia hali ya Mtoto, wacha Mimi nikimbilie Polisi”ย Alisema Mchungaji, akakimbilia kwenye gari na kuondoa gariย kwa kasi sana, Mama Naomi alipoona Mchungaji ameondoka nayeย akaondoka kuelekea kwa James kumpa taarifa.
Neema akajitokeza kisha akajinasbu kua ni lazima Matildaย aondoke Dar.ย
********ย
Mchungaji George alipofika kituo cha polisi alipaki gariย kwenye maegesho, kisha akashuka haraka haraka na kukimbiliaย ndani ya kituo hicho cha polisi. Akapandisha ngazi kabla yaย kukutana na polisiย
“Afande nimekuja haraka sababu bado sijajua sababu yaย kukamatwa kwa huyu Binti” Alisema Mchungaji akiwaย anamwangalia Matilda ambaye alikua amekalishwa chiniย
“Nifuate” Alisema polisi huyo kisha akamnyanyua Matildaย wakaelekea kwenye chumba kimoja ambacho kilionekana waziย kilikua chumba cha mahojiano, Mlango ukafungwa, ndani kulikuaย na askari wawili wengine ambao waliwakuta humoย
“Huyu Binti ni mwizi, mahali anapoishi siyo pake kuna Mtuย amemweka akae hapo lakini mwenye nyumba amelalamika juu yaย upotevu wa vitu vyenye thamani ya Zaidi ya Milioni 10”ย Alisema polisi huyo akiwa na sura kavu sana.ย
“Ameiba?”ย
“Ndiyo”ย
“Afande Mimi siyo mwizi na sijawahi kuiba chochote kile,ย nimeishi pale kwa zaidi ya mwaka mmoja iweje leo ionekaneย Mimi ni Mwizi? James anakosea sana” Alisema kwa uchungu sanaย Matildaย
“Kaa kimya hupaswi kuongea chochote kile hadi paleย aliyekushtaki atakapofika hapa” Alisema polisi huyoย
“Jamani kuweni na huruma, huyu Binti ana Mtoto mdogo ambayeย ni mgonjwa sana na yupo Hospitalini, hizo pesa mlizomkamataย nazo ni michango ya kanisa kwa ajili ya Matibabu” Alisemaย Mchungajiย
“Kwakua umeshafahamu nini kilichopelekea akakamatwa basi niย vema ukakaa kimya huku ukisubiria uendeshwaji wa kesi hii,ย kama unahitaji kuwa shahidi wa hili basi tukutane mahakamani”ย Alisema Polisi huyo ambaye alishapewa Hongo na Neema ili kesiย hiyo iwe haiย
“Nenda nje” Akasema polisi huyo akimtaka Mchungaji aondoke
“Afande kua na moyo wa utu japo hata kidogo, Mtoto wakeย anaangamia kule Hospitali kwa kukosa matibabu, ninaomba sanaย na nipo chini ya Miguu yenu ikibidi hata kua Mdhamini waย hili, hizo pesa nazihitaji zikamtibie Binti yake” Alisemaย Mchungaji George akishinikiza apewe pesa hizo lakini polisiย wakamtoa Nje Mchungaji Georgeย
Matilda alikua Mtu wa kulia muda wote huku akiomba kwa Munguย kuhusu hali ya Binti yake, dakika chache baadaye aliingiaย Neema akiwa ameambatana na yule Mwanaume anayeitwa Masudi,ย akavuta kiti na kuketi, Matilda alishtuka baada ya kumwonaย Neemaย
“Matilda, kama ulifikiria unaweza ukachomoka kwenye hili basiย sahau kabisa” Alisema Neema, polisi wakatoka ili kuwaachiaย wazungumzeย
“Kumbe ni wewe ndiye uliyenifungulia hii kesi isiyo na kichwaย wala Miguu, wewe ni Mzazi mtarajiwa si ndiyo? utajisikiajeย ukitendewa namna nitendewavyo Mimi…Kumbuka Binti yangu yupoย Hospitalini na anahitaji Matibabu…” alisema kwa uchunguย Matilda huku chozi likimvuja, alishindwa kufuta chozi sababuย alifungwa pingu mikononiย
“Kumbe inaumiza eeeh? basi hivi ndivyo ambavyo Mimi piaย naumia ninapokuona mbele ya macho yangu, una chaguo moja laย kufanya, nalo ni kukubali kurudi kwenu kabla hujafikishwaย mahakamani, ukikubali hii kesi naifuta haraka sana, sitakiย kukuona ukiendelea kuwa karibu na James kwa lolote lile”ย Alisema Neemaย
“Dada yangu kama unafikiria Mimi ni dhahifu kwenye hiloย naomba usahau kabisa, ikibidi mniuwe lakini siwezi kuidhurumuย haki ya Mwanangu Kumjua Baba yake” Alisema Matilda, akapigwaย kofi na Neemaย
“Mshenzi mkubwa wewe, sasa endelea kujifanya Mjuaji kwenyeย hili, mwisho wako unakuja” Alisema Neema kisha aliondoka hapoย akiwa na Masudi, walipofika kwenye gari Neema alionekana kuaย na hasira sana sababu lengo halikua kesi bali ni kumtisha tuย Matildaย
“Usiwe na hasira, huu ni mwanzo tu Naamini matesoย atakayoyapata atakubali kuondoka mwenyewe” Alisema Masudi,ย Mwanaume ambaye alionekana kua karibu sana na Neema
“Kama kuteswa inabidi ateswe haswa, kwasababu amekataaย kuondoka kwa uhuru basi ataondoka kwa shari kama atakavyo”ย Alisema Neema kisha aliondoa gari haraka sana.ย
“Nikusaidie nini?” lilikua ni swali aliloulizwa Mama Matildaย baada ya kufika ofisini kwa James, hakukaribishwa ofisiniย bali aliachwa getini azungumzeย
“Ni kuhusu Matilda” Alisema Mama Naomi akiwa anahema “Amefanyaje?”ย
“Amekamatwa na Polisi muda mchache uliopita, hadi sasaย hatujui sababu ya kukamatwa kwake. Nakuomba James, hunijuiย lakini Mimi ni jirani wa Matilda kule anakoishi, fanyaย uwezalo ili aachiwe”ย
“Usinichekeshe ndugu yangu,, yaani umetoka kote huko hadiย hapa ili kuniambia hicho tu? unaonekana kama Mwanamke mwenyeย busara zako lakini sikutegemea kama mwisho wa siku ungesimamaย na Mwizi” Alisema James akionekana hana wasiwasi kabisaย
“Mwizi? nimeishi naye kwa siku zote hakuwahi kuonekana naย tabia hiyo ya wizi, hata kama akawa mwizi lakini ana haki yaย kuokoa Maisha ya Binti yake, fanya kwa ajili ya Patra niย Binti yako yule James” Alisema Mama Naomi, kofi likatuaย kwenye shavu lake la kuliaย
“usirudie tena hiyo kauli, hakuna unachojua kuhusuย Mimi…..Ondoka” Alisema kwa hasira sana Jamesย
“Laiti kama ungelijua Maisha anayopitia Matilda sasa hiviย wala usingethubutu kunipiga, basi siyo Mtoto wako lakiniย kumbuka wewe ndiye uliyemtoa kwao basi thamini utu kamaย Binadamu wa kawaida” Alisema Mama Naomi kwa uchungu sana hukuย Mtoto akiwa analia mgongoniย
“Nini ambacho hujanielewa?” Alisema James kwa hasira akiwaย anamsogelea Mama Naomi, kelele hizo zikamtoa Sekretari hadiย njeย
“Bosi kuna nini?” aliulizaย
“Simjui ananilazimisha nimsaidie, amekua king’ang’anizi sanaย Jack!”
“Halafu kama alikuja jana huyu na Mdada mwingine, suraย nishaikumbuka kumbe walikua wanahitaji msaada? kwaniniย usiwasaidie Bosi?” aliuliza Jackย
“Hujui kitu hakuna msaada unaotolewa kwa kung’ang’ania namnaย hii, Kutoa ni moyo, sikia nenda ofisi zingine hapa hatusaidiiย omba omba” Alisema James kisha akarudi ofisiniย
Jack akamtazama Mama Naomi. Akiwa kama Mwanamke alimuoneaย huruma Mama Naomi na Mtoto aliye mgongoni, akatoa noti yaย elfu tano akampaย
“Chukua hii itakusaidia” Alisema Jackย
“Asante lakini huu siyo msaada ambao Mimi niliutaka kutokaย kwa Bosi wako” Alisema Mama Naomiย
“Ulikua unahitaji msaada gani?” Jack akapata shahuku yaย kutaka kujua zaidi maana hakuna ombaomba ambaye anawezaย kukataa shilingi elfu tano, akasogeaย
“Bosi wako James amezaa na Msichana yule ambaye nilikuja nayeย jana, James amemkataa Mtoto sababu ni mlemavu, Mtoto yupoย mahututi Hospitalini, Yule Msichana amekamatwa na polisi mudaย siyo mrefu ndiyo maana nilikuja hapa ili kumpa taarifaย akamsaidie hata Mtoto sababu anahitaji matibabu, hakuna pesaย ya kumtibia” Alisema kwa uchungu Mama Naomi huku akikaribiaย kudondosha chozi, Jack aliumia sanaย
“Sikia chukua hii kadi yangu, kwa lolote naomba unipigie,ย nenda sababu James ana hasira sana” Alisema Jack, kilaย alivyomtazama Mama Naomi akiwa anaondoka alisikitika kishaย akarudi Ofisini, akamkuta Bosi wake akiwa anataka kutokaย
“Yaani Watu wengine Bwana kutaka kuharibiana siku tu, kwaniย ni lazima kumsaidia Ombaomba….Mimi natoka sijisikii kufanyaย chochote kwa sasa, siku nyingine usiruhusu Omba omba katikaย ofisi yangu”ย
“Sawa Bosi” Aliitikia Jackย
Jua lilikua kali lakini Mchungaji George alihitaji kujuaย hatma ya Maisha ya Matilda, Mateso yalianza upande waย Matilda, alipigwa bila kosa lolote lile. Lengo lilikua niย kumtaka aondoke Dar ili asiwe kero kwa James, ndichoย alichokipanga Neema.
Baada ya Saa nzima aliingia Mama Naomi akamkuta Mchungajiย George akiwa anachomwa na jua la Mchanaย
“Eeeh kulikoni Huko Hospitali kuna usalama?” aliulizaย Mchungaji George kwa Mshtuko sababu alimuacha Mama Naomiย Hospitaliย
“Sijui Mchungaji lakini natumaini hakuna kitakachoharibika,ย Mungu aliye hai anapigana vita nzito muda huu, vipi kuhusuย Matilda?”ย
“Bado yupo kituoni, hizo sauti unazozisikia ni zake,ย anaonekana kua kwenye mateso makali” Alisema Mchungajiย
“Jamani sasa amewakosea nini?”ย
“Wanasema ameiba vitu vyenye thamani kwenye nyumba anayoishi”ย
“Ameiba? si kweli, Maisha anayoishi Matilda ni ishara toshaย kua hawezi kuiba, hawa Watu kwanini waneamua kumkatili Bintiย wa watu jamani”ย
“Hatuna namna Zaidi ya kusubiri muda utupe majibu sahihi,ย Kama hakufanya hivyo basi ataachiwa tu ila kinachonipa hofuย ni kuhusu Binti yake, sijui itakuaje”ย
“Mchungaji hapo ni pazito zaidi sababu uliponiacha Hospitaliย nilitoka na kwenda kwa Mwanaume aliyezaa naye lakini huweziย amini kamkana mbele ya Macho yangu, kanipiga kofi pia”ย Alisema Mama Naomi akiwa anamweka vizuri Mtotoย
“Sijui hata tufanye nini, kwani wazazi wa Matilda wapo wapi?”ย
“Wazazi wake wapo Njombe, pamoja na shida anazopitia lakiniย alisema hawezi kurudi kwao wala kusema chochote kwa Wazaziย wake”ย
“Oooh Mungu wangu, basi wewe ungerudi tu nyumbani Mimiย nitabakia hapa kwa masaa kadhaa kwa ajili ya kujua Hatma yaย Matilda” Alisema Mchungaji Georgeย
“Sawa Mchungaji kwa chochote kile tuwasiliane” Alisema Mamaย Naomi kisha akaondoka kituoni hapo.ย
Upande wa pili, gari moja lilikua likiendeshwa kwa spidiย kubwa sana, ndani yake alikuwepo James akionekanaย kuchanganikiwa, maneno ya Mama Naomi yaliendelea kujirudiaย ndani ya Kichwa chake, akawa anapiga usukani kwa hasira,ย alikanyaga mafuta hadi nyumbani kwake, akateremka harakaย kisha akaingia ndani
Kama akili yake ilivyomtuma ndivyo alivyokuta, Neema alikuaย ameketi huku akitikisa miguu yake, pembeni kukiwa na embeย bichi ambalo lilikua linasukuma tabasamu lake, baada yaย kumwona James akiwa ameingia na taharuki akamuulizaย
“Kulikoni Baby mbona una taharuki?” aliuliza Neema akiwaย ameacha kula embe Bichiย
“Nenda kafute kesi inayomkabili Matilda” Alisema James kishaย akajitupa kochini kama Mtu aliyechoka sanaย
“Unasemaje?”ย
“Ulivyosikia ndivyo nilivyosema, hakuna sababu ya kuendeleaย na kesi, tuangalie namna nyingine ya kumfanya Matilda aondokeย hapa Mjini” Neema akamtazama Kwa hasira Jamesย
“James Mimi natarajia kua Mama wa Mtoto wako, siwezi kuzaaย Mtoto katika familia yenye migogoro namna hii, ikishindikanaย nitoe ujauzito ili ulee Mtoto wako na Matilda” Alisema Neemaย
“Sina maana hiyo Neema, Sina lengo hilo nawe huna sababu yaย kufanya hivyo, tambua kiu yangu ni Mtoto lakini naona Matildaย anateseka sana, Mtoto wake yupo Hospitalini”ย
“Kwahiyo umeanza kua na huruma si ndiyo? Basi hakuna sababuย ya kujificha, jitokeze hadharani ujitangaze kua Bilioneaย mwenye Mtoto Mlemavu, si una shida sana ya Mtoto basi hakunaย sababu ya Mimi kubeba huu mzigo wakati una Mtoto unaye muoneaย huruma” Alisema Neema kwa hasira zaidi, akanyanyuka iliย aondoke lakini James akamshika mkono kwa lengo la kumzuiaย asiondokeย
“Mpenzi hupaswi kua na hasira sababu wewe ni Mama mtarajiwa,ย natamani haya mambo yaishe kwa namna nzuri, basi nitaendaย Polisi kwa ajili ya kuzungumza na Matilda ili aondoke hapaย Mjini” Alisema James lakini Neema akatoa Mkono wa Jamesย akaelekea chumbani.ย ย
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TANO Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx



6 Comments
Sawa
kama ni kwel duuh matlida anapep yake
Aiseee huyu enema anazngua ..s wampe pesa Ile mchungaj jmn ๐ฃ๐ฃ
Moyo wangu unauma hadi joz dah!! Tukija kwenye uhalisia sure ni maisha watu wanapitia jmn
Hadithi nzri nakama ina uhalisia fulani hivi
a1na1b