Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Saba

Vishindo vya miguu vilikoma kwenye mlango wa Chumba nilichopo  kisha funguo ilianza kufungua kitasa taratibu, nilifumba  macho yangu ili nisione kitakacho fanyika pale, niliivuta ile  chupa sawa sawa, mlango ulipofunguliwa nikawa nyuma ya  Mlango, niliposikia akitembea kuingia ndani basi nikaiachia  ile chupa nikiwa nimefumba macho yangu ikatua kwenye kichwa  chake, nikasikia sauti iliyoshindwa kutoka sawa sawa kisha  nilisikia kitu kikianguka kama mzigo, Yes! nilikuwa nimelenga  shabaha yangu vizuri, ikabidi sasa nifumbue macho yangu. Endelea 

SEHEMU YA NANE

Kumbe wakati Jonas ananitafuta mimi, Anko Sanga na Mama  walikuwa wakimfwatilia pia wakiamini ndio tatizo kwenye  mipango yao, kupitia simu ya Konzo aliyonipigia walifanikiwa  kumkamata Konzo, walimtumia kama Mtego ili wamnase Jonas. 

Mama nae alikuwa akiishi nje ya Mji kama ambavyo Anko Sanga  alikuwa akiishi tena kwenye jumba la kifahari sana,  walimchukua Konzo na kwenda nae huko nje ya mji ambako Mama  alikuwa akiishi. Konzo alilazimishwa kuwa mtego wa kumnasa  Jonas ambaye kwa kipindi hicho alikuwa Ndani ya Jiji la  Arusha kunitafuta mimi na Mtoto. 

Konzo alifanya kama ambavyo alilazimishwa, alimpigia simu  Jonas wakutane nje ya Mji akimwambia kuwa ana taarifa  zinazonihusu, hivyo wakafanikiwa kumpata Jonas, walitumia  nguvu zao za kishirikina na kuwapumbaza Konzo na Jonas, Mama  akamchukua Konzo na kwenda kumtupa huko Porini, Jonas  akamfanya kuwa Mwanaume wake. 

Hivyo, Jonas na Mama yangu Mzazi wakawa wanaishi kama Mume na  Mke kama ambavyo Mimi na Anko Sanga tulikuwa tukiishi, wazo  la Jonas la kunitafuta lilifutika kabisa akawa mtumwa kwenye  penzi la Mama yangu, walifanya hivi ili waendelee kuvuna pesa  na kuishi maisha ya kitajiri, mimi ndio nilikuwa mtaji wao  Mkubwa. 

Hakukuwa na Mtu mwingine ambaye angeliweza kunikomboa au  kumkomboa Jonas kutoka kwa Mama yangu, ushetani wao ulikuwa  mbaya sana, tamaa ya pesa iliwafanya wageuke kuwa Wanyama. 

NYUMBANI KWA ANKO SANGA 

Nilikuwa nikihema juu juu kama Mbwa aliyepona kutoka kwenye  umauti, chupa kilikuwa sakafuni kikiwa kimevunjika, woga  ulinijaa na kilichonishangaza zaidi ni Mtu aliye chini pale,  nilimgeuza. 

Hakuwa Anko Sanga bali ni dereva wake aliyeitwa James, ndiye  aliyekuwa akimtuma mara nyingi aje nyumbani anapokuwa  amesafiri 

“OHHH! Mungu wangu” nilisema nikiwa nimeweka Kiganja changu  mdomoni wakati mkono mwingine ukiwa kichwani, nilianza  kumuamsha James ili aamke maana kama Anko Sanga atakuja  akimuona James yupo katika hali ile pengine angenifungia  kabisa chumbani, nilimwamsha kwa muda mrefu lakini hakuamka,  nilianza kuhofia kwa kujua nimemuuwa.

Nilienda dirishani kuchungulia kama Anko Sanga alikuwa akija  au Mtu nwingine yeyote lakini hakukuwa hata na dalili ya Mtu  kuja pale nyumbani. Nilimburuza James hadi bafuni, nilirudi  na kufuta damu iliyokuwa sakafuni, niliondoa vipande vya  vyupa pale sakafuni kisha nilienda bafuni. 

Nilimmwagia maji ya baridi ili aamke, sikuwa na tatizo na  James kabisa, alikuwa akiongea na mimi vizuri hivyo  kumsababishia umauti lilikuwa jambo baya kwangu, ndipo  nilipogundua kuwa James alikuwa amepoteza maisha. 

Niliwaza nifanye nini, nikapata wazo la kutoroka pale ndani,  sijui hata nilikuwa nikichelewa nini wakati lengo langu miaka  yote nitoroke, leo nilikuwa nimeipata hiyo nafasi. Nilikuwa  ninevalia pajama la kulalia, nilimpapasa James na kuchukua  rundo la funguo, sasa mtiti ulikuwa ni kufahamu funguo  zilikuwa zikifungua wapi na wapi maana zilikuwa nyingi. 

Nilirudi haraka kule chumbani ambako nilimpiga chupa James,  kisha nilichungulia dirishani bado hali ilikuwa shwari kabisa  nikaona ndio wakati wangu wa kwenda kukomboa maisha yangu na  ya binti yangu Moyo. 

Nilianza kufungua milango ya ile nyumba, nilikuwa  nikihangaika na kuchukua muda mrefu kufungua mlango mmoja,  yaani nilijawa na woga kupitiliza, mikono ilikuwa ikikosa  nguvu hadi nilikuwa nikidondosha funguo mara kadhaa,  nilifanikiwa kufungua milango miwili ambayo James alipokuwa  akiingia alifungua na kuifunga. 

Wakati namalizia mlango wa mwisho nilisikia mlio wa gari,  ilinibidi nirudi chumbani kuchungulia dirishani maana kile  ndio chumba pekee kilichokuwa kikionyesha sehemu ya mbele  yaani geti na barabara, nilimuona Anko Sanga akishuka kwenye  gari, alienda kuangalia gari yake Rav4 kisha alichukua simu  na kupiga, niliisikia ikiita bafuni, ilikuwa ni simu ya James 

Haraka nilikimbilia bafuni na kuichukua simu ya James,  ilipomaliza kuita niliizima kisha niliipeleka kwenye chumba  kingine, nikaweka mazingira ya Bafu vizuri, maana niliupeleka  mwili wa James kwenye chumba kingine ambacho kilikuwa na bafu  ndani. Haraka nilikimbilia mlangoni na kufunga milango yote,  wakati huo Anko Sanga alikuwa akipandisha ngazi kuja juu.  Nilielekea bafuni kuzuga, nilianza kuoga ili tu kutengeneza  mazingira wakati huo mwili wa James ukiwa kwenye chumba  kingine kabisa tena chumba ambacho kilikuwa hakilaliwi na  Mtu. 

“James yuko wapi?” aliingia hadi bafuni na kuniuliza

“Sijamuona” nilimjibu kwa mkato tu, bado nilikuwa na kisirani  nae kwa kitendo cha kumchukua Binti yangu Moyo 

“Hujamuona wakati gari iko pale nje? nilimtuma mzigo chumbani  kwangu,” 

“Sasa sijamuona nikwambie nimemwona?” 

“Oky!” alielekea chumbani akiwa na funguo za ziada, zile  funguo zingine nilikuwa nazo mimi sikutaka kabisa kuziachia. 

Alipofika chumbani alianza kupatwa na wasiwasi alipiga tena  simu ya James haikupatikana na kibaya zaidi viatu vya James  vilikuwa pale nje, akarudi tena kwangu akiwa na sura ya  kikauzu! 

“James yupo wapi?” aliniuliza lakini nilimkatalia kabisa,  moyoni nilijua kuwa James alikuwa amekufa 

“Sijamuona akiingia humu ndani” nilimjibu, kilichokuwa  kinampa tumaini ni milango kuikuta ikiwa imefungwa vilevile,  alinitazama kisha alinifungia chumbani, wakati huu nilikuwa  nimemaliza kuoga na nilikuwa na zile funguo. 

Nilimsikia akifunga milango kisha aliondoka zake, chumba  nilichokuwa nimefungiwa hakikunipa nafasi ya kumuona akiwa  anatoka getini, ghafla akarudi na kufungua mlango, nilimuona  akivua nguo zake na kubakia kama alivyozaliwa nilijua tu  alitaka penzi, nilimvulia nguo akanifanya hadi alipomaliza  kisha aliondoka zake. 

Nilirudi bafuni kuoga, kisha nilianza harakati za kutaka  kutoroka pale ndani, nilichukua funguo mahali ambapo nilikuwa  nimezificha kisha nilivaa nguo sikuhitaji hata begi lolote  maana ile nafasi pekee niliitafuta kwa kitambo sana. 

Nilifungua milango haraka haraka ili niweze kutoroka pale  nyumbani kwa Anko Sanga, nilifanikiwa kufungua milango yote  hadi wa mwisho ambao ndio ulikuwa ukitazamana na geti kubwa  la kutoka pale kwa Anko Sanga. 

Niliitazama ile nyumba jinsi ilivyogeuka kuwa jela ya Mateso  kwa zaidi ya Miaka mitatu, nilijikuta nikiangusha chozi.  Mateso niliyoyapata pale hayakupata kuelezeka kabisa, moyo  wangu uliteketea kwa maumivu makali zaidi hata ya sindano  izamapo ndani ya jicho, nilipiga magoti nikiwa ninalia. 

Katika hali isiyo ya kufikirika nilihisi kuguswa kwenye bega  langu, hali ya kulia ilikata mara moja huku kiu ya kumjua aliyenishika bega alikuwa nani ilinijia, nilipogeuka  nilikutana na sura kavu ya Anko Sanga ikiwa inanitazama,  wakati namtazama nilijisemea kuwa sitakiwi kuichezea ile  nafasi, nilijifanya naendelea kujawa na woga huku nikimlia  taiming jinsi ya kumkwepa pale ili niweze kutoroka! 

Hesabu zangu zilienda sawa kabisa, alipokuwa akinisogelea  niliachia teke hadi kwenye zizi lake, akaanza kulalamika huku  akiwa amejishika, nilijua ile sehemu ingemsababishia maumivu  ambayo yangenifanya nikimbie haraka kuelekea getini ili  niweze kutoka nje kabisa ya ile nyumba. 

Nilimtazama jinsi alivyokuwa akiugulia maumivu makali ambayo  yalimpeleka hadi chini, akawa ana galagala chini huku akipiga  ukunga wa maumivu. Nilimeza mate kisha nilitoka mbio kuelekea  getini, wakati niko bize pale kufungua geti nilihisi ubaridi  sehemu ya shingo, ghafla maumivu makali yaliyoambata na  kuishiwa nguvu yalianza, nilijikuta nikilegea. 

Nilijitahidi kujishikiza kwenye lile geti ili nisidondoke,  giza zito liliyakumba macho yangu, nilianza kupoteza uwezo wa  kufikiria, nilijikuta hata uwezo wa kusikia ukipotea. Nguvu  kidogo iliyobakia niliitumia kugeuka nyuma, kwa nuru kidogo  ilibakia ndani ya macho yangu nilifanikiwa kumuona Mama yangu  Mzazi, kabla sijapoteza ufahamu wangu nilifanikiwa kugundua  kuwa Mama yangu ndiye aliyesababisha niwe katika hali ile,  mkononi alishikilia kipande cha Mti, Palepale nilidondoka na  kupoteza fahamu zangu! 

Nikiwa kwenye giza zito ndani ya ufahamu wangu nilimkumbuka  Mwanangu Moyo, sikujua Mtoto wangu alikuwa wapi licha ya Anko  Sanga kusema alikuwa kwa Mama yangu, nilihisi uwepo wa Jonas  mbele ya Macho yangu, nilijikuta nikitabasamu!! Ubaridi  ulinifanya nirudishe ufahamu wangu ulionitoroka kwa takribani  masaa matatu. 

Niliiona Sura ya Anko Sanga na Mama yangu wakiwa  wananitazama, sura zao zilijaa uzito wa hali ya juu, pale  pale nikakumbuka kilichotokea masaa kadhaa yaliyopita,  nilijikusanya na kuketi, wakati nakaa vizuri nilihisi kugusa  kitu na nilipogeuka niliuona mwili wa James pale Sakafuni.  Nilianza kufikiria nje ya Box 

“Veronica huwezi kutoroka hapa, hilo kamwe haliwezi kutokea!  Wewe ni adhina muhimu sana kwetu istoshe tuna Mtoto wako,  nadhani huwezi kufanya upuuzi wowote ule kwani kwa kufanya  hivyo utamuacha Binti yako mikononi mwetu” Yalikuwa ni maneno  makali ya Anko Sanga, maneno haya yaliibua hisia nzito sana,  yalinifanya nianze kutokwa na machozi.

“Kwasababu ulitaka kutoroka hapa, nakupa adhabu ya kuishi na  maiti ya James, nilijuwa uwepo wa jambo hili nilipoingia  bafuni na kuuona mwili wa James, hivyo niliweka mtego  makusudi ili nikunase” Aliongeza 

“Mama! Mama! Umenizaa wewe mwenyewe kweli? Unyama gani huu  unanifanyia Veronica wako? Ulinizaa peke yangu na huna binti  mwingine” Nilisema nikiwa ninalia, nilikuwa nimejikunyata,  tatizo kwangu halikuwa Anko Sanga bali ni Mama yangu Mzazi,  nilijiuliza alikuwa ameingiwa na shetani gani hadi anifanyie  yote yale? 

“Nisingekuzaa nisingefanya hivi, kwani Wazazi wako wangepiga  sana kelele…leo nimeamua kufanya kwasababu hakuna wa kupiga  kelele” 

Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TISA

JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

36 Comments

Leave A Reply

Exit mobile version