Ilipoishia “Tulirudi kule kwenye ghorofa la Tancot House ambapo ndiyoย tulilala usiku uliopita, Nilijaribu nguo zote ikapatikanaย moja tu ambayo ilionekana kuwa nzuri sana na yenyeย kunipendeza zaidiย
“Wow!! Hii ndiyo yenyewe Jojo, nina uhakika hawezi kuchomoka,ย sasa unapaswa kuwa makini sana sababu ni lazima akuchukueย kama kimada wa kulala naye Usiku, ndipo utakapo iba hayoย madini, utachunguza kujuwa yalipo, baada ya kufanikishaย zoezi, utafungua dirisha sababu chumba chake kipo masharikiย mwa jengo hilo, utayatupa madini kwa kutumia kifaa ambachoย kitakuwa kimehifadhi kisha utayachukua baada ya kushuka, kuwaย makini sana vinginevyo unaweza ishia huko Hotelini, pia niย lazima ukamilishe zoezi ili uwe huru” alinieleza Sarafina. Endelea
SEHEMU YA KUMI
“Sawa” niliitikia ili kuondoa ngoma juani sababu nilishajuaย utakuwa ni mtihani mzito sana kufanya hivyo.ย
Basi tulienda kula na tuliporudi tulilala, asubuhi alinipaย kadi maalum ya kuingilia Hotelini kwa ajili ya Hafla hiyo.ย
“Kila la kheri Jojo” Alisema Sarafina, sikuwa na maneno mengiย ya kuzungumza sababu nilishapewa maelekezo yote naย nikayaelewaย
“Upande ambao utayatupa madini kuna bustani ya mauwa hivyoย kuwa makini sana uyatupe mahali ambapo utaweza kuyaokotaย kirahisi, utayatupa sababu hutoweza kupita nayo mlangoniย walinzi wake watakukagua”ย
“Ok sawa!”ย
Japo niliikubali kazi ile ili niwe huru ila nilikuona chaย mtema kuni maana jukumu lilikuwa zito sana, niliendeleaย kupiganisha akili yangu, nilifikiria jambo kwa pale kwenyeย hoteli kuna kamera hivyo itakuwa rahisi mimi kuonekana,ย niliwaza nifanye nini maana kama nitaonekama nitatafutwa naย kukamatwa kwa kosa ambalo litawafaidisha wengine, wakatiย naendelea kutafakari niliona picha ya paspot pembeni, ilikuwaย ni picha ya Sarafina. Niliivuta kwa mguu bila Sarafinaย kushtuka kisha niliiweka kwenye mkoba wangu huku nikijuwaย ndani ya akili yangu nitafanya nini ili kuwa salama.ย
Jioni mishale ya saa 12 Jioni, Sarafina alinieleza kuwa ndiyoย muda wa kuelekea Hotelini kwa ajili ya kuiba hayo madini,ย nilijiangalia kwenye kioo nilijikuta nikitabasamu licha yaย hatari iliyo mbele yangu, uzuri wangu, nilifanana sana naย Marehemu Mama yangu.ย
Tulitoka, nje alinipakiza kwenye gari moja ya kifahari sanaย nyeusi.ย
“Mimi siwezi kwenda huko sababu kadi ni moja tu ambayoย nimekupa wewe, ifanye kazi uwe huru Jojo, ukitugeuka basiย juwa msala huu utakuwa wako peke yako” alinisistiza Sarafinaย
“Nimekuelewa Sarafina” Basi, nilifunga mlango kisha safariย fupi sana ya kuelekea Hotelini ilianza, ilituchukua dakikaย nne kufika Hotelini, nilishuka kwenye gari baada yaย kukaguliwa kama Mwana Malikia vile kumbe nilikuwa mwizi tu.ย
Mlango Mkuu wa Kuingilia nilitakiwa kuonesha ile kadi,ย nilifanya hivyo kisha niliruhusiwa kuelekea ndani ambakoย kulikuwa na hiyo Afla iliyo hudhuriwa na viongozi kadhaa naย wafanya biashara wakubwa wa Tanzania. Sikuwahi kuingia sehemuย nzuri na ya kifahari kama ile katika Maisha yangu, ilinifanyaย niwe muoga kiasi chake japo hakuna aliyeshtuka.ย
Hadhi niliyovishwa ilikuwa kubwa sana, mavazi niliyovaaย yaliakisi ukubwa wangu na hadhi yangu, nilionekana ni mwenyeย Maisha mazuri, mzuri na mrembo kuliko Wanawake woteย waliohudhuria kwenye Afla hiyo.ย
Niliketi kwenye meza ambayo haikuwa na Mtu yeyote yule hukuย Watu wakiwa bize na mazungumzo ya Hapa na pale, nilimuonaย huyo Bilionea wa Madini akiwa ameketi anazungumza. Mahaliย nilipochagua kuketi palikuwa na urahisi wa yeye kuniona pindiย atakapogeuza shingo yake, Wanaume wengi walikuwa bizeย kunitazama nami nikajifanya bize na Afla hiyo ambayo ilikuwaย ikiendelea.ย
Walikuja Wanaume kadhaa kuniuliza maswali fulani ambayoย nilijuwa lengo lilikuwa ni kunihitaji kimapenzi ilaย niliwakatalia hata kuketi karibu na Mimi sababu kufanya hivyoย kungemfanya Bilionea pindi atakaponiona asiwe na wazo laย kunihitaji.
Bilionea huyo alikuwa Kijana mtanashati, kichwa changuย kilikuwa na maelekezo yote kutoka kwa Sarafina na Mkuu waย Magereza juu ya kuiba hayo Madini yenye thamani kubwa sanaย japo nilijuwa haitokuwa rahisi kufanya hivyo, nililetewaย Vinywaji na chakula nikawa ninakula ila akili na macho yanguย yakiwa kwa huyo Bilionea Kijana.ย
Nililetewa vimemo kadhaa vya Wanaume vyenye namba, nilivisomaย na kuvitupa sababu hakuna hata kimoja kilichotoka kwa Mlengwaย wangu, niliendelea kusubiria kwa masaa kadhaa huku akionekanaย bize sana kucheka, Moyo wangu ulihitaji uhuru hivyo nilionaย ย
kazi hiyo ingenifanya niwe huru na kurudi Tabora.ย
Nilizuga kufanya vitu kadhaa ikiwemo kwenda chooni ilimradiย anione lakini haikuwezekana hadi pale dakika za mwisho ambapoย aligeuka akaniona kidogo alafu akarudisha macho kwa aliyekuwaย akiongea naye, nilihisi labda hakuuona uzuri wangu, nilianzaย kukata tamaa kumbe alikuwa ameniona ila alikuwa akitafutaย engo nzuri ya kunitazama, nikiwa nimeshakata tamaa natakaย kunyanyuka. Niliona nimtazame kwa mara ya mwisho hukuย nikijiambiaย
“Geuka unitazame basi” Nilisema kwa hisia na kwa kumaanishaย kabisa, ile namtazama nilikutana naye ana kwa ana tenaย akionekana alikuwa akinitazama kwa muda mrefu, basiย nilijitingisha kidogo alafu nikatazama chakula changu, nikawaย na uhakika kuwa ameniona na alikuwa akiniangalia kwaย kunitamani.ย
Basi, Dakika chache alikuja mlinzi wake akaniambiaย
“Bosi anahitaji kuzungumza na wewe” Alisema, ili nisionekaneย mrahisi nilimwambiaย
“Mwambie akome sikuja hapa kwa ajili ya Mtu yeyote yule”ย Nilisema, yule Mlinzi aliganda kidogo kisha akasemaย
“Dada usipoteze bahati yako, Bosi wangu ni Bilionea Mkubwa waย Madini, amekuwa akikuangalia kwa muda mrefu sana” Alisemaย tena, sasa niliona nikubali maana kujizugisha wakatiย kilichonileta kilikuwa ni hicho niliona ni Ujingaย
“Yupo wapi?” niliuliza kanakwamba nilikuwa simjuiย
“Yule Pale kwenye ile Meza” Alisema kisha nilipeleka machoย huko, niligongana naye macho akiwa ananikodolea sana, moyoniย nikasemaย
“Umenasa Bosi”
Basi, nilinyanyuka taratibu nikaelekea kwenye hiyo Meza,ย alitoa walinzi wake akaniambiaย
“Kuwa huru, karibu Naitwa Bilionea Vitalis Kyando” Alisemaย kisha alinipatia Mkono wake, nilimpa wangu tukashikanaย
“Naitwa….Juliana” Nilifikiria kusema jina langu halisiaย nikaona inaweza niletea shida baadaye, niliamuwa kumdanganya.ย
“Ooh Juliana! Nimefurahi kukufahamu, hakika Mungu alikuumbaย kwa utulivu sana, muda mrefu nimekuwa nikikutazama alafuย akili yangu ilikosa utulivu, unastahili kila kilicho boraย Juliana, Niambie unataka nini” Aliniuliza Swali kwa ujasiriย Mkubwa sana, niliwaza vingi kwa haraka sana, nikakumbukaย kauli ya Msonjo kuwa Mimi ni mzuri sana ninapaswa kuishi Dar,ย Nilifikiria nifanyaje na nipo kwenye mpango wa kumuibia iliย niwe huruย
“Asante! kukufahamu pekee ni kitu kinachonitosha” Nilisemaย japo nafsi ilikuwa ikinisuta na kuniita Zuzu wa Mwishoย
“Juliana Usiogope kama unahitaji Biashara, Nyumba, gari zuriย la kutembelea niambie tu kuwa huru labda hujajuwa unaongea naย Mtu gani….Hebu nifuate” Alisema huyo Bilionea, alinyanyukaย kisha nami nilinyanyuka nikajiuliza alikuwa anatakaย kunionesha kitu gani, Basi nilimfuata huku walinzi wakeย wakija kwa nyuma.ย
Tulipanda Lifti hadi ghorofa ya nne ambapo ndipo alipokuwaย amechukua chumba.ย
“Kama walinzi wangu wanakufanya usiwe huru Juliana niambieย sawa?” Alisema Bilionea Vitalis Kyando, niliitikia kwa isharaย ya Kichwa tu hata sikusema chochote huku moyo ukianzaย kunienda mbio maana hao Walinzi walikuwa kama Saba tenaย walioshiba sasa nikawaza endapo nitagundulika naweza kuuwawaย hapo kisha ndoto yangu ya kuwa huru ikazimwa.ย
Tulipofika karibu na Chumba chake aliwaambia walinzi wake.ย
“Msijali nipo sawa” Aliwaambia kisha Sisi tuliingia Chumbaniย kwake, angalau moyo wangu ulichanua kidogoย
“Juliana, pamoja na pesa zangu na umaarufu nilio nao ilaย sijawahi kumuona Mwanamke mzuri kama wewe, nikikusifia sanaย naona nitakufuru ila Hakika Mungu alikupendelea sana” Alisemaย akiwa ananisogelea,, nilishajuwa alichokiwa anakihitajiย kwangu na niliambiwa udhaifu wake upo kwa Wanawake wazuriย weupe
“Unamaanisha nini? na huku umenileta kufanya nini?”ย Nilimuuliza Bilionea Kyandoย
“Oooh Ok!!” Alisema kama Mtu aliyesahau kitu, alielekeaย kwenye kabati alifungua akatoa kibegi kidogo, kisha alikujaย nacho karibu yangu alikifungua akatoa madini ambayo Mkuu waย Magereza na Sarafina waliniambia, Moyo wangu ukasemaย
“Wow!!”ย
“Katika Maisha yako umewahi kushika madini Juliana….hebuย yashike” Alinishikisha yakiwa kwenye mfuko maalum, kiukweliย ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kushika madini tena mengiย kiasi kile, Nilibakia kinywa wazi huku nikipiga hesabuย nafanya nini ilia nimeweza kuyaona kirahisi hivyo.ย
Bilionea aliongea Kama Mtu aliyerukwa na akili kabisa ndiyoย nikaamini udhaifu wa Mtu haujalishi ana nyazifa gani.ย
Aliyachukua madini akayarudisha kwenye kabati, kisha alirudiย nilipokuwa nimesimamaย
“Ndiyo maana nimekwambia sema unataka nini Juliana, Mwanamkeย mzuri kama wewe unastahi kilicho bora, nipo tayari kukupaย kilicho bora na kukutunza hata ukitaka kuishi Kama Mtoto waย Malkia” Alizidi kusema, Nilimwambiaย
“Nahitaji uhuru, hao walinzi wako wananiogopesha sana,ย sijawahi kuishi hivi kabisa sina amani” Nilisema hukuย nikijuwa jibu lake linanipa ishara ya kufanikiwa auย kutokufanikiwa kwa mpango wangu wa kuina Madini yakeย
“Unataka waende wapi na kwanini wakati wapo kwa ajili yaย Ulinzi wangu” Alisema kwa kukaza sauti hadi niliogopaย nikahisi kama amenishtukia hiviย
“Siyo lazima tubishane Mr. Bilionea, kama haiwezekani naombaย niende” Nilisema kwa sauti yenye kujiamini mnoย
“Ok Sawa!!” alikubali niondoke, sasa vitu viwili vilinipingaย na kunilaumu. Moyo ulisema Hapana, miguu ikawa tayariย kuondoka pale Chumbani kwake, Ningefanyaje na tayariย nimeshaweka uamuzi basi nilipiga hatua kama tatu fupiย kuuelekea Mlango ghfla akasemaย
“Juliana!! wewe ni wa thamani huna haja ya kuondoka” Nikiwaย nimesimama nilifurahi sana ndani ya nafsi yangu, alikujaย mlangoni akafungua kisha akawaambia Walinzi wakeย
“Nendeni Chini hadi nitakapowaita”
“Lakini Bosi…”ilisikika sauti ya Mlinzi wake mmoja kishaย Bilionea alimkatishaย
“Mmh!! hakuna cha lakini, nitawapigia simu” Alisema kishaย aliwatazama wakiondoka alafu akafunga mlango.ย
“Umefurahi? naamini sasa utakuwa huru kunipa uzuri wako”ย Alisema Bilionea huyo ambaye kwenye akili yangu nilimuitaย Bilionea Mwendawazimu, anaruhusu vipi Walinzi waondoke kisaย Mwanamke ambaye hata hamjui, niligeuka na kurudiย
Niliketi kitandani, hayo yote nilifundishwa na Sarafinaย sababu kazi hizo alikuwa ameshazizoea.ย
“Nahitaji kuoga kidogo” Nilisemaย
“Oooh Sawa Juliana” Alisema kama kichaa yaani Daah!! kweliย udhaifu hasa kwenye mapenzi ni kitu kibaya sana,ย
“Nikimaliza na wewe unapaswa kwenda kuoga” Nilisema, basiย aliachia tabasamu ila hakusema chochote. Nilibadili nguoย nikaenda kuoga Bafuni nikamuacha pale Kitandani. Basi niliogaย kwa kuzuga kama dakika kumi hivi, kisha nilitoka. Nilimkutaย akiwa kitandani, alikuwa ameshabadilisha nguo zake na kuvaliaย pensi tu.ย
“Nenda kaoge” Nilisema.ย
“Tofauti yako na Malaika ni Majukumu tu, wao wanamsaidiaย Mungu na wewe upo na Mimi hapa” Alisema Bilionea nikiwaย ninajifuta Maji, niliishia kutabasamu tu.ย
“Leo ni siku adhimu sana kwangu Juliana, nina uhakika itakuwaย ni siku ya Kumbukumbu kubwa” Alisema, nilicheka tuu hukuย nikivaa chupi yangu, kisha nilijitupa kitandani kama Mzogaย
“Ngoja nioge haraka” Alisema Bilionea Kisha aliingia Bafuniย kuoga, kitendo bila kuchelewa nilivalia gauni langu kishaย nilielekea kwenye Kabati ambapo alihifadhi madini, Mbinu zoteย nilifundishwa na Sarafina.ย
Nilikagua pale nilipoona aliweka lakini hayakuwepo, hapoย ndipo niliposhtuka kuwa hata yeye alikuwa haniamini, nilianzaย kuyatafuta Fasta fasta huku nikimsikia akiwa anaoga hukuย akiwa anaimba.ย
Nilifanya Haraka mno, nilikagua kabati zima bila mafanikio,ย kwa jinsi ambavyo nilikuwa nimevurugua vitu pindi atakapotokaย Bafuni ni lazima nitakamatwa tu, Nilifikiria nikasema niย lazima niondoke hata kama madini sikuyapata, nilichukua ileย picha ya Sarafina kisha nikaitupa chini, ile nataka kutokaย nililiona lile begi likiwa kwenye ubavu wa kabati, harakaย nililichukua. Nikaenda kufunga mlango wa Bafu kwa nje kishaย nikafungua dirisha, nilipoangalia chini niliiyona ile Bustaniย kisha niliyatupa yale madini yakiwa ndani ya Mfuko tu sababuย sikutaka kulitumia lile begi lake.ย
Wakati naelekea mlangoni nilisikia akiniita nimfungulie,ย nilifungua mlango nikatoka ndani Mbio mbio huku nikiwaย nimeziba sura yangu, nilishuka kwa mguu bila lifti, sasa ileย nafika floo ya mwisho niliwaona wale walinzi wakipandishaย juu, nilijificha mahali kisha nilisubiria hadi walipopitaย wakiwa wanapiga stori, mmoja wao akiwa anasemaย
“Hivi Bosi ana shida gani? hawa wanawake watakuja kumponzaย siku moja” Sikutaka kuendelea kuwasililiza badala yakeย nilikimbilia nje, mlinzi wa Hoteli aliniuliza vipi mbona Haiย hai?ย
“Kuna kitu nimeangusha” Nilimjibu kisha nilizunguka nyumaย nikachukua madini nikayatia kwenye Mkoba wangu.ย
“Umekipata?” aliniuliza yule Mlinziย
“Ndiyo kwaheri” Nilisema nikiwa na haraka sana maana nilijuwaย tu wale walinzi wakifika kule juu kila kitu kitaharibika kamaย nitakuwa sijaondoka.ย
Kulikuwa na tax pale iliyomleta Mtu, niliitumia kuondoka,ย kisha nilienda kushuka kwenye kanisa la Azania Frontย nikamlipa pesa yake yule Dereva, sasa wakati nataka kuekeaย pale nilipomuacha Sarafina niliona askari, sijui askari haoย walikuwa wakimitafuta mimi au walikuwa kwenye majukumu yao yaย Usiku, ile Hofu nikajikuta naita Bajaji nikamwambia anipelekeย Dar City Sinza.ย
ilikuwa ni mishale ya saa 5 Usiku, nilikuwa na hofu maanaย mzigo wa madini nilionao ulikuwa na thamani kubwa sana tenaย hata haukustahili kupanda Bajaji. Mwendo wa dakika 45ย tulifika Sinzaย
Nilimlipa pesa kisha nilienda hapo Dar City, nilimuuliziaย Shonaa nikaambiwa zamu yake ni asubuh hadi mida ya Jioniย hivyo yupo kwake, niliomba namba maana sikuwa na simu, ileย nataka kutoka si nikakutana na Sarafina akiwa na Mkuu waย Magereza, nilijificha maana nilijuwa taarifa ya kuibiwaย madini yule Bilionea iliwafikia alafu sikwenda kuwapa.ย niliwaza nijitoe ili niwape au nifanye nini, nikakumbukaย nilichokifanya kule Hotelini niliweka picha ya Sarafina hivyoย kwa vyovyote Sarafina atatafutwa ili Mimi nipatikane, waoย waliponipita bila kuniona Mimi nilitoka ndani nikakimbiliaย kwenye Bajaji nikamwambia dereva nipeleke Mbeleย
“Mbele gani?” aliniulizaย
“Twende tu hapo mbele haraka” Nilimsistizia yule dereva, basiย aliondoa Bajaji pale akawa anaelekea mitaa ya kumekucha,ย nikamuomba derevaย
“Naomba uipige hii namba” Nilisemaย
Aliichukua ikiwa kwneye karatasi akampigia Shonaa, alipokeaย nikaongea naye nikamwabiaย
“Nipo kwenye matatizo Shonaa, nielekeze Ulipo nije haraka”ย Nilisema, Shonaa alimuelekeza dereva wa Bajaji na uzuriย mazingira hayo hayakuwa mageni ila mwanzo nilijichanganyaย kujuwa hiyo sehemu inaitwaje ndiyo maana sikurudi nilipopataย matatizo kule Ubungo.ย
“Una matatizo gani Dada yangu?” aliniulizaย
“Mazito hata nikikwambia huwezi kunielewa” Nilimwambia yuleย dereva ambaye baada ya kumjibu hivyo hakuuliza kitu kingineย tena.ย
Tulifika alipokuwa anaishi Shonaa, nilimlipa yule Dereva waย Bajaji maana nilikuwa na pesa fulani nilizopewa na Sarafinaย wakati naenda kufanya kazi ya kuiba Madini.ย
Niligonga mlango wa Shonaa kwa kitambo sana bila kuitikiwa,ย akaja yule Mama aliyewahi kunidekisha choo kipindi kileย
“Aah kumbe ni wewe, yumo humo ndani si umewahi kuishi hapaย sasa si uingie” Alisema, yaani alikuwa Mshakunaku vibaya mno.ย Nilisubiria hadi alipoondoka ndipo niliposukuma mlango, kweliย Mlango ulifunguka.ย
Taa zilikuwa zinawaka, pale sebleni hakukuwa na Mtu,ย nilifunga mlango kisha nilienda chumbani kwa Shonaa,ย niligonga napo sikuitikiwa, nilifungua mlango, nilikutana naย kitu kilichonishtua sana, Shonaa alikuwa amelala kitandaniย damu zikiwa zimetapakaaย
“Shonaa! Shonaaa!” Nilimuita, niliona akiwa bado mzima
“Ngoja nikupeleke Hospitali Shonaa umekumbana na nini Mama”ย Nilisema nikiwa kwenye heka heka ila Shonaa alinipa ishara yaย kutulia kwanza kisha aliniambiaย
“Jojo aliyefanya hivi ni Sarafina, anakutafuta wewe una mzigoย wa Madini. Nenda mbali sana na Jiji hili vinginevyo utauwawa”ย Alisema Shonaa kwa shida sanaย
“Siwezi kukuacha Shonaa ukiwa katika hali hii ngojaย nikakuache Hospitali” Nilisema huku chozi likinibubujikaย
“Hapana huna muda Jojo, ondoka. Nikifa nitakufa nikiwaย nakupambania, Kimbia Jojo” Alisema Shonaa, Mwanga ukamulikaย dirishani, nikachungulia nikaona Watu wakija uelekea waย Chumba cha Shonaa.ย
Haraka nilimwambiaย
“Naenda Shonaa nakupenda” Niliielekea ilipo swichi ya Taa yaย nje, niliizima kukawa na giza kisha nikatoka haraka nikapitiaย mlango wa uwani nikakimbia eneo lile.ย
Nilikimbia sana Usiku ule huku nikiwa ninahofia kuhusuย usalama wa Shonaa maana alikuwa akivuja damu nyingi sana.ย
Nilichukua pikipiki nikamwmabia dereva anipeleke Ubungo,ย nilichotaka sasa kilikuwa ni kurudi Tabora tu. Hali ilikuwaย mbaya sana kwangu ndani ya Jiji la Dar, nilijiingiza kwenyeย janga zito sana ambalo lilihatarisha maisha yangu moja kwaย moja, nilijilaumu sana ni bora hata ningekubali kumaliziaย kifungo changu kule Gerezaniย
Tulipofika Ubungo nilikata tiketi kisha nilienda kulala ndaniย stendi karibu na gereji ndogo iliyokuwa ikitengeneza mabasi,ย nilijikunyata kama kifaranga cha kuku, nilimuomba Munguย aliyenisahau anikumbuke ili niweze kuondoka salama kuelekeaย kwetu Tabora maana hali ilizidi kuwa mbaya.ย
Sikupata Usingizi, madini yalikuwa kwenye mkoba wangu, zaidiย ya Bilioni 20 nilikuwa nimekaa nayo pale bila Mtu yeyote yuleย kujuwa kuwa nilikuwa na utajiri Mkubwa sana ambao ulkuwa naย uwezo wa kubadilisha maisha ya Watu wote walio stendi kwaย Usiku ule.ย
Baridi lilikuwa kali sana pale Ubungo lakini halikunizuiaย kuwa makini, gari niliyokata tiketi nilikuwa nikitazamanaย nayo macho. Alfajiri mapema sana nilikurupuka, pembeniย kulikuwa na bomba la Maji, nilifungulia nikapata kuosha usoย wangu ili kuondoa uchafu wa pale nilipokuwa nimekaa.
Macho yangu yalikuwa makali sana kuangalia huku na kule iliย nisije ingia mikononi mwa Watu wanaonitafuta, Picha yanguย ilikuwa imesambazwa kila kona ili nikionekana tu nikamatwe,ย Alfajiri hiyo nilienda kwanza kujisaidia kule chooni.ย Niliporudi niliona makundi ya Askari, hofu niliyonayoย ilinifanya nisimame sehemu ili kuangalia Askari wale walikuwaย wanafanya nini? Nilipoona wameenda mbali kidogo na nilipokuwaย naenda Mimi nilisogea kwenye gari, muda huo tayari walikuwaย wameruhusu Watu kuingia.ย
Sasa wakati naingia humo niliona picha yangu na ya Sarafinaย kuwa tunatafutwa atakayetuona atapata Donge nono, nilizibaย uso wangu nikashuka kwenye gari, nilirudi pale nilipokuwaย nimekaa usiku kucha.ย
Hofu ilinijaa upya, niliona kabisa safari ya Tabora inawezaย kufa tena, nikiwa naendelea kutafakari nilihisi kuguswaย kwenye bega langu. Nilipogeuka nilikutana na Mtu ambayeย alikuwa ana picha yangu, nahisi Mtu huyo alinihisi kuwa ndiyeย Mimi ila kutokana na giza alisemaย
“Samhani nilikufananisha” Alisema kisha alisonga mbele,ย nilitumia mkoba wangu kuficha sura yangu, nilionelea ni boraย nitoweke Ubungo maana kuendelea kuwa Ubungo kungenileteaย Shida kubwa sana, nilisogea geti dogo nikapita nikatokea njeย kabisa, kulikuwa na kigiza fulani hivyo ile hali ilinisaidiaย kujificha ili nisionekane.ย
Polisi walisambazwa kila kona ya Jiji na maeneo ya nje yaย Jiji kutusaka Mimi na Sarafina, kutokana na lile tangazoย nilijuwa wazi kuwa Sarafina alikuwa hajakamatwa. Madini badoย nilikuwa nayo kwenye pochi langu. Niliona ni bora nitembeeย kwa Mguu kuliko kupanda Usafiri maana tayari nilikuwaย natafutwa Nchi nzima na atakayeniona aliahidiwa kupewa zawadiย Nono.ย
ilikuwa ni safari ya Jojo na Madini yangu, nilitembea kamaย Kichaa nikiifuata barabara ya Morogoro, nilipoona Askariย nilichekupa na kuzama ndani kisha baadaye najitokeza naย kuendelea na safari, kulipo pambazuka nilinunua kofiaย nikaivaa angalau ilinisitiri kwa kiasi fulani.ย
Nilibakiwa na pesa kidogo sana ambayo hata isingenifikishaย Morogoro ila nilikuwa na mzigo wa madini yenye thamani yaย Bilioni 20 kwenye Mkoba wngu. Kila mara nilifungua naย kuangalia kama madini yalikuwepo, basi nilipojisikia njaa naย kuchoka nilienda sehemu nikanunua chakula ila sikula paleย nilienda kukaa chini ya Mti mmoja nikapata chakula. Maishaย yangu yalipoteza nuru ila kile kiasi cha madini kilinipaย nguvu ya kuzidi kusonga mbele, mida ya Jioni nilifika Kibahaย Maili moja miguu ikiwa haitamaniki ilikuwa ikiuma sana.ย
“Ooh Mungu nimechoka sasa” Nilisema nikiwa ninakaa kando yaย eneo la Mnada wa nguo, nilikaa hapo hadi giza lilipoingia.ย Chupi ilikuwa ikiniumiza kutokana na Uchafu wa kuivaa kutwaย nzima, kwasababu eneo lile lilikuwa giza basi niliondoa ileย chupi pale mnadani, pia kulikuwa na ronya za nguo ambazoย ziliachwa nilitafuta pensi nikavaa pia tisheti niliipataย nikaavaa na wala sikujali nitaonekanaje ila nilichotaka niย kwenda mbali na Jiji la Dar.ย
Sikutaka kupumzika Kibaha niliendelea mbele, Watuย niliopishana nao walikuwa wakiongea kuhusu Mimi kuiba Madiniย bila kujuwa waliokuwa wakimzungumzia walikuwa wakipishanaย naye.ย
Zile nguo nilienda kuzitupa kwenye daraja moja ambaloย lilikuwa linapitisha maji mengi kisha niliendelea na safariย yangu, gari za polisi zilikuwa zikipita kwa wingi kama vileย kulikuwa na msafara wa Rais wa Nchi kumbe ulikuwa ndio msakoย wangu na kwavile nilipita barabara ya vumbi nikiwa naitazamaย Barabara kuu kwa Mbali niliona jinsi msako ulivyokuwaย ukiendelea.ย
Nilipochoka nililala Kwenye kichaka fulani hadi asubuhi kishaย safari iliendelea, kadiri nilivyokuwa natoka nje ya Jijiย ndivyo nilivyoanza kuhisi kuwa tayari nimejikwamua kutokaย kwenye msako ule mkali, Nilichofikiria sasa kilikuwa niย madini na pesa nitakayoipata.ย
Pesa ilikuwa imeniishia kabisa, nilipofika mbele kidogoย niliona sonara ndogo. Nilikaa sehemu nikapekua yale madiniย nikatafuta dini dogo sana yaani kakipande fulani tu ambachoย nilihisi kuwa pesa yake isingekuwa kubwa sana, niliingia humoย ili niuze. Nilijitahidi sana kukwepa macho ya Mtu wa Sonaraย
Nilimpa lile dini, kwanza alishtuka sana maana lilikuwa niย dini lenye thamani kubwa tofauti na nilivyofikiria, alilipimaย na kugundua kuwa lilikuwa lenyewe siyo feki kisha aliniambiaย
“Dada yangu pesa sina, hili nenda kauze Kwa wale wenye Sonaraย kubwa kabisa” Alikuwa Kijana mmoja wa Kipembaย
“Linagharimu shilingi ngapi?” Nilimuuliza maana nilikuwaย sijui kuhusu Madiniย
“Hili siyo chini ya Milioni 45 ndiyo maana nasema sina helaย ya kukupa” Alijibu yule jamaa, sasa nilifikiria niende hukoย anakosema nilihisi nitakamatwa nikamwambia
“Wewe nipe uliyonayo, ukiuza nitakuja kuchukua hela kwako”ย Nilisema kama vile mzoefu wa hiyo Biashara.ย
“Alivyoskia hivyo alihangaika akafungua droo akatoa milioniย mbili akaniambiaย
“Ipo hii ila nakuhakikishia hadi kufikia jioni litakuwaย limeuzika, tena nitaenda Mjini kuliuza” Alisema.ย
Sikumjibu nilichukua zile pesa nikazitia kwenye Mkoba bilaย hata kuhesabuย
“Ungezihesabu kwanza Dada yangu”ย
“hata Usijali nakuamini” Nilisema kisha niliondoka pale,ย Kumbe nyuma yule Dogo alipiga simu sehemu ambapo angeuza hiloย dini, sasa taarifa zangu zilikuwa zimesambazwa kwa Wauzaย madini nchi nzima, yule jamaa aliambiwa anikamate.ย
Ile anatoka nje tu Mimi ndiyo kwanza nilikuwa nitoka naย Bodaboda, nilipogeuka nilimuona akihangaika kujuwa nimeelekeaย wapi, ni wazi alikuwa hajaniona. Nilimwambia dereva aingieย njia nyingine ili asionione kabisa, kweli dereva alinipitishaย njia nyingine tukaenda kutokea Barabara Kuu.ย
Nilimlipa kisha nilichukua Pikipiki nyingine nikamwambiaย anisogeze mbele kwa kutumia njia za vumbi za Shoti kati,ย mbele ya pesa kila kitu kiliwezekana hadi nilifika Mbeleย zaidi, nikapanda gari ndogo ya abiria hadi Chalinze. Hapoย ย nilikodi Pikipiki inifikishe Morogoro.ย
Nilifika Morogoro mishale ya saa 10 Jioni, nilitafuta gest yaย vichochoroni nikala kisha nikalala zangu bila hata hofu kuwaย ninatembea na mzigo mkubwa wa Madini. Hofu yangu ilikuwa kwaย polisi pekee, nikiwa hapo nilipata kuona taarifa ya Habariย kuwa Sarafina na Mkuu wa Magereza walikuwa wamekatwa baada yaย Sarafina kumtaja Mkuu huyo, Sasa kupitia kamera za Kuleย Hotelini siku ya tukio la kuiba madini sura yangu ilionekanaย nikawa natafutwa Kila kona huku akina Sarafina wakiwa kwenyeย mikono ya Polisi, kilichotakiwa kilikuwa ni Madini ya yuleย Bilionea.ย
Nilizima TV ili nisiendelee kuangalia habari hiyo, Nililalaย hadi Asubuhi, Mapema sana nilianza safari ya kuelekea Taboraย kwa kutumia Basi. Nilifika Tabora usiku sana, nilichukuaย pikipiki hadi nyumbani kwetu, Nilimgongeshea mlango Mamaย Rafia ambaye ndiye jirani yetu kule Tabora nikamwambia
“Nifungulie tafadhali Mama Rafia” Nilisema nikiwa bado ninaย hofu ya kukamatwa, Mama Rafia alifungua kisha aliniulizaย
“Kulikoni Jojo? taarifa zako zimeenea kila kona, Tobra nzima,ย imekuwaje Mwanangu” Alisema Mama Rafia,,ย
“Mama laiti kama ningelijuwa nisingelienda Dar, Maisha yanguย yameharibika baada ya kufika huko” Nilisemaย
“Ni kweli umeiba Madini Mwanangu?” aliniuliza, alikuwa niย jirani pia rafiki wa Marehemu Mama yangu, nisingeliwezaย kumficha. Nilimwambia ukweli na nilimuonesha madiniย
Tuliingia ndani kwake maana alikuwa akiishi peke yake kishaย alinielezaย
“Msonjo amekamatwa Jana Mchana, inasemekana kuwa yeyeย anahusika na anajuwa ulipo”ย
“Hapana Mama, Msonjo sijawasiliana naye kwa zaidi ya mieziย yote niliyokuwa Dar, nimepata mitihani mikubwa sana Mama”ย Nilisemaย
“Sasa Jojo, haya Madini ni mali ya Watu hivyo muda wowoteย unaweza kukamatwa, kuliko ukamatwe kwa kosa dogo ni boraย ukamatwe kwa kosa kubwa” Alisema Mama Rafiaย
“Unamaanisha nini Mama”ย
“Yafiche kiasi alafu mengine kaa nayo ili ukikamatwaย uyaoneshe! utakapotoka huko utajuwa pa kuanzia” Alisema Mamaย Rafia, nilimuamini yeye hivyo nilimpa kiasi cha Madini kishaย mengine niliondoka nayo usiku huo na kwenda nyumbani.ย
Asubuhi Mapema Mlango uligongwa, Sauti ya Mama Rafiaย niliisikia.ย
“Nakuja Mama” Nilisema, kisha nilivaa vizuri maana nilikuwaย nimelala. Nilipofungua mlango nilikutana na Askari wakiwaย wameongozana na Mama Rafiaย
“Huyu hapa!! kiukweli Askari Mimi sitaki Matatizo kabisa,ย huyu Binti anayo hayo madini yanayotafutwa” Alisema Mamaย Rafia, kiukweli nilipigwa na Butwaaย
“Mamaaa”ย
“Siyo Mama, kiukweli Jojo sitaki matatizo na Mtu ndiyo maanaย nimewaambia polisi, ningekaa kimya ningekuja kukamatwa naย Mimi” Wale Polisi waliingia ndani wakachukua mkoba wenyeย Madini, Chozi lilinibubujika sana.ย
“Basi Mama nipe yale madini niliyokupa ili tumrudishieย mwenyewe” Nilisema huku chozi likinivujaย
“Madini? kuna madini uliyonipa Mimi Jojo? ndiyo maanaย niliyakataa mapema haya nikaamuwa kusema kwa polisi” Masikiniย nililia sana Aisee, Mama Rafia alinikana mbele ya Waleย askari. Nilikamatwa kisha nilirudishwa Darย
Nikiwa kituo cha polisi nilikutana na Sarafina na yule Mkuuย wa Magereza pia nilikutanishwa na Biliona niliyemuibiaย Madini. Alihakiki madini akaona hayajatimia hivyo niliteswaย sana ili niseme yalipo, nilimtaja Mama Rafia ila alinikataaย mbele ya Askari, Tulipelekwa mahakamani kila mmoja na kosaย lake, Mimi nilikuwa na kesi ya wizi wa Madini, Sarafinaย alihusika na kifo cha Shonaa pia kupanga njama ya wizi waย madini, Mkuu wa Magereza alikuwa na kesi nzito zilizoihusuย magereza yake, kifo cha Shonaa na Njama za kuiba Madini.ย
Binafsi nilihukumiwa kwenda jela Miaka Mitamo, Sarafinaย alienda jela miaka 25, Mkuu wa Magereza alifungwa kifungo chaย Maisha Jela sababu alikutwa na kesi nyingi za mauwaji.ย
Kila mmoja alipelekwa Gereza lake kutumikia adhabu.ย Nilimpoteza Mama yangu, Nilimpoteza Shonaa, Nilipotezaย thamani yangu, pia nilimpoteza Mama Rafia kisa Madini. Sikuย moja nilitembelewa na Msonjo nikiwa gerezani aliniambia kuwaย Mama Rafia amejenga jumba la kifahari, ana Biashara nyingiย anafanya tena ameahama kabisa Tabora anaishi zake Dodoma.ย
“Msomjo Mimi Mungu amenisahau” Lilikuwa ndiyo neno langu laย Mwisho kulisema, sikuhitaji kuonana na Mtu mwingine tena.ย Hadi sasa unaposoma hadithi hii Mimi ninatumikia adhabu mwakaย wa 8.ย
MWISHO
Mwisho wa HADITHI Hii Ndio Mwanzo Wa HADITHI NYINGINE…. Kukiwa na COMMENTS Nyingi Mpya Inaanza Mapema Tu
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xxย ย Mungu Amenisahau xxย ย Mungu Amenisahau xxย ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xx ย Mungu Amenisahau xxย
ย ย
12 Comments
Jamani, tamthiliya nzuri, natamani ingeendelea
Duh jojo Hattari kweli kweli
๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Mh ivi mnatunga tu au mnaiba maana hii ni mfano wa AI
Heeee
Hongera sana admin kwa kweli inasisimua sana๐ญhadi kusoma unaogoa๐ข
Mwisho wa riwaya hii ndio mwanzo mzuri๐นwa riwaya nyengine
Kila lenye kheir liwe kwako ni nzur san hii riwayaโ๏ธ๐ฏ
Nimelia saaana๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ
Darasa la Saba
Kuna cha kujifunza hapa wanakijiwe
Asante sana ndugu admin ๐๐ป๐๐ป
0yjh7u
g6z02b