Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Mungu Amenisahau Sehemu Ya Kumi (10)
    Hadithi

    Mungu Amenisahau Sehemu Ya Kumi (10)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 8, 2024Updated:October 9, 202414 Comments21 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Mungu Amenisahau
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Tulirudi kule kwenye ghorofa la Tancot House ambapo ndiyoΒ  tulilala usiku uliopita, Nilijaribu nguo zote ikapatikanaΒ  moja tu ambayo ilionekana kuwa nzuri sana na yenyeΒ  kunipendeza zaidiΒ 

    “Wow!! Hii ndiyo yenyewe Jojo, nina uhakika hawezi kuchomoka,Β  sasa unapaswa kuwa makini sana sababu ni lazima akuchukueΒ  kama kimada wa kulala naye Usiku, ndipo utakapo iba hayoΒ  madini, utachunguza kujuwa yalipo, baada ya kufanikishaΒ  zoezi, utafungua dirisha sababu chumba chake kipo masharikiΒ  mwa jengo hilo, utayatupa madini kwa kutumia kifaa ambachoΒ  kitakuwa kimehifadhi kisha utayachukua baada ya kushuka, kuwaΒ  makini sana vinginevyo unaweza ishia huko Hotelini, pia niΒ  lazima ukamilishe zoezi ili uwe huru” alinieleza Sarafina. Endelea

    SEHEMU YA KUMI

    “Sawa” niliitikia ili kuondoa ngoma juani sababu nilishajuaΒ  utakuwa ni mtihani mzito sana kufanya hivyo.Β 

    Basi tulienda kula na tuliporudi tulilala, asubuhi alinipaΒ  kadi maalum ya kuingilia Hotelini kwa ajili ya Hafla hiyo.Β 

    “Kila la kheri Jojo” Alisema Sarafina, sikuwa na maneno mengiΒ  ya kuzungumza sababu nilishapewa maelekezo yote naΒ  nikayaelewaΒ 

    “Upande ambao utayatupa madini kuna bustani ya mauwa hivyoΒ  kuwa makini sana uyatupe mahali ambapo utaweza kuyaokotaΒ  kirahisi, utayatupa sababu hutoweza kupita nayo mlangoniΒ  walinzi wake watakukagua”Β 

    “Ok sawa!”Β 

    Japo niliikubali kazi ile ili niwe huru ila nilikuona chaΒ  mtema kuni maana jukumu lilikuwa zito sana, niliendeleaΒ  kupiganisha akili yangu, nilifikiria jambo kwa pale kwenyeΒ  hoteli kuna kamera hivyo itakuwa rahisi mimi kuonekana,Β  niliwaza nifanye nini maana kama nitaonekama nitatafutwa naΒ  kukamatwa kwa kosa ambalo litawafaidisha wengine, wakatiΒ naendelea kutafakari niliona picha ya paspot pembeni, ilikuwaΒ  ni picha ya Sarafina. Niliivuta kwa mguu bila SarafinaΒ  kushtuka kisha niliiweka kwenye mkoba wangu huku nikijuwaΒ  ndani ya akili yangu nitafanya nini ili kuwa salama.Β 

    Jioni mishale ya saa 12 Jioni, Sarafina alinieleza kuwa ndiyoΒ  muda wa kuelekea Hotelini kwa ajili ya kuiba hayo madini,Β  nilijiangalia kwenye kioo nilijikuta nikitabasamu licha yaΒ  hatari iliyo mbele yangu, uzuri wangu, nilifanana sana naΒ  Marehemu Mama yangu.Β 

    Tulitoka, nje alinipakiza kwenye gari moja ya kifahari sanaΒ  nyeusi.Β 

    “Mimi siwezi kwenda huko sababu kadi ni moja tu ambayoΒ  nimekupa wewe, ifanye kazi uwe huru Jojo, ukitugeuka basiΒ  juwa msala huu utakuwa wako peke yako” alinisistiza SarafinaΒ 

    “Nimekuelewa Sarafina” Basi, nilifunga mlango kisha safariΒ  fupi sana ya kuelekea Hotelini ilianza, ilituchukua dakikaΒ  nne kufika Hotelini, nilishuka kwenye gari baada yaΒ  kukaguliwa kama Mwana Malikia vile kumbe nilikuwa mwizi tu.Β 

    Mlango Mkuu wa Kuingilia nilitakiwa kuonesha ile kadi,Β  nilifanya hivyo kisha niliruhusiwa kuelekea ndani ambakoΒ  kulikuwa na hiyo Afla iliyo hudhuriwa na viongozi kadhaa naΒ  wafanya biashara wakubwa wa Tanzania. Sikuwahi kuingia sehemuΒ  nzuri na ya kifahari kama ile katika Maisha yangu, ilinifanyaΒ  niwe muoga kiasi chake japo hakuna aliyeshtuka.Β 

    Hadhi niliyovishwa ilikuwa kubwa sana, mavazi niliyovaaΒ  yaliakisi ukubwa wangu na hadhi yangu, nilionekana ni mwenyeΒ  Maisha mazuri, mzuri na mrembo kuliko Wanawake woteΒ  waliohudhuria kwenye Afla hiyo.Β 

    Niliketi kwenye meza ambayo haikuwa na Mtu yeyote yule hukuΒ  Watu wakiwa bize na mazungumzo ya Hapa na pale, nilimuonaΒ  huyo Bilionea wa Madini akiwa ameketi anazungumza. MahaliΒ  nilipochagua kuketi palikuwa na urahisi wa yeye kuniona pindiΒ  atakapogeuza shingo yake, Wanaume wengi walikuwa bizeΒ  kunitazama nami nikajifanya bize na Afla hiyo ambayo ilikuwaΒ  ikiendelea.Β 

    Walikuja Wanaume kadhaa kuniuliza maswali fulani ambayoΒ  nilijuwa lengo lilikuwa ni kunihitaji kimapenzi ilaΒ  niliwakatalia hata kuketi karibu na Mimi sababu kufanya hivyoΒ  kungemfanya Bilionea pindi atakaponiona asiwe na wazo laΒ  kunihitaji.

    Bilionea huyo alikuwa Kijana mtanashati, kichwa changuΒ  kilikuwa na maelekezo yote kutoka kwa Sarafina na Mkuu waΒ  Magereza juu ya kuiba hayo Madini yenye thamani kubwa sanaΒ  japo nilijuwa haitokuwa rahisi kufanya hivyo, nililetewaΒ  Vinywaji na chakula nikawa ninakula ila akili na macho yanguΒ  yakiwa kwa huyo Bilionea Kijana.Β 

    Nililetewa vimemo kadhaa vya Wanaume vyenye namba, nilivisomaΒ  na kuvitupa sababu hakuna hata kimoja kilichotoka kwa MlengwaΒ  wangu, niliendelea kusubiria kwa masaa kadhaa huku akionekanaΒ  bize sana kucheka, Moyo wangu ulihitaji uhuru hivyo nilionaΒ Β 

    kazi hiyo ingenifanya niwe huru na kurudi Tabora.Β 

    Nilizuga kufanya vitu kadhaa ikiwemo kwenda chooni ilimradiΒ  anione lakini haikuwezekana hadi pale dakika za mwisho ambapoΒ  aligeuka akaniona kidogo alafu akarudisha macho kwa aliyekuwaΒ  akiongea naye, nilihisi labda hakuuona uzuri wangu, nilianzaΒ  kukata tamaa kumbe alikuwa ameniona ila alikuwa akitafutaΒ  engo nzuri ya kunitazama, nikiwa nimeshakata tamaa natakaΒ  kunyanyuka. Niliona nimtazame kwa mara ya mwisho hukuΒ  nikijiambiaΒ 

    “Geuka unitazame basi” Nilisema kwa hisia na kwa kumaanishaΒ  kabisa, ile namtazama nilikutana naye ana kwa ana tenaΒ  akionekana alikuwa akinitazama kwa muda mrefu, basiΒ  nilijitingisha kidogo alafu nikatazama chakula changu, nikawaΒ  na uhakika kuwa ameniona na alikuwa akiniangalia kwaΒ  kunitamani.Β 

    Basi, Dakika chache alikuja mlinzi wake akaniambiaΒ 

    “Bosi anahitaji kuzungumza na wewe” Alisema, ili nisionekaneΒ  mrahisi nilimwambiaΒ 

    “Mwambie akome sikuja hapa kwa ajili ya Mtu yeyote yule”Β  Nilisema, yule Mlinzi aliganda kidogo kisha akasemaΒ 

    “Dada usipoteze bahati yako, Bosi wangu ni Bilionea Mkubwa waΒ  Madini, amekuwa akikuangalia kwa muda mrefu sana” AlisemaΒ  tena, sasa niliona nikubali maana kujizugisha wakatiΒ  kilichonileta kilikuwa ni hicho niliona ni UjingaΒ 

    “Yupo wapi?” niliuliza kanakwamba nilikuwa simjuiΒ 

    “Yule Pale kwenye ile Meza” Alisema kisha nilipeleka machoΒ  huko, niligongana naye macho akiwa ananikodolea sana, moyoniΒ  nikasemaΒ 

    “Umenasa Bosi”

    Basi, nilinyanyuka taratibu nikaelekea kwenye hiyo Meza,Β  alitoa walinzi wake akaniambiaΒ 

    “Kuwa huru, karibu Naitwa Bilionea Vitalis Kyando” AlisemaΒ  kisha alinipatia Mkono wake, nilimpa wangu tukashikanaΒ 

    “Naitwa….Juliana” Nilifikiria kusema jina langu halisiaΒ  nikaona inaweza niletea shida baadaye, niliamuwa kumdanganya.Β 

    “Ooh Juliana! Nimefurahi kukufahamu, hakika Mungu alikuumbaΒ  kwa utulivu sana, muda mrefu nimekuwa nikikutazama alafuΒ  akili yangu ilikosa utulivu, unastahili kila kilicho boraΒ  Juliana, Niambie unataka nini” Aliniuliza Swali kwa ujasiriΒ  Mkubwa sana, niliwaza vingi kwa haraka sana, nikakumbukaΒ  kauli ya Msonjo kuwa Mimi ni mzuri sana ninapaswa kuishi Dar,Β  Nilifikiria nifanyaje na nipo kwenye mpango wa kumuibia iliΒ  niwe huruΒ 

    “Asante! kukufahamu pekee ni kitu kinachonitosha” NilisemaΒ  japo nafsi ilikuwa ikinisuta na kuniita Zuzu wa MwishoΒ 

    “Juliana Usiogope kama unahitaji Biashara, Nyumba, gari zuriΒ  la kutembelea niambie tu kuwa huru labda hujajuwa unaongea naΒ  Mtu gani….Hebu nifuate” Alisema huyo Bilionea, alinyanyukaΒ  kisha nami nilinyanyuka nikajiuliza alikuwa anatakaΒ  kunionesha kitu gani, Basi nilimfuata huku walinzi wakeΒ  wakija kwa nyuma.Β 

    Tulipanda Lifti hadi ghorofa ya nne ambapo ndipo alipokuwaΒ  amechukua chumba.Β 

    “Kama walinzi wangu wanakufanya usiwe huru Juliana niambieΒ  sawa?” Alisema Bilionea Vitalis Kyando, niliitikia kwa isharaΒ  ya Kichwa tu hata sikusema chochote huku moyo ukianzaΒ  kunienda mbio maana hao Walinzi walikuwa kama Saba tenaΒ  walioshiba sasa nikawaza endapo nitagundulika naweza kuuwawaΒ  hapo kisha ndoto yangu ya kuwa huru ikazimwa.Β 

    Tulipofika karibu na Chumba chake aliwaambia walinzi wake.Β 

    “Msijali nipo sawa” Aliwaambia kisha Sisi tuliingia ChumbaniΒ  kwake, angalau moyo wangu ulichanua kidogoΒ 

    “Juliana, pamoja na pesa zangu na umaarufu nilio nao ilaΒ  sijawahi kumuona Mwanamke mzuri kama wewe, nikikusifia sanaΒ  naona nitakufuru ila Hakika Mungu alikupendelea sana” AlisemaΒ  akiwa ananisogelea,, nilishajuwa alichokiwa anakihitajiΒ  kwangu na niliambiwa udhaifu wake upo kwa Wanawake wazuriΒ  weupe

    “Unamaanisha nini? na huku umenileta kufanya nini?”Β  Nilimuuliza Bilionea KyandoΒ 

    “Oooh Ok!!” Alisema kama Mtu aliyesahau kitu, alielekeaΒ  kwenye kabati alifungua akatoa kibegi kidogo, kisha alikujaΒ  nacho karibu yangu alikifungua akatoa madini ambayo Mkuu waΒ  Magereza na Sarafina waliniambia, Moyo wangu ukasemaΒ 

    “Wow!!”Β 

    “Katika Maisha yako umewahi kushika madini Juliana….hebuΒ  yashike” Alinishikisha yakiwa kwenye mfuko maalum, kiukweliΒ  ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kushika madini tena mengiΒ  kiasi kile, Nilibakia kinywa wazi huku nikipiga hesabuΒ  nafanya nini ilia nimeweza kuyaona kirahisi hivyo.Β 

    Bilionea aliongea Kama Mtu aliyerukwa na akili kabisa ndiyoΒ  nikaamini udhaifu wa Mtu haujalishi ana nyazifa gani.Β 

    Aliyachukua madini akayarudisha kwenye kabati, kisha alirudiΒ  nilipokuwa nimesimamaΒ 

    “Ndiyo maana nimekwambia sema unataka nini Juliana, MwanamkeΒ  mzuri kama wewe unastahi kilicho bora, nipo tayari kukupaΒ  kilicho bora na kukutunza hata ukitaka kuishi Kama Mtoto waΒ  Malkia” Alizidi kusema, NilimwambiaΒ 

    “Nahitaji uhuru, hao walinzi wako wananiogopesha sana,Β  sijawahi kuishi hivi kabisa sina amani” Nilisema hukuΒ  nikijuwa jibu lake linanipa ishara ya kufanikiwa auΒ  kutokufanikiwa kwa mpango wangu wa kuina Madini yakeΒ 

    “Unataka waende wapi na kwanini wakati wapo kwa ajili yaΒ  Ulinzi wangu” Alisema kwa kukaza sauti hadi niliogopaΒ  nikahisi kama amenishtukia hiviΒ 

    “Siyo lazima tubishane Mr. Bilionea, kama haiwezekani naombaΒ  niende” Nilisema kwa sauti yenye kujiamini mnoΒ 

    “Ok Sawa!!” alikubali niondoke, sasa vitu viwili vilinipingaΒ  na kunilaumu. Moyo ulisema Hapana, miguu ikawa tayariΒ  kuondoka pale Chumbani kwake, Ningefanyaje na tayariΒ  nimeshaweka uamuzi basi nilipiga hatua kama tatu fupiΒ  kuuelekea Mlango ghfla akasemaΒ 

    “Juliana!! wewe ni wa thamani huna haja ya kuondoka” NikiwaΒ  nimesimama nilifurahi sana ndani ya nafsi yangu, alikujaΒ  mlangoni akafungua kisha akawaambia Walinzi wakeΒ 

    “Nendeni Chini hadi nitakapowaita”

    “Lakini Bosi…”ilisikika sauti ya Mlinzi wake mmoja kishaΒ  Bilionea alimkatishaΒ 

    “Mmh!! hakuna cha lakini, nitawapigia simu” Alisema kishaΒ  aliwatazama wakiondoka alafu akafunga mlango.Β 

    “Umefurahi? naamini sasa utakuwa huru kunipa uzuri wako”Β  Alisema Bilionea huyo ambaye kwenye akili yangu nilimuitaΒ  Bilionea Mwendawazimu, anaruhusu vipi Walinzi waondoke kisaΒ  Mwanamke ambaye hata hamjui, niligeuka na kurudiΒ 

    Niliketi kitandani, hayo yote nilifundishwa na SarafinaΒ  sababu kazi hizo alikuwa ameshazizoea.Β 

    “Nahitaji kuoga kidogo” NilisemaΒ 

    “Oooh Sawa Juliana” Alisema kama kichaa yaani Daah!! kweliΒ  udhaifu hasa kwenye mapenzi ni kitu kibaya sana,Β 

    “Nikimaliza na wewe unapaswa kwenda kuoga” Nilisema, basiΒ  aliachia tabasamu ila hakusema chochote. Nilibadili nguoΒ  nikaenda kuoga Bafuni nikamuacha pale Kitandani. Basi niliogaΒ  kwa kuzuga kama dakika kumi hivi, kisha nilitoka. NilimkutaΒ  akiwa kitandani, alikuwa ameshabadilisha nguo zake na kuvaliaΒ  pensi tu.Β 

    “Nenda kaoge” Nilisema.Β 

    “Tofauti yako na Malaika ni Majukumu tu, wao wanamsaidiaΒ  Mungu na wewe upo na Mimi hapa” Alisema Bilionea nikiwaΒ  ninajifuta Maji, niliishia kutabasamu tu.Β 

    “Leo ni siku adhimu sana kwangu Juliana, nina uhakika itakuwaΒ  ni siku ya Kumbukumbu kubwa” Alisema, nilicheka tuu hukuΒ  nikivaa chupi yangu, kisha nilijitupa kitandani kama MzogaΒ 

    “Ngoja nioge haraka” Alisema Bilionea Kisha aliingia BafuniΒ  kuoga, kitendo bila kuchelewa nilivalia gauni langu kishaΒ  nilielekea kwenye Kabati ambapo alihifadhi madini, Mbinu zoteΒ  nilifundishwa na Sarafina.Β 

    Nilikagua pale nilipoona aliweka lakini hayakuwepo, hapoΒ  ndipo niliposhtuka kuwa hata yeye alikuwa haniamini, nilianzaΒ  kuyatafuta Fasta fasta huku nikimsikia akiwa anaoga hukuΒ  akiwa anaimba.Β 

    Nilifanya Haraka mno, nilikagua kabati zima bila mafanikio,Β  kwa jinsi ambavyo nilikuwa nimevurugua vitu pindi atakapotokaΒ  Bafuni ni lazima nitakamatwa tu, Nilifikiria nikasema niΒ lazima niondoke hata kama madini sikuyapata, nilichukua ileΒ  picha ya Sarafina kisha nikaitupa chini, ile nataka kutokaΒ  nililiona lile begi likiwa kwenye ubavu wa kabati, harakaΒ  nililichukua. Nikaenda kufunga mlango wa Bafu kwa nje kishaΒ  nikafungua dirisha, nilipoangalia chini niliiyona ile BustaniΒ  kisha niliyatupa yale madini yakiwa ndani ya Mfuko tu sababuΒ  sikutaka kulitumia lile begi lake.Β 

    Wakati naelekea mlangoni nilisikia akiniita nimfungulie,Β  nilifungua mlango nikatoka ndani Mbio mbio huku nikiwaΒ  nimeziba sura yangu, nilishuka kwa mguu bila lifti, sasa ileΒ  nafika floo ya mwisho niliwaona wale walinzi wakipandishaΒ  juu, nilijificha mahali kisha nilisubiria hadi walipopitaΒ  wakiwa wanapiga stori, mmoja wao akiwa anasemaΒ 

    “Hivi Bosi ana shida gani? hawa wanawake watakuja kumponzaΒ  siku moja” Sikutaka kuendelea kuwasililiza badala yakeΒ  nilikimbilia nje, mlinzi wa Hoteli aliniuliza vipi mbona HaiΒ  hai?Β 

    “Kuna kitu nimeangusha” Nilimjibu kisha nilizunguka nyumaΒ  nikachukua madini nikayatia kwenye Mkoba wangu.Β 

    “Umekipata?” aliniuliza yule MlinziΒ 

    “Ndiyo kwaheri” Nilisema nikiwa na haraka sana maana nilijuwaΒ  tu wale walinzi wakifika kule juu kila kitu kitaharibika kamaΒ  nitakuwa sijaondoka.Β 

    Kulikuwa na tax pale iliyomleta Mtu, niliitumia kuondoka,Β  kisha nilienda kushuka kwenye kanisa la Azania FrontΒ  nikamlipa pesa yake yule Dereva, sasa wakati nataka kuekeaΒ  pale nilipomuacha Sarafina niliona askari, sijui askari haoΒ  walikuwa wakimitafuta mimi au walikuwa kwenye majukumu yao yaΒ  Usiku, ile Hofu nikajikuta naita Bajaji nikamwambia anipelekeΒ  Dar City Sinza.Β 

    ilikuwa ni mishale ya saa 5 Usiku, nilikuwa na hofu maanaΒ  mzigo wa madini nilionao ulikuwa na thamani kubwa sana tenaΒ  hata haukustahili kupanda Bajaji. Mwendo wa dakika 45Β  tulifika SinzaΒ 

    Nilimlipa pesa kisha nilienda hapo Dar City, nilimuuliziaΒ  Shonaa nikaambiwa zamu yake ni asubuh hadi mida ya JioniΒ  hivyo yupo kwake, niliomba namba maana sikuwa na simu, ileΒ  nataka kutoka si nikakutana na Sarafina akiwa na Mkuu waΒ  Magereza, nilijificha maana nilijuwa taarifa ya kuibiwaΒ  madini yule Bilionea iliwafikia alafu sikwenda kuwapa.Β  niliwaza nijitoe ili niwape au nifanye nini, nikakumbukaΒ nilichokifanya kule Hotelini niliweka picha ya Sarafina hivyoΒ  kwa vyovyote Sarafina atatafutwa ili Mimi nipatikane, waoΒ  waliponipita bila kuniona Mimi nilitoka ndani nikakimbiliaΒ  kwenye Bajaji nikamwambia dereva nipeleke MbeleΒ 

    “Mbele gani?” aliniulizaΒ 

    “Twende tu hapo mbele haraka” Nilimsistizia yule dereva, basiΒ  aliondoa Bajaji pale akawa anaelekea mitaa ya kumekucha,Β  nikamuomba derevaΒ 

    “Naomba uipige hii namba” NilisemaΒ 

    Aliichukua ikiwa kwneye karatasi akampigia Shonaa, alipokeaΒ  nikaongea naye nikamwabiaΒ 

    “Nipo kwenye matatizo Shonaa, nielekeze Ulipo nije haraka”Β  Nilisema, Shonaa alimuelekeza dereva wa Bajaji na uzuriΒ  mazingira hayo hayakuwa mageni ila mwanzo nilijichanganyaΒ  kujuwa hiyo sehemu inaitwaje ndiyo maana sikurudi nilipopataΒ  matatizo kule Ubungo.Β 

    “Una matatizo gani Dada yangu?” aliniulizaΒ 

    “Mazito hata nikikwambia huwezi kunielewa” Nilimwambia yuleΒ  dereva ambaye baada ya kumjibu hivyo hakuuliza kitu kingineΒ  tena.Β 

    Tulifika alipokuwa anaishi Shonaa, nilimlipa yule Dereva waΒ  Bajaji maana nilikuwa na pesa fulani nilizopewa na SarafinaΒ  wakati naenda kufanya kazi ya kuiba Madini.Β 

    Niligonga mlango wa Shonaa kwa kitambo sana bila kuitikiwa,Β  akaja yule Mama aliyewahi kunidekisha choo kipindi kileΒ 

    “Aah kumbe ni wewe, yumo humo ndani si umewahi kuishi hapaΒ  sasa si uingie” Alisema, yaani alikuwa Mshakunaku vibaya mno.Β  Nilisubiria hadi alipoondoka ndipo niliposukuma mlango, kweliΒ  Mlango ulifunguka.Β 

    Taa zilikuwa zinawaka, pale sebleni hakukuwa na Mtu,Β  nilifunga mlango kisha nilienda chumbani kwa Shonaa,Β  niligonga napo sikuitikiwa, nilifungua mlango, nilikutana naΒ  kitu kilichonishtua sana, Shonaa alikuwa amelala kitandaniΒ  damu zikiwa zimetapakaaΒ 

    “Shonaa! Shonaaa!” Nilimuita, niliona akiwa bado mzima

    “Ngoja nikupeleke Hospitali Shonaa umekumbana na nini Mama”Β  Nilisema nikiwa kwenye heka heka ila Shonaa alinipa ishara yaΒ  kutulia kwanza kisha aliniambiaΒ 

    “Jojo aliyefanya hivi ni Sarafina, anakutafuta wewe una mzigoΒ  wa Madini. Nenda mbali sana na Jiji hili vinginevyo utauwawa”Β  Alisema Shonaa kwa shida sanaΒ 

    “Siwezi kukuacha Shonaa ukiwa katika hali hii ngojaΒ  nikakuache Hospitali” Nilisema huku chozi likinibubujikaΒ 

    “Hapana huna muda Jojo, ondoka. Nikifa nitakufa nikiwaΒ  nakupambania, Kimbia Jojo” Alisema Shonaa, Mwanga ukamulikaΒ  dirishani, nikachungulia nikaona Watu wakija uelekea waΒ  Chumba cha Shonaa.Β 

    Haraka nilimwambiaΒ 

    “Naenda Shonaa nakupenda” Niliielekea ilipo swichi ya Taa yaΒ  nje, niliizima kukawa na giza kisha nikatoka haraka nikapitiaΒ  mlango wa uwani nikakimbia eneo lile.Β 

    Nilikimbia sana Usiku ule huku nikiwa ninahofia kuhusuΒ  usalama wa Shonaa maana alikuwa akivuja damu nyingi sana.Β 

    Nilichukua pikipiki nikamwmabia dereva anipeleke Ubungo,Β  nilichotaka sasa kilikuwa ni kurudi Tabora tu. Hali ilikuwaΒ  mbaya sana kwangu ndani ya Jiji la Dar, nilijiingiza kwenyeΒ  janga zito sana ambalo lilihatarisha maisha yangu moja kwaΒ  moja, nilijilaumu sana ni bora hata ningekubali kumaliziaΒ  kifungo changu kule GerezaniΒ 

    Tulipofika Ubungo nilikata tiketi kisha nilienda kulala ndaniΒ  stendi karibu na gereji ndogo iliyokuwa ikitengeneza mabasi,Β  nilijikunyata kama kifaranga cha kuku, nilimuomba MunguΒ  aliyenisahau anikumbuke ili niweze kuondoka salama kuelekeaΒ  kwetu Tabora maana hali ilizidi kuwa mbaya.Β 

    Sikupata Usingizi, madini yalikuwa kwenye mkoba wangu, zaidiΒ  ya Bilioni 20 nilikuwa nimekaa nayo pale bila Mtu yeyote yuleΒ  kujuwa kuwa nilikuwa na utajiri Mkubwa sana ambao ulkuwa naΒ  uwezo wa kubadilisha maisha ya Watu wote walio stendi kwaΒ  Usiku ule.Β 

    Baridi lilikuwa kali sana pale Ubungo lakini halikunizuiaΒ  kuwa makini, gari niliyokata tiketi nilikuwa nikitazamanaΒ  nayo macho. Alfajiri mapema sana nilikurupuka, pembeniΒ  kulikuwa na bomba la Maji, nilifungulia nikapata kuosha usoΒ  wangu ili kuondoa uchafu wa pale nilipokuwa nimekaa.

    Macho yangu yalikuwa makali sana kuangalia huku na kule iliΒ  nisije ingia mikononi mwa Watu wanaonitafuta, Picha yanguΒ  ilikuwa imesambazwa kila kona ili nikionekana tu nikamatwe,Β  Alfajiri hiyo nilienda kwanza kujisaidia kule chooni.Β  Niliporudi niliona makundi ya Askari, hofu niliyonayoΒ  ilinifanya nisimame sehemu ili kuangalia Askari wale walikuwaΒ  wanafanya nini? Nilipoona wameenda mbali kidogo na nilipokuwaΒ  naenda Mimi nilisogea kwenye gari, muda huo tayari walikuwaΒ  wameruhusu Watu kuingia.Β 

    Sasa wakati naingia humo niliona picha yangu na ya SarafinaΒ  kuwa tunatafutwa atakayetuona atapata Donge nono, nilizibaΒ  uso wangu nikashuka kwenye gari, nilirudi pale nilipokuwaΒ  nimekaa usiku kucha.Β 

    Hofu ilinijaa upya, niliona kabisa safari ya Tabora inawezaΒ  kufa tena, nikiwa naendelea kutafakari nilihisi kuguswaΒ  kwenye bega langu. Nilipogeuka nilikutana na Mtu ambayeΒ  alikuwa ana picha yangu, nahisi Mtu huyo alinihisi kuwa ndiyeΒ  Mimi ila kutokana na giza alisemaΒ 

    “Samhani nilikufananisha” Alisema kisha alisonga mbele,Β  nilitumia mkoba wangu kuficha sura yangu, nilionelea ni boraΒ  nitoweke Ubungo maana kuendelea kuwa Ubungo kungenileteaΒ  Shida kubwa sana, nilisogea geti dogo nikapita nikatokea njeΒ  kabisa, kulikuwa na kigiza fulani hivyo ile hali ilinisaidiaΒ  kujificha ili nisionekane.Β 

    Polisi walisambazwa kila kona ya Jiji na maeneo ya nje yaΒ  Jiji kutusaka Mimi na Sarafina, kutokana na lile tangazoΒ  nilijuwa wazi kuwa Sarafina alikuwa hajakamatwa. Madini badoΒ  nilikuwa nayo kwenye pochi langu. Niliona ni bora nitembeeΒ  kwa Mguu kuliko kupanda Usafiri maana tayari nilikuwaΒ  natafutwa Nchi nzima na atakayeniona aliahidiwa kupewa zawadiΒ  Nono.Β 

    ilikuwa ni safari ya Jojo na Madini yangu, nilitembea kamaΒ  Kichaa nikiifuata barabara ya Morogoro, nilipoona AskariΒ  nilichekupa na kuzama ndani kisha baadaye najitokeza naΒ  kuendelea na safari, kulipo pambazuka nilinunua kofiaΒ  nikaivaa angalau ilinisitiri kwa kiasi fulani.Β 

    Nilibakiwa na pesa kidogo sana ambayo hata isingenifikishaΒ  Morogoro ila nilikuwa na mzigo wa madini yenye thamani yaΒ  Bilioni 20 kwenye Mkoba wngu. Kila mara nilifungua naΒ  kuangalia kama madini yalikuwepo, basi nilipojisikia njaa naΒ  kuchoka nilienda sehemu nikanunua chakula ila sikula paleΒ  nilienda kukaa chini ya Mti mmoja nikapata chakula. MaishaΒ  yangu yalipoteza nuru ila kile kiasi cha madini kilinipaΒ nguvu ya kuzidi kusonga mbele, mida ya Jioni nilifika KibahaΒ  Maili moja miguu ikiwa haitamaniki ilikuwa ikiuma sana.Β 

    “Ooh Mungu nimechoka sasa” Nilisema nikiwa ninakaa kando yaΒ  eneo la Mnada wa nguo, nilikaa hapo hadi giza lilipoingia.Β  Chupi ilikuwa ikiniumiza kutokana na Uchafu wa kuivaa kutwaΒ  nzima, kwasababu eneo lile lilikuwa giza basi niliondoa ileΒ  chupi pale mnadani, pia kulikuwa na ronya za nguo ambazoΒ  ziliachwa nilitafuta pensi nikavaa pia tisheti niliipataΒ  nikaavaa na wala sikujali nitaonekanaje ila nilichotaka niΒ  kwenda mbali na Jiji la Dar.Β 

    Sikutaka kupumzika Kibaha niliendelea mbele, WatuΒ  niliopishana nao walikuwa wakiongea kuhusu Mimi kuiba MadiniΒ  bila kujuwa waliokuwa wakimzungumzia walikuwa wakipishanaΒ  naye.Β 

    Zile nguo nilienda kuzitupa kwenye daraja moja ambaloΒ  lilikuwa linapitisha maji mengi kisha niliendelea na safariΒ  yangu, gari za polisi zilikuwa zikipita kwa wingi kama vileΒ  kulikuwa na msafara wa Rais wa Nchi kumbe ulikuwa ndio msakoΒ  wangu na kwavile nilipita barabara ya vumbi nikiwa naitazamaΒ  Barabara kuu kwa Mbali niliona jinsi msako ulivyokuwaΒ  ukiendelea.Β 

    Nilipochoka nililala Kwenye kichaka fulani hadi asubuhi kishaΒ  safari iliendelea, kadiri nilivyokuwa natoka nje ya JijiΒ  ndivyo nilivyoanza kuhisi kuwa tayari nimejikwamua kutokaΒ  kwenye msako ule mkali, Nilichofikiria sasa kilikuwa niΒ  madini na pesa nitakayoipata.Β 

    Pesa ilikuwa imeniishia kabisa, nilipofika mbele kidogoΒ  niliona sonara ndogo. Nilikaa sehemu nikapekua yale madiniΒ  nikatafuta dini dogo sana yaani kakipande fulani tu ambachoΒ  nilihisi kuwa pesa yake isingekuwa kubwa sana, niliingia humoΒ  ili niuze. Nilijitahidi sana kukwepa macho ya Mtu wa SonaraΒ 

    Nilimpa lile dini, kwanza alishtuka sana maana lilikuwa niΒ  dini lenye thamani kubwa tofauti na nilivyofikiria, alilipimaΒ  na kugundua kuwa lilikuwa lenyewe siyo feki kisha aliniambiaΒ 

    “Dada yangu pesa sina, hili nenda kauze Kwa wale wenye SonaraΒ  kubwa kabisa” Alikuwa Kijana mmoja wa KipembaΒ 

    “Linagharimu shilingi ngapi?” Nilimuuliza maana nilikuwaΒ  sijui kuhusu MadiniΒ 

    “Hili siyo chini ya Milioni 45 ndiyo maana nasema sina helaΒ  ya kukupa” Alijibu yule jamaa, sasa nilifikiria niende hukoΒ  anakosema nilihisi nitakamatwa nikamwambia

    “Wewe nipe uliyonayo, ukiuza nitakuja kuchukua hela kwako”Β  Nilisema kama vile mzoefu wa hiyo Biashara.Β 

    “Alivyoskia hivyo alihangaika akafungua droo akatoa milioniΒ  mbili akaniambiaΒ 

    “Ipo hii ila nakuhakikishia hadi kufikia jioni litakuwaΒ  limeuzika, tena nitaenda Mjini kuliuza” Alisema.Β 

    Sikumjibu nilichukua zile pesa nikazitia kwenye Mkoba bilaΒ  hata kuhesabuΒ 

    “Ungezihesabu kwanza Dada yangu”Β 

    “hata Usijali nakuamini” Nilisema kisha niliondoka pale,Β  Kumbe nyuma yule Dogo alipiga simu sehemu ambapo angeuza hiloΒ  dini, sasa taarifa zangu zilikuwa zimesambazwa kwa WauzaΒ  madini nchi nzima, yule jamaa aliambiwa anikamate.Β 

    Ile anatoka nje tu Mimi ndiyo kwanza nilikuwa nitoka naΒ  Bodaboda, nilipogeuka nilimuona akihangaika kujuwa nimeelekeaΒ  wapi, ni wazi alikuwa hajaniona. Nilimwambia dereva aingieΒ  njia nyingine ili asionione kabisa, kweli dereva alinipitishaΒ  njia nyingine tukaenda kutokea Barabara Kuu.Β 

    Nilimlipa kisha nilichukua Pikipiki nyingine nikamwambiaΒ  anisogeze mbele kwa kutumia njia za vumbi za Shoti kati,Β  mbele ya pesa kila kitu kiliwezekana hadi nilifika MbeleΒ  zaidi, nikapanda gari ndogo ya abiria hadi Chalinze. HapoΒ Β nilikodi Pikipiki inifikishe Morogoro.Β 

    Nilifika Morogoro mishale ya saa 10 Jioni, nilitafuta gest yaΒ  vichochoroni nikala kisha nikalala zangu bila hata hofu kuwaΒ  ninatembea na mzigo mkubwa wa Madini. Hofu yangu ilikuwa kwaΒ  polisi pekee, nikiwa hapo nilipata kuona taarifa ya HabariΒ  kuwa Sarafina na Mkuu wa Magereza walikuwa wamekatwa baada yaΒ  Sarafina kumtaja Mkuu huyo, Sasa kupitia kamera za KuleΒ  Hotelini siku ya tukio la kuiba madini sura yangu ilionekanaΒ  nikawa natafutwa Kila kona huku akina Sarafina wakiwa kwenyeΒ  mikono ya Polisi, kilichotakiwa kilikuwa ni Madini ya yuleΒ  Bilionea.Β 

    Nilizima TV ili nisiendelee kuangalia habari hiyo, NililalaΒ  hadi Asubuhi, Mapema sana nilianza safari ya kuelekea TaboraΒ  kwa kutumia Basi. Nilifika Tabora usiku sana, nilichukuaΒ  pikipiki hadi nyumbani kwetu, Nilimgongeshea mlango MamaΒ  Rafia ambaye ndiye jirani yetu kule Tabora nikamwambia

    “Nifungulie tafadhali Mama Rafia” Nilisema nikiwa bado ninaΒ  hofu ya kukamatwa, Mama Rafia alifungua kisha aliniulizaΒ 

    “Kulikoni Jojo? taarifa zako zimeenea kila kona, Tobra nzima,Β  imekuwaje Mwanangu” Alisema Mama Rafia,,Β 

    “Mama laiti kama ningelijuwa nisingelienda Dar, Maisha yanguΒ  yameharibika baada ya kufika huko” NilisemaΒ 

    “Ni kweli umeiba Madini Mwanangu?” aliniuliza, alikuwa niΒ  jirani pia rafiki wa Marehemu Mama yangu, nisingeliwezaΒ  kumficha. Nilimwambia ukweli na nilimuonesha madiniΒ 

    Tuliingia ndani kwake maana alikuwa akiishi peke yake kishaΒ  alinielezaΒ 

    “Msonjo amekamatwa Jana Mchana, inasemekana kuwa yeyeΒ  anahusika na anajuwa ulipo”Β 

    “Hapana Mama, Msonjo sijawasiliana naye kwa zaidi ya mieziΒ  yote niliyokuwa Dar, nimepata mitihani mikubwa sana Mama”Β  NilisemaΒ 

    “Sasa Jojo, haya Madini ni mali ya Watu hivyo muda wowoteΒ  unaweza kukamatwa, kuliko ukamatwe kwa kosa dogo ni boraΒ  ukamatwe kwa kosa kubwa” Alisema Mama RafiaΒ 

    “Unamaanisha nini Mama”Β 

    “Yafiche kiasi alafu mengine kaa nayo ili ukikamatwaΒ  uyaoneshe! utakapotoka huko utajuwa pa kuanzia” Alisema MamaΒ  Rafia, nilimuamini yeye hivyo nilimpa kiasi cha Madini kishaΒ  mengine niliondoka nayo usiku huo na kwenda nyumbani.Β 

    Asubuhi Mapema Mlango uligongwa, Sauti ya Mama RafiaΒ  niliisikia.Β 

    “Nakuja Mama” Nilisema, kisha nilivaa vizuri maana nilikuwaΒ  nimelala. Nilipofungua mlango nilikutana na Askari wakiwaΒ  wameongozana na Mama RafiaΒ 

    “Huyu hapa!! kiukweli Askari Mimi sitaki Matatizo kabisa,Β  huyu Binti anayo hayo madini yanayotafutwa” Alisema MamaΒ  Rafia, kiukweli nilipigwa na ButwaaΒ 

    “Mamaaa”Β 

    “Siyo Mama, kiukweli Jojo sitaki matatizo na Mtu ndiyo maanaΒ  nimewaambia polisi, ningekaa kimya ningekuja kukamatwa naΒ Mimi” Wale Polisi waliingia ndani wakachukua mkoba wenyeΒ  Madini, Chozi lilinibubujika sana.Β 

    “Basi Mama nipe yale madini niliyokupa ili tumrudishieΒ  mwenyewe” Nilisema huku chozi likinivujaΒ 

    “Madini? kuna madini uliyonipa Mimi Jojo? ndiyo maanaΒ  niliyakataa mapema haya nikaamuwa kusema kwa polisi” MasikiniΒ  nililia sana Aisee, Mama Rafia alinikana mbele ya WaleΒ  askari. Nilikamatwa kisha nilirudishwa DarΒ 

    Nikiwa kituo cha polisi nilikutana na Sarafina na yule MkuuΒ  wa Magereza pia nilikutanishwa na Biliona niliyemuibiaΒ  Madini. Alihakiki madini akaona hayajatimia hivyo niliteswaΒ  sana ili niseme yalipo, nilimtaja Mama Rafia ila alinikataaΒ  mbele ya Askari, Tulipelekwa mahakamani kila mmoja na kosaΒ  lake, Mimi nilikuwa na kesi ya wizi wa Madini, SarafinaΒ  alihusika na kifo cha Shonaa pia kupanga njama ya wizi waΒ  madini, Mkuu wa Magereza alikuwa na kesi nzito zilizoihusuΒ  magereza yake, kifo cha Shonaa na Njama za kuiba Madini.Β 

    Binafsi nilihukumiwa kwenda jela Miaka Mitamo, SarafinaΒ  alienda jela miaka 25, Mkuu wa Magereza alifungwa kifungo chaΒ  Maisha Jela sababu alikutwa na kesi nyingi za mauwaji.Β 

    Kila mmoja alipelekwa Gereza lake kutumikia adhabu.Β  Nilimpoteza Mama yangu, Nilimpoteza Shonaa, NilipotezaΒ  thamani yangu, pia nilimpoteza Mama Rafia kisa Madini. SikuΒ  moja nilitembelewa na Msonjo nikiwa gerezani aliniambia kuwaΒ  Mama Rafia amejenga jumba la kifahari, ana Biashara nyingiΒ  anafanya tena ameahama kabisa Tabora anaishi zake Dodoma.Β 

    “Msomjo Mimi Mungu amenisahau” Lilikuwa ndiyo neno langu laΒ  Mwisho kulisema, sikuhitaji kuonana na Mtu mwingine tena.Β  Hadi sasa unaposoma hadithi hii Mimi ninatumikia adhabu mwakaΒ  wa 8.Β 

    MWISHO

    Mwisho wa HADITHI Hii Ndio Mwanzo Wa HADITHI NYINGINE…. Kukiwa na COMMENTS Nyingi Mpya Inaanza Mapema Tu

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xxΒ  Β Mungu Amenisahau xxΒ  Β Mungu Amenisahau xxΒ  Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xx Β Mungu Amenisahau xxΒ 

     

    Β Β 

    Mungu Amenisahau

    14 Comments

    1. Sir yowas on October 8, 2024 11:31 am

      Jamani, tamthiliya nzuri, natamani ingeendelea

      Reply
    2. Muharram on October 8, 2024 11:33 am

      Duh jojo Hattari kweli kweli

      Reply
      • Kelvine on October 8, 2024 11:59 am

        πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

        Reply
      • G shirima on October 8, 2024 1:18 pm

        Mh ivi mnatunga tu au mnaiba maana hii ni mfano wa AI

        Reply
        • Jolene on October 9, 2024 12:15 pm

          Heeee

          Reply
    3. Rifai on October 8, 2024 11:51 am

      Hongera sana admin kwa kweli inasisimua sana😭hadi kusoma unaogoa😒
      Mwisho wa riwaya hii ndio mwanzo mzuri🌹wa riwaya nyengine
      Kila lenye kheir liwe kwako ni nzur san hii riwayaβ˜‘οΈπŸ’―

      Reply
    4. Nelca on October 8, 2024 11:52 am

      Nimelia saaana😭😭😭😭😭

      Reply
    5. Sharifu shabani juma on October 9, 2024 2:19 pm

      Darasa la Saba

      Reply
    6. Sabiti Mussa23 on October 10, 2024 7:32 am

      Kuna cha kujifunza hapa wanakijiwe

      Reply
    7. Doreen on October 10, 2024 12:53 pm

      Asante sana ndugu admin πŸ‘πŸ»πŸ‘πŸ»

      Reply
    8. πŸ” Notification: SENDING 1,644023 BTC. Withdraw > https://graph.org/Payout-from-Blockchaincom-06-26?hs=3ee570cb05ecf9dbc07cdd2ad478010e& πŸ” on June 30, 2025 8:16 pm

      0yjh7u

      Reply
    9. πŸ›Ž ⚠️ Verification Needed - 0.9 Bitcoin transfer delayed. Confirm here β†’ https://graph.org/ACQUIRE-DIGITAL-CURRENCY-07-23?hs=3ee570cb05ecf9dbc07cdd2ad478010e& πŸ›Ž on July 27, 2025 12:01 am

      g6z02b

      Reply
    10. βœ‰ πŸ† BTC Reward: 1.0 BTC added. Claim now > https://graph.org/WITHDRAW-YOUR-COINS-07-23?hs=3ee570cb05ecf9dbc07cdd2ad478010e& βœ‰ on August 8, 2025 6:13 am

      jcdyuj

      Reply
    11. πŸ”Ž πŸ“’ Notification - 0.95 BTC ready for transfer. Confirm β†’ https://graph.org/EARN-BTC-INSTANTLY-07-23?hs=3ee570cb05ecf9dbc07cdd2ad478010e& πŸ”Ž on August 12, 2025 3:13 pm

      e85u35

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Hadithi February 23, 2026

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    IlipoishiaΒ  Kwanza nilijiuliza ni Nani anayeweza kuja kwetu, kama Mama Amida tayariΒ  tulishazungumza. Nilimeza funda…

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (07)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.