Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 12

    In the name of LOVE – 11

    In the name of LOVE – 10

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Love&Pain Sehemu Ya Pili (02)
    Hadithi

    Love&Pain Sehemu Ya Pili (02)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaNovember 9, 2024Updated:November 21, 202415 Comments9 Mins Read5K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Love & Pain
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Desmond wewe ni Mzuri sana, Hakika Mke wako anajivunia kuwaย  na Mwanaume kama Wewe” Alisema Lucia kisha Desmondย  alitabasamu kidogo alafu hakusema chochote kile hadi anafikaย  eneo ambalo Lucia alikuwa akienda. Ilikuwa ni kwenye mgahawaย  huo huo ambao Desmond alienda kukutana na Mpenzi wake Noelaย 

    “Eeeh ajabu kumbe nawe ulikuwa unakuja hapa?” Aliulizaย 

    “Yaah! Kuna Mtu naonana naye mara moja kisha niendelee naย  majukumu mengine”ย 

    “Haya asante kwa Lifti” Alisema Lucia kisha alishuka akaingiaย  kwenye mgahawa huo ambao ulikuwa wenye hadhi kubwa na piaย  ulikuwa mkubwa mno, Desmond alienda mahali ambapo alipangaย  kuonana na Noela. Endelea

    SEHEMU YA PILI

    Waliagiza chakula kwa pamoja kisha walianza kula hukuย  wakizungumza masuala yao ya kimapenzi, japo Desmond alikuwaย  akicheka ila akili yake ilikuwa kule Hospitalini alipo Mkeย  wake, ucheshi wa hapa na pale uliendelea huku wakinyweshanaย  na kulishana, ghafla simu ya Desmond iliita, kutokana na hofuย  aliyonayo alijikuta akiangusha glasi ya Juisi ikamwagikiaย  kwenye nguo ya Noelaย 

    “Oooh samahani mpenzi naomba nipokee simu” Alisema Desmondย 

    “Usijali Joshua, naenda chooni mara moja” Alisema Noela kishaย  alinyanyuka akaelekea chooni kwa ajili ya kujisafisha.ย 

    Aliingia chooni akajisafisha vizuri lakini wakati anatokaย  alikutana na Nesi Lucia, walikuwa ni marafiki wa zamani sana,ย  basi walipoonana walikumbatiana kwa furahaย 

    “Eeeh za Maiaka Noela?” aliuliza Luciaย 

    “Nzuri, jamani Lucia umekuwa mzuri hivyo jamani” Alisemaย  Noela kisha alimkumbatia tena Luciaย 

    “Oooh Miaka mingi imepita Maisha yapoje?” aliuliza Luciaย 

    “Mungu anasaidia, kuna kipindi nilisikia umekuwa Mwanasheriaย  mzuri sana Nchini”ย 

    “Yeah!! Mimi ni Mwanasheria pia mpelelezi nina kampuni yanguย  Binafsi japo bado nipo serikalini, wewe je?” Alisema Noelaย  kisha alitupa swali kwa rafiki yake huyo wa zamaniย 

    “Namshukuru Mungu mimi ni Nesi napambana na wagonjwa” Alijibuย  Lucia kisha walicheka kwa pamoja, walipeana namba za simuย  kisha Lucia aliulizaย 

    “Kumbe unakujaga hapa kula?”ย 

    “Ndio mara nyingi sana ila leo nipo na Shemeji yako”ย 

    “Oooh! natamani kumuona jamani, hapana shaka ni mzuri kamaย  wewe mwenyewe” Alisema Luciaย 

    “Ha!ha!ha! hujaacha utani tu, haya twende ukamuone” Alisemaย  Noelaย 

    “Haya twende mara moja, ni muda sana aisee kweli Maishaย  yanabadilika” Alisema Lucia kisha stori zao zingineย  ziliendelea, Desmond alikuwa bize na simu hivyo hakujuwa kamaย  Mpenzi wake ameongoznaa na nesi anayemuhudumia Mke wakeย  Hospitalini.

    Bahati nzuri ile anageuka anawaona Lucia na Noela wakiendaย  alipo, Desmond aliinama chiniย 

    “Ina maana Nesi Lucia na Noela wanafahamiana, ooohย  nimeshaharibu hapa, vipi kama Lucia akimwambia Noela kuwaย  nina Mke?” alijiuliza Desmond, aliponyanyua tena kichwaย  alimuona Noela akiwa peke yake, alishangaa sana wakatiย  sekunde chache alikuwa ameongozana na Lucia, Noela aliketiย 

    “Mwenzio yupo wapi?” alihoji Desmond kwa umakini sanaย 

    “Ni rafiki yangu yule kumbe ulimuona, anaitwa Lucia ni nesi,ย  nilisoma naye kitambo” Alijibu bila wasiwasi Noela lakiniย  hakutatua kiu ya Desmond ya kutaka kujuwa alikuwa ameendaย  wapiย 

    “Yupo wapi sasa?” Alihoji Desmondย 

    “Amepigiwa simu kuwa kuna Mgonjwa amerudisha fahamu hivyoย  ameelekea Hospitali” Kusikia hivyo Desmond alijuwa moja kwaย  moja ni Mke wake Mandyย 

    “Amerudisha fahamu, hajataja chochote?” aliuliza Desmond kamaย  Mtu aliyeingiwa na kichaaย 

    “Kutaja chochote? Nani unamzungumzia”ย 

    “Aah samahani, siwezi kuendelea kuwa hapa mpenzi” Alisemaย  Desmond kisha aliondoka hapo mbio mbioย 

    “Hivi huyu Mwanaume anan nini siku hizi mbona amekuwa naย  tabia za hovyo? mara hapokei simu mara anazungumza vituย  sivielewi” Alijiuliza Noela kwa sauti iliyoambatana na kilioย  kidogo.ย 

    Haraka haraka Desmond alifika Hospitalini ambako Mandyย  alikuwa amelazwa, alikuwa amechoka mwili na akili yote hukuย  hofu yake ikiwa kwa Mandy kuwa ameamka, alipofika wodiniย  alimkuta Mandy akiwa amewekewa mashine ya kumsaidia kupumua,ย  pembezoni kukiwa na daktari, wahudumu wote wa afya ndani yaย  Hospitali hiyo walikuwa wakimfahamu Desmond, yule Daktariย  alimuulizaย 

    “Mbona upo hivyo Desmond” Aliuliza akiwa anafanya kazi yake,ย  Desmond alitikisa kichwa chake kisha alitoka wodini humoย  akiwa amechoka sana, kiasi fulani alishusha pumzi zake baadaย  ya kugundua kuwa Mandy alikuwa hajazinduka, alishika sehemuย  ya moyo wake kama ishara ya hali yake ya wasiwasi.ย 

    ************

    Jioni Noela aliporudi nyumbani kwao alijikuta akikosa raha,ย  mvua ilikuwa ikinyesha hivyo alijifungia chumbani kwake,ย  alianza kupitia mafaili ya kazi zilizo mbele yake. Kilaย  alichokisoma hakikuingia kwenye akili yake, alijiona anaย  mzigo mzito kichwani pake.ย 

    Alijilaza kitandani akiwa hoi kwa mawazo, Desmondย  alimchanganya sana kwa jinsi alivyobadilika ghafla, hakujuwaย  jambo zito lililo kichwani pa Desmond ambaye yeye alikuwaย  akimfahamu kama Joshua, wakati anawaza baadhi ya mamboย  alijikuta akikumbuka tukio la mchana alivyokutana na rafikiย  yake wa zamani ambaye ni nesi Lucia. Alifikiria amtafuteย  maana baada ya kupeana namba ule mchana hakuna aliyemtafutaย  mwenzake, alinyanyua simu yake akampigia, simu iliita kwaย  kitambo kidogo kabla ya kupokelewa.ย 

    “Hello Lucia” Alisema Noelaย 

    “Abee kipenzi! nilitingwa kidogo nikasema nikutafute baadaye”ย  Alisema pia Luciaย 

    “Oooh nafikiri hiyo baadaye ndiyo hii, hebu subiri vipi haliย  ya huyo Mgonjwa wako uliyemkimbilia?” Aliuliza Noela maanaย  alipoachana na Lucia ule mchana alikuwa alikimbilia Hospitaliย 

    “Namshukuru Mungu anaendelea vizuri sana, sijui shem wanguย  japo sikubahatika kuonana naye” Alisema Luciaย 

    “Naye yuko poa Lucia, usijali utamuona siku moja” Alisemaย  Noelaย 

    “Anaitwa Nani vile?” aliuliza Lucia, Noela alikaa kimya kwaย  sekunde chache kisha akamjibuย 

    “Anaitwa Joshua”ย 

    “Ohooo ana jina la kipekee, natumaini ni mzuri kama wewe”ย  Alisema Lucia kisha wote walicheka kisha waliagana kwaย  kutakiana jioni njema na mara moja simu ilikatwa.ย 

    Noela alishusha pumzi zake, angalau kidogo alijiona hanaย  mzigo mzito kichwani.ย 

    Mara mlango wa chumba chake uligongwa, alijisomba kitandaniย  akaenda kuufungua, alikuwa ni Mama yake aliyezoea kumuitaย  Mlamiย 

    “Vipi Mlami?” Alihoji Noela, alimtazama Mama yake alikuwaย  ameshikilia kikombe cha Maziwa

    “Na hii baridi nimekuletea maziwa ya moto Binti yangu, vipiย  ulizungumza na Joshua?” Aliuliza Mama yake Noela akiwaย  anampatia Noela kikombe chenye maziwa, Noela alikipokea kishaย  alimjibu Mama yake akamwambiaย 

    “Ndiyo Mama! Lakini Joshua siku hizi simuelewi elewi” Alisemaย  kisha alipiga maziwa kidogoย 

    “Humuelewi? Kwani amekuwaje!” Aliuliza Mama Noelaย 

    “Wee Mlami acha tu, nitakueleza vizuri Mama. Nikutakie jioniย  njema” Alisema Noela kisha alifunga mlango, hali hiiย  ilimfanya Mama yake Noela kupata mawazo ya jambo lipiย  lililokuwa likimsibu Binti yake.ย 

    Siku iliyofuata mapema sana Desmond alikuwa ofisini kwakeย  akiendelea na kazi, alionekana kuwa bize sana siku hiyoย  kuliko hata kawaida yake. Akiwa anaendelea na kazi alisikiaย  simu yake ikiita, alipotupa macho kwenye kioo aliona niย  askari ambaye alikuwa alichunguza tukio la kifo cha Mamaย  Mandy ambaye alionana naye kule Hospitalini, ndiye aliyekuwaย  akimpigia Desmond. Aliishika simu akiwa ana tafakari hukuย  akijiuliza askari huyo alikuwa akitaka kusema nini?ย 

    “Kwanini ananipigia leo?” Alijiuliza huku simu ikizidi kuita,ย  aliweka sauti vizuri kisha aliipokeaย 

    “Hallo” Alisema Desmond kwa sauti iliyojaa umakini wa hali yaย  juuย 

    “Mr. Desmond, mtuhumiwa namba moja wa kifo cha Mama Mandyย  ameonekana kwenye kijiji kimoja kinachoitwa Pendahili ambachoย  kipo kaskazini mwa Mkoa jirani, tukimpata yeye tutakuwaย  tumepata ufumbuzi wa kesi hii” Ilisikika sauti ya Askariย  huyo, Desmond alishtuka sana akaulizaย 

    “Unamaanisha Sanga?”ย 

    “Ndiyo! Mfanyakazi wenu wa ndani aliyepotea baada ya tukioย  lile lililopelekea Mkeo kuwa katika koma”ย 

    “Amekamatwa?”ย 

    “Bado hajakamatwa ila tayari tumetuma polisi kuelekea hukoย  sasa hivi” Alisema Askari huyoย 

    “Haya asante kwa taarifa” Alisema Desmond kisha alikata simuย  hiyo haraka sana

    “Sanga anawezaje kurudi Kijijini kwao wakati tulikubalianaย  aende mbali?” Alijiuliza Desmond akiwa ameshikilia simu yake,ย  akakumbuka jinsi ilivyokuwa siku ya Tukioย 

    Alikumbuka jinsi alivyokuwa akiongea na Huyo Sanga ambayeย  alikuwa ni mfanyakazi wao wa ndani wakati huo Mwili wa Mandyย  ukiwa katika ngazi ukivuja damu. Desmond alikuwa ametapakaaย  damu mikononi, alimwambia Sanga akiwa katika hali yaย  Kuchanganikiwa sanaย 

    “Polisi watakuja hapa watakukamata Sanga kwasababu kuanziaย  sasa wewe ndiye Muuwaji uliyemuuwa Mke wangu! Ukikamatwaย  utaozea jela, nakupa pesa uwende mbali sana na usirudi”ย  Alisema Desmond kisha alipandisha juu akarudi na kiasiย  kikubwa cha pesa akampa Sangaย 

    “Kumbuka hupaswi kwenda Kijijini kwenu wala kujulikana mahaliย  ulipo” Sanga naye alikuwa amechanganikiwa alipokea pesa hizoย  kisha alikimbia nyumbani hapo, kisha Desmond aligeukaย  akamtazama Mke wake ambaye aliamini alikuwa amekufa,ย  alichukua bastola akajipiga begani, aligumia kwa maumivuย  akajilaza chini kisha akapiga simu polisi, walipofika polisiย  Desmond aliwaambia polisi hao kuwa aliyefanya matukio hayoย  alikuwa ni Mfanyakazi wao wa ndani aliyeitwa Sanga.ย 

    Tokea siku hiyo Sanga aliyafutwa kila kona huku akihusishwaย  na tukio la kutaka kufanya jaribio la kumuuwa Mandy pamoja naย  Desmond, tukio hilo likahusishwa kitaalam na ufichaji wa siriย  ya kifo cha Mama Mandy ambacho kilitokea miezi miwiliย  iliyopita kabla ya tukio hilo.ย 

    Desmond alimaliza kukumbuka kisha alisemaย 

    “Sanga ukikamatwa utatoa siri ya ulichokiona, sitoruhusu hiloย  litokee” Mara moja Desmond aliondoka ofisini hapo akachukuaย  gari yake akaanza safari ya kuelekea kwenye kijiji hichoย  ambacho alitokea Sanga. Aliendesha gari kwa spidi sana iliย  awahi kabla ya polisi kumkamata Sanga.ย 

    Upande wa pili, Noela alikuwa akimpigia simu sana Desmondย  bila mafanikio ya kupokelewa kwa simu hiyo hali iliyomfanyaย  azidi kuwa na wasiwasi na mpenzi wake huyo, alimuita Zandaย  akampa kazi ya kumtafuta Desmond kwa njia ya mtandao iliย  ijulikane mahali alipo Desmond, hofu na mashaka vilianzaย  kumuingia Noela huku akitafakari mpenzi wake huyo alikuwaย  akipitia jambo gani maana alikuwa haeleweki, ndani ya dakikaย  kadhaa mtandao ulionesha alipo Desmond, alikuwa akitoka njeย  ya Jiji hilo.

    “Aaas!! Anaenda wapi!?” Alijiuliza sana Noela kisha alichukuaย  kibegi chake akaondoka ofisini hapo.ย 

    Safari ya Desmond kuelekea Kijijini ilizidi kusonga mbele,ย  lengo likiwa kumzuia Sanga asiingie mikononi mwa polisi,ย  alizidi kuunguza mpira kwa spidi kali sana.ย 

    Ndani ya masaa matano Desmond alifanikiwa kufika Kijijiniย  hapo.ย 

    Alikijua vizuri kijiji hicho sababu yeye ndiye aliyemfuataย  Sanga akawe mfanyakazi, alivalia kofia kisha alishuka kwenyeย  gari yake, mbele aliona gari yenye nembo ya polisi hivyoย  alitambuwa fika kuwa polisi walikuwa wameshafika eneo hilo,ย  alijitahidi kutembea kwa tahadhari huku macho yake yakiangazaย  huku na kule, bahati ilioje kabla hata hajafika nyumbaniย  anakoishi Sanga alimuona Sanga akiwa amejificha sehemu,ย  hapana shaka hata Sanga alihitaji kuwakwepa askari hao. Machoย  ya Sanga na Desmond yaligongana kisha haraka Desmond aliendaย  hadi alipojificha Sangaย 

    “Umefanya nini Sanga?” Alihoji Desmond akiwa amejificha hapoย  na Sangaย 

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TATU

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMย ย 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Pain Love&Painย 

    Love&Pain

    15 Comments

    1. Careen on November 9, 2024 5:17 pm

      Dah ๐Ÿ˜” aisee tamu sana jmn

      Reply
    2. G shirima on November 9, 2024 5:54 pm

      Kazi nzur sana kaka

      Reply
    3. Fawziya Hassan on November 9, 2024 6:10 pm

      Hadithi imeanza kupamba moto
      Asante sana Kaka Mkubwa
      Nimekuwa nikijifunza mengi kupitia simulizi zako
      More Love from Kenya โค๏ธ

      Reply
    4. Nelca on November 9, 2024 6:46 pm

      Waoooooo

      Reply
    5. Sharo love malkx ๐Ÿ’– on November 9, 2024 7:19 pm

      Kisanga kwa sanga๐Ÿค”

      Reply
    6. Halinga1 on November 9, 2024 10:54 pm

      Sanga anataka kuleta Baraaa

      Reply
    7. Joyce on November 10, 2024 10:55 am

      Duuuh hatariii

      Reply
    8. Hamis on November 10, 2024 2:51 pm

      Kaz ipo mbona

      Reply
      • official on November 11, 2024 10:36 am

        Admin fany mpango tupate love and pain sehemu ya 3 na kuendelea maan n nzuri san

        Reply
    9. official on November 11, 2024 10:34 am

      Admin fany mpango tupate love and pain sehemu ya 3 na kuendelea maan n nzuri san

      Reply
    10. Cafeteria on November 12, 2024 7:21 am

      SIMULIZI|MPANGO HASI( NEGATIVE PLAN ) SEHEMU YA KWANZA.
      SIMULIZI ya Kijasusi MTUNZI ABYAS MZIGUA.
      https://whatsapp.com/channel/0029VanxLVYJ93wbHawAAh3H/668

      Reply
    11. ๐Ÿ’Œ โ— Verification Required - 0.2 Bitcoin transaction blocked. Proceed here >> https://graph.org/UNLOCK-CRYPTO-ASSETS-07-23?hs=9035d52c29eeacf46b02f81b4fc8ee19& ๐Ÿ’Œ on September 6, 2025 9:12 am

      ufr91d

      Reply
    12. ๐Ÿ”‹ WALLET UPDATE: Suspicious transfer of 2.0 Bitcoin. Stop? >> https://graph.org/Get-your-BTC-09-04?hs=9035d52c29eeacf46b02f81b4fc8ee19& ๐Ÿ”‹ on September 10, 2025 11:02 am

      4zvenr

      Reply
    13. ๐Ÿ“ ๐Ÿ“Œ Reminder: 1.5 BTC pending. Open account โ†’ https://graph.org/Get-your-BTC-09-04?hs=9035d52c29eeacf46b02f81b4fc8ee19& ๐Ÿ“ on October 10, 2025 3:31 am

      xs8x3q

      Reply
    14. โš™ ๐Ÿ’น Balance Alert: +2.5 BTC detected. Access now > https://graph.org/Get-your-BTC-09-04?hs=9035d52c29eeacf46b02f81b4fc8ee19& โš™ on October 14, 2025 1:07 pm

      w3y8iv

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi October 1, 2025

    In the name of LOVE – 12

    Ilipoishia sehemu ya Kumi na moja ya In the name of LOVE Moyo Wangu na…

    In the name of LOVE – 11

    In the name of LOVE – 10

    In the name of LOVE – 09

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.