Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi
Caren alisimama baada ya kuniona simjibu alichokua akinisemesha, nilianza kuhema kwa kasi,ย hofu ilikua imenitawala vya kutosha.ย
โKuna nini Celin?โ aliniuliza, nilimjibu Caren kwa sauti ya chini iliyojaa hofu na mtetemo waย Uwoga uliopitiliza.ย
โKuna Mtu nyuma yetuโ Nilitamani kulia kwa jinsi woga ulivyokua umenishika, Caren aligeukaย nyuma kisha akarejesha macho kwangu. Akaangua kicheko na kuanza kuongea kama mlevi . Endelea
SEHEMU YA PILI
โKumbe umekunywa pombe Celin, Ha!ha! Hakuna Mtu. Ulisema hautumii pombe mbonaย umelewa ha!ha!ha!โ Haraka niligeuka nyuma, hapakua na yeyote yule, lakini hisia yangu yaย ndani iliniambia yule Mzee analifahamu jambo fulani kuhusu nyumba yetu. Nilitabasamu ili tuย kumfanya Caren aamini kua nilikua nimelewa kidogo.ย
Tuliporudi ndani tulikuta Watu wakiendelea na tafrija hiyo fupi, baadaye mishale kama ya saaย tano hivi walitawanyika na kutuacha Wana Familia pekee, Mimi, Baba na Mama. Kwakua Usikuย ulikua mwingi, Baba akatuambia tukalale, asubuhi tutafanya kazi ya kuweka mazingira sawa.ย Mimi niliingia chumbani kwangu, chumba changu kilikua juu.ย
Baada ya kuingia chumbani nilijikuta nikiendelea kufikiria hatua za yule Mzee, bahati nzuriย dirisha langu lilikua likiitazama vizuri nyumba ya yule Mzee, nilisogea taratibu hadi dirishaniย kisha nilichungulia, palikua kimya sana. Hapakua na dalili ya Mtu yeyote yule, nilisimama hapoย kwa zaidi ya dakika kumi lakini sikuambulia chochote kile.ย
Nilikata shauri nikaingia bafuni kuoga kisha nilipomaliza nilirudi kitandani na kupumzika. ***ย
Nilichokiona, nilichokihisi kilibakia ndani yangu. Sikupenda kuwaingiza wazazi wangu kwenyeย presha ya aina yoyote ile, kama ukweli nitautafuta mwenyewe.ย
Siku iliyofuata ilianza kwa baridi kali sana, nilipaswa kuelekea chuoni. Nilijiandaa, baada yaย dakika kama kumi nilikua tayari kwa ajili ya kuondoka na kuelekea chuoni.ย
Niliwaaga wazazi wangu kisha niliondoka. Nilipofika nje nilipata wazo la kubadilisha njia,ย niligeuka na kuelekea upande wa nyumba ya yule Mzee, mara zote nyumba yake ipo kimya.ย Hapasikiki sauti ya aina yoyote ile, nilipiga hatua zangu za taratibu nikiwa nimevalia viatu virefuย kama buti hivi, suruali nyeusi na shati jekundu kisha koti la kunikinga na baridi.ย
Nafsi yangu ilizidi kuniambia kua kuna jambo napaswa kulijua kuhusu nyumba yetu mpya, Mtuย pekee ambaye alionesha hisia ya kujua jambo alikua ni huyu Mzee wa ajabu. Basi, nilipofikaย aneo la geti lake niliona pameandikwa โMwanzo wa Mwishoโย ย
โMwanzo wa Mwisho?โ niliyarudia maandishi yaliyopo getini, nilihema. Yalikua ni manenoย magumu kiasi kwamba sikuelewa chochote kile, hisia mbaya dhidi ya huyu Mzee ilichipua zaidiย ndani yangu. Wakati huo jua lilikua likianza kuchomoza kwa mbali, palikua na mwanga waย kutosha, upepo wa hapa na pale.ย
Niligeuka kuangalia nyumbani kwetu, kisha nilitazama tena pale getini, sikupata tafsiri ya harakaย haraka juu ya yale maneno. Nilimeza funda zito la mate, nilitazama saa yangu, ilisoma ni saaย 2:13 Asubuhi.ย
Niliona bado nina muda wa kutosha kabla ya kuelekea chuoni pengine naweza kuzungumza naย yule Mzee angalau nipate ufumbuzi wa maswali magumu yaliyojaa kichwani pangu. Nilisita-sitaย lakini niliweza kugonga geti
Palikua kimya sana kama sehemu isiyotembelewa na Mtu kabisa. Niligonga tena, nikagongaย zaidi kwa kutumia mkono wangu wa kushoto huku nikisemaย
โKuna yeyote?โ nilikua makini sikutaka wazazi wangu wajue chochote kile, palikua kimya sana.ย Nilikata tamaa, sikuona dalili ya kufunguliwa Geti hilo dogo. Nililipa mgongo lile geti kishaย niliondoka hapo, nikasogea Barabara kuu nikapanda treni iliyokua ikielekea katikati ya Jiji, hukoย ndiko nilikokua ninasoma.ย
Niliketi siti namba 25, kando yangu alikuwepo Bibi mmoja. Nilimsalimu kwa heshima sana,ย baada ya treni kuondoka aliniulizaย
โKuna jambo linakutatiza?โ sijui aliweza vipi kujua kua nilikua natatizwa na jambo fulani,ย niliachia tabasamu kiasi ili kumjibu yule Bibi.ย ย
โKiasi, hata hivyo ni jambo la kawaidaโ nilimjibu, hakusema chochote. Alikaa kimya namiย nilikaa kimya nikisubiria kusikia angesema nini lakini aliendelea kukaa kimya. Dakika kamaย kumi hivi, yule Bibi akaniambiaย
โNashuka kituo kinachofuata, kua makini sana Mjukuu wangu. Unakaribia kupoteza Watuย uwapendao kwa mpigo, kua jasiri. Wakati mwingine Maisha yanatupeleka shimoni makusudiโย Moyo wangu ulilipuka mithiri ya Volkano, simjui yule Bibi. Aliwezaje kuongea maneno mazitoย kiasi kile, Watu niliowapenda sana walikua ni Wazazi wanguย
โSamahani unasemaje?โ nilimkujia sura yangu, aliachia tabasamu tu akaniambiaย
โHuwezi kuwaokoa, Hatma imewafikiaโ maneno yake yalikua mazito sana, kiasi kwambaย yalinifanya nilegee mwili mzima. Nilihisi ganzi moyoni mwangu, huzuni na hisia ya hasira.ย Nikiwa ninaendelea kuyarudia maneno yake, mara treni ilikua imefika kituoni, yule Bibiย alishuka kisha alisimama akinipungia mkono wa kuniaga.ย
Moyo uliniuma sana, hata safari yangu ya kuelekea chuoni niliiona kua ilikua nzito sana. Hapoย hapo nikaitoa simu yangu kwenye begi nikampigia Mama yangu kumuuliza kama walikuaย salama. Mama alinitoa hofu, hata sauti yake ilionesha palikua shwari kabisa.ย
Pumzi niliyoishusha ilikua kubwa, ilishuka kama gia ya gari. Kifua kilikua kizito, presha siyoย presha, yale maneno yalikua yanazidi kunipigia kelele masikioni mwangu. Ndani ya siku mbiliย nilikutana na mauzauza ya kutisha, nilipiga moyo konde nikiamini hakuna anayeweza kuijuaย hatma ya Mtu mwingine isipokua Mungu pekee.ย
Nilipofika chuoni, nilikua na maswali mengi kichwani. Nilijiinamia kwenye meza, nilihisi kamaย nilikua nimebeba mzigo mzito sana kichwani mwangu. Nikiwa hapo alikuja Caren, akanifanyiaย utani ambao haukua kipaumbele kwanguย
โUna shida gani Celin?โ aliniuliza, niliweka mikono yangu usoni, nilitamani kumueleza Carenย lakini sikupata ujasiri wa kufanya hivyo.ย
โCelin, niambie una tatizo gani?โ aliniuliza tena, bado nilikua kimya nikimwangalia.ย
โJana usiku ulikua hivi, unanificha kitu. Hata hivyo nimepewa hii barua nikupatieโ Nilishtukaย kidogoย
โImetoka wapi?โย ย
โNimepewa na Bibi mmoja hapo nje amesema nikupatie weweโ Nilishtuka sana, niliogopa kishaย nilikimbilia nje ya geti la chuo, nilitazama huku na kule kama ningemwoma huyo Bibi, nilikuaย na uhakika huwenda ni yule Bibi niliyekutana naye kwenye Treni muda mchache uliopita. Maraย Caren alifikaย
โSikuelewi Celin, kuna nini?โ aliniuliza, nilimsogelea nikiwa nina hisia ya hofu na Mashakaย makubwa.ย
โYupoje?โย
โMwembamba, amevaa koti la suti lililochakaa. Gauni la bluu, halafu amevalia raba chiniโ sifaย alizozitaja Caren zilifanana na sifa za yule Bibi niliyekutana naye kwenye treni.ย
โCaren kuna kitu hakipo sawa, nilikutana na huyo Bibi kwenye treni. Ameongea maneno yaย kutisha sana, nipe hiyo Baruaโ Haraka Caren alinipatia Barua kisha niliifungua haraka,ย nilikutana na karatasi nyeupe iliyoandikwa jina moja โZENAโย
โZenaโ nilisema kwa hofu, nilirudi nyuma nyuma nikiwa nina hofu hadi pale nilipofika mwishoย nikakutana na ukuta wa uzio wa chuo, Caren alisogea naye akiwa kwenye Mshangao mkubwaย sana. Jina la Zena liliandikwa kwa herufi kubwa na wino mwekundu. Chozi lilikua linanitokaย huku ile kauli kua nitapoteza niwapendao kwa Mpigo ilikua ikijirudia akilini mwangu.ย
Zena ni rafiki yetu, tokea nimefika chuo sikumwona. Nikamuuliza Carenย
โUmemwona popote?โย
โNani?โย
โZenaโย
โHapana, nilijaribu kumpigia nilipofika chuo lakini simu yake ilikua ikiita tu. Hebu niweke waziย kuna nini?โ Caren aliniuliza kwa hofu huku akiweka mikono yake kichwake pake, alikua njiaย panda nami sikua na muda wa kumweleza zaidi.ย
โTwende kwake Caren, tafadhali twendeโ nilisema huku chozi likizidi kunibubujika. Nilikua naย uchungu moyoni mwangu, nilianza kuwa na wasiwasi kua kuna jambo lililomfika zena. Manenoย ya yule Bibi yalizidi kujirudia akilini mwangu. Nilisimamisha Taxi haraka, tuliingia kwenye Taxiย huku Caren akinilazimisha niseme kinachoendelea, nilikua ninalia tu.
โSasa Celin, usiposema nitajua nini. Yule Bibi ni Nani yako, kwanini amekutumia Barua yenyeย jina la Zena?โ aliniuliza Caren alikua amejawa na hofu, wasiwasi kwa pamoja. Niligeukaย kumtazama huku chozi likinibubujikaย ย
โSali, lisimfike lolote. Dunia inanigeuka Carenโ nilisema kwa Uchungu, sikuweza kuongeaย zaidi. Nilihisi uzito uliopitiliza, nilihisi kuchanganikiwa huku sura na maneno ya yule Bibi kizeeย yakizidi kuendelea kutembea kichwani kwangu.ย ย
Zena alikua anaishi kilomita chache kutoka pale chuoni, wastani wa nusu saa tulikuaย tumeshafika mahali alipokua amepanga. Niligonga geti kwa nguvu kisha tulisubiria kwa sekundeย kadhaa kisha geti lilifunguliwa na Mama mwenye nyumba.ย
Alionesha tabasamu mbele yetu sababu alikua akitufahamu, tulikua tukienda hapo mara kwaย mara lakini safari hii hakuna aliyerudisha tabasamu. Tulimpita kama wanariadha wa mbio ndefuย za Marathon, breki tulifunga mlangoni kwa Zenaย
Tulisimama kwa sekunde kadhaa za kuhesabu, mlango ulionekana kua wazi sababu palikua naย upenyo mdogo. Tulitazamana, sura ya Caren ilijaa maswali mengi yasiyo na Majibu, sikuwezaย kumweleza chochote kile hadi muda huo.ย
Nilipopiga hatua kuusogelea mlango, Caren alinishika mkono akaniulizaย
โNini kinaendelea Celin?โ Alianza kuniuliza kwa sauti ya chini iliyojaa kilio cha hisia kali yaย hofu na woga kwa pamoja. Ni kama Caren alikua amenielewa, nilitikisa kichwa kumdhihirishiaย kua Zena alikua shidani. Chozi lilikua likitububujika, nyuma yetu alifika Mama mwenye nyumbaย
โMabinti, kuna nini?โ aliuliza yule Mama Mtu mzima, ndiye mmiliki wa nyumba ambayo Zenaย alikua amepanga kwa ajili ya masomo ya Chuo. Niligeuka kumtazama huku chozi likinibubujika,ย naye Mama akautazama Mlango wa Zena, akiwa kama Mtu mzima alikua ameelewa kua Zenaย alikua matatizoni na pengine alikua ameshakufa.ย ย
Macho yake pia yalimlenga kwa Mchozi. Nilielekeza macho yangu mbele kisha niliufunguaย mlango taratibu, nikautosa mguu wangu ndani ya chumba, nilichokiona kilinifanya nipige yoweย kali la kuchanganikiwa.ย
Kila mmoja wetu aliingia kushuhudia kile ambacho macho yangu yalikuwa shuhuda wa kwanza.ย Zena alikua akiningโinia kwenye kitanzi cha Khanga kilichofungwa kwenye feni, alikuaย akizungushwa huku na kule kama Mzigo usio na thamani tena, ama kweli utu wa Mtu ni uhaiย wakeย
Zena alikua amekufa muda mrefu sana, binafsi nililia kwa uchungu sana. Mama mwenyeย nyumba akakimbilia kumwita Mjumbe na mwenyekiti wa Mtaa. Bila hata kutumia vipimoย walithibitisha kifo cha Zena, rafiki aliyenipokea chuoni na kunifundisha Maisha ya Chuo jinsiย yalivyo.
Tulipishana Mwaka mmoja wa kuingia chuoni, alinitendea wema kila nyakati. Hata wakatiย ambao alipaswa kufurahi alinipa furaha yake na kisha yeye alibakiwa na huzuni yangu.ย Nilimwona akiwa anafunguliwa kutoka juu ya feni akiwa amevalia gauni lake jekundu.ย
Hakika maneno ya yule Bibi yalianza kutimia, nilimpoteza mmoja nimpendaye. Nilijiegemezaย ukutani nikilia kwa kwikwi nikiushuhudia mwili wa Zena ukiondolewa na Askari Polisiย waliokua hapo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa.ย
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TATUย
COMMENTS ZIWE NYINGI SASAย
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx


42 Comments
Very good https://shorturl.at/2breu
Mh atali
Mmmm, hii noma, hachia kipande kingine tuone nani anafata kufa baada ya ZENA, Hooo Zena R.I.P !!!
Hatari๐๐
Daah ๐๐ฅบ๐ฅบ zena R.I.P who is next ๐ฅบ
Achia nyingine kijiweni tupo pamoja
Daah hii kalii
imeanxa kaa story naona imeanza kugeuka kua zile hallowin movieza wazungu ๐๐
Daah ๐๐ฅบ๐ฅบ zena R.I.P who is next ๐ฅบ
Achia nyingine kijiweni tupo pamoja km
Daah!bonge la storry
โค๏ธ
Ooh I can’t wait
OMG ๐ณ
Daah ๐๐ฅบ๐ฅบ zena R.I.P who is next ๐ฅบ
Achia nyingine kijiweni tupo pamoja
Duuuuh
Dunia inamgeuka Celin
Aah hakika ipo vyema๐ค
Kama muvi flani ivi ๐
Dondosha cha tatu
Duuuu
Hakika utu wa mtu ni uhai wake.
Ntakutafuta mkuu tuandae bajeti tufanye movie hii story
Mwanzoni nilihofia nikajua ni wazaz wakeโค๏ธโ๐ฅโค๏ธโ๐ฅ
Anewei RIP Kwa Zena na pole Kwa Celin..
Mola ampe ujasiri kwakwel.๐ฅฒ๐ฅฒ๐๐
Good https://lc.cx/xjXBQT
hii nimeikubali
Nomaah san jmn R.I.P zenaa joomn
Nimeipenda iko vizur sana mkuu
Amini hiki chuma
Jamn inatishaaaa km tamthiliya vile mmh kweli maisha ni uhai
Halafu mm naisoma usiku ๐ฅท
Aah hii riwaya ni nzuri sana ina mafunzo makubwa sana ndani yake.
Mbona inaogopesha
Kwani ufalime wa zombie imeishia wap
Very good https://is.gd/N1ikS2
Awesome https://is.gd/N1ikS2
Very good https://is.gd/N1ikS2
Good https://is.gd/N1ikS2
Very good https://is.gd/N1ikS2
๐ค๐
Awesome https://is.gd/N1ikS2
Nyumba ya kununua sio mzuri sana
Bora ukajenge ya kwako tu..
Very good https://is.gd/N1ikS2
Very good https://is.gd/N1ikS2
Iko powa sana tatu please