Ilipoishia “Sikuwa na maswali mengi kuwa chapati zinaenda kuliwa na Nani sababu hata ule Mchichaย nilikua na uhakika kuwa unaliwa na Misukule niliyoiona Usiku. Nilihisi kukonda kwa siku mojaย tu ya hekaheka, nilitoka nikafungua geti kisha nikatoka ndani, taratibu nikawa naeleka kwa yuleย Mama anayeuza Chapati nyumba kama ya Nne hivi kutoka nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu.ย
Macho yangu yaliitazama sana ile nyumba ya Mzee Mwinyimkuu, nje Watu walikuaย wakiendelea na shughuli zao, niliamini hakuna anayejuwa kinachoendelea. Nilitamaniย nimsimulie Mtu pengine nimwombe msaada lakini nikakumbuka onyo nililopewa na Mzeeย Mwinyimkuu, Ah! Hamu iliniisha. Endelea
SEHEMU YA TANO
โKaribu Bintiโ alisema yule Mama, sikuachia tabasamu kama lile la siku ya kwanza nililompaย huyu Mama, moyo wangu ulikataa kuigiza furaha wakati napitia nyakati ngumu sana na zaย mateso makali sana.ย
โAhsante, nataka chapati za hii helaโ nilisema kwa sauti isiyo changamka, yule Mama akapokeaย pesa kisha akawa ananichukulia chapati alizozitengeneza tayari, lakini akaacha akaniulizaย
โUpo sawa?โ swali hili liliniumiza sana, nikawaza nimjibu nini ila nilishaonywa kuwa nikisemaย chochote Wazazi wangu watauawa. Kwa simulizi nilizosikia kuhusu Uchawi inawezekana kabisaย wakauawa wakiwa Mbali hivyo niliogopa sana. Wakati nawaza yule Mama akanishtua kwaย kunitikisa maana nilishazama kimawazoย
โUpo hapa kweli Binti?โ nikashtuka na kujibaraguza kama Mtu aliye sawa huku nikijuwa fikaย kuwa nausaliti moyo wangu.ย
โNdiyo, nipo Mama. Samahani naomba chapati niwahi nimeacha chai jiko la gesiโ nilisema,ย nilishakuwa na uhakika kuwa pengine Mzee Mwinyimkuu aliweka mtego wake kwangu ndiyoย maana akaniacha huru nje
โMh!โ akaguna tu kisha hakusema kingine, halafu akanifungia chapati za Elfu tano akaniwekeaย kwenye mfuko.ย
โKaribu tena, Naitwa Mama Ashura. Ukikwama usisite nitakupa msaadaโ alisema yule Mamaย akanipa mfuko, Uwiiโผ alinigusa ndani ya Moyo wangu kwa jinsi nilivyokua natamani kupataย msaada Mimi kwa yanayonisibu lakini sikujua napataje msaada Mimi, naanzaje? Nikajichekeshaย tu kama mwehu kisha nikageuka na kuondoka pale.ย ย
Kitendo cha Kumpa mgongo Mama muuza chapati aliyejitambulisha kama Mama Ashura, choziย lilinilenga. Safari ya kurudi ndani ilijaa maumivu makali sababu narudi tena kuivaa hofu naย mateso ndani ya Nyumba ya Mzee Mwinyimkuu. Nilitamani kukimbia lakini niliwaza Wazaziย wangu, sikuwa na tumaini kiukweli.ย
Nilifungua geti na kuingia ndani kisha nikafunga geti, nilivyofunga geti chozi lilinibubujika sanaย nikalifuta kwa kutumia mtandio wangu. Ilikua kama Mishale ya saa Tatu na dakika zake hivi,ย nilichemsha chai na kumpa Mzee Mwinyimkuu sebleniย
โKula chapati moja, zilizobakia peleka kwenye kile chumba. Weka na maji ya kunywa kishaย ondoka, ukimaliza njooโ alisema akiwa anakula chapati zake, nilifuata maagizo sababu hapakuaย na jambo jipya. Nilishajua zinaliwa na Misukule ambao Mzee MwinyiMkuu ameniambia nifanyeย nao mapenzi.ย ย
Nilipomaliza sikula, nikarudi sebleni kumsikiliza.ย
โKaa hapoโ akaniamuru niketi kwenye kochi la kizamani, akagida funda kadhaa za chai kishaย akasema tenaย
โHii simu imekumbana na Nini?โย ย
โIlianguka Babaโ nilijibu kwa heshima na wogaย
โUtaongea na Wazazi wako kwa kutumia simu yangu, Baba yako anaumwa na kama utafanyaย zihaka nitamwondoa. Wasalimie waambie simu imeharibika ili wasisumbue, ole wako uonesheย wasiwasi wowote uleโ Nilishtuka, likanitoka neno bila kutarajia sababu nilikua nampenda sanaย Baba yangu Jamani, sijui alipata wapi namba ya Mama yanguย
โBaba anaumwa?โ Weee, nilikiona cha moto, alinimwagia chai ya moto usoni. Nilitapa tapa kwaย maumivuย
โKimyaโผ mshenzi wewe, unauliza ulichokisikia?โ alisema Mzee MwinyiMkuu, sijui nikwambieย nini Msomaji. Huyu Mzee alikua katili haswaa kuanzia sura yake hadi matendo yake, Watu kamaย hawa nilikua nawaona kwenye filamu tu na wala sikutegemea kama wangekuwepo kweli hapaย Duniani.
Niliacha Kulia lakini maumivu ya moto yalikua makali sana japo taratibu yalianza kupoa, kishaย nikasikia simu ikiwa imeshapigwa inaita, aliweka Loud Spika ili naye ayasikie mazungumzo,ย hapo ndipo nilipoisikia sauti ya Mama yangu, chozi lilikua linanibubujika tu. Mama aliitaย ย
โHelloโย
โAbee Mamaโ nilimwitika Mama yangu kwa sauti niliyoshindwa kujizuia kabisa, nililia kwaย mengi sana. Kwanza niliwakumbuka sana wazazi wangu japo ni muda mchache tu umepita naย pili ninayoyapitia sikuwa na Mtu wa kumwambia wakati wazazi wangu wapoย
โHee! Saida Mwanangu, Unalia nini Mama na hii namba ya Nani?โ Mama aliitambua sautiย yangu na pia aligundua ninalia, yule Mzee akanikazia macho yakeย
Jamani sauti ya Mama yangu ilizidi kunichoma Moyoni, nilishindwa hata kuongea, laiti kamaย Mama yangu angelijua nipo chini ya Ulinzi sijui ingekuwaje.ย
โSaida unalia nini Mwanangu, Mumeo amekufanya nini?โ Si unajua ndoa ina siku tatu tu hivyoย ni lazima Mama ahisi pengine nina tatizo na Salehe, nikafuta chozi nikasema neno moja tu kwaย Mama kisha niliangua Kilioย
โNimewakumbuka sana Mama na Babaโฆโ Nililia kama Mtoto mdogo, Mama naye akalia, Mimiย ndiye Mtoto wao pekee na pendwa hivyo hawakuwahi kukaa mbali na Mimi nami sikuwahiย kukaa mbali nao hata mara moja, walinilea kama mboni ya Jicho.ย
โSaida hata sisi wazazi wako tunakuwaza sana, nyumba imepooza mno lakini hakuna jinsi niย lazima Maisha yendelee. Usilie najuwa utazoea hayo unayoyapitia, najua una upweke sanaโย Mama alisema, laiti angejua kuwa naishi nusu mfu na nusu Mtu angelia sana.ย
โSawa Mama lakini siwezi kuacha kuwawaza kila siku ziendazo kwa Mungu, naomba sanaย muwe na afya njema siku zoteโ angalau kidogo sauti ya kilio ilianza kuniacha, kimafua kwaย mbali tu ndiyo kilikuwepo.ย
โAmen Mwanangu, hata hivyo Baba yako anaumwaโ alichokisema Mama ndicho alichokuaย ameniambia Mzee Mwinyimkuu, halafu safari hii akajifanya hana habari na mimi baliย anaendelea kunywa chai, nilimtazama kwa jicho baya la hasira lakini sikuwa na cha kumfanyaย
โEeh imekuwaje tena Mama?โย
โAsubuhi ameanguka chooni, yupo amelala na anahisi mkono mmoja hauna nguvuโ alisemaย Mama, Roho iliniuma sana. Chozi tu ndilo lililokuwa linanibubujika kwa wingiย
โMungu ni Mwema Mama, atapona Insha Allahโ nilisema kwa hisia huku nikijuwa ni fitina zaย kichawi za Mzee Mwinyimkuu.ย ย
โAmen, hii namba ya Nani? Nimejaribu kukupigia hupatikani.โย
โHii namba ni ya Mkwe Wangu. Nilidondosha simu ikapasuka, hata hivyo Mume wanguย amesafiri kwa dharura jana hivyo akirudi nitapata simu nyingine. Ukinihitaji piga humu Mamaโย ย
โSawa Mwananguโฆndoa unaionaje Saida?โ Lilipofika hili swali moyo wangu ulisinyaa ghafla,ย niliumia sana kuulizwa kuhusu ndoa wakati nayoyapitia ni magumu kuliko magumu ya ndoa.ย Mzee Mwinyimkuu akanikata jicho huku akinionya kwa kidoleย
โNina furaha sana Mama, familia inanionesha upendo wa hali ya juu sana. Samhani Mamaย naelekea jikoni mara mojaโ nilisema na kumuaga Mama, nilijijua kuwa ningeangua kilio chaย Mtu mzima sababu nilisema uwongo kitu ambacho sikipendi hasa kumuongopea Mama yangu.ย ย
Nilikata simu kisha niliiweka mezani.ย
โKama utaendelea hivyo basi hatutagombana Mimi na wewe lakini kama utakuwa mkaidi basiย utakiona cha Mtema Kuniโ alisema Mzee Mwinyimkuu, nilinyanyuka taratibu nikatembea hadiย jikoniย
Chai ilikuwa hapo inaniangalia lakini njaa haikuwepo kabisa, Taswira ya Maisha yanguย ilibadilika mno. Nikajuta kwanini niliolewa Mimi Huuuhโผย
Nilikaa kwenye kigoda na kuanza kulia kwa sauti ya chini, huhโผ nilishindwa kujizuia kusemaย ukweli, maumivu yalikua makubwa kiasi kwamba chozi lilinibubujika bila hata kubisha hodi.ย
**ย
Baada ya kupita siku mbili, zikatimia siku tatu ambazo Mzee Mwinyimkuu aliniambia kuwaย napaswa kufanya mapenzi na Misukule wake, hiyo siku nilisoma kila aya kwenye Quraanย tukufu, nilipiga kila goti ili Mungu aniondoe ndani ya ile nyumba lakini haikua hivyo.ย Aliniambia Usiku ndiyo nitafanya kitu hicho, akanipa dawa fulani alizozijua yeye akasemaย napaswa kunywa kabla ya kuingiliwa na Msukule ili nisije pata Ujauzitoย ย
Akanipa pia Kaniki nyeusi nijifunge bila kuvaa chochote ndani, kisha akaniambiaย
โJiandae saa moja Usiku utaingia kwenye kile chumba. Una uwezo wa kuhudumia Wanaumeย wangapi kwa mara moja?โ Aliniuliza, haki ya Mungu nilijawa na hasira isiyo kifani. Kwanzaย sikuwahi kufanya mapenzi kabla ya kuingiliwa na yule Msukule Usiku ule nikifikiria ni Saleheย hivyo sijui chochote kile kuhusu Mapenziย ย
โNakuuliza wewe!โ Akanishtua, nikashtuka haswa maana nilijua kama nitaendelea kuwa kimyaย pengine ningekutana na kofi lake, nikajikuta naropoka tuย
โWatatuโ Nikaliona tabasamu kwenye uso wa Mzee Mwinyimkuu.ย
โHaya pumzika hakikisha umekula vizuri, tuna masaa mawili tu kufika Usikuโ alisema kishaย aliniacha chumbani kwangu nikiendelea kukonda kwa mawazo. Kaniki ilikua mkononi mwanguย nikiwaza eti nakuwa mtumwa wa mapenzi kwa Misukule, kipindi hicho nilishaacha kumuwazaย Salehe sababu Baba yake aliniambia kuwa walikua timu moja kuniingiza matatizoni.
Yale masaa mawili yalikwisha, roho iliniuma na hofu juu, nililia jamani. Halafu sasa huyu Mzeeย alianzisha tabia moja, aliacha kugonga mlango wa chumba changu badala yake aliigia tu kamaย upo wazi. Alinikuta nimekaaย
โJitayarishe Bintiโ alikuja kuniambia hivyo tu, nilimeza funda zito la mate. Laiti kamaย ningelikua huru basi ningeli mrushia tusi la nguoni lakini nilikua kifungoni japo nilikua na uhuruย wa kuchagua kati ya kupoteza Wazazi wangu au kujipotza mimi mwenyewe ndani ya ile nyumbaย ya Kichawiย
Basi, nilifanya kama alivyosema. Niliivaa ile kaniki kama khanga vile nikiwa nimeyafungaย matiti yangu. Sijui aliona nachelewa basi akaja mkuku-mkuku na kunipeleka kwenye kileย chumba ambacho siku ile niliwaona Misukule.ย
โSaida, kama utakua Binti mzuri nakuahidi utaishi kwa raha sana na wazazi wako watakuwa hai.ย Unatakiwa utambue jambo moja kuwa unapofanya mapenzi na hawa Misukule wanapata nguvuย zaidi ya kunipa utajiri na nguvu za Kichawi. Huu ni ufalme niliourithi kutoka kwa Baba yangu,ย nami nitamrithisha Salehe hivyo ni lazima hizi nguvu zitunzwe na kulindwa zaidi ya chochoteย kile. Usiogope ila nitakuwa mkali kama utanifanya nisuburi zaidiโ alisema Mzee Mwinyimkuuย akiwa anatoa sauti ya kawaida iliyojaa Ulaghai mtupuย
Akawasha zile udi zake akaweka kila pande ya chumba kisha akaniambia nikae katikati yaย Chumba kama siku ile ya kwanza. Sijui nikwambiaje uelewe kuwa Mzee Mwinyimkuu alikuwaย na sura mbaya ya kutisha kiasi kwamba akikutazama kwa macho yake mekundu ni lazimaย uogope na ujasiri ukuishe, na kingine yeye kukupa pigo ni dakika moja tu wala hawazi.ย
Chozi lilinitoka siwezi kuongopa, haikua kawaida. Mara ghafla wakatokea misukule Watatuย wakiwa uchi wa Myama, ilikua kama filamu ya maigizo hivi lakini ndiyo ukweli wenyeweย unaouma zaidi moyoni, nahisi walikua wanajuwa walichoitiwa. Niliona Midudu yao ikiwaย imesimama sana, halafu ni mikubwa Jamani Oooohโผย
Nilianza kuogopa huku nikimwambia yule Mzeeย
โSamahani Baba naweza kufanya kila kitu lakini hii siwezi, nihurunie Mtoto wa mwenzakoย Mimi. Niache nirudi kwetuโ nilisema nikiwa ninalia, Msukule mmoja akanivaa kwa nguvu naย kuniondoa ile Khaniki, nikabaki Uchi wa Mnyama kama alivyotaka Mzee Mwinyimkuu.ย Niliingiliwa kwa nguvu na wale Misukule huku nikipiga kelele za kuomba Msaada, kwa jinsiย nilivyogumia nina uhakika kuwa majirani walisikia maana nilikua na maumivu makali sanaย
Walinichana huku chini, damu zilinitoka nikiwa nimelala sakafuni. Nililia kwa kwikwi sitakujaย kusahau namna nilivyojisikia Usiku ule. Yule Mzee akanifuata na kunitaka nikae kimyaย vinginevyo angenichoma kile kisu, nilijinyamazisha haraka sana huku nikimuomba yule Mzee
โKwanini unanitendea unyama kiasi hivi, nimekukosea nini Mimi? Naomba nirudi kwetu Mimiย siwezi jamani Aaaahโผโ yaani kama angelikuwa ni Mtu mwenye roho nzuri basi angelinihurumiaย mara moja na kuniacha niondoke lakini akanipa Mtihani mwingine mgumu sana ambao uliniachaย na kilema cha Maisha hadi hivi leoย
Kitu cha kwanza alichofanya ni kuzungumza maneno yake wale Misukule wakaondoka kamaย walivyokuja kupitia pembe za ukuta, lakini pili Mzee Mwinyimkuu aliniambiaย
โKama utaendelea kunisumbua basi hapa patakuwa Jahannam yako na hutokaa utoke Mileleย Daima. Kingine napaswa kukuvuna viungo kila unapofanya mapenzi na Misukule, sikuย nikimaliza nitakuacha urudi kwenuโ Nilijiuliza anivune viungo kivipi, kauli yake ilinianbia kwaย haraka kuwa Kifo kilikua kimenigongea hodi, kipo karibu zaidi na Mimi.ย
โUnasema nini?โ niliuliza nikiwa ninalia kwa sauti ya Chini.ย
Haraka yule Mzee akanipulizia unga fulani aliokuwa ameushikilia mkono wa kushoto, ulikuaย mweupe ulionifikia hadi usoni kwangu. Nikajikuta nikiwa nimelegea vya kutosha kiasi kwambaย sijitambui, hatimaye giza tu lilinitanda na sikujua kilichokuwa kimeendelea nyuma yangu.
Comments ziwe nyingi hapa
Nini Kitaendelea?USIKOSE SEHEMU YA SITA YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx
24 Comments
Duuuh ni nomaaa
Duuu ni balaaa๐ฅ
duh jmn pole sana
Masikin saida๐๐๐ค
Duh jamani!
๐๐ญ
Maskini Saida jamani hadi huruma ๐
Simulizi ya vitisho yenye mazingatio makubwa
Duh๐ฅ๐ฅ
Amekupofusha mbwa huyo . Dah! Huyo bwaanako salehe Yuko wp jmn kwnn lkn? MUNGU akutowe huko peke yake yy tu ndo anaweza Kwa kweli
Hongera sn Admin . Story inafundiaha sn hii
https://dm.wa.link/tlvtqh
Mh wew mtunzi mbona inatisha ivi kama naona live
Muendelezo plzzzz
Mhh,mungu tunusuru sisi waja wako kwa kila hatua ya maisha yetu
Inatisha sana
Haa hii nishida sasa
Mmhh! Dunia๐ฅบ
Mwendelezo mkuu .
Mnachelewa kutuma vipange jamani, tunasubiri sana aisee
Hili ni funzo kubwa sana kwetu ndo maana wazee wetu kuoa walikua mpaka wachunguze familia au ukoo
Hizi pesa ni shidaaa xnaa aisee
Uchawi ni balaa
x2mk3k
isrprk