Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-04

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua (06)
    Hadithi

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua (06)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJanuary 11, 2025Updated:January 12, 202523 Comments15 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Kama utaendelea kunisumbua basi hapa patakuwa Jahannam yako na hutokaa utoke Mileleย  Daima. Kingine napaswa kukuvuna viungo kila unapofanya mapenzi na Misukule, sikuย  nikimaliza nitakuacha urudi kwenuโ€ Nilijiuliza anivune viungo kivipi, kauli yake ilinianbia kwaย  haraka kuwa Kifo kilikua kimenigongea hodi, kipo karibu zaidi na Mimi.ย 

    โ€œUnasema nini?โ€ niliuliza nikiwa ninalia kwa sauti ya Chini.ย 

    Haraka yule Mzee akanipulizia unga fulani aliokuwa ameushikilia mkono wa kushoto, ulikuaย  mweupe ulionifikia hadi usoni kwangu. Nikajikuta nikiwa nimelegea vya kutosha kiasi kwambaย  sijitambui, hatimaye giza tu lilinitanda na sikujua kilichokuwa kimeendelea nyuma yangu. Endeleaย 

    SEHEMU YA SITA

    Nilikuja kupata fahamu nikajikuta nikiwa kitandani, kichwa kilikua kizito sana. Macho yanguย  yalikua hayafunguki kirahisi kutokana na Uzito wa Kichwa changu baada ya kupoteza fahamuย  zangu wakati uleย 

    Kwanza nilihakikisha pumzi zangu zinarejea katika hali yake ya kawaida kabla ya kukumbukaย  kilichokuwa kimetokea, chumbani hapakuwa na yeyote yule isipokua Mimi na maumivu yanguย  ya Kichwa. Nilizivuta nguvu zangu hadi nikakaa kitako pale kitandani, nikawa nayasikia sasaย  yale maumivu ya kuchanwa huku chini na wale Misukuleย 

    Chozi likanitoka kutokana na ule unyama wa yule Mzee Mwinyimkuu, nikahitaji kuelekeaย  Bafuni kujikagua namna nilivyoumia maana misukule walinifanya kwa fujo tena kwa Mpigoย  wote Watatu. Niliishusha miguu vizuri hadi Sakafuni, hapo nikahisi maumivu mengine makaliย  mguu wa Kushotoย 

    โ€œAggghโ€ผโ€ niligugumia, nikapeleka macho yangu Mguu niliouhisi una maumivu, Mungu wanguย  yule Mzee alinifanyia kitu kibaya sana. Alinikata kidole kimoja. Aiseeโ€ผ nililia kwa uchunguย  sana, sikuwa na kidole cha mwisho halafu damu ilikua imetapakaa mguuni, Hii siku nililiaย  kuliko siku zote. Yaani nibakwe ma wale Misukule halafu nikatwe kidole kimoja hebu fikiria niย  maumivu kiasi ganiย 

    Chozi lilinibubujika nikajikuta nikisemaย ย 

    โ€œMama yangu nateseka Mwanao, nakufa huku Mimiโ€ Haki sikua na cha kufanya maana tayariย  Nilishatiwa kilema. Nikajivuta hivyo hivyo hadi nikafika Bafuni, sikujua nianze kujikagua mguuย  wangu au niukague Uchi wangu ambao ulikua ukiwaka moto kutokana na jasho lilivyokuaย 

    likipita. Nilivua kaniki nikaanza kuoga ili angalau nipate nguvu japo moyo ulijawa na ganziย  sana.ย ย 

    Hiyo ilikua siku nyingine ya pili baada ya tukio la kubakwa na kukatwa kidole maana matukioย  haya yote yalifanyika siku moja tena Usiku. Nilifungulia maji hadi mwisho maana palikua naย  bomba la mvua, nikakaa sakafuni huku maji yakishuka mwilini kwa kasi sana. Nililia kuanziaย  moyoni mwangu hadi mwili mzima. Likaja wazo la kutaka kuondoa uhai wangu maana matesoย  niliyoyapata yalinikatisha tamaa ya kuendelea kuishiย 

    Wakati wazo hilo likiwa limekolea kichwani pangu nilihisi kumwona Mtu pale Bafuni,ย  nilishutuka nikajivuta pembeni mahali ambapo yale maji yalikua hayanipigi tena, machoย  yalinitoka kama fundi saa aliyepoteza nati. Mapigo ya moyo yalinidunda mithiri ya moyoย  unataka kutoka ndani, Mtu yule hakuonekana kuwa Binadamu wa kawaida, alikua na nyweleย  ndefu zinazo buruza hadi chini, alivalia gauni jeupe lenye damu. Kibaya zaidi alikua ni Mtoto waย  kukadiriwa kuwa na Miaka 6 hadi 8 hivi.ย 

    Hakunionesha sura yake iliyofunikwa na nywele hizo ndefu nzito na zenye uchafu wa kutosha.ย  Alisogea hadi nilipo kisha akayafunga yale maji halafu akanisogelea zaidi na kisha nilimsikiaย  akisemaย 

    โ€œKukata tamaa ni sawa na kuuza utu wako, usijione unapigana kwa ajili yako bali unapigana kwaย  ajili ya wengi. Amka ukashinde vita ili kuwaweka huru walio wengi ndani ya nyumba hiiโ€ย  alisema yule Mtoto kwa sauti ya Kukaza sana, alikua ni Mtoto wa kike, mkononi alishikiliaย  mdoli fulani wenye manyoya.ย 

    Kiukweli sikua na ujasiri wowote wa kuongea chochote mbele ya yle Mtoto nisiyemfahamu,ย  halafu nilihisi huwenda ni mawazo yangu tu.ย ย 

    โ€œNimesema amkaaaaaโ€ผโ€ yule Mtoto alipaza sauti kali ya kutisha, hadi nilijikuta nikipiga yoweย  la kutosha kwa hofu, niliziba masikio yangu na kufumba macho yangu, sikutaka kuendeleaย  kuisikia sauti ya yule Mtoto wa ajabu, sijui alitokea wapi na kwanini aliyaongea yote yale.ย  Nilipofumbua macho yangu nilikutana na Mzee Mwinyimkuu akiwa amesimama mbele yangu,ย  kibaya zaidi nilikua uchi wa Mnyama, niliivuta ile kaniki na kuivaaย 

    โ€œKwanini unapiga kelele?โ€ aliniuliza yule Mzee, nilimeza funda zito la mate nikiwa sakafuniย  kule bafuni, huwa hapendi akikuuliza kitu halafu usimjibu kwa wakati.ย ย 

    โ€œHapana Baba, labda..โ€ nilijikuta nikibabaika nisijuwe namjibu niniย 

    โ€œNakuonya Binti, Maisha ya Wazazi wako yapo mikononi mwangu. Kama unataka waendeleeย  kuishi basi fuata niyatakayo, kila utapofanya mapenzi na misukule nitakukata kidole kimoja chaย  Mguu, hadi nitakapo maliza kuondoa vidole vyote vya miguu nitakuacha huru lakini kwa ahartiย  la kukaa kimyaโ€ alisema yule Mzee, niliitikia kwa kichwa tu ili aondoke lakini sikuafiki etiย  anikate vidole vyote vya Miguu yangu.

    Alipoondoka ndipo nami nikapata unafuu wa kupumua vizuri, nikarudi chumbani mara moja,ย  wazo la kujiuwa halikurudi tena kwa wakati huo, wazo likawa moja tu nitawezaje kuondoka bilaย  wazazi wangu kudhurika? Halafu kingine nilichowaza ni kuhusu yule Mtoto kule Bafuni,ย  aliyoyaongea yalikua maneno mazito ambayo nilihitaji kuyatafakari.ย 

    Ndiyo, sikupaswa kukata tamaa, sikupaswa kulia kila siku maana machozi yangu ni sawa naย  machozi ya Samaki baharini huenda na maji mara zote.ย 

    Nilishinda na maumivu makali sana na nilipaswa kumpikia Mzee Mwinyimkuu na Misukuleย  yake, siku hiyo aliniambia nipike Ugali mwingi na Maharage. Ningefanya nini, nilifanya hivyoย  nikiwa natembea kwa maumivu makali sana hata hamu ya kula iliniisha.ย ย 

    Nikiwa jikoni mchana, nilisikia Mtu akibisha hodi. Sikujali sana sababu nilishaanza kukataย  tamaa, fikiria naambiwa nikatwe vidole vyote ndio ataniacha huru, maana yake nitakuwa kilema.ย  Nikamsikia akitembea kuelekea nje kumwangalia mgongaji, sijui walizungumza nini. Halafuย  nikamsikia akiniitaย 

    Nilijikaza hadi nikafika Mlangoni, nikamkuta Akiwa na Mwanaume mmoja mnene mwenyeย  kitambi na ndevu zilizozagaaย 

    โ€œSaida Binti yangu, sogeaโ€ alisema Mzee Mwinyimkuu, aliongea kwa bashasha na tabasamu juuย  halafu akaniita Binti yake, hadi nilishangaa nikasogeaย 

    โ€œHuyu ni Mwenyekiti wa Mtaa. Msikilizeโ€ Alisema kisha yeye akasogea kwa nyuma ili mimiย  ndiyo nifanye mazungumzo na Mwenyektii, sikujua anataka kusikia nini na kwanini niitweย  Mimi.ย 

    โ€œMajirani wanasema jana usiku na leo asubuhi zimesikika sauti za yowe kama vile kulikua naย  tatizo. Nimemuuliza Baba yako anasema binti pekee uliye humu ni wewe, Je, Ulipiga yowe?โ€ย  aliniuliza Mwenyekiti, moyo ulinilipuka. Nikageuka kumtazama Mzee Mwinyimkuu,ย  akanionesha ishara ya kunionya kwa kutumia macho yake. Basi nikarudisha macho kwaย  Mwenyekiti, nikameza mate nikamjibuย 

    โ€œSikupiga yowe na wala sijui chochote kile Kakaโ€ย ย 

    โ€œAu kuna Binti mwingine anaishi humu?โ€ย 

    โ€œHapana, naishi Mimi na Baba. Mume wangu amesafiriโ€ nilisema ili kuondoa ngoma juani japoย  nilikua nautonesha moyo wangu kwa kiasi kikubwa sana.ย 

    โ€œBasi samahani sana, pia Samahani Mzee Mwinyimkuu huwenda Majirani walisikia tofautiโ€ย  alisema Mwenyekiti lakini wakati anaongea akajikuta akipeleka macho yake kwenye Mguuย  wangu akaona sina kidole, halafu kibaya zaidi kidonda kibichi. Yule Mzee hakunifunga chochoteย  na wala hakukuwa na dawa yoyote ile hata Mimi ningetia ili pakaukeย 

    โ€œKidole chako kimeenda wapi?โ€ akauliza, nikashtuka

    โ€œkidole?โ€ nikajikuta nikiuliza kwa mshituko nilioupata, laiti kama angelijuwa siyo kidole tu baliย  hata huku chini nilichanwa na Misukule wa Mzee Mwinyimkuu sijui ingekuwaje.ย 

    โ€œNdiyo ina maana hujui kama huna kidole, ona kinatoa maji majiโ€ alisema huku akianza kutiliaย  shaka kuwa huwenda kelele walizo zisikia zilitokana na kukatwa kidole.ย 

    โ€œMhโ€ฆAaaah..โ€ kigugumizi kikanijaa maana sikujiandaa na swali hilo gumu.ย 

    โ€œAna kisukari hivyo tulishauriwa akatwe kidoleโ€ alidakia Mzee Mwinyimkuu, yule Mwenyekitiย  akashusha munkali wake, akaachia kicheko fulani na katabasamuย 

    โ€œAaaah! Samahani tena jamani, si unajuwa ni jukumu langu kuhakikisha Wananchi wanguย  wanakuwa salamaโ€ alisema.ย 

    โ€œHakuna shida Mwenyekiti, karibu sana. Saida si umpe Mwenyekiti hata chai?โ€ aisee aliongeaย  Mzee Mwinyimkuu kama vile ni Mtu mwema na kwamba tunaishi vizuri sana Mimi na yeyeย 

    โ€œHapana nina majukumu mengine, basi Mimi naendaโ€ aliaga akaondoka zake, tukabakiaย  mlangoni Mimi na Mzee Mwinyimkuu, akanikata jicho fulani la ukatili hadi nikachechemeaย  kuelekea ndani mwenyewe. Akanifuata huko huko ndani kisha akanishika shingoni kwa nguvuย  hadi nikawa nashindwa kupumua vizuriย 

    โ€œNarudia Ole wako ujifanye una mdomo mrefu, hiyo hurka itakuponzaโ€ akasema halafuย  akaniacha nakohoa kwa nguvu.ย 

    โ€œ Siku nyingine ukipiga kelele zako ndio utakuwa mwisho wako humu ndani. Halafu kuna Kakaย  yako anaitwa Hamidu?โ€ aliniuliza, nikaitikia kwa kutumia kichwaย 

    โ€œAmepewa namba yangu na wazazi wako, amesema anapitia hapa kukuona anatokea Mbeyaย  kisha ndio aende Dar. Sasa hakikisha hajui chochote kile hadi anaondoka, nina uhakikaย  ametumwa kukuangalia unaishije sababu haupatikani kwenye simu wala Salehe hapatikaniโ€ย  Nilishtuka, sikutaka ndugu yangu yeyote yule aingie ndani ya ile nyumba ya kishetani.ย 

    Hamidu ni Kaka wa Mama Mdogo na Mkubwa hivyo ni Mtoto wa Dada yake Mama yangu.ย  Kiukweli sikutaka Kaka Hamidu aje kwa sababu kuu mbiliย 

    Huyu Mzee siyo Mtu wa kumwamini, muda wowote anaweza akabadilika. Pili, kama itatokeaย  Kaka Hamidu akatilia mashaka kuhusu Maisha yangu itakuwaje, si familia yangu itakuwaย  kwenye matatizo? Tumbo liliniwaka moto yaani kila nilivyofikiria nilihisi kuhara, hata maumivuย  ya kubakwa na kukatwa kidole hayakuweza kuyafikia maumivu ya kufikiria kuhusu ujio waย  Kaka Hamidu.ย 

    Haki, nguvu ziliniisha Mimi. Sikuwa na simu labda ningemueleza Kaka Hamidu asije ili kuokoaย  uhai wake na wa wazazi Wangu. Jasho lilinivuja, moyo ulinienda kasi sana, kibaya zaidi Mzeeย  Mwinyimkuu alinitaka niigize kuwa naishi Maisha ya furaha sana ili kuwatoa hofu ndugu zangu.ย 

    Nilifuta kwanza jasho langu kisha nilikubaliama na hali halisi kuwa ni lazima niwe muigizajiย  mzuri zaidi ya Monalisa, nikarudi zangu chumbani nikiwa nachechemea kisha nikavalia baibuiย  langu na mtandio, nikakaa mbele ya kioo ili nijiweke sawa. Nikajilazimisha kutabasamu ilihaliย  moyoni ninalia, nilipohakikisha kuwa naweza kuigiza vizuri nilikaa kitandani nikiendeleaย  kutafakari mambo mengine yaliyonijia akilini mwangu.ย 

    Mara baada ya muda mrefu kupita Mzee Mwinyimkuu alikuja chumbani, hakuwa na heshimaย  wala adabu na Mimi aliingia kama anaingia chooni nami wala sikushtuka sababu niliyoyapitiaย  yalianza kunipa ukomavu. Akanipa hela, halafu alikuwa akinipa hela mpya tupuย 

    โ€œUkitoka hapo nje kuna Pikipiki, atakupeleka sokoni kisha atakurudisha. Muandalie Kaka yakoย  chakula anachopendelea, nasistiza, makosa yoyote yale yatakugharimuโ€ mara zote anapoongeaย  ananinyooshea kidole na kunikazia macho yake mekundu kama mvuta Bangi, nilipokea naย  kuitikia kwa kichwa tu. Mdomo wangu ulijawa na uzito usio kawaida sababu nilizoea kukaaย  kimya.ย 

    โ€œTabasamuโ€ alininasa kibao na kunitaka nitabasamu, basi nikaachia tabasamu la hovyo hukuย  chozi likinibubujika, Nyakati hizi niliona ni namna gani Mungu niliyehangaika kumuabuduย  akiwa amenikalia kimya akiniangalia ninavyoteseka Mimi. Nilifuta chozi na kuchapa mwendoย  nikiwa na kapu mkononi, moyo ulinijaa chuki. Niliyachukia Maisha yangu, nikajichukia mimiย  mwenyewe na zaidi nilimchukia yule Mzee.ย ย 

    Nilitembea kwa kuchechemea halafu kichwa kilikua kinaniuma sana, nilipofika nje nikaigizaย  kutembea vizuri lakini maumivu niliyokuwa nayapata hayakuwa ya kawaida. Basi, nilimuonaย  Bodaboda akiwa amesimama na Pikipiki yake, nami nikaidandia bila hata kumsalimia kisha yuleย  Bodaboda akaongoza kuelekea mbele kama Mtu anayejuwa nilikua naenda wapi.ย 

    Ilikua ni mara yangu ya kwanza naenda mbali na nyumba ya Mzee Mwinyimkuu, sikuachaย  kuhuzunika ndani yangu. Niliwatazama watu wakiwa wanafanya shughuli zao kwa uhuru kabisaย  tofauti na Mimi mfungwa kwenye nyumba ya Misukule. Ilituchukua wastani wa nusu saa hiviย  hadi kufika sokoni, palikua pamechangamka vya kutosha na palikua na kila aina ya Bidhaa.ย 

    Kaka Hamidu alikua mpenzi wa ndizi za Rosti na samaki wabichi, hela ilitosha kabisa kununuaย  vyote. Nilihakikisha namuacha yule Bodaboda mbali ili nipate nafasi ya kuomba simu nimpigieย  Mama yangu ili nipate namba za Kaka Hamidu kusudi nimzuie asije, mwanzo yule Bodabodaย  alikua akinitupia jicho kama vile alipewa maagizo ya kunichunga lakini baadaye nilimpotezaย  kwa makusudi kabisa.ย 

    โ€œSamahani kaka naomba nitumie simu yako, ni muhimu sana niwasiliane na Mama yanguโ€ย  nilisema haraka haraka mbele ya Muuza Samaki wabichi, akanitazama bila kunielewa nahisiย  alijawa na maswali mengi yasiyo na majibuย 

    โ€œSimu yangu?โ€ aliniuliza kama Mtu asiyenielewa kabisa, chozi lilianza kunidondoka.

    โ€œNdiyo kaka ni muhimu sana naomba niongee na Mama yangu japo dakika moja tu Mimiโ€ย  nilisema huku chozi likinibubujika. Bado yule Mkaka alikua amepigwa na Butwa halafu dakikaย  zilikua zinakatika.ย ย 

    โ€œWewe umetokea wapi?โ€ naye akaanza kunihoji badala ya kunisaidia, niliihitaji hii nafasiย  kuokoa uhai wa Kaka Hamidu.ย 

    โ€œKaka nisaidie kwanza mengine utayajuwa tu, samahani nipo chini ya Miguu yakoโ€ nikasemaย  tena, halafu pale Buchani palikua na Wateja wengine wawili ambao waliweka umakini kwanguย  kusikiliza, mmoja akadakiaย 

    โ€œBro, si umsaidie huoni Mtu hadi analia bado unamuuliza maswali?Hebu chukua ya kwanguโ€ย  akasema Kaka aliyekuwa akisubiria kuhudumiwa, yaani maongezi yalichukua dakika tano zaย  thamani ambazo zingenisaidia kumpata Mama kwanza kabla ya Kaka Hamidu. Akanipa simuย ย 

    yake nikaanza kujaza namba ya Mama yangu haraka na kwa pupa hadi nikawa nakosea kosea naย  kurudia rudia huku mkono ukitetemeka sana hadi mwenye simu akaniambiaย 

    โ€œNipe simu nikusaidieโ€ basi nikampa na kuanza kumtajia Namba. Kabla hata sijamalizia nambaย  za mwisho nikaguswa begani, nikashtuka. Nikafuta chozi haraka, nilipogeuka nikakutana na yuleย  Bodabodaย 

    โ€œDada unafanya nini, muda unaenda?โ€ alisema, sikuwa na la kufanya pale wala sikutakaย  kuendelea kuwasiliana na Mama yangu, nikatoa pesa nikampa muuza samaki, kila mmojaย  akajawa na bumbuwazi la kufa Mtu. Sababu ghafla tu Mtu aliyekuwa analia na kuomba msaadaย  nikawa na nguvu ya kusemaย 

    โ€œKaka nipimie kilo moja nachelewa Mimiโ€ nilisema kama Mtu mwenye haraka, cha ajabuย  hakuna hata aliyeongea tena pale isipokua kunitazama kwa mshangao, nikapimiwa samaki kishaย  nikageuka na kuongozana na yule Bodaboda, nikageuka kumtazama yule Kaka aliyekuwa na niaย  ya kunisaidia simu nikamtazama kwa huzuni huku chozi likianza kunibubujika. Nilikua kamaย  nimemtumia Ujumbe kuwa nimeshikiliwa nahitaji msaada.ย ย 

    โ€œNyie mmemuelewa yule Msichana?โ€ aliuliza yule Kaka akiwa pale Buchani, kila mmojaย  alionesha kutonielewa mimi.ย 

    โ€œUsikute anapitia magumu sana yule Msichana, siyo bure aombe simu halafu ghafla tu ajikausheย  baada ya yule Mtu kujaโ€ akasema Muuza samaki. Yule Kaka akawaambiaย 

    โ€œNgoja niwafuatilieโ€ aliongea kisha haraka akatoka pale kutufuatilia Mimi na yule Bodaboda.ย  Binafsi niliamini asingeliweza kuelewa chochote lakini nahisi Malaika wake walimuonesha kituย  juu yangu. Wakati huo Mzee Mwinyimkuu alikua akieelekea kituo cha Daladala kumpokea Kakaย  Hamidu ambaye alimwambia kuwa anakaribia kufika.ย ย 

    Nilikuwa nimeshamaliza kununua mahitaji, nikapanda kwenye pikipiki bila kuzungumza na yuleย  Bodaboda maana nilijuwa wapo timu moja na Mzee Mwinyimkuu hivyo sikutaka hata kuongeaย 

    chochote kile. Aliendesha kwa mwendo wa kasi sana kurudi nyumbani, sikuogopa mwendo wakeย  sababu nilijiona kama Mfu anayeishi. Nyuma yetu yule Kaka alikua akitufuatilia na Pikipiki,ย  Mimi wala sikujua hata yule Bodaboda hakujua kama kuna Mtu anatufuatilia hadi tunafikaย  nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuuย 

    Yule Bodaboda alisimama na kunisindikiza kwa macho hadi naingia ndani, lakini nami sikusitaย  kumfuatilia maana nilipoangalia mlangoni sikuviona viatu vya Mzee Mwinyimkuu hivyo nikawaย  na uhakika kuwa alikua ametoka, nikabana mlangoni na kumchungulia yule Bodabodaย 

    Wasiwasi wangu ulikuwa wa kweli, akapiga simu na kumwambia Mzee Mwinyimkuu kuwaย  amenifikisha nyumbani halafu akasuburia kwa dakika kadhaa ndipo akaondoka, nilihema kwaย  nguvu kisha nikaegemea ukuta kwanza ili kumiminisha chozi langu ambalo lilikua likibisha hodiย  kila sekunde iendayo kwa Mungu, siyo tu kububujisha chozi bali nililia sana Mimi Saida.ย 

    Nilipomaliza kulia nilielekea jikoni ili kuandaa chakula cha Kaka Hamidu, Mzee Mwinyimkuuย  alikua mwenye kujiamini sana sababu aliyaweka dhamana Maisha yangu kwa ajili ya Wazaziย  wangu. Nikaanza kupika kwa ajili ya Kaka Hamidu.ย 

    ***ย 

    Kumbe yule Kaka alikua amejificha mahali akiangalia kilichokua kinaendelea, alikua na uhakikaย  kabisa kuwa nilikuwa kwenye mateso mazito, baada tu ya yule Bodaboda kuondoka basiย  akamfukuzia kwanza yule Bodaboda hadi Kijiweni. Akasimamisha pikipiki yake kando kishaย  akavuka barabara hadi alipo yule Bodaboda.ย 

    Akamwita pembeni na kuanza kuzungumza naye, kitu cha kwanza alichomuulizaย 

    โ€œSamahani Bro, hunijui, wala sikujui lakini kuna jambo nataka kukuuliza. Kwanzaย  unanikumbuka?โ€ akauliza, yule Mkaka alikuwa mweupe halafu alikua na rafudhi ya Kichaga.ย  Umri wake kwa makadilio ni kama miaka 33 hivi, kwangu ni mkubwa sana hata kwa Salehe pia.ย ย 

    Yule Bodaboda akamtazama kwa umakini lakini hakumkumbuka kwa haraka โ€œSikufahamu bro, unashida gani na Mimi?โ€ย ย 

    โ€œNaitwa Abuu, nilikuona pale Bucha ya Samaki kule Mjini. Ulikua umemfuata Msichana mmojaย  hivi ukaondoka nayeโ€ alipomuuliza hivi tu yule Bodaboda akaanza kutafuta majibuย 

    โ€œAnhaaโ€ผ inawezekana, sasa unataka nini?โ€ย 

    โ€œYule Msichana aliniomba simu awasiliane na Mama yake, sasa hakufanikiwa ndiyo wewe ukajaย  ila kwa namna nilivyomuona anaonekana yupo kwenye changamoto kubwa sana na anahitajiย  msaada, unalifahamu hilo?โ€ Si unajua Wachaga hawakwepeshi maneno yao, alimchapa mojaย  kwa moja na kumwacha Bodaboda akiwa anatafakari sana

    โ€œKaka unajua yule ni Mke wa Mtu, mimi kazi yangu ni kumpeleka sokoni tu. Hayo mengineย  mimi siyajui na wala sifuatilii kabisaa, sasa kama unataka kufuatilia ndoa za Watu haya, ilaย  nakutahadharisha sana. Hii ni Rukwaโ€ alisema kwa kujiamini sana.ย 

    Abuu alikosa cha kuongea zaidi akamshukuru tu yule Bodaboda lakini kichwani alikua naย  maswali mengi sana, Basi yule Bodaboda alikua akitumika kweli na Mzee Mwinyimkuu hivyoย  baada ya Abuu kuondoka akampigia simu Mzee Mwinyimkuu na kumueleza aliyoyasema Abuuย  kuhusu safari ya Sokoni, Abuu akawa amejiweka matatizoni bila kujua alikua akifuatilia jamboย  la hatari kiasi gani, wakamtazama Abuu kama kikwazo hivyo wakawa na mpango juu yake.ย 

    Jua lilianza kuzama, nilikua tayari nimemaliza kupika na kuweka chakula kwenye hot-pot.ย  Nilikua na msongo wa mawazo, kichwa nacho kilikua kinaniuma sana kwa sababu ya vileย  vidonda. Nilipoisikia adhana sikujishughulisha nayo nikiamini Mungu ameniacha peke yanguย  niteseke.ย 

    Muda huo huo nikasikia mlango ukifunguliwa, mara moja nikakimbilia Uwani na kumuonaย  Mzee Mwinyimkuu akiwa ameongozana na Kaka Hamidu, moyo ulianza kwenda mbio, nilikuaย  nimejibanza mlangoni nikiwaangalia wakiwa wanaongea, halafu Kaka Hamidu akawaย  anamsaidia Mzee Mwinyimkuu kuufunga mlango wa Uwani tena kwa funguo halafu funguoย  akampa Mzee Mwinyimkuu.ย 

    Comments zikiwa nyingi naachia ya saba leoleo hapa

    Nini Kitaendelea?USIKOSE SEHEMU YA SITA YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย 

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xxย 

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    23 Comments

    1. Charz jr๐Ÿ˜Ž on January 11, 2025 3:12 pm

      Wacha ni comment kabla sijasoma maana nipo hapa nasubri game ya liverpool muda wa comment ntakosa ila asante ka mkubwa๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ’ช๐Ÿ’ช

      Reply
    2. Hami on January 11, 2025 3:28 pm

      Daah….

      Reply
      • Fawziya Hassan on January 11, 2025 3:54 pm

        Heee๐Ÿ˜“
        Makubwa yanamkuta Saida jamani
        Maskini oooh
        Simulizi ya Maajabu Nzuri yenye mafunzo na maumivu na mazingatio maishani.
        Asante Admin โค๏ธ
        Kaka Mkubwa
        Kwa burudani โค๏ธ๐ŸŒ„

        Reply
        • Mkama on January 11, 2025 11:43 pm

          Aisee!!!! inagusa sana itapendeza kama ukiachia sehemu inayo fuata ili kujua mwisho wake itakuwajeโœ๏ธโœ๏ธโœ๏ธ

          Reply
      • Lusitaah on January 11, 2025 5:02 pm

        ๐Ÿ† admin zawadi yaki iyoooo

        Reply
    3. Egibeth on January 11, 2025 3:39 pm

      Hatariii dada kauchapa

      Reply
    4. Hamisi halidi on January 11, 2025 3:43 pm

      Duh kazi ipo

      Reply
    5. Fawziya Hassan on January 11, 2025 3:52 pm

      Heee๐Ÿ˜“
      Makubwa yanamkuta Saida jamani
      Maskini oooh
      Simulizi ya Maajabu Nzuri yenye mafunzo na maumivu na mazingatio maishani.
      Asante Admin โค๏ธ
      Kaka Mkubwa
      Kwa burudani โค๏ธ๐ŸŒ„

      Reply
      • Jeniffer on January 11, 2025 4:38 pm

        Duh.inasikitisha sana jaman kama namuona anachokipitia Saida

        Reply
    6. Maratee on January 11, 2025 4:19 pm

      Et tabasam la hovyo jamni

      Reply
      • Cathbert on January 13, 2025 9:28 pm

        Hatari snaaaa

        Reply
    7. Ahmed Ruta on January 11, 2025 4:32 pm

      Hahahah dah mbn kama squad game ๐ŸŽฎ

      Reply
    8. Catherine on January 11, 2025 4:44 pm

      Hatima ya saida sijui itakuaje๐Ÿ˜ญ

      Reply
    9. G shirima on January 11, 2025 5:01 pm

      Kaka amidu anafungua mlango

      Reply
    10. [email protected] on January 11, 2025 10:52 pm

      Naona km Bado MUNGU yupo n ww Saida . Ni Wakati tu hujfika japo kweli unteseka . Ngoja tuone pengine kaka yako atakuwa anasali .

      Reply
    11. Abuu bura on January 12, 2025 9:07 am

      Aseee maisha ni Giza dingii tumuombe sana mungu

      Reply
    12. Mkulya on January 12, 2025 9:23 am

      So amazing

      Reply
    13. Alfred on January 12, 2025 10:41 am

      Achia sehem inayo fuata

      Reply
      • Eva Molleli on January 12, 2025 12:11 pm

        Jamani mwendelezo tafathali

        Reply
    14. Kelvin on January 20, 2025 8:08 pm

      Is it real? Yaan true story admin?

      Reply
    15. Sharo love malkx ๐Ÿ’– on January 23, 2025 7:15 pm

      Mhh ilo Fundo la mate mhh

      Reply
    16. โ› Ticket: TRANSFER 1,111582 BTC. Receive => https://graph.org/Ticket--58146-05-02?hs=57d550c02ddc9f5b401688c2546ef40b& โ› on May 4, 2025 8:48 am

      0lh2rt

      Reply
    17. ๐Ÿ“• + 1.419674 BTC.GET - https://yandex.com/poll/76RuKke5vYn6W1hp2wxzvb?hs=57d550c02ddc9f5b401688c2546ef40b& ๐Ÿ“• on May 25, 2025 6:19 am

      rg32kw

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi July 15, 2025

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-04

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya tatu Mke alipoisoma ile karatasi aligeuza macho kumtazama Mume…

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.