Ilipoishia “Utamzoea, si unajuwa wazee wa zamani. Pengine hakutaka wewe ushike begi kwasababu zilizoΒ kaa kitamaduni tu za Kizamani au kabila letu lakini ni mcheshi utamzoea kwa muda atakaokaaΒ hapa.Β Β
βIna maana atakuwa anaishi hapa na Sisi?βΒ
βNdiyo, ila muda mchache tu atakua ameondoka. Vipi umeshakula?β Basi kuzungumza naΒ Salehe kulinifanya nisahau kilichotokea, tuliongea sana hadi Mchana tuliposikia adhana. SaleheΒ akawa wa kwanza kunikumbusha kufanya Ibada, nilitabasamu nikashusha pumzi kidogo hukuΒ dimpozi zangu zikionekana . EndeleaΒ
SEHEMU YA PILI
Ilikua ni ndoto yangu siku moja nifanye ibada na Mwanaume aliyeniowa, moyoni nilimshukuruΒ Mungu kunipa Mume kama Salehe anayejua wajibu wa Mke na Dini yake. Basi tuliongozanaΒ hadi chumbani kujiandaa, haikuchukua muda mrefu tukawa tumeshapata udhu kwa ajili ya Ibada.Β
βTwende sebleni, Baba naye anatusubiriaβ alisema, sikuacha kutabasamu. Kwangu niliiona niΒ Familia bora sana, Baba alitusalisha sote hadi tulipomaliza kisha tukarudi Chumbani Mimi naΒ Mume wanguΒ
βMume wangu, sijui jiko liko wapi, sijui chochote. Mimi ni Mwanamke raha yangu ni kupikaΒ chakula mle nyoteβ nilisema nikiwa nalivua Baibui langu na kulitupa kitandaniΒ
βUsijali, leo pumzika sote tunaelewa. Kuanzia kesho utaanza kupika na kufanya kazi nyingine,Β subiria nakuletea Chakulaβ alisema Salehe kisha aliondoka zake, aliniacha natabasamu kwa raha.Β Nikajisemea moyoni tuΒ
βKumbe ndoa ni tamu kiasi hikiβ kicheko cha raha kilinitoka Mtoto wa kike, nikabdilisha nguoΒ kisha nikawasha simu na kuzungumza na Wazazi wangu maana tokea nimefika sikuwajulishaΒ sababu simu ilikua imezima chaji. Wazazi wangu walifurahi sana na kunisihi niwe mvumilivu.Β
Salehe alikuja na chakula kinachotoa mvuke kuashiria kuwa kilitoka jikoni muda huo huo, pilauΒ la nyama ya Mbuzi na kachumbari yenye pilipili nyingi kama nipendavyo, alinipatia naΒ kunifanya macho yanitoke. Nilimeza mate kwa uchuΒ
Sikutaka kuuliza alikitoa wapi na kama alikipika alipika saa ngapi, nilikifakamia kama kilivyoΒ bila hata aibu. Sasa nimwonee aibu Mume wangu jamani si nitachekwa na Dunia nzima, sasaΒ baada ya kushiba ndio nikakumbuka kumuuliza
βHivi hiki chakula kimetoka wapi Mume wangu au umenunua maana kusema kimepikwa hapa niΒ Uwongo, pilau nishindwe kusikia harufu yake wakati kinapikwa MmhβΌβ Salehe alitabasamu tu,Β akaninawisha Maji halafu akaniulizaΒ
βUmeshiba eeh?βΒ
βSaaaana, asante kwa Chakula Mume wanguβ nilisema nikiwa namwachia tabasamu MumeΒ wangu. Tulikuwa chumbani wawili tuΒ
Akaondoa vyombo bila kunipa jibu lolote lile, sikujali sana.Β
***Β
Usiku ulipoingia nilikua na uhakika kuwa Ndiyo utakuwa usiku wetu wa kwanza kama Mume naΒ Mke, nilikua tayari kuiondoa bikira yangu kwa ajili ya Mume wangu. Sasa nikae na Bikira hadiΒ lini na nimeshaolewa, nilijifanyia Usafi nikamsubiria Mume wangu amalize mazungumzo naΒ Baba yake Mzee Mwinyimkuu kisha tuzagamuane kwa mara ya kwanza.Β
Masaa yalienda hadi nilihisi Usingizi unaninyemelea, nikajiegesha kidogo maana Jumbe zoteΒ nilizomtumia hakuzijibu. Nilikuja kushtuka nikakuta kuna Mwanaume ananikula, sikuwezaΒ kujizuia nilimpa ushirikiano. Nilijua tu ni Salehe awe nani mwingine, alikua fundi haswa naΒ alinikula haraka haraka kama mwizi vile, nilikua nimezima Taa hivyo palikua giza tupu naΒ sikuweza kuona taswira yoyote isipokua raha ya ajabu sanaΒ
Nilitolewa Bikira yangu kwa mazingira hayo, kisha baada ya kumaliza alikimbilia bafuni namiΒ kwa haraka nikawasha taa kuangalia kama kuna damu inatoka ili nisichafue shuka. Hapakua naΒ Damu yoyote ile, lakini nilikipata cha moto nikawa natabasamu tu. Nikiwa hapo nilikuaΒ namsuburia Salehe aniambie kwanini amenikula guzani tena nikiwa Usingizini hadi nimeshtukaΒ wakati mimi ni Mke wakeΒ Β
Siyo kwamba aliniudhi, la hasha ila tu si unajuwa asijeniona kama Napenda sanaΒ kuzagamuana.basi nilisubiria kwa kitanbo kidogo kama dakika ishirini hivi hadi nikajiulizaΒ
βAnakinawa kitu gani hadi sasa hatoki bafuni?β Bafu lilikua mle mle chumbani. BasiΒ nikaikusanya shuka ili nijifunge nimfuate bafuni, mara ghafla mlango wa chumba ulifunguliwa.Β Nilipatwa na Mshangao mkubwa sana, eti Salehe ndiyo alikua akiingia Chumbani tena akiwa naΒ nguo zake zilezile alizoondoka nazo kuelekea kuzungumza na Baba yakeΒ
Niliyapeleka macho bafuni huku nikijiuliza ni Nani niliyekuwa nafanya naye mapenzi mudaΒ mchache uliopita, hata Salehe alinishangaa akaniulizaΒ
βVipi mbona umepigwa na Butwaa unashangaa nini?β sikujua nimjibu nini, nikakimbilia bafuni,Β sikukuta Mtu yeyote yule na hapakua na dalili hata ya Maji pale chini, Uwii niliishiwa pozi hukuΒ mwili ukitetemeka. Salehe alinifuata Bafuni huku akiniulizaΒ
βWewe una nini?βΒ
βMh Mh niko sawa tu, ndio umemaliza muda huu kuzungumza na Baba?β nikajibalaguza kwaΒ hofu sana kumuuliza swali hili ila moyo wangu uliniambia kuwa ndani ya ile nyumba palikua naΒ manbo ya mazingaombwe sababu haiwezekani nifanye mapenzi na Mtu ambaye alipotea ghaflaΒ BafuniΒ
Huu siyo mkasa wa kujitungia, nimkasa wa kweli wa Maisha yangu. Nataka ujifunze kuhusuΒ ndoa na Mtu usiye mjua, unaweza fikiria ni mambo ya kusadikika lakini yalinikuta haya mamboΒ Rukwa kwenye ndoa yangu ya kwanza, sitakuja kusahau.Β
Basi tulirudi hadi kitandani, wenge zito likiwa limeigubika sura yangu. Wasiwasi ulizidi kutanda.Β Ningewezaje kumweleza Mume wangu Salehe, angemiamini? Hapana isingelikua rahisi kiasiΒ hichoΒ
βMke wangu nataka tuzungumze jamboβ alisema Salehe alipomaliza kuvua nguo zake, nilitikisaΒ kichwa changu ili aniambie tu maana kichwa kilinijaa mambo mengi na maswali magumuΒ yanayohitaji majibu ya haraka. Siku ya kwanza Rukwa ilianza kwa ugumu sana na ndiyo kwanzaΒ ni Usiku wa kwanzaΒ
βKesho naenda Sumbawanga, kuna jambo Baba amenitaka nikalifanye ndiyo maanaΒ nimechelewa sanaβ alisema SaleheΒ
βOoh! Sawa Mume wangu, utarudi lini?β nilijikaza sana hadi kuunganisha sentensi hii naΒ kumuuliza swali, kigugumizi cha ghafla hakikuniacha kabisa. Halafu kwa mbali nilianza kuhisiΒ homa kali ila nilijikaza tu.Β Β
βBaada ya siku tatu, sikuweza kumkatalia. Nimekubali ili Baba aridhike tu ila kukuacha MkeΒ wangu siyojambo rahisi kwanguβ Alisema, siyo kwamba nilikua namsikiliza Salehe bali niliwazaΒ ni Nani yule nilifanya naye mapenziΒ
Haikua ndoto kabisa sababu niliushika mwili wa yule Mwanaume aliyepotelea bafuni. UsikuΒ ulikua mrefu kwangu, maswali hayakuniisha Mimi hadi kulipo pambazuka, kama kawaida yaΒ Salehe hakunigusa kabisa. Kwanza nilishukuru sababu nisingefurahia kutokana na msongo waΒ mawazo niliokuwa naoΒ
Niliamka mapema kuagana na Mume wangu Salehe, alipoondoka nilienda tena bafuni kukaguaΒ huku nikijikumbusha Usiku wa jana, kwa hakika yule Mtu alikimbilia bafuni lakini kwaniniΒ hakuwepo nilipoenda lilikuwa ni swali nililojiuliza sana bila kupata jibu lolote lile. NilibakiaΒ nimesimama mlangoni nikilitazama lile bafuΒ
βSasa nilikua nafanya Mapenzi na Nani mbona sielewi Mimi?β sikuwa na budi bali kukosaΒ majibu tu, nikajiwekea moyoni kuwa ipo siku nitaufahamu ukweli.Β Β
Jua lilipo chomoza nilivalia nguo za kufanya shughuli za nyumbani, kwakuwa tayari MumeΒ wangu alinionesha mahali lilipo jiko nilielekea huko, nilikagua vitu vya jikoni kama mpishiΒ
nikaanza na kuweka chai jikoni huku nikifikiria ni vitafunwa gani Baba Mkwe angependeleaΒ asubuhi hiyoΒ
Nilipaswa kumuuliza kwanza hivyo nilienda kumgongea mlango huku nikiwa na hofu asijeΒ akanifokea kama alivyofanya jana, alifungua mlango harakaΒ Β
βShikamoo Babaβ nilimsalimia kwa haraka sana tena kwa heshima zote huku nikipeleka naΒ magoti yangu uelekeo wa chini kisha nikarudi juu, nilimfanya atabasamu kidogoΒ
βMarhaba Saida, umeamkaje?βΒ
βNamshukuru Mungu nimeamka Salama BabaβΒ
βUsiku wako wa kwanza Rukwa umeendaje!β Nilianza kuonesha tabasamu kabla ya kumjibuΒ
βMungu ni Mwema Baba, samahani Baba nilikua nauliza unatumia kitafunwa gani asubuhi yaΒ leo?βΒ Β
βOoh! Chochote tu mpendwa wangu, maandazi, chapati, mkate Mimi nakula tuβ alisema,Β niliweka mikono yangu mbele kwa heshima muda wote nilipokua naongea naye. NiliachiaΒ katabasamu kisha nikamwambiaΒ
βBasi sawa Baba, naomba nikakuangalizieβΒ
βHaya Mama, ukitoka tu hapo nje mkono wa Kulia kuna Mama anatengeneza Chapati nzuri sanaΒ unaweza kwenda hapoβΒ Β
βSawa Babaβ Basi nilimwacha Baba Mkwe akiufunga mlango wake kisha mimi nilirudiΒ Chumbani kuchukua pesa ambayo Mume wangu aliniachia halafu nilielekea nje kununuaΒ chapati, japo nilikua natembea lakini mwili ulikua na maumivu makali kama homa fulani hivi.Β Β
Nilijikaza hadi nilipofika kununua Chapati nilipoelekezwa, nilimsalimia vizuri maana ndiyoΒ majirani wenyewe hao, nikachukua chapati za kututosha Mimi na Baba Mkwe wangu lakiniΒ wakati naondoka yule Mama Muuza chapati akaniita, nilikua nimeshampa mgongo hivyoΒ niligeuka na kurudi maana nilishapiga hatua kadhaa mbeleΒ
βAbee Mamaβ Niliitika wito, yule Mama akanitaka nisogee zaidi kanakwamba kuna jamboΒ analotaka nilisikie Mimi tu, basi nilisogea na kwa uzuri tulikua wawili japo kwa pembeni palikuaΒ na vijana wengine wakiwa wanatia zogo masuala ya MpiraΒ
βSamahani Binti, ndiyo mara ya kwanza nakuona. Wewe ni Mgeni hapa mtaani?β aliniuliza ilaΒ nilianza kuhisi pengine ana jambo fulani lisilo la kawaida pengine anataka kusema, nilisitaΒ kidogo lakini nikajikuta nikiachia tabasamu kama ilivyo kawaida yanguΒ Β
βNdiyo, Mimi ni mgeniβΒ
βUnaitwa Nani?β
βNaitwa SaidaβΒ
βHayo maua mwilini ni ishara kuwa umeolewa siku chache zilizopita si ndiyo?β Jamani yuleΒ Mama simfahamu lakini alinidadisi ndani ya muda mfupi na kugundua yote hayo.Β
βNdio, nimeolewa na Salehe wa nyumba ile paleβ sikutaka kona kona maana nilijua angeniulizaΒ naishi wapi nikaona nirahisishe maongezi tu.Β Β
βMh! Sawa Mwanangu nisikuchelewesheβ alisema halafu muda huo huo akapoa mwili mzimaΒ kama siyo yeye aliyekua akinichangamkia. Nilitamani kumuuliza kwanini ameguna ila nilihisiΒ nitazidi kuchelewa maana niliweka chai kwenye jiko la Gesi. Haraka nikamuaga yule MamaΒ kisha nilirejea nyumbani kuepua chai.Β
Nilikuta tayari chai ilikua imesha chemka niliiweka kwenye chupa, nakumbuka nilikuaΒ nimenunua chapati Nane, siyo kwamba mimi nilikua mlaji sana ila hofu yangu ilikua kwa BabaΒ Mkwe sikuujua uwezo wake.Β Β
Nilipomaliza tu kuweka chai ndani ya chupa papo hapo Mlango uligongwa, nikapaza sautiΒ
βNakujaaaβ Niliamua kwanza nimuwekee Baba Mkwe chai Mezani, nilimtengea chai sebleni naΒ kumwekea chapati tano kisha nikamgongea mlango na kumueleza chai ipo tayari Sebleni, basiΒ nikaelekea moja kwa moja hadi Mlangoni kuitika witoΒ
Nilipofika nilikutanaa na yule Mama muuza mboga mboga wa jana, niliachia katabasamuΒ nikamsalimia.Β
βVipi na leo hamchukui? Jamani nyie ni wateja wangu wakubwa sana wa Mboga mboga. TokeaΒ mmeacha kununua Biashara imekua ngumu mnoβ alisema yule Mama, nilicheka tuΒ nikamwambiaΒ
βMwenye nyumba alisafiri Mama, basi naomba Mchicha wa Elfu mojaβ nilisema maanaΒ niliamini ungetosheleza kwa Watu wawiliΒ
βWa elfu Moja?βΒ
βNdiyo mbona umeshtuka?βΒ
βMh! Kwani yule Kijana yuko wapi sijamuona muda, yeye alikua anachukua Mchicha hadi waΒ Elfu Kumiβ alisema yule Mama, sikuweza kujizuia ilibidi nicheke maana Mchicha wa Elfu kumiΒ ungetosha kulisha mifugo na siyo kula Binadamu wawili, ni mwingi Jamani.Β
βUsicheke kama unabisha Muulize, ni mteja wangu wa muda mrefu sana huwa anachukua hataΒ beseni zima nakua namaliza mapemaβ Niliacha kucheka maana ilionekana alikua akimaanishaΒ anachoongea, nikasema
βSawa Mama, kwasasa hayupo amesafiri labda akirudi maana mimi sijui kuhusu hilo ilaΒ nimeshangaa huo Mchicha mwingi hivyo huwa anaupeleka wapi Mamaβ nilisema nikiwaΒ nachagua Mchicha nilioutaka, mara nilisikia Mtu akikohoa nyuma yangu kama ishara kuwaΒ nigeuke ……Β
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TATU YA NILIOLEWANA MTU NISIYEMJUA… USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kupiga Simu Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza HapaΒ
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx
18 Comments
Jamani Saida kaolewa kwenye MISUKULE hatari.
Leo naona ni fupi jamani
Simulizi tamu.
Fupi jamani mwaka mpya tunaomba uturefushie kidg
JIni
Maneno yamepangika hakika.
Kazi nzuri sana
Y Leo ni fupi sn alafu mwendelezo unachekewesha mpk mtu unasahau . Hila simulizi ni tamu sn hongera .
Nina wsws na ba mkwe aisee kuwa ndo mtoa bikira
Hahaha ana nunua mchicha wa elfu 10 ana lisha kijiji
Anamuachaje mkewe na baba mkwee jmn
Hili la mchicha wa elfu kumi hata mimi nimecheka
ππ
Y Leo ni fupi sn alafu mwendelezo unachekewesha mpk mtu unasahau . Hila simulizi ni tamu sn hongera .
Kumeanza kuchangamka sasa
19697786
Ameyatimbaaaaaa
Mchicha elf 10 sio.kwel atakuw anamivugo
Yer kaz nzuri
Kazi anayo
Saidia π
Duuuh mchicha wa 10 huyo atakuwa na misukulee