Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Love&Pain Sehemu Ya Kwanza (01)
    Hadithi

    Love&Pain Sehemu Ya Kwanza (01)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaNovember 8, 2024Updated:November 21, 202411 Comments14 Mins Read5K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Love & Pain
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Usiku mmoja, Mwanaume mmoja alikuwa akitoka Hospitalini,Β  alionekana kwenda hapo kwa ajili ya kumuona Mtu mmojaΒ  aliyemfahamu sana tena alikuwa Mtu wa karibu sana kwake.Β  Mwanaume huyo alionekana kuwa mwenye mawazo fulani kichwaniΒ  pake, alikuwa amevalia koti la suti na jinzi chini akipigiliaΒ  raba kali yenye mg’ao.Β 

    Ilitosha kujiridhisha kuwa Mwanaume huyo alikuwa na hela zaΒ  kutosha, tembea yake ilikuwa ya taratibu mno, ukimtazamaΒ  vizuri utagundua alikuwa na vita kichwani pake, alipofikaΒ  kwenye korido aligeuka na kutazama nyuma kisha alitaja jinaΒ  mojaΒ 

    “Mandy!” Alilitaja jina hilo kisha alihema kiasi, kishaΒ  aliendelea mbele kuuelekea mlango wa kutoka Hospitalini hapo.Β  Alikutana na nesi mmoja akiwa amebakisha hatua chache kutoka,Β  nesi huyo alimuita Mwanaume huyo jina lakeΒ 

    “Desmond!!” Alipomuita ni kama alimzindua kutoka Mawazoni,Β  Mwanaume huyo aliyeitwa Desmond alijichekesha kidogo kabla yaΒ  kusalimiana na nesi huyoΒ 

    “Aaah!! Lucia, Habari yako!” Alisalimia DesmondΒ 

    “Nzuri mbona una mawazo hivyo au kuna taarifa yoyote mbayaΒ  kumuhusu Mandy?” Aliuliza nesi huyo aliyeonesha kumfahamuΒ  Vizuri DesmondΒ 

    “Aaah! Hapana hali yake ipo vilevile, nimechoka tu naΒ  majukumu ya hapa na pale” Alisema DesmondΒ 

    “Pamoja na yote Desmond, wewe ni Mwanaume mzuri sana, unajaliΒ  mno maana huishi kuja kumuona Mandy kwa kipindi chote ambachoΒ  amekuwa hapa” Alisema LuciaΒ 

    “Ndiyo jukumu langu, nahitaji kwenda sasa” Alisema Desmond,Β  waliagana hapo kisha Desmond aliondoka zake huku LuciaΒ  akimtazama Desmond kwa jicho la kuhitaji kumwambia kituΒ  lakini alishindwa.

    Yalikuwa ni majira ya saa tano za Usiku, muda huo mvuaΒ  ilianza kuchapa kidogo na kumfanya Desmond akimbilie kwenyeΒ  gari yake, aliondoka Hospitalini hapo Usiku huo huku akiwaΒ  kwenye gari alionekana kukumbuka jambo liliomuumiza, sauti yaΒ  daktari ilijirudia kichwani pakeΒ 

    “Mandy anaweza kupata ufahamu ndani ya siku chache zijazo,Β  hii ni habari njema Desmond” Alionekana kutofurahishwa naΒ  taarifa ya Mgonjwa huyo kuwa sawa, alipiga usukani kwa hasiraΒ  kisha alielekea moja kwa moja kwenye jumba lake la kifahariΒ  lililopo karibu na fukwe, ndipo alipokuwa akiishi.Β 

    Alipoingia alitazama ukutani, aliiyona picha aliyopiga yeyeΒ  na huyo Mgonjwa aliyeitwa Mandy, mgonjwa huyo alikuwa waΒ  kike, picha hiyo ilieleza kuhusu Mandy na Desmond, Naam!Β  Walikuwa ni wana ndoa, Desmond aliitoa picha hiyo akaitupaΒ  kutoka juu ya ghorofa hilo hadi chiniΒ 

    “Mandy huwezi kuwa hai tena ni lazima nikumalize” AlisemaΒ  Desmond kwa hasira na hisia kali huku akionesha wazi kuwaΒ  kulikuwa na jambo ambalo lilijificha kuhusu Yeye na mke wakeΒ  huyo aliyeitwa Mandy.Β 

    Alikunywa pombe sana usiku huo huku simu yake ikiwa bizeΒ  kuita lakini hakuipokea kabisa, alikunywa na kulewa sanaΒ  akawa hajitambui, alilala hapo sebleni hadi asubuhi.Β 

    **********Β 

    Ilikuwa ni asubuhi ya siku iliyofuata, ndani ya ofisi mojaΒ  alikuwepo Mwanamke mzuri sana aliyeitwa Noela, Mwanamke huyuΒ  alikuwa ni Mwanasheria. Alikuwa akifanya kazi yake hapoΒ  ofisini huku akili yake ikionesha wazi kuwa haikuwa naΒ  utulivu, mara zote alikuwa akijaribu kupiga simu bilaΒ  kupokelewa, baadaye alikuja jamaa mmoja aliyeitwa Zanda,Β  walikuwa ni marafiki waliokuwa wakifanya kazi ofisi moja yaΒ  Wanasheria wa kujitegemea, mara moja Zanda aligundua NoelaΒ  hakuwa sawa aliketi akamuulizaΒ 

    “Vipi Noela una tatizo?” Alihoji Zanda huku akimtazama UsoniΒ  NoelaΒ 

    “Aaah! Nipo sawa Zanda usijali” Alijibu NoelaΒ 

    “Noela nimefanya kazi na wewe kwa muda mrefu hivyo nakujuwaΒ  vizuri sana, leo haupo sawa” Alisistiza Zanda, NoelaΒ  alimkubalia Zanda kuwa hayupo sawa ila ni mambo madogo tuΒ  atayatatua.

    Baada ya kupita muda kidogo Noela aliondoka ofisini akiagaΒ  kuwa anajisikia vibaya. Zanda alimshangaa sana Noela,Β  alimkodolea macho akiwa anaondoka na gari yake kishaΒ  alitikisa kichwa chake, Noela aliendelea kupiga simu bilaΒ  kupokea majibu yoyote yale hadi anafika nyumbani kwao,Β  alikuwa akiishi na Mama yake Mzazi ambaye alipendelea sanaΒ  kumuita MlamiΒ 

    Mama yake ( Mlami ) aligundua haraka kuwa Noela hayupo sawaΒ  kifikra, alimuuliza akiwa amejilaza sofaniΒ 

    “Kuna nini Noela huonekani kuwa sawa kabisa, unaonekana niΒ  mwenye mawazo mengi kichwani mwako” Alihoji Mama yake NoelaΒ  huku akimkata jicho la udadisi binti yake huyo wa pekeeΒ  ambaye alikuwa akimpenda sana baada ya Baba yake kufariki.Β 

    “Ni Joshua Mama, tokea jana hapokei simu zangu. Sijui yukoΒ  wapi” Alijibu Noela kama vile alikuwa amechokozwa na MamaΒ  yake, alimpigia tena huyo JoshuaΒ 

    “Ulijaribu kwenda kwake?” Aliuliza Mama yake, NoelaΒ  alimtazama Mama yake kwa jicho la kukata tamaa kishaΒ  akatikisa kichwa ishara ya kuwa hakwenda nyumbani kwa JoshuaΒ  kisha alimwambia Mama yakeΒ 

    “Msichana wake wa kazi anasema hakurudi tokea alipotoka janaΒ  asubuhi” Alijibu NoelaΒ 

    “Sasa atakuwa wapi na kwanini hapokei simu zako jamani”Β  Alisema Mama yake NoelaΒ 

    “Mama tokea jana nimechanganikiwa kabisa, ngoja tuΒ  nikapumzike maana nimeshindwa hata kufanya kazi leo kwasababuΒ  yake” Alisema NoelaΒ 

    “Haya sawa Mwanangu! Usijali sana huwenda yupo bize” AlisemaΒ  Mama yake Noela kisha Noela alionesha tabasamu feki akaelekeaΒ  chumbani kwake.Β 

    Ndani ya jumba la kifahari la Desmond, alikuwa ndiyo anaamkaΒ  kutoka usingizini, alikuwa amelala palepale sebleni kutokanaΒ  na pombe kumzidia. Aliamka akiwa mchovu sana lakini alipoamkaΒ  tu alitaja jina la Mke wake Mandy kisha alitafuta simu yakeΒ  ambayo ilikuwa kando yake kisha akapiga Hospitalini kwa NesiΒ  LuciaΒ 

    “Vipi hali ya Mke wangu” Aliuliza Desmond huku akiwa na hofuΒ  sana

    “Mandy anaendelea na matibabu, bado hajapata ufahamu Desmond”Β  ilisikika sauti kutoka upande wa pili, ilikuwa ni sauti yaΒ  Nesi huyo iliyotoka kwa kubembeleza sanaΒ 

    “Asante! Kwa lolote unitaarifu mapema sana” Alisema DesmondΒ  kisha alikata simu bila kusikiliza kingine kutoka kwa LuciaΒ 

    “Mandy kwanini hukufa? Kwanini upo hai? Kwa vyovyote vileΒ  huwezi kutoboa siri nitakuuwa tu” Alisema Desmond kwa jazbaΒ  kisha alikagua vizuri simu yake, alikutana na simu nyingiΒ  ambazo hazikujibiwa, moja ilikuwa ya Noela, alikutana naΒ  meseji nyingi kisha alitabasamu tu. Akaelekea kuoga kishaΒ  alitoka kwenye jumba hilo ambalo alikuwa akiishi hapoΒ 

    Safari ya Desmond ilikuwa ni kuelekea nyumbani kwa Noela,Β  kitendo cha Mama kusikia mlio wa gari kilimfanya achungulie,Β  alipoliona gari la Desmond haraka alikimbilia chumbani kwaΒ  Noela akamwambiaΒ 

    “Joshua amefika” Alisema Mama huyo, Noela hakuaminiΒ  alichokisikia naye alikimbilia nje, alimuona Desmond ambayeΒ  yeye alikuwa akimfahamu kwa jina la Joshua.Β 

    Alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha sana kisha choziΒ  lilimbubujika, alionesha ni wazi kuwa alikuwa akimpenda sanaΒ  Mwanaume huyo kisha alimuulizaΒ 

    “Joshua nimekutafuta sana ulikuwa wapi Mpenzi, nimeingiwa naΒ  hofu mno” Desmond alicheka kidogoΒ 

    “Nimeamini kuwa unanipenda sana Noela, nilifanya kusudi iliΒ  nipime upendo wako” Alisema Huyo aliyefahamika kwa jina laΒ  Joshua lakini kule Hospitali alijulikana kama Desmond, hebuΒ  tusonge na Uhondo wa Hadithi hii.Β 

    Mama yake Noela alisimama akiwaangalia wapendanao hao, kishaΒ  moyo wake ulikubali kuwa walikuwa wakipendana sana,Β  alitabasamu alafu akatangulia ndani huku Desmond ( Joshua )Β  na Noela wakifuatia.Β 

    Walishinda hapo pamoja siku hiyo, walikula, walicheza pamojaΒ  na kupeana mapenzi motomoto kisha baadaye waliondoka naΒ  kuelekea kwenye nyumba ambayo Desmond alikuwa akiishi, hiiΒ  ilikuwa ni nyumba tofauti na ile aliyokuwa akiishi na MkeΒ  wake.Β 

    TURUDI MIAKA KADHAA ILIYOPITA

    Ndani ya Kijiji kimoja, kulikuwa na familia moja iliyoishiΒ  kwa shida sana. Familia hii ilikuwa ya Watu wawili tu, BabaΒ  na Mwanaye. Walikuwa wameketi nje ya Banda lao, ukimyaΒ  ulikuwa umetawala sana hapo, Mtoto huyo mwenye miaka 11Β  alimuuliza Baba yake.Β 

    “Baba tutaenda wapi?” Aliuliza akiwa anamtazama Bba yakeΒ  aliyekaa juu ya gogo la MtiΒ 

    “Unafikiria tutaenda wapi Desmond? Kifo cha Mama yakoΒ  kimeleta mkosi sana kwetu kila kitu kimeharibika” AlisemaΒ  Baba huyo, Mtoto huyo aliyeitwa Desmond ndiye huyu ambaye niΒ  Mume wa Mandy aliyeko Hospitalini, kumbe jina lake halisi niΒ  Desmond na siyo Joshua.Β 

    “Usiseme hivyo Baba! Huwenda Mungu alipanga iwe hivi” AlisemaΒ  Mtoto DesmondΒ 

    “Alipanga tufukuzwe hapa Kijijini? Una mawazo ya kipumbavuΒ  sana, huu ni mkosi aliouleta Mama yako!! Leo utakula HizoΒ  kauli zako” Alisema Baba yake huyo kisha aliondoka zake naΒ  kumuacha Desmond akizidi kutafakari. Maisha yao yalikuwa DuniΒ  sana, Desmond alidondosha chozi kisha alikimbilia kwenyeΒ  kaburi la Mama yake ambalo halikuwa mbali na banda lao,Β  alipiga magoti kisha alisemaΒ 

    “Mama si hujakosea si ndiyo? Kwanini Baba anakuhukumuΒ  hivi….Mama nauchukia umasikini, nakuahidi sitokufaΒ  masikini” Alisema Desmond kisha aliondoka kaburini hapo.Β 

    TURUDI MAISHA YA SASAΒ 

    Hiyo ilikuwa ni kumbukumbu ambayo Desmond alikuwa akiikumbukaΒ  alipokuwa akiitazama picha ya pamoja aliyopiga na Mama yake.Β  Aliichukua picha hiyo iliyo ndani ya waleti yake kishaΒ  alisemaΒ 

    “Mama natamani ungekuwepo uone Maisha ninayoishi, nimekuwaΒ  tajiri nina kila kitu ila sina Baba wala Mama, Baba yanguΒ  alikufa kwa pombe kali….” Alipokuwa akiyasema maneno hayaΒ  Noela alikuwa akiingia chumbani, Desmond hakushtuka kamaΒ  Noela alikuwa ameingia, Noela alimsikia Desmond akisemaΒ 

    “Kipo kirusi Mama, nahangaika kukiondoa ili niwe huru zaidi”Β  Alisema Desmond lakini ghafla alihisi kuna Mtu anamsikiliza,Β  ni kweli alipogeuka alimuona Noela akiwa anamtazama, DesmondΒ  alionekana kuwa mwenye siri nzito sana ndani yake, siriΒ Β ambayo hakutaka Mtu yeyote aijuwe huku lengo lake kuu likiwaΒ  ni kumuuwa Mke wake.

    “Kirusi? Ukiondoe?” Aliuliza Noela, Desmond alimtazama NoelaΒ  kwa Makini sana akagundua alikuwa hajaelewa lakini macho yaΒ  Desmond yalikuwa yakivujisha chozi, Noela alimpatia kitambaaΒ  Desmond ili afute chozi hilo, aliketi akamuuliza tenaΒ 

    “Kirusi gani untaka ukiondoe?” Aliuliza Noela, DesmondΒ  alifuta chozi kisha alimwambia NoelaΒ 

    “Mimi na marehemu Mama yangu tulikuweka ahadi kuwa nitakuwaΒ  na pesa nyingi sana na pia nitaowa, pesa ninazo lakiniΒ  sijaowa, kwangu nachukulia kama kirusi kwenye ahadi yangu”Β  Alisema Desmond, Basi Noela alitabasamu tuΒ 

    “Kubali nikuowe Noela ili uwe wangu peke yangu, jinsiΒ  ninavyokupenda nahisi Dunia yote nimeiweka kiganjani pangu”Β  Yalikuwa ni maneno matamu sana aliyoyatoa Desmond iliΒ  kumfanya Noela asihisi chochote kile, kweli Noela alihamaΒ  kihisia akasahau kila kituΒ 

    “Naanzaje kukataa Joshua? Nipo tayari uniowe hata kesho.Β  Nikikumbuka jinsi tulivyokutana moyo wangu unajawa na furahaΒ  na amani sana. Nakupenda pia Joshua” Alisema Noela kishaΒ  alimkumbatia Desmond.Β 

    Sura ya Desmond ilibadili taswira kutoka kutabasamu hadi kuwaΒ  mtu aliye siriazi na jambo lililo akilini mwake.Β 

    Majukumu ya kazi yaliendelea kwa pande zote yaani kwa DesmondΒ  na kwa upande wa Noela, kumpata Desmond kulimpa furaha sanaΒ  Noela akawa anachapa kazi zake.Β 

    Mchana wa siku hiyo, Desmond alienda Hospitalini kamaΒ  kawaida, alipewa nafasi ya kumuona Mke wake Mandy. Alikuwa naΒ  hasira na Mwanamke huyo. Mandy alikuwa amepoteza fahamu kwaΒ  zaidi ya miezi mitano hivyo kwa kipindi chote alikuwaΒ  Hospitalini tu, Desmond alisogea akaketi kwenye kiti kimojaΒ  ambacho kilikuwa kando ya kitanda cha Mke wake, alikunja nneΒ  kisha akamwambia MandyΒ 

    “Nina uhakika unanisikia Mandy! Katika vitu sitamani kuonaΒ  katika Maisha yangu basi ni uhai wako, natamani uwe umekufaΒ  na usiamke tena hapo Kitandani” Alisema Desmond akiwaΒ  amevalia suti nyeusi zilizomkaa vizuri, alikuwa kijana mwenyeΒ  muonekano mzuri sana. Desmond alisimama kisha alimsogeleaΒ  Mandy

    “Siri unayoijuwa kuhusu Mama yako ibaki kuwa siri yaΒ  Ulimwengu mzima, sipo tayari kuyaharibu Maisha yanguΒ  kwasababu yako. Asante kwa utajiri mkubwa ulioniachia Mandy,Β  nasikitika sababu uliyemuamini siku zote hakuwa na mapenzi naΒ  wewe, sikuwahi kukupenda Mandy….Nilizipenda pesa zako tu”Β  Alisema Desmond kisha alivuta pumzi zake huku choziΒ  likimlenga, licha ya uamuzi huo mgumu bado alionesha kuumiaΒ  ndani ya Moyo wakeΒ 

    Ghafla aliona Mandy akitingisha kidole, hii ilimshtua sanaΒ  Desmond, miezi yote Mandy hakuwahi kutingisha hata kope zaΒ  macho yake, ilionesha wazi hata alichokizungumza DesmondΒ  alikuwa akikisikia. Akiwa anaendelea kushangaa Desmond alionaΒ  macho ya Mandy yakifunguka huku yakibubujikwa na mchozi,Β  Mandy alikuwa ni Mwanamke mzuri mwenye weupe wa asili, choziΒ  la Mandy lilionesha wazi kuwa lilibeba maumivu makali sanaΒ 

    “Mandy umeamka? Ina maana siri yangu utaisema!! HapanaΒ  Unakufa” Alisema Desmond ndani ya moyo wake huku akiwaΒ  amevurugwa sana, aliangalia huku na kule kisha alichukua mtoΒ  na kumziba pumzi Mandy ili afe pale kitandani. MandyΒ  alihangaika kwa nguvu chache aliyokuwa nayo lakini hakuwezaΒ  kufanya lolote zaidi ya kuziona pumzi zake zikifika mwisho,Β  Desmond alidhamiria kumuuwa Mandy mchana huo ili hiyo siriΒ  yake isijulikane.Β 

    Mara Desmond alisikia chupa ikivunjika, alipogeuka alimuonaΒ  nesi Lucia akiwa anaokota vipande vya vyupa pale mlangoni.Β  Haraka aliacha jaribio la kutaka kumuuwa Mke wake Mandy.Β  Aliuweka mto pembeni, alikuwa akitokwa na jasho jingi kishaΒ  alimtazama Mandy alionekana kuzima, Desmond aligeuza machoΒ  alimuona nesi Lucia akisogea hapoΒ 

    “ooh Desmond” Alisema Nesi Lucia huku akiwa anaweka vifaa juuΒ  ya meza iliyo pembe ya ukuta, alipomtazama vizuri DesmondΒ  alimuona akiwa anatokwa na jasho jingi sana, alishangaa kishaΒ  alipeleka macho yake kwenye AC, kisha alirudisha kwa Desmond.Β  Alionekana kushangaa jasho la Desmond lilitoka wapi ikiwaΒ  chumba hicho kilikuwa hakina joto kabisaΒ 

    “Kulikoni Desmond mbona unavuja jasho hivyo” Aliuliza NesiΒ  Lucia akiwa anamtazama kwa makini DesmondΒ 

    “Aaah- aaah…Jasho….unajuwa!! Lucia sijisikii vizuriΒ  naomba nipumzike nje” Alisema Desmond kisha alitoka lakiniΒ  Nesi Lucia aliendelea kujiuliza maswali yasiyo na majibu,Β  mwisho alipuuzia jambo hilo.

    Alienda kumtazama Mandy, alionekana kupowa huku mapigo yaΒ  moyo yakienda sawa kwa maana Desmond hakufanikiwa jaribio laΒ  kuondoa uhai wa Mandy, alibadilisha dripu na kufanya mamboΒ  mengine kisha naye alitoka. Hali ya Mandy haikujulikana kwaΒ  wakati huo kuwa ataamka lini wala saa ngapi laiti kamaΒ  taarifa ya kuamka kwake ingewafikia madaktari basi tumainiΒ  lingekuwa kubwa sana.Β 

    Akiwa nje ya wodi ile, Desmond aliendelea kutafakari kuhusuΒ  usalama wa Mandy, alifikiria kama Mandy alikuwa amekufa auΒ  alikuwa hajafa na kama hajafa basi siri yake iliyojifichaΒ  kuhusu Mama yake Mandy ingefichuka, akiwa hapo alisikia sautiΒ  ikimuitaΒ 

    “Mr Desmond” Alipogeuka alimuona Mtu mmoja akiwa amemsimamia,Β  alishtuka sana sababu hakutarajia kumuona Mtu huyo kwa wakatiΒ  huoΒ 

    “Mbona umeshtuka au hukutarajia kuniona?” Alihoji Mtu huyoΒ  aliyekuwa Mwanaume mwenye sauti nzitoΒ 

    “Hapana ila nilikuwa mawazoni ndiyo maana nimeshtuka” AlisemaΒ  Desmond kisha aliketi vizuri ili Mwanaume huyo naye aketiΒ 

    “Hali ya Mkeo vipi?” Aliuliza Mwanaume huyoΒ 

    “Mke wangu anaendelea…Hali yake bado ipo vile vile” AlijibuΒ  DesmondΒ 

    “Mkeo ni shahidi namba moja wa kifo cha Mama yake, mara yaΒ  mwisho alituma ujumbe kituo cha polisi kuwa anamjuwa MuuwajiΒ  wa Mama yake, baada ya hapo ndiyo tukio la wewe kupigwaΒ  risasi na Mke wako kupigizwa ukutani lilipotokea, Mkeo ni MtuΒ  muhimu zaidi katika kesi ile” Alisema Mwanaume huyo ambayeΒ  sasa alitambulika kuwa ni askariΒ 

    “Yaah! Ni kweli, ilikuwa ni siku ngumu sana katika MaishaΒ  yangu ni kama nilimpoteza Mke wangu tokea siku ile hadi hiviΒ  leo” Alijikakamua Desmond kisha alijibu, huyu DesmondΒ  alionekana wazi kutambua juu ya kifo cha Mama yake MandyΒ  lakini kwanini hakutaka ukweli uwekwe wazi? Au yeye ndiyeΒ  aliyemuuwa Mama yake Mandy? Kwanini Amuuwe? TUSONGE MBELEΒ 

    “Kwa lolote usisite kutujulisha Mr. Desmond” Alisema AskariΒ  huyo kisha aliondoka hapo. Kumbe nesi Lucia alikuwaΒ  anamuangalia Desmond akizungumza na polisi kisha alipoondokaΒ  yeye alimfuata Desmond alipokaa

    “Desmond najuwa unavyojisikia, najuwa unaumia sana lakiniΒ  Mkeo atakuwa sawa tu siku moja mtarudi kuwa kama zamani”Β  Alisema Nesi Lucia, Desmond alimtazama Lucia kisha alijisemeaΒ  moyoniΒ 

    “Ungejuwa ninavyotamani afe wala usingesema hayo maneno”Β  Kabla hajamjibu chochote Lucia alipokea simu ya NoelaΒ 

    “Hello” Alisema Desmond baada ya kupokea simu hiyoΒ 

    “Desmond nakusubiria Mgahawani” Alisema Noela kisha DesmondΒ  alijibuΒ 

    “Sawa nakuja”Β 

    “Unaenda wapi?” Alihoji LuciaΒ 

    “Mjini”Β 

    “Hata mimi ninaenda huko kwa ajili ya chakula, tafadhali nipeΒ  lifti” Alisema LuciaΒ 

    “Haya sawa!” alisema Desmond kisha waliongozana hadi kwenyeΒ  gari ya Desmond na safari ya Kuelekea Mjini ilianza.Β 

    Wakiwa barabarani Nesi Lucia macho yake yote yalikuwa kwaΒ  Desmond, alimpenda sana Mwanaume huyo lakini alishindwaΒ  kumwambia sababu alikuwa Mume wa Mtu istoshe alikuwaΒ  akimuuguza Mke wake huyo.Β 

    Desmond aligundua hilo akamuuliza LuciaΒ 

    “Kwanini unaniangalia hivyo?”Β 

    “Desmond wewe ni Mzuri sana, Hakika Mke wako anajivunia kuwaΒ  na Mwanaume kama Wewe” Alisema Lucia kisha DesmondΒ  alitabasamu kidogo alafu hakusema chochote kile hadi anafikaΒ  eneo ambalo Lucia alikuwa akienda. Ilikuwa ni kwenye mgahawaΒ  huo huo ambao Desmond alienda kukutana na Mpenzi wake NoelaΒ 

    “Eeeh ajabu kumbe nawe ulikuwa unakuja hapa?” AliulizaΒ 

    “Yaah! Kuna Mtu naonana naye mara moja kisha niendelee naΒ  majukumu mengine”Β 

    “Haya asante kwa Lifti” Alisema Lucia kisha alishuka akaingiaΒ  kwenye mgahawa huo ambao ulikuwa wenye hadhi kubwa na piaΒ  ulikuwa mkubwa mno, Desmond alienda mahali ambapo alipangaΒ  kuonana na Noela.Β 

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA PILIΒ 

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

    Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xxΒ 

    Love&Pain Simulizi ya Love&Pain

    11 Comments

    1. Sir yowas on November 8, 2024 3:35 pm

      Hakika hujawahi kutuangusha

      Reply
      • G shirima on November 8, 2024 11:12 pm

        Well done

        Reply
    2. Fawziya Hassan on November 8, 2024 4:01 pm

      Love and Pain
      Inaonyesha ni Story nzito yenye burudani na Mafunzo ndani yake.
      Asante sana Kaka Mkubwa
      More Love from Kenya β™₯️
      NAOMBA KWA SIKU ZIWE SEHEMU 2.

      Reply
    3. John Didas on November 8, 2024 4:22 pm

      Kali sana

      Reply
    4. Angel on November 8, 2024 8:53 pm

      Dah..imeanz kwa kusisimua san

      Reply
    5. Massay on November 8, 2024 9:10 pm

      Nice

      Reply
    6. Ander on November 8, 2024 11:17 pm

      πŸ‘

      Reply
    7. Sharo love malkx πŸ’– on November 9, 2024 11:05 am

      Mr KIJIWENI uyo ni
      Diamondi na Nandy
      πŸ‘πŸ‘

      Reply
    8. Hamis on November 10, 2024 2:37 pm

      Mbona story nzur sana iih

      Reply
    9. ZEDIX mg on November 11, 2024 9:33 am

      well done

      Reply
    10. Michael on November 13, 2024 2:56 pm

      π‘¨π’Šπ’”π’†π’†π’† π’Žπ’π’•π’πŸ’₯πŸ’₯πŸ‘Œ

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneΒ  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.