Ilipoishia “Ndani ya masaa matano Desmond alifanikiwa kufika KijijiniΒ hapo.Β
Alikijua vizuri kijiji hicho sababu yeye ndiye aliyemfuataΒ Sanga akawe mfanyakazi, alivalia kofia kisha alishuka kwenyeΒ gari yake, mbele aliona gari yenye nembo ya polisi hivyoΒ alitambuwa fika kuwa polisi walikuwa wameshafika eneo hilo,Β alijitahidi kutembea kwa tahadhari huku macho yake yakiangazaΒ huku na kule, bahati ilioje kabla hata hajafika nyumbaniΒ anakoishi Sanga alimuona Sanga akiwa amejificha sehemu,Β hapana shaka hata Sanga alihitaji kuwakwepa askari hao. MachoΒ ya Sanga na Desmond yaligongana kisha haraka Desmond aliendaΒ hadi alipojificha SangaΒ
“Umefanya nini Sanga?” Alihoji Desmond akiwa amejificha hapo na Sanga.Β EndeleaΒ Β
SEHEMU YA TATUΒ
“Ndiyo Desmond! Uchunguzi unaendelea hivyo ni lazima tutoeΒ taarifa kila hatua” Alieleza askari huyo kwa njia ya simu,Β Desmond alitamani kumwambia Askari huyo asirushe chochoteΒ lakini alishindwa sababu angeulizwa kwanini anataka taarifaΒ zisiruke alafu angekosa jibu la kumpa, alikata simuΒ akairudisha kwenye mfuko wake.Β
Siku zilienda, Desmond na Noela walipanga kuvishana pete yaΒ uchumba ili mahusiano yao yatambulike, japo Desmond alikuwaΒ na Mke tena aliyefunga naye ndoa kanisani ila hakutaka kusemaΒ chochote kile, akili yake ilizidi kumwambia kuwa MandyΒ atakufa muda wowote ule, walipanga siku ya tukio hilo, hofuΒ ya Desmond ikawa kwa Lucia kama atapewa hiyo taarifa alafuΒ akahudhuria sherehe hiyo fupi ya kuvishana pete na kamaΒ unavyojuwa Lucia alikuwa akifahamu kuwa Desmond ana Mke tenaΒ yupo Hoi Hospitalini.Β
Miongoni mwa Watu ambao Noela aliwaarika alikuwa ni LuciaΒ sababu alikuwa ni rafki yake wa zamani, Desmond alimwambiaΒ Noela hana sababu ya kuarika Watu wengi hivyo sababu niΒ sherehe fupi ambayo inawahusu wao na baadhi ya ndugu.Β
“Sijawahi kuvishwa pete katika Maisha yangu Joshua, weweΒ ndiye Mwanaume wangu wa kwanza kunipeleka kwenye ulimwenguΒ huu hivyo ni fahari kwangu kuona marafiki zangu wanakujaΒ hapa” Alisema Noela siku moja baada ya Desmond kulalamikaΒ kuwa anaarika Watu wengi.Β
“Najuwa Mpenzi wangu lakini tukio hili ni la kushuhudiwa naΒ Watu wachache sana, Aaah…” Alisema Desmond huku badoΒ akitafunwa na hofu ya Lucia kuarikwaΒ
“Joshua nimearika marafiki wachache sana, usiwe na wasiwasiΒ kuhusu hilo. Nakuelewa Mume wangu mtarajiwa” Alisema NoelaΒ kisha alisema
“Naenda chooni mara moja” Aliaga kisha aliondoka lakiniΒ aliacha Kitabu chenye majina ya Watu walioarikwa kwenyeΒ shughuli hiyo, haraka Desmond alikifunua, kama alivyofikiriaΒ ndivyo ilivyokuwa, Lucia aliarikwa kwemye shughuli hiyo, jinaΒ lake lilikuwa la tatu kutoka juu akimaanisha kuwa ni miongoniΒ mwa Watu muhimu zaidi kwake, kijasho kilimtoka Desmond,Β alifikiria haraka haraka afanye nini ili kumzuia LuciaΒ asiende kwenye tukio hilo la kuvishana pete maana kama LuciaΒ ataenda basi mambo mawili yatajulikana, kwanza ni jina lakeΒ halisi ambalo siyo Joshua na pili ni kwamba ana Mke hivyoΒ haruhusiwi kuowa Mke mwingine kwa mujibu wa sheria za dini yaΒ Kikristo.Β
Walikuwa kwenye moja ya Bustani nzuri wakizungumza, DesmondΒ alikaa kwenye kiti akiwa amechoka mwili na akili, akakumbukaΒ Maswali aliyoulizwa na Lucia juu ya jaribio la kutaka kuuawaΒ kwa Mandy, moja kwa moja alijuwa mambo mengi yanaendaΒ kujulikana kama ataruhusu Lucia kuwepo kwenye Shughuli hiyo,Β akiwa anaendelea na tafakari Noela alirudi akamkuta DesmondΒ akiwa katika hali ya mawazo sanaΒ
“Kulikoni Bebe?” Alihoji, kijasho kilikuwa kikimtoka Desmond,Β Noela alimpa kitambaa Desmond ili ajifute jashoΒ
“Unaumwa?” Aliuliza tena NoelaΒ
“Ndiyo ghafla tu sijisikii vizuri, usijali nitakuwa sawa”Β Alisema Desmond kisha alijifuta jasho alafu akashushia majiΒ ya baridi, Noela aliketi, aliona kitabu kimefunguliwaΒ
“Au kwasababu umeona nimearika idadi kubwa ya Watu Joshua?”Β Aliuliza Noela akiwa mwenye wasiwasi huwenda Desmond anaΒ hasiraΒ
“Hapana Noela ni tofauti na ufikiriavyo, ni ghafla tuΒ najisikia vibaya” Alisema Desmond, Noela alisemaΒ
“Ngoja nimpigie rafiki yangu ni nesi”Β
“Rafiki yako nesi?” Alihoji Desmond akiwa katika hali tofautiΒ kabisa hata Noela alishangaa maana Mtu ambaye alionekana kuwaΒ na hali mbayaΒ
“Mbona umeshtuka sana niliposema nampigia rafiki yangu nesi?Β Si wewe ulikuwa katika hali ya homa?” Kiukweli Noela alizidiΒ kumshangaa DesmondΒ
“Hukuwahi kuniambia kama una rafiki yako Nesi” AlisemaΒ Desmond, Noela alitabasamu akagundua ni kweli hakuwahiΒ
kumwambia Desmond istoshe alikutana na rafiki yake huyo sikuΒ chache zilizopitaΒ
“Oooh ni kweli, ni rafiki niliyesoma naye. Tulipotezana mudaΒ mrefu sana ni majuzi tu ndiyo tumeonana. Hata hivyoΒ nimemuarika kwenye shughuli yetu lakini nakumbuka kamaΒ niliwahi kukwambia, atakuja utamuona anaitwa Lucia” AlielezaΒ Noela kisha alimpigia Lucia lakini kabla hata simu haijaitaΒ Desmond alimkatisha NoelaΒ
“Huna haja ya kumsumbua nitakuwa sawa tu” Alisema DesmondΒ huku akitafakari kuhusu Lucia, aliona wazi vita kubwa inaendaΒ kupigwana mbeleniΒ
“Hivi unajua Joshua sikuelewi, unatokwa jasho namna hiyo lafuΒ hutaki nimuite Lucia?” Aliuliza NoelaΒ
“Nimesema nitakuwa sawa, tunaweza ondoka hapa” AlisemaΒ Desmond kisha alisimama, Noela naye alisimama japo kwaΒ kuchukia kisha waliongozana hadi kwenye gari ya Desmond,Β walianza safari ya kuondoka pale kuelekea nyumbani anakoishiΒ Noela, baada ya kumaliza mizunguko yote alirudi kwenye nyumbaΒ aliyokuwa akiishi na Mandy.Β
Kuna dokumenti alizihitaji akaenda kufungua kabati la MandyΒ ambalo alikuwa akiweka baadhi ya vitu vyake muhimu kishaΒ alitoa Mkataba wenye umiliki wa Mali za Mandy yakiwemoΒ Mashamba, kampuni ya Kuuza Vipuri vya Magari na Mgodi mmoja.Β
Alipozipata nyaraka hizo muhimu alizipitia, alithibitishaΒ ndizo alizokuwa akizihitaji kwa wakati huo, kisha alimpigiaΒ Mtu mmoja simu akasemaΒ
“Joel ninazo, nakuja ofisini kwako” Alisema Desmond kishaΒ alikata simu, aliingia kwenye gari akaelekea kwa Joel ambayeΒ alikuwa ni Mwanasheria wa Mandy.Β
Alifika ofisini kwa Mwanasheria huyo aliyeitwa Joel, alikuwaΒ ni Mtu makini aliyefahamu kilichotokea kati ya Mandy na MumeΒ wake Desmond, walitazmana huku nafsi zao zikizungumza,Β walionesha kujuwa hasa walichodhamiria kufanya. HarakaΒ Desmond alizama kwenye mkoba wake akatoa zile nyaraka muhimuΒ za Mandy.Β
Joel aliketi akazipitia kisha akamwambia Desmond baada yaΒ dakika kadhaa za ukimya kupitaΒ
“Ni zenyewe” Alisema hivyo huku akizidi kutafakari jambo,Β Desmond aligundua kisha akamuuliza
“Unafikiria nini Joel?” Alimuuliza Mwanaume huyo mweupeΒ mwenye mvi kiasi ambaye umri wake ulienda kidogoΒ
“Nafikiria kuhusu Mandy, tunachofanya ni kumzika akiwa hai,Β nakumbuka mengi ya zamani” Alisema Joel huku akifuta choziΒ jicho mojaΒ
“Wewe ni mshamba sana Joel, hukuzaliwa kuwa masikini. HuoniΒ aibu? Huhisi haya machoni pako? Mwaga wino hatukuanza leo”Β Alisistiza Desmond huku akizidi kumshangaa Joel, basi JoelΒ alichukua peni akaiweka juu ya nyaraka hizo akamwambiaΒ DesmondΒ
“Hiki ninachokifanya kinaenda kubadili kila kitu katikaΒ Maisha yangu, uadilifu na uaminifu wangu kwa Mandy unazikwaΒ baada ya kutia saini nyaraka hizi Desmond. Natamani kurudiΒ nyuma na kuzuia hili lisitokee” Alisema Joel huku akizidiΒ kujilaumuΒ
“Mandy ni wa leo wa kesho, unataka afe ili nihangaike naΒ familia yake si ndiyo?” Alisema Desmond kisha alimlazimishaΒ Joel kutia saini ya makubaliano kuwa Mandy amempa mali hizoΒ Mume wake Desmond, kwa Mamlaka aliyonayo Joel alitia sainiΒ
“Ooooh!! Sasa umefanya kwa upande wako, kilichobakia ni kuleΒ Hospitali, twende tukamalize mchezo” Alisema Desmond kishaΒ alisimamaΒ
“Desmond una uhakika kuwa Mandy atakufa?” Joel aliulizaΒ
“Asipokufa atakuwa na mapungufu kwenye ubongo wake, ni lazimaΒ atapoteza kumbukumbu tu” Alisema Desmond kwa kujiaminiΒ
“Baada ya hapa nitakupatia kiasi kikubwa cha pesa kishaΒ utakuwa na jukumu la kuitunza siri hii” Alisema Desmond kishaΒ walitoka wakaelekea kule Hospitalini.Β
Walipofika walimkuta Lucia akiendelea kumuangalia Mandy maanaΒ ndiyo jukumu lake kuu alilopewa, Lucia aliwatazama Desmond naΒ Joel Mwanasheria.Β
“Samahani Lucia kuna jambo Mwanasheria wa Mandy amekujaΒ kufanya” Alisema Desmond, Lucia alishtuka akamuuliza DesmondΒ
“Unahisi Mandy hatoweza kuamka?” Alihoji akiwa kama muuguziΒ namba moja wa Mandy, alihisi kuna jambo lisilo la kawaidaΒ ndiyo maana Mwanasheria huyo alienda Hospitalini. DesmondΒ alimvuta pembeni Lucia akamwambia
“Siyo kila jambo linaendeshwa kimihemko Lucia, mambo mengineΒ unapaswa kuyaangalia tu. Wewe ni nesi na utabakia kuwa nesi”Β Alisema Desmond kwa sauti iliyojaa ukomavu huku akiwaΒ amemshika mkono kwa nguvu LuciaΒ
“Hata kama Desmond, nimemungalia Mke wako kwa kipindi kirefu.Β Lipo tumaini ndani yake, kuwa na subra” Alijibu LuciaΒ
“Unajuwa nini wewe Lucia? Unajuwa nini kuhusu familia yangu!?Β Kumuuguza Mandy ni jukumu lako sababu unalipwa msharahaΒ hufamyi bure hapa” Alisema Desmond kwa sauti ile ileΒ
“Desmond! Desmond vuta subra Mkeo ataamka tena” Alisema LuciaΒ akionesha kuumizwa sana, mara nyingi Mtu anapokuwa mgonjwaΒ sana alafu Mwanasheria akaja basi kunakuwa na uwezekanoΒ Mkubwa sana kuwa kuna mjadala wa mali za mgonjwa, LuciaΒ aliligundua hiloΒ
Basi Desmond na Lucia walirudi huku Lucia akitaka kusema kituΒ lakini Desmond hakutaka kumsikiliza Lucia, Mwanasheria JoelΒ alitoa wino kisha alipakaza kwenye kidole cha Mandy. AkawekaΒ saini kwenye zile karatasi, Desmond alikabidhiwa karatasiΒ hizo kisha alizisoma tena, Lucia alichungulia kuona kulikuwaΒ kumeandikwa kitu gani kwenye karatasi hizo.Β
Aliona maandishi yaliyosomekaΒ
“MAKABIDHIANO YA MALI KATOKA KWA MANDY KWENDA KWA DESMOND”Β
Alishtuka sana Lucia, alimtazama mara mbili mbili Desmond,Β jinsi alivyokuwa amemchukulia Mwanzo aliona kabisaΒ alimchukulia tofauti kabisa kwa jinsi alivyo sasa, alimuonaΒ Desmond kuwa ni mkatili na jambo ambalo alikuwa analifanyaΒ pale lilijaa tamaa za kutosha, alishindwa hata aseme nini.Β Baada ya kumaliza Desmond na Mwanasheria Joel waliondokaΒ Wodini, Lucia alichoka roho na mwili huku akihisi kabisaΒ viungo havifanyi kazi tena.Β
Alijikutana akikaa chini taratibu huku akijawa na mshangaoΒ mno, aliona kabisa kitendo kile kilifanywa bila ridhaa yaΒ Mandy. Alifuta chozi lake lililoanza kumdondoka kishaΒ alijishangaa ni kwanini alikuwa akilia, alinyanyuka kishaΒ alimtazama sana Mandy, alimuonea huruma. Alitamani aamke iliΒ ashuhudie kilichokuwa kinafanywa na Mume wake, akili ya LuciaΒ ikamwambiaΒ
“Basi Desmond anaeeza akamuuwa Mke wake kama amewezaΒ kumsainisha akiwa hoi kitandani basi anaweza akaondoa uhaiΒ wake” Akili ya Lucia ilifika ukomo wa kutafakari jambo hilo.
Usiku Lucia aliondoka Hospitalini akiwa hoi Bin taabani,Β alipitia baa akaagiza pombe akanywa maana jambo lile halikuwaΒ la kawaida hasa kwa Mawanaume ambaye alimpenda ila hakuwahiΒ kumwambia, aliona moyo wake ulikosea njia kisha alijichekaΒ akiwa anaendelea kupata pombe taratibu, kisha baadaye alikodiΒ Pikipiki ikamrejesha nyumbani kwao.Β
Mama yake alishangaaa sana kumuona Lucia akiwa amelewa kiasiΒ kile, alikuwa amelewa kupita maelezo hata dereva wa pikipikiΒ alimpa tahadhari Mama Lucia kuwa Binti huyo alikuwa amekunywaΒ sana hivyo awe naye makini wakati anampeleka ndani.Β
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA NNE
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & PainΒ
6 Comments
Nice
Pesa imekuwa adui na katili kupitilizaπ₯π’
Anyway Asante Kaka Mkubwa kwa stori nzuri yenye mafunzo maumivu ndani yake
More Love from Kenya β€οΈ
“Kuna mpango mkubwa unaoandaliwa na mataifa makubwa kuirudia na kuigawanya Africa kama walivyofanya katika mkataba wao wa Berlin miaka ya 1884-1885 na mara hii kutaka kuiangamiza kabisa…..
….Hatimaye msichana ambaye ana asili ya kiafrika anayechukua masomo yake katika mojawapo ya mataifa yao anagundua na ANAAMUA KUUZUIA MPANGO HUO!!!!”
Hahahah JE HII ITAKUA ZAIDI YA ILE YA MAYA WA ULAYA???? USIIKOSE HII KITU CHALII YANGU!!!
https://whatsapp.com/channel/0029VanxLVYJ93wbHawAAh3H/665
Like moja hapa kisha follow channel kama bado usiikose hii ….
hivi karibuni usiikose!!!
Mmmmh hatari pesa ni adui jamani
Lucia si achie ubuyu tuu
πππ
54cxym