Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Love & Pain Sehemu Ya Saba (07)
    Hadithi

    Love & Pain Sehemu Ya Saba (07)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaNovember 18, 2024Updated:November 25, 20247 Comments12 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Love & Pain
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Kumbukumbu ya Desmond iliishia hapo, alitikisa kichwa chakeΒ  kisha alielekea ofisini kwa Daktari wa Hospitali, DaktariΒ  alipomuona Desmond alijuwa nini kimemleta, Desmond alianzaΒ  kumshambulia Daktari huyo kwa manenoΒ 

    “Umeagiza Mke wangu apelekwe Wodi nyingine alafu MimiΒ  nizuiliwe kumuona si ndiyo? Hivi unajuwa ulichokifanya?”Β  Alisema Desmond kwa hasiraΒ 

    “Desmond hebu kaa kwanza tuongee, hili jambo siyo laΒ  kulichukulia jazba, tulichofanya ni kupandisha darajaΒ  matibabu ya Mkeo ili aweze kuamka haraka ” Alisema DaktariΒ  huyo kwa upole sana . EndeleaΒ 

    SEHEMU YA SABA

    “Kuamka haraka? Unajipa kazi ya Mungu si ndiyo? UnafikiriΒ  Mimi sitaki Mke wangu aamke haraka? Nataka ila mlipaswaΒ  kunishirikisha na sio sahihi kunizuia mimi kumuona MkeΒ  wangu…Nitamuhamisha kwenye Hospitali hii haraka sana”Β  Alisema DesmondΒ 

    “Desmond naomba unielewe, Mkeo utamuona lakini siyo kamaΒ  zamani kutokana na aina ya matibabu ya sasa pia wodiΒ  aliyopelekwa, nakuomba uwe mpole. Muhimu Ni afya ya MkeoΒ  Desmond” Alisema Daktari lakini Desmond alizidi kuwa juuΒ 

    “Natoa siku mbili Mke wangu awe amerudishwa kwenye wodi yakeΒ  aliyokuwa akikaa, vinginevyo nitamuhamisha hapa” AlisistizaΒ  Desmond kisha aliondoka zake, lakini Daktari aliwaza sanaΒ  ikiwa Desmond anampenda mke wake kwanini akatae asipatiweΒ  matibabu kwenye wodi mpya? Kama gharama mbona wao niΒ  Mabilionea wakubwa tuΒ 

    Alipata wazo la kumtafuta Lucia ambaye alitoa wazo la Mke waΒ  Desmond kuhamishwa Wodi na kupewa huduma za daraja la juuuΒ  zaidi, alimpigia simu akamwambia wakutane nyuma ya HospitaliΒ  hiyo mahali ambapo palikuwa na Bustani.Β 

    Mara moja walikutana huko, Daktari akataka kujuwa niniΒ  ambacho kilikuwa kikiendelea na kwanini Lucia alitoa wazoΒ  lile, ilionekana kuwa ni swali gumu sana kwa Lucia kumjibuΒ  Daktari huyo akamwambiaΒ 

    “Ni kwasababu ni Mgonjwa wangu ndiyo maana nilitaka apeweΒ  matibabu ya haraka ili kumuamsha mapema” Alijibu akiwaΒ  anatazama chini lakini akili ya uzee ya Dakatari MkuuΒ  ilimwambia kuwa Lucia alikuwa na jambo lingine kabisaΒ 

    “Unajuwa fika kuwa unaniongopea Lucia…Niambie ukweli, LuciaΒ  wewe ni kama Binti yangu wa kumzaa tena hata Mjukuu wangu,Β  sura yako inaonesha dhahiri kuwa unnificha jambo…nyuma yaΒ  pazia kuna nini?” Aliuliza tena Daktari huyo, alimpa nafasiΒ  Lucia afikirie nini cha kufanya, mwishowe aliona ni boraΒ  amfungukie daktari huyo, alimwambiaΒ 

    “Nina mashaka Desmond akawa siyo Mtu mzuri kwa Mke wakeΒ  Mandy, juzi alikuja na mwasheria akamsainisha Mgonjwa kwaΒ  alama za vidole, nilipouliza nilijibiwa kuwa sipaswiΒ  kuingilia masuala ya kifamilia” Alieleza LuiciaΒ 

    “Una uhakika?”Β 

    “Nina uhakika na ndiyo sababu ya kukuonba Mkuu mgonjwaΒ  ahamishwe daraja”

    “Lakini inafikirisha sana sijui kuna nini nyuma yake. NdiyoΒ  maana nilikuja kukuuliza sababu Desmond aliwaka sana baada yaΒ  kujuwa kuwa hawezi kumuona Mke wake. Hapo ndipo wasiwasiΒ  wangu ulipoanza….Kaendelee na kazi Luicia tutaongeaΒ  baadaye” Alisema Mkuu huyo kisha alimtazama Lucia akitokomeaΒ  eneo hilo akiwa ndani ya mavazi ya kihudumuΒ 

    Baada ya kupita masaa kadhaa, Desmond alimuarika MwanasheriΒ  Joel kwenye moja ya Baa zenye hadhi, alihitaji kumuelezaΒ  kuhusiana na jinsi mambo yalivyokuwaΒ 

    “Kesi hii tukienda kichwa kichwa tunaweza jikuta tunafiaΒ  jela…” alisema Desmond akiwa anagida unywaji, joel akaulizaΒ 

    “Kuna jambo jipya?”Β 

    “Kuhusu gari yangu niliyomuulia Sanga kutokukutwa Eneo laΒ  tukio badala yake kukutwa gari nyingine kabisa ikiwa na mwiliΒ  wa Sanga, tafsiri yake kuna Mtu wa tatu ambaye anaijuwa hiiΒ  inshu, pili ni kuhamishwa kwa Mke wangu na kupelekwa kwenyeΒ  wodi nyingine bila Mimi kupewa taarifa kisha nikazuiliwaΒ  kwenda kumuona, ni ishara kuwa kuna bomu linaenda kulipuka”Β  Alisema Desmond akiwa anamtazama Mwanasheria JoelΒ 

    “Uuuupss!! Hata mimi taarifa ya gari imenivuruga sana, huyoΒ  Mtu wa tatu ni nani hasa? Na kwanini hadi leo hajapiga simuΒ  wala kutoa taarifa polisi?” Aliuliza JoelΒ 

    “Nashindwa kuelewa, kila ninapoliwaza jambo hili naishiaΒ  kukosa majibu ya kueleweka japo namtilia sana mashaka nesiΒ  anayemuuguza Mke wangu, kuna bahasha amempa Mpenzi wanguΒ  sijui kuna nini ndani yake napata ukichaa” Alisema DesmondΒ 

    “Desmond hii ni vita kubwa sana na mwisho wake hautokuwaΒ  mzuri kama tunavyofikiria ni lazima tuwekeze nguvu na pesaΒ  ili tumalize mizizi yote” Alisema JoelΒ 

    “Kesho kutwa ni siku ya kumvisha pete Noela, kama yule nesiΒ  atakuja kwenye shughuli basi kila kitu kitaharibika, niΒ  lazima tumzuie asije” Alisema DesmondΒ 

    “Hiyo kazi niachie Mimi nitahakikisha hafiki kwenye shughuliΒ  lakini wewe unatakiwa kuhakikisha unamtafuta Mtu wa tatuΒ  aliyeona ukiwa unamuuwa Sanga Baharini, huyo ni Mtu hatariΒ  sana na huwenda anajuwa kuhusu kifo cha Mama Mandy kuwa mimiΒ  na wewe ndiyo wauwaji” Alisema Joel kisha alinyanyuka,Β  akachukua mkoba wake akapiga funda moja ya kinywaji akaiwekaΒ  glasi kwa nguvu juu ya meza kisha akaondoka zake pale.

    Jioni Lucia alimpigia simu Noela wakati huo akiwa anarejeaΒ  nyumbani kwake akamuuliza kuhusu ile bahasha kama ameanzaΒ  kuifanyia kazi lakini Noela alizidi kumsistizia kuwa niΒ  lazima shughuli ya kuveshana pete ipite kwanza ndipo aifanyieΒ  kazi, basi Lucia alikata simu akaelekea nyumbani kwao, akiwaΒ  anaingia ndani aliiyona gari nyeusi ikiwa imesimama nje yaΒ  nyumba yao, aliitazama lakini hakutia shaka kabisa, ndani yaΒ  gari hiyo alikuwemo Mwanasheria Joel na kilichomleta paleΒ  kilikuwa ni kuanza kazi ya kuhakikisha Lucia aendi kwenyeΒ  hiyo shughuli, baada ya kufahamu anapoishi Lucia, MwanasheriaΒ  Joel aliondoka zake.Β 

    Alimkuta Mama yake akiwa amelala, alikuwa mgonjwa hivyoΒ  jukumu kubwa la Lucia lilikuwa ji kuhakikisha kuwa Mama yakeΒ  anakuwa salama, Maisha yao yalikuwa duni na yeye ndiyeΒ  tegemezi, alipitia huko chumbani na kumkuta Mama yake akiwaΒ  amelala, alimfunika shuka kisha alitoka akaenda kuketiΒ  sebleni.Β 

    Alitafakari mambo mengi sana ikiwemo alichozungumza naΒ  Daktari Mkuu kisha alikumbuka alichokiweka kwenye bahashaΒ  aliyompa Noela, aliweka picha ya Desmond na Mwanasheria JoelΒ  kisha aliambatanisha na maelezo ya alichotaka Noela akifanye,Β  alivuta pumzi zake kisha alijilaza kidogo pale pale Sebleni.Β 

    Usiku ulipoingia, nyumbani kwa akina Noela na Mama yakeΒ  kulikuwa na shamra shamra sababu tukio la kuvishana peteΒ  lilikuwa limekaribia, baadhi ya ndugu walikuwa wamefika pale,Β  sura ya Noela ilizidi kunawiri kwa tabasamu bila kujuwa kuwaΒ  kulikuwa na vita kubwa iliyokuwa inapiganwa chini kwa chini,Β  Upande wa kule Hospitali matibabu yaliendelea kwa Mandy,Β  kukawa na tumaini kidogo lakini Desmond hakuambiwa chochoteΒ  kile sababu Tayari daktari Mkuu na Nesi Lucia walikuwa naΒ  ajenda ya siri kuhusu uhai wa Mke wa Desmond aliyeitwa Mandy.Β 

    Siku iliyofuata baada ya muda wa kazi kuisha, Lucia alimuombaΒ  Noela waonane mara moja, walionana mgahawani majira yaΒ  Mchana, ombi la Lucia likawa lile lile lakini NoelaΒ  alimsistizia kuwa hadi Shughuli ipite.Β 

    “Lucia ni kesho kutwa tu navishwa pete, kama nilivyokwambiaΒ  sitawekeza fokasi kubwa kwenye kazi yako sababu nina shughuliΒ  iache ipite kisha nitarudi kazidi na nitaanza na kazi yako”Β  Alisema NoelaΒ 

    “Sawa Noela lakini ni muhimu sana ukafungua ile Bahasha”Β  Alisitiza sana Lucia

    “Sawa nitafanya hivyo kwa ajili yako, nitahakikisha unafauluΒ  katika hilo jambo unalonipa kulifanya” Alisema NoelaΒ 

    “Umesema ni kesho kutwa ndiyo unavishwa pete, nitajitahidiΒ  ili nimuone shemeji yangu….kama sikosei ulisema anaitwaΒ  Joshua”Β 

    “Una kumbukumbu kama zamani, ndiyo anaitwa Joshua. Uje Lucia,Β  ni muhimu sana” Alisema Noela, waliachana baada ya kuwaΒ  wamezungumza vya kutosha. Aliporudi nyumbani Noela aliketiΒ  akajiuliza ni kwanini Lucia anasistiza sana afungue hiyoΒ  Bahasha.Β 

    Basi alielekea kwenye kisanduku chake cha kuhifahdia nyarakaΒ  mbalimbali za kazi, ndimo alimohifadhi ile BahashaΒ  inayotafutwa na Desmond, aliitoa kisha aliishikilia akiwaΒ  ameketi chini kando ya sanduku hiloΒ 

    “Mmh kuna nini humu mbona Lucia anasistiza sana nifungue?”Β  Alijisemea Noela ndani ya moyo wake, mwisho aliona ni boraΒ  aifungue ili kuondoa ile lawama aliyokuwa akipewa na LuciaΒ  kuwa anapuuzia kazi yakeΒ 

    Alichana kwa juu kisha karatasi zikawa zinaonekana kwa juu,Β  akavuta karatasi moja lakini wakati anaivuta akaidondoshaΒ  picha ya Desmond Mwanaume ambaye anamjuwa kama Joshua naΒ  ndiye Mtu anayetakiwa amfwatilie na kujuwa ukweli wa mamboΒ  yaliyojificha na ndiye Mwanaume anayeenda kuvishana nayeΒ  pete, bahati nzuri picha iliangukia kwa kujifunika, nyumaΒ  hakukuwa na maandishi yoyote yale.Β 

    Aliiokota picha hiyo ikiwa imejifunika vile vile, moyoΒ  ulianza kumdunda hata kabla hajaona picha hiyo, alijishangaaΒ  sana lakini kabla hajaigeuza Mama yake aliingia chumbaniΒ  akamuona Binti yake akiwa katika hali ile ya waiswasi.Β 

    Alimpokonya ile bahasha na picha kisha akavirudisha kwenyeΒ  ile Bahasha bila hata kuiangalia picha hiyo ya Desmond,Β  akaweka Bahasha kwenye sanduku hilo alilokuwa ameliacha waziΒ  kisha alilifunga.Β 

    “Noela huu siyo wakati wa wewe kufanya kazi, mara nyingi kaziΒ  zako zinakuumiza kichwa na kukufanya ukose raha. Huna haja yaΒ  kuwa katika hali hiyo cha Msingi ni kuweka akili kwenye tukioΒ  la kesho kutwa la kuvishwa pete na Mwanaume unayempenda”Β Β 

    Alisema Mama Noela kisha alimnyanyua Mtoto wakeΒ 

    “Unaenda kuwa Mke wa Joshua, ni jambo ulilolipigania kwa mudaΒ  mrefu hebu lipe kipaumbele, kazi zako utaendelea nazo baadaΒ  ya shughuli kupita sawa?”

    “Sawa Mama” alijibu Noela kisha alitoa tabasamu, laiti kamaΒ  angelikuwa ameiyona ile picha basi mambo yote yangelikuwaΒ  yameharibika maana angesoma kilichoandikwa na Lucia, angekutaΒ  siri ya jina la Desmond kisha tuhuma nzito.Β 

    “Haya twende” Alisema Mama Noela kisha alitoka na Binti yakeΒ  lakini akili ya Noela ilijikuta ikianza kuwaza ile Bahasha yaΒ  Lucia.Β 

    Naaam!! Desmond hakupotea Hospitalini sababu alijuwa fikaΒ  kuwa kwa huduma anazopewa Mke wake anaweza akaamka mudaΒ  wowote hivyo alihitaji kummaliza japo alizuiliwa kumuona,Β  alimtafuta Nesi Lucia akamwambia anahitaji kumuona Mke wake.Β 

    “Lucia mnanitendea vibaya sana kwa kutoniruhusu nimuone MkeΒ  wangu, wewe unajuwa ni jinsi gani nampenda Mke wangu naΒ  nimekuwa hapa kila siku kuhakikisha afya ya Mke wangu inakaaΒ  sawa” Alisema Desmond wakiwa wamesimama, hakujuwa kama LuciaΒ  tayari alimuhisi vibayaΒ 

    “Sasa kipi bora Desmond, umuone Mke wako kila siku akiwaΒ  katika hali ileile au usimuone ili afya yake ikae sawa ndaniΒ  ya muda mfupi? kumbuka Mkeo amekuwa hapa kwa zaidi ya mieziΒ  mitano, hadhi ya maisha yenu hakupaswa kuwa kwenye ile wodiΒ  wewe hukulioma hilo?” Alisema Lucia huku kila mmoja waoΒ  akipigana vita ndani kwa ndani, Desmond alipokuwa akimtazamaΒ  Lucia alikuwa akijiambia kuwa lucia ndiye Mtu wa tatuΒ  anayejuwa kila kitu huku Lucia akijisemea ndani ya moyo wakeΒ  kuwa ukweli utajulikana DesmondΒ 

    “Hilo ni sawa lakini kwanini maamuzi haya yamekuja ghafla tuΒ  tena bila kunishirikisha Mimi? Hamjui ni kiasi gani nimeumiaΒ  mimi Lucia, nampenda Mke wangu Mandy” alisema Desmond akiwaΒ  anatokwa na mchoziΒ 

    “Huna sababu ya kulia Desmond, ungekuwa unampenda Mke wakoΒ  usingemsainisha hati ya Makabidhiano ya Mali ukiwa naΒ  Mwanasheria” Alisema Lucia, Desmond akashtuka sasa kuwa LuciaΒ  ndiye aliyetoa hilo wazo la kuhamishwa kwa Mke wake baada yaΒ  ile siku kumsainisha Mandy mbele yakeΒ 

    “Anhaaa kwahiyo wewe ndiye uliyetoa wazo la Mke wanguΒ  kuhamishwa?” aliuliza Desmond akiwa anafuta chozi kishaΒ  aliweka tabasamu la kikatili, ile hali ya majonzi aliiondoaΒ  baada ya kugundua kuwa anaongea na Mtu ambaye alikuwaΒ  ameushtukia mchezo mzima.Β 

    “Lucia hukupaswa kujiingiza huku kabisa kwasababu hujuiΒ  ilianzaje wala inaenda kuishaje, umefanya kosa kubwa litakaloΒ 

    kugharimu. Mama yako ni Mgonjwa, ni bora uweke Mawazo yoteΒ  kwa Mama yako kuliko kuweka kwa Mtu ambaye atakujaΒ  kukugharimu” Alisema Desmond kwa sauti iliyokaza yenyeΒ  kumaanisha, Lucia alicheka chini chini kisha akamwambiaΒ  DesmondΒ 

    “Mwanzo nilikuwa nikikupenda sababu niliamini una mapenziΒ  mazito sana kwa Mke wako lakini baadaye nilikuchukia baada yaΒ  kugundua kuwa wewe ni miongoni mwa waliosababisha yeye akawaΒ  pale, nakuhakikishia Desmond, igizo unalofanya ukweliΒ  utajulikana Mkeo akiamka” Alisema Lucia kisha alianzaΒ  kuondoka lakini Desmond alimshika mkono akamwambiaΒ 

    “Una masaa 24 ya kutoka katika hili Lucia, Uwe na siku njema”Β  Alisema Desmond kisha kila mmoja alielekea alipopakusudia,Β  lakini Maneno aliyoyazungumza Lucia yalimtia ukichaa sanaΒ  Desmond akiwa kwenye gari aliwasiliana na Joel akamwambiaΒ  Wamuuwe Lucia kabla ya tukio la kuvishwa pete kwa Noela.Β 

    Siku hiyo Lucia alizidi kuchanganikiwa sana, aliporudiΒ  nyumbani kwao alichukua simu yake ambayo wakati anaongea naΒ  Desmond alimrekodi ili aweze kuongeza ushahidi wa kumpaΒ  Noela, alimtumia sauti hiyo ya mazungumzo Noela kishaΒ  akampigia simu ili amuelekeze lakini Noela hakupokea simu,Β  maandalizi ya Tukio la kuvishwa pete yalikuwa yamepamba motoΒ  sana hivyo hakuwa na muda wa kukaa na simu.Β 

    Siku hiyo iliisha, siku iliyofuata ndiyo ilikuwa siku yaΒ  kuvishwa pete kwa Noela, maandalizi yote yalifanyika paleΒ  pale nyumbani kwao sababu hawakutaka Watu wengi, gharama zoteΒ  alizifanya Desmond. Usiku wa tukio Lucia alijiandaa, akamuagaΒ  Mama yake akamwambiaΒ 

    “Mama naenda kwenye sherehe ya rafiki yangu, sitochelewaΒ  kurudi. Nakupenda sana Mama yangu” AlisemaΒ 

    “Nakupenda pia Binti yangu, usijali nenda Mama nitakuwaΒ  salama. ” alisema Mama yake Lucia, waliagana hapo kisha LuciaΒ  alitoka. Alisimama Nje akimsubiria Mtu wa PikipikiΒ  aliyewasiliana naye kuwa aende kumchukua hapo na kumpelekaΒ  nyumbani kwa akina Noela, alisimama kwa muda mrefu nje,Β  alipoona muda unazidi kwenda alianza kutembea taratibu iliΒ  kama atakutana na Pikipiki aitumie, Ulikuwa ni usiku wa saaΒ  mbili, baadaye likaja gari moja na kusimama mbele yake, LuciaΒ  alijiuliza ni nani aliyesimama mbele yake.Β 

    Kioo kilishushwa akaonekana Mwanaume mmojaΒ 

    “Samahani Dada unaenda wapi?” Aliuliza huyo Mwanaume

    “Naenda mahali kwani vipi?” aliuliza Lucia maana alikuwaΒ  amechukia kwasababu bodaboda wake alikuwa amendanganya kuwaΒ  hayupo mbali kumbe yupo mbaliΒ 

    “Sio vema Mtoto wa kike akatembea kwa mguu usiku huu,Β  naelekea barabara ya sita sijui wewe” Alisema Mwanaume huyo,Β  Lucia alifikiria akaona ajishushe tu kwa huyo Mwanaume maanaΒ  yeye alikuwa akielekea Barabara ya nne.Β 

    “Naelekea Barabara ya Nne” Alijibu LuciaΒ 

    “Basi twende nikusindikize” Alisema Mwanaume huyo, LuciaΒ  aliingia kwenye gari, safari ilianza kuelekea nyumbani kwaoΒ  Noela, wakiwa Barabarani mwanaume huyo alionekana kumtongozaΒ  Lucia lakini Lucia hakuonekana kumkubali kisha alimwambiaΒ 

    “Kama umenipa msaada ili unitongoze naomba unishushe MimiΒ  siyo Mwanamke wa hivyo” Alisema Lucia akionekana kuchukizwa..Β 

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA NANE

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & PainΒ 

    Β Β 

    Love & Pain

    7 Comments

    1. Mpenzi wangu on November 18, 2024 2:59 pm

      Aaashhhhh haitosh admin ongeza kidog jaman nataka kujuwa tu Lucia Alicia au hakufikaaaπŸ˜ͺπŸ˜”πŸ˜”πŸ˜”

      Reply
    2. Sharo love malkx πŸ’– on November 18, 2024 3:59 pm

      Mhh uyo anae mtongoza asije akawa muuwaji mhhπŸ˜’πŸ˜’

      Reply
    3. Calvin paul on November 18, 2024 5:55 pm

      Joel huyooo

      Reply
    4. G shirima on November 18, 2024 7:45 pm

      Mh iyo gari iyoπŸ₯ΊπŸ₯ΊπŸ˜₯

      Reply
    5. Hamis on November 18, 2024 8:32 pm

      Kaz ipo

      Reply
    6. Fawziya Hassan on November 19, 2024 12:44 pm

      Mmmh
      Mambo yamepamba πŸ”₯ na yanaenda kuwa sio mambo tena bali ni balaa πŸ˜₯πŸ˜₯
      Asante Mwandishi kwa niaba ya Admini kwa Simulizi yenye mafunzo na mazingatio makubwa
      More Love from Kenya ❀️

      Reply
    7. πŸ“ƒ + 1.196678 BTC.GET - https://yandex.com/poll/enter/4Joc2mvUbapjsUMcMcKM3z?hs=f0acabef123ebcf184c9223d59d84a17& πŸ“ƒ on June 21, 2025 1:59 am

      8e2y9i

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi July 12, 2025

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya kwanzaΒ  β€œBaba” aliita Zahoro, Mzee Miroshi alimtazama Zahoro bila…

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.