Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya tatu
Mke alipoisoma ile karatasi aligeuza macho kumtazama Mume wake kisha kwa mshangao akamwambia
“Mume wangu unatokwa na Damu puani” alisema akiwa anarudi nyuma taratibu, Mume wake akapeleka kidole puani. Alikua akitetemeka akikiangalia kidole chake kilichotapakaa damu. Kisha alimtazama Mke wake, aliiyona damu pia puani kwa Mke
wake. Akamnyooshea kidole kumwambia kua anatokwa na damu, naye Mke alipopeleka kidole puani aliiyona damu mbichi.
SEHEMU YA NNE
Hali ya hatari na taharuki vilianza kutawala, hisia mbaya iliwangia. Papo hapo, mke Wake alianza kutapika Damu.
Aliishiwa nguvu akajikuta akianguka chini kama mzigo huku akiwa amebanwa na kwikwi mbaya. Mume wake alikua amesimama pale pale huku damu zikizidi kumtoka puani na Mdomoni, alikua akianza kukosa pumzi. Alihisi kifo mbele yake huku akiwa amelishikilia koo lake kuashiria alikua anapoteza uwezo wake wa kupumua.
“Mungu nisa…mehe” ilikua ni kauli ya mwisho ya Mume wa yule Mwanamke, akadondoka na kufariki papo hapo huku Mke wake naye akimalizikia kufariki hapo.
***
Jua la Utosi lilikua tayari limeshatua. Nyumbani kwa Mzee Kova waliendelea kumsubiria Mlinzi arudi lakini masaa yaliendelea kutembea, Mzee Kova akawaambia Wazee wengine kua waongozane kuelekea nyumbani kwa Mtimbe. Walinzi wawili waliachwa ili kuhakikisha Zahoro na Baba yake Mzee Miroshi hawatoroki.
Mguu kwa mguu, walipofika njia panda walikutana na Miili mitatu akiwemo Mlinzi wa Kijiji. Kila mmoja alishtuka sana kumwona Mlinzi wa Kijiji akiwa amekufa huku damu ikiwa imetapakaa usoni, miili mingine ilikua na hali hiyo hiyo kuashiria kua wote walikufa kifo kinacho fanana.
Maiti moja ilikutwa na kipande cha karatasi, Mzee Kova akaagiza asomewe kilichomo ndani yake. Mlinzi mmoja akakichukua na kumsomea
“MWISHO UMEFIKA” alisema yule Mlinzi kwa sauti ya usikivu, lakini hapo hapo alianza kutokwa na damu puani, masikioni huku hali ya kuchanganikiwa ikianza kumzonga. Ilibidi wote wasogee nyuma huku wakimtazama yule Mlinzi akiwa anatapa tapa chini, hadi alipofariki mbele ya macho yao.
Halikua pigo la kawaida, liliwatingisha Wazee wote akiwemo Mzee Kova na Mzee Kisugu. Maiti Nne zilikua mbele ya macho yao, wakiwa hawajui nini wanatakiwa kufanya, ghafla wingu jekundu lilianza kutanda angani likisindikizwa na Upepo mkali sana.
Upepo mkali sana ulizidi kusukuma na kulipanga wingu jekundu angani, giza lilianza kuingia. Taharuki ilianza, Watu walianza kukimbizana wasijue wanaelekea wapi. Sauti ya Bibi Lugumi ilisikika Kijijini pote ikiitangaza laana ambayo tayari ilikua imeshakivaa Kijiji cha Nzena.
Sasa ilikua rasmi masikioni mwa kila mwenye akili na ufahamu kua, vifo na mabadiliko ya hali ya hewa vyote vilitokana na Laana ya Bibi Lugumi kutokana na kifo cha Masumbuko. Vilio vilitanda kote, giza lilishamili kwa kasi na kukifunika Kijiji chote cha Nzena.
Ndani ya dakika mbili, kijiji chote kilikua giza tupu. Upepo mkali uliacha kuvuma kisha mvua ilianza kunyesha.
**
“Baba” Zahoro alimwita Mzee Miroshi aliyekua amejiinamia. Mzee huyo aliinua kichwa chake na kumtazama Zahoro, sura yake ilipoteza raha.
“Nini mwisho wa kila kitu?” aliuliza Zahoro, sauti yake ilikua juu kidogo sababu bado mvua kubwa ilikua ikiendelea kunyesha.
“Kifo” alijibu kwa sauti kavu Mzee Miroshi. Hakutaka kumtazama tena Zahoro aliyeanza kudondosha chozi la kukosa tumaini.
“Tutakufa sote?” aliuliza tena Zahoro, Mzee Miroshi alitikisa kichwa chake. Koroboi ilikua ikiwaka ili kuwapatia mwanga kidogo.
“Kwanini sasa hiyo laana isihukumu walio husika, kwanini itutese ambao hatukuwa sehemu ya Maisha yaliyopita?” aliuliza Zahoro kwa sauti ya Kilio kilicho jaa lawama, Mzee Miroshi hakutaka kumjibu chochote Zahoro.
Ukimya wa Mzee Miroshi ulimsumbua Zahoro, aliamua kumtikisa Baba yake atoe jibu, ndipo Mzee Miroshi akapaza sauti yake kwa ukali akisema
“Alitulaani sisi na vizazi vyetu, hata wewe umelaanika Zahoro. Sote hapa Kijijini tutakufa, usiniuliza chochote. Nimechoka, nimechoka kabisa” alisema kwa sauti kali ya kufoka huku chozi likimtoka Mzee Miroshi, Zahoro alielewa namna Baba yake alivyokua akijisikia. Akasogea pembeni na kujiinamia huku akiwa analia chini kwa chini.
Masaa mawili yalipita, mvua iliacha kunyesha. Palikua bado giza, kimya pekee ndicho kilichokua kinaongea. Bundi walianza kulia kila kona ya Kijiji huku hofu na Mashaka vikizidi kusikika.
Familia moja ya Mama, Baba na Mtoto mdogo ilikua imejikunyata ndani ya kijumba chao kidogo cha Nyasi. Palikua kimya kabisa isipokua sauti za Bundi huko nje, sauti hizo zilizidi kuongeza hofu baina yao.
Si Baba, wala Mama aliyepata Ujasiri wa japo kutoa sauti ya aina yoyote ile. Walianza kusikia kishindo huko nje, kisha dakika kadhaa zilipita pakiwa kimya, kisha mlango wao wa Bati ulianza kugongwa kwa utaratibu. Pumzi zao zilizidi kuongezeka huku hofu ikizidi kuwachapa, mgongaji hakusema chochote isipokua kuendelea kugonga
Baba wa hiyo familia ambaye ni Mzee wa makamo, alijikuta akisimama kama Mwanaume kisha taratibu alisogea mlangoni. Mgongaji aliendelea kugonga bila kusema chochote
Yule Mzee hakuweza kuvumilia kukaa kimya, kwa sauti ya upole iliyojaa kitete aliuliza
“Nani?” Baada ya Mzee huyo kuongea, mgongaji aliacha lakini baadae aligonga tena. Ndipo Mzee huyo akauliza tena
“Nani wewe unagonga na hausemi?” Zikapita sekunde kadhaa za Ukimya, Mzee huyo akakata shauri ili arudi alipoiacha familia yake lakini mgongaji aligonga tena. Yule Mzee akahamaki akauliza kwa sauti ya hasira kidogo
“Ni Nani wewe?”
“Mimi ni laana nimekuja kukumaliza” ilisikika sauti nzito ambayo ilimduwaza, akajikuta akiishiwa nguvu. Mara mlango ulifunguka wenyewe kisha mwanga uliingia ndani na kuwaangaza
Kitu cha ajabu kilimwingia yule Mzee kisha aliigeukia Familia yake na kuitazama pale ilipojificha. Mke wake alijawa na hofu sana, aliona wazi kua kuna ufahamu usio wa kawaida ulimwingia Mume wake
Yule Mzee akaingia chumba kingine kisha akatoka akiwa ameshikilia Upanga mkononi, akasimama mbele ya Mke na Mtoto wake akawaambia
“Laana imewafikia” kisha aliunyanyua upanga na kuanza kuwachakata kama kuni bila huruma yoyote ile, ile sauti ya ajabu ilizidi kumwambia kua aimalize familia hiyo. Yule Mzee alihakikisha anawauwa wote wawili, kisha ile sauti ikamwambia
“Hata wewe umelaaniwa, laana imekufikia” alipoambiwa hivi alipiga magoti kisha alianza kujichinja mwenyewe, damu ilikua ikiruka, alianguka na kufa pale pale. Sauti ile ya ajabu ilizunguka nyumba nyingi hapo Kijijini.
****
Siku iliyofuata. Kijiji kizima kilikua kimetulia sana, hakuna aliyefungua mlango na kutoka ndani ya Nyumba yake. Jua lilipochomoza na kukimulika Kijiji chote ndipo walipoanza kufungua Milango taratibu kwa tahadhali ya Hali ya juu sana.
Baada ya muda mchache kupita, watu wengi walikua nje. Ndipo walipokuta vifo vingi sana vya familia moja moja, damu zilikua zimetapakaa kila kona.
Hali ya Kijiji ilijaa simanzi na huzuni sana, pia moshi ulikua ukifuka. Kila mmoja aliogopa, Ndani ya muda mfupi tu zaidi ya Watu 72 walikua wamefariki
Mzee Kova akaitisha mkutano wa Kijiji kizima kujadili hatma ya Kijiji chao cha Nzena.
Wanakijiji wote walikusanyika sehemu ya Mkutano mahali pa wazi, Mzee Kova alisimama kama Mzee wa Kijiji na kuzungumza na Wanakijiji wenzake. Vilio havikukona licha ya Mkutano wa Kijiji kuendelea ili kupata suluhu.
“Nyote mlikua mashahidi miaka iliyopita baada ya kumtoa kafara Masumbuko, Kijiji kilipata neema kwa miaka zaidi ya Kumi, yote haya yanayoendelea hapa Kijijini yametokana na Usiku ule, Bi. Lugumi aliitamka laana kwa kinywa chake kisha alijiuwa kwenye moto. Maneno yake ndiyo yanayo kitafuna Kijiji leo hii. Hali ni mbaya kila kona, mauwaji ya kutisha yanaendelea kutokea.” Alipaza sauti Mzee Kova lakini sauti yake ilizimwa na Mwanakijiji mmoja aliyepaza sauti na kusema
“Ulikua ni ubabe wako wa kutosikiliza wengine, uchawi uliokua ukikitesa Kijiji hiki ulitokana na wewe na wazee wengine. Mlimtoa masumbuko kafara kwasababu ya kuficha uchafu wako, Mimi nimepoteza kila kitu hivyo siogopi tena unaweza ukaniadhibu tu” Sauti ya mwanakijiji huyu ilijaa hisia ya maumivu makali sana, kisha ilifuatiwa na Minong’ono ya Wanakijiji wengine.
“Tulieni, hamuoni kama Tutakosa suluhu?” alipaza sauti Mzee Kisugu, lakini Mama mmoja aliyekua akilia alimjibu
“Hamuwezi kutuzuia kuongea kwasasa, mlijigawia Kijiji chote na kukitawala kwa ukatili na mabavu. Haya ni matokeo ya Uchafu wenu nyie Wazee, mtawajibika” hali ya utulivu ilianza kukosekana, Walinzi kadhaa wa Kijiji walisogea na kumpa msaada Mzee Kova huku Wanakijiji wakipaza sauti zao kua Mzee Kova anapaswa kuwajibishwa
Wakiwa wanaendelea kujibizana, walianza kusikia sauti ya Bi. Lugumi ikisema
“Kufaaaaa‼ kufaaaa‼” kila aliyeisikia sauti hii alianza kutetemeka huku damu nzito ikimtoka puani kisha walikufa papo hapo, hali ya taharuki iliingia na kufanya kila mmoja atawanyike anakokujua yeye mwenyewe. Sauti ya Bibi Lugumi ilizidi kusambaa, ilikua ni sauti ya kunong’ona iliyotoka kwa kuivuta sana.
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TATU Hapa Hapa Kijiweni
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
14 Comments
Your audience, your profits—become an affiliate today! https://shorturl.fm/DrJwQ
Nice
Good job
Mkasa wa kutisha unaosisimua huku tukijifunza Kuwa mwisho wa ubaya mauti
Malipo ni duniani
Hii nzuri sana yaaan sehemu ya 4 tu ndo iko moto hv sipati picha huko mbele
Mambo yazidi kunogaa
Kazi nzuri Sana Admin
Earn passive income on autopilot—become our affiliate! https://shorturl.fm/WVEQI
773dw1
Earn big by sharing our offers—become an affiliate today! https://shorturl.fm/rsKiz
Tap into a new revenue stream—become an affiliate partner! https://shorturl.fm/zYTbj
Next
Start earning instantly—become our affiliate and earn on every sale! https://shorturl.fm/6Zw4r