Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-09

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-08

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-07

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Sita-06)
    Hadithi

    Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Sita-06)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaApril 30, 2025Updated:April 30, 202521 Comments13 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi 05

    Taratibu nilitembea kuelekea mbele ya gari kumsikiliza yule Mwanaume, alikua mnene kiasi naย  pia alikua na ndevu nyingi mfupi wa wastani, alikua ananukia manukato makali sana. Nilitembeaย  taratibu huku nikijikwaa jiwe dogo lililonipa mwendo zaidi hadi nilisogea kabisa karibu yake,ย  akanipa pole huku akigeuka na kunitazama nikitembea taratibu hadi nilipofika mbele yake.ย 

    โ€œUsiwe na wasiwasi Celin, usiogope sababu nusura ya Maisha yenu yapo mikononi mwakoโ€ niliyafinya macho yangu kwa mshangao mkubwa sana, moyo ulilipuka ghafla na kuanza kwendaย  mbioย 

    โ€œUnamaanisha nini?โ€ nilimuuliza nikiwa na mhemko wa alichoniambia, tayari nilikuaย  nimepoteza marafiki zangu wawili.ย  Endelea

    SEHEMU YA SITA

    โ€œNinachomaanisha ni hiki, Sisi tulizaliwa wawili tu. Mimi pamoja na Dada yangu Sabra, Babaย  yetu alikua tajiri sana. Mama yetu alifariki muda mrefu, Baba yetu hakutaka kuowa kabisa.ย  Alitulea kwa mikono yake hadi tulipokua wakubwaโ€ alisema huku nikimwona kama Mtuย  anayekaribia kulia. Nilimeza mate huku nikiwa na shahuku kubwa ya kusikia alichokusudiaย  kukisema. Kisha aliendeleaย 

    โ€œPesa hugeuza Dunia juu chini, Usiku mmoja. Kaka yake Baba yetu alimuuwa Baba yetuย  akimtuhumu kujilimbikizia mali ambazo alirithi kutoka kwa Baba yao. Usiku ule bado unaishiย  ndani yangu, Mimi na Dada yangu Sabra tulishuhudia ukatili ule. Baba mkubwa akaagizaย  tusakwe mle ndani tuuawe, tulikimbilia chumba cha chini ambacho mara zote Baba alisema kuaย 

    kama itatokea shida basi tukimbilie humo kujificha, wakati huo Mimi nilikua na Miaka 11 naย  Sabra alikua na Miaka 15.โ€ Alipofika hapa alijiinamia, alikua akilia. Nilitamani kumshika naย  kumtuliza lakini alikua Mtu mgeni kwangu istoshe nilikua nikimwogopa. Niliishia kumtazama tuย  hata neno la kuongea sikuwa nalo.ย 

    Aliinua kichwa chake kunitazama, nusura nikimbie. Alikua na macho meupe yasiyo na kiini.ย ย 

    โ€œUsikimbie, huu ndiyo ukweli pekee unaoweza kunusuru Maisha yenu Celinโ€ alisema, niliitikiaย  kwa kutumia kichwa lakini moyoni nilikua nimejawa na hofu sana, miguu yangu ilitamaniย  kukimbia kuliko kusimama mbele ya yule Mwanaume.ย 

    โ€œJitihada zetu hazifukua dafu, walitukamata. Walituambia tupige magoti, tulifanya hivyo kishaย  Baba yetu Mkubwa alifika kule chini kisha alituambia hakukusudia kutudhuru sisi isipokuaย  tulishuhudia kifo cha Baba yetu. Aliamuru wale watu watuuwe, walichinja shingo zetu naย  kumaliza Uhai wetu kule chiniโ€ niliachama, hewa ya ghafla iliingia kwa mshangao mkubwa, inaย  maana nilikua nazungumza na Mfu? Nilijiuliza ndani yangu lakini cha ajabu alinijibu kama vileย  nilizungumza kwa sautiย 

    โ€œNdiyo, Mimi ni mfu. Msaada wangu ni wewe Celin. Walituzika kule kule chini kisha waliuzibaย  mlango wa kuelekea kule chini, sijui kuhusu Baba yetu alienda kutupwa wapi. Lakini kule chiniย  tulizikwa Mimi na Dada yangu Sabra. Nasfi zetu zimeishi kwenye ile nyumba kwa miaka mingi,ย ย 

    kila aliyeamia kwenye ile nyumba alikutana na mikasa ya ajabu kila uchwao, wengiย  walikimbia.โ€ย ย 

    โ€œHakuna aliyepata ujasiri wa kufwatilia chochote kile. Nafsi zetu ziliwasumbua sana, ndipo Babaย  Mkubwa alipotafuta Mganga kwa ajili ya kuizindika ile nyumba lakini hata zindiko lakeย  halifukufanya kazi isipokua lilitengeneza jini ambalo wewe umekutana nalo mara kadhaa. Jiniย  mzee aliyeishi kwenye ile nyumba na kuzidi kuuwa Watu, hata Baba Mkubwa aliuawa na lileย  jini, ni jini hatari sana ambalo linaondoa Kila anayeishi ndani ya ile nyumba. Awali Babaย  mkubwa aliishi mule lakini aliikimbia nyumba mwenyewe kutokana na mauza uza, aliiachaย  nyumba yenyeweโ€ย 

    โ€œKatika harakati za kupambana na lile jini nilijikuta nikiondoka kwenye kaburi na sijui nawezaย  vipi kurudi tena ndani ya ile nyumba. Ujasiri wako, udadisi wako ulinivutia sana Celin, naombaย  unisaidie jamboโ€ alisema, hadi kufikia hapo nilikua na simulizi halisi ya ile nyumba ambayoย  niliitilia sana shaka tokea mwanzo.ย ย 

    โ€œNitasaidia nini, siwezi kupambana na vitu kama hivyo. Sina hiyo nguvu Mimiโ€ nilisema,ย  alinitazama kisha akaniulizaย 

    โ€œUnajua wazazi wako wanapitia nini ndani ya ile nyumba? Usije ukawapoteza kirahisi hivyoย  Celin, Baba na Mama yako wanahitaji msaada na msaada pekee ni wewe kuitoa nafsi ya Dadaย  yangu, ikiwa huru tunaweza kupambana na jini linalouwa kila anayeifahamu siri ya ile nyumba.ย  Jini hilo ni Bibi Mzee, ameuwa kila Mtu anayehoji kuhusu nyumba ile, nimekuokoa padogo sanaย 

    lakini bado atakuwinda akumalizeโ€ chozi lilianza kunibubujika, sikuwaamini Wazazi wanguย  lakini niligundua walikua hawana hatia, pengine hilo jini ndilo linalowatumikisha.ย 

    โ€œUsilie Celin, nitakupa njia ya nini ufanye unapofika ndani ya chumba ambacho huwa unamsikiaย  Mwanamke akiimba au kulia, huyo ni Dada yangu Sabra. Amekuwa Mtumwa wa huyo jini katiliย  aliyepandikizwa na Baba Mkubwaโ€ Alisema, nilijaza hewa kifua changu maana niliyoyasikiaย  yalikua ni mambo ya kutisha sana.ย 

    Ilikua ni kama nasoma kitabu cha Riwaya ya kutisha kilichoandikwa kwa mtiririko wa ajabuย  sana, mishipa ya kichwa ilinisimama. Nguvu zilikua zikiniondoka taratibu huku nikihema juuย  juu, alichokisema ndicho nilichokua nikikitafuta kukisikia lakini baada ya kukisikia nilitamaniย  nisingelisikia kabisa.ย 

    Hadithi ya kuogofya iliyoondoa wapendwa wangu pamoja na Dalali aliyetutafutia nyumba.ย  Haikua rahisi kuelewa, sikuacha kumtazama yule Mwanaume ambaye kwa mujibu wa hadithiย  yake ni Mtu aliyekufa muda mrefu, ni nafsi inayohangaika kumtafuta Dada yake aliyezikwaย  chini ya nyumba yetu tuliyoinunua. Sikutaka kujua nyumba ipo chini ya naniย ย 

    Kila nilichokisikia kuhusu nyumba yetu kilinipa uhakika wa kile alichoongea, kuhusuย  Mwanamke anayeimba na kulia hilo ni jambo dhahiri sana. Nilipata kujua kuhusu jini Mzeeย  anayeishi ndani ya nyumba yetu na kufanya Mauwaji.ย ย 

    โ€œKuna Mzee nyumba jirani, unamfahamu?โ€ nilimuuliza.ย 

    โ€œNdiyoโ€ผ Unachokiona ni fikra zako na jinsi ambavyo jini yule mbaya anataka uone. Hakunaย  uhalisia kwani Mzee yule alifariki Miaka mingi, nyumba yake iko tupu, inakaliwa na huyu jiniย  ambaye ndiye aliyemuuwa huyo Mzeeโ€ nilipepesa macho yangu, kila kitu kilikuwa kipyaย  masikioni mwangu.ย 

    Chozi lilinitoka, alinipa nafasi ya kumuuliza nisichokijua. Alikua akinitazama huku akisubiriaย  swali langu.ย 

    โ€œKuhusu wazazi wangu?โ€ japo sikutaka kusikia sana kuhusu Wazazi wangu, nilihisi ingeniumizaย  sana. Yule Mwanaume alinitazama akaniambiaย 

    โ€œNi watumwa, unapaswa kuwakomboa kabla hawajatoweka. Kwakua ameshajua wewe unajuaย  kuhusu siri ya ile nyumba unaweza ukawa na muda mchache sana wa kuwasaidia.โ€ Alisema,ย  nilizidi kuumia ndani ya nafsi yangu. Baba yangu aliniumiza zaidi sababu alitumia pesa zake zaย  kustaafu kununua nyumba ya ndoto zake lakini nyumba hiyo ndiyo chanzo cha Matatizo yote.ย ย 

    โ€œCelinโ€ aliniita na kuniondoa kwenye fikra za kuogofya. Nilimtazama, nilimwona kamaย  Mkombozi wangu ambaye anaweza kuyarudisha Maisha yangu ya furaha ya huko nyuma.ย 

    โ€œAbee!โ€ niliitika kwa utuo, chozi lilikua likinibubujika tu.

    โ€œKulia hakuwezi kuokoa Wazazi wako na wapendwa wengine. Vaa Ujasiri, ukiweza kumalizaย  hili nitakupa shukuraniโ€ alisema, niliyatafakari maneno yake. Ni kweli nilihitaji kuuvaa Ujasiriย  wa hali ya juu sana lakini haiwezi kuondoa huzuni iliyojaa ndani yangu. Niliitikia kwa kutumiaย  kichwa kisha akaniambiaย 

    โ€œNitakua nawe bega kwa bega hadi mwisho, ikiwa utashindwa nitashindwa pia, ukishindaย  nitashinda na weweโ€ kisha aliingiza mkono mfukoni na kunipatia ushanga mwembambaย  uliotungwa vizuri.ย ย 

    โ€œNipe mkono wa kuliaโ€ kisha alimalizia na ishara ya Kichwa huku akinyoosha Mkono kuuombaย  mkono wangu, alionesha kuhitaji kunivisha ule Ushanga wenye rangi nyeupe. Japo bado nilikuaย  namwogopa lakini nilimpatia mkono wangu. Halafu akanifunga ule Ushanga mkononi kamaย  kembe hivi.ย 

    โ€œHuo ndiyo Ulinzi wako Celin. Rudi nyumbani ishi kama kawaida lakini nitakua nawasilianaย  nawe mara kwa mara kukwambia nini cha kufanyaโ€ alisema huku nikiwa nautazama uleย  ushanga, nilipoinua kichwa changu sikumwona tena yule Mwanaume hata lile gari halikuwepoย  tena. Nilijikuta mwenyewe msituniย 

    Nilianza kuhangaika kutafuta pa kutokea, niliongoza ile barabara tuliyokuja nayo, nilikuaย  ninahema huku nikiwa nina hofu sana. Nilianza kukimbia, nilipojikwaa nilinyanyuka hadiย  nilipofika Barabara kuu iliyokua ikielekea Mjini.ย 

    Nilipunga Mkono wangu kuomba msaada, hatimaye nilipata msaada wa โ€˜liftiโ€™. Gari moja ndogoย  iliyobeba wanafamilia ilinisaidia hadi nikafika Mjini. Niliwashukuru kwa msaada wao,ย  nilitazama juu palikua na jua kali, saa yangu iliniambia kua ni saa sita Mchana. Niliufunguaย  mkoba wangu, nikaitoa simu na kumpigia Mama yangu. Niliposikia sauti yake nilishusha pumziย  zangu maana aliniambia wapo salama, nami nilimwambia kua ndiyo nimetoka chuoni narudiย  nyumbani.ย 

    Nilielekea kituo cha treni, kisha nilipanda treni hadi mitaa ya nyumbani, nikatembea kidogo hadiย  nilipofika nyumbani, nilisimama getini nikiiangalia nyumba yetu. Chanzo cha yote ni hiyoย  nyumba. Ilikua ni nyumba nzuri iliyojaa utulivu kwa nje lakini ndani ilikua na vibweka vyaย  kutisha, masikio yangu yalianza kupiga kelele mithiri ya filimbi za sungusungu.ย 

    Sikujua ilikua ni ishara gani, sijui ni kitu gani kilinifanya niangalia pembeni ule upande waย  nyumba ya yule Mzee, nilimwona yule Mzee akiwa amesimama akinitazama bila hata kupepesaย  macho. Sasa nilikua na siri ya huyu Mzee kua si Mtu halisi bali ni mzimu wa Mzee aliyeuawa naย  yule Jini Mzee.ย 

    Alikua kimya sana, akinitazama bila kupepesa macho yake. Ghafla akatoweka katika mazingiraย  tata, nilishtuka sana nusura nizimie. Hayakua mambo ya kawaida, nilizoea kuyatazama kwenyeย  filamu na tamthilia za kizungu. Kisha nilisikia geti likitoa sauti ya maumivu ya Bawaba kamaย 

    vile lilikua likisukumwa na Upepo hivi. Ile sauti ilikua ndiyo sauti pekee iliyotawala masikioย  yangu.ย 

    Niliingiwa na shahuku na kusogea, bado masikio yalikua yakipiga kelele sana. Nilianza kupigaย  hatua za taratibu kuelekea nyumbani kwa yule Mzee ili nione geti hilo lilikua likipiga keleleย  kwasababu ya upepo gani wakati palikua tulivu sana, nikakumbuka siku ile niliona geti hiloย  likiwa limejaa kutu, inawezekana vipi likapiga kelele hivyo?ย 

    Nilijiuliza nikiwa ninazidi kupiga hatua za kuhesabu, moja mbili, moja mbili nikiwa nazidiย  kutembea mwili nao ulikua ukisisimka sana kuashiria nilikua naikaribia hatari. Katika hali isiyoย  ya kawaida kabla hata sijafika getini, nilikua ubavuni naelekea nikaona kitambaa kikipepea paleย  getini, hakikua kitambaa kidogo kilikua kikubwa na jinsi macho yangu yalivyoniambia nilionaย  gauni jeupe, ilikua ni ishara kua palikua na Mtu aliyejibanza getini ili anishambulie.ย 

    Nilisimama, ghafla nilianza kusikia sauti ya ajabu iliyojaa ushawishi sana. Sauti hiyo ilikua niย  sauti ya kizee ikiniambiaย 

    โ€œCelin, njoooooโ€ผ njoo Binti, unakaribiaโ€ ni sauti ya taratibu sana iliyotoka kwa kunongโ€™oneza,ย  sauti hiyo ilikua ikisikika kila sehemu, ilikua inazidi kunivuta katika hali ya ajabu sana nizidiย  kuelekea getini. Vitu viwili vilitokea, mwili wangu ulikua unakataa lakini akili ilikua inatakaย  kwenda, niliharibiwa kisaikolojia nikajikuta nikijivuta kusogea.ย 

    Namna nilivyoyaona mazingira ilikua kama vile nipo Dunia ya peke yangu, isiyo na Mtuย  mwingine. Niliona giza la ajabu na mwanga hafifu, kipande cha gauni kiliendelea kupepea. Sautiย  ya yule Bibi Kizee jini iliendelea kuniangamiza kisaikolojia, jasho lilikua likinitoka. Nilikuaย  naendelea kupiga hatua za mvutano, kumbe wakati yote yanaendelea Mama yangu alikuaย  ghorofani akinitazama kwa Mshangao.ย 

    Nilikua namsikia akiniita lakini nguvu ya ile sauti ya yule Bibi ilinizidia kiasi kwamba nilitamaniย  kupaza sauti kumwambia Mama kua anisaidie lakini nilishindwa, hata kugeuka kumtazamaย  Mama kilikua kipengeleze kizito sana. Shingo yangu ilikaza ikitazama mbele, udenda ulikuaย  ukinitoka.ย 

    Hakika huyu Jini alikua na nguvu za ajabu sana. Alikua akiniita huku akicheka kanakwambaย  alikua na uhakika kua ameniweza, nilijitahidi sana kupambana na nafsi yangu lakini sauti yakeย  ilikua na nguvu ya ajabu sana.ย ย 

    Nilisogea karibu kabisa na geti, hatua moja ndiyo iliyobakia kufika alipo yule jini, gauni lakeย  lilikua likipepea huku sauti yake ikizidi kuwa karibu zaidi. Niliweka mikono yangu masikioni,ย  nilijua nateswa na ile sauti lakini sikua na nguvu ya kupambana nayo.ย 

    Nilikua natetemeka, nilijaribu kujizuia kwa nguvu lakini nilikua sina hiyo nguvu zaidi yaย  kunyanyua mguu ili nifike alipo yule Jini. Ghafla nilishikwa na kuvutwa nyuma, fahamuย  zilinirudia, hali ya hewa ilitulia, sauti ilikatika sikuisikia tena.ย 

    Mbele yangu alikua amesimama Mama pamoja na Baba yangu, macho yalinitoka pima kamaย  fundi cherahani anayetungisha uzi kwenye zindano, udenda ulikua ukinitoka nikawahi harakaย  kuufuta lakini tayari Baba na Mama walikua wameshaniona katika hali ile ya uzezeta.ย 

    Walikua kimya wakiniangalia nilivyokua najihangaisha kujiweka sawa kanakwamba kila kituย  kilikua vizuri. Mama aliniambiaย 

    โ€œTumeona kila kitu, unajaribu kuficha nini?โ€ sauti ya Mama yangu ilinisuta, alizungumza kamaย  Mama aliyegundua Uwongo wa Binti yake, macho ya Baba yangu yalikua kwangu piaย  akiniangalia kwa mshangao pia.ย 

    Niliinamia chini, aibu ilikua imenishika vibaya sana. Baba akaniulizaย 

    โ€œMkononi umevaa nini Celin?โ€ macho yangu nikayapeleka mkononi, nikagundua alikuaย  akiuongelea ule Ushanga niliopewa kama Ulinzi na yule Mwanaume nisiyemjua jina.ย 

    Nilimtazama Baba kisha Mama, halafu nikasema โ€œNi urembo tu huu Babaโ€ sauti yangu naย  matendo yangu yaliwaambia uhalisia wangu kua kuna jambo nalificha. Haikuishia hapo, Mamaย  alienda mbali zaidi akasemaย 

    โ€œHii siyo mara ya kwanza nakuona unanyata kuelekea kwenye nyumba jirani, Celin unafichaย  nini ambacho huwezi kuzungumza na Sisi? Umepoteza marafiki wawili kwa mpigo, kuna niniย  kinachoendelea?โ€ Maswali ya Mama yangu yalikua kama Mshale ulionichoma kooni,ย  nilikaukwa mate na maneno ya kujibu.ย ย 

    Niliishia kuwatazama, mara radi zilisikika. Wingu zito hata lilikotokea hakuna aliyejua, papoย  hapo mvua ilianza kunyesha, hakuna aliyetaka kuikimbia mvua. Sote tulisimama tukitazamana,ย  Wazazi wangu walihitaji majibu kutoka kwangu.ย 

    โ€œMama, tutaongea ndani mvua inazidi kua kubwaโ€ nilisema kisha nilikimbilia ndani nikiwaachaย  wazazi wangu wakiwa wamesimama. Nilipanda ghorofani hadi chumbani kwangu, niliwatazamaย  Wazazi wangu pale nilipowaacha lakini sikuwaona, nikahisi huwenda nao wamekimbilia ndani.ย 

    Niliiangalia nyumba jirani, kichwani nilikua na majibu kua nyumba ile ilikua ikikaliwa na yuleย  jini Muuwaji. Cha kushangaza niliwaona wazazi wangu wakiwa wamesimama getini, ni kamaย  vile walihitaji kujua nilikua nafuatilia kitu gani, moyo ulinilipuka mithiri ya Volkano kali yaย  moto.ย 

    Mvua ilikua ikiwapiga, kibaya zaidi mbele yao alikua amesimama Yule Bibi Kizee akiwaย  amevalia gauni jeupe akiwaita Wazazi wangu kwa kutumia mkono wa kushoto huku akirudiย  nyuma nyuma. Kilichowakuta Wazazi wangu ndicho kilichokua kinanivuta na Mimi,ย  niliwashuhudia Wazazi wangu wakiwa kama mazombi.ย 

    Hawajitambui, walikua wakilifungua lile geti huku macho yao yakiwa kwa yule Bibi Kizee, tenaย  walikua na haraka sana wamfikie. Walikua wakiielekea hatari ile ile ambayo wao waliniokoaย 

    nayo, sasa ulikua ni wajibu wangu kuwasaidia. Haraka nilifungua mlango na kuanza kushushaย  ngazi niwawahi wazazi wangu wasiingie mikononi mwa yule Bibi kizeeย 

    Niliteremka ngazi haraka haraka hadi nikafika chini, moja kwa moja nikakimbilia getini,ย  nikalifungua geti haraka Halafu nikakimbilia getini kwa yule Mzee. Nilipofika niliwaona Wazaziย  wangu wakiwa wamesimama nyuma ya yule Bibi Kizee Muuwaji. Walikua wameinamishaย  shingo zao, mvua bado ilikua ikinyesha, geti lilikua wazi.ย 

    Walikua wakitazama chini, yule Bibi alikua akinitazama halafu aliangusha kicheko kikubwa.ย  Alikua na sauti mbaya mithiri ya radi, ghafla alianza kutokwa na kucha ndefu, sura yake ilikuaย  ndefu, nywele ndefu zilizo dhohofika, macho yake yalikua mekundu, meno yalichomoka.ย 

    Alikua na sura mbaya ambayo ilitosha kuniambia kua ni kweli ndiye Jini Muuwaji. Alikua kamaย  amewateka Wazazi wangu kifikra. Nilianza kuogopa, alikua akinisogelea taratibuย 

    Nilikua nikihema, Wazazi wangu walikua wamesimama vile vile kama Watu wasiojitambua.ย  Yule Bibi aliendelea kunisogelea huku mguu wake mmoja akiwa anauburuza. Ulikua kama unaย  dosari ya ukilema hivi, nilikua kwenye butwaa ambayo ilihitaji Mtu anitingishe ndiyo nitokeย  katika ile hali tata.ย 

    Fumba na kufumbua Macho yule Bibi Kizee alikua amejaa machoni pangu akinimulika naย  macho yake makali, nilishtuka na kutoka katika ile hali ya Butwaa. Nilipohitaji kukimbiaย  alinishika mkono na kunivuta kwake lakini alipigwa na shoti kali, niliona moto mkaliย  uliomsukuma na kumtupa chini.ย 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya SABA

    COMMENTS ZIWE NYINGI SASAย 

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย 

    Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx

    riwaya mpya Riwaya Nyumba Ya Majini Kijiweni Riwaya ya Fungate Riwaya Ya Kisasi Changu riwaya za kusoma mtandaoni

    21 Comments

    1. Mtubaki on April 30, 2025 8:00 pm

      Admin wa kwanza apa ntagi mm sehemu inayofuata ๐Ÿ˜nzur sana nmeipenda

      Reply
    2. Gilbert2464 on April 30, 2025 8:32 pm

      Awesome https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    3. Yuster on April 30, 2025 9:22 pm

      Familia ya Celin ina kumbwa na majanga

      Reply
    4. Giovanni4490 on April 30, 2025 10:10 pm

      Very good https://is.gd/N1ikS2

      Reply
      • Hamisi halidi on May 1, 2025 10:24 am

        Aha kwel balaha

        Reply
    5. Laila2163 on April 30, 2025 10:32 pm

      Good https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    6. Dawn469 on April 30, 2025 11:41 pm

      Awesome https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    7. Piana on April 30, 2025 11:56 pm

      ๐Ÿ‘Œ๐Ÿ‘Œ๐Ÿ‘Œ

      Reply
    8. Cooper3193 on May 1, 2025 12:32 am

      Awesome https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    9. Shedrack on May 1, 2025 12:41 am

      Dah๐Ÿ˜ฎ admin endelea7๏ธโƒฃ

      Reply
    10. Kson on May 1, 2025 1:44 am

      Admin ya 7 admin

      Reply
    11. Claudia2418 on May 1, 2025 5:18 am

      Good https://is.gd/N1ikS2

      Reply
    12. Bitidhan on May 1, 2025 6:44 am

      Nzuri sanaa jmn

      Reply
    13. Alhaji Kising'a on May 1, 2025 7:52 am

      safi

      Reply
    14. Marco on May 1, 2025 8:54 am

      Daaah hii ni Kali next please ๐Ÿ™๐Ÿ™ 7

      Reply
    15. Sumaiya on May 1, 2025 9:23 am

      Episode ya 7 jamn

      Reply
    16. Aura on May 1, 2025 10:54 am

      ๐Ÿ˜“๐Ÿ˜“๐Ÿ˜“๐Ÿ˜“๐Ÿคฆโ˜น๏ธ

      Reply
    17. Hamisi halidi on May 1, 2025 7:11 pm

      Duh kaz ipo

      Reply
    18. Cathbert on May 2, 2025 3:59 pm

      Mzuri

      Reply
    19. Sir on May 3, 2025 5:04 am

      Good

      Reply
    20. Juma mfamao on May 7, 2025 12:36 pm

      Kijiweni

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi July 23, 2025

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-09

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya nane โ€œNakufahamu Zahoro, wewe ndiye jibu la Laana hii.…

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-08

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-07

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-06

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.