August 3 Mwaka 2018 Young Africans iliachana na jumla ya wachezaji 14 kisha wakabaki na majina ya wachezaji wasiozidi 17 ndani ya kikosi chao ambao, katika orodha ile ya wachezaji walioachwa kulikuwa na majina kama David Molinga, Mrisho Ngasa, Jaffary Mohamed, Tariq Seif, Andrew Vicent, Papy Kabamba Tshishimbi na Mohamed Issa ambao mikataba yao ilimalizika na hawakuongezewa
Kipindi hiko Young Africans ilisitisha mikataba yao ni Raphel Daud, Yikpe Gislain, Ali Ali, Patrick Sibomana, Muharami Issa, Ally Mtoni Sonso(Marehemu) na Eric Kabamba! Hapo katika idadi ile ya wachezaji 17 waliobaki ni wanne tu ndio walikuwa Raia wa Kigeni ambao ni Haruma Niyonzima, Farouk Shikalo, Lamine Moro na Bernard Morrison
Baada ya hapo Timu ilicheza misimu mitatu(2018/19, 2019/20 na 2020/21) bila Ubingwa wa Ligi Kuu, walikubali kufanya mabadiliko na hata hiyo Miaka mitatu bila Ubingwa bado waliishi kwenye nafasi mbaya na walifanya mabadiliko ya wachezaji wengi sana ndani ya kikosi
Walicheza ‘Four Seasons’ bila Ubingwa wa Ligi Kuu na waliamua kufanya kitu cha tofauti baada ya kufeli! Kwanza kurudisha mashabiki karibu na Timu yao, kufanya uchaguzi wa Viongozi ambao wana maono ya kupeleka chapa ya klabu yao mbali zaidi na kufanya Usajili wa wachezaji Bora tofauti na walioondoka! Timu ikarudi kwenye mstari mpaka sasa inafanya vizuri
Simply! Mantiki yangu ni kwamba kwa sasa SIMBA SC wanatakiwa kufanya maamuzi ya haraka hasa ndani ya uwanja, Timu inahitaji kubadili eneo kubwa sana la wachezaji waliopo ambao tayari wameipa Timu nyakati zao bora! Simba inahitaji ‘Quality Players’ wengi ambao wataiaogeza chapa ya MNYAMAA zaidi ya hapo ilipo
Kwakuwa eneo kubwa la wachezaji inaonekana linatakiwa kupungua pale basi wakati ndio huu! Wachezaji wengi ambao wameingia ndani ya Klabu wamefeli kati ya 100%, naona wamefeli 70% na wamefaulu 30% wamefaulu
Simba SC iwapo watafeli tena kwenye eneo la Usajili basi hizi nyakati zitaendelea kuishi kwao, Abdelhack Benchikha anahitaji sura mpya ili kurudisha ubora wa Timu na kusukuma ‘Vision & Mission’ ya Klabu hasa kwenye CAF Tournaments! That is Truth about LUNYASI
SOMA ZAIDI: Waraka Mzito Wa Hamisi Kigwangalla Kuhusu “Kuinunua Simba”



