Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Ni Wakati Wa Simba Kumuamini Kocha Mzawa?
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Ni Wakati Wa Simba Kumuamini Kocha Mzawa?

    Living ShayoBy Living ShayoApril 28, 2024Updated:April 28, 20246 Comments3 Mins Read999 Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Makocha wa klabu ya Simba
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Moja Ya muhimili mkubwa sana kwenye timu ni Uongozi imara wa timu husika lakini mafanikio yote Ya timu yanabebwa na muhimili muhimu kikosini ambapo msingi huo ni Kocha mkuu wa kikosi cha timu hiyo. Mafanikio yote Ya timu yanaanzia nje ila eneo mama zaidi ni ndani Ya uwanja ambapo uimara wake uundwa na Kocha mkuu.

    Klabu ya Simba SC hivi sasa inapitia kipindi kigumu sana na eneo Lao ni ndani Ya uwanja, kikosi kimekuwa na matokeo yasiyo na muendelezo bora wa kiuchezaji na kimatokeo pia na jambo ilo limepelekea kutokuwa na utulivu na kupelekea kubadilishwa kwa benchi la ufundi Mara kwa mara.

    Mara zote hizo walizoamua kubadilisha benchi la ufundi wamekuwa wakiajiri zaidi makocha wa nje au makocha wa kigeni kuanzia Pablo Martin, Roberto Oliviera na sasa Abdelhak Benchinka. Hata hivyo moja Ya njia Ya mafanikio ya timu ni kuwa na muendelezo wa kusimamia falsafa zao kwa usahihi na hiyo inaanzia kwa kuwa na Kocha mwenye mbinu na mifumo ambayo iko au inaendana na falsafa ya timu husika na jambo la pili ni kuwa na wachezaji sahihi kwa ajili ya falsafa  hiyo.

    Wapi Simba SC wanahitaji kuboresha kwa sasa? Jambo la kwanza kabisa ni kuwa na Kocha mkuu mwenye staili ya uchezaji ambayo inaendana na Faslafa ya timu hiyo. Simba SC chini ya Kocha Benchinka ni dhahiri kuwa Falsafa ya timu hiyo imekuwa haionekani kabisa, kwanini ? Falsafa mama ya Simba SC ni kucheza soka la chini la kuvutia kwa kuanzia chini huku wakiwa na utajiri wa kumiliki eneo la kiungo kama eneo mama la kuanzisha au kutengeneza mashambulizi na ndiyo maana wamepita wachezaji kadhaa wenye uwezo mkubwa wa kuonyesha soka safi kama Clatous Chama, Rally Bwalya, Haruna Chanongo, Emmanuel Okwi, Ibrahim Ajibu, Ramadhani Singano, Amri Kiemba na wengine wengi.

    Nani mtu muhimu kuirudisha “Style” ya uchezaji ya Simba SC kwa sasa ? Jibu ni Kocha ambaye ana uwezo wa kuisimamia Falsafa ya timu. Sasa swali lipo hapa ni wakati wa kumpa nafasi Kocha Mzawa ?

    Jibu langu siyo tu wakati huu bali hata nyuma ilikuwa inafanyika hivyo na tumeona wamekuwa wakifanya vizuri kiuchezaji na mfano wake ni Kibadeni, Matola na Juma Mgunda. Hivyo jambo muhimu siyo wao kupewa timu bali kupewa imani, ushirikiano na mahitaji yote muhimu ambayo wanapewa makocha wageni na mengine ambayo kama Kocha ataona yahitaji kwenye timu.

    Wako makocha wengi wazawa wenye uwezo mkubwa wa kuziongoza timu ya Simba SC na namna yao ya uchezaji kwa vilabu mbalimbali walivyopita na kufundisha vinalandana na namna Simba SC wanavyocheza wakipata timu kubwa na kupewa mahitaji yote muhimu kwa wakati na kuaminiwa basi wanaweza kuifikisha mbali mfano wao ni kama Mecky Mexime, Juma Mgunda ni kati ya makocha ni naona wanaweza kama wataaminiwa.

    Imani, matumaini, mshikamano na subra ni njia imara ya kuwapaisha wazawa wetu, kama tunaweza kuwaamini wageni na kuwapa nafasi wanaweza kufanya vizuri

    SOMA ZAIDI: Akiondoka Benchika , Tutegemee Simba Gani Msimu Ujao?

    Abdelhak Benchikha cv ya kocha mpya simba kocha kuondoka simba

    6 Comments

    1. NAUSHAD on April 28, 2024 1:43 pm

      Kama kocha wa kigeni anapewa resources zote na anaaminiwa why sio mzawa. I think MGUNDA is man for the job aaminiwe, apewe usaidizi akaongeze ujuzi naimani anakitu. Best coach Best coach MGUNDA

      Reply
    2. NAUSHAD on April 28, 2024 1:47 pm

      Makocha wanakuja na wanaondoka matola ni yule yule hamshtukii 😂.

      Reply
      • Met Millz on April 28, 2024 2:57 pm

        Si wameshachukua muungano wanataka nn Tena 😅

        Reply
    3. SUREBOY 🥸🤏 on April 28, 2024 1:54 pm

      Kocha hata awe wewe admn tukikupawachezaji wazurii unatamba mfano nkikupa kosi la gamondiii wewe utakwama wapiiii😂

      Unafikiri benchika ni mbovuuu mpeleke pale yanga uone,🪘🪘🪘

      Reply
    4. [email protected] on April 28, 2024 8:59 pm

      Namuona kijana wangu bocco uwanjan Tena n’a kitambaa châle 👀👀

      Reply
    5. Pingback: Tukiyafanya Haya Kiwango Cha Mpira Tanzania Kitapanda - Kijiweni

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.