Ilipoishia “Najuwa unaumia Jojo ila utazoea tu sababu hata Mimi nilikuwaย kama wewe siku ya kwanza naanza kazi, nilikuwa mnyonge,ย sikuzoea kuvaa hivi ila ilinibidi nikubali hali halisi”ย
Alisema Shonaa akiwa ananiangalia vizuri kama vile alikuwaย akinikagua, nilionesha lile tabasamu fekiย
“Kuna nini?” Nilimuuliza, alinishika nywele zangu akazibanaย kwa kutumia mpira aliokuwa ameushika mkononiย
“Wewe ni mzuri sana Jojo” Alisema kisha aliachia tabasamuย lililotoka moyoni mwake kabisa, hata mimi niliachia tabasamuย lililotoka moyoniย
“Asante!” Nilimshukuru, tulikuwa wawili tu sababu wengineย walienda zamu ya Jioni hiyo kurudi hadi asubuhi.
Endeleaย
SEHEMU YA TATU
“Vumilia Jojo utakuwa sawa tu” Alisema tena Shonaa kishaย alinyanyuka akatoka ndani, alikuwa na moyo wa peke yake, kunaย wakati nilijiona nipo sawa pindi ninapozungumza na Shonaa.ย
Nilijilaza kitandani, kutokana na ule uchovu nilijikutaย nikipitiwa na Usingizi, niliamka mishale ya saa tatu usiku,ย nilimuona Shonaa akivaa nguo, alivalia Baibui hadiย nilishangaa, nilihitaji kumuuliza anaenda wapi?ย
“Shonaa unaenda wapi tena?” Nilimuuliza nikiwa ninatabasamu,ย kiufupi alipendeza sanaย
“Naenda kwa Bwana wangu” Alijibu akiwa anajipodoa,ย nilinyanyuka kwanza ili niseme kituย
“Bwana wako? Ina maana umeolewa?”ย
“Hapana ni Boyfriend tu, vipi mbona unanishangaa?”ย
“Umependeza sana unaonekana ni mwenye Heshima kubwa snaaย Shonaa” Nilisema, nilimfanya achekeย
“Ndio nina heshima kwani naonekana sina heshima?” Aliniulizaย
“Hapana…ninachomaanisha yale mavazi ya kazini yanakufanyaย uwe tofauti sana na jinsi ulivyo sasa” Nilisemaย
“Jojo Maisha haya yatakufundisha vitu vingi sana, yatumieย vizuri uone kile ambacho macho yako ya kawaida hayaweziย kuona”ย
“Una maana gani Shonaa?”ย
Shonaa hakunijibu chochote, alipomaliza kujiandaa aliondokaย zake, nilipata muda wa kuwa peke yangu, usiku huo niliona niย bora niwasiliane na Msonjo ili anipe mrejesho wa kileย alichozungumza na Bosi Muntaza, nilipiga simu lakiniย haikupokelewa hadi baadaye kidogo aliponipigia yeyeย
“Griii! Grii!” Ulikuwa ni mlio wa simu yangu, ilikuwa tayariย nimepitiwa na Usingizi, niliamka na kuipokeaย
“Hallo Msonjo” Nilisema kwa sauti ya uchovuย
“Mambo Jojo” Alisema Msonjoย
“Mambo mabaya Msonjo vipi umeshaongea na Bosi anipe nauli?”
“Nimeongea naye ila kasema hawezi kupoteza pesa yake kwa Mtuย ambaye hajafanya kazi yoyote” Alinijibu Msonjo, moyo uliniumaย sanaย
“Sasa Msonjo….huwezi kuazima sehemu nikifika nitakurudishiaย tafadhari”ย
“Mmh! Jojo nisikuongopee hapa sina wa kumuazima pesa,ย ninachoweza kukushauri ni kwamba fanya kazi kwa muda iliย uweze kuipata hiyo pesa”.ย
“Yaani Msonjo katika vitu nimebugi katika Maisha yangu basiย ni kuja huku Dar, naona kama nipo kwenye chumba chenye gizaย na joto kali, najiona mwenyewe tu na sina Mtu wa kunisaidia”ย Nilisema, Chozi lilianza kunilenga, Msonjo aligundua kuwaย nakaribia kulia kutokana na jinsi sauti yangu ilivyokuwaย ikitoka.ย
“Jojo huna sababu ya Kulia, pambana huko Dar….pengineย baadaye unaweza ukabadilisha kauli baada ya kuona mamboย yanakunyookea, cha Msingi sasa hivi kaza Buti” Alisema Msonjoย kwa maneno rahisi sana, niliona siwezi kuupata Msaadaย niliokuwa nautaka kutoka kwake nilimuagaย
“Msonjo….nakutakia Usiku mwema” Nilisema kishaย jilisikikizia jibu la Msonjo lakiji hakujibu chochote kile,ย nilikata simu na kuanza kulia, niliona kama Msonjo alikuwaย ameniuza Jiji Dar, nililitazmaa Begi langu, nilikumbuka ninaย elfu kumi tu tena hata Jiji silijui kabisaa.ย
“Eeh Malaika wa Mama yangu naomba Mniongoze, nahisi kushindwaย na kukata tamaa kabisa, Mungu unaniona?” Nilisema huku choziย likinibubujika, ilikuwa mishale ya saa nne za Usiku. Mlangoย uligongwa tena mgongaji aliita jina la Shonaa, ilikuwa niย sauti ya Mama wa Makamo aliyeonesha kuwa na jazba ya jamboย fulani mana jinsi alivyoita Mmh!!ย
“Shonaa hayupo” Nilijibu nikiwa chumbaniย
“Njoo wewe” Alisema Mama huyo kwa shari sana, sikumjuwa naย wala hakuwa akinijuwa, basi niliingiwa na woga sana nilitokaย ndani.ย
“Shikamoo Mama” Nilimsalimu kwa adabu sanaย
“Shikamoo mwenyewe, kama unaona hiyo shikamoo Mali basi ikateย iweke kwenye sufuria igeuke nyama ya Mbuzi…hivi nyieย mnatuchukuliaje humu ndani?” Aliuliza kwa shari ile ile
“Kwani kuna nini Mama yangu” Nilimuuliza maana woga ulikuwaย umenishikaย
“Hebu twende” Alinishika mkono kwa nguvu akawa ananipelekaย njia ya Chooni, aliniingiza hadi chooniย
“Nini kile?” Alionesha kidole kwenye karo la Choo, Aah yaaniย kulikuwa na haja kubwa iliyokuwa haijamwagiwa majiย
“Hizo pombe mnazokunywa sisi tumekunywa kitambo na tukaziachaย sababu hazina faida yoyote, wenyewe mnaona Ujanja si ndiyo?ย Sasa safisha hapo haraka sana nataka kuoga” Alisema Mama huyoย kwa hasira sanaย
“Lakini Mama mimi ni mgeni hapa na sijui chochote kile”ย Nilijitetea kwa sauti ya chini sana, mkononi nilikuwaย nimeshikilia simu yangu ndogo, sasa yule Mama alinisukumizaย nishike Fagio, simu ikaangukia kwenye shimo la chooย
“Simu yangu” Nilisema kwa maumivu makali sana, simu ileย ilikuwa ndio msaada mkubwa kwangu kuwasiliana na Msonjo naย Watu wengine ambao walikuwa Tabora.ย
“Nyooo! Usinilegezee sauti, hebu fanya Usafi fastaa” Alisemaย Mama huyo, kwa jisni alivyochukia ilinilazimu haraka sanaย kushika fagio, Mama huyo alitoka nje. Macho yangu yalijaaย machozi ya maumivu makali sana niliwaza ndani ya akili yanguย
“Haya ndiyo Maisha gani jamani ni Bora ningekufa njaa Tabora,ย Mama umeniacha unaona sasa yanayonikuta Mwanao” Nilijisemeaย huku chozi likizidi kunibubujika, nilifanya Usafi nikiwaย ninalia hadi nilipomaliza kisha nilitokaย
“Subiria hapo hapo niangalie Kama umesafisha vizuri” Alisemaย Mama huyo kisha aliingia chooni kuangalia, baada ya sekundeย chache alitokaย
“Bahati yako, haya sepa” Alisema, nilimuogopa mno, ilinibidiย haraka nishike njia ya kurudi ndani, nyuma nilisikia sautiย yake akicheka kisha alisemaย
“Mjini shule” Jamani niliumia sana, moyo ulimwaga chozi laย damu lenye Maumivu, nilikuwa Msichana mpole sana ambayeย sikuweza kujibizana na Mtu yeyote yule.ย
Nilipofika chumbani niliongeza kilio, Chozi lilinimwagikaย nikiwa nimejitupa kitandani. Jiji la Dar liligeuka kuwaย chungu sana kwangu, kabla hata sijatulia nilisikia tenaย Mlango ukigongwa, niliogopa sana nilijifuta chozi harakaย kisha niliuliza
“Nani?” Niliuliza kwa sauti ya upole mno tena iliyojaa wogaย
“Fungua wewe” nilisikia sauti ya Mdada mmoja ambayeย tulimuacha akiwa amelala asubuhi, ilikuwa ni sautiย iliyoambatana na Ulevi.ย
Mara moja nilienda kumfungulia, ile nafungua tu nilikutana naย tusi la nguoni, tena aliyetukanwa alikuwa ni Marehemu Mamaย yangu Masikiniย
“Malaya wewe! Unajiona mzuri ndio hufungui mlango eeeh?”ย Alisema yule Mdada, nilichukia sana kisha nilienda chumbaniย wala sikutaka kubishana naye. Alikuwa ameongozana naย Mwanaume, wote walikuja chumbani.ย
Yaani kilichonikausha kilio changu kilikuwa ni kitendo chaoย cha kuondoa nguo zao zote kisha kuanza kufanya mapenzi mbeleย yangu bila hata Aibu, sikuweza kuwavumilia nilitoka chumbani,ย kelele zao zilikuwa juu hata sebleni niliona hapakuwa salamaย kwangu, nilienda nje kabisa. Ndani ya muda mfupi nilikutanaย na matukio yaliyoniacha kinywa wazi, mambo ambayo nilikuwaย nasimuliwa na Watu kuwa wameona katika filamu ndiyo nilikuwaย nikiyashuhudia kwa macho yangu, nilitamani sana kumpigia simuย Shonaa nimueleze maana angalau yeye tulikuwa tukiiva chunguย kimoja lakini ndiyo hivyo tena simu ilikuwa imeingia Chooni.ย
Nilikaa nje kwa zaidi ya Masaa mawili nikiwa ninalia, baadayeย nilirudi ndani, palikuwa pametulia, basi nilifunga mlangoย kisha nilijilaza kwenye kochi nikiwa nimevalia zangu dera.ย
Sijui hata ilikuwa ni saa ngapi, nilishtuka tu nilihisi mkonoย ukinichezea makalio yangu, nilipoamka nilimuona yule Mwanaumeย ambaye alikuja na yule Mdada. Nilimuulizaย
“Wewe ni Nani na Unataka nini?” Niliuliza huku nikiwaย nimejaza woga kwenye kifua changu, nilijisogeza nyuma kabisaย ya Kochiย
“Shiii” Alinipa ishara kuwa sipaswi kusema chochote kile,ย alitoa kisu akaniambiaย
“Ukipiga kelele Nakuchoma kisu sasa hivi” Alisema akiwaย ananionesha na ishara kabisa jinsi atakavyo nichoma hichoย kisu.ย
Kwa mara ya kwanza katika Maisha yangu niliona Munguย amenitazama, yule Mdada alikuwa ameamka hakumuona Mtu wakeย hivyo akaja sebleni na kukuta yule jamaa akiwa amenishikiliaย kisu, aliposikia sauti ya Mwanamke wake alikitupa kile kisu.ย
Bahati nzuri taa ilikuwa inawaka maana nilikuwa siwezi kulalaย bila taa, alikiona kile kisuย
“Unaniacha chumbani unakuja kwa huyu Malaya si ndiyo?”ย Alisema yule Mdada, nilihema juu juuย
“Unafanya nini hapa?” Alihoji yule Mdada, alimshushia kipigoย yule Mwanaume hadi nilishangaa, Mwanamke anaweza vipi kumpigaย Mwanaume namna ile? Hadi niliingilia kati maana alishamtoaย damu kinywaniย
“Wewe malaya hayakuhusu haya, una kesi na Mimi kwahiyo subiriย hivyo hivyo” Alisema yule Mdada, basi aliendelea kumpiga,ย alipochoka alimwambiaย
“Tembea nisikuone tena hapa Shwaini Mkubwa wewe” Alisema yuleย Mdada, yule Jamaa aliposikia hivyo aliona kama vile alikuwaย ametembelewa na Malaika mtoa roho alafu akamuacha basiย alijipigiza kwenye mlango akafungua na kukimbia zake,ย nilijikuta nikicheka japo kwa sauti ya chini maana Yule Mdadaย naye alicheka kidogo kisha aliacha kucheka alafu akaniangaliaย kwa jicho kaliย
“Ukijilegeza utaliwa!” Alisema yule mdada kisha aliongozaย kuelekea chumbaniย
“Samahani”nilisema kwa woga, alisimamaย
“Unaitwa Nani?” Nilimuuliza, alicheka kisha alinijibu “Sarafina” Alijibu na kuingia chumbani.ย
Japo mambo yale yalikuwa mageni kwangu na yenye kuniumiza ilaย yalinifundisha vitu vingi sana ambavyo hata kama ningesomaย hadi ngazi ya digrii nisingeliweza kujifunza. Usingiziย haukuja kabisaa nilikaa macho hadi niliposikia adhanaย wakiazini msikiti wa jirani ndipo nilipofahamu kuwa palikuwaย pamepambazuka.ย
Tulikuwa na zamu ya kwenda kule Dar City Mimi na Shonaa,ย nilijiandaa. Muda ulienda nikiwa ninamsubiria Shonaa, Juaย lilipoanza kutua Shonaa alirudi akiwa mwenye furaha,ย alinionesha kiasi cha pesa alichokiingiza.ย
Kilikuwa ni zaidi ya laki moja, niliitamani pesa hiyo maanaย kama ningeliipata basi ingenitosha kwa Nauli ya kuelekeaย Tabora, aliketi lakini aliniona nikiwa sina fruaha kabisa. Nini Kitaendelea
Usikose SEHEMU YA NNE ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx
8 Comments
Kazi nzur sanah panaanza kuchangamka
Mimi mgeni jamn lakin nimeipenda san
Adimin una pepo yako pekee
Jinsi ilvyo nikiisoma navuta picha kma naitzma kwnye Tv ani
Ni dar tu ndo wanaume wanapigwa na wanawake
Daah masikin msonjo umemponza mtoto wa watu
ntbybi
kubf9f