Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua (04)
    Hadithi

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua (04)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJanuary 8, 2025Updated:January 8, 202516 Comments6 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Shiii‼” Baba Mkwe akanipa ishara katili ya kunitaka nikae kimya vinginevyo kile kisuΒ  kingeingia mwilini mwangu. Kisha akachuchumaa na kuniambia

    β€œLeo utajuwa ni kwanini uliolewa Binti” Alisema halafu akayaongea maneno fulaniΒ  nisiyoyaelewa, nakumbuka kabisa hayakuwa maneno ya lugha ya Kiswahili bali lughaΒ  nisiyoifahamu na wala si Kiingereza wala Kiarabu. Wale Watu wakasimama kisha wakaendaΒ  kupotelea kwenye kona za kile chumba kilichojaa harufu ya Udi. EndeleaΒ 

    SEHEMU YA NNEΒ 

    Nilikua kama naangalia filamu vile, hata wewe msomaji unaweza fikiria ilikua ni filamu naΒ  ninakusimulia hapa. Hapana ni Simulizi ya kweli, simulizi hii ikusaidie kufanya chaguo sahihiΒ  wakati wa kuolewa au Kuowa ili usije pitia kama Mimi, haya mambo siyo tu kwa MwanamkeΒ  hata Mwanaume anaweza tendewa hivi. Tuendelee sasaΒ 

    Mate hayakumezeka wala pumzi hazikutulia, yule Mzee alikua amenikata jicho kali kishaΒ  kaniambia kwa maneno yenye vituo vingi kuashiria kuwa anamaanisha anachokisema,Β  akaniambiaΒ 

    β€œUmeolewa ili uje kuishi na Misukule hapa, huu ndiyo utajiri wangu. Wewe siyo wa kwanzaΒ  kuolewa na Salehe, walioenda kinyume walifia humu na kupotea kabisa wao pamoja na FamiliaΒ  zao” Yaani nilizidi kuishiwa nguvu, Mungu wangu jasho lilinitoka kama nimemwagiwa maji.Β  Kisha Mzee akaendeleaΒ 

    β€œHii ni nyumba yangu Mimi siyo ya Salehe, yule ni Mtoto wangu na ndiye anayenisaidia Mimi.Β  Utakua unafanya mapenzi na Msukule mmoja mmoja Kila baada ya Siku tatu. UsijaribuΒ  kutoroka ndani ya nyumba hii wala kutoa siri popote, narudia kwa Msistizo ili ueleweΒ  ninachomaanisha. Utawaponza Wazazi wako kwa Ujinga wako mwenyewe” Chozi lilizidiΒ  kunitoka kisha yule Mzee akasimama akaninyooshea KidoleΒ 

    β€œUtafanya niyatakayo ili kuilinda familia yako, hutaruhusiwa kutumia simu na hutatoka njeΒ  isipokua kwa maagizo maalum kutoka Kwangu” kisha yule Mzee aliondoka zake na kunichaΒ  ndani ya kile chumba, wala hakunifungia kuonesha kuwa anajiamini na anachokisema. KiukweliΒ  Nililia sana kwa kwikwi, nililia Mno sababu niliona wazi kuwa ili wazazi Wangu wawe salama napaswa kutumikia Misukule ya yule Mzee na kama nataka kuwa huru basi nitawapoteza WazaziΒ  wangu ambao hawakuwa na Hatia yoyote ile.Β 

    Katika Maisha yangu niliutunza usichana wangu kwa ajili ya Mume wangu lakini nililazinikaΒ  kuutoa kwa Misukule, nilijilaumu kwa kumwamini Salehe, nilimlaani sana. Nikiwa ninaliaΒ  akaingia tena yule Mzee akiwa amehamaki akaniulizaΒ 

    β€œSimu yako ipo wapi?” alishikilia kisu mkononi, sikupepesa maneno nilimpa simu mara mojaΒ  kisha akaondoka nayo. Wala hakufunga mlango aliuwacha wazi ikiwa ni ishara ya kuniruhusuΒ  kuwa huru ndani ya nyumba lakini siyo kuondoka, ndiyo kwa mara ya kwanza katika MaishaΒ  yangu niliushuhudia Uchawi wa waziwazi.Β 

    Basi, nilirudi chumbani nikiwa ninalia, nilikua mwenyewe kwenye Maisha yangu. Sikuwa naΒ  Mtu wa kumueeleza ninayopita, sikuwa na msaada na pengine kaburi langu lingekuwa ndani yaΒ ile nyumba. Kitu cha kwanza kufanya kilikua ni kufuta chozi langu, kwanini niliruhusuΒ  lidondoke chozi langu lenye thamani kubwa. Hata ningelia vipi isingelisaidia Mimi kuponaΒ Β 

    Nilijiegemeza kwenye Mto nikatafakari mengi, nikapata jibu la uhakika kabisa kuwa siku ileΒ  nilifanya mapenzi na Msukule na ndiye aliyenitoa Usichana wangu kwa mara ya kwanzaΒ  nikifikiria ni Salehe. Kitu fulani cha uchungu kilijaa kifuani pangu, hakika nilitendewa unyamaΒ  sana na Salehe na Baba yake. Nilijua Baba na Mama wangekuwa na wasiwasi na Mimi kamaΒ  nitakaa kwa siku nyingi pasi na kuwasiliana nao lakini ningefanya nini sasa na ilinibidi nikae naoΒ  mbali ili kuokoa Maisha yao.Β Β 

    β€œEeh Mungu, umeniptisha kwenye Mtihani gani sasa. Hukuona mitihani mingine rahisi kwanguΒ  isipokua huu?” Nilituma lawama ma maswali kwa Mungu wangu, kumbe ukiona MtuΒ  anamkufuru Mungu si kwa kutaka bali kwa kukosa majibu sahihi ya kuondoka kwenye matatizo.Β Β 

    ***Β 

    Masaa yalienda, sikupata hata lepe la kuusingizia Usingizi yaani nilikua na kichwa kizito sanaΒ  japo Usiku ulikua umeenda. Hakuna sauti ya kutisha niliacha kuisikia Usiku huu, yaani MzeeΒ  Mwinyimkuu alinionesha Uchawi dhahiri kabisa. Sauti za Watoto Wachanga nilizisikia bilaΒ  kificho, nyimbo za ajabu ajabu ziliimbwa na kuchezwa nikajiona kama nimeshafika kuzimu.Β  Nikazikumbuka Riwaya kadhaa nilizokua nazisoma mtandaoni na stori za hapa na pale juu yaΒ  Uchawi, nilikua siziamini lakini hatimaye nilijikuta ndani ya moja ya Riwaya ya kutisha sana.Β 

    Mimi Saida nilikosa majibu ya maswali yote hata yale madogo niliyojiuliza. Bundi walisikikaΒ  Usiku kucha, hadi kuna pambazuka nilikua macho hata taa sikuizima kwa kuhofia kuingiliwaΒ  tena na yule Msukule. Kukesha macho usiku mzima haikua rahisi, macho yalivimba hasaΒ  ukizingatia nililia sanaΒ 

    Niliogopa kutoka chumbani, sikuwa na amani kama siku ya kwanza. Nilikaa kitandani nikipigaΒ  Mihayo, mara Mlango uligongwa, nilishtuka nkasema moyoni sasa naenda kupelekwa kwaΒ  Misukule, hofu ikaamka upya ndani yangu lakini nikamsikia Mzee Mwinyimkuu akisemaΒ 

    β€œAmka uandae chai haraka” alisema kwa jazba fulani baada ya kugonga kwa kitambo kishaΒ  nikayasikia makubhasi yake yakifanya safari kutoka mlangoni kwangu. Moyo ulinidunda sanaΒ  kiukweli, sikuwa na raha wala amani yoyote ile. Ningefanya nini zaidi ya kuamka na kwendaΒ  kumwandalia chai yule Mzee, Binafsi sikuhisi njaa kabisa licha ya kutokula jana kutwa nzima.Β 

    Niliufungua Mlango taratibu sana, nikasikia kama Mtu anafanya Usafi hivi, nilipoangalia vizuriΒ  niliona tu ufagio pekee ukifagia bila kumwona aliyeushikilia ule ufagio, nusura nizame tenaΒ  ndani kwa woga lakini nikapata kiu ya kuona zaidi. Huuuβ€Ό! Uchawi unatisha sana naΒ  nimeushuhudia laivu bila chenga, niliporudisha macho tena sikuona chochote isipokua nyumbaΒ  ilikua safi sana

    Basi nikaanza safari fupi ya kupita koridoni na kuelekea jikoni kuandaa chai ya MzeeΒ  Mwinyimkuu. Ile naingia tu nikakutana naye ndunda ndunda.Β 

    β€œMuda wote ulikua unafanya nini wewe?” aliniuliza kwa hasira sana kama vile tulikuaΒ  tumegombana. Hofu ilinianza upya hata sikuweza kutoa sauti yoyote ile, nikainamia chini,Β  Jamani nilikuja kushtukizwa na kibao cha shavu la kushoto hadi nikahisi giza. Alinipiga kibaoΒ  kizito hadi nikapepesuka pembeni, mateso makali yalianza kwanguΒ 

    Sikuweza kutoa sauti yoyote ile isipokua chozi na maumivu yaliyojaa ndani ya Moyo wangu.Β 

    β€œUsiniletee upumbavu, hukuja kulala hapa wala kutembea. Kumbuka maneno yangu, UtafiaΒ  humu ukileta kiburi, pesa hii hapa Nunua chapati urudi haraka” alisema Mzee Mwinyimkuu,Β  akanipa Elfu tano mpya kabisa. Kisha yeye aliondoka zake akaelekea sebleni, alionekanaΒ  anajiamini na maneno yake ndiyo maana aliniruhusu nitoke nikamnunulie Chapati, wakati natakaΒ  kutoka akapaza sauti yake akaniambia ninunue chapati za hela yoteΒ 

    Sikuwa na maswali mengi kuwa chapati zinaenda kuliwa na Nani sababu hata ule MchichaΒ  nilikua na uhakika kuwa unaliwa na Misukule niliyoiona Usiku. Nilihisi kukonda kwa siku mojaΒ  tu ya hekaheka, nilitoka nikafungua geti kisha nikatoka ndani, taratibu nikawa naeleka kwa yuleΒ  Mama anayeuza Chapati nyumba kama ya Nne hivi kutoka nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu.Β 

    Macho yangu yaliitazama sana ile nyumba ya Mzee Mwinyimkuu, nje Watu walikuaΒ  wakiendelea na shughuli zao, niliamini hakuna anayejuwa kinachoendelea. NilitamaniΒ  nimsimulie Mtu pengine nimwombe msaada lakini nikakumbuka onyo nililopewa na MzeeΒ  Mwinyimkuu, Ah! Hamu iliniisha……….Β 

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TANO YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza HapaΒ 

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    16 Comments

    1. Mama eddy on January 8, 2025 3:22 pm

      Duuuh kuna kitu cha kujifunza apa

      Reply
      • Ahmed Ruta on January 8, 2025 3:28 pm

        Ndo Iko nilichowambia ndo Cha kujifunza

        Reply
      • Fatbaloz on January 8, 2025 5:01 pm

        Gud gud

        Reply
    2. Ahmed Ruta on January 8, 2025 3:27 pm

      Kwaiyo apo mabinti mjufunze msitunze bikra nadhan nyie wenyewe mmejionea kwa mwenzenu Saida YANGU NI AYO

      Reply
      • Fawziya Hassan on January 8, 2025 4:11 pm

        Jamani Saida hadi hurumaπŸ˜”πŸ˜”
        Uchawi upo kweli tuwe makini na wanaume watakao tuowa
        Simulizi ya vitisho yenye maajabu na mafunzo makubwa kwa wanwake na wanaume wanaopenda Mimama.

        Reply
        • LEVI COLISON NDOKOLE on January 8, 2025 10:32 pm

          Huwezi jua tabia za mtu hvihvi tu

          Reply
      • Fawziya Hassan on January 8, 2025 4:21 pm

        Salehe Namba mbili ni Wewe

        Reply
      • [email protected] on January 8, 2025 9:49 pm

        Ya Leo fupi sn Admin jmn Hila ianzidi kunoga . Nawza tu Saida kwann anashinda ht kusema MUNGU nisaidie . Dah! Hapo kwenye kuwapa misukule kwa zamu shindwa shetani .🀭

        Reply
      • [email protected] on January 8, 2025 10:23 pm

        Sa itakuwaje

        Reply
    3. Hamisi halidi on January 8, 2025 6:09 pm

      Yaleo fupi sna boss

      Reply
    4. Frae on January 9, 2025 7:55 am

      Wendelezo kak

      Reply
    5. Cathbert on January 13, 2025 7:42 pm

      Kikubwa kuomba Mungu

      Reply
    6. πŸ–± Ticket: TRANSACTION 1,569368 BTC. Next >>> https://graph.org/Payout-from-Blockchaincom-06-26?hs=0e4476252400ba80a2cc5a0ed1a892cb& πŸ–± on July 8, 2025 9:34 am

      nc4vte

      Reply
    7. πŸ“€ System Alert - 1.9 Bitcoin withdrawal attempt. Deny? => https://graph.org/TAKE-YOUR-BITCOIN-07-23?hs=0e4476252400ba80a2cc5a0ed1a892cb& πŸ“€ on August 12, 2025 5:35 pm

      if7dcv

      Reply
    8. πŸ“ πŸ” Security Required - 0.6 BTC transaction held. Proceed here > https://graph.org/UNLOCK-CRYPTO-ASSETS-07-23?hs=0e4476252400ba80a2cc5a0ed1a892cb& πŸ“ on August 28, 2025 4:51 am

      hrr09y

      Reply
    9. mitolyn reviews on January 25, 2026 10:45 pm

      **mitolyn reviews**

      Mitolyn is a carefully developed, plant-based formula created to help support metabolic efficiency and encourage healthy, lasting weight management.

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Hadithi February 23, 2026

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    IlipoishiaΒ  Kwanza nilijiuliza ni Nani anayeweza kuja kwetu, kama Mama Amida tayariΒ  tulishazungumza. Nilimeza funda…

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (07)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.