Ilipoishia “Utamzoea, si unajuwa wazee wa zamani. Pengine hakutaka wewe ushike begi kwasababu zilizoย kaa kitamaduni tu za Kizamani au kabila letu lakini ni mcheshi utamzoea kwa muda atakaokaaย hapa.ย ย
โIna maana atakuwa anaishi hapa na Sisi?โย
โNdiyo, ila muda mchache tu atakua ameondoka. Vipi umeshakula?โ Basi kuzungumza naย Salehe kulinifanya nisahau kilichotokea, tuliongea sana hadi Mchana tuliposikia adhana. Saleheย akawa wa kwanza kunikumbusha kufanya Ibada, nilitabasamu nikashusha pumzi kidogo hukuย dimpozi zangu zikionekana . Endeleaย
SEHEMU YA PILI
Ilikua ni ndoto yangu siku moja nifanye ibada na Mwanaume aliyeniowa, moyoni nilimshukuruย Mungu kunipa Mume kama Salehe anayejua wajibu wa Mke na Dini yake. Basi tuliongozanaย hadi chumbani kujiandaa, haikuchukua muda mrefu tukawa tumeshapata udhu kwa ajili ya Ibada.ย
โTwende sebleni, Baba naye anatusubiriaโ alisema, sikuacha kutabasamu. Kwangu niliiona niย Familia bora sana, Baba alitusalisha sote hadi tulipomaliza kisha tukarudi Chumbani Mimi naย Mume wanguย
โMume wangu, sijui jiko liko wapi, sijui chochote. Mimi ni Mwanamke raha yangu ni kupikaย chakula mle nyoteโ nilisema nikiwa nalivua Baibui langu na kulitupa kitandaniย
โUsijali, leo pumzika sote tunaelewa. Kuanzia kesho utaanza kupika na kufanya kazi nyingine,ย subiria nakuletea Chakulaโ alisema Salehe kisha aliondoka zake, aliniacha natabasamu kwa raha.ย Nikajisemea moyoni tuย
โKumbe ndoa ni tamu kiasi hikiโ kicheko cha raha kilinitoka Mtoto wa kike, nikabdilisha nguoย kisha nikawasha simu na kuzungumza na Wazazi wangu maana tokea nimefika sikuwajulishaย sababu simu ilikua imezima chaji. Wazazi wangu walifurahi sana na kunisihi niwe mvumilivu.ย
Salehe alikuja na chakula kinachotoa mvuke kuashiria kuwa kilitoka jikoni muda huo huo, pilauย la nyama ya Mbuzi na kachumbari yenye pilipili nyingi kama nipendavyo, alinipatia naย kunifanya macho yanitoke. Nilimeza mate kwa uchuย
Sikutaka kuuliza alikitoa wapi na kama alikipika alipika saa ngapi, nilikifakamia kama kilivyoย bila hata aibu. Sasa nimwonee aibu Mume wangu jamani si nitachekwa na Dunia nzima, sasaย baada ya kushiba ndio nikakumbuka kumuuliza
โHivi hiki chakula kimetoka wapi Mume wangu au umenunua maana kusema kimepikwa hapa niย Uwongo, pilau nishindwe kusikia harufu yake wakati kinapikwa Mmhโผโ Salehe alitabasamu tu,ย akaninawisha Maji halafu akaniulizaย
โUmeshiba eeh?โย
โSaaaana, asante kwa Chakula Mume wanguโ nilisema nikiwa namwachia tabasamu Mumeย wangu. Tulikuwa chumbani wawili tuย
Akaondoa vyombo bila kunipa jibu lolote lile, sikujali sana.ย
***ย
Usiku ulipoingia nilikua na uhakika kuwa Ndiyo utakuwa usiku wetu wa kwanza kama Mume naย Mke, nilikua tayari kuiondoa bikira yangu kwa ajili ya Mume wangu. Sasa nikae na Bikira hadiย lini na nimeshaolewa, nilijifanyia Usafi nikamsubiria Mume wangu amalize mazungumzo naย Baba yake Mzee Mwinyimkuu kisha tuzagamuane kwa mara ya kwanza.ย
Masaa yalienda hadi nilihisi Usingizi unaninyemelea, nikajiegesha kidogo maana Jumbe zoteย nilizomtumia hakuzijibu. Nilikuja kushtuka nikakuta kuna Mwanaume ananikula, sikuwezaย kujizuia nilimpa ushirikiano. Nilijua tu ni Salehe awe nani mwingine, alikua fundi haswa naย alinikula haraka haraka kama mwizi vile, nilikua nimezima Taa hivyo palikua giza tupu naย sikuweza kuona taswira yoyote isipokua raha ya ajabu sanaย
Nilitolewa Bikira yangu kwa mazingira hayo, kisha baada ya kumaliza alikimbilia bafuni namiย kwa haraka nikawasha taa kuangalia kama kuna damu inatoka ili nisichafue shuka. Hapakua naย Damu yoyote ile, lakini nilikipata cha moto nikawa natabasamu tu. Nikiwa hapo nilikuaย namsuburia Salehe aniambie kwanini amenikula guzani tena nikiwa Usingizini hadi nimeshtukaย wakati mimi ni Mke wakeย ย
Siyo kwamba aliniudhi, la hasha ila tu si unajuwa asijeniona kama Napenda sanaย kuzagamuana.basi nilisubiria kwa kitanbo kidogo kama dakika ishirini hivi hadi nikajiulizaย
โAnakinawa kitu gani hadi sasa hatoki bafuni?โ Bafu lilikua mle mle chumbani. Basiย nikaikusanya shuka ili nijifunge nimfuate bafuni, mara ghafla mlango wa chumba ulifunguliwa.ย Nilipatwa na Mshangao mkubwa sana, eti Salehe ndiyo alikua akiingia Chumbani tena akiwa naย nguo zake zilezile alizoondoka nazo kuelekea kuzungumza na Baba yakeย
Niliyapeleka macho bafuni huku nikijiuliza ni Nani niliyekuwa nafanya naye mapenzi mudaย mchache uliopita, hata Salehe alinishangaa akaniulizaย
โVipi mbona umepigwa na Butwaa unashangaa nini?โ sikujua nimjibu nini, nikakimbilia bafuni,ย sikukuta Mtu yeyote yule na hapakua na dalili hata ya Maji pale chini, Uwii niliishiwa pozi hukuย mwili ukitetemeka. Salehe alinifuata Bafuni huku akiniulizaย
โWewe una nini?โย
โMh Mh niko sawa tu, ndio umemaliza muda huu kuzungumza na Baba?โ nikajibalaguza kwaย hofu sana kumuuliza swali hili ila moyo wangu uliniambia kuwa ndani ya ile nyumba palikua naย manbo ya mazingaombwe sababu haiwezekani nifanye mapenzi na Mtu ambaye alipotea ghaflaย Bafuniย
Huu siyo mkasa wa kujitungia, nimkasa wa kweli wa Maisha yangu. Nataka ujifunze kuhusuย ndoa na Mtu usiye mjua, unaweza fikiria ni mambo ya kusadikika lakini yalinikuta haya mamboย Rukwa kwenye ndoa yangu ya kwanza, sitakuja kusahau.ย
Basi tulirudi hadi kitandani, wenge zito likiwa limeigubika sura yangu. Wasiwasi ulizidi kutanda.ย Ningewezaje kumweleza Mume wangu Salehe, angemiamini? Hapana isingelikua rahisi kiasiย hichoย
โMke wangu nataka tuzungumze jamboโ alisema Salehe alipomaliza kuvua nguo zake, nilitikisaย kichwa changu ili aniambie tu maana kichwa kilinijaa mambo mengi na maswali magumuย yanayohitaji majibu ya haraka. Siku ya kwanza Rukwa ilianza kwa ugumu sana na ndiyo kwanzaย ni Usiku wa kwanzaย
โKesho naenda Sumbawanga, kuna jambo Baba amenitaka nikalifanye ndiyo maanaย nimechelewa sanaโ alisema Saleheย
โOoh! Sawa Mume wangu, utarudi lini?โ nilijikaza sana hadi kuunganisha sentensi hii naย kumuuliza swali, kigugumizi cha ghafla hakikuniacha kabisa. Halafu kwa mbali nilianza kuhisiย homa kali ila nilijikaza tu.ย ย
โBaada ya siku tatu, sikuweza kumkatalia. Nimekubali ili Baba aridhike tu ila kukuacha Mkeย wangu siyojambo rahisi kwanguโ Alisema, siyo kwamba nilikua namsikiliza Salehe bali niliwazaย ni Nani yule nilifanya naye mapenziย
Haikua ndoto kabisa sababu niliushika mwili wa yule Mwanaume aliyepotelea bafuni. Usikuย ulikua mrefu kwangu, maswali hayakuniisha Mimi hadi kulipo pambazuka, kama kawaida yaย Salehe hakunigusa kabisa. Kwanza nilishukuru sababu nisingefurahia kutokana na msongo waย mawazo niliokuwa naoย
Niliamka mapema kuagana na Mume wangu Salehe, alipoondoka nilienda tena bafuni kukaguaย huku nikijikumbusha Usiku wa jana, kwa hakika yule Mtu alikimbilia bafuni lakini kwaniniย hakuwepo nilipoenda lilikuwa ni swali nililojiuliza sana bila kupata jibu lolote lile. Nilibakiaย nimesimama mlangoni nikilitazama lile bafuย
โSasa nilikua nafanya Mapenzi na Nani mbona sielewi Mimi?โ sikuwa na budi bali kukosaย majibu tu, nikajiwekea moyoni kuwa ipo siku nitaufahamu ukweli.ย ย
Jua lilipo chomoza nilivalia nguo za kufanya shughuli za nyumbani, kwakuwa tayari Mumeย wangu alinionesha mahali lilipo jiko nilielekea huko, nilikagua vitu vya jikoni kama mpishiย
nikaanza na kuweka chai jikoni huku nikifikiria ni vitafunwa gani Baba Mkwe angependeleaย asubuhi hiyoย
Nilipaswa kumuuliza kwanza hivyo nilienda kumgongea mlango huku nikiwa na hofu asijeย akanifokea kama alivyofanya jana, alifungua mlango harakaย ย
โShikamoo Babaโ nilimsalimia kwa haraka sana tena kwa heshima zote huku nikipeleka naย magoti yangu uelekeo wa chini kisha nikarudi juu, nilimfanya atabasamu kidogoย
โMarhaba Saida, umeamkaje?โย
โNamshukuru Mungu nimeamka Salama Babaโย
โUsiku wako wa kwanza Rukwa umeendaje!โ Nilianza kuonesha tabasamu kabla ya kumjibuย
โMungu ni Mwema Baba, samahani Baba nilikua nauliza unatumia kitafunwa gani asubuhi yaย leo?โย ย
โOoh! Chochote tu mpendwa wangu, maandazi, chapati, mkate Mimi nakula tuโ alisema,ย niliweka mikono yangu mbele kwa heshima muda wote nilipokua naongea naye. Niliachiaย katabasamu kisha nikamwambiaย
โBasi sawa Baba, naomba nikakuangalizieโย
โHaya Mama, ukitoka tu hapo nje mkono wa Kulia kuna Mama anatengeneza Chapati nzuri sanaย unaweza kwenda hapoโย ย
โSawa Babaโ Basi nilimwacha Baba Mkwe akiufunga mlango wake kisha mimi nilirudiย Chumbani kuchukua pesa ambayo Mume wangu aliniachia halafu nilielekea nje kununuaย chapati, japo nilikua natembea lakini mwili ulikua na maumivu makali kama homa fulani hivi.ย ย
Nilijikaza hadi nilipofika kununua Chapati nilipoelekezwa, nilimsalimia vizuri maana ndiyoย majirani wenyewe hao, nikachukua chapati za kututosha Mimi na Baba Mkwe wangu lakiniย wakati naondoka yule Mama Muuza chapati akaniita, nilikua nimeshampa mgongo hivyoย niligeuka na kurudi maana nilishapiga hatua kadhaa mbeleย
โAbee Mamaโ Niliitika wito, yule Mama akanitaka nisogee zaidi kanakwamba kuna jamboย analotaka nilisikie Mimi tu, basi nilisogea na kwa uzuri tulikua wawili japo kwa pembeni palikuaย na vijana wengine wakiwa wanatia zogo masuala ya Mpiraย
โSamahani Binti, ndiyo mara ya kwanza nakuona. Wewe ni Mgeni hapa mtaani?โ aliniuliza ilaย nilianza kuhisi pengine ana jambo fulani lisilo la kawaida pengine anataka kusema, nilisitaย kidogo lakini nikajikuta nikiachia tabasamu kama ilivyo kawaida yanguย ย
โNdiyo, Mimi ni mgeniโย
โUnaitwa Nani?โ
โNaitwa Saidaโย
โHayo maua mwilini ni ishara kuwa umeolewa siku chache zilizopita si ndiyo?โ Jamani yuleย Mama simfahamu lakini alinidadisi ndani ya muda mfupi na kugundua yote hayo.ย
โNdio, nimeolewa na Salehe wa nyumba ile paleโ sikutaka kona kona maana nilijua angeniulizaย naishi wapi nikaona nirahisishe maongezi tu.ย ย
โMh! Sawa Mwanangu nisikuchelewesheโ alisema halafu muda huo huo akapoa mwili mzimaย kama siyo yeye aliyekua akinichangamkia. Nilitamani kumuuliza kwanini ameguna ila nilihisiย nitazidi kuchelewa maana niliweka chai kwenye jiko la Gesi. Haraka nikamuaga yule Mamaย kisha nilirejea nyumbani kuepua chai.ย
Nilikuta tayari chai ilikua imesha chemka niliiweka kwenye chupa, nakumbuka nilikuaย nimenunua chapati Nane, siyo kwamba mimi nilikua mlaji sana ila hofu yangu ilikua kwa Babaย Mkwe sikuujua uwezo wake.ย ย
Nilipomaliza tu kuweka chai ndani ya chupa papo hapo Mlango uligongwa, nikapaza sautiย
โNakujaaaโ Niliamua kwanza nimuwekee Baba Mkwe chai Mezani, nilimtengea chai sebleni naย kumwekea chapati tano kisha nikamgongea mlango na kumueleza chai ipo tayari Sebleni, basiย nikaelekea moja kwa moja hadi Mlangoni kuitika witoย
Nilipofika nilikutanaa na yule Mama muuza mboga mboga wa jana, niliachia katabasamuย nikamsalimia.ย
โVipi na leo hamchukui? Jamani nyie ni wateja wangu wakubwa sana wa Mboga mboga. Tokeaย mmeacha kununua Biashara imekua ngumu mnoโ alisema yule Mama, nilicheka tuย nikamwambiaย
โMwenye nyumba alisafiri Mama, basi naomba Mchicha wa Elfu mojaโ nilisema maanaย niliamini ungetosheleza kwa Watu wawiliย
โWa elfu Moja?โย
โNdiyo mbona umeshtuka?โย
โMh! Kwani yule Kijana yuko wapi sijamuona muda, yeye alikua anachukua Mchicha hadi waย Elfu Kumiโ alisema yule Mama, sikuweza kujizuia ilibidi nicheke maana Mchicha wa Elfu kumiย ungetosha kulisha mifugo na siyo kula Binadamu wawili, ni mwingi Jamani.ย
โUsicheke kama unabisha Muulize, ni mteja wangu wa muda mrefu sana huwa anachukua hataย beseni zima nakua namaliza mapemaโ Niliacha kucheka maana ilionekana alikua akimaanishaย anachoongea, nikasema
โSawa Mama, kwasasa hayupo amesafiri labda akirudi maana mimi sijui kuhusu hilo ilaย nimeshangaa huo Mchicha mwingi hivyo huwa anaupeleka wapi Mamaโ nilisema nikiwaย nachagua Mchicha nilioutaka, mara nilisikia Mtu akikohoa nyuma yangu kama ishara kuwaย nigeuke ……ย
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TATU YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx
19 Comments
Jamani Saida kaolewa kwenye MISUKULE hatari.
Leo naona ni fupi jamani
Simulizi tamu.
Fupi jamani mwaka mpya tunaomba uturefushie kidg
JIni
Maneno yamepangika hakika.
Kazi nzuri sana
Y Leo ni fupi sn alafu mwendelezo unachekewesha mpk mtu unasahau . Hila simulizi ni tamu sn hongera .
Nina wsws na ba mkwe aisee kuwa ndo mtoa bikira
Hahaha ana nunua mchicha wa elfu 10 ana lisha kijiji
Anamuachaje mkewe na baba mkwee jmn
Hili la mchicha wa elfu kumi hata mimi nimecheka
๐๐
Y Leo ni fupi sn alafu mwendelezo unachekewesha mpk mtu unasahau . Hila simulizi ni tamu sn hongera .
Kumeanza kuchangamka sasa
19697786
Ameyatimbaaaaaa
Mchicha elf 10 sio.kwel atakuw anamivugo
Yer kaz nzuri
Kazi anayo
Saidia ๐
Duuuh mchicha wa 10 huyo atakuwa na misukulee
f8e24l