IlipoishiaΒ
“Sikia Jojo, ukiishi kwa kuhitaji huruma ya wengine utaishiaΒ kuishi Maisha ya hovyo sana. Lengo la kukutoa mle ni kutakaΒ kufanya na wewe baadhi ya Majukumu kisha utaachiliwa huru”Β Nilishtuka sana kusikia kuna majukumu nataka kupewa, nilifutaΒ chozi kisha nilimuulizaΒ
“Majukumu?”Β
“Ndiyo! Kwasasa angalia Afya yako kwa mwezi mzima kishaΒ utakapokuwa sawa nitakuchukua tena” Hakunipa hata nafasi yaΒ kumuuliza chochote kile, aliondoka zake. Yule Mdada mwingineΒ alisogea akaniambiaΒ
“Unapaswa kwenda Hospitali” Alininyanyua kisha alinitoa pale,Β Ulikuwa ni usiku mwingi sana, nilipelekwa Kwenye hospitali yaΒ pale pale Magereza.Β Β EndeleaΒ
SEHEMU YA TISA
Nilitibiwa kwa muda wa wiki kama mbili hivi, afya yanguΒ ilikaa sawa, nilikula ninachokitaka. Mwili wangu ulirudi,Β baada ya mwezi mzima wa kuwa pale Hospitali nilirudishwaΒ Ndani ya Gereza, nilirudi kwa akina Isabela ambao hawakuaminiΒ kama Nimerudi nikiwa mzima tena mwenye afya.Β
“Umewezaje Jojo? Tulijuwa huwezi kurudi tena kama wengineΒ walivyopotea hapa gerezani!” Alisema IsabelaΒ
“Ni stori ndefu sana Isabela ila nimeambiwa nitapewa majukumuΒ ya kufanya” nilisemaΒ
“Nje au ndani ya gereza?” AliniulizaΒ
“Sijui Isabela, Baada ya afya kuimarika zaidi nitaambiwa”Β
“Sikia Jojo yaani Mkuu wa hili gereza nasikia ndiyo mchezoΒ wake, anawachukua wafungwa aliowachagua kisha anawatumikishaΒ kazi za hatari huko nje kisha wanamletea pesa! AnayesimamiaΒ ni Sarafina” Alisema Isabela.Β
“Kiukweli sijui Isabela, ngoja tuone na kama nitapata hiyoΒ nafasi ya kutoka hapa sitotamani kurudi tena, sitotamani tenaΒ kuendelea kubakia hapa Dar” nilisemaΒ
“Unafikiria kufanya nini?”Β
“Kurudi Tabora” Nilisema.Β
Basi Maisha yaliendelea, nilikuwa sifanyi kazi yoyote ndaniΒ ya Gereza zaidi ya kula chakula kizuri na kulala. Mwili wanguΒ ulijengeka sana, nikawa na Afya nzuri sana, Uzuri wanguΒ ulirejea kwa kishindo sana tena nilizidi kunawiri na kuwaΒ mweupe.Β
Mchana wa siku moja, Sarafina alikuja Kwenye chumba chetu,Β nilikuwa peke yangu tu sababu niliambiwa nisifanye kaziΒ yoyote ile. Nilipomuona nilijuwa ndio alikuwa amekuja kunipaΒ hiyo kazi ya kufanya, nilikaa vizuriΒ
“Naona sasa Afya yako ipo sawa Jojo, unaweza kuongozana naΒ Mimi” Alisema kisha tuliongozana, tulienda hadi kwenye OfisiΒ ya Mkuu wa Magereza.Β
Ilikuwa ndiyo mara ya kwanza namuona huyo Mkuu wa Magereza,Β alionekana kuwa Mtu wa dili sana, basi tuliketi kisha MkuuΒ huyo alisemaΒ
“Sarafina hapa umecheza kama Pele, huyu ndiye niliyekuwaΒ namtaka. Nimeambiwa unaitwa Jojo, umefungwa kwa kosa laΒ kukamatwa ukiwa unajiuza, unapaswa kutumikia Kifungo chaΒ Miaka mitatu ila nataka kukupa ofa. Kuna kazi nataka kukupa,Β ukiifanya nitakuachia huru” Alisema Mkuu huyo, niliposikiaΒ kuwa nitaachiwa huru nilijawa na shahuku sana ya kutakaΒ kujuwa nilitakiwa kupewa kazi gani.Β
“Sarafina utampa mpango wenyewe kisha utamuandaa kuifanyaΒ kazi” Alisema Mkuu huyo kisha Mimi na Sarafina tulitoka,Β tulienda mahali ambapo kulikuwa na Bustani ndogo nyuma yaΒ kantini ya Askari.Β
“Jojo, ubaya wangu ndiyo uzuri wangu inategemea unanitazamaΒ vipi, nilikuwa na uwezo wa kukuacha ufe mle kwenye chumbaΒ lakini nilikutoa sababu nilitaka uwe huru” Alisema SarafinaΒ kisha aliendelea kusemaΒ
“Kuna mfanyabiashara wa Madini anaitwa Vitalis Kyando, niΒ Bilionea wa madini. Anakuja hapa Dar kesho kutwa kwa ajili yaΒ mauzo ya Madini, ni Mtu mwenye ulinzi mkali sana. AtafikiaΒ Hyat Hotel, ataishi hapo kwa siku mbili kabla ya kukutana naΒ Waarabu kutoka Moroco ambao ndiyo Wateja wake. TutakuingizaΒ hapo kwa kazi moja tu, kutumia uzuri wako kumnasa kablaΒ hajafanya Biashara. Tunayataka hayo Madini ambayo yanatajwaΒ kuwa na thamani ya Bilioni 20 za Kitanzania, unapaswaΒ kuyaiba. Ukishafanikisha utaachwa huru utaendelea na MaishaΒ yako” Alisema SarafinaΒ
“Huuuuh!” Nilishusha pumzi zangu, jukumu hilo lilikuwa zitoΒ sana kwangu, nilimwambia SarafinaΒ
“Sidhani kama nitaweza Sarafina”
“Utaweza tu sababu unahitaji kuwa huru haraka iwezekanavyo”Β Alikazia msumariΒ
“Nenda, Usiku tutaondoka hapa” Alisema Tena SarafinaΒ
“Kabla ya kazi hiyo naomba kuonana na Shonaa, nimesahauΒ anapoishi, nahitaji kumshukuru kwa wema alionifanyia”Β Nilisema kisha nilimuona Sarafina akifikiriaΒ
“Sawa! Lakini hupaswi kufanya ujanja wowote sababu ukifanyaΒ hivyo utatajwa kuwa ulitoroka Gerezani, utakamatwa naΒ kurudishwa huku tena utaongezewa miaka ya kukaa hapa, ShonaaΒ hapaswi kujuwa chochote kile” Alisema SarafinaΒ
“Sawa nimekuelewa” nilimjibu kisha alinirudisha kwenye chumbaΒ cha gereza, nilikuta wenzangu wakiwa wamerudi kutoka kwenyeΒ kazi ngumuΒ
“Ulikuwa wapi Jojo!” Aliniuliza IsabelaΒ
“Nipo Usijali Isabela, asante kwa ukarimu na moyo wako, usikuΒ wa leo nitaenda kutekeleza jukumu zito sana. Kama nitarudi auΒ sitorudi usiache kuniombea” Nilisema, Isabela aliendeleaΒ kuniuliza maswali lakini sikutaka kusema kingine.Β
Basi, Usiku ulipoingia Alitumwa Mtu kuja kuniita, niliendaΒ kuonana na Sarafina kisha tulitoka na gari la Mkuu waΒ Magereza. Alienda kutuacha kwenye ghorofa moja karibu naΒ kanisa la Azania Front mjini Posta.Β
Tulipanda juu kulikuwa na chumba kimoja ambachoΒ kilitengenezwa ili tuishi humo hadi tutakapo maliza mpangoΒ huo. Tulilala hapo Mimi na Sarafina, asubuhi nilimkumbushaΒ kuhusu kwenda kumuona Shonaa, aliniambia nijiandae sababuΒ baada ya kwenda huko tutaenda kariakoo kutafuta nguo zaΒ kuvaa, wakati huo nilikua nimevalia nguo zake.Β
Alinipeleka Sinza majira ya saa tatu asubuhi, tulikuwa kwenyeΒ gari nikapata kumuona Shonaa kwa mbali akiwa anacheka naΒ baadhi ya Wateja, Chozi lilinibubujika sana.Β
“Una nusu saa pekee ya kwenda kwa Shonaa kisha urudi ndani yaΒ gari tuondoke” Alisema SarafinaΒ
“Asante Sarafina” nilisema kisha nilifuta chozi languΒ
Nilitembea taratibu kisha nilisimama karibu na Shonaa nikiwaΒ ninamtazama jinsi alivyokuwa anacheka, nilikumbuka jinsiΒ alivyojitoa kunisaidia hadi alinipa nauli ya kurudi Tabora ila Bahati mbaya yalitokea ya kutokea nilishindwa kuondokaΒ hadi kujikuta kwenye matatizo makubwa mno.Β
Basi nilijitoa pale kisha nilimkimbilia na kumkumbatia kwaΒ nyuma, chozi lilinibubujika. Alishangaa ni naniΒ aliyemkumbatiaΒ
“Nimekumis sana Shonaa” nilisema, aliitambua sauti yanguΒ haraka akaniitaΒ
“Shonaa” kisha haraka akageuka, akanishika mkono akanipelekaΒ nyuma ya Jengo.Β
“Nimekutoa sababu Bosi yupo sitaki aanze kuniuliza maswaliΒ kuhusu wewe, siamini Jojo kama nimekuona tena leo” alisemaΒ kisha alinikumbatia tenaΒ
“Za siku nyingi Jojo, umependeza sana. Ndiyo maanaΒ nilikwambia urudi nyumbani si unaona ulivyo nawiri” AlisemaΒ Shonaa bila kujuwa kuwa sikuwahi kuondoka kwa kipindi choteΒ hichoΒ
“Ndio maana siwezi kukusahau Shonaa, ushauri wako umenisaidiaΒ sana. Nimerudi kukushukuru”Β
“Basi nilisubiria sana simu yako hadi nikapatwa na mashakaΒ umekumbwa na nini?” Basi nilicheka tu ili kumfanya ShonaaΒ asiingiwe na hofuΒ
“Yaani simu ile niliipoteza ndio nikapoteza na namba yakoΒ kabisa”Β
“Masikini pole sana Jojo, unaishi wapi kwa sasa?”Β
“Nimekuja tu kwa Dada yangu mmoja hivi wa kule Tabora”Β Niliangalia saa yangu niliona muda wa kuwa pale ulikuwaΒ umeisha, ili nisiharibu mambo nilimwambia ShonaaΒ
“Dada yangu ananisubiria kwenye gari kule kwahiyo ngojaΒ nirudi tutaonana siku nyingine”Β
“Ngoja nije kumuona Dada yako basi” Alisema ShonaaΒ
“Hapana usijali Shonaa, utamuona siku nyingine” BasiΒ niliondoka zangu pale kwenye gariΒ
“Hujamwambia Chochote?” Aliuliza Sarafina
“Hapana sijamwambia chochote” nilimjibu, safari ya kutokaΒ Sinza kuelekea Kariakoo ilianza, nililikariri lile eneoΒ ambalo tulienda ili kama kitatokea chochote basi nimtafuteΒ Shonaa.Β
Tulienda kwneye maduka yanayouza nguo nzuri za kiarabu,Β nilichagua na zingine alinichagulia Sarafina ili kesho yakeΒ niende Hyat Hotel. Niliambiwa paliandaliwa sherehe fulani yaΒ kuadhimisha miaka kadhaa ya Hoteli hiyo hivyo miongoni mwaΒ watakaokuwepo atakuwa ni huyo Bilionea wa madini.Β
Tulirudi kule kwenye ghorofa la Tancot House ambapo ndiyoΒ tulilala usiku uliopita, Nilijaribu nguo zote ikapatikanaΒ moja tu ambayo ilionekana kuwa nzuri sana na yenyeΒ kunipendeza zaidiΒ
“Wow!! Hii ndiyo yenyewe Jojo, nina uhakika hawezi kuchomoka,Β sasa unapaswa kuwa makini sana sababu ni lazima akuchukueΒ kama kimada wa kulala naye Usiku, ndipo utakapo iba hayoΒ madini, utachunguza kujuwa yalipo, baada ya kufanikishaΒ zoezi, utafungua dirisha sababu chumba chake kipo masharikiΒ mwa jengo hilo, utayatupa madini kwa kutumia kifaa ambachoΒ kitakuwa kimehifadhi kisha utayachukua baada ya kushuka, kuwaΒ makini sana vinginevyo unaweza ishia huko Hotelini, pia niΒ lazima ukamilishe zoezi ili uwe huru” alinieleza SarafinaΒ
Nini Kitaendeea?Β Nione COMMENT NYINGI LEO au MSHAICHOKA TUACHE KUIPOST?Β
Usikose SEHEMU YA KUMI ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xxΒ
13 Comments
Hatujacboka admin endelea kuleta vitu
Mh bilioni 20
Mtunz uko sawa
Dah tamu sana ila fupi admin
Jojo analo mbonaπ
Amepewa kazi ngumu yakuweka maisha yake rehani
Naona kabisaa hatoboi na anakula adhabu nyingine jela
Duh patamu apo alaf mbna fup asee ππ
Aysee natamani kiliona picha likichezwa laivu. Kwanjinsi ulivyo waumba wahusika duuh simchezo hongera mtunzi. Ila episode zimekuwa fupi!!!!!!π
Ukiskia kusahauliwa na Mungu Niko huku , siyo kuumwa malaria kidogo unalialia
3unsid
cji8mn
ycb6az