Usiku mmoja, Mwanaume mmoja alikuwa akitoka Hospitalini,ย alionekana kwenda hapo kwa ajili ya kumuona Mtu mmojaย aliyemfahamu sana tena alikuwa Mtu wa karibu sana kwake.ย Mwanaume huyo alionekana kuwa mwenye mawazo fulani kichwaniย pake, alikuwa amevalia koti la suti na jinzi chini akipigiliaย raba kali yenye mg’ao.ย
Ilitosha kujiridhisha kuwa Mwanaume huyo alikuwa na hela zaย kutosha, tembea yake ilikuwa ya taratibu mno, ukimtazamaย vizuri utagundua alikuwa na vita kichwani pake, alipofikaย kwenye korido aligeuka na kutazama nyuma kisha alitaja jinaย mojaย
“Mandy!” Alilitaja jina hilo kisha alihema kiasi, kishaย aliendelea mbele kuuelekea mlango wa kutoka Hospitalini hapo.ย Alikutana na nesi mmoja akiwa amebakisha hatua chache kutoka,ย nesi huyo alimuita Mwanaume huyo jina lakeย
“Desmond!!” Alipomuita ni kama alimzindua kutoka Mawazoni,ย Mwanaume huyo aliyeitwa Desmond alijichekesha kidogo kabla yaย kusalimiana na nesi huyoย
“Aaah!! Lucia, Habari yako!” Alisalimia Desmondย
“Nzuri mbona una mawazo hivyo au kuna taarifa yoyote mbayaย kumuhusu Mandy?” Aliuliza nesi huyo aliyeonesha kumfahamuย Vizuri Desmondย
“Aaah! Hapana hali yake ipo vilevile, nimechoka tu naย majukumu ya hapa na pale” Alisema Desmondย
“Pamoja na yote Desmond, wewe ni Mwanaume mzuri sana, unajaliย mno maana huishi kuja kumuona Mandy kwa kipindi chote ambachoย amekuwa hapa” Alisema Luciaย
“Ndiyo jukumu langu, nahitaji kwenda sasa” Alisema Desmond,ย waliagana hapo kisha Desmond aliondoka zake huku Luciaย akimtazama Desmond kwa jicho la kuhitaji kumwambia kituย lakini alishindwa.
Yalikuwa ni majira ya saa tano za Usiku, muda huo mvuaย ilianza kuchapa kidogo na kumfanya Desmond akimbilie kwenyeย gari yake, aliondoka Hospitalini hapo Usiku huo huku akiwaย kwenye gari alionekana kukumbuka jambo liliomuumiza, sauti yaย daktari ilijirudia kichwani pakeย
“Mandy anaweza kupata ufahamu ndani ya siku chache zijazo,ย hii ni habari njema Desmond” Alionekana kutofurahishwa naย taarifa ya Mgonjwa huyo kuwa sawa, alipiga usukani kwa hasiraย kisha alielekea moja kwa moja kwenye jumba lake la kifahariย lililopo karibu na fukwe, ndipo alipokuwa akiishi.ย
Alipoingia alitazama ukutani, aliiyona picha aliyopiga yeyeย na huyo Mgonjwa aliyeitwa Mandy, mgonjwa huyo alikuwa waย kike, picha hiyo ilieleza kuhusu Mandy na Desmond, Naam!ย Walikuwa ni wana ndoa, Desmond aliitoa picha hiyo akaitupaย kutoka juu ya ghorofa hilo hadi chiniย
“Mandy huwezi kuwa hai tena ni lazima nikumalize” Alisemaย Desmond kwa hasira na hisia kali huku akionesha wazi kuwaย kulikuwa na jambo ambalo lilijificha kuhusu Yeye na mke wakeย huyo aliyeitwa Mandy.ย
Alikunywa pombe sana usiku huo huku simu yake ikiwa bizeย kuita lakini hakuipokea kabisa, alikunywa na kulewa sanaย akawa hajitambui, alilala hapo sebleni hadi asubuhi.ย
**********ย
Ilikuwa ni asubuhi ya siku iliyofuata, ndani ya ofisi mojaย alikuwepo Mwanamke mzuri sana aliyeitwa Noela, Mwanamke huyuย alikuwa ni Mwanasheria. Alikuwa akifanya kazi yake hapoย ofisini huku akili yake ikionesha wazi kuwa haikuwa naย utulivu, mara zote alikuwa akijaribu kupiga simu bilaย kupokelewa, baadaye alikuja jamaa mmoja aliyeitwa Zanda,ย walikuwa ni marafiki waliokuwa wakifanya kazi ofisi moja yaย Wanasheria wa kujitegemea, mara moja Zanda aligundua Noelaย hakuwa sawa aliketi akamuulizaย
“Vipi Noela una tatizo?” Alihoji Zanda huku akimtazama Usoniย Noelaย
“Aaah! Nipo sawa Zanda usijali” Alijibu Noelaย
“Noela nimefanya kazi na wewe kwa muda mrefu hivyo nakujuwaย vizuri sana, leo haupo sawa” Alisistiza Zanda, Noelaย alimkubalia Zanda kuwa hayupo sawa ila ni mambo madogo tuย atayatatua.
Baada ya kupita muda kidogo Noela aliondoka ofisini akiagaย kuwa anajisikia vibaya. Zanda alimshangaa sana Noela,ย alimkodolea macho akiwa anaondoka na gari yake kishaย alitikisa kichwa chake, Noela aliendelea kupiga simu bilaย kupokea majibu yoyote yale hadi anafika nyumbani kwao,ย alikuwa akiishi na Mama yake Mzazi ambaye alipendelea sanaย kumuita Mlamiย
Mama yake ( Mlami ) aligundua haraka kuwa Noela hayupo sawaย kifikra, alimuuliza akiwa amejilaza sofaniย
“Kuna nini Noela huonekani kuwa sawa kabisa, unaonekana niย mwenye mawazo mengi kichwani mwako” Alihoji Mama yake Noelaย huku akimkata jicho la udadisi binti yake huyo wa pekeeย ambaye alikuwa akimpenda sana baada ya Baba yake kufariki.ย
“Ni Joshua Mama, tokea jana hapokei simu zangu. Sijui yukoย wapi” Alijibu Noela kama vile alikuwa amechokozwa na Mamaย yake, alimpigia tena huyo Joshuaย
“Ulijaribu kwenda kwake?” Aliuliza Mama yake, Noelaย alimtazama Mama yake kwa jicho la kukata tamaa kishaย akatikisa kichwa ishara ya kuwa hakwenda nyumbani kwa Joshuaย kisha alimwambia Mama yakeย
“Msichana wake wa kazi anasema hakurudi tokea alipotoka janaย asubuhi” Alijibu Noelaย
“Sasa atakuwa wapi na kwanini hapokei simu zako jamani”ย Alisema Mama yake Noelaย
“Mama tokea jana nimechanganikiwa kabisa, ngoja tuย nikapumzike maana nimeshindwa hata kufanya kazi leo kwasababuย yake” Alisema Noelaย
“Haya sawa Mwanangu! Usijali sana huwenda yupo bize” Alisemaย Mama yake Noela kisha Noela alionesha tabasamu feki akaelekeaย chumbani kwake.ย
Ndani ya jumba la kifahari la Desmond, alikuwa ndiyo anaamkaย kutoka usingizini, alikuwa amelala palepale sebleni kutokanaย na pombe kumzidia. Aliamka akiwa mchovu sana lakini alipoamkaย tu alitaja jina la Mke wake Mandy kisha alitafuta simu yakeย ambayo ilikuwa kando yake kisha akapiga Hospitalini kwa Nesiย Luciaย
“Vipi hali ya Mke wangu” Aliuliza Desmond huku akiwa na hofuย sana
“Mandy anaendelea na matibabu, bado hajapata ufahamu Desmond”ย ilisikika sauti kutoka upande wa pili, ilikuwa ni sauti yaย Nesi huyo iliyotoka kwa kubembeleza sanaย
“Asante! Kwa lolote unitaarifu mapema sana” Alisema Desmondย kisha alikata simu bila kusikiliza kingine kutoka kwa Luciaย
“Mandy kwanini hukufa? Kwanini upo hai? Kwa vyovyote vileย huwezi kutoboa siri nitakuuwa tu” Alisema Desmond kwa jazbaย kisha alikagua vizuri simu yake, alikutana na simu nyingiย ambazo hazikujibiwa, moja ilikuwa ya Noela, alikutana naย meseji nyingi kisha alitabasamu tu. Akaelekea kuoga kishaย alitoka kwenye jumba hilo ambalo alikuwa akiishi hapoย
Safari ya Desmond ilikuwa ni kuelekea nyumbani kwa Noela,ย kitendo cha Mama kusikia mlio wa gari kilimfanya achungulie,ย alipoliona gari la Desmond haraka alikimbilia chumbani kwaย Noela akamwambiaย
“Joshua amefika” Alisema Mama huyo, Noela hakuaminiย alichokisikia naye alikimbilia nje, alimuona Desmond ambayeย yeye alikuwa akimfahamu kwa jina la Joshua.ย
Alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha sana kisha choziย lilimbubujika, alionesha ni wazi kuwa alikuwa akimpenda sanaย Mwanaume huyo kisha alimuulizaย
“Joshua nimekutafuta sana ulikuwa wapi Mpenzi, nimeingiwa naย hofu mno” Desmond alicheka kidogoย
“Nimeamini kuwa unanipenda sana Noela, nilifanya kusudi iliย nipime upendo wako” Alisema Huyo aliyefahamika kwa jina laย Joshua lakini kule Hospitali alijulikana kama Desmond, hebuย tusonge na Uhondo wa Hadithi hii.ย
Mama yake Noela alisimama akiwaangalia wapendanao hao, kishaย moyo wake ulikubali kuwa walikuwa wakipendana sana,ย alitabasamu alafu akatangulia ndani huku Desmond ( Joshua )ย na Noela wakifuatia.ย
Walishinda hapo pamoja siku hiyo, walikula, walicheza pamojaย na kupeana mapenzi motomoto kisha baadaye waliondoka naย kuelekea kwenye nyumba ambayo Desmond alikuwa akiishi, hiiย ilikuwa ni nyumba tofauti na ile aliyokuwa akiishi na Mkeย wake.ย
TURUDI MIAKA KADHAA ILIYOPITA
Ndani ya Kijiji kimoja, kulikuwa na familia moja iliyoishiย kwa shida sana. Familia hii ilikuwa ya Watu wawili tu, Babaย na Mwanaye. Walikuwa wameketi nje ya Banda lao, ukimyaย ulikuwa umetawala sana hapo, Mtoto huyo mwenye miaka 11ย alimuuliza Baba yake.ย
“Baba tutaenda wapi?” Aliuliza akiwa anamtazama Bba yakeย aliyekaa juu ya gogo la Mtiย
“Unafikiria tutaenda wapi Desmond? Kifo cha Mama yakoย kimeleta mkosi sana kwetu kila kitu kimeharibika” Alisemaย Baba huyo, Mtoto huyo aliyeitwa Desmond ndiye huyu ambaye niย Mume wa Mandy aliyeko Hospitalini, kumbe jina lake halisi niย Desmond na siyo Joshua.ย
“Usiseme hivyo Baba! Huwenda Mungu alipanga iwe hivi” Alisemaย Mtoto Desmondย
“Alipanga tufukuzwe hapa Kijijini? Una mawazo ya kipumbavuย sana, huu ni mkosi aliouleta Mama yako!! Leo utakula Hizoย kauli zako” Alisema Baba yake huyo kisha aliondoka zake naย kumuacha Desmond akizidi kutafakari. Maisha yao yalikuwa Duniย sana, Desmond alidondosha chozi kisha alikimbilia kwenyeย kaburi la Mama yake ambalo halikuwa mbali na banda lao,ย alipiga magoti kisha alisemaย
“Mama si hujakosea si ndiyo? Kwanini Baba anakuhukumuย hivi….Mama nauchukia umasikini, nakuahidi sitokufaย masikini” Alisema Desmond kisha aliondoka kaburini hapo.ย
TURUDI MAISHA YA SASAย
Hiyo ilikuwa ni kumbukumbu ambayo Desmond alikuwa akiikumbukaย alipokuwa akiitazama picha ya pamoja aliyopiga na Mama yake.ย Aliichukua picha hiyo iliyo ndani ya waleti yake kishaย alisemaย
“Mama natamani ungekuwepo uone Maisha ninayoishi, nimekuwaย tajiri nina kila kitu ila sina Baba wala Mama, Baba yanguย alikufa kwa pombe kali….” Alipokuwa akiyasema maneno hayaย Noela alikuwa akiingia chumbani, Desmond hakushtuka kamaย Noela alikuwa ameingia, Noela alimsikia Desmond akisemaย
“Kipo kirusi Mama, nahangaika kukiondoa ili niwe huru zaidi”ย Alisema Desmond lakini ghafla alihisi kuna Mtu anamsikiliza,ย ni kweli alipogeuka alimuona Noela akiwa anamtazama, Desmondย alionekana kuwa mwenye siri nzito sana ndani yake, siriย ย ambayo hakutaka Mtu yeyote aijuwe huku lengo lake kuu likiwaย ni kumuuwa Mke wake.
“Kirusi? Ukiondoe?” Aliuliza Noela, Desmond alimtazama Noelaย kwa Makini sana akagundua alikuwa hajaelewa lakini macho yaย Desmond yalikuwa yakivujisha chozi, Noela alimpatia kitambaaย Desmond ili afute chozi hilo, aliketi akamuuliza tenaย
“Kirusi gani untaka ukiondoe?” Aliuliza Noela, Desmondย alifuta chozi kisha alimwambia Noelaย
“Mimi na marehemu Mama yangu tulikuweka ahadi kuwa nitakuwaย na pesa nyingi sana na pia nitaowa, pesa ninazo lakiniย sijaowa, kwangu nachukulia kama kirusi kwenye ahadi yangu”ย Alisema Desmond, Basi Noela alitabasamu tuย
“Kubali nikuowe Noela ili uwe wangu peke yangu, jinsiย ninavyokupenda nahisi Dunia yote nimeiweka kiganjani pangu”ย Yalikuwa ni maneno matamu sana aliyoyatoa Desmond iliย kumfanya Noela asihisi chochote kile, kweli Noela alihamaย kihisia akasahau kila kituย
“Naanzaje kukataa Joshua? Nipo tayari uniowe hata kesho.ย Nikikumbuka jinsi tulivyokutana moyo wangu unajawa na furahaย na amani sana. Nakupenda pia Joshua” Alisema Noela kishaย alimkumbatia Desmond.ย
Sura ya Desmond ilibadili taswira kutoka kutabasamu hadi kuwaย mtu aliye siriazi na jambo lililo akilini mwake.ย
Majukumu ya kazi yaliendelea kwa pande zote yaani kwa Desmondย na kwa upande wa Noela, kumpata Desmond kulimpa furaha sanaย Noela akawa anachapa kazi zake.ย
Mchana wa siku hiyo, Desmond alienda Hospitalini kamaย kawaida, alipewa nafasi ya kumuona Mke wake Mandy. Alikuwa naย hasira na Mwanamke huyo. Mandy alikuwa amepoteza fahamu kwaย zaidi ya miezi mitano hivyo kwa kipindi chote alikuwaย Hospitalini tu, Desmond alisogea akaketi kwenye kiti kimojaย ambacho kilikuwa kando ya kitanda cha Mke wake, alikunja nneย kisha akamwambia Mandyย
“Nina uhakika unanisikia Mandy! Katika vitu sitamani kuonaย katika Maisha yangu basi ni uhai wako, natamani uwe umekufaย na usiamke tena hapo Kitandani” Alisema Desmond akiwaย amevalia suti nyeusi zilizomkaa vizuri, alikuwa kijana mwenyeย muonekano mzuri sana. Desmond alisimama kisha alimsogeleaย Mandy
“Siri unayoijuwa kuhusu Mama yako ibaki kuwa siri yaย Ulimwengu mzima, sipo tayari kuyaharibu Maisha yanguย kwasababu yako. Asante kwa utajiri mkubwa ulioniachia Mandy,ย nasikitika sababu uliyemuamini siku zote hakuwa na mapenzi naย wewe, sikuwahi kukupenda Mandy….Nilizipenda pesa zako tu”ย Alisema Desmond kisha alivuta pumzi zake huku choziย likimlenga, licha ya uamuzi huo mgumu bado alionesha kuumiaย ndani ya Moyo wakeย
Ghafla aliona Mandy akitingisha kidole, hii ilimshtua sanaย Desmond, miezi yote Mandy hakuwahi kutingisha hata kope zaย macho yake, ilionesha wazi hata alichokizungumza Desmondย alikuwa akikisikia. Akiwa anaendelea kushangaa Desmond alionaย macho ya Mandy yakifunguka huku yakibubujikwa na mchozi,ย Mandy alikuwa ni Mwanamke mzuri mwenye weupe wa asili, choziย la Mandy lilionesha wazi kuwa lilibeba maumivu makali sanaย
“Mandy umeamka? Ina maana siri yangu utaisema!! Hapanaย Unakufa” Alisema Desmond ndani ya moyo wake huku akiwaย amevurugwa sana, aliangalia huku na kule kisha alichukua mtoย na kumziba pumzi Mandy ili afe pale kitandani. Mandyย alihangaika kwa nguvu chache aliyokuwa nayo lakini hakuwezaย kufanya lolote zaidi ya kuziona pumzi zake zikifika mwisho,ย Desmond alidhamiria kumuuwa Mandy mchana huo ili hiyo siriย yake isijulikane.ย
Mara Desmond alisikia chupa ikivunjika, alipogeuka alimuonaย nesi Lucia akiwa anaokota vipande vya vyupa pale mlangoni.ย Haraka aliacha jaribio la kutaka kumuuwa Mke wake Mandy.ย Aliuweka mto pembeni, alikuwa akitokwa na jasho jingi kishaย alimtazama Mandy alionekana kuzima, Desmond aligeuza machoย alimuona nesi Lucia akisogea hapoย
“ooh Desmond” Alisema Nesi Lucia huku akiwa anaweka vifaa juuย ya meza iliyo pembe ya ukuta, alipomtazama vizuri Desmondย alimuona akiwa anatokwa na jasho jingi sana, alishangaa kishaย alipeleka macho yake kwenye AC, kisha alirudisha kwa Desmond.ย Alionekana kushangaa jasho la Desmond lilitoka wapi ikiwaย chumba hicho kilikuwa hakina joto kabisaย
“Kulikoni Desmond mbona unavuja jasho hivyo” Aliuliza Nesiย Lucia akiwa anamtazama kwa makini Desmondย
“Aaah- aaah…Jasho….unajuwa!! Lucia sijisikii vizuriย naomba nipumzike nje” Alisema Desmond kisha alitoka lakiniย Nesi Lucia aliendelea kujiuliza maswali yasiyo na majibu,ย mwisho alipuuzia jambo hilo.
Alienda kumtazama Mandy, alionekana kupowa huku mapigo yaย moyo yakienda sawa kwa maana Desmond hakufanikiwa jaribio laย kuondoa uhai wa Mandy, alibadilisha dripu na kufanya mamboย mengine kisha naye alitoka. Hali ya Mandy haikujulikana kwaย wakati huo kuwa ataamka lini wala saa ngapi laiti kamaย taarifa ya kuamka kwake ingewafikia madaktari basi tumainiย lingekuwa kubwa sana.ย
Akiwa nje ya wodi ile, Desmond aliendelea kutafakari kuhusuย usalama wa Mandy, alifikiria kama Mandy alikuwa amekufa auย alikuwa hajafa na kama hajafa basi siri yake iliyojifichaย kuhusu Mama yake Mandy ingefichuka, akiwa hapo alisikia sautiย ikimuitaย
“Mr Desmond” Alipogeuka alimuona Mtu mmoja akiwa amemsimamia,ย alishtuka sana sababu hakutarajia kumuona Mtu huyo kwa wakatiย huoย
“Mbona umeshtuka au hukutarajia kuniona?” Alihoji Mtu huyoย aliyekuwa Mwanaume mwenye sauti nzitoย
“Hapana ila nilikuwa mawazoni ndiyo maana nimeshtuka” Alisemaย Desmond kisha aliketi vizuri ili Mwanaume huyo naye aketiย
“Hali ya Mkeo vipi?” Aliuliza Mwanaume huyoย
“Mke wangu anaendelea…Hali yake bado ipo vile vile” Alijibuย Desmondย
“Mkeo ni shahidi namba moja wa kifo cha Mama yake, mara yaย mwisho alituma ujumbe kituo cha polisi kuwa anamjuwa Muuwajiย wa Mama yake, baada ya hapo ndiyo tukio la wewe kupigwaย risasi na Mke wako kupigizwa ukutani lilipotokea, Mkeo ni Mtuย muhimu zaidi katika kesi ile” Alisema Mwanaume huyo ambayeย sasa alitambulika kuwa ni askariย
“Yaah! Ni kweli, ilikuwa ni siku ngumu sana katika Maishaย yangu ni kama nilimpoteza Mke wangu tokea siku ile hadi hiviย leo” Alijikakamua Desmond kisha alijibu, huyu Desmondย alionekana wazi kutambua juu ya kifo cha Mama yake Mandyย lakini kwanini hakutaka ukweli uwekwe wazi? Au yeye ndiyeย aliyemuuwa Mama yake Mandy? Kwanini Amuuwe? TUSONGE MBELEย
“Kwa lolote usisite kutujulisha Mr. Desmond” Alisema Askariย huyo kisha aliondoka hapo. Kumbe nesi Lucia alikuwaย anamuangalia Desmond akizungumza na polisi kisha alipoondokaย yeye alimfuata Desmond alipokaa
“Desmond najuwa unavyojisikia, najuwa unaumia sana lakiniย Mkeo atakuwa sawa tu siku moja mtarudi kuwa kama zamani”ย Alisema Nesi Lucia, Desmond alimtazama Lucia kisha alijisemeaย moyoniย
“Ungejuwa ninavyotamani afe wala usingesema hayo maneno”ย Kabla hajamjibu chochote Lucia alipokea simu ya Noelaย
“Hello” Alisema Desmond baada ya kupokea simu hiyoย
“Desmond nakusubiria Mgahawani” Alisema Noela kisha Desmondย alijibuย
“Sawa nakuja”ย
“Unaenda wapi?” Alihoji Luciaย
“Mjini”ย
“Hata mimi ninaenda huko kwa ajili ya chakula, tafadhali nipeย lifti” Alisema Luciaย
“Haya sawa!” alisema Desmond kisha waliongozana hadi kwenyeย gari ya Desmond na safari ya Kuelekea Mjini ilianza.ย
Wakiwa barabarani Nesi Lucia macho yake yote yalikuwa kwaย Desmond, alimpenda sana Mwanaume huyo lakini alishindwaย kumwambia sababu alikuwa Mume wa Mtu istoshe alikuwaย akimuuguza Mke wake huyo.ย
Desmond aligundua hilo akamuuliza Luciaย
“Kwanini unaniangalia hivyo?”ย
“Desmond wewe ni Mzuri sana, Hakika Mke wako anajivunia kuwaย na Mwanaume kama Wewe” Alisema Lucia kisha Desmondย alitabasamu kidogo alafu hakusema chochote kile hadi anafikaย eneo ambalo Lucia alikuwa akienda. Ilikuwa ni kwenye mgahawaย huo huo ambao Desmond alienda kukutana na Mpenzi wake Noelaย
“Eeeh ajabu kumbe nawe ulikuwa unakuja hapa?” Aliulizaย
“Yaah! Kuna Mtu naonana naye mara moja kisha niendelee naย majukumu mengine”ย
“Haya asante kwa Lifti” Alisema Lucia kisha alishuka akaingiaย kwenye mgahawa huo ambao ulikuwa wenye hadhi kubwa na piaย ulikuwa mkubwa mno, Desmond alienda mahali ambapo alipangaย kuonana na Noela.ย
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA PILIย
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xxย
11 Comments
Hakika hujawahi kutuangusha
Well done
Love and Pain
Inaonyesha ni Story nzito yenye burudani na Mafunzo ndani yake.
Asante sana Kaka Mkubwa
More Love from Kenya โฅ๏ธ
NAOMBA KWA SIKU ZIWE SEHEMU 2.
Kali sana
Dah..imeanz kwa kusisimua san
Nice
๐
Mr KIJIWENI uyo ni
Diamondi na Nandy
๐๐
Mbona story nzur sana iih
well done
๐จ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ฅ๐ฅ๐