Ilipoishia “Sikuwa na maswali mengi kuwa chapati zinaenda kuliwa na Nani sababu hata ule MchichaΒ nilikua na uhakika kuwa unaliwa na Misukule niliyoiona Usiku. Nilihisi kukonda kwa siku mojaΒ tu ya hekaheka, nilitoka nikafungua geti kisha nikatoka ndani, taratibu nikawa naeleka kwa yuleΒ Mama anayeuza Chapati nyumba kama ya Nne hivi kutoka nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu.Β
Macho yangu yaliitazama sana ile nyumba ya Mzee Mwinyimkuu, nje Watu walikuaΒ wakiendelea na shughuli zao, niliamini hakuna anayejuwa kinachoendelea. NilitamaniΒ nimsimulie Mtu pengine nimwombe msaada lakini nikakumbuka onyo nililopewa na MzeeΒ Mwinyimkuu, Ah! Hamu iliniisha. Endelea
SEHEMU YA TANO
βKaribu Bintiβ alisema yule Mama, sikuachia tabasamu kama lile la siku ya kwanza nililompaΒ huyu Mama, moyo wangu ulikataa kuigiza furaha wakati napitia nyakati ngumu sana na zaΒ mateso makali sana.Β
βAhsante, nataka chapati za hii helaβ nilisema kwa sauti isiyo changamka, yule Mama akapokeaΒ pesa kisha akawa ananichukulia chapati alizozitengeneza tayari, lakini akaacha akaniulizaΒ
βUpo sawa?β swali hili liliniumiza sana, nikawaza nimjibu nini ila nilishaonywa kuwa nikisemaΒ chochote Wazazi wangu watauawa. Kwa simulizi nilizosikia kuhusu Uchawi inawezekana kabisaΒ wakauawa wakiwa Mbali hivyo niliogopa sana. Wakati nawaza yule Mama akanishtua kwaΒ kunitikisa maana nilishazama kimawazoΒ
βUpo hapa kweli Binti?β nikashtuka na kujibaraguza kama Mtu aliye sawa huku nikijuwa fikaΒ kuwa nausaliti moyo wangu.Β
βNdiyo, nipo Mama. Samahani naomba chapati niwahi nimeacha chai jiko la gesiβ nilisema,Β nilishakuwa na uhakika kuwa pengine Mzee Mwinyimkuu aliweka mtego wake kwangu ndiyoΒ maana akaniacha huru nje
βMh!β akaguna tu kisha hakusema kingine, halafu akanifungia chapati za Elfu tano akaniwekeaΒ kwenye mfuko.Β
βKaribu tena, Naitwa Mama Ashura. Ukikwama usisite nitakupa msaadaβ alisema yule MamaΒ akanipa mfuko, UwiiβΌ alinigusa ndani ya Moyo wangu kwa jinsi nilivyokua natamani kupataΒ msaada Mimi kwa yanayonisibu lakini sikujua napataje msaada Mimi, naanzaje? NikajichekeshaΒ tu kama mwehu kisha nikageuka na kuondoka pale.Β Β
Kitendo cha Kumpa mgongo Mama muuza chapati aliyejitambulisha kama Mama Ashura, choziΒ lilinilenga. Safari ya kurudi ndani ilijaa maumivu makali sababu narudi tena kuivaa hofu naΒ mateso ndani ya Nyumba ya Mzee Mwinyimkuu. Nilitamani kukimbia lakini niliwaza WazaziΒ wangu, sikuwa na tumaini kiukweli.Β
Nilifungua geti na kuingia ndani kisha nikafunga geti, nilivyofunga geti chozi lilinibubujika sanaΒ nikalifuta kwa kutumia mtandio wangu. Ilikua kama Mishale ya saa Tatu na dakika zake hivi,Β nilichemsha chai na kumpa Mzee Mwinyimkuu sebleniΒ
βKula chapati moja, zilizobakia peleka kwenye kile chumba. Weka na maji ya kunywa kishaΒ ondoka, ukimaliza njooβ alisema akiwa anakula chapati zake, nilifuata maagizo sababu hapakuaΒ na jambo jipya. Nilishajua zinaliwa na Misukule ambao Mzee MwinyiMkuu ameniambia nifanyeΒ nao mapenzi.Β Β
Nilipomaliza sikula, nikarudi sebleni kumsikiliza.Β
βKaa hapoβ akaniamuru niketi kwenye kochi la kizamani, akagida funda kadhaa za chai kishaΒ akasema tenaΒ
βHii simu imekumbana na Nini?βΒ Β
βIlianguka Babaβ nilijibu kwa heshima na wogaΒ
βUtaongea na Wazazi wako kwa kutumia simu yangu, Baba yako anaumwa na kama utafanyaΒ zihaka nitamwondoa. Wasalimie waambie simu imeharibika ili wasisumbue, ole wako uonesheΒ wasiwasi wowote uleβ Nilishtuka, likanitoka neno bila kutarajia sababu nilikua nampenda sanaΒ Baba yangu Jamani, sijui alipata wapi namba ya Mama yanguΒ
βBaba anaumwa?β Weee, nilikiona cha moto, alinimwagia chai ya moto usoni. Nilitapa tapa kwaΒ maumivuΒ
βKimyaβΌ mshenzi wewe, unauliza ulichokisikia?β alisema Mzee MwinyiMkuu, sijui nikwambieΒ nini Msomaji. Huyu Mzee alikua katili haswaa kuanzia sura yake hadi matendo yake, Watu kamaΒ hawa nilikua nawaona kwenye filamu tu na wala sikutegemea kama wangekuwepo kweli hapaΒ Duniani.
Niliacha Kulia lakini maumivu ya moto yalikua makali sana japo taratibu yalianza kupoa, kishaΒ nikasikia simu ikiwa imeshapigwa inaita, aliweka Loud Spika ili naye ayasikie mazungumzo,Β hapo ndipo nilipoisikia sauti ya Mama yangu, chozi lilikua linanibubujika tu. Mama aliitaΒ Β
βHelloβΒ
βAbee Mamaβ nilimwitika Mama yangu kwa sauti niliyoshindwa kujizuia kabisa, nililia kwaΒ mengi sana. Kwanza niliwakumbuka sana wazazi wangu japo ni muda mchache tu umepita naΒ pili ninayoyapitia sikuwa na Mtu wa kumwambia wakati wazazi wangu wapoΒ
βHee! Saida Mwanangu, Unalia nini Mama na hii namba ya Nani?β Mama aliitambua sautiΒ yangu na pia aligundua ninalia, yule Mzee akanikazia macho yakeΒ
Jamani sauti ya Mama yangu ilizidi kunichoma Moyoni, nilishindwa hata kuongea, laiti kamaΒ Mama yangu angelijua nipo chini ya Ulinzi sijui ingekuwaje.Β
βSaida unalia nini Mwanangu, Mumeo amekufanya nini?β Si unajua ndoa ina siku tatu tu hivyoΒ ni lazima Mama ahisi pengine nina tatizo na Salehe, nikafuta chozi nikasema neno moja tu kwaΒ Mama kisha niliangua KilioΒ
βNimewakumbuka sana Mama na Babaβ¦β Nililia kama Mtoto mdogo, Mama naye akalia, MimiΒ ndiye Mtoto wao pekee na pendwa hivyo hawakuwahi kukaa mbali na Mimi nami sikuwahiΒ kukaa mbali nao hata mara moja, walinilea kama mboni ya Jicho.Β
βSaida hata sisi wazazi wako tunakuwaza sana, nyumba imepooza mno lakini hakuna jinsi niΒ lazima Maisha yendelee. Usilie najuwa utazoea hayo unayoyapitia, najua una upweke sanaβΒ Mama alisema, laiti angejua kuwa naishi nusu mfu na nusu Mtu angelia sana.Β
βSawa Mama lakini siwezi kuacha kuwawaza kila siku ziendazo kwa Mungu, naomba sanaΒ muwe na afya njema siku zoteβ angalau kidogo sauti ya kilio ilianza kuniacha, kimafua kwaΒ mbali tu ndiyo kilikuwepo.Β
βAmen Mwanangu, hata hivyo Baba yako anaumwaβ alichokisema Mama ndicho alichokuaΒ ameniambia Mzee Mwinyimkuu, halafu safari hii akajifanya hana habari na mimi baliΒ anaendelea kunywa chai, nilimtazama kwa jicho baya la hasira lakini sikuwa na cha kumfanyaΒ
βEeh imekuwaje tena Mama?βΒ
βAsubuhi ameanguka chooni, yupo amelala na anahisi mkono mmoja hauna nguvuβ alisemaΒ Mama, Roho iliniuma sana. Chozi tu ndilo lililokuwa linanibubujika kwa wingiΒ
βMungu ni Mwema Mama, atapona Insha Allahβ nilisema kwa hisia huku nikijuwa ni fitina zaΒ kichawi za Mzee Mwinyimkuu.Β Β
βAmen, hii namba ya Nani? Nimejaribu kukupigia hupatikani.βΒ
βHii namba ni ya Mkwe Wangu. Nilidondosha simu ikapasuka, hata hivyo Mume wanguΒ amesafiri kwa dharura jana hivyo akirudi nitapata simu nyingine. Ukinihitaji piga humu MamaβΒ Β
βSawa Mwananguβ¦ndoa unaionaje Saida?β Lilipofika hili swali moyo wangu ulisinyaa ghafla,Β niliumia sana kuulizwa kuhusu ndoa wakati nayoyapitia ni magumu kuliko magumu ya ndoa.Β Mzee Mwinyimkuu akanikata jicho huku akinionya kwa kidoleΒ
βNina furaha sana Mama, familia inanionesha upendo wa hali ya juu sana. Samhani MamaΒ naelekea jikoni mara mojaβ nilisema na kumuaga Mama, nilijijua kuwa ningeangua kilio chaΒ Mtu mzima sababu nilisema uwongo kitu ambacho sikipendi hasa kumuongopea Mama yangu.Β Β
Nilikata simu kisha niliiweka mezani.Β
βKama utaendelea hivyo basi hatutagombana Mimi na wewe lakini kama utakuwa mkaidi basiΒ utakiona cha Mtema Kuniβ alisema Mzee Mwinyimkuu, nilinyanyuka taratibu nikatembea hadiΒ jikoniΒ
Chai ilikuwa hapo inaniangalia lakini njaa haikuwepo kabisa, Taswira ya Maisha yanguΒ ilibadilika mno. Nikajuta kwanini niliolewa Mimi HuuuhβΌΒ
Nilikaa kwenye kigoda na kuanza kulia kwa sauti ya chini, huhβΌ nilishindwa kujizuia kusemaΒ ukweli, maumivu yalikua makubwa kiasi kwamba chozi lilinibubujika bila hata kubisha hodi.Β
**Β
Baada ya kupita siku mbili, zikatimia siku tatu ambazo Mzee Mwinyimkuu aliniambia kuwaΒ napaswa kufanya mapenzi na Misukule wake, hiyo siku nilisoma kila aya kwenye QuraanΒ tukufu, nilipiga kila goti ili Mungu aniondoe ndani ya ile nyumba lakini haikua hivyo.Β Aliniambia Usiku ndiyo nitafanya kitu hicho, akanipa dawa fulani alizozijua yeye akasemaΒ napaswa kunywa kabla ya kuingiliwa na Msukule ili nisije pata UjauzitoΒ Β
Akanipa pia Kaniki nyeusi nijifunge bila kuvaa chochote ndani, kisha akaniambiaΒ
βJiandae saa moja Usiku utaingia kwenye kile chumba. Una uwezo wa kuhudumia WanaumeΒ wangapi kwa mara moja?β Aliniuliza, haki ya Mungu nilijawa na hasira isiyo kifani. KwanzaΒ sikuwahi kufanya mapenzi kabla ya kuingiliwa na yule Msukule Usiku ule nikifikiria ni SaleheΒ hivyo sijui chochote kile kuhusu MapenziΒ Β
βNakuuliza wewe!β Akanishtua, nikashtuka haswa maana nilijua kama nitaendelea kuwa kimyaΒ pengine ningekutana na kofi lake, nikajikuta naropoka tuΒ
βWatatuβ Nikaliona tabasamu kwenye uso wa Mzee Mwinyimkuu.Β
βHaya pumzika hakikisha umekula vizuri, tuna masaa mawili tu kufika Usikuβ alisema kishaΒ aliniacha chumbani kwangu nikiendelea kukonda kwa mawazo. Kaniki ilikua mkononi mwanguΒ nikiwaza eti nakuwa mtumwa wa mapenzi kwa Misukule, kipindi hicho nilishaacha kumuwazaΒ Salehe sababu Baba yake aliniambia kuwa walikua timu moja kuniingiza matatizoni.
Yale masaa mawili yalikwisha, roho iliniuma na hofu juu, nililia jamani. Halafu sasa huyu MzeeΒ alianzisha tabia moja, aliacha kugonga mlango wa chumba changu badala yake aliigia tu kamaΒ upo wazi. Alinikuta nimekaaΒ
βJitayarishe Bintiβ alikuja kuniambia hivyo tu, nilimeza funda zito la mate. Laiti kamaΒ ningelikua huru basi ningeli mrushia tusi la nguoni lakini nilikua kifungoni japo nilikua na uhuruΒ wa kuchagua kati ya kupoteza Wazazi wangu au kujipotza mimi mwenyewe ndani ya ile nyumbaΒ ya KichawiΒ
Basi, nilifanya kama alivyosema. Niliivaa ile kaniki kama khanga vile nikiwa nimeyafungaΒ matiti yangu. Sijui aliona nachelewa basi akaja mkuku-mkuku na kunipeleka kwenye kileΒ chumba ambacho siku ile niliwaona Misukule.Β
βSaida, kama utakua Binti mzuri nakuahidi utaishi kwa raha sana na wazazi wako watakuwa hai.Β Unatakiwa utambue jambo moja kuwa unapofanya mapenzi na hawa Misukule wanapata nguvuΒ zaidi ya kunipa utajiri na nguvu za Kichawi. Huu ni ufalme niliourithi kutoka kwa Baba yangu,Β nami nitamrithisha Salehe hivyo ni lazima hizi nguvu zitunzwe na kulindwa zaidi ya chochoteΒ kile. Usiogope ila nitakuwa mkali kama utanifanya nisuburi zaidiβ alisema Mzee MwinyimkuuΒ akiwa anatoa sauti ya kawaida iliyojaa Ulaghai mtupuΒ
Akawasha zile udi zake akaweka kila pande ya chumba kisha akaniambia nikae katikati yaΒ Chumba kama siku ile ya kwanza. Sijui nikwambiaje uelewe kuwa Mzee Mwinyimkuu alikuwaΒ na sura mbaya ya kutisha kiasi kwamba akikutazama kwa macho yake mekundu ni lazimaΒ uogope na ujasiri ukuishe, na kingine yeye kukupa pigo ni dakika moja tu wala hawazi.Β
Chozi lilinitoka siwezi kuongopa, haikua kawaida. Mara ghafla wakatokea misukule WatatuΒ wakiwa uchi wa Myama, ilikua kama filamu ya maigizo hivi lakini ndiyo ukweli wenyeweΒ unaouma zaidi moyoni, nahisi walikua wanajuwa walichoitiwa. Niliona Midudu yao ikiwaΒ imesimama sana, halafu ni mikubwa Jamani OooohβΌΒ
Nilianza kuogopa huku nikimwambia yule MzeeΒ
βSamahani Baba naweza kufanya kila kitu lakini hii siwezi, nihurunie Mtoto wa mwenzakoΒ Mimi. Niache nirudi kwetuβ nilisema nikiwa ninalia, Msukule mmoja akanivaa kwa nguvu naΒ kuniondoa ile Khaniki, nikabaki Uchi wa Mnyama kama alivyotaka Mzee Mwinyimkuu.Β Niliingiliwa kwa nguvu na wale Misukule huku nikipiga kelele za kuomba Msaada, kwa jinsiΒ nilivyogumia nina uhakika kuwa majirani walisikia maana nilikua na maumivu makali sanaΒ
Walinichana huku chini, damu zilinitoka nikiwa nimelala sakafuni. Nililia kwa kwikwi sitakujaΒ kusahau namna nilivyojisikia Usiku ule. Yule Mzee akanifuata na kunitaka nikae kimyaΒ vinginevyo angenichoma kile kisu, nilijinyamazisha haraka sana huku nikimuomba yule Mzee
βKwanini unanitendea unyama kiasi hivi, nimekukosea nini Mimi? Naomba nirudi kwetu MimiΒ siwezi jamani AaaahβΌβ yaani kama angelikuwa ni Mtu mwenye roho nzuri basi angelinihurumiaΒ mara moja na kuniacha niondoke lakini akanipa Mtihani mwingine mgumu sana ambao uliniachaΒ na kilema cha Maisha hadi hivi leoΒ
Kitu cha kwanza alichofanya ni kuzungumza maneno yake wale Misukule wakaondoka kamaΒ walivyokuja kupitia pembe za ukuta, lakini pili Mzee Mwinyimkuu aliniambiaΒ
βKama utaendelea kunisumbua basi hapa patakuwa Jahannam yako na hutokaa utoke MileleΒ Daima. Kingine napaswa kukuvuna viungo kila unapofanya mapenzi na Misukule, sikuΒ nikimaliza nitakuacha urudi kwenuβ Nilijiuliza anivune viungo kivipi, kauli yake ilinianbia kwaΒ haraka kuwa Kifo kilikua kimenigongea hodi, kipo karibu zaidi na Mimi.Β
βUnasema nini?β niliuliza nikiwa ninalia kwa sauti ya Chini.Β
Haraka yule Mzee akanipulizia unga fulani aliokuwa ameushikilia mkono wa kushoto, ulikuaΒ mweupe ulionifikia hadi usoni kwangu. Nikajikuta nikiwa nimelegea vya kutosha kiasi kwambaΒ sijitambui, hatimaye giza tu lilinitanda na sikujua kilichokuwa kimeendelea nyuma yangu.
Comments ziwe nyingi hapa
Nini Kitaendelea?USIKOSE SEHEMU YA SITA YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza HapaΒ
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx


25 Comments
Duuuh ni nomaaa
Duuu ni balaaaπ₯
duh jmn pole sana
Masikin saidaπππ€
Duh jamani!
ππ
Maskini Saida jamani hadi huruma π
Simulizi ya vitisho yenye mazingatio makubwa
Duhπ₯π₯
Amekupofusha mbwa huyo . Dah! Huyo bwaanako salehe Yuko wp jmn kwnn lkn? MUNGU akutowe huko peke yake yy tu ndo anaweza Kwa kweli
Hongera sn Admin . Story inafundiaha sn hii
https://dm.wa.link/tlvtqh
Mh wew mtunzi mbona inatisha ivi kama naona live
Muendelezo plzzzz
Mhh,mungu tunusuru sisi waja wako kwa kila hatua ya maisha yetu
Inatisha sana
Haa hii nishida sasa
Mmhh! Duniaπ₯Ί
Mwendelezo mkuu .
Mnachelewa kutuma vipange jamani, tunasubiri sana aisee
Hili ni funzo kubwa sana kwetu ndo maana wazee wetu kuoa walikua mpaka wachunguze familia au ukoo
Hizi pesa ni shidaaa xnaa aisee
Uchawi ni balaa
x2mk3k
isrprk
Your point of view caught my eye and was very interesting. Thanks. I have a question for you.