Ilipoishia “Wala hakuongea chochote akaanza kuniandalia chakula nile, nilikua nahema kwa shida sana.Β
βKunywa Majiβ alisema, alikua haniangalii usoni, nilikua na kiu ya maji lakini kiu kubwa ilikuaΒ ni kumuuliza Nauawa lini, nilimuulizaΒ
βMnanimalizia lini nikapumzike?β Kiukweli sikuwa na afya nzuri, ndani ya siku chacheΒ nilikonda. Yule Bodaboda akanitazama kisha akaniambiaΒ
βKifo ni siri ya Mungu, hakuna anayeijuwa kesho itakuwajeβ alisema kisha akanipa maji, sikuwaΒ na nguvu ya kushika kikombe akaninywesha. Jinsi alivyonihudumia alionesha anahitaji niwe hai. EndeleaΒ
SEHEMU YA NANE
Niliyafakamia yale maji kwanza hadi yalinipalia, halafu nikahema. Akanitolea vidonge vyaΒ kunituliza maumivu. Sikusita kumeza kiukweli maana nilikua na maumivu makali sana kishaΒ nilimshika mkono nikamuulizaΒ
βNingekuwa mdogo wako ungenifanyia hivi, unajua najisikiaje Kaka?ββ Chozi lilikuaΒ linanibubujika bila kuacha, akaniondoa mkono wangu kwa kutumia mkono wake mwingineΒ kisha akasimama, akaniambiaΒ
βKula upate nguvuβ hakuzungumza tena, alisimama kisha alipiga hatua lakini alipofika mlangoniΒ alisimama. Kama kuna kitu alitaka kuniambia lakini alighaili, hakujibu swali langu aliondoka naΒ kuufunga mlango kwa funguo, unajua hata kama angeuacha wazi sikuwa na nguvu ya kukimbiaΒ kwa namna nilivyokua sina nguvu.Β Β
Nilisikia akiondoka, nililia sana Mimi. Hakuna siku inapita bila kudondosha chozi langu,Β nilimpoteza Kaka Hamidu na nilijiona ni mkosaji, nilijilaumu sababu bila kuolewa na SaleheΒ basi Kaka Hamidu angekuwa hai hadi sasa. Kidogo zile dawa zilipunguza maumivu ya mwiliΒ lakini siyo maumivu ya Moyo wanguΒ Β
Haikuchukua hata dakika nyingi nilisikia yowe la Mwanaume mmoja, yowe lile lilisikika mojaΒ kwa moja kutoka kwenye ile nyumba niliyohifadhiwa Mimi. Moyo ulinilipuka, niliamini ilikuaΒ ni nyumba ya Mateso makali zaidi hata nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu. Nilisimama hataΒ nguvu sikujuwa ilitokea wapiΒ
Nilisogea mlangoni ili kuisikia zaidi ile sauti, ndiyo! Ilitoka ndani ya moja ya vyumba vya ileΒ nyumba, nilitamani kupaza sauti ila sikujua alikua akifanywa nini. Nilijiuliza
βNani yupo ndani ya hii nyumba, anamfanya nini huyu anayepiga yoweβ Ilikua ni sawa naΒ kujitekenya kisha kucheka mwenyewe, jibu lingetokea wapi ikiwa hata mimi mwenyewe sijuiΒ nipo wapiΒ
Yule Mwanaume baada ya kupiga yowe alianza kusemaΒ
βMsaada,Nani yupo ananisikia?β aliendelea kusema hivi, nikapata picha huwenda hata yeyeΒ mwenyewe hajui amefikaje na Nani amemleta ndani ya hii nyumba. Kupitia dirishani nilianzaΒ kuona jua namna lilivyokuwa likifanya safari ya kwenda kupumzika baada ya kuipiga ardhi kwaΒ siku nzima.Β
Namna nyumba hii ilivyo ilionekana kujengwa kwa ajili ya kazi ya kuhifadhi Binadamu, hataΒ dirisha lake lilikua kama la Mahabusu, lilikua dogo lanye nondo,hapakuwa na taa ndani yaΒ chumba kiasi kwamba giza litakapoingia basi patakuwa giza tupu. Nilijikuta nikikaa mwenyeweΒ bila hata kuambiwa, kwa namna ilivyo hata ukipiga kelele vipi huwezi kupata Msaada wowote.Β
Kwanza sikujuwa Mtu yule alikua ni Nani, sauti yake haikufanana na ya Kaka Hamidu. Wala siΒ ya Mtu niliyehisi kuwa niliwahi zungumza naye.Β Β
**Β
Usiku ulipoingia ndiyo nililiona joto la jiwe, niliandamwa na ndoto za ajabu hadi niliamka, siyoΒ Mimi tu hata yule Mwanaume alikua akigugumia nahisi naye alikua kwenye hali kama yangu.Β Niliamka na kukaa kitako nikaegemea ukutaΒ
Nikiwa hapo nilianza kuona nuru ya mwanga, ikianza taratibu hadi ikaenea chumba chote, hapaΒ nilikua na uhakika kuwa haikuwa ndoto tena bali ni tukio halisi. Nilimuona tena yule MtotoΒ mdogo anayetisha, safari hii alinionesha sura yake, nilikua kwenye Mshangao wa hali ya juuΒ sanaΒ
βUmeshindwa kutoka hapa, umeshindwa kujaribu kufanya chochote. Wewe ni Mtu wa aina gani,Β unataka kila Mtu afe kama Kaka yako Hamiduβ Ooh! Jamani nilishtuka, kama ningekua ninaΒ presha kwa haya yote ningekuwa tayari nimepotea kwenye uso wa Dunia, namna alivyokuaΒ anaongea alionesha alikua na tumaini na Mimi kwenye jambo fulani hasa la kuokoa uhai waΒ wengine lakini Mimi mwenyewe nilikua nimeshajikatia tamaa. Japo nilijawa na woga lakiniΒ nilimuulizaΒ
βWewe ni Nani, umetokea wapi?β nilipomuuliza alidondosha chozi la damu, alikua Mtoto waΒ ajabu sanaΒ
βMimi ni Ashura Mtoto wa Mama Muuza chapati. Nenda kamwambie Mama yangu kuwa badoΒ naishi kwenye nyumba ya Mzee Mwinyimkuu, Mimi sijafaβ alisema kwa kupaza sauti kaliΒ ambayo ilinifanya nishindwe kuhimili zile kelele, pale pale nilijikuta nikiishiwa nguvu naΒ kupoteza fahamu. Kitu pekee kilichobakia kwenye akili yangu ni ,kumbukumbu juu ya yuleΒ Mama anayeishi nyumba jirani na Mzee Mwinyimkuu, Mama aliyekuwa akiniuzia Chapati
NdiyoβΌ yeye ni Mama Ashura, nakumbuka alinitajia jina hili lakini sikuwahi kumuuliza huyoΒ Ashura yupo wapi, huyu Mtoto wa ajabu alijitambulisha kwangu kama Ashura na alinitakaΒ nimwambie Mama yake kuwa anaishi ndani ya nyumba ya Mzee Mwinyimkuu.Β
***Β
Baba yangu aliendelea kuumwa, Mama alikua anamuuguza huku akinitafuta Mimi kwa simuΒ lakini aliendelea kutonipata, zilipita wiki mbili bila kupata mawasiliano yoyote yale. SaleheΒ hakupatikana, hata Mzee Mwinyimkuu hakupatikana, Kaka Hamidu naye ilikua kama ndiyoΒ Β
kichocheo kipya cha hofu kwa Familia yangu. Mara ya mwisho aliwaeleza anakuja kuonana naΒ Mimi lakini baada ya hapo hawakujua kilichomfika na kupelekea kutopatikana kwenye simuΒ kwa wiki mbili.Β
Vikafanyika vikao vya kututafuta Mimi na Kaka Hamidu maana hawakujua naishi RukwaΒ sehemu gani na pia Kaka Hamidu alikutwa na nini. Ni Mimi pekee ndiye niliyekuwa najua KuaΒ Kaka Hamidu alikua ameuawa.Β
Familia ikamtuma Mjomba wetu aliyeitwa Kambona, alikua Mtu mzima na mwenye busaraΒ zake.Β Β
Akasafiri kutoka Dar-es-salaam hadi Rukwa akiwa na picha yangu, akaanza kunitafuta bilaΒ mafanikio kwa zaidi ya siku kumi. Mwishowe akaenda kituo cha Polisi maana sasa hakunaΒ aliyekua na amani bila kujua tupo wapi, wote waliamini wakinipata Mimi watajua mahali alipoΒ Kaka Hamidu maana mara ya mwisho aliwaambia anakuja kwangu. Polisi wakaanza kunitafutaΒ kila kona ya Rukwa lakini hakuna aliyeweza kujua niko wapi, lakini kupitia jina la Mwinyimkuu Ambalo Salehe alilitaja alipokua ananichumbia, ikawawezesha kufika hadi nyumbani kwa huyuΒ Mzee.Β
Hapa ndipo mahali ambapo nilikuwepo kabla ya kuhamishwa, nyumba hii ndimo alimouawaΒ Kaka Hamidu tena kikatili sana na Mzee Mwinyimkuu. Walipofika walimkuta tena walaΒ hakuwa na wasiwasi kabisa, najua alitumia akili sana kunihamisha vinginevyo polisiΒ wangenikuta mleΒ
βWewe ndiye Mwinyimkuu?β aliuliza polisi baada ya salamu fupiΒ
βMnasemaje?β aliwauliza, alikua haogopi chochote wala Mtu yeyote yule, jeuri na katili mno βSaida anaishi hapa?β akauliza Polisi mmoja.Β
βYeye ni Nani?β akawaulizaΒ
βUnajibu kwa dharau kiasi hicho Mzee, Saida ni Mpwa wangu Mimi. Ameolewa na KijanaΒ anaitwa Salehe, upelelezi umeonesha kuwa ni Kijana wako huyo Salehe halafu unauliza niΒ Nani?β akaingilia kati mjomba Kambona na kumshika shati Mzee Mwinyimkuu, PolisiΒ wakaokoa
βUnanivunjia heshiam si ndiyo?β akauliza Mzee Mwinyimkuu kwa hasiraΒ
βSiyo heshima tu, ntaivunja hata hii nyumba kama hutonipatia Saida wanguβ Mjomba KambonaΒ hakupoa kabisa, alijawa na hasira sana.Β
βHuyo Salehe unamfahamu?β Polisi wakamuuliza Mjomba KambonaΒ
βNdiyo, nimeozesha mwenyewe. Picha si hii hapa ya ndoaβ akatoa picha, ile picha akapewaΒ Mzee Mwinyimkuu.Β
βUmemtambua mtajwa pichani?β akauliza Polisi mmoja, Mzee Mwinyimkuu akaangua kichekoΒ kisha akaita kwa sautiΒ
βSalehe, hebu njoo uone maajabu ya Duniaβ akaitikia Mtu kutokea ndani na kuwafanya Polisi naΒ Mjomba Kambona wakae mkao wa kula kumuona Salehe. Ikachukua kama sekunde kadhaa tuΒ Kijana mmoja akatoka ndani, Kijana aliyekuja hakufanana na Salehe wa kwenye picha.Β Β
βUnamfahamu Saida?β akauliza Mzee Mwinyimkuu akimuuliza huyo Kijana aliyemtambulishaΒ kama Salehe, kiukweli hakuwa yule Salehe aliyeniowa kabisa yaani sura tofauti.Β
βHapana, kuna nini?β akauliza huyo Salehe, kiukweli Mjomba Kambona alinywea. Lakini PolisiΒ mmoja akasemaΒ
βOngozana na Mimi Kijanaβ akamshika mkono Salehe na kwenda naye nje. Lengo la Polisi niΒ kutaka utambuzi kwa Majirani maana Upelelezi wao uliwaambia Salehe wa kwemye pichaΒ anapatikana kwa Mzee Mwinyimkuu. Wakafika hadi nyumbani kwa Mama Ashura maana ndipoΒ palikua na Watu njeΒ
Walipomuona Yule Kijana akiwa na Polisi vijana walikimbia hadi yule Polisi akashangaa, hataΒ Mama Ashura naye alikua anataka kukimbia ila Polisi akamzuia Mama Ashura na KumwambiaΒ asikimbie ana maswali kadhaa anataka kumuuliza, ndipo Mama Ashura akabakia lakini kwa hofuΒ sanaΒ
βUnamtambua nani pichani?β Yule Polisi akampa picha yule Mama, Mama Ashura akaipokeaΒ picha japo kwa wasiwasi lakini alipoiangalia ile picha alishtuka sana, akameza funda la mate.Β Β
βHapanaββakajibu lakini kwa hofu sana kiasi kwamba yule polisi akahisi pengine kuna jamboΒ analificha. Kilichomshtua Mama Ashura ni kuniona Mimi kwenye ile picha ya ndoa ambayoΒ Mjomba Kambona aliwapatia polisiΒ
βNa huyu Kijana hapa?β akauliza Polisi, Mama Ashura akamtazama yule Kijana. AkaachiaΒ tabasamu la hofu kisha akajibuΒ
βNi Salehe, anaishi paleβ akaonesha na kidole kabisa. Majibu haya yakamuacha yule polisiΒ kinywa wazi, basi akarudi hadi nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu. Hakuna ushahidi waΒ anachosema Mjomba Kambona. Lakini Mjomba akawaaambia
βNina namba ya huyu Mzee alikua anawasiliana na Mama yake Saida, hii namba nimepewa naΒ Mama Saida. Jina ni hilo la Mwinyimkuuβ akasema Mjomba japo kwa sauti ya kupoa, ikabidiΒ Polisi waipige ile namba.Β
Ikapokelewa na Mtu mwingine kabisa tena Mwanamke akimuuliza yule Polisi Nani wewe?Β Yalikua kama maigizo ya Filamu lakini lilikua tukio la kweli, nyakati zote hizo MzeeΒ Mwinyimkuu alikua akitabasamu akiwa anamtazama Mjomba Kambona.Β Β
βMnaona anavyo nitazama, huyu anajua kila kituβ akasema Mjomba lakini hakuwa na ushahidi,Β maneno yake yalikua ni sawa na kuupaka upepo rangi. Muda wote Mzee katili alikuaΒ akitabasamu kwa mpango fulani ulio kichwani pakeΒ
Polisi walikosa ushahidi, ikaonekana kuwa Mjomba Kambona aliyakosea maelezo yake. KibayaΒ zaidi hata picha aliyowaonesha Polisi kuwa ndiye aliyeniowa ilikanwa kwa kuoneshwa SaleheΒ mwingine na kilichotia nguvu kukosekana ushahidi ni maneno ya Mama Ashura. AngefanyajeΒ Mjomba wangu zaidi ya kutoa kitambaa na kujifuta jasho ila moyoni aliamini MzeeΒ Mwinyimkuu alikua anajua wapi nilipo, pia hapakua na ushahidi mwingine sababu MzeeΒ Mwinyimkuu hakuhudhuria ndoa yanguΒ Β
Polisi wakamwambia Mjomba KambonaΒ
βTutaendelea na Uchunguzi, kwasasa wewe liachie jeshi la Polisi. Tutakupa taarifa ya UchunguziΒ juu ya Saida pia huyo Kaka yakeβ haikua kauli yenye matumaini, ilimvunja moyo sana MjombaΒ Kambona. Akamwambia Mzee MwinyimkuuΒ
βSaida hawezi kutoweka kirahisi, lipo unalolijua. Siondoki Rukwa hadi nihakikishe nampataΒ Mpwa wanguβ alisema hivyo kisha aliongozana na Polisi kuondoka, Salehe feki na MzeeΒ Mwinyimkuu wakatazamana kisha wakawa wanawatazama namna Polisi na Mjomba KambonaΒ walivyokuwa wanaondoka.Β Β
Wala hawakufika mbali, kabla hata hawajapanda kwenye gari ya Polisi. Mjomba KambonaΒ alianguka na kufariki papo hapo akitokwa na Mapovu mdomoni. Licha ya jitihada za jeshi laΒ polisi kumkimbiza Hospitali lakini alikua tayari amefarikiΒ
Taarifa ikarudi Dar-es-salaam kuwa Mtu waliyemtuma kuja kututafuta Mimi na Kaka HamiduΒ alikua tayari ameshafariki. Yalikua ni majonzi juu ya Majonzi, taarifa hii ilipomfikia Baba yanguΒ alifariki pia kwa presha. Bundi aliizingira familia yangu, misiba miwili ndani ya siku moja,Β Mzee Mwinyimkuu akashinda tena kwa kishindo kikubwa sana.Β
**Β
Nilihesabu siku ambazo nilikua ndani ya ile nyumba ya mateso, zilitimia siku saba ngumu.Β Nilikonda nikawa kama Mtoto mdogo, niliishiwa nguvu. Kilichokuwa kimebakia kwangu ilikuaΒ ni kufa tu. Kila nilipoamka nilijikuta nimeshaondolewa kidole kimoja, pumua yangu ikawa yaΒ
shida sana. Nikakosa uwezo wa kuwatambua Watu kirahisi, yule Bodaboda aliendelea kunileteaΒ chakula kila siku lakini pia sauti ya Mwanaume mmoja kugumia ilikua ni sauti ya Kila sikuΒ
Lilikua ni jambo la kawaida sana yeye kupaza sauti, sikuwahi kufahamu alikua akipitia matesoΒ gani, ila dakika za mwisho niligundua kuwa naye alikua akipelekewa chakula na huyu huyuΒ Bodaboda anayeniletea Mimi chakula.Β
Sikuweza kusimama tena, vidonda vilianza kutoa funza sababu sikuwa na dawa yoyote isitosheΒ joto la mle ndani liliniathiri kwa kiasi kikubwa, Mwenzenu niliwahi kufika Jehannam nikiwaΒ Hai.Β
Basi siku moja yule Bodaboda alikuja, siku yenyewe palikua na mvua kubwa. Aliingia akiwaΒ ameloa sana anatetemeka kwa Baridi, japo nilikua katika nyakati za mwisho kabisa za uhaiΒ wangu lakini niliweza kugundua kuwa Baridi lilikua tatizo kubwa kwake. Alikua akiniandaliaΒ chakula huku akitetemeka nikagundua anasumbuliwa na tatizo linalo sababishwa na Baridi.Β
Akajikaza, akaniwekea chakula. Alipaswa kunilisha sababu Mimi nilikua siwezi tena hataΒ kushika kijiko, nilikonda mno hadi mishipa ya Damu ilikua ikionekana. Akajitahidi kuniinua iliΒ kunikalisha kitako niweze kuegemea ukuta anilishe vizuri, siku hii nilipanga kuacha kula ili nifeΒ mapema maana mateso yalinizidi kabisa, Jamani naposema nilikonda basi ujue nilikonda nikawaΒ na kilo chache sana halafu kichwa kikawa kikubwa.Β
Nilitamani kumuuliza ana shida gani, huyu Mtu hakuwahi kunitesa wala hakuwahi kunisemeaΒ jambo baya isipokua alikua hajibu maswali yangu yote niliyokuwa namuuliza.Β
Hali yake ilianza kuwa mbaya, akashindwa hata kunishikilia akaanguka chini na kuanza kugalaΒ gala kwa maumivu Makali sana, mlango ulikuwa wazi hakuufunga sababu alipoingia alikuaΒ tayari ana hiyo hali ya Maumivu, niliona ni nafasi ya kutoroka lakini sikuwa na akiba yoyote yaΒ nguvu iliyobakiaΒ
Nikatamani kuendelea kuishi ghafla tu, namna pekee ya kuendelea kuwa hai ni kutoroka. HukoΒ nje mvua ilikua ikinyesha na kusababisha kelele kubwa sana kwenye Bati. Sikuwa na nguvu yaΒ kusimama, nikaona ni bora nijiburuze nione kama naweza kufika njeΒ
Yule Bodaboda alipoona naanza kujiburuza akajua nataka kumtoroka, akili yake ikatamaniΒ anizuie lakini mwili ulimsaliti, nguvu zilimwisha akiwa sakafuni anapumua kwa shida sana.Β Nikaendelea kujivuta taratibu huku nikiwa ninasali Mungu niliyemkatia tamaa azidi kunipaΒ nguvu, unajua kwanini niliamini naweza kuondoka pale?Β
Kwasababu hapakua na mtu mwingine aliyekuwa anakuja isipokua yeye, hivyo hakuna tena waΒ kunizuia, halafu niliwaza kufika chumba ambacho yule Mwanaume anagumia ili kama yeye anaΒ nguvu tusaidiane kutoroka.Β
Nilijiburuza kama nyoka hadi nilipotoka nje ya chumba kile, palikua na funguo kwenye kitasa.Β Nikapata akili ya dharura kuwa huwenda funguo ile inaweza nisaidia kufungua milango mingineΒ
maana ilikua na funguo tatu zilizowekwa sehemu moja, naipataje Funguo ni lazima nisimameΒ niichomoeΒ
Kivumbi kilianzia hapo, nilikonda Mimi kiasi kwamba upepo unaweza nipeperusha, MalaikaΒ Mtoa roho alikua amenisimamia akiniuliza nasimama au achukue roho yangu, sijui nguvuΒ zilitoka wapi nikasimama kwa kuyumba huku nikitetemeka. Nikachomoa funguo, ile natakaΒ kupiga hatua nikaangukaΒ
Basi nikagugumia kwa maumivu, nilihitaji kufanya haraka maana kama yule Bodaboda atapataΒ nguvu basi sitaweza tena kuondoka, nikamkumbuka Mama na Baba yangu, nikamkumbuka KakaΒ Hamidu. Ghafla nguvu zikaamkaΒ
Nikajikaza na kuanza kujiburuza sakafuni kama nyoka vile, kwa mwendo huo huo nilijikutaΒ nikikiacha chumba kwa mbali kidogo, sikuufunga ule mlango wa chumba nilichomuachaΒ Bodaboda.Β Β
Basi nilipofika kama chumba cha tano hivi nikasikia Mtu akiugonga mlango kwa nguvu hukuΒ akisemaΒ
βNjoo unitoe humu Mshenzi wewe, mtauwa wangapi. Siku ikifika mtakufa kama Kukuβ alisemaΒ kwa hisia sana lakini hakujuwa kuwa Mimi nilikua tayari nipo mlangoni. Mlango ulikuaΒ umefungwa, korido lilikuwa refu halafu vyumba vilikua mbali mbali. Nilijitahidi sana kusimamaΒ nifungue mlango lakini nilikua nakosa nguvu, nilijaribu kama mara tatu lakini niliishia kuangukaΒ
Wakati nikiwa nimeanguka nikageuka nyuma, ndipo nilipomuona yule Bodaboda akijikongojaΒ kwa maumivu kuja nilipo, alikua amelishikilia tumbo lake. Hapo sasa yule Malaika mtoa rohoΒ nikamuona kama anachukua koleo kwa ajili ya kuichukua roho yangu.Β
Sauti ya yule Mwanaume ilizidi kusema, kibaya zaidi Mimi ndiye mwenye funguo halafu sautiΒ yangu ilikua haitoki. Nikasema kama sisimami basi siondoki. Yule Bodaboda akawa anazidi kujaΒ upande wangu kwa kasi akionekana kuanza kupiga hatua za nguvu. Nikamtaja Mungu nikasemaΒ
βMungu nipe nguvu niishinde hii vitaβ nikajivuta haraka nikasimama nikiwa ninayumba,Β nikaanza kusaka tundu la kuweka funguo maana nguvu yenye ilikua sifuri, nikawa najitahidiΒ huku nikiwa natetemeka. Mara naingiza mara nakosea, huku yule Bodaboda akizidi kunisogelea,Β hata nilipopaatia nilikua nimeingiza funguo isiyo yake.Β
Akawa karibu zaidi kiasi kwamba akipiga hatua tatu anakuwa amenifikia na kunizuia kuufunguaΒ mlango, nikapapasia kwa bahati nzuri nikapatia funguo nikavuta nguvu za mwisho nikatekenyaΒ kitasa lakini tayari Bodaboda alikua ameshanivaa na kuniangusha chini, Bahati nzuri ule mlangoΒ ulikua tayari umeshafungukaΒ
Akatoka mwanaume mmoja na kuanza kumkita mateke yule Bodaboda hadi akamtupilia mbaliΒ huko akiwa hoi sana anatokwa na damu mdomoni, eneo la Korido lilikua linawaka taa isipokuaΒ
vyumbani tu. Sikuamini macho yangu Mtu ambaye nilikuja kumuona na kumtambua japoΒ nilimuona mara moja tuΒ Β
Alikua ni yule Mwanaume niliyemuazimaga simu kule Buchani, Ndio! Ni Abuu, masikini nayeΒ alikua mateka wa Mzee Mwinyimkuu baada ya kujulikana ananifuatilia Mimi, kwa muda mfupiΒ naye alikua amepungua sana japo alikua na nguvu.Β
Hakuniuliza chochote zaidi ya kuninyanyua na kuweka mkono wangu kwapani kwake tukawaΒ tunaelekea nje, mvua bado ilikua inanyesha. Tulipokua tunakaribia kutoka kabisa tukamuonaΒ Mtu anakuja Mbio, tena akikimbia kwenye mvua, ikatubidi tujifiche nyuma ya Mlango waΒ kutokeaΒ
Yule Mtu alipofika, breki ya kwanza ilikua vyumbani kisha akamrudia yule Bodaboda aliyekuwaΒ anagala gala. Akamuuliza kwa hasiraΒ
βUmefanya nini Mpuuzi wewe?β aliuliza kwa sauti ambayo niliitambua, ilikua ni sauti ya MzeeΒ Mwinyimkuu. Nilishtuka na kupata nguvu, nilipokumbuka kuwa yeye ndiye mtesi wangu basiΒ mkojo ulinibana. Ghafla tu nikajiona ni Binadamu ninayehitaji kujiteteaΒ
βNenda, hatuwezi kuondoka wote. Kaiambie Dunia kuhusu huyu Mzee, kama nitarudi tutakutanaΒ na kama nitafia hapa basi Roho yangu itakua salamaβ alisema Abuu, roho iliniuma. Sikua naΒ uwezo wa kuzungumza. Mdomo wangu wa juu na chini nilihisi kama vimeungana sababu nilikuaΒ na vidonda mdomoni hivyo kukaa kimya ndiyo yalikua maisha yangu.Β
Nikaitikia kwa kutumia kichwa kisha nikasimama kama Mzimu, Mungu akaamua kunikumbuka.Β Akanipa nguvu na ujasiri, alichotaka Abuu ni kumzuia Mzee Mwinyimkuu. Wakati naanza safariΒ Mzee Mwinyimkuu akaja mbio nahisi alikua anaanza kutusaka, sijui alijuaje kuwa tunatoroka.Β Huyu Mzee alikua Mchawi haswa, aliponikaribia tayari Abuu alimdaka Mzee MwinyimkuuΒ wakaanza kupalangana, muda huo nami nikaanza kujivuta kuondoka pale taratibu hadi nikaingiaΒ kwenye mvua.Β
Ulikua mchana lakini anga lilikua na wingu la kutosha kiasi kwamba palikua na giza fulaniΒ isitoshe palikua Porini. Nilipopigwa na mvua nikapata nguvu ya kuanza kuchanganya MiguuΒ yangu vizuri. Nikaanza kukimbia huku nikiyumba kama mleviΒ
Sijui nilikimbia umbali gani lakini nilikimbia bila kuangalia nyuma, nilikimbia sana hadiΒ nilichoka kabisa nikaanguka na kupoteza fahamu zangu.Β
Nilirudisha fahamu na kuanza kujitambua nikiwa naburuzwa kwa kasi sana, watu walikua kamaΒ vile wamenizunguka. Walikua na mavazi ya kufanana, nilikua kwenye kitanda kiendacho kwaΒ kasi mno, nikawasikia wakisemaΒ
βApelekwe ICU Haraka sana, kazi ianze mara mojaβ niligundua nilikua Hospitalini, waleΒ wauguzi walionekana kunikatia tamaa sababu nilikua na hali mbaya sana. Lakini mimiΒ
mwenyewe nilijiona ni mzima wa Afya zote, mahali nilipokuwepo palikua ni hatari zaidi yaΒ Kuzimu.Β Β
Chozi lilinibubujika nikafumba macho yangu huku nikimshukuru Mungu. Madaktari walifanyaΒ kazi yao kwa wiki tatu kuhakikisha najitambua zaidi, wakaniweka kwenye uangalizi maalumΒ kwa kipindi chote hicho hadi nilipokumbuka yaliyonisibu.Β
Nikawaandikia jina Langu, mahali nilipotoka maana nilikua siwezi kuzungumza tena, HospitaliΒ ikasambaza jina na taarifa zangu ndipo Mama yangu alipokuja Mbeya akiongozana na NduguΒ wengine kunitambua. Mama alilia sana, sikuwahi kumuona Mama yangu akilia namna ile, yaleΒ Maisha yaliniathiri sana kisaikolojia. Nikapoteza uwezo wa kuzungumza kabisa. Taarifa ya KifoΒ cha Baba ilinihuzunisha mno, ikanitoa chozi.Β
Polisi walipokuja niliandika maelezo yangu, ilikua baada ya wiki sita. Mwezi mmoja na sikuΒ kadhaa, afya yangu ilianza kukaa sawa lakini sikuwa na Uwezo wa kuzungumza chochoteΒ isipokua kuandika. Polisi walinichukua ili nikawapeleke mahali nilipoteswa yaani nyumbani kwaΒ Mzee MwinyimkuuΒ Β
Mimi na Mama tulienda, palikua ni pale pale kwa Mzee Mwinyimkuu. Namba ya nyumba ilikuaΒ ni ile ile, mazingira yale yale, chozi lilinibubujika sana hadi Mama akashindwa kujizuia.Β Β
Nilikua natembezwa kwenye kiti cha Walemavu maana bado miguu ilikua haipo sawa pia sikuaΒ na vidole nilikua najiuguza. Nikampa ishara Mama yangu kuwa anipeleke kwanza nyumbaΒ jirani, pale kwa muuza chapati, nilimkuta Mwanamke mwingine kabisa akitengeneza chapati,Β nikaandika kwenye karatasiΒ
βMama Ashura yupo wapi?β nilikua na ujumbe wa Mtoto wake Ashura nilitaka kwanza nimpeΒ ujumbe, wakati huo polisi walikua wameizingira nyumba ya Mzee Mwinyimkuu. MamaΒ akamsomea yule Mwanamke, lakini cha ajabu eti akadai yeye ndiye Mama Ashura, nilishtukaΒ alafu kingine kilichonipa mshituko ni kumuona Ashura mwenyewe, alikua ni Ashura yule yuleΒ niliyemuona Nyumbani kwa Mzee MwinyimkuuΒ
Haya mambo yalinifanya nianze kuonekana akili yangu bado haiko sawa, nikajitahidiΒ kuwaambia kwa maandishi lakini niliishia kupewa pole tu, kisha nikapelekwa kwa MzeeΒ Mwinyimkuu. Nako nikakutana na stori mpya kabisaΒ
Kwanza ile nyumba si ya Mzee Mwinyimkuu, hawamfahamu. Wao wanaishi hapo Kwa MiakaΒ mingi, nilitokwa na Mchozi, nyumba ile ile mazingira yale yale lakini stori tofauti. NikaombaΒ niingizwe ndani, nikapelekwa kwenye chumba nilichokuwa nalalaΒ
Nikakuta magunia ya vyakula, tena kilikua chumba chenye makorokoro mengi sana naΒ hakikuonekana kua chumba cha kulala Mtu. Mama akaniambiaΒ
βSaida, najua umeteseka sana huku lakini hukumbuki chochote tena. Siku ukikumbuka nakuahidiΒ tutarudi, yule Kijana na Baba yake watalipaβ Kauli ya Mama yangu ilinimaliza akili yangu,Β
nilifikia hatua nikakubali kuwa akili yangu haipo sawa, inawezekanaje kila kitu kibadilike kwaΒ haraka vile. Hakuna aliyeniaminiΒ
Lakini sasa wakati natoka nikajikuta nikipeleka macho yangu jikoni, nikaiona ile sufuria kubwaΒ ambayo kwa mara ya kwanza nilipika mchicha mwingi, nikashtuka alafu nikauona MchichaΒ mwingi ukiwa kwenye Beseni. Kilichonishtua ni kwamba nilimuona Msichana wa umri wanguΒ akiutengeneza.Β
Nilijikuta nikipiga yowe kali sana. Hali ya afya yangu ikawa sio nzuri nikarudishwa tenaΒ Hospitali. Tokea siku ile nilikua Msichana ninayekaa kimya hadi leo hii nawasimulia hiki kisa,Β sikumpata Mzee MwinyiMkuu wala Salehe, lakini sitakubali. Siku moja nitarudi Rukwa iliΒ walipe kwa maumivu na mateso makali ninayoyapitia hadi sasa.Β
Kwasasa nimerudishwa kwetu Dar-es-salaam, niko Magomeni. Maisha yangu yamekuwa yaΒ Ukimya sana, Sijazungumza tena tokea siku ile nilipozungumza kwa mara ya mwisho Rukwa,Β sijaandika chochote na wala sitaki kusema chochote kile ila kupitia mkasa huu nataka ujifunze.Β
Kamwe kwenye Maisha yako usiolewe au kuowa Mtu usiye mfahamu, Dunia ni Kichaka chaΒ Mateso. Wasichana wengi wanayapitia mateso niliyoyapitia, wengi wanauawa, wengi wanapataΒ ugonjwa wa akili. Hata wanaume wapo waliopoteza kila kitu, Siku nikifungua kinywa changuΒ nitawasimulia mengi, kwasasa naishia hapa, naweka kalamu yangu chini.Β
AHSANTE……….MWISHO
Comments zikiwa nyingi TUNAANZA MPYA Chaap
USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kutuma Message WhatsApp Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza HapaΒ
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xxΒ Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx
 
		
 
									 
					
24 Comments
Hadi mwili umenisisimka π
Kaka umetisha
Wowoooh fupi na inafundisha sana nmepata somo apa nmejifunza mengi poleee saida wetu.
Hatar sana,, mungu amekpgania pakubwa,, mm kama kijana ambae sjaoa hakka nmepata kitu kwa riwaya hii,, mungu akupe maisha mazur
Dag
pole sana
Jamani hatujajua mwisho wa kijana aliyemukoa Saida,,, mwandishi ungesogeza kidogo
Lini utafungua kiywa Chako tuendelee maan bado nataka kujua zaid
Hahahahahaπ π π π umepigaje apooooooooooooooβοΈπππππ
Navuta picha mwandishi mwili wako ulikua kama wa Ile muv BABU SISU
Hii ya leo machozi yamenibubujika sijui nisemeje lakin naamin Allah anajua zaid yaliyopo mioyon mwetu wanadamu
Maskini Saida jamani π₯
Simulizi ya Maajabu Nzuri yenye mazingatio makubwa jamani
Uchawi upo
Ila uchawi wa MwinyiMkuu ni zaidi ya Uchawi
Mungu atunusuru maisha yetu na Wachawi
Mungu AWAANGAMIZE WASHIRIKINA WOTE MOTONI.
Ameen.
Safi sana mtunzi tumejifunza sana mim pamoja nawasomaji wenzangu Big up
Inauzunisha sana pole saida π’
Kazi mzuri na pole sana
πππππππππnimelia kama mtoto
Daah atali
Ni hatar
Munguu hamtupii mja wake hakika Munguu ni mwemaa
π₯Ήnianze kwa kuhiluzunika ,ila mtu kuna sehem nmecheka dadeq, KWAMBA NYIE WASHENZ NIFUNGUENI MTAKUF KAMA KUKU , YAN MUUNI YUPO KWENY MATATZO ILA BADO AJAL, KWEL MAN IS STRONG NATURAL
Kwani story ni yakwel
Dah sijui niseme nini
Mhhh ila pole
http://terios2.ru/forums/index.php?autocom=gallery&req=si&img=4457
gx3yc0