Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya nne
Wakiwa wanaendelea kujibizana, walianza kusikia sauti ya Bi. Lugumi ikisemaย
โKufaaaaaโผ kufaaaaโผโ kila aliyeisikia sauti hii alianza kutetemeka huku damu nzitoย ikimtoka puani kisha walikufa papo hapo, hali ya taharuki iliingia na kufanya kilaย mmoja atawanyike anakokujua yeye mwenyewe. Sauti ya Bibi Lugumi ilizidi kusambaa,ย ilikua ni sauti ya kunongโona iliyotoka kwa kuivuta sana.ย
SEHEMU YA TANO
Kelele za Wanakijiji ziliwashtua Mzee Miroshi na Zahoro wakiwa wamefungiwa ndani yaย chumba kimoja nyumbani kwa Mzee Kova, Zahoro akamwambia Baba yakeย
โNi lazima tujiokoe kutoka hapa Babaโ alisema kisha alitafuta kitu kitakachomsaidiaย kuuvunja ule Mlango, macho yake makubwa yalikiona kipanda cha mbao kilichokuaย kimeegemezwa ukutani, akakichukua. Kilikua ni kipande kilichotokana na fanicha zaย ย
zamani, haraka akasogea mlangoni huku akimtazama Baba yake Mzee Miroshi ambayeย tayari alikua ameshaishiwa nguvu huku akitoa hewa nzitoย
โBaba usijali tutatoka salama Hapaโ alisema Zahoro, kisha alimsogeza kando Baba yakeย ili atakapouvunja mlango Baba yake asiathirwe na vipande vitakavyoruka. Akavutaย nguvu kisha akaukita mlango kwa kutumia kipande cha mbao, mlango ukatikisikaย
Kelele zilizoendelea kusikika huko nje zilimpa nguvu Zahoro ya kuendelea kuuvunjaย Mlango ili waondoke kifungoni. Hapakua na Mlinzi hapo nje kwasababu taharukiย ilikuwa imewasomba wote na kuiacha nyumba hiyo yenyewe.ย
Zahoro aliendelea kugonga mlango kwa nguvu zaidi, kila pigo liliufanya mlangoย kudhoofika. Jasho lilimtoka huku mikono yake ikianza kuuma, lakini hakuacha. Alijuaย kuwa muda ulikuwa hauko upande wao. Baada ya mapigo kadhaa, mlango ulianzaย kulegea na hatimaye kupasuka vipande vipande. Haraka akamshika baba yake mkonoย na kumsaidia kusimama.ย
โTwende Baba, hatuna muda!โ alisema kwa sauti ya dharura. Zahoro alimsaidia Babaย yake kutoka ndani ya chumba kisha wote walisimama huku macho yao yakijawa naย Mshangao. Moshi mkubwa ulikua ukifuka Kijijini, Mlinzi mmoja wa kijiji ambayeย aliachwa kwa ajili ya kuwalinda walimkuta akiwa amelala chini huku Damu nzitoย ikimtoka puani na Mdomoni.ย
Mzee Miroshi aligeuza shingo yake kwa uchovu akimtazama Zahoro ambaye aliguswa naย Mtazamo wa Baba yake, macho yao yalipokutana kila mmoja alisubiria kusikia kutokaย kwa mwenzake. Ghafla sauti ya muito wa simu ilisikika kutoka kwenye mfuko wa surualiย wa Zahoro.ย
Mzee Miroshi alikaza macho ya Mshangao, hakuwahi kumwona Zahoro akiwa na simuย hata siku moja. Zahoro alipepesa macho taratibu kumwonesha Baba yake kua alikuaย akiitumia simu hiyo kisiri, haraka aliitoa kutoka mfuko wa siri maarufu kama โDocho’
Ilikuwa ni simu ndogo sana. Mzee Miroshi akampa ishara Zahoro aipokee haraka โ pengine wangepata msaada wa kutoka hapo kijijini. Zahoro aliweka simu sikioni, lakiniย kabla hajaongea chochote, alishtuka kuona kivuli kikisogea mbele yake.ย
Mzee Kova alikuwa amesimama hapo, uso wake ukiwa na uamuzi usiotikisika. Mikonoย yake ilikuwa thabiti, ikishikilia bunduki aina ya Gobole, ambayo sasa ilikuwaย imeelekezwa moja kwa moja kwa Zahoro.ย
โUsithubutu kuendelea,โ Mzee Kova alisema kwa sauti nzito, yenye mamlaka.ย
Zahoro alihisi mgongo wake ukilowa jasho, lakini akajitahidi kutokupoteza mwelekeo.ย Akatazama moja kwa moja machoni mwa Mzee Kova, akijaribu kutafuta dalili yoyote yaย huruma. โMzee Kova, hatutaki matatizo. Tunajaribu tu kuondoka hapa,โ alisema kwaย sauti tulivu lakini thabiti.ย
Mzee Kova hakutikisika. โHamna pa kwenda. Mnafikiria mnaweza kutoroka baada yaย yote yaliyotokea?โ aliuliza huku akiimarisha mshiko wake kwenye Gobole.ย
Mzee Miroshi aliyekuwa kimya muda wote, alisogea mbele kidogo, akiinua mkono wakeย kwa ishara ya utulivu. โMzee Kova, umetufahamu kwa miaka mingi. Unajua kuwa sisi siย maadui zako. Tafadhali, tuache tuondoke.โย
Mzee Kova akahamaki huku akihisi pengine Mzee Miroshi alikua anapanga njama yaย kumzubaisha ili waondoke, akaikaza Gobole huku kidole kikiwa tayari kufyatua risasi,ย akawa anaiamisha Bunduki kutoka kwa Zahoro kuelekea kwa Mzee Kovaย
โNipatie hiyo simu vinginevyo nitamuuwa Baba yakoโ alisema Mzee Kova kwa sautiย iliyoashiria muda wowote anaweza kutenda ikiwa mzaha utatokea. Kwa jinsi Zahoroย anavyompenda Baba yake, alimpatia ile simu Mzee Kova ambaye alikua makini sana.ย
Akamuuliza Zahoroย
โHakuna simu inayofanya kazi hapa Kijijini, simu yako imewezaje kuita?โ Zahoroย alijawa na hofu huku akitetemeka. Jasho la mgongo lilikua likimvujaย
โMzee Kova, Kijana wangu si adui yako. Alikua Mdogo wakati ule, tafadhari sanaย hurumia Maisha yakeโ alisema Mzee Miroshi, akapigwa na Mdomo wa goboleย akaanguka chini.ย ย
โHii Biashara haikuhusu kabisa Miroshi, kaa kimya.โ Kisha akamgeukia Zahoro,ย akakaza Mikono yake kwenye Gobole huku akimtazama kwa jicho kali.ย
โWewe kosa lako ni kuona laana ikiwa inaingia, nina uhakika unajua njia ya kutoka hapaย Kijijiniโ alisema Mzee Kova, kelele za WanaKijiji ziliendelea kuongezeka, vilio na Moshiย viliendelea kujaza taharuki.
Sauti ya Bibi Lugumi ilikua ikiendelea kusikika taratibu ikija nyumbani kwa Mzee Kova,ย kila mmoja aliisikia sauti hiyo, ni sauti nyemelezi isiyo na kelele. Sauti ya kunongโonaย inayouwa Mamia ya Wanakijiji wa Kijiji cha Nzena. Mzee Kova akataka kufanya harakaย ili sasa Zahoro aseme njia ya kutoka hapo Kijijini ili awe salama na Laana ambayo yeyeย ndiye aliyeisababisha kwa kumuuwa Masumbuko.ย
Zahoro alikua kimya akiisikia sauti hiyo iliyokua ikikaribia hapo, sauti hii ni ile sautiย aliyoisikia ndotoni. Ni sauti iliyomsumbua, hakutaka kuisikia. Akaziba masikio yakeย
โHutaki kusema si ndiyo? Sasa nakuuwaโ akasema Mzee Kova, kitendo bila kuchelewa Mzee Miroshi akaivuta Miguu ya Mzee Kova ili Zahoro akimbie. Mzee Kova akaanguka,ย Gobole lake ikadondokea pembeni.ย
Ghafla wote wakasimama huku wakiangalia juu, kitendo kilichomshangaza sana Zahoro,ย akajiuliza maswali mengi huku akiwa ameziba masikio yake. Akashuhudia Damuย zikianza kuwatoka. Hata dakika moja haikufika, walianguka chini na kuanzaย kutapatapa. Kwa macho yake Zahoro alishuhudia kivuli chenye taswira ya Bibi Lugumiย aliyemwona ndotoni, alikua akitabasamu huku akiongea maneno yake ambayo Zahoroย hakutaka kuyasikia kabisaย
Macho yalimtoka pima Zahoro, alirudi nyuma huku akijibamiza ukutani. Alihisi haliย isiyo ya kawaida, mwili ulikua mzito akitokwa na jasho jingi huku kile kivuli kikimtakaย Zahoro atoe mikono yake Masikioni aisikie ile sauti ya ajabu inayouwa. Zahoro hakutakaย kuisikia ile sauti hivyo alijitahidi sana kupambanaย
Kadili kivuli kilivyosogea ndivyo ambavyo alikua akipata maumivu makali ya kichwa,ย mwisho alipiga kelele yenye sauti kali ya kugumia. Pale pale alipoteza fahamu zake naย kuanguka chini kama mzigo.ย
***ย
Nje Ya Kijiji.ย
Magari ya Ulinzi na Usalama yalikua eneo ambalo Kijiji cha Nzena kilikuwepo kabla yaย kutoweka kwake. Bado ilibakia kua simulizi ya kushangaza kwa wengi. Waziri waย Maliasili alikua akifikiria kwa kina ni sayansi ya aina gani ambayo imekipoteza Kijijiย kilichobeba rasilimali kubwa ya Madini, wafanya Biashara na wamiliki wa Migodiย walikua wamepotelea humo.ย
Simu zilikua hazipatikani, akasogea kwa mmoja wa washauri wake akamwulizaย
โHaihusiani na Uchawi?โ aliuliza kwa sauti ambayo ilionesha wazi kuwa alikosa majibuย ya kawaida. Aliongea akiwa anapandisha suruali yake nyeusi, akaweka koti lake vizuri.ย Huku nje ilikua ni saa Mbili asubuhi, jua lilikua limechomoza vyema sasa.ย
โMh! Hili jambo ni gumu sana kulipatia majibu ya haraka, kupotea kwa Kijiji ni hadithiย za kwenye vitabu vya kale lakini leo tumeshuhudia hili jambo la kushangazaโ alijibuย Mshauri wa Waziri, akaweka mawani yake vizuri halafu akaendeleaย
โPengine tunaweza kupata Majibu kwa njia hiyo, hebu tuifanyie kaziโ alisema, harakaย Waziri akamjibu kwa sauti ya kishindo
โAtafutwe na afichwe kwa siri ili hili jambo liwe siri baina yetu.โย ย
โOndoa shaka Mkuuโ akasema kisha akapiga simu mahali ili kuhitaji Mganga waย Kienyeji mwenye uwezo Mkubwa sana wa kuangalia mambo yasiyoonekana kwa machoย ya kawaida.ย ย
Ilichukua takribani masaa mawili hadi kumpata na kumfikisha kwenye gari ya Waziri waย Maliasili. Gari hiyo ilikua kubwa yenye nafasi ya kutosha, Mganga akaelezwa ni jamboย gani aliloitiwa hapo.ย
Yule Mganga akacheka kidogo kama ilivyo kawaida ya waganga, kisha akatulia naย kuwaambiaย
โNiliona kuhusu Kijiji hiki, hakipo. Kukiona ni Mjaaliwaโ alisema kwa kujiamini, kwaย sauti ya upole sana iliyojaa huzuni. Waziri akashtuka kisha akamwulizaย
โUnamaanisha nini?โ alihoji akiwa ameshupaza shingo yake huku makunyanzi yakiwaย yamefunga uso wake. Mganga akameza mate kidogo halafu akasemaย
โKijiji hiki, kimepokea laana ya Miaka mingi kwa kifo cha Kijana Masumbuko aliyekuaย mlemavu wa ngozi. Tangu hapo Bibi yake alikilaani Kijiji hiki kisha alijichoma Moto naย kufa, sasa ile laana imekifanya Kijiji hiki kupotelea kuzimu. Laiti kama mgepata japoย nafasi ya kusikia sauti za vilio, mateso na maumivu wanayo kutana nayo mgelia machoziย ya Damu.โ Alisema kisha alisikitika kwa kichwa chakeย
โHakuna anayeweza kwenda huko wala kutoka huko. Historia itafutika, Kijiji cha Nzenaย kimeshapotea. Msihangaike sababu hakuna atakayetoka hai na kurudi Dunianiโย alisema, Waziri na Mshauri wake walitazamana. Walielezwa kila kitu na hawakuwa naย swali lolote lile, Mganga akarudishwa walipomtoa.ย
Ukimya ukatawala, kila mmoja alikaa kimya baada ya kujua kuwa hakuna chochoteย wanachoweza kukifanya ili kukipata Kijiji hicho tajiri. Agizo la Rais lilikua niย kuhakikisha wanapata ufumbuzi wa Kisayansi lakini hadi muda huo Sayansi haikutoaย majibu, majibu pekee ambayo waliyapata ni ya kiganga.ย
Waziri akajitupa kitini huku akifumba macho yake, hakujua atamweleza vipi Rais waย Ganza, utajiri uliopotea kwenye Kijiji cha Nzena ni utajiri mwingi sana wa Madini.ย
Mara mlango wa gari ulifunguliwa haraka sana, Waziri na Mshauri walishtuka. Mtuย mmoja kutoka kwenye timu yake alikuja ghafla na kumwambia kua kuna Mtu kutokaย Kijiji cha Nzena amepiga simu. Macho yalimtoka Waziri wa Maliasili, ingewezekanajeย kua simu itoke kuzimu? Alikua kama Mtu aliyezinduliwa kutoka usingizi wa Pono,ย akatupa swali moja ngangariย
โUnasemaje?โย ย
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TATU Hapa Hapa Kijiweni
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
76 Comments
Good job ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Tamu
Aloooooo hii mambo ni ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅAfu nikukumbushe ni sehemu ya Sita ndo inafata na si sehemu ya tatu kama ulivosema
Bonge la move
Simulizi nzuri Sana sema imekuwa fupi
Mbna kama zahoro atapona๐ค
Good story
Boost your income effortlesslyโjoin our affiliate network now! https://shorturl.fm/m2tJf
Drive sales, earn bigโenroll in our affiliate program! https://shorturl.fm/xYLqR
https://shorturl.fm/UdQFq
https://shorturl.fm/1eb7S
https://shorturl.fm/gUgcb
https://shorturl.fm/RHot4
https://shorturl.fm/u2mR6
https://shorturl.fm/6Ij8t
https://shorturl.fm/n18PQ
https://shorturl.fm/lLCPQ
https://shorturl.fm/VDFz4
https://shorturl.fm/YSHok
https://shorturl.fm/qMyW8
https://shorturl.fm/QPd5u
https://shorturl.fm/8z1AV
https://shorturl.fm/mU0Th
https://shorturl.fm/o6Pa2
https://shorturl.fm/W8CvZ
https://shorturl.fm/DZT98
https://shorturl.fm/dun6S
https://shorturl.fm/sYo2L
https://shorturl.fm/45riq
https://shorturl.fm/ibdka
https://shorturl.fm/QpYwV
https://shorturl.fm/93dBl
https://shorturl.fm/BZcIn
https://shorturl.fm/i5ly7
https://shorturl.fm/ptVVr
https://shorturl.fm/LbsZr
https://shorturl.fm/yhxOF
https://shorturl.fm/6o3Jf
https://shorturl.fm/rB0xk
https://shorturl.fm/fEb6q
https://shorturl.fm/kCC0O
https://shorturl.fm/NR2u3
https://shorturl.fm/p9E8w
https://shorturl.fm/tbLWx
https://shorturl.fm/TBImU
https://shorturl.fm/us6pn
https://shorturl.fm/643Zb
https://shorturl.fm/RT29D
https://shorturl.fm/Os806
https://shorturl.fm/FYm24
https://shorturl.fm/JkkWy
https://shorturl.fm/Ge56k
https://shorturl.fm/PnAnI
https://shorturl.fm/pK2t7
https://shorturl.fm/ocsH9
https://shorturl.fm/mos1j
https://shorturl.fm/HfmZn
https://shorturl.fm/qqf35
https://shorturl.fm/mfI4Q
https://shorturl.fm/gwE4n
https://shorturl.fm/3Nb4c
https://shorturl.fm/KwpEn
https://shorturl.fm/YGoz4
https://shorturl.fm/IegeZ
https://shorturl.fm/Nll2t
https://shorturl.fm/ZmiSh
https://shorturl.fm/E0888
https://shorturl.fm/Gg3yo
https://shorturl.fm/Y3zyG
https://shorturl.fm/PZWoO
https://shorturl.fm/n7iyP
https://shorturl.fm/JtN4E
https://shorturl.fm/HdajW
https://shorturl.fm/LXJF8
https://shorturl.fm/hYYqX
https://shorturl.fm/RfKcn