Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Mungu Amenisahau Sehemu Ya Tatu (03)
    Hadithi

    Mungu Amenisahau Sehemu Ya Tatu (03)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaSeptember 26, 2024Updated:October 1, 20247 Comments8 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Mungu Amenisahau
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Najuwa unaumia Jojo ila utazoea tu sababu hata Mimi nilikuwaΒ  kama wewe siku ya kwanza naanza kazi, nilikuwa mnyonge,Β  sikuzoea kuvaa hivi ila ilinibidi nikubali hali halisi”Β 

    Alisema Shonaa akiwa ananiangalia vizuri kama vile alikuwaΒ  akinikagua, nilionesha lile tabasamu fekiΒ 

    “Kuna nini?” Nilimuuliza, alinishika nywele zangu akazibanaΒ  kwa kutumia mpira aliokuwa ameushika mkononiΒ 

    “Wewe ni mzuri sana Jojo” Alisema kisha aliachia tabasamuΒ  lililotoka moyoni mwake kabisa, hata mimi niliachia tabasamuΒ  lililotoka moyoniΒ 

    “Asante!” Nilimshukuru, tulikuwa wawili tu sababu wengineΒ  walienda zamu ya Jioni hiyo kurudi hadi asubuhi.

    EndeleaΒ 

    SEHEMU YA TATU

    “Vumilia Jojo utakuwa sawa tu” Alisema tena Shonaa kishaΒ  alinyanyuka akatoka ndani, alikuwa na moyo wa peke yake, kunaΒ  wakati nilijiona nipo sawa pindi ninapozungumza na Shonaa.Β 

    Nilijilaza kitandani, kutokana na ule uchovu nilijikutaΒ  nikipitiwa na Usingizi, niliamka mishale ya saa tatu usiku,Β  nilimuona Shonaa akivaa nguo, alivalia Baibui hadiΒ  nilishangaa, nilihitaji kumuuliza anaenda wapi?Β 

    “Shonaa unaenda wapi tena?” Nilimuuliza nikiwa ninatabasamu,Β  kiufupi alipendeza sanaΒ 

    “Naenda kwa Bwana wangu” Alijibu akiwa anajipodoa,Β  nilinyanyuka kwanza ili niseme kituΒ 

    “Bwana wako? Ina maana umeolewa?”Β 

    “Hapana ni Boyfriend tu, vipi mbona unanishangaa?”Β 

    “Umependeza sana unaonekana ni mwenye Heshima kubwa snaaΒ  Shonaa” Nilisema, nilimfanya achekeΒ 

    “Ndio nina heshima kwani naonekana sina heshima?” AliniulizaΒ 

    “Hapana…ninachomaanisha yale mavazi ya kazini yanakufanyaΒ  uwe tofauti sana na jinsi ulivyo sasa” NilisemaΒ 

    “Jojo Maisha haya yatakufundisha vitu vingi sana, yatumieΒ  vizuri uone kile ambacho macho yako ya kawaida hayaweziΒ  kuona”Β 

    “Una maana gani Shonaa?”Β 

    Shonaa hakunijibu chochote, alipomaliza kujiandaa aliondokaΒ  zake, nilipata muda wa kuwa peke yangu, usiku huo niliona niΒ  bora niwasiliane na Msonjo ili anipe mrejesho wa kileΒ  alichozungumza na Bosi Muntaza, nilipiga simu lakiniΒ  haikupokelewa hadi baadaye kidogo aliponipigia yeyeΒ 

    “Griii! Grii!” Ulikuwa ni mlio wa simu yangu, ilikuwa tayariΒ  nimepitiwa na Usingizi, niliamka na kuipokeaΒ 

    “Hallo Msonjo” Nilisema kwa sauti ya uchovuΒ 

    “Mambo Jojo” Alisema MsonjoΒ 

    “Mambo mabaya Msonjo vipi umeshaongea na Bosi anipe nauli?”

    “Nimeongea naye ila kasema hawezi kupoteza pesa yake kwa MtuΒ  ambaye hajafanya kazi yoyote” Alinijibu Msonjo, moyo uliniumaΒ  sanaΒ 

    “Sasa Msonjo….huwezi kuazima sehemu nikifika nitakurudishiaΒ  tafadhari”Β 

    “Mmh! Jojo nisikuongopee hapa sina wa kumuazima pesa,Β  ninachoweza kukushauri ni kwamba fanya kazi kwa muda iliΒ  uweze kuipata hiyo pesa”.Β 

    “Yaani Msonjo katika vitu nimebugi katika Maisha yangu basiΒ  ni kuja huku Dar, naona kama nipo kwenye chumba chenye gizaΒ  na joto kali, najiona mwenyewe tu na sina Mtu wa kunisaidia”Β  Nilisema, Chozi lilianza kunilenga, Msonjo aligundua kuwaΒ  nakaribia kulia kutokana na jinsi sauti yangu ilivyokuwaΒ  ikitoka.Β 

    “Jojo huna sababu ya Kulia, pambana huko Dar….pengineΒ  baadaye unaweza ukabadilisha kauli baada ya kuona mamboΒ  yanakunyookea, cha Msingi sasa hivi kaza Buti” Alisema MsonjoΒ  kwa maneno rahisi sana, niliona siwezi kuupata MsaadaΒ  niliokuwa nautaka kutoka kwake nilimuagaΒ 

    “Msonjo….nakutakia Usiku mwema” Nilisema kishaΒ  jilisikikizia jibu la Msonjo lakiji hakujibu chochote kile,Β  nilikata simu na kuanza kulia, niliona kama Msonjo alikuwaΒ  ameniuza Jiji Dar, nililitazmaa Begi langu, nilikumbuka ninaΒ  elfu kumi tu tena hata Jiji silijui kabisaa.Β 

    “Eeh Malaika wa Mama yangu naomba Mniongoze, nahisi kushindwaΒ  na kukata tamaa kabisa, Mungu unaniona?” Nilisema huku choziΒ  likinibubujika, ilikuwa mishale ya saa nne za Usiku. MlangoΒ  uligongwa tena mgongaji aliita jina la Shonaa, ilikuwa niΒ  sauti ya Mama wa Makamo aliyeonesha kuwa na jazba ya jamboΒ  fulani mana jinsi alivyoita Mmh!!Β 

    “Shonaa hayupo” Nilijibu nikiwa chumbaniΒ 

    “Njoo wewe” Alisema Mama huyo kwa shari sana, sikumjuwa naΒ  wala hakuwa akinijuwa, basi niliingiwa na woga sana nilitokaΒ  ndani.Β 

    “Shikamoo Mama” Nilimsalimu kwa adabu sanaΒ 

    “Shikamoo mwenyewe, kama unaona hiyo shikamoo Mali basi ikateΒ  iweke kwenye sufuria igeuke nyama ya Mbuzi…hivi nyieΒ  mnatuchukuliaje humu ndani?” Aliuliza kwa shari ile ile

    “Kwani kuna nini Mama yangu” Nilimuuliza maana woga ulikuwaΒ  umenishikaΒ 

    “Hebu twende” Alinishika mkono kwa nguvu akawa ananipelekaΒ  njia ya Chooni, aliniingiza hadi chooniΒ 

    “Nini kile?” Alionesha kidole kwenye karo la Choo, Aah yaaniΒ  kulikuwa na haja kubwa iliyokuwa haijamwagiwa majiΒ 

    “Hizo pombe mnazokunywa sisi tumekunywa kitambo na tukaziachaΒ  sababu hazina faida yoyote, wenyewe mnaona Ujanja si ndiyo?Β  Sasa safisha hapo haraka sana nataka kuoga” Alisema Mama huyoΒ  kwa hasira sanaΒ 

    “Lakini Mama mimi ni mgeni hapa na sijui chochote kile”Β  Nilijitetea kwa sauti ya chini sana, mkononi nilikuwaΒ  nimeshikilia simu yangu ndogo, sasa yule Mama alinisukumizaΒ  nishike Fagio, simu ikaangukia kwenye shimo la chooΒ 

    “Simu yangu” Nilisema kwa maumivu makali sana, simu ileΒ  ilikuwa ndio msaada mkubwa kwangu kuwasiliana na Msonjo naΒ  Watu wengine ambao walikuwa Tabora.Β 

    “Nyooo! Usinilegezee sauti, hebu fanya Usafi fastaa” AlisemaΒ  Mama huyo, kwa jisni alivyochukia ilinilazimu haraka sanaΒ  kushika fagio, Mama huyo alitoka nje. Macho yangu yalijaaΒ  machozi ya maumivu makali sana niliwaza ndani ya akili yanguΒ 

    “Haya ndiyo Maisha gani jamani ni Bora ningekufa njaa Tabora,Β  Mama umeniacha unaona sasa yanayonikuta Mwanao” NilijisemeaΒ  huku chozi likizidi kunibubujika, nilifanya Usafi nikiwaΒ  ninalia hadi nilipomaliza kisha nilitokaΒ 

    “Subiria hapo hapo niangalie Kama umesafisha vizuri” AlisemaΒ  Mama huyo kisha aliingia chooni kuangalia, baada ya sekundeΒ  chache alitokaΒ 

    “Bahati yako, haya sepa” Alisema, nilimuogopa mno, ilinibidiΒ  haraka nishike njia ya kurudi ndani, nyuma nilisikia sautiΒ  yake akicheka kisha alisemaΒ 

    “Mjini shule” Jamani niliumia sana, moyo ulimwaga chozi laΒ  damu lenye Maumivu, nilikuwa Msichana mpole sana ambayeΒ  sikuweza kujibizana na Mtu yeyote yule.Β 

    Nilipofika chumbani niliongeza kilio, Chozi lilinimwagikaΒ  nikiwa nimejitupa kitandani. Jiji la Dar liligeuka kuwaΒ  chungu sana kwangu, kabla hata sijatulia nilisikia tenaΒ  Mlango ukigongwa, niliogopa sana nilijifuta chozi harakaΒ  kisha niliuliza

    “Nani?” Niliuliza kwa sauti ya upole mno tena iliyojaa wogaΒ 

    “Fungua wewe” nilisikia sauti ya Mdada mmoja ambayeΒ  tulimuacha akiwa amelala asubuhi, ilikuwa ni sautiΒ  iliyoambatana na Ulevi.Β 

    Mara moja nilienda kumfungulia, ile nafungua tu nilikutana naΒ  tusi la nguoni, tena aliyetukanwa alikuwa ni Marehemu MamaΒ  yangu MasikiniΒ 

    “Malaya wewe! Unajiona mzuri ndio hufungui mlango eeeh?”Β  Alisema yule Mdada, nilichukia sana kisha nilienda chumbaniΒ  wala sikutaka kubishana naye. Alikuwa ameongozana naΒ  Mwanaume, wote walikuja chumbani.Β 

    Yaani kilichonikausha kilio changu kilikuwa ni kitendo chaoΒ  cha kuondoa nguo zao zote kisha kuanza kufanya mapenzi mbeleΒ  yangu bila hata Aibu, sikuweza kuwavumilia nilitoka chumbani,Β  kelele zao zilikuwa juu hata sebleni niliona hapakuwa salamaΒ  kwangu, nilienda nje kabisa. Ndani ya muda mfupi nilikutanaΒ  na matukio yaliyoniacha kinywa wazi, mambo ambayo nilikuwaΒ  nasimuliwa na Watu kuwa wameona katika filamu ndiyo nilikuwaΒ  nikiyashuhudia kwa macho yangu, nilitamani sana kumpigia simuΒ  Shonaa nimueleze maana angalau yeye tulikuwa tukiiva chunguΒ  kimoja lakini ndiyo hivyo tena simu ilikuwa imeingia Chooni.Β 

    Nilikaa nje kwa zaidi ya Masaa mawili nikiwa ninalia, baadayeΒ  nilirudi ndani, palikuwa pametulia, basi nilifunga mlangoΒ  kisha nilijilaza kwenye kochi nikiwa nimevalia zangu dera.Β 

    Sijui hata ilikuwa ni saa ngapi, nilishtuka tu nilihisi mkonoΒ  ukinichezea makalio yangu, nilipoamka nilimuona yule MwanaumeΒ  ambaye alikuja na yule Mdada. NilimuulizaΒ 

    “Wewe ni Nani na Unataka nini?” Niliuliza huku nikiwaΒ  nimejaza woga kwenye kifua changu, nilijisogeza nyuma kabisaΒ  ya KochiΒ 

    “Shiii” Alinipa ishara kuwa sipaswi kusema chochote kile,Β  alitoa kisu akaniambiaΒ 

    “Ukipiga kelele Nakuchoma kisu sasa hivi” Alisema akiwaΒ  ananionesha na ishara kabisa jinsi atakavyo nichoma hichoΒ  kisu.Β 

    Kwa mara ya kwanza katika Maisha yangu niliona MunguΒ  amenitazama, yule Mdada alikuwa ameamka hakumuona Mtu wakeΒ  hivyo akaja sebleni na kukuta yule jamaa akiwa amenishikiliaΒ  kisu, aliposikia sauti ya Mwanamke wake alikitupa kile kisu.Β 

    Bahati nzuri taa ilikuwa inawaka maana nilikuwa siwezi kulalaΒ  bila taa, alikiona kile kisuΒ 

    “Unaniacha chumbani unakuja kwa huyu Malaya si ndiyo?”Β  Alisema yule Mdada, nilihema juu juuΒ 

    “Unafanya nini hapa?” Alihoji yule Mdada, alimshushia kipigoΒ  yule Mwanaume hadi nilishangaa, Mwanamke anaweza vipi kumpigaΒ  Mwanaume namna ile? Hadi niliingilia kati maana alishamtoaΒ  damu kinywaniΒ 

    “Wewe malaya hayakuhusu haya, una kesi na Mimi kwahiyo subiriΒ  hivyo hivyo” Alisema yule Mdada, basi aliendelea kumpiga,Β  alipochoka alimwambiaΒ 

    “Tembea nisikuone tena hapa Shwaini Mkubwa wewe” Alisema yuleΒ  Mdada, yule Jamaa aliposikia hivyo aliona kama vile alikuwaΒ  ametembelewa na Malaika mtoa roho alafu akamuacha basiΒ  alijipigiza kwenye mlango akafungua na kukimbia zake,Β  nilijikuta nikicheka japo kwa sauti ya chini maana Yule MdadaΒ  naye alicheka kidogo kisha aliacha kucheka alafu akaniangaliaΒ  kwa jicho kaliΒ 

    “Ukijilegeza utaliwa!” Alisema yule mdada kisha aliongozaΒ  kuelekea chumbaniΒ 

    “Samahani”nilisema kwa woga, alisimamaΒ 

    “Unaitwa Nani?” Nilimuuliza, alicheka kisha alinijibu “Sarafina” Alijibu na kuingia chumbani.Β 

    Japo mambo yale yalikuwa mageni kwangu na yenye kuniumiza ilaΒ  yalinifundisha vitu vingi sana ambavyo hata kama ningesomaΒ  hadi ngazi ya digrii nisingeliweza kujifunza. UsingiziΒ  haukuja kabisaa nilikaa macho hadi niliposikia adhanaΒ  wakiazini msikiti wa jirani ndipo nilipofahamu kuwa palikuwaΒ  pamepambazuka.Β 

    Tulikuwa na zamu ya kwenda kule Dar City Mimi na Shonaa,Β  nilijiandaa. Muda ulienda nikiwa ninamsubiria Shonaa, JuaΒ  lilipoanza kutua Shonaa alirudi akiwa mwenye furaha,Β  alinionesha kiasi cha pesa alichokiingiza.Β 

    Kilikuwa ni zaidi ya laki moja, niliitamani pesa hiyo maanaΒ  kama ningeliipata basi ingenitosha kwa Nauli ya kuelekeaΒ  Tabora, aliketi lakini aliniona nikiwa sina fruaha kabisa. Nini Kitaendelea

    Usikose SEHEMU YA NNE ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx

    Mungu Amenisahau

    7 Comments

    1. Taysonny on September 26, 2024 5:25 pm

      Kazi nzur sanah panaanza kuchangamka

      Reply
      • Marry on September 28, 2024 5:27 pm

        Mimi mgeni jamn lakin nimeipenda san

        Reply
    2. Kelvin Mushi on September 26, 2024 8:49 pm

      Adimin una pepo yako pekee

      Reply
    3. Dj Shoti on September 27, 2024 1:04 am

      Jinsi ilvyo nikiisoma navuta picha kma naitzma kwnye Tv ani

      Reply
    4. G shirima on September 27, 2024 3:36 pm

      Ni dar tu ndo wanaume wanapigwa na wanawake

      Reply
    5. Joel on October 1, 2024 5:10 pm

      Daah masikin msonjo umemponza mtoto wa watu

      Reply
    6. πŸ” + 1.39158 BTC.GET - https://yandex.com/poll/DCTzwgNQnzCykVhgbhD581?hs=49f5ff0450c4a51fbb2ff91326959a58& πŸ” on June 1, 2025 9:08 pm

      ntbybi

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneΒ  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.