Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-05

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-04

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Love&Pain Sehemu Ya Pili (02)
    Hadithi

    Love&Pain Sehemu Ya Pili (02)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaNovember 9, 2024Updated:November 21, 202411 Comments9 Mins Read5K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Love & Pain
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Desmond wewe ni Mzuri sana, Hakika Mke wako anajivunia kuwaΒ  na Mwanaume kama Wewe” Alisema Lucia kisha DesmondΒ  alitabasamu kidogo alafu hakusema chochote kile hadi anafikaΒ  eneo ambalo Lucia alikuwa akienda. Ilikuwa ni kwenye mgahawaΒ  huo huo ambao Desmond alienda kukutana na Mpenzi wake NoelaΒ 

    “Eeeh ajabu kumbe nawe ulikuwa unakuja hapa?” AliulizaΒ 

    “Yaah! Kuna Mtu naonana naye mara moja kisha niendelee naΒ  majukumu mengine”Β 

    “Haya asante kwa Lifti” Alisema Lucia kisha alishuka akaingiaΒ  kwenye mgahawa huo ambao ulikuwa wenye hadhi kubwa na piaΒ  ulikuwa mkubwa mno, Desmond alienda mahali ambapo alipangaΒ  kuonana na Noela. Endelea

    SEHEMU YA PILI

    Waliagiza chakula kwa pamoja kisha walianza kula hukuΒ  wakizungumza masuala yao ya kimapenzi, japo Desmond alikuwaΒ  akicheka ila akili yake ilikuwa kule Hospitalini alipo MkeΒ  wake, ucheshi wa hapa na pale uliendelea huku wakinyweshanaΒ  na kulishana, ghafla simu ya Desmond iliita, kutokana na hofuΒ  aliyonayo alijikuta akiangusha glasi ya Juisi ikamwagikiaΒ  kwenye nguo ya NoelaΒ 

    “Oooh samahani mpenzi naomba nipokee simu” Alisema DesmondΒ 

    “Usijali Joshua, naenda chooni mara moja” Alisema Noela kishaΒ  alinyanyuka akaelekea chooni kwa ajili ya kujisafisha.Β 

    Aliingia chooni akajisafisha vizuri lakini wakati anatokaΒ  alikutana na Nesi Lucia, walikuwa ni marafiki wa zamani sana,Β  basi walipoonana walikumbatiana kwa furahaΒ 

    “Eeeh za Maiaka Noela?” aliuliza LuciaΒ 

    “Nzuri, jamani Lucia umekuwa mzuri hivyo jamani” AlisemaΒ  Noela kisha alimkumbatia tena LuciaΒ 

    “Oooh Miaka mingi imepita Maisha yapoje?” aliuliza LuciaΒ 

    “Mungu anasaidia, kuna kipindi nilisikia umekuwa MwanasheriaΒ  mzuri sana Nchini”Β 

    “Yeah!! Mimi ni Mwanasheria pia mpelelezi nina kampuni yanguΒ  Binafsi japo bado nipo serikalini, wewe je?” Alisema NoelaΒ  kisha alitupa swali kwa rafiki yake huyo wa zamaniΒ 

    “Namshukuru Mungu mimi ni Nesi napambana na wagonjwa” AlijibuΒ  Lucia kisha walicheka kwa pamoja, walipeana namba za simuΒ  kisha Lucia aliulizaΒ 

    “Kumbe unakujaga hapa kula?”Β 

    “Ndio mara nyingi sana ila leo nipo na Shemeji yako”Β 

    “Oooh! natamani kumuona jamani, hapana shaka ni mzuri kamaΒ  wewe mwenyewe” Alisema LuciaΒ 

    “Ha!ha!ha! hujaacha utani tu, haya twende ukamuone” AlisemaΒ  NoelaΒ 

    “Haya twende mara moja, ni muda sana aisee kweli MaishaΒ  yanabadilika” Alisema Lucia kisha stori zao zingineΒ  ziliendelea, Desmond alikuwa bize na simu hivyo hakujuwa kamaΒ  Mpenzi wake ameongoznaa na nesi anayemuhudumia Mke wakeΒ  Hospitalini.

    Bahati nzuri ile anageuka anawaona Lucia na Noela wakiendaΒ  alipo, Desmond aliinama chiniΒ 

    “Ina maana Nesi Lucia na Noela wanafahamiana, ooohΒ  nimeshaharibu hapa, vipi kama Lucia akimwambia Noela kuwaΒ  nina Mke?” alijiuliza Desmond, aliponyanyua tena kichwaΒ  alimuona Noela akiwa peke yake, alishangaa sana wakatiΒ  sekunde chache alikuwa ameongozana na Lucia, Noela aliketiΒ 

    “Mwenzio yupo wapi?” alihoji Desmond kwa umakini sanaΒ 

    “Ni rafiki yangu yule kumbe ulimuona, anaitwa Lucia ni nesi,Β  nilisoma naye kitambo” Alijibu bila wasiwasi Noela lakiniΒ  hakutatua kiu ya Desmond ya kutaka kujuwa alikuwa ameendaΒ  wapiΒ 

    “Yupo wapi sasa?” Alihoji DesmondΒ 

    “Amepigiwa simu kuwa kuna Mgonjwa amerudisha fahamu hivyoΒ  ameelekea Hospitali” Kusikia hivyo Desmond alijuwa moja kwaΒ  moja ni Mke wake MandyΒ 

    “Amerudisha fahamu, hajataja chochote?” aliuliza Desmond kamaΒ  Mtu aliyeingiwa na kichaaΒ 

    “Kutaja chochote? Nani unamzungumzia”Β 

    “Aah samahani, siwezi kuendelea kuwa hapa mpenzi” AlisemaΒ  Desmond kisha aliondoka hapo mbio mbioΒ 

    “Hivi huyu Mwanaume anan nini siku hizi mbona amekuwa naΒ  tabia za hovyo? mara hapokei simu mara anazungumza vituΒ  sivielewi” Alijiuliza Noela kwa sauti iliyoambatana na kilioΒ  kidogo.Β 

    Haraka haraka Desmond alifika Hospitalini ambako MandyΒ  alikuwa amelazwa, alikuwa amechoka mwili na akili yote hukuΒ  hofu yake ikiwa kwa Mandy kuwa ameamka, alipofika wodiniΒ  alimkuta Mandy akiwa amewekewa mashine ya kumsaidia kupumua,Β  pembezoni kukiwa na daktari, wahudumu wote wa afya ndani yaΒ  Hospitali hiyo walikuwa wakimfahamu Desmond, yule DaktariΒ  alimuulizaΒ 

    “Mbona upo hivyo Desmond” Aliuliza akiwa anafanya kazi yake,Β  Desmond alitikisa kichwa chake kisha alitoka wodini humoΒ  akiwa amechoka sana, kiasi fulani alishusha pumzi zake baadaΒ  ya kugundua kuwa Mandy alikuwa hajazinduka, alishika sehemuΒ  ya moyo wake kama ishara ya hali yake ya wasiwasi.Β 

    ************

    Jioni Noela aliporudi nyumbani kwao alijikuta akikosa raha,Β  mvua ilikuwa ikinyesha hivyo alijifungia chumbani kwake,Β  alianza kupitia mafaili ya kazi zilizo mbele yake. KilaΒ  alichokisoma hakikuingia kwenye akili yake, alijiona anaΒ  mzigo mzito kichwani pake.Β 

    Alijilaza kitandani akiwa hoi kwa mawazo, DesmondΒ  alimchanganya sana kwa jinsi alivyobadilika ghafla, hakujuwaΒ  jambo zito lililo kichwani pa Desmond ambaye yeye alikuwaΒ  akimfahamu kama Joshua, wakati anawaza baadhi ya mamboΒ  alijikuta akikumbuka tukio la mchana alivyokutana na rafikiΒ  yake wa zamani ambaye ni nesi Lucia. Alifikiria amtafuteΒ  maana baada ya kupeana namba ule mchana hakuna aliyemtafutaΒ  mwenzake, alinyanyua simu yake akampigia, simu iliita kwaΒ  kitambo kidogo kabla ya kupokelewa.Β 

    “Hello Lucia” Alisema NoelaΒ 

    “Abee kipenzi! nilitingwa kidogo nikasema nikutafute baadaye”Β  Alisema pia LuciaΒ 

    “Oooh nafikiri hiyo baadaye ndiyo hii, hebu subiri vipi haliΒ  ya huyo Mgonjwa wako uliyemkimbilia?” Aliuliza Noela maanaΒ  alipoachana na Lucia ule mchana alikuwa alikimbilia HospitaliΒ 

    “Namshukuru Mungu anaendelea vizuri sana, sijui shem wanguΒ  japo sikubahatika kuonana naye” Alisema LuciaΒ 

    “Naye yuko poa Lucia, usijali utamuona siku moja” AlisemaΒ  NoelaΒ 

    “Anaitwa Nani vile?” aliuliza Lucia, Noela alikaa kimya kwaΒ  sekunde chache kisha akamjibuΒ 

    “Anaitwa Joshua”Β 

    “Ohooo ana jina la kipekee, natumaini ni mzuri kama wewe”Β  Alisema Lucia kisha wote walicheka kisha waliagana kwaΒ  kutakiana jioni njema na mara moja simu ilikatwa.Β 

    Noela alishusha pumzi zake, angalau kidogo alijiona hanaΒ  mzigo mzito kichwani.Β 

    Mara mlango wa chumba chake uligongwa, alijisomba kitandaniΒ  akaenda kuufungua, alikuwa ni Mama yake aliyezoea kumuitaΒ  MlamiΒ 

    “Vipi Mlami?” Alihoji Noela, alimtazama Mama yake alikuwaΒ  ameshikilia kikombe cha Maziwa

    “Na hii baridi nimekuletea maziwa ya moto Binti yangu, vipiΒ  ulizungumza na Joshua?” Aliuliza Mama yake Noela akiwaΒ  anampatia Noela kikombe chenye maziwa, Noela alikipokea kishaΒ  alimjibu Mama yake akamwambiaΒ 

    “Ndiyo Mama! Lakini Joshua siku hizi simuelewi elewi” AlisemaΒ  kisha alipiga maziwa kidogoΒ 

    “Humuelewi? Kwani amekuwaje!” Aliuliza Mama NoelaΒ 

    “Wee Mlami acha tu, nitakueleza vizuri Mama. Nikutakie jioniΒ  njema” Alisema Noela kisha alifunga mlango, hali hiiΒ  ilimfanya Mama yake Noela kupata mawazo ya jambo lipiΒ  lililokuwa likimsibu Binti yake.Β 

    Siku iliyofuata mapema sana Desmond alikuwa ofisini kwakeΒ  akiendelea na kazi, alionekana kuwa bize sana siku hiyoΒ  kuliko hata kawaida yake. Akiwa anaendelea na kazi alisikiaΒ  simu yake ikiita, alipotupa macho kwenye kioo aliona niΒ  askari ambaye alikuwa alichunguza tukio la kifo cha MamaΒ  Mandy ambaye alionana naye kule Hospitalini, ndiye aliyekuwaΒ  akimpigia Desmond. Aliishika simu akiwa ana tafakari hukuΒ  akijiuliza askari huyo alikuwa akitaka kusema nini?Β 

    “Kwanini ananipigia leo?” Alijiuliza huku simu ikizidi kuita,Β  aliweka sauti vizuri kisha aliipokeaΒ 

    “Hallo” Alisema Desmond kwa sauti iliyojaa umakini wa hali yaΒ  juuΒ 

    “Mr. Desmond, mtuhumiwa namba moja wa kifo cha Mama MandyΒ  ameonekana kwenye kijiji kimoja kinachoitwa Pendahili ambachoΒ  kipo kaskazini mwa Mkoa jirani, tukimpata yeye tutakuwaΒ  tumepata ufumbuzi wa kesi hii” Ilisikika sauti ya AskariΒ  huyo, Desmond alishtuka sana akaulizaΒ 

    “Unamaanisha Sanga?”Β 

    “Ndiyo! Mfanyakazi wenu wa ndani aliyepotea baada ya tukioΒ  lile lililopelekea Mkeo kuwa katika koma”Β 

    “Amekamatwa?”Β 

    “Bado hajakamatwa ila tayari tumetuma polisi kuelekea hukoΒ  sasa hivi” Alisema Askari huyoΒ 

    “Haya asante kwa taarifa” Alisema Desmond kisha alikata simuΒ  hiyo haraka sana

    “Sanga anawezaje kurudi Kijijini kwao wakati tulikubalianaΒ  aende mbali?” Alijiuliza Desmond akiwa ameshikilia simu yake,Β  akakumbuka jinsi ilivyokuwa siku ya TukioΒ 

    Alikumbuka jinsi alivyokuwa akiongea na Huyo Sanga ambayeΒ  alikuwa ni mfanyakazi wao wa ndani wakati huo Mwili wa MandyΒ  ukiwa katika ngazi ukivuja damu. Desmond alikuwa ametapakaaΒ  damu mikononi, alimwambia Sanga akiwa katika hali yaΒ  Kuchanganikiwa sanaΒ 

    “Polisi watakuja hapa watakukamata Sanga kwasababu kuanziaΒ  sasa wewe ndiye Muuwaji uliyemuuwa Mke wangu! UkikamatwaΒ  utaozea jela, nakupa pesa uwende mbali sana na usirudi”Β  Alisema Desmond kisha alipandisha juu akarudi na kiasiΒ  kikubwa cha pesa akampa SangaΒ 

    “Kumbuka hupaswi kwenda Kijijini kwenu wala kujulikana mahaliΒ  ulipo” Sanga naye alikuwa amechanganikiwa alipokea pesa hizoΒ  kisha alikimbia nyumbani hapo, kisha Desmond aligeukaΒ  akamtazama Mke wake ambaye aliamini alikuwa amekufa,Β  alichukua bastola akajipiga begani, aligumia kwa maumivuΒ  akajilaza chini kisha akapiga simu polisi, walipofika polisiΒ  Desmond aliwaambia polisi hao kuwa aliyefanya matukio hayoΒ  alikuwa ni Mfanyakazi wao wa ndani aliyeitwa Sanga.Β 

    Tokea siku hiyo Sanga aliyafutwa kila kona huku akihusishwaΒ  na tukio la kutaka kufanya jaribio la kumuuwa Mandy pamoja naΒ  Desmond, tukio hilo likahusishwa kitaalam na ufichaji wa siriΒ  ya kifo cha Mama Mandy ambacho kilitokea miezi miwiliΒ  iliyopita kabla ya tukio hilo.Β 

    Desmond alimaliza kukumbuka kisha alisemaΒ 

    “Sanga ukikamatwa utatoa siri ya ulichokiona, sitoruhusu hiloΒ  litokee” Mara moja Desmond aliondoka ofisini hapo akachukuaΒ  gari yake akaanza safari ya kuelekea kwenye kijiji hichoΒ  ambacho alitokea Sanga. Aliendesha gari kwa spidi sana iliΒ  awahi kabla ya polisi kumkamata Sanga.Β 

    Upande wa pili, Noela alikuwa akimpigia simu sana DesmondΒ  bila mafanikio ya kupokelewa kwa simu hiyo hali iliyomfanyaΒ  azidi kuwa na wasiwasi na mpenzi wake huyo, alimuita ZandaΒ  akampa kazi ya kumtafuta Desmond kwa njia ya mtandao iliΒ  ijulikane mahali alipo Desmond, hofu na mashaka vilianzaΒ  kumuingia Noela huku akitafakari mpenzi wake huyo alikuwaΒ  akipitia jambo gani maana alikuwa haeleweki, ndani ya dakikaΒ  kadhaa mtandao ulionesha alipo Desmond, alikuwa akitoka njeΒ  ya Jiji hilo.

    “Aaas!! Anaenda wapi!?” Alijiuliza sana Noela kisha alichukuaΒ  kibegi chake akaondoka ofisini hapo.Β 

    Safari ya Desmond kuelekea Kijijini ilizidi kusonga mbele,Β  lengo likiwa kumzuia Sanga asiingie mikononi mwa polisi,Β  alizidi kuunguza mpira kwa spidi kali sana.Β 

    Ndani ya masaa matano Desmond alifanikiwa kufika KijijiniΒ  hapo.Β 

    Alikijua vizuri kijiji hicho sababu yeye ndiye aliyemfuataΒ  Sanga akawe mfanyakazi, alivalia kofia kisha alishuka kwenyeΒ  gari yake, mbele aliona gari yenye nembo ya polisi hivyoΒ  alitambuwa fika kuwa polisi walikuwa wameshafika eneo hilo,Β  alijitahidi kutembea kwa tahadhari huku macho yake yakiangazaΒ  huku na kule, bahati ilioje kabla hata hajafika nyumbaniΒ  anakoishi Sanga alimuona Sanga akiwa amejificha sehemu,Β  hapana shaka hata Sanga alihitaji kuwakwepa askari hao. MachoΒ  ya Sanga na Desmond yaligongana kisha haraka Desmond aliendaΒ  hadi alipojificha SangaΒ 

    “Umefanya nini Sanga?” Alihoji Desmond akiwa amejificha hapoΒ  na SangaΒ 

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TATU

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&PainΒ 

    Love&Pain

    11 Comments

    1. Careen on November 9, 2024 5:17 pm

      Dah πŸ˜” aisee tamu sana jmn

      Reply
    2. G shirima on November 9, 2024 5:54 pm

      Kazi nzur sana kaka

      Reply
    3. Fawziya Hassan on November 9, 2024 6:10 pm

      Hadithi imeanza kupamba moto
      Asante sana Kaka Mkubwa
      Nimekuwa nikijifunza mengi kupitia simulizi zako
      More Love from Kenya ❀️

      Reply
    4. Nelca on November 9, 2024 6:46 pm

      Waoooooo

      Reply
    5. Sharo love malkx πŸ’– on November 9, 2024 7:19 pm

      Kisanga kwa sangaπŸ€”

      Reply
    6. Halinga1 on November 9, 2024 10:54 pm

      Sanga anataka kuleta Baraaa

      Reply
    7. Joyce on November 10, 2024 10:55 am

      Duuuh hatariii

      Reply
    8. Hamis on November 10, 2024 2:51 pm

      Kaz ipo mbona

      Reply
      • official on November 11, 2024 10:36 am

        Admin fany mpango tupate love and pain sehemu ya 3 na kuendelea maan n nzuri san

        Reply
    9. official on November 11, 2024 10:34 am

      Admin fany mpango tupate love and pain sehemu ya 3 na kuendelea maan n nzuri san

      Reply
    10. Cafeteria on November 12, 2024 7:21 am

      SIMULIZI|MPANGO HASI( NEGATIVE PLAN ) SEHEMU YA KWANZA.
      SIMULIZI ya Kijasusi MTUNZI ABYAS MZIGUA.
      https://whatsapp.com/channel/0029VanxLVYJ93wbHawAAh3H/668

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi July 17, 2025

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-05

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya nne Wakiwa wanaendelea kujibizana, walianza kusikia sauti ya Bi.…

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-04

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.