Ilipoishia Nyumba Juu Kaburi
Tulipishana Mwaka mmoja wa kuingia chuoni, alinitendea wema kila nyakati. Hata wakatiย ambao alipaswa kufurahi alinipa furaha yake na kisha yeye alibakiwa na huzuni yangu.ย Nilimwona akiwa anafunguliwa kutoka juu ya feni akiwa amevalia gauni lake jekundu.ย
Hakika maneno ya yule Bibi yalianza kutimia, nilimpoteza mmoja nimpendaye. Nilijiegemezaย ukutani nikilia kwa kwikwi nikiushuhudia mwili wa Zena ukiondolewa na Askari Polisiย waliokua hapo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa.ย Endelea
SEHEMU YA TATU
Mimi na Caren tulibakia chumbani kwa Zena tukilia, haikua rahisi kuamini kua Zena alikuaย amekufa kikatili sana kwa kujinyonga. Mara simu yangu ilianza kuita kutoka kwenye mkobaย wangu niliokua nimeutupia pembeni, nilishtuka sana. Niliacha kulia nikauvuta mkoba kishaย nikaitoa simu yangu ambayo bado ilikua ikiendelea kuitaย
Moyo ulinipiga โPaaaโผโ nilipoona ni Mama yangu ndiye aliyekua akinipigia. Sikutaka kusikiaย taarifa nyingine mbaya. Niliiacha simu iite hadi ilipo acha kuita, niliirudisha kwenye mkobaย mara moja halafu fikra zangu zikawa nyumbani kwetu.ย
Maneno ya yule Bibi yalikua na nguvu ya kunizunguka kichwani, nilihisi nyumbani kwetuย hapako salama. Niliumia ndani ya moyo wangu huku nikiitupa miguu yangu sakafuni.ย ย
Sikujua ni Nani alikua anafuata baada ya Zena, yule Bibi ni Nani na kwanini haya mauzauzaย yameanza baada ya kuhamia kwenye ile nyumba. Maswali haya yote nilijua ni Nani anapaswaย kuyajibu. Ni yule Mzee wa nyumba jirani, huwenda anafahamu jambo fulani la kutisha kuhusuย nyumba yetu.ย
Nilinyanyuka kutoka sakafuni, nikamtazama Caren aliyekua amelegea kutokana na kukosaย nguvu kwa kile kilichotokea, tulimpoteza rafiki mzuri sana katika mazingira ya kutatanisha.ย Nilimwambia Carenย
โNataka kupata majibu ya haya yote Caren, siwezi kuruhusu hii hali iendeleeโ sauti yangu ilitokaย kwa hisia kali ya maumivu, nilifuta chozi langu. Caren naye alisimama. Tulikua wawili tu ndaniย ya kile chumba cha Zena.ย ย
โUkweli upi, ni kuhusu yule Bibi au kifo cha Zena?โ aliniuliza, nilimtazama kwa sekundeย kadhaa kisha nilimwambiaย
โVyote kwa pamoja, jina la Zena lilikua kwenye ile Barua uliyopewa na yule Bibi wa ajabu.ย Sijui, lakini nahisi kuna shida sehemuโ Umakini wa Caren uliongezeka, akanitazama kwaย shahuku akaniulizaย
โShida Sehemu?โย ย
โNdiyo, baada ya kuhamia kwenye ile nyumba nilianza kupata hisia ya ajabu. Sitaki kuwaambiaย Wazazi wangu kuhusu hilo lakini nahisi kuna Mtu anajua jambo kuhusu ile nyumba, Carenย nisikilize Mimiโ nilisema kisha nilimshika mabega Caren ili nimueleze zaidi. Nilimfanya Carenย kua Mshirika wangu
โKuna Mzee nyumba jirani nina wasiwasi anajua jambo, ile nyumba sio ya kawaida kabisa.ย Sitaki Wazazi wangu wajuwe sababu watachanganikiwa. Tunaweza kuutafuta ukweli?โย nilimuuliza, alinitazama kwa tafakari fupi kisha aliniambiaย ย
โKama hisia zako zinakwambia hivyo Celin, sina chaguoโ nilimkumbatia Caren, angalau nilipataย Mtu anayeweza kunielewa.ย
Nilirudi nyumbani jioni, hofu na mashaka viliendelea kunitafuna hadi nafika nyumbani.ย Niliogopa kukuta Watu wengi pale nyumbani, niliogopa kusikia sauti ya Kilio, niliogopaย kupoteza Mtu mwingine. Nilipofika getini kwetu, nilisimama kidogo huku macho yanguย yakielekea nyumbani kwa yule Mzee.ย
Palikua kimya, hapakua na dalili ya Mtu. Nilijiweka sawa kiakili ili Wazazi wangu wasigundueย lolote, sikutaka wajuwe kuhusu kifo cha Zena wala jambo lolote lile lenye utata. Nilipoingiaย Bustanini niliitazama sana nyumba yetu, nafsi yangu iliniambia kuna jambo lisilo kawaidaย kuihusu hii nyumba lakini sikua na ushahidi wa kuthibitisha hilo.ย
Nilipata amani nilipowakuta Wazazi wangu wakiwa wameketi sebleni wanaangalia taarifa yaย Habari, angalau moyo wangu ulipata kupumzika.ย
Niliwasalimia kisha nilipandisha ngazi nikaelekea chumbani kwangu. Nilisimama kando yaย dirisha nikiitazama nyumba ya yule Mzee, bado ilikua kimya. Palikua na majani mengi sakafuniย kuashiria kua eneo hilo halikufanyiwa usafi kwa muda mrefu.ย
Baada ya kusimama kwa muda kidogo nilirudi na kuketi kitandani nikiwa nakumbuka matukioย ya siku nzima, chozi lilinitoka tena. Kusema ukweli kifo cha Zena kiliniumiza sana, kuna namnaย nilijiona Mimi ni Mkosaji. Basi nilijiegesha kidogo, nikajikuta nikipitiwa na Usingizi.ย
Nilishtuka, bado palikua na giza. Mwili ulikua umechoka sana, hisia ya kua nililala muda mrefuย ilinijia. Nilijinyoosha kidogo kabla ya kuchukua simu na kuangalia saaย
Niliona ilikua ni saa 7:11 Usiku, nilinyanyuka taratibu kutoka kitandani kisha nikasogea paleย dirishani na kuangalia nyumbani kwa yule Mzee. Bado palikua kimya, hapakua na dalili yoyoteย ile, Mbwa walikua wakibweka sana.ย
Nilifungua mlango taratibu kisha kwa mwendo wa kuchoka nilishusha ngazi, taa zilikua tayariย zimezimwa kuashiria kua Wazazi wangu walikua wameshalala, swali pekee nililojiulizaย
โInawezekanaje Wazazi wangu walale bila kuniamsha?โ Sikupata jibu la haraka, nilitembeaย taratibu baada ya kufika sebleni kisha niliwasha taa, kisha nililielekea friji nikachukua maji yaย Baridi na kuyanywa. Angalau niliusikia mwili wangu ukiwa umepoaย
Nilifikiria kuwagongea mlango wazazi wangu lakini niliona nitawasumbua, badala yake niliketiย kwenye sofa. Bado taswira ya kifo cha Zena ilikua ikiendelea kunisakama.
Nikiwa hapo nilianza kuhisi mwili wangu ukisisimka sana kama vile nilikua napandwa naย sisimizi, kichwa kilianza kua kizito huku nikianza kuisikia sauti fulani ya ajabu. Nilisikia sautiย ya kugonga, ilisikika ikigongwa kwa utaratibu sanaย
โMhโผ hii sauti inatokea wapi?โ nilijiuliza, nilisimama taratibu huku sauti ya kochi ikisikikaย wakati nanyanyuka. Niliisikilizia vizuri ile sauti niligundua ilikua ikitokea kwenye chumbaย kimoja pale eneo la chini.ย ย
Chumba hicho tulihifadhia baadhi ya vitu ambavyo hatuvitumii mara kwa mara, mfano wa stooย hivi. Woga ulianza kunijia kisha nilianza kusikia sauti ya Mwanamke akiimba, sikujua alikuaย akiimba nyimbo gani lakini sauti ilikua ikitoka mule mule chumbani.ย ย
Ilikua ni sauti laini inayoimba kwa umaridadi sana, mapigo ya moyo wangu yaliongezeka sana,ย yalikua yakidunda kama ngoma. Hata pumzi ziliongezeka, woga ulinishika sana, mwiliย uliendelea kusisimka kwa kasi huku nikihisi kama nina hali ya kuchanganikiwa. Nilipiga hatuaย za taratibu sana kuelekea nilipoisikia sauti ile, korido ilikua tupu isipokua Mimi pekee.ย
Nilimeza funda zito la mate ili kujipa utulivu ambao kwa hali ilivyo ulihitajika sana, hatua zanguย zilikua za kusuasua sana huku nikitembea kama Mtu nsiye na uhakika wa kufika ninapohitaji.ย Nilizidi kutembea taratibu sana kuuelekea mlango, mara nilisikia sauti nyuma yanguย
โCelin?โ ilikua ni sauti ya Mama yangu aliyeonekana kusimama kwa sekunde kadhaaย akinitazama kwa kunishangaa, uso wake haukuwa na hofu kama wangu, jasho lilikua likinitoka. Kwa mara nyingine tena nilijiapiza kua siwezi kumweleza chochote kile Mama yangu.ย
โMamaaโผโ nilimwita kwa sauti ya mshituko kidogo, sikutegemea angekua akinitazama.ย Mkononi alikua ameshikilia glasi yenye maji ya Baridi. Taratibu alisogea akionesha kuwa alikuaย na maswali ya kuniuliza, aliponifikia aliniulizaย
โKuna nini mbona unaonekana kama ni Mtu unayevizia Usiku huu?โ swali la Mama lilinifanyaย nigundue kuwa alikua hajasikia chochote kile. Ile sauti haikusikika tenaย
โHakuna Mama, sio kituโ nilisema kisha nilitaka kuondoka lakini Mama akanisimamishaย
โKuna jambo unanificha Celin, nakujua nje na ndani, wewe ni Binti yangu ukisema ukweli najuaย na ukisema uwongo vile vile najua. Nieleze, ulikua unavizia nini?โ nilimshika Mama begaย nikamwambiaย
โMama usijali, hakuna jambo lolote lile. Nipo sawaโ nilisema kisha nilipandisha ngazi nikarejeaย chumbani, nilijuwa nyuma yangu Mama alikua na maswali mengi ambayo sikutaka kuendeleaย kuyasikia. Nilipofika Chumbani, haraka nilichukua simu yangu na kumpigia Caren lakiniย hakuipokeaย
Niliitupa simu kitandani, kisha nilisogea dirishani. Niliitazama tena nyumba ya yule Mzee,ย niliamini alikua na majibu mengi ya maswali yangu, nilisimama kwa dakika kama tatu hivi kishaย
nilikata tamaa, nikataka kufunga dirisha lakini ghafla nilihisi kama kuna Mtu amesimamaย dirishani kwenye nyumba ya yule Mzee akinitazama.ย
Nikishtuka sana, nyumba yake ilikua ya kawaida sio ya ghorofa. Dirisha moja lilikua likiwakaย taa, hapo ndipo nilipomwona Mtu akinitazama. Ilionesha wazi kua alikua anajua kua nina tabiaย ya kuichunguza nyumba hiyo, nikajificha kidogo na kuanza kuchunguza kwa siri.ย
Nilishtuka sana, niliyemwona akinitazama alikua ni yule Bibi niliyepanda naye kwenye Treni,ย ndiye aliyenitamkia maneno ya ajabu na ndiye aliyempa Caren bahasha yenye karatasi yenyeย jina la Zena. Kwa namna yoyote ndiye anayehusika na kifo cha Zena, moyo ulilipuka mithiri yaย Volkano nikiwa nimejibanza, niliipa mgongo nyumba ya yule Mzeeย
Mapigo ya moyo wangu yaliongezeka kasi, nilifumba macho ili kuvuta nguvu ya kirejeaย kumtazama tena, nilipopeleka tena macho yangu yule Bibi hakuwepo, isipokua ile taa iliyokuaย ikiwaka kwa mwanga mkali ilikua ikiangaza.ย
Japo nilikua mwoga sana Maishani mwangu lakini nilipata ujasiri wa kutaka kuelewa zaidi,ย nilipata wazo la kwenda kwenye ile nyumba. Usiku ulizidi kuwa mwingi, sikutaka Mtu yeyoteย yule ajuwe kuwa ninatoka. Nilichukua koti langu kisha nikalivaa, nilivuta pumzi nikiwaย nimesimama tayari kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwa yule Mzee.ย ย
Simu yangu ilinidokeza kua ilikua imeshapata saa Nane kasoro za Usiku. Nilijiambia kuwaย liwalo na liwe lakini ni lazima niujuwe mzizi wa yote, nisingeliweza kukubali kupotezaย wapendwa wangu, nilifungua mlango taratibu huku nikiisikia sauti ya Baba yangu akikoroma.ย
Sikua na shaka yoyote kua alikua amelala, hofu yangu ilikua kwa Mama yangu. Nilihakikishaย nakua makini sana, nilizichunga hatua zangu za taratibu hadi nilipofika chini, kisha nilifunguaย mlango ambao ulinitii bila kupiga kelele zozote zile, nilipiga hatua za haraka baada ya kutoka njeย hadi nilipoondoka ndani ya Uzio wa nyumba yetu.ย
Nyumba ya jirani, mbwa alikuwa akiendelea kubweka tena alibweka kwa kasi sana, sauti yaย Bundi ilikua ikiendelea kusikika pia, ulikua ni Usiku mwingi kiasi kwamba hapakua na yeyoteย nje isipokua Mimi na shahuku yangu. Upepo wa hapa na pale ulikua ukiendelea kuvuma taratibu,ย ulifanya hali ya Ubaridi iongezeke.ย
Nilipofika nje kabisa, niliitazama nyumba yetu. Akili na nafsi yangu viliniambia haikua nyumbaย ya kawaida, basi nilishupaza shingo yangu kuelekea nyumbani kwa yule Mzee, nilikua naย uhakika wa kupata Majibu ya maswali yangu usiku huu. Taratibu niliendelea kupiga hatuaย
Nilipofika mbele ya nyumba ya yule Mzee nilisimama kwanza huku nikijiuliza mara mbili mbiliย kama nilikua tayari kufanya nilichokua nataka kukifanya. Nilijiambia ndani yangu kwa sautiย isiyo na mawimbi ya njeย
โNi lazima niwe jasiri, vinginevyo naweza kupoteza kila nikipendachoโ ilikua ni sauti iliyojaaย ujasiri mwingi ndani yangu. Macho yangu yaliendelea kuitazama ile nyumba kisha nilisukumaย
geti, halikua geti kubwa, geti dogo lililozungushiwa na uzio wa Miti fulani yenye miiba ndogoย ndogoย
Urefu wa geti iliishia kifuani pangu, nilipolisukuma nilipokelewa na sauti ya Bawaba za geti hiloย ambazo zilipiga kelele fulani ya maumivu ya kufunguliwa mithiri ya nyumba isiyo kaliwa naย yeyote yule. Sauti hii ilinipa maswali mengi, nilichukua simu na kuwasha tochi nione kama hisiaย zangu zilikua sahihi.ย ย
Macho yangu yalishuhudia kile ambacho nafsi yangu iliniambia, geti lilizungukwa na kutu,ย Bawaba zilifichwa na kutu. Hapana shaka geti hili halikufunguliwa kwa muda mrefu, sasaย nilijiuliza nikiwa nimesimama pale pale getini.ย
โInawezekanaje? Ina maana walio ndani wanapitia wapi kama geti hili halifunguliwi?โ Lilikuaย swali la kwanza la Msingi, bado nilikua njia panda. Sikutaka kurudi nyuma, niliazimia ni lazimaย niichunguze nyumba pamoja na wanaoishi ndani ya hii nyumba.ย ย
Nilipiga hatua za kunyata, nikafanikiwa kufika mlango mkubwa wa kuingilia ndani ya nyumbaย hii. Nilipofika hapa niliwaza kidogo, jibu nililolipata ni kulielekea dirisha lile ambalo nilimwonaย yule Bibi wa ajabu, basi taratibu nilianza kutembea kwa mwendo wa kunyata hadi nilipolifikiaย dirisha.ย
Bado palikua panawaka taa, taratibu nilianza kuchungulia ndani, sikumwona yeyote yule lakiniย mazingira yote yaliniambia kua ndani ya nyumba palikua na Mtu au Watu kama ambavyoย nilimwona yule Bibi nikiwa chumbani kwangu.ย
Nilisimama hapo kwa dakika kadhaa, palikua kimya sana. Bado upepo wa taratibu ulikuaย ukiendelea, nilipata wazo la kuuelekea mlango hivyo nilirudi hadi mlangoni. Nilisimama kwaย sekunde kadhaa, kisha nilijaribu kutekenya kitasa cha mlangoย
Cha ajabu, Mlango ulifunguka kirahisi sana. Baada ya kufungua mlango niliweza kuangaza kwaย ndani ya nyumba hiyo, nilikutana na sebule inayowaka taa kali, palikua na Kochi moja jekunduย lililo chakaa sana, niliona sahani juu ya meza, nilimuona paka akiwa ameketi kando ya meza.ย
Paka huyo alikua ametulizana sana, alikua akinitazama kwa macho yake makali ya kungโaa.ย Uwepo wa Paka ilikua ni ishara nyingine kua nyumba hii inakaliwa na Mtu, paka hawezi ishiย mahali ambapo hakuna chakula. Nilishusha pumzi zangu huku moyo ukiendelea kunigonga sana.ย
Bado kichwa changu kiliendelea kugonga kwa maswali yasiyo na majibu ya Uhakika, wazo laย kuingia ndani ya nyumba hiyo lilinijia, moyo haukuacha kudunda kwa nguvu, kijashoย chembamba kilikua kinanitoka, nilipoanza kupiga hatua niliingiwa na Ubaridi, kwa nguvu sanaย nilivutwa nje na kuzibwa mdomo wangu kisha nikasogezwa pembeni, nikafichwa nyuma ya Uaย moja.ย
Hata nilipojaribu kufurukuta sikuweza kisha nikaisikia sauti ya Caren
โShiiโผ ni Mimiโ aliongea kwa sauti ya kunongโoneza. Aliniachia, hapo hapo kabla sijamuulizaย alifikaje, sote tulimwona Yule Mzee akiwa ameshikilia tochi, alikua akichungulia pale mlangoniย nilipotaka kuingilia, kwa namna nilivyomwona ni kama alihisi uwepo wa Mtu. Alimulika tochi huku na kule lakini hakufanikiwa kutuona kisha aliufunga mlango wa Nyumba yake.ย
Hapo tuliachia pumzi ndefu maana tulikua tumezibana kuhofia asije akatushtukia.ย
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TATUย
COMMENTS ZIWE NYINGI SASAย
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx




39 Comments
Firee๐ฅ
Ni nzur saana
Very good https://lc.cx/xjXBQT
It is so very good and attractive
Nasoma naogopa mwenyewe
Dah n ๐ฅ
๐๐๐
Hakika ipo vyema ๐ค
Hakika ipo vyema ๐ค
Hii ni motoo
Alooooooo mambo ni๐ฅ๐ฅ๐ฅ kaka mkubwaaa
KAKA MKUBWA EEEEE…
TUANDALIE NA STORY ZA UJASUSI๐๐ฝโโ๏ธ๐๐ฝโโ๏ธ๐ฅท๐ฝ๐ฅท๐ฝ๐ฅท๐ฝNAZIKUBARI MNOOOO NA NAZITAMANI SANAAAAA๐ช๐ฝ๐ช๐ฝ๐ช๐ฝ๐ช๐ฝ๐๐ฝ๐๐ฝ๐๐ฝ๐๐ฝ๐๐ฝ
Nzurii jmn lkn inanitishaaaaa mpk watu tunamalizaaa bando
Awesome https://lc.cx/xjXBQT
Very good https://short-url.org/10VGf
Duh๐ฅ๐ฅ
Nzuri sana
.
๐ฏ
ase ni balaa๐ฏ
Usiku wa manane huo Caren katokea wapi, kajuaje kama Celin yupo kwenye nyumba jirani ?
Hii ya moto kwelikweli.
Good https://t.ly/tndaA
Jmn woiiiiii ya mot san
Twende kazii master
Good https://t.ly/tndaA
Type muendelezo
Awesome https://t.ly/tndaA
I’m very pleased to discover this website. I want to to thank you
for your time just for this wonderful read!! I definitely appreciated every little bit
of it and i also have you bookmarked to check out new stuff on your site.
Good https://rb.gy/4gq2o4
Iko poa xnaa
Write more, thats all I have to say. Literally, it seems as though you relied on the video to make your point.
You clearly know what youre talking about, why waste your intelligence on just posting videos to your site when you could be giving us something
informative to read?
http://w1.paitowarnasgp.cfd/
Hmm is anyone else having problems with the pictures on this blog loading?
I’m trying to determine if its a problem on my end or if
it’s the blog. Any responses would be greatly appreciated.
http://w2.prediksijitutogel.xyz/
https://t.me/s/TgGo1WIN/21
ะัะธัะธะฐะปัะฝัะน Telegram ะบะฐะฝะฐะป 1win Casinะพ. ะะฐะทะธะฝo ะธ ััะฐะฒะบะธ ะพั 1ะฒะธะฝ. ะคัะธัะฟะธะฝั, ะฐะบััะฐะปัะฝะพะต ะทะตัะบะฐะปะพ ะพัะธัะธะฐะปัะฝะพะณะพ ัะฐะนัะฐ 1 win. ะ ะตะณะธัััะธััะนัั ะฒ ะฒะฐะฝ ะฒะธะฝ, ัะพะฒะตััะธ ะฒั ะพะด ะฒ ะพะดะธะฝ ะฒะธะฝ, ะฟะพะปััะฐะน ะฑะพะฝัั ะธัะฟะพะปัะทัั ะฟัะพะผะพะบะพะด ะธ ะฝะฐัะฝะธัะต ะธะณัะฐัั ะฝะฐ ัะตะฐะปัะฝัะต ะดะตะฝัะณะธ.
https://t.me/s/Official_1win_kanal/3651
sd7iy8
xy9m1t
3xj9a0
Hello pals!
I came across a 149 very cool resource that I think you should take a look at.
This tool is packed with a lot of useful information that you might find insightful.
It has everything you could possibly need, so be sure to give it a visit!
[url=https://www.pandaancha.mx/noticias/que-hacer-solicitar-retiro-casino-en-linea.html]https://www.pandaancha.mx/noticias/que-hacer-solicitar-retiro-casino-en-linea.html[/url]
Furthermore remember not to overlook, everyone, โ one always are able to within this particular piece discover responses to your the very confusing questions. We tried to explain the complete data in the most very easy-to-grasp method.
Hello pals!
I came across a 149 fantastic page that I think you should check out.
This site is packed with a lot of useful information that you might find valuable.
It has everything you could possibly need, so be sure to give it a visit!
[url=https://www.hockey-live.sk/news/2344-na-co-sa-zamerat-pri-stavkach-na-hokej]https://www.hockey-live.sk/news/2344-na-co-sa-zamerat-pri-stavkach-na-hokej[/url]
And remember not to forget, folks, which one always may within this piece find solutions for the the absolute complicated queries. Our team made an effort โ lay out the complete content using the extremely accessible method.