Ilipoishia “Sikujuwa hata mtandio wangu niliudondoshea wapi, nilikuwaย kama Chizi maana wakati nalia nilitimua sana nywele zangu.ย Nilikaa hapo kama Bubu, niliwaza sana hadi kichwa kiliachaย kufikiria tena, Sikujuwa niende wapi maana Sikuwa na namba yaย Mtu yeyote yule Kichwani, sikuwa na kumbukumbu ilipo Ileย kumbi ya Sterehe maana nilienda mara moja tu, kingine sikuwaย na kumbukumbu pale nilipokuwa naishi na Shonaa palikuwaย panaitwaje maana napo nilikaa kwa siku mbili tu, nilikuwaย Mgeni Dar, Nilimkumbuka sana Shonaa hadi Chozi likawaย linanidondoka tu. Endelea
SEHEMU YA TANO
Laiti kama Shonaa angekuwepo asingeruhusu napata tabu,ย nilijilaumu hata kwanini nilishuka kwenda kujisaidia, Maishaย yangu yaliingia kwenye Dunia nyingine ngumu zaidi tofauti naย Mwanzo, niliivua ile Rozali kisha niliitupa kwenye mtaroย mdogo ulio mbele yangu, niliona Mungu amenisahau katikaย Hesabu zake au alikuwa akinifanyia makusudiย
“Sasa kwanini ulimchukua Mama yangu, hukujuwa kamaย nitateseka? Kama Mungu una nguvu nitoe hapa nipae hadiย Tabora” Nilisema maneno ambayo hata Kichaa haweziย kuyafikiria, niligumia kwa nguvu sana hadi Watu walio karibuย walisimama kuniangalia kwa muda kisha waliondoka zao.ย
Nilikaa pale kwa zaidi ya Masaa matatu, baadaye alikujaย Mwanaume mmoja alikaa kando yangu, alikuwa bize na simu yakeย hata hakunisalimia. Nilipata akili ya kumsalimiaย
“Mambo Kaka?” Nilisalimia nikiwa namtazamaย
“Powa” Alijibu bila hata kunitazama Usoni, niliona poteleaย mbali nimuombe msaada tu hata kama anaonekana ana dharauย
“Naitwa Jojo, Kaka yangu naomba msaada nilikuwa nasafiriย naenda Tabora bahati mbaya nimeachwa na gari, sina ndugu hapaย Mjini wala sijui leo nitakula nini na nitalala wapi”ย Niliposema hivi alinitazama, nililiona jicho lake laย kunichunguzaย
“Una shida kweli wewe?” Aliniuliza kwa sauti kavu sana,ย mkononi alikuwa na tatuu, alikuwa na kifua cha kujaza alafuย alikuwa mweusi hivi, nilimjibu
“Ndio”ย
“Subiri kuna mzigo napokea” Alisema yule Mkaka, niliona kamaย ngekewa vile maana nilishakata tamaa kabisa, kusikia Mtuย atanisaidia ilikuwa faraja kubwa kwangu. Ilituchukua nusu saaย tukiwa kimya huku yeye akiendelea kuchezea simu yake.ย
Alikuja Mwanaume mwingine aliyefanana na yeye, alimpatiaย Boksi hivi dogo kisha aliondoka jamaa yule alafu yule Mkakaย akaniambiaย
“Twende” alisema kikauzu sana, unafikiria nilitilia shakaย msaada wake? Wala sikuwa na mashaka hata kidogo, nilimfuataย kwa nyuma. Kumbe alikuja na Pikipiki yake aliiacha nje,ย alinipa lile boksi dogo kisha aliniambia nipande kwa nyuma.ย Nilipanda kisha safari ya kuelekea nisipopajua ilianza,ย angalau chozi lilikuwa limekauka, niliona mwangaza mpyaย katika Maisha yangu.ย
Ilikuwa ni safari ndefu kutoka Ubungo, nilisoma vibao vyaย Njiani ili kujuwa tupo wapi, niliona tupo mwenge kishaย baadaye niliona Mbezi Africana, hapo ndipo safari yetuย ilipoishia kwenye nyumba moja hivi ambayo ilikuwa kimya sana.ย Aliniambia nimpe Boksi lake baada tu ya kushuka, kishaย aliekelea kufungua geti, tuliingia humo. Ilionekana ni nyumbaย ambayo haikuwa na Mtu kabisa maana alifungua milango yoteย hadi tulipofika sebleni kisha alisemaย
“Karibu” Alisema alafu alijitupa kwenye kochi, akawaย analifungua Boksi lile alilopewa na yule jamaa kule Ubungo.ย
Alitoa vitu kama Unga fulani hivi ila hata sikutaka sanaย kujiuliza maswali mengi, akaingia chumba kimoja alafu akatokaย akiwa ameshikilia kisu, nilihofia sana maana nilikumbuka lileย tukio la Kutaka kubakwa kule kwa Shonaa. Yule Mkaka alikujaย karibu yangu akavuta kiti kisha akakaa mbele yangu, hofuย ilianza kunijaaย
“Umesema unaitwa Nani?” Aliniulizaย
“Naitwa Jojo” nilijibu kwa woga sanaย
“Jojo…sasa Jojo, mimi najuwa kama wewe ni Askari na kwaniniย uko hapa, umetumwa kunipeleleza si ndiyo?” Aliniuliza yuleย Mkaka ambaye hata Jina lake sikulifahamu, stori ya Maishaย yangu ilianza kunichanganya maana kila nilipoenda nilikutanaย na kikwazo kikubwa zaidi.
“”Mimi siyo Polisi Kaka yangu, Nahitaji msaada wa Mimi kurudiย Tabora kama hauwezi kunisaidia basi niruhusu niondoke”ย Niliona ni bora hata kuondoka kuliko kuendelea kuwa paleย
“Wengi waliotumwa kwangu walipotea kama ambavyo wewe unaendaย kupotea,”.ย
“Unamaanisha nini?” Niliuliza kwa hofu kubwa sana, nilionaย sasa Maisha yangu yanaenda kufika kikomoย
“Mimi ndiye Juma Baro, najua nini nafanya” alinivamia,ย nilijitahidi kupiga kelele kuomba msaada, alinikamata vizuriย kisha aliniweka unga kwenye pua yangu, sikuchukua raundi,ย nilihisi mwili hauna nguvu kisha niliona giza zito, sikujuwaย kilichoendelea.ย
Niliporudisha fahamu zangu nilijikuta kwenye chumba chenyeย giza, ghafla taa iliwashwa, Yule Mkaka aliyejitaja kuwa niย Juma Baro alisimama kando yangu. Nilikuwa nimechoka sana,ย nilikuwa nahema juu juu, alinimwagia maji ya Baridi, angalauย alifanya mwili wangu uanze kuwa sawa.ย
“Kaka yangu naomba uniruhusu niomdoke Mimi siyo Polisi”ย Nilisema.ย
“Najuwa wewe siyo polisi, dakika chache nimelitambua hilo,ย lakini bahati mbaya ni kuwa umejuwa baadhi ya vitu na wapiย yalipo makazi yangu, sitokuruhusu kwenda popote badala yakeย utaishi hapa” Alisema, nilishtuka nikamwambiaย
“Sijui chochote kuhusu wewe Kaka yangu, naomba tafadhali sanaย uniache niende nikatafute msaada sehemu nyingine, nakuombaย Kaka yangu nipo chini ya Miguu yako” Nilisema, alikuwaย amenifunga kamba mikononi na miguuni.ย
“Hutoweza kutoka hapa tena utaishi hapa kama Mke wangu”ย Alisema Juma Baroย
“Tafadhali Sana Kaka yangu nakuomba usifanye hivyo, nina apaย kwa Mungu wangu kuwa sijui chochote, ninachotaka ni kurudiย Tabora tu”ย
“Mungu? Kumbe Mungu wako yupo? Yupo wapi sasa? Basi huyoย Mungu amekusahau, angekuwa anakukumbuka angekutoa hapa kwenyeย hiki chumba” Alisema Juma Baro kisha aliondoka na kufungaย mlango kwa nje, kamba zilikuwa zimeniumiza mno mikononi,ย kauli moja ya Juma Baro ilijirudia katika akili yangu kuwaย “MUNGU AMENISAHAU” Ndiyo niliitafakari sana, niliona inaย ukweli ndani yake sababu kama angekuwa ananikumbuka basiย angenitoa kwenye matatizo na kuniweka salama, kwaniniย anazamisha Maisha yangu kila wakati.ย
Niliishi pale kwa Juma Baro kama Mfungwa ndani ya Chumbaย chenye giza, nilililaani Jiji la Dar-es-salaam, nilimlaaniย Msonjo kwa kunileta katika Jiji hili lenye kila aina yaย ukatili. Alikuwa akija kuniletea chakula, alikuwa akija kwaย siku mara mbili, sikujuwa ilikuwa ni siku gani, sikujuwaย ulikuwa ni wakati gani, chumba hicho kilitengenezwa mfano waย chumba cha Kulala maabusu, hakikuwa na Choo, dirisha lakeย lilikuwa juu sana hata sikuweza kuangalia nje.ย
Nilikuwa najisaidia kwenye ndoo kisha anakuja kuchukua,ย anaenda kumwaga, sikujuwa nilikuwa kwenye ile nyumba yaย mwanzo au alinipeleka kwenye nyumba nyingine, Basi niliishiย Maisha hayo.ย
Usiku mmoja alikuja, alinifungua kamba mikononi kishaย alinitoa humo akiwa amenifunga kitambaa usoni, alinipelekaย kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa kizuri sana, kilikuwaย na kila kitu akaniambiaย
“Kuanzia leo utakuwa unaishi hapa”ย
“Kwanini unanifanyia hivi Kaka yangu, unajuwa ni kiasi ganiย nateseka Mimi?” Nilisema kwa maumivu makali sana ndani yaย moyo wangu.ย
“Unayajua mateso wewe? Katika watu nimeishi nao vizuri weweย namba moja, unajuwa kwanini?” Aliniuliza akiwa amenisogelea,ย nilitikisa kichwa changu ishara kuwa sijuiย
“Kwasababu wewe ni Mzuri sana Jojo, ni hasara kubwa kuishi naย wewe katika mateso makubwa ndiyo maana nimekuleta hapa”ย alisema, kusema ule ukweli woga uliniisha kabisa sababuย sikuwa na uwezo wa kufanya chochote kile. Alianza kunishikaย shika kitu ambacho kilinifanya nichukie, nilimpiga kofiย
“Ukiendelea kunishika nitakufanya kitu kibaya” Nilisema, Jumaย Baro alipandwa na hasira akanitandika kofi na Mimi kishaย alinitupa kitandani, alitumia nguvu zote aliniondoa nguoย zangu na kunibaka.ย
Ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kuingiliwa na mwanaume,ย tena kwa kubakwa, nilipata uchungu na maumivu makali sanaย katika sehemu zangu za siri, roho iliniuma sana. Damuย zilinitoka lakini hata hakujali aliondoka zake na kufunga mlango, katika mateso ambayo yaliniumiza moyo na akili yanguย ni pamoja na kubakwa, nilijiona nimeondolewa thamani yangu,ย nilijiona nimepoteza kila kitu katika Maisha yanguย
Nililia sana, mwili ulishika moto vibaya mno. Baadaye alikujaย akanipa dawa za kutuliza maumivu kisha aliondoka zakeย
Hayo yalikuwa ndiyo Maisha yangu nyumbani kwa Juma Baro,ย niligeuzwa kuwa Mtumwa wake wa ngono, alinifanya apendavyoย tena bila kujali kuwa nilikuwa ninaumia sana kuingiliwa bilaย ridhaa yangu. Nilipiga sana kelele lakini sikuuona msaadaย wowote ukija mle ndani, nilienda mwisho nilikata tamaa yaย kutoka kabisa.ย
Niliishi hapo kwa miezi miwili nikiwa sijui siku wala muda,ย niliona jua likizama na kuchomoza. Madirisha yalikuwaย yamewekwa nondo ngumu na kioo hivyo hata ningefanyajeย nisingeliweza kufungua na kutoka, niliishia kufungua dirishaย na kuangalia mwanga wa jua tuu.ย
Juma alipojisikia kufanya mapenzi alikuja na kunitumia vileย apendavyo yeye hadi pale anapokuwa ameridhika ndiyoย anaondoka, nilizoea maisha hayo hata nikawa silii hovyo tenaย sababu tumaini la kuondoka hapo halikuwepo kabisa, sikumtajaย tena Mungu katika Maisha yangu sababu niliona hanisikii tena.ย
Kufanywa bila kinga kulisababisha nipate mimba, nilimuelezaย Juma Baro kuwa Mimi ni Mjamzito, alichukia sana akawaย ananiambia kuwa nimefanya makusudi wakati anajuwa fikaย alikuwa akinifanya Bila kinga. Roho iliniuma sana akaniambiaย atanipa vidonge nitoe ujauzito, sikuwa na pingamizi istosheย sikupenda kuzaa na Mtu katili kama Juma Baro, Basi jioniย aliniletea vidonge nikameza, cha ajabu mimba haikutoka kabisaย wala sikuhisi maumivu yoyote yale wakati nilikuwa nikisikiaย kuwa Mtu anapotoa Mimba anapata maumivu ya Tumbo ila kwanguย haikuwa hivyo kabisa, nilirudia kumeza kwa hasira yaniย sikutaka kuwa na kiumbe cha Juma Baro.ย
Asubuhi nilipoamka niliona damu kidogo sehemu nyeti ilaย ilitoka bila maumivu yoyote. Juma alipokuja aliniulizaย
“Hivi umemeza vidonge wewe?” Aliniuliza kwa dharau sana kamaย vile mimi nilikuwa nataka kuzaa na yeyeย
“Ndiyo” nilimjibu kwa kifupi sanaย
“Yaani umeze vidonge na uwe sawa hivyo, unanitania si ndiyo?”ย Aliuliza Juma Baro, nilinyanyuka nikamsogelea bila woga
“Unafikiri nataka kuzaa na Mwanaume katili kama wewe? Ungejuaย jinsi ninavyo kuchukia hata usingenisemesha, natamani hiiย Mimba itoke kimiujiza” Nilisema kwa hasira mbele yakeย
“Ok! Ngoja” Alisema Juma kisha alisogea mezani akachukuaย vidonge kama vitano kisha akaniambiaย
“Meza hivi vidonge mbele yangu vinginevyo nitaitoa hiyo mimbaย kwa mikono yangu” Alisema kwa jazba, nilivichukua vidonge kwaย hasira sana kisha nikachukua maji na kuvimeza vyoteย
“Ungejua natamani kufa kuliko kuendelea kuwa hapa, kama kunaย sumu nipe ninywe nife, bora kufa kuliko kuishi maishaย yaliyojaa mateso kama haya” Nilisema, Juma alinisogelea kishaย akaniulizaย
“Unataka kufa?”ย
“Ndiyo! Kama siyo kunifunga mikono na miguu ningekuwaย nimeshaondoa Maisha yangu” Nilisema huku chozi likinimwagikaย
“Nakurahisishia kazi” Alisema Juma, aliacha mlango wazi kishaย alitoka, niliketi kitandani, alirudi na Madawa ya kulevyaย
“Tumia haya, dakika chache utakuwa umefika kwa Mungu wako”ย Alinipatia kifuko kidogo sana kilichofungwa Unga huo,ย kiukweli nilisema tu yale maneno ila kufa sikufikiria kabisaย niliamini ipo siku nitatoka pale, hivyo nilibakia nikiwaย nimesimama tu na kumtazama Mwanaume huyo kwa jinsi alivyoamuaย kuwa katili wa Maisha yangu.ย
“Unasubiria nini?” Vuta huo Unga, natumaini nitakaporudiย nitakuja kutoa maiti yako na kwenda kuitupa” Alisema Jumaย kisha aliondoka zake na kunifungia mlango.ย
Nilichoka sana nilijitupa kitandani, sikuwa na ujanja walaย sikujua nafanya nini, nilisikia mlio wa gari yake kisha getiย kufunguliwa akawa ameondoka zake, ilikuwa ni ngumu sana Mimiย kujuwa nipo wapi sababu dirishani niliona ukuta mrefu,ย sikuona nje. Hata hivyo nilijiuliza kwa kelele nilizokuwaย napiga kama nyumba ile ingekuwa kwenye makazi ya Watu basiย wangenisikia na kunisaidia haraka sana.ย
Ilikuwa ni wakati wa jua kuwaka, baadaye lilizima na gizaย liliingia, mlio wa gari niliusikia kisha geti lilifunguliwa,ย baadaye mlango wa chumba nilichopo ulifunguliwa, alikuwa niย Juma Baro, aliponiona alinicheka, nilimtazama kwa hasira sana
“Nilijuwa utakuwa umeshakufa Jojo, nilijiandaa kukuchimbiaย kaburi hapahapa nyumbani kwangu nikuzike, inaelekea una damuย kali sana hadi dawa hazikufanya kazi si ndiyo?” Aliulizaย nikiwa nimejilaza tu nikiwa namtazama, aliuchukua ule ungaย wake kisha akaniambiaย
“Ngoja nikuoneshe kitu” Alinifuata akanifunga miguu na mikonoย yangu, yalikuwa ni maisha niliyoyazoea wala sikuwa mkorofiย hadi alipomaliza, nikawa siwezi kufanya chochote. Alitoboaย kifuko kisha akatoa unga kwa kutumia kidole chakeย
“Usihangaike sawa?” Alisema, sikujuwa alikuwa anatakaย kunifanyia nini, nilishtuka aliponikamata kichwa naย kunipakaza ule unga eneo la pua, nilihisi maluwe luwe ambayoย sikuwahi kuyahisi kabla, Niliona nyumba inageuka alafu mwiliย ukawa unawasha sanaย
“Unanifanyia nini Mshenzi wewe” Nilisema kwa sauti kavuย iliyotoka kwa nguvu sana nikaambatanisha na keleleย
“Shiii!” Alinitaka kunyamaza kisha aliniweka tena, basiย nililegea mno nikajikuta napoteza uwezo wa kufikiria.ย
Alinifanyia huo mchezo kwa siku saba mfululizo hadi nilijionaย mdhahifu sana, kisha aliniacha. Cha ajabu ambachoย kilinishangaza nilijiona nakuwa na hamu ya kupakwa yaleย madawa, nilikuwa nahisi mwili una baridi mno, nikawaย natetemeka mwili mzima na vipere vya msisimko vilikuwaย vikinitoka, kwa mara ya kwanza nilipata maumivu makali yaย tumbo kisha niliona mabonge ya Damu yakinitoka huku chini,ย nilijisafisha ila mwili haukuwa na nguvu hata kidogo,ย nilijuwa tu yale maumivvu yalitokana na mimba kuharibika.ย
Aliponiletea chakula nilimwambia Juma Baro kuwa mwili wanguย ni dhahifu sana, alicheka tu kisha aliondoka zake, nahisiย alikuwa anajuwa alichokiwa akikifanya kwangu. Hali ileย iliendelea kwa wiki mbili mfululizo, siku moja alikujaย akanipa kifuko cha Madawa ya kulevya akaniambiaย
“Tumia utakuwa sawa” Kutokana na jinsi nilivyokuwa natetemekaย na kuhangaika ilinibidi nikubali kutumia madawa ya kulevya,ย basi nikawa naweka puani ndiyo najisikia unafuu na uchangamfuย wa hali ya juu sana. Nikawa na nguvu ila nikawa sipendi kulaย chakula zaidi ya kupenda sana kuvuta yale madawa ambayoย alikuwa akiniletea kwa kunikadilia sana, siku nyingineย alikuwa haniletei hivyo nilishi kwa kuhangaika sana paleย chumbani na kuishiwa nguvu, nilikuwa napiga mlango kwa nguvuย ili aniletee madawa, nilijiona nimekuwa Mwanamke wa hovyoย sana.
โขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโข
Alitumia mwanya huo kunitumia kingono kisha ananiahidi kunipaย madawa ya kulevya, basi nilimpa penzi la kweli kabisa Jumaย Baro kisha ananipa madawa ya kulevya na pombe, alipoonaย nimekuwa Mtumwa akaniambia naweza kutoka na kwenda sebleniย kukaa, basi nikawa natoka chumbani naenda sebleni nakaa hapoย kwa muda fulani kisha narudi chumbani kwangu. Nilianza kuwaย mlevi wa pombe na madawa ya kulevya, siku nyingine Jumaย alikuja chumbani kwangu na kuvuta pamoja na Mimi, tukawaย marafiki mnoย
Nilijiona nimekuwa wa hovyo kuanzia mwili na akili yangu,ย nikawa nawaza pombe, madawa ya kulevya na kufanya mapenzi tu.ย Alikuwa akileta zile pombe kali sana!ย
Nakumbuka siku moja ilikuwa Usiku, Juma alikuwa Chumbaniย kwake na Mimi nilikuwa chumbani kwangu, alikuja harakaย chumbani kwangu akaniambia kuwa polisi wanakuja, nilishajengaย uadui na hao polisi kutokana na vitu nilivyokuwa natumia,ย nilimuulizaย
“Tufanye nini sasa?”ย
“Tuondoke hapa haraka” Alisema Juma Baro, mara moja alirudiย chumbani kwake na kuchukua Bastola yake, aliniambia nichukueย vitu muhimu. Tukaelekea getini, ikawa ndiyo mara yangu yaย kwanza kupunga upepo wa nje kwa zaidi ya mieizi mitano nikiwaย nafungiwa ndani tu, ile anafungua geti na kutoka alipigwaย risasi ya tumbo. Nilitupa vitu nilivyobeba kisha nikakimbiliaย nyuma ya nyumba, huko nikapanda juu ya Ukuta huku majibizanoย ya Risasi kati ya Juma Baro na polisi yakiwa yanaendelea,ย nilichumpa hadi nje, niliangukia kwenye kifusi cha mchangaย ambacho kilinisomba kwa safari hadi chini ambako kulikuwa naย kama machimbo ya Mchanga hivi, eneo hilo lilikuwa kimya mnoย alafu kulikuwa na pori, hakukuwa na nyumba yoyote eneo hilo,ย taa zilikuwa zikiwaka kwa mbali sana.ย
Niligeuka nilipotoka, nikaanza safari ya kukimbia kutoka paleย na kuzifuata taa ambazo zilionesha kuwa ni makazi ya Watu,ย ujasiri ulinikamata kwa kiasi kikubwa ila tochi za polisiย zilinifuata porini, kelele za mbwa zilisikika huku ile milioย ya risasi ikiwa imekata kabisa nikajuwa tu lazima Juma Baroย atakuwa ameuwawa.ย
Nilikimbia kwa umbali mrefu bila kupumzika ila baadayeย nilihisi nguvu zikiniisha, tochi za polisi sikuziona tena,ย nilijitahidi kuendelea kukimbia ila baadaye nilianguka naย kujigonga kwenye mti. Nilipoteza fahamu zangu sikujuwaย kilichoendelea.
Fahamu ziliponirudia nilijikuta nikiwa kitandani, pembezoniย mwangu alikuwepo Baba mmoja na Mama mmoja ambao walikuwaย wakiniangalia sana. Sikujuwa hapo ni wapi na wale Watu niย akina Nani, nilijaribu kujiinua ila maumivu ya kichwaย yalinizuiaย
“Polepole Binti utakuwa sawa tu” Alisema Huyo Babaย
“Nipo wapi na nyie ni akina Nani?” Niliuliza huku nikiwaย ninawatazamaย
“Upo sehemu salama sana, Naitwa Baba Nesha na Huyu ni Mamaย Nesha” Alisema Baba huyo kisha Huyo aliyemtambulisha kamaย Mama Nesha alisemaย
“Jinsi ulivyokuwa katika hali mbaya sikutegemea kama ungeamkaย na kujitambua, ulikuwa umepoteza fahamu kwa siku mbili”ย Alisema, nilishtuka sanaย
“Siku mbili?” Niliuliza kama vile sikusikia sawa sawaย alichokisemaย
“Ndiyo, siku mbili”ย
“Jumaa….” nilitaka kuuliza kuhusu Juma Baro ilaย nilipokumbuka kuwa Mwanaume yule alikuwa Muuza Unga nikaachaย
“Leo ni Juma tatu Binti” alijibu Baba Nesha akihisi labdaย nilitaka kuuliza ni Siku ganiย
“Hapa ni Rufiji”ย
“Rufiji?”ย
“Ndiyo kwanini umeshangaa? Tulikukuta Shambani kwetu ndiyoย tukakuleta hapa Binti” Alisema Baba Nesha, nyumba yao ilikuwaย nzuri sana na ilionesha walikuwa ni Watu wenye uwezo mkubwaย kifedha.ย
“Unaitwa Nani Binti na nini kilikusibu?” Aliuliza Baba Neshaย akionesha kuwa na hamu kubwa ya kutaka kujuwa, niliwaangaliaย ikanijia akili ya ghafla kuwa nisijimalize sana maanaย wanaweza kunichoma kwa polisiย
“Naitwa Jojo” nilijibuย
“Nini kimekusibu?” Aliuliza yule Mamaย
“Sikumbuki chochote” Nilisema kisha walitazamana
“Pole sana basi taratibu utakuwa unarejesha kumbukumbu”ย Nilikuwa na kovu upande wa kulia lililotokana na vurugu zaย kule nyumbani kwa Juma Baro kipindi cha nyuma nililishika,ย nililetewa Chakula lakini nilipokula nilitapika kutokana naย ile hali ya kutumia madawa ya kulevya kwa wingi.ย
Walihisi labda ninaumwa, wakanitengenezea vyakula vilainiย sana ambavyo angalau nilikula kidogo, niliishi hapo kwa Babaย Nesha na Mke wake, walinichukulia kama Binti yao. Baba Neshaย alikuwa ni Mtu wa kusafiri safiri kwasbabu alikuwa ni derevaย wa Mabasiย
Ile hali ya kuhitaji Madawa ya kulevya ilianza kunitesa,ย bahati nzuri wenyeji walikuwa wanywaji wa pombe hivyo angalauย nilijituliza kwa kunywa pombe kali, lakini japo nilitumiaย pombe ila nilihisi mwili unakosa nguvu, nashikwa na baridiย mara kwa mara.ย
“Unaumwa Jojo?” Aliniuliza Mama Nesha siku moja tukiwa jikoni “Hapana Mama nipo sawa” nilimjibuย
“Nakuona ukiwa hauna amani, unatetemeka utasemaje upo sawaย Jojo? Kama unajisikia homa basi nikupeleke Hospitali maanaย usije zidiwa usiku na Baba Nesha hayupo ikawa shida” Alisemaย Mama Nesha akiwa anaendelea kupika, mimi nilikuwa nimekaa tuย
“Hapana Mama usijali nipo sawa tu” nilimwambiaย
“Haya! Ila Jojo tunakutendea vizuri hapa nyumbani?”ย
“Ndio Mama, siku 17 nilizokaa hapa naona nipo nyumbani,ย nashukuru sana nina amani ya Moyo wangu” Nilimwambia hukuย vipele vikianza kunitoka yaani vile vya msisimko wa kuhitajiย madawa na hivyo ndivyo nilivyokuwa nikijisikia.ย
“Haya Nenda kapumzike” Alisema Mama Nesha ila kwa jinsiย nilivyokuwa najisikia niliona bila kupata Madawa ya kulevyaย ningekuwa katika hali mbaya zaidi baada ya masaa kadhaaย mbele.ย
“Mama naenda Dukani kununua Juisi” Nilisemaย
“Haya Jojo” Alijibu Mama Nesha, ila akili yangu ilijuwaย nataka kufanya nini, kuna hela ambayo aliniachia Baba Neshaย kama Elfu 40 niliona ni bora niutumie muda huo kutafutaย Madawa ya kulevya. Nilikumbuka kuna sehemu Niliambiwaย nisipite na Mama Nesha kwasababu Watu wa hapo ni wahuniย wavuta Bangi hivyo nilijuwa tu nikienda huko nitapata madawaย kirahisi mno, kingine nilishazijuwa mbinu na mameno yaย kuzungumza ambayo Wahuni wangemielewa kwa haraka sana.ย
Haraka nikiwa nimevalia pensi na tisheti nilielekea huko,ย kweli niliona Kijiwe cha Watu watatu hivi ambao baada yaย kuniona Mimi walikaa tayari, nilitoa ishara ya vidole ambayoย Juma Baro aliniambia, ilikuwa ni ishara ya kuwaambia kuwaย kuna amani, ishara hiyo ilikuwa ikitumiwa na Wauza ungaย pekee, walipoona Ishara hiyo walikaa kisha nilisogea hadiย hapo, nilinunua kete mbili za madawa kwa shilingi elfu 20ย kisha nilirudi kwa Mama Nesha nikiwa na shahuku ya kutulizaย kiu yangu.ย
“Jojo?” Alisema Mama Nesha baada ya kusikia mlangoย ukifunguliwaย
“‘Ni Mimi Mama, nimerudi” Nilisema mkononi nikiwa na Juisiย ili kusiwe na maswaliย ย
Nini Kitaendelea?
Usikose SEHEMU YA SITA ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx


6 Comments
Unatusahau sana kama mungu wa Jojo mzee๐๐๐,,,tuletee kula siku hii kitu bhna๐คฃ
Kaaaaah
Hauna baya mtunzi
Kila siku boss
Woowh hadithi nzuri sana
zl3ius