Ilipoishiaย
“Sikia Jojo, ukiishi kwa kuhitaji huruma ya wengine utaishiaย kuishi Maisha ya hovyo sana. Lengo la kukutoa mle ni kutakaย kufanya na wewe baadhi ya Majukumu kisha utaachiliwa huru”ย Nilishtuka sana kusikia kuna majukumu nataka kupewa, nilifutaย chozi kisha nilimuulizaย
“Majukumu?”ย
“Ndiyo! Kwasasa angalia Afya yako kwa mwezi mzima kishaย utakapokuwa sawa nitakuchukua tena” Hakunipa hata nafasi yaย kumuuliza chochote kile, aliondoka zake. Yule Mdada mwingineย alisogea akaniambiaย
“Unapaswa kwenda Hospitali” Alininyanyua kisha alinitoa pale,ย Ulikuwa ni usiku mwingi sana, nilipelekwa Kwenye hospitali yaย pale pale Magereza.ย ย Endeleaย
SEHEMU YA TISA
Nilitibiwa kwa muda wa wiki kama mbili hivi, afya yanguย ilikaa sawa, nilikula ninachokitaka. Mwili wangu ulirudi,ย baada ya mwezi mzima wa kuwa pale Hospitali nilirudishwaย Ndani ya Gereza, nilirudi kwa akina Isabela ambao hawakuaminiย kama Nimerudi nikiwa mzima tena mwenye afya.ย
“Umewezaje Jojo? Tulijuwa huwezi kurudi tena kama wengineย walivyopotea hapa gerezani!” Alisema Isabelaย
“Ni stori ndefu sana Isabela ila nimeambiwa nitapewa majukumuย ya kufanya” nilisemaย
“Nje au ndani ya gereza?” Aliniulizaย
“Sijui Isabela, Baada ya afya kuimarika zaidi nitaambiwa”ย
“Sikia Jojo yaani Mkuu wa hili gereza nasikia ndiyo mchezoย wake, anawachukua wafungwa aliowachagua kisha anawatumikishaย kazi za hatari huko nje kisha wanamletea pesa! Anayesimamiaย ni Sarafina” Alisema Isabela.ย
“Kiukweli sijui Isabela, ngoja tuone na kama nitapata hiyoย nafasi ya kutoka hapa sitotamani kurudi tena, sitotamani tenaย kuendelea kubakia hapa Dar” nilisemaย
“Unafikiria kufanya nini?”ย
“Kurudi Tabora” Nilisema.ย
Basi Maisha yaliendelea, nilikuwa sifanyi kazi yoyote ndaniย ya Gereza zaidi ya kula chakula kizuri na kulala. Mwili wanguย ulijengeka sana, nikawa na Afya nzuri sana, Uzuri wanguย ulirejea kwa kishindo sana tena nilizidi kunawiri na kuwaย mweupe.ย
Mchana wa siku moja, Sarafina alikuja Kwenye chumba chetu,ย nilikuwa peke yangu tu sababu niliambiwa nisifanye kaziย yoyote ile. Nilipomuona nilijuwa ndio alikuwa amekuja kunipaย hiyo kazi ya kufanya, nilikaa vizuriย
“Naona sasa Afya yako ipo sawa Jojo, unaweza kuongozana naย Mimi” Alisema kisha tuliongozana, tulienda hadi kwenye Ofisiย ya Mkuu wa Magereza.ย
Ilikuwa ndiyo mara ya kwanza namuona huyo Mkuu wa Magereza,ย alionekana kuwa Mtu wa dili sana, basi tuliketi kisha Mkuuย huyo alisemaย
“Sarafina hapa umecheza kama Pele, huyu ndiye niliyekuwaย namtaka. Nimeambiwa unaitwa Jojo, umefungwa kwa kosa laย kukamatwa ukiwa unajiuza, unapaswa kutumikia Kifungo chaย Miaka mitatu ila nataka kukupa ofa. Kuna kazi nataka kukupa,ย ukiifanya nitakuachia huru” Alisema Mkuu huyo, niliposikiaย kuwa nitaachiwa huru nilijawa na shahuku sana ya kutakaย kujuwa nilitakiwa kupewa kazi gani.ย
“Sarafina utampa mpango wenyewe kisha utamuandaa kuifanyaย kazi” Alisema Mkuu huyo kisha Mimi na Sarafina tulitoka,ย tulienda mahali ambapo kulikuwa na Bustani ndogo nyuma yaย kantini ya Askari.ย
“Jojo, ubaya wangu ndiyo uzuri wangu inategemea unanitazamaย vipi, nilikuwa na uwezo wa kukuacha ufe mle kwenye chumbaย lakini nilikutoa sababu nilitaka uwe huru” Alisema Sarafinaย kisha aliendelea kusemaย
“Kuna mfanyabiashara wa Madini anaitwa Vitalis Kyando, niย Bilionea wa madini. Anakuja hapa Dar kesho kutwa kwa ajili yaย mauzo ya Madini, ni Mtu mwenye ulinzi mkali sana. Atafikiaย Hyat Hotel, ataishi hapo kwa siku mbili kabla ya kukutana naย Waarabu kutoka Moroco ambao ndiyo Wateja wake. Tutakuingizaย hapo kwa kazi moja tu, kutumia uzuri wako kumnasa kablaย hajafanya Biashara. Tunayataka hayo Madini ambayo yanatajwaย kuwa na thamani ya Bilioni 20 za Kitanzania, unapaswaย kuyaiba. Ukishafanikisha utaachwa huru utaendelea na Maishaย yako” Alisema Sarafinaย
“Huuuuh!” Nilishusha pumzi zangu, jukumu hilo lilikuwa zitoย sana kwangu, nilimwambia Sarafinaย
“Sidhani kama nitaweza Sarafina”
“Utaweza tu sababu unahitaji kuwa huru haraka iwezekanavyo”ย Alikazia msumariย
“Nenda, Usiku tutaondoka hapa” Alisema Tena Sarafinaย
“Kabla ya kazi hiyo naomba kuonana na Shonaa, nimesahauย anapoishi, nahitaji kumshukuru kwa wema alionifanyia”ย Nilisema kisha nilimuona Sarafina akifikiriaย
“Sawa! Lakini hupaswi kufanya ujanja wowote sababu ukifanyaย hivyo utatajwa kuwa ulitoroka Gerezani, utakamatwa naย kurudishwa huku tena utaongezewa miaka ya kukaa hapa, Shonaaย hapaswi kujuwa chochote kile” Alisema Sarafinaย
“Sawa nimekuelewa” nilimjibu kisha alinirudisha kwenye chumbaย cha gereza, nilikuta wenzangu wakiwa wamerudi kutoka kwenyeย kazi ngumuย
“Ulikuwa wapi Jojo!” Aliniuliza Isabelaย
“Nipo Usijali Isabela, asante kwa ukarimu na moyo wako, usikuย wa leo nitaenda kutekeleza jukumu zito sana. Kama nitarudi auย sitorudi usiache kuniombea” Nilisema, Isabela aliendeleaย kuniuliza maswali lakini sikutaka kusema kingine.ย
Basi, Usiku ulipoingia Alitumwa Mtu kuja kuniita, niliendaย kuonana na Sarafina kisha tulitoka na gari la Mkuu waย Magereza. Alienda kutuacha kwenye ghorofa moja karibu naย kanisa la Azania Front mjini Posta.ย
Tulipanda juu kulikuwa na chumba kimoja ambachoย kilitengenezwa ili tuishi humo hadi tutakapo maliza mpangoย huo. Tulilala hapo Mimi na Sarafina, asubuhi nilimkumbushaย kuhusu kwenda kumuona Shonaa, aliniambia nijiandae sababuย baada ya kwenda huko tutaenda kariakoo kutafuta nguo zaย kuvaa, wakati huo nilikua nimevalia nguo zake.ย
Alinipeleka Sinza majira ya saa tatu asubuhi, tulikuwa kwenyeย gari nikapata kumuona Shonaa kwa mbali akiwa anacheka naย baadhi ya Wateja, Chozi lilinibubujika sana.ย
“Una nusu saa pekee ya kwenda kwa Shonaa kisha urudi ndani yaย gari tuondoke” Alisema Sarafinaย
“Asante Sarafina” nilisema kisha nilifuta chozi languย
Nilitembea taratibu kisha nilisimama karibu na Shonaa nikiwaย ninamtazama jinsi alivyokuwa anacheka, nilikumbuka jinsiย alivyojitoa kunisaidia hadi alinipa nauli ya kurudi Tabora ila Bahati mbaya yalitokea ya kutokea nilishindwa kuondokaย hadi kujikuta kwenye matatizo makubwa mno.ย
Basi nilijitoa pale kisha nilimkimbilia na kumkumbatia kwaย nyuma, chozi lilinibubujika. Alishangaa ni naniย aliyemkumbatiaย
“Nimekumis sana Shonaa” nilisema, aliitambua sauti yanguย haraka akaniitaย
“Shonaa” kisha haraka akageuka, akanishika mkono akanipelekaย nyuma ya Jengo.ย
“Nimekutoa sababu Bosi yupo sitaki aanze kuniuliza maswaliย kuhusu wewe, siamini Jojo kama nimekuona tena leo” alisemaย kisha alinikumbatia tenaย
“Za siku nyingi Jojo, umependeza sana. Ndiyo maanaย nilikwambia urudi nyumbani si unaona ulivyo nawiri” Alisemaย Shonaa bila kujuwa kuwa sikuwahi kuondoka kwa kipindi choteย hichoย
“Ndio maana siwezi kukusahau Shonaa, ushauri wako umenisaidiaย sana. Nimerudi kukushukuru”ย
“Basi nilisubiria sana simu yako hadi nikapatwa na mashakaย umekumbwa na nini?” Basi nilicheka tu ili kumfanya Shonaaย asiingiwe na hofuย
“Yaani simu ile niliipoteza ndio nikapoteza na namba yakoย kabisa”ย
“Masikini pole sana Jojo, unaishi wapi kwa sasa?”ย
“Nimekuja tu kwa Dada yangu mmoja hivi wa kule Tabora”ย Niliangalia saa yangu niliona muda wa kuwa pale ulikuwaย umeisha, ili nisiharibu mambo nilimwambia Shonaaย
“Dada yangu ananisubiria kwenye gari kule kwahiyo ngojaย nirudi tutaonana siku nyingine”ย
“Ngoja nije kumuona Dada yako basi” Alisema Shonaaย
“Hapana usijali Shonaa, utamuona siku nyingine” Basiย niliondoka zangu pale kwenye gariย
“Hujamwambia Chochote?” Aliuliza Sarafina
“Hapana sijamwambia chochote” nilimjibu, safari ya kutokaย Sinza kuelekea Kariakoo ilianza, nililikariri lile eneoย ambalo tulienda ili kama kitatokea chochote basi nimtafuteย Shonaa.ย
Tulienda kwneye maduka yanayouza nguo nzuri za kiarabu,ย nilichagua na zingine alinichagulia Sarafina ili kesho yakeย niende Hyat Hotel. Niliambiwa paliandaliwa sherehe fulani yaย kuadhimisha miaka kadhaa ya Hoteli hiyo hivyo miongoni mwaย watakaokuwepo atakuwa ni huyo Bilionea wa madini.ย
Tulirudi kule kwenye ghorofa la Tancot House ambapo ndiyoย tulilala usiku uliopita, Nilijaribu nguo zote ikapatikanaย moja tu ambayo ilionekana kuwa nzuri sana na yenyeย kunipendeza zaidiย
“Wow!! Hii ndiyo yenyewe Jojo, nina uhakika hawezi kuchomoka,ย sasa unapaswa kuwa makini sana sababu ni lazima akuchukueย kama kimada wa kulala naye Usiku, ndipo utakapo iba hayoย madini, utachunguza kujuwa yalipo, baada ya kufanikishaย zoezi, utafungua dirisha sababu chumba chake kipo masharikiย mwa jengo hilo, utayatupa madini kwa kutumia kifaa ambachoย kitakuwa kimehifadhi kisha utayachukua baada ya kushuka, kuwaย makini sana vinginevyo unaweza ishia huko Hotelini, pia niย lazima ukamilishe zoezi ili uwe huru” alinieleza Sarafinaย
Nini Kitaendeea?ย Nione COMMENT NYINGI LEO au MSHAICHOKA TUACHE KUIPOST?ย
Usikose SEHEMU YA KUMI ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xxย
13 Comments
Hatujacboka admin endelea kuleta vitu
Mh bilioni 20
Mtunz uko sawa
Dah tamu sana ila fupi admin
Jojo analo mbona๐
Amepewa kazi ngumu yakuweka maisha yake rehani
Naona kabisaa hatoboi na anakula adhabu nyingine jela
Duh patamu apo alaf mbna fup asee ๐๐
Aysee natamani kiliona picha likichezwa laivu. Kwanjinsi ulivyo waumba wahusika duuh simchezo hongera mtunzi. Ila episode zimekuwa fupi!!!!!!๐
Ukiskia kusahauliwa na Mungu Niko huku , siyo kuumwa malaria kidogo unalialia
3unsid
cji8mn
ycb6az