Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Ligi Za Kuziepuka Wakati Wa Betting
    Chuo cha Kubeti

    Ligi Za Kuziepuka Wakati Wa Betting

    MhaririBy MhaririJanuary 29, 2024Updated:June 12, 20242 Comments3 Mins Read8K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Ligi
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Zipo ligi mbalimbali duniani ambazo wawekezaji wa mikeka hupenda kuzitumia katika kubashiri lakini wamekua wakikutana na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata matokeo ambayo sio ya kutarajiwa na wadau wa ubashiri. Leo hii wacha tutazame ligi za kuepuka wakati ukiwa unasuka mikeka ya betting na baadhi ya sababu kwanini uziepuke ligi hizo.

    Ligi Kuu ya China (Chinese Super League)

    Hii ndio ligi kubwa zaidi nchini China ambayo ina timu 16 zinazoshindana pamoja kuhakikisha kuwa wanakua mabingwa nchi hii. Ukiachilia mbali kupoteza umaarufu mkubwa kama zamani lakini bado inawavutia baadhi ya wachezaji wakubwa ambao wanakwenda kufata mishahara mikubwa katika ligi hii. Unajua kwanini ni moja ya ligi sikupendekezi ubashiri sana? Ni kwasababu ya sifa iliyonayo ligi hii ya kuwa na changamoto ya upangaji wa matokeo na rushwa jambo ambalo inafanya ubashiri kuwa mgumu.

    Ligi Kuu ya Urusi (Russian Premier League)

    Ukizungumzia majina kama Andrei Arshavin na Aleksandr Kokorin basi huwezi kuacha kutaja ligi hii kubwa na ngazi ya juu zaidi ya mpira wa miguu katika nchi ya Urusi. Hii inashirikisha timu 16 zinazopambania ubingwa wa ligi hii na inafahamika zaidi kama ligi ambayo mara nyingi huwa ina magoli mengi sana katika baadhi ya mechi.

    Ligi hii ilishawahi kupata shutuma za upangaji wa matokeo ya mechi na shutuma za ruswa kutoka kwa wachezaji na viongozi wa timu hivyo bado inaingia katika ile orodha ya ligi ngumu zaidi kubashiri nazo.

    Ligi Kuu ya Mexico ( Liga MX)

    Siku zote ukiitaja tu nchi ya Mexico basi kila mmoja huja na fikra yake kuhusu nchi hii ambayo huwa na makundi mengi ya kihuni. Katika nchi yao Liga MX ndio ngazi ya juu kabisa ya soka ambayo inafuatiliwa kwa ukaribu zaidi ikiwa na timu 18, haifahamiki sana kwenye haya mambo lakini mfumo wake wa uendeshaji wa ligi unachangia kwa namna moja au nyingine kuruhusu upangaji wa matokeo.

    Ligi Kuu ya Uturuki (Turkish Super Liga)

    Ligi hii inazikutanisha timu 20 zinazopambania ubingwa wa nchi hii na ndio ligi kubwa zaidi nchini Uturuki. Ni moja kati ya ligi ambayo ishawahi kukutana na changamoto kubwa ya upangaji wa matokeo katika misimu kadhaa iliyopita ambapo zilikua tuhuma kubwa sana katika ligi hii ambayo ilitoa wachezaji wenye majina makubwa n ahata kusumbua katika ngazi ya mpira wa miguu barani Ulaya.

    Ligi Kuu ya Romania (Liga1)

    Nayo inaingia katika orodha ya ligi za kuwa nazo makini wakati ukiwa unataka kubashiri kuhusu mikeka ya ushindi, licha ya kuwa inakua haifahamiki sana kama ligi nyingine hapo juu lakini imekua miongoni mwa ligi ambayo inapambana sana kiuchumi kuhakikisha wanakua na ligi bora lakini pia na changamoto kubwa sana ya upangaji wa matokeo jambo liliopelekea kuingia katika orodha hii.

    SOMA ZAIDI: Ligi Bora Za Kubetia Kufungana GG 2024

    ligi kuu

    2 Comments

    1. Rumbyambya Jr on June 12, 2024 1:57 pm

      😂Admin Ligi ya Ghana na Ivory Coast je

      Reply
    2. John makuza on June 12, 2024 2:39 pm

      Ni kweli na wikii hii nzma mikaka inachanika tu adimini nn tufanye zaid ila pia nataman siku mkiweka mkeka wa uhakika bhx adimini weka namba kabisa ya kukutumia hata soda🤣🤣🤣🤣

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.